?> URAIA STANDARD FIVE EXAMS SERIES
URAIA STANDARD FIVE EXAMS SERIES

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA

MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA DARASA LA TANO

URAIA NA MAADILI

MUDA:1:30                                                             

JINA_____________________________________SHULE_________________________

MAELEZO

1. Jaza taarifa zako muhimu katika karatasi ya kujibia uliyopewa

2. Jibu maswali yote kulingana na maelekezo ya kila sehemu

3. Zingatia unadhifu wa kazi yako

4. Katika swali la 1-40 andika herufi ya jibu sahihi

5. Kwa swali la 41-45 andika majibu katika nafasi iliyoachwa wazi

 

Chagua jibu sahihi katika swali la 1-40 kisha andika jibu katika nafasi uliopewa

 1. Zipi kati ya nchi zifuatazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola?................  (a) Botswana na Burundi (b) Botswana na Zambia (c) Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (d) Malawi na Burundi (e) Zambia na Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo
 2. Makubaliano ya kuanzisha Umoja wa Mataifa yalifanyika (a) New York (b) San Francisco (c) San Diego (d) Washington (e) Los Angeles
 3. Ni chombo gani chenye jukumu la kumchagua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa? (a) Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa. (b) Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. (c) Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. (d) Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa. (e) Mahakama Kuu ya Kimataifa.
 4. Tanzania inapata faida gani kwa kuongeza biashara yake ya kimataifa? (a) Kuongeza majengo (b) Kupunguza wajasiriamali wa ndani (c) Kuongeza deni (d) Kupunguza mikataba ya kibiashara (e) Kuongeza fedha za kigeni
 5. Mojawapo ya changamoto za ushirikiano wa umoja wa mataifa ni; (a) Mikopo yenye riba kubwa (b) Migogoro ya mipaka (c) Ujirani mwema (d) Kukuza biashara
 6. Sera ya Tanzania ya Uhusiano wa kimataifa ilitungwa mwaka (a) 1995 (c) 1977 (c) 2015 (d) 2005
 7. Hali ya kuwa na tabia zinazojali hali ya mtu huitwa: (a) Nasaba (b) Upendo (c) Utu (d) umoja
 8. Mfumo wa kijamii wa kutoa vitu au huduma kwa upendeleo kwa msingi wa rangi, jinsia au kabila unaitwa; (a) Ubepari (b) Utajiri (c) Ubaguzi (d) Uonevu
 9. Lipi kati ya hayo linaweza kusababisha ubaguzi? (a) Umaskini (b) Upendo (c) Tofauti za kidini (d) Kutii sheria
 10. Tunaonesha kuthamini utu wa mtu tukifanya matendo gani?(a) Tunapoangalia mwonekano wake (b) Tunapoonesha kumjali bila kumbagua (c) Tunapoangalia mavazi na sura yake
 11. Unapoona mtu mwenye asili ya China anaongea Kiswahili inamaanisha nini? (a) Hajui lugha yake ya kichina (b) Anakipenda Kiswahili kuliko Kichina (c) Anaimarisha uhusiano wa kiutamaduni na nchi yetu (d) mvumizi
 12. Ipi kati ya zifuatazoni faida ya kuchangamana na watu wa asili tofauti? (a) Upendo na kuheshimiana (b) Ubaguzi (c) Kuwa na moyo wa kutokuthamini utu (d) kuwa mtulivu.
 13. Sifa mojawapo ya mtu anayeomba uraia wa Tanzania: (a) Aukubali uraia wanchi alikotoka kwa maandishi (b) Sio lazima kutangaza kwenye vyombo vya habari (c) Awe hajawahi kukutwa na kosa lolote la jinai toka aingie nchini
 14. Mgawanyo wa madaraka husaidia: (a) Kuepusha kuingiliana katika kutekeleza majukumu (b) Kupunguza kazi na kupinga unyonyaji (c) Mtu mwenye madaraka kunyenyekewa (d) Kukuza ugomvi
 15. Kazi ya vyama vya siasa nchini ni Pamoja na: (a) Kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo (b) Kuitisha mikutano ya hadhara na kuhamasisha maandamano ya uvunjifu wa amani nchini (c) Kuomba kura kwa wananchi wakati wa uchaguzi tu. (d) kuanzisha vurugu
 16. Hali au tabia ya kuzungumza bila kificho huitwa? (a) Unafiki (b) Lofa (c) Uwazi (d) Uzabinazabina
 17. Kipi kati ya vifuatavyo ni chombo cha kisheria kinachohusika na kusimamia haki? (a) Polisi (b) Bunge (c) Shule (d) Mahakama
 18. Ipi kati ya zifuatazo ni sababu za ongezeko la matendo ya ukiukwaji wa haki za binadamu? (a) Kulipa kodi stahiki (b) Watoto kutopelekwa shule za bweni (c) Watu kujichukulia sheria mkononi (d) Upendo kwa watu wenye mahitaji maalumu
 19. Yafuatayo ni madhara ya kutokuwa muwazi: (a) Kusifiwa na kuharibu (b) Kuleta migongano (c) Uzembe na uhalifu (d) Mshikamano na uvivu
 20. Ipi kati ya tabia zilizoorodheshwa inaonesha uvunjifu wa sheria za shule? (a) Kuwahi sana shuleni (b) Kusoma kwa bidi (c) Utoro na kupigana (d) Kujisomea nyumbani baada ya masomo
 21. Kanuni zinazowekwa shuleni na nyumbani husaidia nini? (a) Kufuata utaratibu na kudhibiti nidhamu (b) Ukiukaji wa haki za mtoto (c) Ubabe wa wazazi au walezi (d) Kuleta fujo
 22. Ari ya kufanya kazi inaitwa? (a) Hamu (b) Bidii (c) Morali (d) Mori
 23. Fedha au mavuno yatokanayo na kazi unayofanya huitwa (a) Mali (b) Mshahara (c) Kipato (d) Malipo
 24. Tathmini shuleni inapaswa kuwa; (a) Kazi za darasani tu (b) Kazi za darasani na nje ya darasa (c) Kazi za viwanjani (d) Katika mitihani tu
 25. Kuangalia kitu kwa undani kisha kukadiria thamani yake au ubora wake huitwa (a) Kuchunguza (b) Mpangokazi (c) Tathmini (d) Morali
 26. Hali inayopunguza ukamilifu wa kitu inaitwa? (a) Shida (b) Kudorora (c) Kupooza (d) Kipato
 27. Hali isiyo na jibu la haraka huitwa: (a) Taaluma (b) Fursa (c) Utata (d) Changamoto
 28. Tunaweza kukabiiana na changamoto za maisha kwa; (a) Kushirikisha wakubwa zetu (b) Kutumia madawa ya kulevya (c) Kusali (d) Kuvumilia
 29. Kipi kitatokea ikiwa tutashindwa kutatua changamoto za maisha? (a) Vidonda vya tumbo (b) Shinikizo la damu (c) Kushindwa kutimiza majukumu (d) Yote hayo
 30. Lengo la uvumilivu ni (a) Kuvumilia mateso (b) Kukata tama (c) Kutafuta njia sahihi za kutatua shida (d) Kufikia malengo
 31. Ni kitendo kipi sio sahihi? (a) Kuheshimu sala za wakristo (b) Kudharau mavazi ya kiislamu (c) Kutopiga kelele darasani (d) Kutumia lugha ya taifa
 32. Lipi kati ya haya ni matendo ya uvumulivu? (a) Kulalamika (b) Kuheshimu itikadi na mila za watu (c) Kuwasema wengine (d) Kujiona bora
 33. Ipi kati ya hizi ni utovu wa nidhamu? (a) Kuvaa nguo za nyumbani shuleni (b) Kuzingatia usafi wa mwili (c) Kuwahi shuleni (d) Kutii kengele  shuleni
 34. Migogoro shuleni itakwisha endapo: (a) Wanafunzi wote wakorofi hawatafukuzwa shule (b) Walimu watashirikiana na baadhi ya wazazi (c) Shuleni kutakuwa na uwazi na uongozi unaofuata sheria na haki (d) Watu wote watamtii mkuu wa shule
 35. Kiongozi bora ni: (a) Mtu anayependwa na watu wengi (b) Mtu anayetawala kwa kufuata haki (c) Mtu anayechaguliwa kwa kura nyingi (d) Mtu anayependelea marafiki
 36. Mwalimu mkuu ana majukumu ya: (a) Kupokea fedha za ada na kuzitumia kwa matumizi yake binafsi (b) Kuongoza na kusimamia mambo yote shuleni (c) Kuadhibu wanafunzi kwa uonevu (d) Kufundisha walimu wengine
 37. Viongozi wote wanapaswa kuzingatia: (a) Maendeleo yao tu (b) Misingi ya utawala bora (c) Utawala wa kiimla (d) Upendeleo
 38. Mtu kuwa na utayari wa kupokea majukumu hufuatana na: (a) Kujitambua na kuwa na utayari wa kupokea ushauri (b) Kushindana na wenzako (c) Kukataa ushauri kutoka kwa mtu yeyote (d) Kukubali bila pingamizi
 39. Mojawapo ya misitu ya kupandwa Tanzania ni (a) Zaraninge (b) Pugu-kisarawe (c) Msitu wa kibena (d) Udzungwa
 40. Ni kitendo gani kati ya hivi huchangia kuharibu rasilimali ardhi? (a) Kulima matuta kwa kukinga mteremko (b) Kuchoma misitu wakati wa kusafisha mashamba (c) Kuweka mbolea ya samadi shambani (d) Kutumia mbolea ya dukani

Picha hii hapa chini inaonyesha watu wakifanya tukio la kidemokrasia. Itumie kujibu swali la 41-45

 1. Taja kitendo kinachoendelea kwenye picha hapo juu
 2. Toa faida mbili za kitendo hiki katika kukuza demokrasia
 3. Taja vyama viwili vikuu vya kisiasa nchini Tanzania
 4. Taja sifa mbili za mpiga kura Tanzania
 5. Tanzania hufanya uchaguzi wa rais na wabunge kila baada ya miaka mingapi?

LEARNINGHUBTZ.CO.TZURAIA STANDARD FIVE EXAM SERIES 57

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA

MTIHANI WA NUSU MUHULA WA KWANZA- MACHI-2022

URAIA NA MAADILI DARASA LA TANO

SEHEMU A: CHAGUA JIBU SAHIHI KUTOKA YALE ULIOPEWA

 1. Wasichana wanaweza kujiepusha na mimba za mapema kwa; A. Kuwa na marafiki waaminifu b. Kwenda disko na jamaa zao c. Kupokea zawadi kutoka kwa wavulana d. Kuepuka matembezi yasiyo ya lazima usiku. e. kukaa pweke
 2. Kwanini tunapaswa kuvaa mavazi yaliyo na staha? A.Yanaonyesha kujiheshimu b. Yanasaidia kuepuka magonjwa c. Ili tupendwe d. Ili tuvutie watu e. ni ushamba
 3. Kabila gani huvaa kaniki kwenye ngoma za asili? A. Maasai b. Wagogo c. Wanyasa d. Wasukuma e. wachaga.
 4. Mabadiliko ya kimwili ya mtoto wa kiume na wa kike kuingia utu uzima huitwa a. Jinsia b. Kuvunja ungo c. Utu uzima d. Balehe e. ujana
 5.  Ipi sio staha katika jamii a. Kuvalia nguo inayokustiri b. Kucheza na wavulana sehemu za uchochoro c. Kuwasalimia watu kwa heshima d. Kupenda watu wote e. kuvaa vibaya
 6. Tunapaswa kuonesha upendo kwa watu a. Wenye mahitaji maalum b. Ndugu wa karibu c. Watu wanotupenda d. Watu wote bila ubaguzi. d. marafiki.
 7. Wafuatao wana mahitaji maalum isipokuwa: a. Wazee b. Watoto c. Watu wenye ulemavu wa akili d. Yatima na maskini. e. watu wote
 8. Tofauti gani sio ya  kimaumbile kati ya mwanaume na mwanamke? A. Kupata hedhi b. Kupata mimba c. Uwezo wa kuzaa d. Kunyonyesha e. kuolewa.
 9. Umuhimu wa bendera ya rais ni . a. Kutembelea katika ziara mbalimbali tu b. Kuonyesha mamlaka ya rais  c. kutangaza nchi d. Kuhamasisha mwenge wa uhuru e. kuonyesha uhuru
 10. Chimbuko la sheria zote nchini Tanzania ni; a. Fedha ya Tanzania b. Katiba ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania. C. Vyama vya siasa d. rais. E. bunge
 11. Rangi ya bluu iliyopo katika bendera ya taifa uwakilisha; a. Watanzania b. Madini c. Maji ambayo ni mito, maziwa na bahari nchini Tanzania d. utajiri e. wanyama pori
 12. Alama ambayo hutumika kuonyesha umiliki wa mali na nyaraka za serikali tu ni; a. Picha ya makamu wa rais b. Bendera ya taifa c. Nembo ya Taifa d. twiga e. punda
 13. Ni ishara gani inayoonyesha kwamba taifa limepatwa na msibu mkubwa? A. Bendera zote kupepea nusu mlingoti b. Bendera ya taifa kupepea nusu mlingoti c. Bendera ya taifa kutopandishwa kabisa siku ya tukio. Watu kubaki nyumbani e. watu kunyamaza siku nzima
 14. Ni siku ambazo viongozi hupata fursa kueleza mafanikio na changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi a. Siku za kukimbizwa mwenge wa uhuru tu b. Sikukuu ya mapinduzi ya Zanzibar tu c. Sikukuu za kitaifa d. sikukuu ya iddi e. sikukuu ya kristmas
 15. Msaidizi wa mkuu wa mkoa katika shughuli zake za utendaji ni nani? A. ofisa elimu mkoa b. katibu tawala wa mkoa c.mkuu wa idara ya utawala na utumishi mkoa d. mhasibu. E. ofisa afya wa mkoa
 16.  Mwenyekiti wa halmashauri ngazi ya wilaya huongoza akina nani? A. wenyeviti wa mtaa b. makatibu tawala c. madiwani wa halmashauri d. mtendaji wa kata e. wanakijiji.
 17. Katika ofisi ya kata, nani ni mtendaji mkuu? A. Diwani b. Ofisa mtendaji wa kata c. Ofisa mazingira wa kata d. Ofisa maendeleo wa kata. Katibu
 18. Wakuu wa idara katika halmashauri za wilaya huwajibika kwa nani? A. mkurugenzi wa halmashauri b. mkuu wa wilaya c. mkuu wa mkoa d. ofisa tawala wa wilaya e. diwani
 19. Mkurugenzi wa halmashauri anapatikanaje? A. kwa kupigiwa kura na madiwani b. kwa kuajiriwa na menejimenti ya utumishi wa umma c. kwa kuteuliwa na rais d. kwa kupigiwa kura na wananchi katika halmashauri inayohusika e. kuteuliwa na bunge.
 20. Katibu wa vikao vya baraza la madiwani ni nani? A. Mwenyekiti wa Halmashauri b. Diwani wa viti maalum c. Katibu tawala d. Mkurugenzi wa Halmashauri. e. diwani aliyeteuliwa.
 21. Kujijali na kuwajali wenzako kunasaidia mwanafunzi: a. Kufanya mambo yanayokubalika katika jamii b. Kuogopwa c. Kutenda uovu d. Kuwa mkorofi e. kuwa jasiri
 22. Kugombana na wenzako mara kwa mara unapokuwa shuleni au nyumbani ni tabia: a. Isiyokubalika b. Inayoonesha kujali wenzako c. Ya upendo d. Ya unyenyekevu au kishujaa e. heshima.
 23. Matendo yafuatayo yanakuza uhusiano na watu wengine: a. Kushirikiana, kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu, kuheshimiana na kujiunga katika vikundi vya kusaidiana b. Kuonesha upendo, kuheshimiana, ugomvi na unafiki c. Kuwasaidia watu wenye mahitaji, kusema uongo, kushirikiana na kuheshimiana d. Kuwasaidia watu wote na kuwafanyia unafiki. e.kuwa mpole
 24. Moja ya faida za kujiunga na klabu za masomo shuleni ni: a. Kukuza uelewa na uongo b. Kukuza uelewa na kujiamini c. Kushindana kwa majibizano ya ujeuri d. Kuwa maarufu na kuvunja haki za binadamu e.kugandamiza haki za kibinadamu
 25. Ni njia mojawapo ya kutomsaidia mwanafunzi mwenye matatizo: a. Kumshika mkono b. Kumkumbatia c. Kumshauri namna ya kutatua tatizo d. Kumtenga e. kumbeza
 26. Unapo shiriki katika shughuli za maendeleo ya jamii unaleta; a. Mshikamano na uzalendo b. Shida kwa wananchi c. Mtandao wa ombaomba d. utengano e. umasikini
 27. Shughuli za kibinadamu ambazo huchangia uchafuzi wa vyanzo vya maji ni kama vile: a. Kufua nguo, kupanda miti kuzunguka eneo la vyanzo vya maji b. Kulima na kufua nguo kando kando ya mto c. Kutunza mazingira ya asili na kunywesha mifugo d. Kupanda miti e. ukulima.
 28. Mamlaka inayohusika na usimamizi na utunzaji mazingira nchini huitwa: a. Mamlaka ya mapato ya Tanzania b. Wizara ya afya c. Baraza la usimamizi wa mazingira la taifa d. Tume ya taifa ya mazingira e. baraza la wauguzi.
 29. Ni vyema tuka boresha njia za uchimbaji wa madini ilikusaidia: a. Uchimbaji wa madini kuwa endelevu na wenye ufanisi b. Kutopata fedha za kutosha c. Kukosa ajira kwa wingi d. Kutofuta umaskini e. kujenga uadui.
 30. Ukataji wa miti ovyo na uchomaji wa misitu huweza kusababisha: a. Ukame na baa la njaa b. Mvua nyingi na kupata eneo kubwa la kulima c. Kupata mavuno mengi d. umasikini
 31. Shughuli za maendeleo ya jamii ni Pamoja na: a. Kuiba na kutapeli wenzako b. Kuharibu mazingira c. Kusafisha barabara, mitaro na mazingira d. ujambazi.  E. usafi
 32. Ipi kati ya hizi ni miongoni mwa rasilimali zilizopo Tanzania? A. Misitu b. Mbao c. Mkaa d. Nyasi e. majani.
 33. Ipi kati ya hizi ni faida ya misitu? A. Kutupatia madini b. Kutupatia mbao c, Kutupatia nafaka d. Kuikata e. kuitunza
 34. Tunawezaje kuhifadhi misitu? A. Kwa kukata miti b. Kwa kuchoma misitu c. Kwa kupanda miti d. Kulima ndani ya misitu e. kulima
 35. Ni kitendo gani kati ya hivi huchangia kuharibu rasilimali maji? A. Kukata miti kwenye vyanzo vya maji b. Kutochoma moto misitu c. Kutotiririsha maji machafu d. Kutunza miti e. kuharibu msitu.
 36. Ni kitendo gani kati ya hivi huchangia kuharibu rasilimali ardhi? A. Kulima matuta kwa kukinga mteremko b. Kuchoma misitu wakati wa kusafisha mashamba c. Kuweka mbolea ya samadi shambani d. Kutumia mbolea ya dukani e. kufuga wanyama wengi
 37. Madini ya almasi huchimbwa wapi Tanzania? A. Mererani b. Mwanza c. Shinyanga d. Arusha e.
 38. Usimamizi wa majukumu shuleni hufanywa na; a. Walimu peke yao b. Wanafunzi wenyewe tu c. Walimu wakishirikiana na viongozi wa serikali ya wanafunzi d. Wazazi e. walinzi
 39. Viongozi wote wanapaswa kuzingatia: a. Maendeleo yao tu b. Misingi ya utawala bora c. Utawala wa kiimla d. Upendeleo e. uadui
 40. Utii wa sheria: a. Haubagui kiongozi au mwananchi b. Bila shuruti hauwezekani c. Unasababisha ucheleweshaji wa majukumu d. Ni wa kiimla e. ni ushamba

 

SEHEMU B. JIBU MASWALI YOTE KWA UFASAHA.

 1. Katiba ya kwanza ya Tanzania iliandikwa mwaka gani?.................................
 2. Watanzania wengi wana uraia wa aina gani?......................................................
 3. Nini maana ya utamaduni……………………………………………………………………………….
 4. Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia chakula huitwa?...........................
 5. Makao makuu ya umoja wa afrika mashariki yapo wapi?

LEARNINGHUBTZ.CO.TZURAIA STANDARD FIVE EXAM SERIES 48

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA

MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA DARASA LA TANO

URAIA NA MAADILI

MUDA:1: 30                                                             

JINA_____________________________________SHULE__________________

Chagua Jibu Sahihi

 1. Msaidizi mkuu wa mkoa katika shughuli zake za utendaji ni nani?
 1. Ofisa elimu mkoa
 2. Katibu tawala wa mkoa
 3. Mkuu wa idara ya utawala na utumishi mkoa
 4. Ofisa afya wa mkoa
 1. Mwenyekiti wa halmashauri ngazi ya wilaya huongoza akina nani?
 1. Wenyeviti wa mtaa
 2. Makatibu tawala
 3. Madiwani wa halmashauri
 4. Mtendaji wa kata
 1. Katika ofisi ya kata, nani ni mtendaji mkuu?
 1. Diwani
 2. Ofisa mtendaji wa kata
 3. Ofisa mazingira wa kata
 4. Ofisa maendeleo wa kata
 1. Mkurugenzi wa halmashauri anapatikanaje?
 1. Kwa kupigiwa kura na madiwani
 2. Kwa kuajiriwa na menejimenti ya utumishi wa umma
 3. Kwa kuteuliwa na rais
 4. Kwa kupigiwa kura na wananchi kattika halmashauri inayohusika
 1. Katibu wa vikao vya baraza la madiwani ni nani?
 1. Mwenyekiti wa halmashauri
 2. Diwani wa viti maalumu
 3. Katibu tawala
 4. Mkurugenzi wa halmashauri
 1. Kanuni zinazowekwa shuleni na nyumbani husaidia nini?
 1. Kufuata utaratibu na kudhibiti nidhamu
 2. Ukiukaji wa haki za mtoto
 3. Ubabe wa wazazi au walezi
 4. Kuleta fujo
 1. Lipi kati ya haya yaliyoorodheshwa ni tendo la kutetea haki zako na za Watoto wenzako:
 1. Kukosekana utawala bora
 2. Kutii sheria na kutozitumia
 3. Kusaidia kutoa taarifa kwenye mamlaka zinazohusika
 4. Kulia kwa uchungu
 1. Ipi kati ya tabia zilizoorodheshwa inaonesha uvunjifu wa sheria za shule?
 1. Kuwahi sana shuleni
 2. Kusoma kwa bidi
 3. Utoro na kupigana
 4. Kujisomea nyumbani baada ya masomo
 1. Lipi kati ya haya ni matendo ya uvumulivu?
 1. Kulalamika
 2. Kuheshimu itikadi na mila za watu
 3. Kuwasema wengine
 4. Kujiona bora
 1. Ni kitendo kipi sio sahihi?
 1. Kuheshimu sala za wakristo
 2. Kudharau mavazi ya kiislamu
 3. Kutopiga kelele darasani
 4. Kutumia lugha ya taifa
 1. Tunapopata changamoto katika maisha tunapaswa?
 1. Kulia
 2. Kukata tama
 3. Kuwa mvumilivu na kutafuta suluhisho
 4. Kudai haki
 1. Lengo la uvumilivu ni
 1. Kuvumilia mateso
 2. Kukata tama
 3. Kutafuta njia sahihi za kutatua shida
 4. Kufikia malengo
 1. Kunapo tokea mabadiliko katika jamii tunapaswa
 1. Kukata tama
 2. Kujiamini
 3. Kuyapinga
 4. Kulia

 

 1. Mtu kuwa na utayari wa kupokea majukumu hufuatana na:
 1. Kujitambua na kuwa na utayari wa kupokea ushauri
 2. Kushindana na wenzako
 3. Kukataa ushauri kutoka kwa mtu yeyote
 4. Kukubali bila pingamizi
 1. Usimamizi wa majukumu shuleni hufanywa na;
 1. Walimu peke yao
 2. Wanafunzi wenyewe tu
 3. Walimu wakishirikiana na viongozi wa serikali ya wanafunzi
 4. Wazazi
 1. Viongozi wote wanapaswa kuzingatia:
 1. Maendeleo yao tu
 2. Misingi ya utawala bora
 3. Utawala wa kiimla
 4. Upendeleo
 1. Utii wa sheria:
 1. Haubagui kiongozi au mwananchi
 2. Bila shuruti hauwezekani
 3. Unasababisha ucheleweshaji wa majukumu
 4. Ni wa kiimla
 1. Ipi sio manufaa ya ushirikiano wa Tanzania na Mataifa Mengine?
 1. Kupata masoko ya bidhaa
 2. Kuboresha usalama na amani
 3. Kupata mikopo
 4. Kupoteza utamaduni wake
 1. Sera ya Tanzania ya Uhusiano wa kimataifa ilitungwa mwaka
 1. 1995
 2. 1977
 3. 2015
 4. 2005
 1. Kipi hakipo kwenye sera ya Tanzania ya uhusiano wa kimataifa?
 1. Kulinda uhuru na usalama wa nchi
 2. Kuimarisha umoja wa mataifa na ushirikiano
 3. Kumaliza upinzani
 4. Kupigania uboreshaji wa umoja wa mataifa
 1. Mojawapo ya changamoto za ushirikiano wa umoja wa mataifa ni;
 1. Mikopo yenye riba kubwa
 2. Migogoro ya mipaka
 3. Ujirani mwema
 4. Kukuza biashara
 1. Ipi kati ya hizi ni miongoni mwa rasilimali zilizopo Tanzania?
 1. Misitu
 2. Mbao
 3. Mkaa
 4. Nyasi
 1. Ipi kati ya hizi ni faida ya misitu?
 1. Kutupatia madini
 2. Kutupatia mbao
 3. Kutupatia nafaka
 4. Kuikata
 1. Tunawezaje kuhifadhi misitu?
 1. Kwa kukata miti
 2. Kwa kuchoma misitu
 3. Kwa kupanda miti
 4. Kulima ndani ya misitu
 1. Ni kitendo gani kati ya hivi huchangia kuharibu rasilimali maji?
 1. Kukata miti kwenye vyanzo vya maji
 2. Kutochoma moto misitu
 3. Kutotiririsha maji machafu
 4. Kutunza miti
 1. Kujijali na kuwajali wenzako kunasaidia mwanafunzi:
 1. Kufanya mambo yanayokubalika katika jamii
 2. Kuogopwa
 3. Kutenda uovu
 4. Kuwa mkorofi
 1. Kugombana na wenzako mara kwa mara unapokuwa shuleni au nyumbani ni tabia:
 1. Isiyokubalika
 2. Inayoonesha kujali wenzako
 3. Ya upendo
 4. Ya unyenyekevu au kishujaa
 1. Matendo yafuatayo yanakuza uhusiano na watu wengine:
 1. Kushirikiana, kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu, kuheshimiana na kujiunga katika vikundi vya kusaidiana
 2. Kuonesha upendo, kuheshimiana, ugomvi na unafiki
 3. Kuwasaidia watu wenye mahitaji, kusema uongo, kushirikiana na kuheshimiana
 4. Kuwasaidia watu wote na kuwafanyia unafiki
 1. Moja ya faida za kujiunga na klabu za masomo shuleni ni:
 1. Kukuza uelewa na uongo
 2. Kukuza uelewa na kujiamini
 3. Kushindana kwa majibizano ya ujeuri
 4. Kuwa maarufu na kuvunja haki za binadamu
 1. Ni njia mojawapo ya kutomsaidia mwanafunzi mwenye matatizo:
 1. Kumshika mkono
 2. Kumkumbatia
 3. Kumshauri namna ya kutatua tatizo
 4. Kumtenga
 1. Namna bora ya kushirikiana na majirani zako unapokuwa nyumbani:
 1. Kuwakimbia wanapokuwa na shida
 2. Kutowapokea mizigo
 3. Kujumuika nao katika matukio ya shida na raha
 4. Kuwakwepa pale wanapoomba msaada
 1. Unapo shiriki katika shughuli za maendeleo  ya jamii unaleta;
 1. Mshikamano na uzalendo
 2. Shida  kwa wananchi
 3. Mtandao wa ombaomba
 4. umasikini
 1. Shughuli za kibinadamu ambazo huchangia uchafuzi wa  vyanzo vya maji ni kama vile:
 1. Kufua nguo, kupanda miti kuzunguka eneo la vyanzo vya  maji
 2. Kulima na kufua  nguo kando kando  ya mto
 3. Kutunza mazingira ya asili na kunywesha  mifugo
 4. Kupanda miti
 1. Mamlaka inayohusika na usimamizi na utunzaji mazingira nchini huitwa:
 1. Mamlaka ya mapato ya Tanzania
 2. Wizara ya afya
 3. Baraza la usimamizi wa mazingira la taifa
 4. Tume ya taifa ya mazingira
 1. Ni vyema tuka boresha njia za uchimbaji wa madini ilikusaidia:
 1. Uchimbaji wa madini kuwa endelevu na wenye ufanisi
 2. Kutopata fedha za kutosha
 3. Kukosa ajira kwa wingi
 4. Kutofuta umaskini
 1. Hali inayopunguza ukamilifu wa kitu inaitwa?
 1. Shida
 2. Kudorora
 3. Kupooza
 4. Kipato
 1. Kuangalia kitu kwa undani kisha kukadiria thamani yake au ubora wake huitwa
 1. Kuchunguza
 2. Mpangokazi
 3. Tathmini
 4. Morali
 1. Utaratibu wa kufanya kazi kwa hatua ili kufikia lengo lililokusudiwa ni;
 1. Ratiba
 2. Bajeti
 3. Mpangokazi
 4. Kipaumbele
 1. Faida ya kutathmini kwa mtoto ni;
 1. Kujiamini
 2. Kuacha uvivu
 3. Kudekezwa
 4. Kutofanya kazi
 1. Tathmini shuleni inapaswa kuwa;
 1. Kazi za darasani tu
 2. Kazi za darasani na nje ya darasa
 3. Kazi za viwanjani
 4. Katika mitihani tu

 

Katika swali la 41-45, andika jibu sahihi.

41.  Taja madhara manne ya kutohifadhi taka kwa usahihi

42.  Orodhesha dalili tatu za  balehe kwa mvulana na kwa msichana

43.  Andika sababu tatu za kufanya usafi wa sare za shule

44.  Taja mambo matatu ya kuzingatia wakati wa kufua sare za shule.

45.  Taja aina kuu mbili za taka

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZURAIA STANDARD FIVE EXAM SERIES 42

OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MITIHANI YA KUJIPIMA MSINGI

MTIHANI WA NUSU MUHULA WA KWANZA -MACHI 2021

URAIA NA MAADILI – DARASA LA TANO

FOMATI MPYA

MUDA1:30 MASAA MACHI 2021

JINA …………………………...SHULE ………………………...

MAELEZO

 1. Mtihani huu una sehemu Mbili A na B na jumla ya maswali matano
 2. Sehemu ya A ina alama 40 na sehemu B ina alama 10
 3. Jibu maswali yote kulingana na maelezo ya kila swali
 4. Mtihani wote una alama 50

SEHEMU A. CHAGUA JIBU SAHIHI KATI YA CHAGUZI ULIZOPEWA

 1. Tunapaswa kuonesha upendo kwa watu
 1. Wenye mahitaji maalum
 2. Ndugu wa karibu
 3. Watu wanotupenda
 4. Watu wote bila ubaguzi.
 1. Wafuatao wana mahitaji maalum isipokuwa:
 1. Wazee
 2. Watoto
 3. Watu wenye ulemavu wa akili
 4. Yatima na maskini.
 1. Tofauti gani sio ya kimaumbile kati ya mwanaume na mwanamke?
 1. Kupata hedhi
 2. Kupata mimba
 3. Uwezo wa kuzaa
 4. Kunyonyesha
 1. Tendo gani kati ya haya halionyeshi usawa wa kijinsia.
 1. Kutoa elimu sawa kwa mtoto wa kike na kiume
 2. Kutambua kuwa mwanaume na mwanamke wote ni binadamu
 3. Majukumu ya jikoni kuachiwa wasichana
 4. Kutobagua wasichana katika elimu
 1. Moja ya mabadiliko ya wasichana wanapo balehe ni
 1. Kuongezeka kwa kimo
 2. Kuonyesha heshima zaidi
 3. Kupata hedhi
 4. Kuwa na mpenzi wa jinsia tofauti.
 1. Wasichana wanaweza kujiepusha na mimba za mapema kwa;
 1. Kuwa na marafiki waaminifu
 2. Kwenda disko na jamaa zao
 3. Kupokea zawadi kutoka kwa wavulana
 4. Kuepuka matembezi yasiyo ya lazima usiku.
 1. Kwanini tunapaswa kuvaa mavazi yaliyo na staha?
 1. Yanaonyesha kujiheshimu
 2. Yanasaidia kuepuka magonjwa
 3. Ili tupendwe
 4. Ili tuvutie watu
 1. Kabila gani huvaa kaniki kwenye ngoma za asili?
 1. Maasai
 2. Wagogo
 3. Wanyasa
 4. Wasukuma
 1. Mabadiliko ya kimwili ya mtoto wa kiume na wa kike kuingia utu uzima huitwa
 1. Jinsia
 2. Kuvunja ungo
 3. Utu uzima
 4. Balehe
 1. Ipi sio staha katka jamii
 1. Kuvalia nguo inayokustiri
 2. Kucheza na wavulana sehemu za uchochoro
 3. Kuwasalimia watu kwa heshima
 4. Kupenda watu wote
 1. Maana ya utamaduni ni:-
 1. Ushabiki wa kitu au jambo unalolipenda
 2. Mtindo wa jumla wa maisha ya watu katika jamii au taifa Fulani
 3. Shughuli za asili zinazofanywa na watu
 4. Yote sahihi
 1. Baadhi ya alama zipatikanazo kwenye fedha ya Tanzania ni
 1. Twiga Tembo, Nembo ya taifa na sura ya rais
 2. Nembo , nyumbu na kifaru
 3. Mwenge , twiga na sokwe
 4. Mwenge wa uhuru
 1. Umuhimu wa bendera ya rais ni
 1. Kutembelea katika ziara mbalimbali tu
 2. Kuonyesha mamlaka ya rais
 3. Kuhamasisha mwenge wa uhuru
 4. Kuonyesha heshima kwa rais
 1. Chimbuko la sheria zote nchini Tanzania ni;
 1. Fedha ya Tanzania
 2. Katiba ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania.
 3. Vyama vya siasa
 4. Bunge
 1. Rangi ya bluu iliyopo katika bendera ya taifa uwakilisha;
 1. Watanzania
 2. Madini
 3. Maji ambayo ni mito, maziwa na bahari nchini Tanzania
 4. Uoto wa asili
 1. Alama ambayo hutumika kuonyesha umiliki wa mali na nyaraka za serikali tu ni;
 1. Picha ya makamu wa rais
 2. Bendera ya taifa
 3. Nembo ya Taifa
 4. Ndege ya Taifa
 1. Ni ishara gani inayoonyesha kwamba taifa limepatwa na msibu mkubwa?
 1. Bendera zote kupepea nusu mlingoti
 2. Bendera ya taifa kupepea nusu mlingoti
 3. Bendera ya taifa kutopandishwa kabisa siku ya tukio
 4. Watu kutokwenda kazini
 1. Ni siku ambazo viongozi hupata fursa kueleza mafanikio na changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi
 1. Siku za kukimbizwa mwenge wa uhuru tu
 2. Sikukuu ya mapinduzi ya Zanzibar tu
 3. Sikukuu za kitaifa
 4. Sikukuu ya krismas
 1. Zipi kati ya hizi ni mila zisizofaa katika jamii?
 1. Kufanya kazi kwa ushirikiano
 2. Kuwakeketa wasichana
 3. Kuhamasisha wanaume na wanawake kushirikiana kufanya kazi za nyumbani hili kujiongezea kipato.
 4. Kuoa jinsia moja
 1. Mifano ya vikundi vinavyoweza kuundwa shuleni ni kama;
 1. Skauti, klabu za mazingira, klabu ya TAKUKURU.
 2. Klabu za masomo
 3. Upatu, ushirikiano na vyama vya siasa
 4. Skauti, singeli na ngoma za asili.
 1. Msaidizi wa mkuu wa mkoa katika shughuli zake za utendaji ni nani?
 1. ofisa elimu mkoa
 2. katibu tawala wa mkoa
 3. mkuu wa idara ya utawala na utumishi mkoa
 4. ofisa afya wa mkoa
 1. Mwenyekiti wa halmashauri ngazi ya wilaya huongoza akina nani?
 1. wenyeviti wa mtaa
 2. makatibu tawala
 3. madiwani wa halmashauri
 4. mtendaji wa kata
 1. Katika ofisi ya kata, nani ni mtendaji mkuu?
 1. Diwani
 2. Ofisa mtendaji wa kata
 3. Ofisa mazingira wa kata
 4. Ofisa maendeleo wa kata
 1. Wakuu wa idara katika halmashauri za wilaya huwajibika kwa nani?
 1. mkurugenzi wa halmashauri
 2. mkuu wa wilaya
 3. mkuu wa mkoa
 4. ofisa tawala wa wilaya
 1. Mkurugenzi wa halmashauri anapatikanaje?
 1. kwa kupigiwa kura na madiwani
 2. kwa kuajiriwa na menejimenti ya utumishi wa umma
 3. kwa kuteuliwa na rais
 4. kwa kupigiwa kura na wananchi katika halmashauri inayohusika
 1. Katibu wa vikao vya baraza la madiwani ni nani?
 1. Mwenyekiti wa Halmashauri
 2. Diwani wa viti maalum
 3. Katibu tawala
 4. Mkurugenzi wa Halmashauri.
 1. Anayesimamia manunuzi yote yanayofanywa na ofisi ya mkuu wa mkoa ni;
 1. Katibu tawala mkoa
 2. Ofisa ugavi mkuu
 3. Mganga mfawidhi
 4. Mkaguzi wa ndani
 1. Kuna aina ngapi za uongozi katika kata?
 1. 3
 2. 5
 3. 4
 4. 2
 1. Lugha inayowaunganisha watanzania wote ni?
 1. Kihehe
 2. Kiswahili
 3. Kisukuma
 4. Kiingereza
 1. Ufundi wa kuwasilisha hisia na mawazo yaliyomo katika fikra huitwa:
 1. Mila
 2. Desturi
 3. Sanaa
 4. Utamaduni.
 1. Asili, mila, jadi Imani na desturi za jamii Fulani huitwa?
 1. Utamaduni
 2. Desturi
 3. Sanaa
 4. Mila
 1. Jambo la kawaida linalotendwa kila siku na jamii huitwa?
 1. Lugha
 2. Sanaa
 3. Desturi
 4. Mila
 1. Wareno walifika pwani ya Africa Mashariki mwaka?
 1. 1540
 2. 1498
 3. 1497
 4. 1690
 1. Lengo la waarab wa Omani kuja pwani ya afrika ilikuwa
 1. Kilimo
 2. Uvuvi
 3. Biashara
 4. Upagazi.
 1. Mreno wa kwanza kufika katika pwani ya Afrika mashariki alijulikana kama
 1. William Mackinnon
 2. Charles Stokes
 3. Vasco Dagama
 4. Karl Peters
 1. Wareno walifika katika Mji wa kilwa mnamo karne ya
 1. 15
 2. 16
 3. 19
 4. 18
 1. Nini maana ya uhusiano?
 1. Hali ya watu wawili na Zaidi wenye malengo ya Pamoja
 2. Hali ya kugombana baina ya mt una mtu
 3. Hali ya kufanya kazi peke yako
 4. Mshikamano
 1. Alikua kiongozi wa kabila la kizigua Tanga
 1. Mangi meli
 2. Isike
 3. Bwana Heri
 4. Mkwawa
 1. Kiongozi wa Kichaga aliyepatikana Kibosho Kilimanjaro
 1. Mirambo
 2. Mangi Sina
 3. Mangi Meli
 4. Abushiri
 1. Ni tabia gani kati ya hizi haziharibu Mazingira?
 1. Kukata miti
 2. Kufuga Wanyama wengi
 3. Kupanda miti
 4. Kulima sehemu za milima

SEHEMU B.

Jibu maswali yafuatayo kwa ufasaha.

Tazama picha ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata

 1. Kitendo hiki kinaitwaje
 2. Je unadhani kitendo hiki ni sahii
 3. Taja njia za kutunza mazingira
 4. Kwanini watu uharibu mazingira?
 5. Taja madhara yatokanayo na uharibifu wa mazingira.

LEARNINGHUBTZ.CO.TZURAIA STANDARD FIVE EXAM SERIES 30

OFISI YA RAISI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA KUJIPIMA DARASA LA TANO

APRIL-2020    MUDA:SAA 2:00

URAIA NA MAADILI

MAELEZO KWA MTAHINIWA

 1. MTIHANI HUU UNAMASWALI JUMLA YA 50
 2. JIBU MASWALI YOTE
 3. ANDIKA MAJIBU KWA HERUFI KUBWA
 4. KAZI YAKO IWE SAFI.

1. SEHEMU YA A.

 1. Ni ishara gani inayoonesha kwamba taifa limepatwa na msiba mkubwa?
 1. Bendera zote kupepea nusu mlingoti
 2. Bendera ya taifa kupepea nusu mlingoti
 3. Bendera ya taifa kutopandishwa kabisa siku ya tukio
 4. Wananchi  kuto toka nje
 5. Wananchi kuomboleza
 1. Umuhimu wa bendera ya rais ni:
 1. Kutembelea katika ziara mbalimbali tu
 2. Kuonesha mamlaka ya rais
 3. Kuhamasisha mwenge wa uhuru
 4. Inaonyesha umoja
 5. Kumtambulisha rais
 1. Rangi  ya bluu iliyokatika bendera ya Tanzania huwakilisha
 1. Watanzania
 2. Madini
 3. Maji
 4. Mito
 5. Damu iliyomwagwa  kwa kupigania uhuru

       4.   Mwenge wa uhuru uliwashwa kwa mara ya kwanza lini?

 1. 9/12/1962
 2. 9/12/1961
 3. 26/4/1964
 4. 24/04/1999
 5. 12/12/1961

5.    Katibu kata anachaguliwa na:

 1.  Wanachama wa chama tawala
 2.   Mkutano mkuu wa kata
 3.  Wananchi wa kata ile
 4.   Mkutano wa kijiji wa mwaka 
 5.  Kamati ya kijiji

6.  Kamati ya maendeleo ya kata inaundwa na wafuatao isipokuwa:

 1.   Katibu kata
 2.   Afisa mtendaji wa Kata
 3.   Katibu Kata wa viti maalumu
 4.   Afisa mtendaji wa Mkoa
 5.   Kamanda wa Polisi wa Mkoa

7.  Kauli mbiu ya Tanzania iliyopo kwenye nembo ya taifa ni:

 1.  uhuru na maendeleo
 2.  uhuru na kazi
 3. uhuru na umoja 
 4.  uhuru na amani
 5. umoja na amani

8.   Ushiriki wa wanafunzi kwenye kuchagua viongozi wao shuleni huimarisha:

 1.  uongozi wa kikatiba shuleni
 2.  kiongozi mkuu wa uongozi wa shule
 3.  ukiritimba shuleni
 4.  usalama shuleni
 5.  uongozi bora shuleni

9.  Kiongozi mkuu wa shule ni:

 1. mwalimu mkuu msaidizi
 2. mwalimu wa taaluma
 3. kiranja mkuu
 4. mwalimu mkuu
 5. mwalimu wa nidhamu 

10. Nini faida ya mgawanyo wa kazi katika familia?

 1. Hudhoofisha familia
 2. Huchochea utengano
 3. Huleta udikteta
 4. Huleta maendeleo
 5. Huleta mitafaruku

11.  Kazi ya kamati ya shule ni:

 1. Kusimamia maendeleo ya taaluma
 2. Kutoa ushauri juu ya maambukizi ya UKIMWI
 3. Kuidhinisha uteuzi wa waalimu 
 4. Kusimamia nidhamu ya waalimu
 5. Kusimamia ujenzi na maendeleo ya shule.

12.  Ngaoya taifa inawakilisha:

 1. umoja, uhuru, uwezo na mamlaka ya taifa
 2. uhuru, umoja na rasilimali za taifa
 3. uwezo, uhuru, uoto wa asili na mamlaka ya taifa
 4. uhuru, umoja na mamlaka ya taifa 
 5. uhuru na umoja

13. Chanzo cha familia ni:

 1. ndugu na rafiki
 2. ukoo na kabila 
 3. baba na mama
 4. watoto
 5. wazee na vijana

14. Mwakilishi wa wananchi katika vikao vya Wilaya vya Serikali za Mitaa ni ....

 1.  Mkuu wa Wilaya.
 2.  Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji.  
 3. Afisa Mtendaji Kata.
 4. Mwenyekiti wa Wilaya wa Chama Tawala.
 5.  Diwani wa Kata.

15. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya au Manispaa huteuliwa na .. ...

 1.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 2. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
 3.  Baraza la Madiwani la Halmashuri au Manispaa husika. 
 4.  Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
 5.  Katibu Mkuu Kiongozi.

16. Ni wakati gani Bendera ya Taifa hupeperushwa nusu mlingoti? 

 1. Wakati wa ziara za viongozi wa mataifa mengine. 
 2.  Rais anapotangaza hali ya hatari.
 3.  Linapotokea janga la kitaifa au tukio la huzuni. 
 4.  Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa wa Taifa.
 5.  Rais anapokuwa nje ya nchi.

17. Ni wakati gani Bendera ya Taifa hupeperushwa nusu mlingoti? 

 1. Wakati wa ziara za viongozi wa mataifa mengine. 
 2.  Rais anapotangaza hali ya hatari.
 3.  Linapotokea janga la kitaifa au tukio la huzuni. 
 4.  Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa wa Taifa.
 5.  Rais anapokuwa nje ya nchi.

18. Lengo kuu Ia kuanzisha Serikali za Mitaa Tanzania ni

 1.  kuimarisha demokrasia     
 2.  kukusanya kodi ya maendeleo
 3.  kuimarisha polisi jamii        
 4.  kuboresha usafi wa miji 
 5.  kuongeza ajira

  19.  Faida ya ushirikiano kati ya shule na jumuiya inayozunguka shule ni pamoja na:

 1.  ulinzi na usalama wa shule kuimarika
 2.  ongezeko Ia idadi ya watoto wanaoandikishwa shule
 3.  nafasi za ajira kwa jamii inayozunguka shule kuongezeka 
 4.  shughuli za biashara kuzunguka eneo Ia shule kuongezeka
 5.  walimu wengi kupata nyumba za kupanga jirani na shule

20. Jukumu la ulinzi katika familia ni la nani?

 1.  Baba na watoto.          
 2. Baba, jamaa na marafiki.
 3.  Watoto, mama na jirani              
 4.  Kila mtu katika familia 
 5.  Watoto, jamaa na marafiki

SEHEMU B. ANDIKA NDIYO AU HAPANA.

 1.  Upendo halisi ni kujipenda mwenyewe……………… 
 2. Majukumu ya kijinsi hubadilika…………… 
 3. Mavazi mengine huvaliwa na wanawake na wanaume………… 
 4. Vazi la lubega halivaliwi na wa masai……………… 
 5. Mwenyekiti wa baraza la madiwani na kamati ya fedha a mipango ni mkurugenzi wa halmashauri………… 
 6. Jukumu la ofisa elimu ni kupambana na magonjwa mfano ukimwi…………… …………………..
 7. Mkuu wa mkoa uteuliwa na rais…………………… 
 8. Mkuu wa wilaya uapishwa na mkuu wa mkoa…………………………………………………………………..
 9. Katibu tawla wa wilaya ni mshauri mkuu  wa mkuu wa wilaya………………… 
 10. Ofisa tarafa anajukumu la kusimamia maofisa watendaji wa kata, vijiji, na vitongoji………… ………….

SEHEMU C.

ORODHA A

ORODHA B

 1. Mwaka mpya
 2. Kumbukumbu ya siku ya mapinduzi ya Zanzibar
 3. Kumbukumbu ya kifo cha rais wa kwanza wa Zanzibar( sheik abeid amani karume)
 4. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
 5. Siku ya wafanyakazi duniani
 6. Maonyesho ya biashara ya kimataifa
 7. Siku ya wakulima Tanzania
 8. Kumbukumbu ya kifo cha rais wa kwanza wa Tanzania.
 9. Uhuru wa Tanganyika
 10. Ajali ya MV Bukoba
 1. 21/05/1996
 2. 1/01/
 3. 1/5/
 4. 8//08/
 5. 9/12/
 6. 12/01/
 7. 26/04/
 8. 7/04/
 9. 14/10/1999
 10. 7/07

SEHEMU D.

Jaza nafasi zifuaatazo..

 1. Mnyama wa taifa ni………………… …………………..
 2. Bendera ya taifa ina rangi ngapi?...................................... 
 3. Upande wa kaskazini Tanzania inapakana na nch gani………………… 
 4. Kiongozi mkuu wa kata anaitwa nani?......................... 
 5. Afisa mtendaji wa kata anafanya kazi chini ya kiongozi gani?...................... 
 6. Kiongozi wa kisiasa katika kata?.............................. 
 7. Taja kazi ya ofisa elimu kata…………………… ……
 8. Ni nani katibu wa vikao vya baraza la madiwani ?....................... 
 9.  Nani anaapisha mkuu wa mkoa?................................... 
 10. Nani anamteuwa mkuu wa mkoa?............................

LEARNINGHUBTZ.CO.TZURAIA STANDARD FIVE EXAM SERIES 5

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256