?>
OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA-MEI-2024
SOMO: KISWAHILI DARASA: V
MAELEKEZO:
SEHEMU A:
IMLA
1. Sikiliza kwa makini kifungu cha habari utakacho somewa na Mwalimu kisha jibu swali (i) hadi (v)
(i) Ni wapi mafuriko makubwa yamepiga?
(ii) Watu wangapi wamelazimika kuhama makazi yao kutokana na mafuriko?
(iii) Ni nini kilichofanikiwa kuharibiwa na mafuriko?
(iv) Nini kinachosababisha hali ya mafuriko kuwa mbaya zaidi?
(v) Mamlaka zinaonya nini kuhusu hatari ya mafuriko?
SEHEMU B:
SARUFI, MISAMIATI NA MATUMIZI YA LUGHA
2. Chagua herufi ya jibu sahihi kisha jaza katika mabano.
i. Tulipokuwa tukijisomea aliniambia nikamilishe sentensi hii” babu na bibi kumwona shangazi kesho. A. Walikwenda B. Na C. Huenda D. Watakwenda
ii. Mwalimu aliuliza neno lipi linakamilisha sentensi hii kwa usahihi? Baba yangu alikula wali _____kijiko A. Na B. Kwa C. Mwa D. Pamoja
iii. Dereva ni kwa mwendesha vyombo vya nchi kavu rubani ni kwa mwendesha ndege. Je, nahodha ni kwa A. Manju B. Vyombo vya majini C. Ni kwa mabaharia D. Vyombo vya angani
iv. Upi ni ukanushi sahihi wa neno “Ataimba” A. Huimba B. Hataimba C. Ataimba D. Hajaimba
v. Rafiki yangu alinionesha zeruzeru tulipokuwa kanisani. Kisha nilimuuliza neno lipi ni kisawe cha zeruzeru? A. Chotara B. Suriama C. Albino D. Muakasti
vi. Mwalimu alisema yakinisha sentensi ifuatayo “Elimu haina mwisho” A. Elimu si mwisho C. Elimu ina mwisho B. Elimu inafika mwisho D. Elimu ni mwisho
vii. Nilipenda kujua kama unafahamu neno mchwa linaundwa na silabi zipi? A. M,ch,wa B. M,c,h,w,a C. M,chwa D. Mchwa
viii. Jamila anafanya kazi katika maktaba ya taifa. Je, Jamila ni nani? A. Mkutubi B. Maktabalisti C. Mfanyakazi D. Mnajimu
ix. Mzee Kalumanzila anatibu watu kwa kutumia mitishamba. Je, neno “Kalumanzila” lina silabi ngapi? A. Tatu B. Nne C. Tano D. Kumi na moja
x. Bibi yake Sampuluna ni mzee sana hawezi hata kulima shamba tena. Je, neno gani lina maana sawa na mwanamke mzee? A. Abu B. Shaibu C. Buda D. Ajuza
xi. Kitoto chake kinacheza mpira vizuri. Wingi wa neno lililopigiwa mstari ni upi? A. Mtoto B. Chitoto C. Vitoto D. Watoto
xii. Mtakapokuja kwenye mazishi msigombanie mali za watu. Neno lililopigiwa mstari lina silabi mwambatano ngapi? A. Mbili B. Tatu C. Moja D. Nne
xiii. Samaki mkunje angalli mbichi. Wingi wa sentensi hii ni upi? A. Samaki wakunje angali wabichi C. Masamaki yakunje yangali mabichi B. Samaki mkunje wabichi D. Samaki wabichi yakunjwe
xiv. Mjomba alipanda juu ya mnazi kuangua nazi. Je, mtu anayeangua nazi anaitwaje? A. Muanguaji B. Mkwezi C. Mgemaji D. Mkunazi
xv. Umoja wa sentensi hii ni upi? Wajuaji wale hawatafanikiwa A. Wajuaji hawa hawatafanikiwa C. Hatafanikiwa mjuaji B. Mjuaji huyu hatafanikiwa D. Mjuaji huyu atafanikiwa
SEHEMU C: METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
3. Jibu maswali yote kwa kuchagua jibu sahihi;
i. Wanafunzi wote wa darasa la nne tulikata shauri kusoma kwa bidi ili tufaulu mitihani yetu. Je, nahau kata shauri ina maana gani? A. Kubaliana B. Shirikiana C. Amua D. Kata tamaa
ii. Mwanaheri ni mtoto wa kwanza katika familia yao. Je, Mwanaheri hujulikana kama A. Kitinda mimba B. Kilembwe C. Mwanambee D. Mziwanda
iii. Mzee Umbe alirudi mapema nyumbani mara baada ya kumwaga unga kazini kwake. Je, nahau mwaga unga ina maana gani? A. Kuwahi kazini B. Kumaliza kazi mapema C. Kufukuzwa kazi D. Ajiriwa
iv. Lipi kati ya haya yafuatayo ni jibu la kitendawili hiki” Gari moshi relini? A. Treni B. Zipu C. Msitu D. Reli
v. Liwali amekonda sana lakini hana dawa. Je, jibu la kitendawili hiki ni lipi? A. Sisimizi B. Siafu C. Sindano D. Pini
vi. Mzee Jamali alisema loo! nalipa faini kosa lisijui. Ndipo tulipokumbuka jibu la kitendawili hiki ni A. Usingizi B. Kutereza C. Kujikwaa D. Kuanguka
vii. Tulipofika stesheni tulikuta treni la abiria likianza safari, ghafla rafiki yangu aliniambia gari moshi relini. Ndipo nilipojua anataka jibu la kitendawili hicho. A. Dereva B. Sisimizi C. Siafu D. Zipu
viii. Tulipofungwa karata na baba nililalamika sana ndipo mama aliposema “Asiyekubali kushindwa A. Hawezi B. Hathaminiki C. Hatashinda D. Si msindani
ix. Maige huuza bidha kwa bei ya rejareja kwa kuzunguka nazo mtaani. Je Maige ni nani? A. Dalali B. Machinga C. Muuzaji D. Mhandisi
x. Mama Jamila hapendi watoto wamwage chakula pindi wanapo shiba. Hupenda kuwaambia wakifunike na kukihifadhi kwa matumizi ya baadae. Je, ni methali gani itatumika kusisitiza maelezo hayo. A. Haba na haba hujaza kibaba C. Chovya chovya humaliza buyu la asali B. Chembe na chembe mkate hua D. Akiba haiozi
4. Tumia maneno yaliyopo kwenye mabano ili kujaza sehemu zilizoachwa wazi
Muda, Mvua, Mbayuwayu, Vitoweo, Hasira, Kunepa, Ujumbe, Kiongozi, Kucheza, kumbukumbu
i. Alijiweka mbele kila wakati ili achaguliwe kuwa................................ wao.
ii. Tawi lilianza............................. baada ya kutua ndege wengi.
iii. Alipotuamuru tuondoke tulijawa na ...............................................
iv. Hatukuona ndege yoyote isipokuwa .............................................tu wakila kumbikumbi.
v. Tulipopata .....................................wa kuuguliwa kwake sote tulikwenda kumsalimia.
SEHEMU D: UTUNGAJI
5. Panga sentensi zifuatazo katika mtiririko maalumu kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E
i. Baada ya kusubiri kwa nusu saa basi liliwasili na nikapanda basi hilo kwenda Bunda.
ii. Abilia wote walishuka kwenye basi.
iii. Liliwasili mjini Mwanza, gari moshi lilisimama taratibu na kutangaza kuwa hapo ndipo mwisho wa basi.
iv. Nami nilishuka na kwenda moja kwa moja kwenye kituo cha basi.
v. Mimi na abiria wenzangu tulisafiri kwa Amani na kufika Bunda salama jioni.
SEHEMU E: UFAHAMU
6. Soma habari ifuatayo kwa usahihi kisha jibu maswali utakayoulizwa.
Hapo zamani za kale kulitokea mgogoro mkubwa sana kati ya ndege na wanyama. Juhudi za kumaliza mgogoro huu zilionekana kugonga mwamba na hatimaye vita ilianza. Wakati majeshi hayo mawili ya wanyama na ndege yakijiandaa kupigana, popo alisita kuchagua upande wa kujiunga na kivita. Jeshi la ndege lilifika nyumbani kwa popo na kumwambia. “Twende vitani ewe popo ndege mwezetu”. Popo alikataa na kusema “mimi ni mnyama na si ndege kama ninyi”. Baadaye jeshi la wanyama lilifika nyumbani kwa popo na kumwambia ni ndege na wala si mnyama kama ninyi”. Basi kukawa na ngurumo za kutisha za wanyama shupavu kama vile simba, duma na tembo, na ndege shupavu kama vile tai na mbuni. Majike wenye ndama na majike wenye makinda walihisi kiama chao kimefika.
Kwa bahati nzuri sana, katika dakika za mwisho kuelekea vita, muafaka ulifikiwa kati ya pande zote mbili na vita ikaepukikwa. Kukawa na Amani badala ya mapigano. Makundi yote mawili yakawa na shamrashamra za kusheherekea kuepukana na mgogoro. Kuona hivyo, popo naye alitamani kuwa sehemu ya shamrashamra hizo. Alikwenda kwa ndege akitaka kujiunga nao lakini ndege walimfukuza. Baadaye akaenda kwenye kundi la wanyama nao walimfukuza. Popo akabaki kuwa njia panda kwani hakuruhusiwa kujiunga na kundi la ndege au kundi la wanyama.
MASWALI
i. Mwandishi ameeleza katika habari kuwa kulikuwa na mgogoro. Je, mgogoro uliotokea hapo zamani uliwahusu kina nani?
ii. Mwandishi amesema juhudi zote ziligonga mwamba. Je, maneno yaliyopigiwa mstari yana maanisha nini?
iii. Katika hadithi uliyoisoma wametumia neno “kiama” Je neno kiama lina maana gani?
iv. Kutokana na hadithi uliyosoma nani alibaki njia panda?
v. Kutokana na habari uliyosoma hadithi hii inahusu nini?
Kifungu cha habari
Mafuriko makubwa yamepiga mkoa wa Pwani, yakiacha maafa makubwa kwa nyuma. Maelfu ya watu wamelazimika kuhama makazi yao, huku nyumba na miundombinu mingi ikiharibiwa. Mvua kubwa inayoendelea kunyesha inazidisha hali hiyo, huku mamlaka zikiwaonya wakazi kuhusu hatari ya mafuriko zaidi.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FIVE EXAM SERIES 102
MTIHANI WA UMAHIRI KWA SHULE ZA MSINGI
MTIHANI WA MWISHO MUHULA MEI , 2024
SOMO : KISWAHILI DARASA : P 5
JINA: ___________________________ TAREHE: __________
SEHEMU A: UFAHAMU WA KUSIKILIZA,SARUFI,LUGHA YA KIFASIHI,UTUNGAJI
a) wanaume b) wasichana c) watoto
d) wafungwa e) wachezaji [ ]
a) mafuta b) matope c) wadudu
d) maji e) uvundo [ ]
a) sura zao b) umri wao c) wanakotoka
d) nyumbani kwao e) jinsia yao [ ]
a) mama yao b) mwalimu c) wapita njia
d) Bibi Huruma e) mama Mkosi [ ]
a) walikataa b) walitoka wakavaa nguo zao c) walipiga kelele
d) walishangilia e) walimtukana yule Bibi [ ]
SARUFI NA MSAMIATI
a) kujionesha b) kujiringa c) kujificha d) kujiumiza
e) kujifanya wajua [ ]
a) anatembea haraka b) anatembea kwa madaha [ ]
c) anatembea kwa vichekesho d) anarukaruka e) anatembea kwa shida
a) Mariamu si mrembo b) Mariamu ni mbaya c) Mariamu anarembua
d) Mariamu harembui e) Mariamu hawezi kuwa mrembo [ ]
a) Mariamu hapandi mlimani b) Mariamu anateremka bondeni
c) Mariamu anaogopa mlimani d) Mariamu hateremki bondeni
e) Mariamu anapanda bondeni [ ]
a) u b) a c) ni d) wa e) tu [ ]
a) uliopita b) ujao c) uliopo d) mtimilifu e) wa mazoea [ ]
a) jiwe b) chuma c) mtego d) kamba e) bunduki
a) Fundi cherehani b) Fundi seremala c) Dobi
d) Fundi Mwashi e) Tabibu [ ]
a) Mwalimu b) Tabibu c) Mkufunzi d) Rubani e) Nahodha
a) msemaji b) mmbea c) mzushi d) mwongeaji e) Mpiga stori
a) jasiri b) mvivu c) mchapakazi d) mroho e) mchoyo
a) yatima b) mpweke c) mwenye mkosi [ ]
d) mkosefu e) Mwangaji
a) vinyweleo b) nywele c) kanywele d) unywele e) kanyweleo
a) wali b) ndizi c) sufuria d) ugali e) karanga
a) viumbe b) viumbe hai c) wanyama
d) mimea e) wanyama pori [ ]
a) na b) ta c) li d) me e) hu [ ]
a) nne b) tatu c)tano d) saba e) moja
a) ta b) hu c) wa d) a e) fa [ ]
a) wimbo b) nahau c) methali d) stori e) hadithi
a) Hadithi! Njoo, uongo njoo, utamu kolea
b) Hadithi Njoo, ukweli njoo, utamu kolea
c) Hadithi Kwaheri, uongo njoo, utamu baadaye
d) Hadithi karibu, ukweli karibu , utamu ni sasa
e) Hadithi Njoo, uongo na ukweli simulia mpaka kuchwee
METHALI, NAHAU , MISEMO NA VITENDAWILI
a) ni kubwa b) halikuli likakwisha c) hukuchekea
d) usipende kukutana nalo e) usilitanie [ ]
a) hulia juani b) hulia kivulini c) ni mchoyo d) ni mvumilivu
e) hulia popote [ ]
a) kibaya chafuata b) kibaya chajitembeza c) kibaya ki nyuma yake
d) kwa haraka chanunuliwa e) wakati mwingine chakosa soko
a) ni mwongo b) ni mwizi c) ni mchoyo d) ni mlemavu
e) anachekesha
a) gari b) meza c) yai d) mwavuli e) chupa
31.Alikuwa popo katika uchaguzi mkuu wa darasa kuwa popo ina maana gani
a).kuwa mgonjwa b) kupenda kuning’inia c) Kuwa kigeugeu d) Kuwa mbishi e) mwongo
32.Tegua kitendawili kifuatacho”Nyumbani kwangu kuna jinni mnywa maji”_
a).Kibatari b) kikombe c) mtungi d) kinywa e) tochi
SOMA SHAIRI HILI KISHA JIBU MASWALI
Elimu pana ajabu, huwezi yote kujua,
Utaipata aibu, ukijifanya wajua,
Daima tafuta jibu, ya lile usolijua,
Elimu pana ajabu, huwezi yote kujua.
MASWALI
a) afya b) uvivu c) elimu d) nidhamu e) utu
a) nne b)) mbili c) ubeti mmoja d) nane e) tatu
a) jawabu b) ajabu c) ugumu d) mazuri e) hatari
:UTUNGAJI
Panga sentensi hizi kwa mtiririko mzuri kwa (A, B, C, D, E)
36 | 37 | 38 | 39 | 40 |
|
|
|
|
|
SEHEMU B : UFAHAMU
Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata
Mimi ni simba , mnyama anayesifika sana, ninayo ngurumoya kutisha, nikiwa jike sina nywele ndefu , nikiwa dume nywele zangu ndefu. Mimi ni mfalme wa porini
Mimi ni mbwa, ninasifika kwa ukali, ninapenda kuishi na binadamu, Mimi ni mlinzi namwindaji mashuhuri. Ninamlinda binadamu na mali zake.
Mimi ni kondoo nasifika kwa upole wangu. Huishi na binadamu, Nywele zangu ni sufu.
Mimi ni ng’ombe chakula changu ni nyasi, ninapokula hucheua, huishi na binadamu, humpatia maziwa na mbolea.
Mimi ni twiga, mnyama aishiye porini, ni mrefu sana kuliko wanyama wote porini. Pia mimi ni alama ya nchi ya Tanzania.
MASWALI
DARASA LA 5 UFAHAMU WA KUSILIKIZA
Watoto walikuwa wakioga na kuogelea kwenye dimbwi karibu na nyumbani kwao. Walizama na kuibuka kwenye yale maji machafu. Miili yao ilijaa matope. Haikuwa rahisi kutambua sura zao. Bibi Huruma alipokuwa anapita pale akawaona wale watoto "Loo ! nyie watoto mtaleta balaa! Maji hayo yana wadudu wengi, Tokeni haraka"Wale watoto walitoka wakavaa nguo zao.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FIVE EXAM SERIES 97
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA
DARASA LA TANO-NOVEMBA-2023
KISWAHILI
SEHEMU A (ALAMA 5)
Ufahamu wa kusikiliza
Jongoo na Nyoka
Hapo zamani za kale, Jongoo na Nyoka walikuwa marafiki. Jongoo katika maumbile yake alijaliwa kuwa na macho lakini hakuwa na miguu. Tofauti na Jongoo. Nyoka alijaliwa kuwa na miguu lakini hakuwa na macho. Marafiki hawa walifanya kazi bega kwa bega. Jongoo na nyoka walikuwa na rafiki yao aliyeitwa Mwewe. Siku moja Jongoo na Nyoka walienda kumtembelea Mwewe. Nyoka alitembea polepole japokua alikuwa na miguu mingi. Alifanya hivyo kwa kuogopa kujikwaa. Jongoo alikuwa anatembea harakaharaka kwa sababu alikuwa anaona kila kitu.
MASWALI
SEHEMU B
SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA
Chagua jibu sahihi
SEHEMU C
Lugha ya kifasihi, methali, Nahau na vitendawili
SEHEMU D: Utungaji
Sentensi zifuatazo zimeandikwa bila kufuata mtiririko sahihi. Zipange kwa kuzipa A, B, C, D na E
SEHEMU E: Ufahamu
Soma kifungu cha habari kisha jibu maswali
Sheku ni mtoto wa pili katika familia ya Bwana Shenya na Bibi Pachu kwa Bahati mbaya, wazazi wake waliaga dunia akiwa na umri wa mwaka mmoja. ALipoanza masomo yake ya sekondari, mjomba wake aliamua kumueleza jambo alilokuwa nalo kwa kipindi kirefu. Jambo hilo lilihusu kifo cha wazazi wake. Mjomba wake Sheku alimueleza jambo hilo kwa upole sana. Alimwambia, Sheku mwanangu, wazazi wako walipata ajali ya gari mwaka 1990 na kufariki papo hapo . nimekulea tangu ukiwa na umri wa mwaka mmoja hadi leo. Nilishindwa kukuambia jambo hili kwa sababu ulikuwa bado mdogo. Hata hivyo nitaendelea kukulea na kukusomesha mwanangu.
MASWALI
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FIVE EXAM SERIES 82
OFISI YA RAIS, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA NUSU MUHULA WA PILI
DARASA LA TANO
AGOSTI-2023
Sikiliza kwa makini ufahamu unaosomwa na mwalimu kisha ujibu maswali yaani swali la 1 hadi 5
(a) ninyi (b) wewe (c) sisi (d) wao (e) wale
11.“ Mimi nitachelewa sana kuja kwenu”, alisema mwalimu wa darasa. Sentensi hii ipo katika
kauli gani?
a) tamaa (b) shauku (c) mwisho (d) mwanzo (e) mzizi [ ]
a) Umehahirishwa (b) umewahirishwa (c) umeahirishwa (d) umeridhishwa (e) umeairishwa [ ]
a) nane (b) nne (c) sita (d)mbili (e) zote [ ]
a) ungelipata (b) ungapata (c)ungalipata (d) usingelipata (e) ungepata [ ]
a) kilema (b) mwendawazimu (c) kikongwe (d) kibogoyo (e) ajuza [ ]
(a) –na- (b) –ta- (c) –me- (d) –li- (e) hu- [ ]
a) ingia (b)wanaingia (c)wote (d) ukumbini (e) hawa [ ]
a) mikia za ng‟ombe zimekatika (b) mikia ya ng‟ombe imekatika [ ]
(c) mimikia ya ming‟ombe imekatika (d) limkia la ng‟ombe limeakatika
(e) mkia za ng‟ombe imekatika
a) Nomino (b) kiwakilishi (c) kihisihi (d)kitenzi (e) kivumishi [ ]
a) na (b) wa (c) kwa (d) ya (e) pamoja na [ ]
a) bahari (b) jua (c) redio (d) mwezi (e) usingizi [ ]
a) hakuna masika (b) penye miti (c) penye upele (d) penye wengi (e) palipo na mvua [ ]
a) anapishana (b) anaridhi (c)anafanana (d) anasawidi (e) anarithi [ ]
a) upepo (b) mkufu (c) mwiko (d) kinyonga (e)mvua [ ]
a) Umoja (b) kutumia mali ovyo (c) kuweka akiba kidogo kidogo (d) utengano (e) kutotosheka [ ]
a) kufanya uzinzi (b) kuiba nyakati za usiku (c) kutoa rushwa [ ]
(d) kufanya mipango ya siri (e) kula kiapo
a) hakosi kuliwa (b) hupotea njia (c) hufungwa kamba mguuni [ ]
(d) hakosi kamba mguuni (e) huliwa na wenyeji
a) Ajihami bila silaha (b hutembea haraka kila siku (c) hutembea na nyumba mgongoni [ ]
(d) popoo mbili zavuka macho (e) mama hachoki kunibeba
a) ahadi ni deni (b) mganga hajigangi (c) asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu
(d) mgaagaa na upwa hali wali mkavu (e) pruuuuu mpaka maka [ ]
a) Fedha lukuki (b) fedha nyingi (c) fedha zote (d) sarafu nyingi e) fedha chache [ ]
(a) Omboleza (b) Furahi (c) fikiria (d) fanya kazi (e) bembeleza [ ]
Panga sehemu za barua zifuatazo kwa mtiririko unaofaa kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E
36. YAH: MAOMBI YA KAZI YA UANDISHI WA MITIHANI …………………………………………..
37. Mkurugenzi , kampuni ya BRAINMASTER, S.L.P 280 MANZESE ………..
38. Wako mtiifu SUYURISH RAMADHANI MCHOKAA…………………………..
39. S.L.P 4302 DAR ES SALAAM ……………………………………………………
40. Tarehe 08/10/2010 ……………………………………………………..
SEHEMU C: USHAIRI:
Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata
Maisha yaliyo bora, maneno yatamkika,
Walitaka zetu kura, kapuni wakatuweka,
Twaishi kama chokora, na siku zinakatika,
Hakuna maisha bora, haya ni bora maisha.
Tanzania nchi yangu, yenye wingi wa maneno,
Amani hili ni jungu, latukwaza si mfano,
Mikononi nina pingu,yako’pi yenu maono,
Hakuna maisha bora, haya ni bora maisha.
MASWALI
41. Shairi hili linazungumzia nini? ____________________________________________
42. Kila mshororo katika ubeti wa shairi hili una mizani ngapi? ___________________________
43. Taja Vina vya kati katika ubeti wa pili ? ________________________________________
44. Ipi maana ya nahau kuweka kapuni kama ilivyotumika katika shairi hapo juu ?______________
_______________________________________________________________________
45. Mstari uliokolezwa wino katika kila ubeti wa shairi hili hujulikana kama: _________________
__________________________________________________________________________________
UFAHAMU WA KUSIKILIZA V
Tangu kugunduliwa kwa ugonjwa wa Upungufu wa Kinga Mwilini miaka 27 iliyopita, ugonjwa ambao dalili zake ni nyingi, mfano kupungua uzito , kukohoa, kuhara, kukonda, kukohoa kwa muda mrefu na homa za mara kwa mara. Janga hili limeua watu wengi wakiwemo matajiri, wataalamu, wasomi na wasiosoma, akina yakhe na watoto.
Janga hili la kitaifa na kimataifa limefanya wanasayansi wasugue vichwa kutafuta dawa bila mafanikio, serikali pamoja na mashirika ya kimataifa yametumia rupia nyingi kutoa elimu ya ugonjwa huu na madhara yake kwa jamii hayajatatuliwa. Ama kweli la kuvunda, halina ubani.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FIVE EXAM SERIES 78
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MITIHANI WA MWISHO WA MWAKA
KISWAHILI
DARASA LA TANO
2022
JIBU MASWALI YOTE
SEHEMU A
Sikiliza kwa makini habari inayosomwa na msimamizi kisha jibu maswali 1 – 5 kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.
Mkutano ulianza asubuhi sana. Wajumbe walipewa habari mbalimbali. Hadi saa sita mchana kikao kilikuwa kimeisha tayari. Mwenyekiti aliahirisha kikao hicho hadi wakati mwingine. Wajumbe wote walifurahi sana. |
Chagua herufi ya jibu sahihi na kisha andika karatasi ya kujibia.
Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali ya namba 31 – 35
Elimu pana ajabu, huwezi yote kujua
Wala usistaajabu, mtu kukuelezea
Kuwa kupata aibu, mkate hutoujua
Elimu pana ajabu huwezi yote kujua
Ukitaka kuamini, haya ninayokueleza
Waliosoma vyuoni, hawachoki kuuliza
Huyu bora kiwandani, ofisini hataweza
Elimu pana ajabu, huwezi yote kujua
Rubani hana dosari, kushindwa kuongoza meli
Somea udaktari, wa kupasua misuli,
Figo zitakuadhiri, japo unayo akili,
Elimu pana ajabu, huwezi yote kujua
Elimu pana ajabu, huwezi yote kujua
Utaipata aibu, ukijifanya wajua,
Daima tafuta jibu, ya lile usolijua
Elimu pana ajabu, huwezi yote kujua
SEHEMU B
UTUNGAJI
Panga sentensi hizi ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E ili ujibu maswali 36 – 40
SEHEMU C
UFAHAMU
Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali 41 – 45 kwa kuandika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasi yako ya kujibia.
Walanguzi ni watu wanaonunua vitu au mavuno kwa bei nafuu na kuyauza kwa bei ya juu ili kupata faida kubwa iwezekanavyo. Watu hawa hufurahia wazalishaji au wakulima wanapokosa soko la mazo.
Mkulima anaweza kukingwa kwa kuthibitishiwa hakika ya soko la mazo yake. Ndiyo maana serikali imeanzisha na kuhimiza maendeleo ya vyama vya ushirika. Kama vyama vya ushirika vingestawi, wakulima na wazalishaji wengi wangeuza mazao yao kwenye vyama hivyo. Hapo ndipo mzalishaji angepata haki kwani angekuwa na sauti ya kupanga malengo ya uzalishaji, gharama zake na hata bei ya mazao hayo.
Wazalishaji wangeweza kuuza mazao yao kwenye vyama vy msingi vya ushirika. Chama cha Msingi cha Ushirika ni wakala wa chama Kikuu cha Ushirika. Chama kikuu cha Ushirika hukilipa Chama cha Msingi cha ushirika kwa vile chama hicho hufanya kazi nyingi kwa niaba ya Chama Kikuu, kama vile kusafirisha mazao na hata kuyahifahsi
Fdha zinazopatikana kutokana na ushuru wa aina hii huingia katika mfuko ya Chama cha Msingi cha Ushirika. Wanaushirika wana fursa ya kupanga matumizi na mapato ya chama chao kwa kadiri ya mahitaji yao.
MASWALI
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FIVE EXAM SERIES 63
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA
MTIHANI WA NUSU MUHULA WA KWANZA DARASA LA TANO
KISWAHILI
MUDA:1: 30
JINA_____________________________________SHULE_________________________
MAELEKEZO:
SEHEMU A: FASIHI NA MSAMIATI
Sikiliza kwa makini kifungu cha habari utakachosomewa kisha jibu swali la 1 – 5
1.Zamani watu waliamini kuwa dunia ni tambarareni kama
(a)Ardhi (b)Meza (c)Ukuta (d)sakafu
2.Wataalamu wa mambo ya anga walithibitisha kuwa dunia ni kama
(a)tufe (b)yai (c)mzunguko (d)chungwa
3.Watu wengi waliamini kuwa mtu angeweza kwenda hadi angeangukia kwenye (a)tufe (b)uso wa dunia (c)shimo kubwa (d)mbingu
4.Wengine waliamini kuwa kama wangeendelea kwenda mwishowe ungegusa (a)tufe (b)mbingu (c)mawingu (d)shimo kubwa
5.Kichwa cha habari hii kingefaa kuwa kipi? (a)dunia (b)umbo la dunia (c)dunia tambarare (d)tufe
Katika swali la - 30 chagua herufi ya jibu sahihi
6.Shaibu anakusanya mazao yake shambani. Nini kinyume cha neno Shaibu
(a)babu (b)ajuza (c)banati (d)barobaro
7.Neno lenye maana sawa na mawio ni lipi. (a)asubuhi (b)jioni (c)mchana (d)alasiri
8.Wiki ijayo mtafanya mtihani wa somo la kiswahili. Sentensi hii ipo katika nafsi gani
(a)nafsi tatu wingi (b)kwanza umoja (c)pili wingi (d)kwanza wingi
9.Wabunge waliandika “Waraka” kwa Rai. Neno lililopigiwa mstari lina maana ipi. (a)Barua (b)zawadi (c)mswada (d)sheria
10Muda mfupi ataingia msikitini. Sentensi hii ipo katika wakati gani?
(a)ujao (b) mtimilifu (c)uliopita (d)mazoea
11.Anna na Rehema wanakimbizana. Neno lililopigiwa mstari lipo katika kauli gani. (a)Kutendeana (b)kutendewa (c)kutendana (d)kutendea
12.Katika sentensi “Sita kuwepo” kiambishi kinachoonyesha ukanushi ni kipi.
(a)ta (b)po (c)ku (d)si
13.Mwanamke yule alikaa .............. baada ya kufiwa na mume wake (a)eda (b)head (c)arobaini (d)fungate
14.Baraka aliona ................. kuwa miongoni mwa aliofaulu somo la hesabu
(a)fadhili (b)fahari (c)fahiri (d)fadhila
15.Mchezo wa simba na Yanga ............ kutokana na klabu ya yanga kugoma kucheza sa 1:00 usiku
(a)ulihahirishwa (b)uliahirishwa (c)uliairishwa (d)uliahilishwa
16.Hisan haifi. Methali hii in amaana gani? (a)timiza ahadi yako (b)weka akiba (c) ukifanya mema utakumbukwa daima (d) ringia utajiri wako.
17.Vijana wengi wana tabia nzur. Maneno “Wengi” na Nzuri” ni aina ya maneno gani?
(a)Vivumishi (b)nomino (c)viwakilishi (d)vielezi.
18.Kiti cha dhahabu hakikaliwi na watu. Kitendawili hiki kina maana ya
(a)jua (b)miba (c)moto (d)nyuki
19.Heri kufa macho kuliko ............ metahali hii inakamilishwa na kifungu kipi cha maneno
(a)kuumia moyo (b)kufa jicho (c)kujikwaa ulimi (d)kufa moyo
20.Kisawe cha neno “Faragha” Ni ..............
(a)hadarani (b)pembezoni (c)mafichoni (d)kivulini
21.Mtu ............ anaruhusiwa kuishu mahali ............... ilimradi tu hajavunja sheria na taratibu za nchi. Maneno yanayokamilisha tungo hii ni yapi kati ya haya yafuatayo.
(a)yoyote, popote (b)yeyote, popote (c)popote, yoyote(d)popote, yeyote
22.Tutaimba kabla ya kuondoka shuleni. Katika neno “Tutaimba” silabi inayoonyesha nafsi ni ipi.
(a)tu (b)a (c)na (d)tu na na
23. “Uma sikio” nini maana ya nahau hii .................
(a)ng’ata sikio (b)toa sikio (c)kula sikio (d)nong’oneza
24.kuku wangu ameangua kifaranga. Upi ni wingi wa sentensi hii
(a)kuku zangu zimeangua vifaranga (b)kuku wetu wameangua vifaranga
(c)makuku yetu yameangua mavifaranga (d)kuku zetu zimeangua vifaranga
25.Nyumba hii ni ya ............ kubwa sana. Neno lipi linakamilisha senensi hii
(a)samani (b)zamani (c)shamini (d)thamani
26.Neno “Aliyeng’ang’ania” lina silabi ngapi? (a)nne (b)tatu (c)sita (d)saba
27.Maneno “Mzuri mweupe, mwembamba, mkali” yakitumika pamoja na majina katika sentensi huwa
(a)Kielezi (b)nomino (c)kiwakilishi (d)kivumishi.
28.Ng’ombe dume aliyehasiwa na kufanya shudhuli nzito za kilimo huitwaje
(a)fahali (b)beberu (c)gegedu (d)maksai
29.Neno “msonobari” lina aina ngapi za irabu (a)1 (b) 2 (c)4 (d)3
30.Tegua kitendawili kifuatacho. “Jini mnywa damu haangazi bila damu”
(a)kisima (b)kinywa na maneno (c)mto (d)kibatari
USHAIRI
Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu swali la 31 – 35
Kiswahili lugha pana, wote tunaifahamu
Na sisi tunakiona, kwa pamoja twafahamu,
Uhuru tulipigana, na Nyerere afahamu,
Kiswahili lugha yetu, Watanzania twaringa
Wasanii watetea, Kiswahili kutumika,
Hata vijijini pia, Kiswahili chasifika,
Wazungu watamania, lulu zetu kusifika,
Kiswahili lugha yetu, watanzania twaringi
MASWALI
31.Shairi hili lina beti ngapi? (a) mbili (b)tatu (c)saba (d)moja
32.Ni wapi ambako kiswahili chasifika?(a)mjini (b)mashambani (c)vijijini (d)vyuoni
33.Kina cha mwisho katika ubeti wa pili ni (a) ia (b)ika (c)ka (d) a
34.Shairi hili lina mizani mingapi? (a)16 (b)17 (c)18 (d)8
35Nani wanaotajwa kukitamani kiswahili. (a)waarabu (b)wazungu (c)watanzania (d)wasanii
SEHEMU B UTUNGAJI.
Panga sentensi zifuatazo kwa kuzipa herufi A,B,C,D na E ili zilete mtiririko mzuri
36.Hivyo alimwandikia shangazi yake aliyeko Dodoma
37. Watahiniwa wote walifanya mitihani siku hyo
38Barua hiyo ilihusu mambo muhimu yaliyohitajika shuleni
39.Nyamizi alikuwa mmoja wa watahiniwa hao
40.Matokeo yalipotolewa alibahatika kuchagulia miongoni mwa watahiniwa
SEHEMU C. UFAHAMU
Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu swali la 41 – 45 kwa kuandika jibu sahihi.
Siku moja mganga mkuu wa Zahanati alishauri uongozi wa kiji kujenga wodi mbili. Alishauri ijengwe wodi ya waototo na akina mama. Mganga mkuu alishauri hivyo ili kuwaondolea adha wazazi wenye watoto wadogo na wajawazito. Hii inatokana na huduma ya kliniki kupatikana mbali
Viongozi wa kijiji waliunga mkono wazo lake na kuwasihi wanakijiji kuchangia kwa moyo mweupe ilikufanikisha zoezi hili na wananchi walifanya jitihada na kujitoa kwa hali na mai. Maana waliamini kuwa mtaka cha uvunguni sharti ainame na pia umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
MASWALI
41.Kichwa cha habari hii ni kipi? ...................................
42.Kwa nini mganga mkuu alishauri uongozi wa kijiji kujenga wodi ya watoto na wajawazito ..................
43.Taja nahau mbili zilizotumika katika habari hiii
44.Mwandishi ana maana gani anaposema walifanya jitihad ...............................
45. Andika kisawe cha neno “Aidha” ....................................................................
KISWAHILI DARASA LA TANO
MAELEKEZO KWA MSIMAMIZI
Zingatia yafuatayo kabla ya kusoma maelekezo kwa watahiniwa:
MAELEKEZO KWA WATAHINIWA
KIFUNGU CHA HABARI
Wakati elimu haijakua, watu hawakujua kuhusu Dunia yetu. Walikuwepo walioamini kuwa Dunia ni tambarare kama meza, wakiamini kuwa mtu anaweza kutembea hadi akafika mwisho wa Dunia na kuanguka kwenye shimo kubwa. Wengine waliamini kuwa kama ungeendelea kwenda, mwishowe ungegusa Mbingu. Baadaye wataalamu wa anga walithibitisha kuwa, Dunia ni umbo la duara kama tufe.
1
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FIVE EXAM SERIES 53
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA
MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA DARASA LA TANO
KISWAHILI
MUDA:1:30
JINA_____________________________________SHULE_________________________
MAELEKEZO:
SEHEMU A: SARUFI NA FASIHI
C. Hapana hapana D.Ng’a
C. Sinzia D.maumbile
C. A-WA D.LI-YA
Nyumbani mwangu mnashetani ambaye daima anakunywa maji yangu
C. Taa D.mtungi
Kipofu ______ tulimwona amerudi
C. Ambako D.aliye
Wajomba zako
C. Wajombazo D.mjombako
C. Donya D. malaika
A kunjakunja B.kunjia
C. kunjiana D. kunjisha
SEHEMU B. METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
Kamilisha methali zifuatazo
Tunga sentensi kwa kutumia sentensi zifuatazo
Tegua vitendawili vifuatavyo
SEHEMU C. USHAIRI
SEHEMU D. UTUNGAJI
Panga hatua za kufanya ufupisho kwa mtiririko sahihi
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FIVE EXAM SERIES 39
MINISTRY OF EDUCATION, REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT
STANDARD FIVE EXAMINATION SERIES
KISWAHILI, MID TERM SEPTEMBER 2021
ANSWER ALL QUESTIONS
SEHEMU A: SARUFI
Chagua jibu sahihi
SEHEMU B LUGHA YA KIFASIHI METHALI NAHAU NA VITENDAWILI
Kamilisha methali
Tegua vitendawili
Toa maana ya nahau zifuatazo
SEHEMU C UTUNGAJI
Sentensi zifuatazo zimeandikwa bila kufuata mtiririko sahihi. Zipange kwa kuzifa A, B, D, na E
SEHEMU D USHAIRI
Soma shairi kwa makini kisha ujibu maswali utakayoulizwa
Mtihani umefika, tumekaa darasani,
Kiswahili twaandika, lugha yetu ya thamani,
Vijana hebu amka, na kalamu mkononi,
Msome bila pambao, msikalie maneno.
Maswali
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FIVE EXAM SERIES 34
OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MITIHANI YA KUJIPIMA MSINGI
MTIHANI WA NUSU MUHULA WA KWANZA -MACHI 2021
KISWAHILI – DARASA LA TANO
FOMATI MPYA
MUDA 1: 30 MASAA MACHI 2021
JINA …………………………... SHULE ………………………...
MAELEZO
SEHEMU A MSAMIATI:
Chagua herufi ya jibu sahihi
1. Ndani ya pochi mama aliweka fedha na nguo ………. A. yake B. zake C. ake D. yetu [ ]
2. Bakari na mwasiti walipewa ……….. kali. A. adhabu B. adabu C. azabu D. asabu [ ]
3. Kuna msemo usemao, siku za mwizi ni ……… A. kumi B. nyingi C. arobaini D. hamsini [ ]
4. Mtu asiye na meno huitwa ………. A. kibogoyo B. kipofu C. kiwete D. kiziwi [ ]
5. Katika ajali ya treni rafiki yangu ……… kichwa. A. alivunjika B. alipasuka C. alikatika D. aliruka [ ]
6. Mwalimu mkuu aliwaita wale …………
A. kufika shuleni. A. cWaliochelewa B. watakaochelewa C. dwachelewaji D. wasiochelewa [ ]
7. Endapo ………. Mtihani mtashangilia. A. mtafauru B. mtafaulu C. mkifaulu D. nimefaulu [ ]
8. Mtoto mwenye adabu ……….
A. hupendwa na watu nwengi B. hupigwa na mwalimu C. hulia ovyo D. hukimbia ovyo [ ]
9. Mvungu ni sehemu ya ………
A. kndo ya kitanda B. mbele ya kitanda C. juu ya kitanda D. chini ya kitanda [ ]
10. Nini maana ya kutia nanga ……….… A. kutia uzito jambo
B. kufika mwisho wa jambo C. kuanza kutenda jambo D. kuzorotesha jambo [ ]
11. …………… mama yangu alipopona malaria.
A. Ningefarijika B. Nitafarijika C. Ninafarijika D. Nilifarijika [ ]
12. …….... Wasiofuata sheria za barabarani husababisha ajali.
A. Marubani B. Manahodha C. Madereva D. Mabaharia [ ]
13. Mtu anayeongaoza meli huitwa ……… A. rubani B. nahodha C. dereva D. utingo [ ]
14. Nimepatwa na ……. Kutokana na msiba wa mjomba.
A. majozi B. furaha C. njaa D. homa [ ]
15. Usipoziba ………. Utajenga ukuta. A. mwanya B. ufa C.nafasi D. upenyo [ ]
16. Mkoa wa Iringa ni mojawapo ya mikao iliyoko nyanda za juu …….
A. kaskazini B. mashariki C. mashariki D. kusini [ ]
17. Alitembea …….. miguu kutoka shuleni hadi nyumbani. A. na B. wa C. kwa D. cha[ ]
18. Mtoto huyu alikuwa na bidii darAsani …….. hakufaulu mtihani.
A. hata vile B. hata hivyo C. hivyo D. angalau [ ]
19. Kama ungaliomba kitabu kile …… A. ningelikupa B. ningalikupa C. nitakupa D. nakupa[ ]
20. Hadi sasa hakuna mtu ………..aliyekamatwa kuhusika na wizi ule.
A. yeyote B. wowote C. vyovyote D. yoyote [ ]
21. Mwalimu aliwataka wanafunzi wamsikilize kwa makini? Sentensi hii ipo katika kauli ipi?
A. taarifa B. halisi C. kutendwa D. [ ]
22. Sikuweza kutambua ni nani amelala kitandani kwa sababu alijifunika shuka………..
A. lote B. gubigubi C. zima D. nzima [ ]
23. Kisawe cha neno shaibu ni ………. A. barabara B. banati C. ajuza D. kogori [ ]
24. Neno “haiba” lina maana sawa na neno lipi kati ya haya?
A. amani na utulivu B. urembo wa mavazi C. urembo wa sura D. mwenendo mzima [ ]
25. Matonya alioa msichana wa hirima yake”. Neno hirima lian maana sawa na ………..?
A. kabila B. nasaba C. rika D. jinsi [ ]
26. Furaha alishikwa na “fadhaa” alipobaini ameuziwa mali ya wizi neno “fadhaa” katika sentensi hii lina maana ya ……… A. mshangao B. hofu C. ghadhabu D. chuki [ ]
27. Mbuzi dume huitwa bebebru, je ng’ombe dume huitwa? ………….
A. fahari B. fahali C. furaha D. ng’ombe [ ]
28. John ni mahiri wa kughani mashairi na tenzi. Neno “mahiri” lina maana ya …………
A. sahihi B. nadhibu C. bingwa D. mjinga [ ]
29. Panga herufi hizi ili zilete neno sahihi la Kiswahili “masuria”
A. sufuria B. misumari C. masaria D. suriama [ ]
30. Umoja wa neno “nyayo” ni upi?......... A. unyayo B. upele C. nyanya D. kinyayo [ ]
SEHEMU B:
METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
31. Nahau ipi inabeba ujumbe wa mtu kufanya mipango ya siri yenye hili………..
A. kula kiapo B. kula yamini C. kula ugali D. kula njama [ ]
32. “Kaa chonjo” nahau hii ina maana gani?.......... A. jihadhari B. kaa vizuri C. kazana D. jitahidi[ ]
33. James ameniunga mkono katika suala hili, mana yake ni ……..
A. amenipiga B. amemkwepa C. amekubaliana na mimi D. amenichangamkia [ ]
34. Kamilisha methali hii “ Asiyeuliza……….”
A. ni mpole B. hajaelewa C. hana ajifunzalo D. ameelewa [ ]
35. Kamilisha methali isemayo “Baniani mbaya ……..
A. dawa ya moto B. kulia kweupe C. kiatu chake dawa D. ukamuuliza dawa [ ]
36. Tegua kitendawili hiki; Huuawa na uzazi wake……….. A. kinyonga B. konokono C. nzi D. papasi [ ]
37. Mwanzo wa methali “………. ujue anatunga sheria” ni upi?
A. kuuliza B. ukiona kobe kainama C. mwenda pole D. kobe tembea haraka [ ]
38. Rafiki yangu ni mharibifu lakini bado namhitaji. Tegua kitendawili ……….
A. kobe B. moto C. papai D. kinyonga [ ]
39. Nini maana ya nahau “ponea chupuchupu”……..
A. kumpongeza B. wahi hospitali C. nusurika D. kunywa supu [ ]
40. Kuongeza maneno ya uongo katika jambo. Nahau ipi yenye maana hiyo?..................
A. kata shauri B. piga uvivu C. tia chumvi D. piga winda [ ]
SEHEMU C: UTUNGAJI
Umepewa habari yenye sentensi tano zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo, katika swali la 41 – 45 zipange csentensi hizo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kuzipa herufi A, B, C, D, E
41. Ukataji miti kwa wingi kwa ajili ya shighuli za ujenzi na shughuli zingine huweza kusababisha nchi yetu ya Tanzania kuwa jangwa________
42. Kutokana na miti, watu hujenga nyumba nzuri za kila namna zinazopendeza na za kudumu_________
43. Hivyo ni muhimu kwa kila mtu kupanda mti kila anapopakata mti kwani nchi isiyo na miti ni sawa na mtu ambaye hana mpangilio wa mambo yake_______
44. Miti ina faida nyingi sana kwa binadamu__________
45. Hivyo kila mmoja wetu atunze mazingira yetu yawe ya kuvutia kwa kutunza miti, kila mtu anaweza________ kupendezesha mazingira kwa pamoja inawezezkana kubadilisha nchi yetu kuwa ya kijani kupitia utunzaji wa miti______________
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FIVE EXAM SERIES 24
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA
MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA DARASA LA TANO
KISWAHILI
MUDA:1:30
JINA_____________________________________SHULE_________________________
MAELEKEZO:
SEHEMU A: FASIHI NA MSAMIATI
Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye mabano
15.tutalima shamba la shule.
SEHEMU B: METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
SEHEMU C: USHAIRI
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali hapo chini.
Kazi zote duniani, namba wani mkulima,
Anapita kila fani, hata kama hakusoma,
Kula haendi sokoni, au kuomba kwa Juma,
Zunguka dunia nzima, kazi bora ni kilimo
Maswali
SEHEMU D: UTUNGAJI
Zipange sentensi zifuatazo kwa mtiririko wa mawazo kwa kuzipa herufi A, B, C, D na C
SEHEMU E: UFAHAMU
Soma kwa makini habari kisha jibu maswali utakayoulizwa.
Ngonjera ni ushairi wa majibizano ambao una pande mbili zinazojibizana kuhusu jambo fulani, upande mmoja huwa sahihi na wa pili huwa umepotoka. Lengo la majibizano ni kuusahihisha upande uliopotoka. Hili linapotokea, ngonjera huwa imefikia kilele chake. Ngonjera zilitumika sana katika uenezaji wa siasa ya ujamaa Tanzania mnamo miaka ya 1970. Ngonjera huwa tofauti kidogo na malumbano kwa sababu katika malumbano, washairi hujibizana, na si lazima wapate suluhisho la majadiliano yao.
MASWALI
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FIVE EXAM SERIES 18
OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
KISWAHILI- MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA
DARASA LA SITA
MUDA: 1.30
MAELEKEZO
SEHEMU A. SARUFI
Chagua jibu sahii katika maswali yafuatayo;
1. Wanafunzi waliopiga kelele darasani walipewa………………………..
2. Neon “waliandikiwa” lipo katika wakati upi kati ya nyakati zifuatazo.
3. Dada wa baba yako utamwitaje?
4. Wingi wa maneno “Mchanga mwingi” ni upi kati ya maneno yafuatayo?
5. Wageni wanaotembelea mbuga za wanyama huitwaje?
6. Mama yangu…………………..chakula kizuri jana jioni.
7. Siku ya pili baada ya leo huitwa?
8. Wingi wa neon ufundi ni upi kati ya maneno yafuatayo?
9. Ni neno lipi kati ya maneno yafuatayo yenye maana inayojumuisha maneno upinde, bunduki, mkuki na mshale,
10. Mwakani…………….darasa la tano. Ni neno lipi linakamilisha sentensi hii kwa usahii?
11. …………likilia kuna jambo
12. Mtu anayeendesha ndege huitwa…………………..
13. Ni marufuku mifugo yote………………….karibu na hifadhi za taifa.
14. Watu wengi walilima…………………yam to rufiji
15. Ziwa Tanganyika liko upande wa ………………..mwa nchi ya Tanzania
16. Ipi ni sentensi sahihi kati ya hizi iliyoandikwa katika wakati uliopita nafasi ya kwanza umoja?
17. Katika sentensi hizi, ipi ina vitu vinavyohesabika?
18. Katika shairi, vina ni………………………
19. Kamilisha methali ifuatayo.”Mchagua nazi huinukia..”
20. “Kiti cha mjomba wangu ni kizuri” nini wingi wa sentensi hii?………….
SEHEMU B.
Andika neno moja linalowakilisha kundi la maneno yafuatayo ………… …………
21. Darasa, nyumba, ofisi, vyoo……………
22. Mende, siafu, nyuki,kipepeo……………
23. Jumatatu, jumanne,alhamisi………………
24. Sato,perege, kambale,kamba………………
25. Shati, suruali, kaptula, sketi…………………
Kamilisha methali na vitendawili vifuatavyo.
26. Mwana kidonda mjukuu……………
27. Mchagua jembe………………………
28. Haba na haba………………
29. Nina chemchem isiyokauka………………
30. Tajiri wa rangi……………………
SEHEMU C.
Kamilisha nafasi zilizoachwa wazi kwa kuchagua jibu lililo sahihi kutoka katika kisanduku kifuatacho.
Kusengenya,mtu,uyoga,katani,Kuishi,miaka mingi, kumsuta mtu, barabara,kilema, mwizi, kuwa tajiri sana |
31. Nahau, ‘’Ana mkono mrefu maana yake ni ipi?...................
32. Kitendawili kisemacho “kamba yangu ni ndefu lakini haifungi kuni maana yake ni ipi…….
33. Nahau kula chumvi nyingi maana yake ni……….
34. Kitendawili kisemacho “nyumba yangu ina nguzo moja” jibu lake ni lipi?……………
35. Nahau “kumkalia kitako” maana yake ni ipi?...........................
SEHEMU D.
Tumia maneno uliyopewa kwa kula sentensi kujaza nafasi zilizoachwa wazi.
36. Watoto ______ chakula kitamu (wanapenda, watalia, wanaimba, walitenda)
37. Otaigo alipofika sokoni_________mjomba anauza viatu (atamkuta, hukuta, alimkuta, angemkuta)
38. Baba yake Eliza_____________ akida (ataita, anaitwa, anaitika, ameitwa)
39. Kesho jioni___________ mtoni (nitakwenda, nilienda, nimekwenda, nimeenda)
40. Leo Mwalimu __________elimu kwa vitendo. (himiza, alihimiza, huhimiza, anahimiza)
41. Mwasije atakapokuwa mkubwa_________ ghorofa (anajenga, hujenga, atajenga, akijenga)
42. Kijana yule angalighani shairi__________mtukutu (asingalikuwa,asingelikuwa, asingekuwa,angekuwa)
43. Mama____________sasa hivi kwenda dukani (aliondoka, alikwishaondoka, ameondoka, keshaondoka)
44. Kila siku ________ shuleni kwa miguu. (tulikwenda, tumekwenda, tunakwenda, tutakwenda.)
45. Jana ________kitabu kinachoelezea utii wa watoto kwa wazazi na walimu. (nimesoma, nilisoma, nitasoma anasoma.)
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FIVE EXAM SERIES 10
OFISI YA RAISI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA KUJIPIMA DARASA LA TANO
APRIL-2020 MUDA:SAA 2:00
KISWAHILI
MAELEZO KWA MTAHINIWA
SEHEMU A.
Chagua jibu sahii kutoka kwenye majibu uliopewa.
1. Ni sentensi ipi iliyo sahihi kimuundo kati ya zifuatazo?
2. Wingi wa sentensi "Mbuzi wamepotea" ni upi?
3. Wewe unasoma kwa bidii"wingi wa sentensi hii ni upi?
4. "Wasichana saba wamechaguliwa kujiunga na kozi ya uhandisi." Neno na ni aina gani ya neno?
5. Neno lipi kati ya haya halilandani na mengine?
6. "Maji yakimwagika hayazoolekl hii ina maana gani kati ya zifuatayo?
7. Kiwanda hutoa ajira kwa wananchi "kiwanda" ni aina gani ya neno?
8.Kisawe cha neno "ndovu" ni kipi kati ya maneno yafuatayo?
9..Kisawe cha neno ”mviringo” ni kipi?
10. Wakikua mama yao huwatupa mbali kwa kishindo.Jibula kitendawili hiki ni lipi?
11. Wakikua mama yao huwatupa mbali kwa kishindo.Jibula kitendawili hiki ni lipi?
12. "Anatengeneza mchuzi mtamu sana lakini hapiki jikoni" kitendawili hiki jibu lake ni lipi?
13. "Ukiona vyaelea vimeundwa" methali hii ina maana gani?
14. Katika sentensi zifuatazo ipi ina maana sahihi?..
15. Ni neno lipi kati ya yafuatayo ni kisawe cha neno "hifadhi"? .
16. "Mjukuu wangu hupenda kuniamkia kila mara." Sentensi hiyo ipo katika kauli gani?
17. "Mwanamuziki hodari aliimba nyimbo vizuri.” Kielezi katika sentensi hii ni kipi? ........
18. Mama Ntilie akiondoka, uondoke naye. Sentensi hii ipo katika wakati gani? ........
19. Mpira umegonga mwamba nusura goli liingie. Neno lipi linaonesha kitendwa? ........
20. Ni neno lipi kati ya haya yafuatayo ni tofauti na mengine? ........
SEHEMU B.
Tunga sentensi kwa kutumia maneno ya sehemu A na B ili kukamilisha maana.
Na. | SEHEMU A | SEHEMU B |
|
|
SEHEMU D.
Jibu maswali yafuatayo kwa ndio au hapana.
SEHEMU E. Kamilisha methali zifuatazo
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FIVE EXAM SERIES 2