?>
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA KUJIPIMA KWA SHULE ZA MSINGI,
NUSU MUHULA WA KWANZA – MACHI-2024
MUDA: ..........
SUBJECT: SAYANSI DARASA LA: 4
JINA: ………………………………………………….. TAREHE: ......................
Chagua herufi ya jibu sahihi
1. Kipimajoto kina mrija ambao una kimiminika ndani, kinachoitwa
(A)Sentigrade (B) Rekoda (C) usindikaji (D) zebaki
2. _______ ni hali ya hewa inayotuzunguka kwa muda mfupi.
(A) hali ya hewa (B) mwanga wa jua (C) kipima joto (D) joto
3. Ni ipi kati ya zifuatazo sio njia ya kuharibu mazingira?
(A) kukata miti (B) kuchoma msitu(C) kupanda miti (D) kufuga kupita kiasi
4. Mwelekeo wa upepo hupimwa kwa kutumia chombo kinachoitwa _____
(A) kipimo cha mvua(B) Vane ya upepo (C) mwelekeo wa dira (D) uchunguzi
5. Utumiaji wa kemikali zenye sumu katika uchafuzi wa uvuvi
(A) maji (B) hewa (C) nchi kavu (D) samaki
6. Kiasi cha maji katika hewa ambayo ni katika mfumo wa mvuke inaitwa
(A) unyevu (B) mawingu (C) mvua (D)upepo
7. Joto hupimwa ndani
(A) milimita za zebaki (B) digrii za sentigredi (C) kilogramu za sentigredi (D) milimita za sentigredi
8. Mwanga na joto linalotokana na jua wakati hakuna mawingu ni
(A) unyevu (B) mvua (C) mawingu juu ya (D) mwanga wa jua
9. Ni aina gani ya hali ya hewa ambayo huwalazimisha watu kuvaa jaketi, gumbooti na kubeba miavuli?
(A) upepo (B) mawingu (C) Jua (D) mvua
10. Kitengo cha kipimo kwa kasi ya upepo ni
(A) milimita (B) mwelekeo wa dira (C) digrii sentigredi (D)kilomita /saa(km/saa).
Oanisha maneno katika safu A na maelezo katika safu B hili kupata jibu sahihi.
SAFU A | SAFU B |
| A. Utamaduni B. Mwendo wa hewa karibu nasi C. Chochote kinachotuzunguka D. Pima shinikizo la anga E. Kujenga ushirikiano F. Ni mchakato wa kuchimba madini kutoka ardhini. G. Tovuti ya kihistoria H. Kipima joto I. Inatumika kwa kizazi kijacho J. Hygrometer |
3.Chagua neno sahihi hapa chini ili kujaza nafasi iliyotolewa kinasa mwanga wa jua, kituo cha hali ya hewa, mtaalamu wa hali ya hewa, harusi, kilimo.
1. ___________ Sherehe wakati mwanamume na mwanamke wanapooana
2. Mtu anayesoma hali ya hewa anaitwa _______________
3. Jina la mahali ambapo hali ya hewa inarekodiwa ni nini? _______________
4. Kilimo na ufugaji hurejelewa kuwa _________ shughuli
5. ______________________________ ni chombo kinachotumiwa kupima mwanga wa jua.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 97
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
UPIMAJI WA DARASA LA NNE NUSU MUHULA
MACHI -2024
KISWAHILI
MUDA:..................
JINA_____________________________________
MAELEKEZO:
SEHEMU A:
IMLA
1. Sikiliza kwa makini sentensi utakazosomewa kisha andika kwa usahihi.
i.
ii.
iii.
iv.
v.
SEHEMU B:
SARUFI, MISAMIATI NA MATUMIZI YA LUGHA
2. Chagua herufi ya jibu sahihi kisha jaza katika mabano.
i. Tulipokuwa tukijisomea aliniambia nikamilishe sentensi hii” babu na bibi kumwona shangazi kesho. A. Walikwenda B. Na C. Huenda D. Watakwenda
ii. Mwalimu aliuliza neno lipi linakamilisha sentensi hii kwa usahihi? Baba yangu alikula wali _____kijiko A. Na B. Kwa C. Mwa D. Pamoja
iii. Dereva ni kwa mwendesha vyombo vya nchi kavu rubani ni kwa mwendesha ndege. Je, nahodha ni kwa A. Manju B. Vyombo vya majini C. Ni kwa mabaharia D. Vyombo vya angani
iv. Upi ni ukanushi sahihi wa neno “Ataimba” A. Huimba B. Hataimba C. Ataimba D. Hajaimba
v. Rafiki yangu alinionesha zeruzeru tulipokuwa kanisani. Kisha nilimuuliza neno lipi ni kisawe cha zeruzeru? A. Chotara B. Suriama C. Albino D. Muakasti
vi. Mwalimu alisema yakinisha sentensi ifuatayo “Elimu haina mwisho” A. Elimu si mwisho C. Elimu ina mwisho B. Elimu inafika mwisho D. Elimu ni mwisho
vii. Nilipenda kujua kama unafahamu neno mchwa linaundwa na silabi zipi? A. M,ch,wa B. M,c,h,w,a C. M,chwa D. Mchwa
viii. Jamila anafanya kazi katika maktaba ya taifa. Je, Jamila ni nani? A. Mkutubi B. Maktabalisti C. Mfanyakazi D. Mnajimu
ix. Mzee Kalumanzila anatibu watu kwa kutumia mitishamba. Je, neno “Kalumanzila” lina silabi ngapi? A. Tatu B. Nne C. Tano D. Kumi na moja
x. Bibi yake Sampuluna ni mzee sana hawezi hata kulima shamba tena. Je, neno gani lina maana sawa na mwanamke mzee? A. Abu B. Shaibu C. Buda D. Ajuza
xi. Kitoto chake kinacheza mpira vizuri. Wingi wa neno lililopigiwa mstari ni upi? A. Mtoto B. Chitoto C. Vitoto D. Watoto
xii. Mtakapokuja kwenye mazishi msigombanie mali za watu. Neno lililopigiwa mstari lina silabi mwambatano ngapi? A. Mbili B. Tatu C. Moja D. Nne
xiii. Samaki mkunje angalli mbichi. Wingi wa sentensi hii ni upi? A. Samaki wakunje angali wabichi C. Masamaki yakunje yangali mabichi B. Samaki mkunje wabichi D. Samaki wabichi yakunjwe
xiv. Mjomba alipanda juu ya mnazi kuangua nazi. Je, mtu anayeangua nazi anaitwaje? A. Muanguaji B. Mkwezi C. Mgemaji D. Mkunazi
xv. Umoja wa sentensi hii ni upi? Wajuaji wale hawatafanikiwa A. Wajuaji hawa hawatafanikiwa C. Hatafanikiwa mjuaji B. Mjuaji huyu hatafanikiwa D. Mjuaji huyu atafanikiwa
SEHEMU C: METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
3. Jibu maswali yote kwa kuchagua jibu sahihi;
i. Wanafunzi wote wa darasa la nne tulikata shauri kusoma kwa bidi ili tufaulu mitihani yetu. Je, nahau kata shauri ina maana gani? A. Kubaliana B. Shirikiana C. Amua D. Kata tamaa
ii. Mwanaheri ni mtoto wa kwanza katika familia yao. Je, Mwanaheri hujulikana kama A. Kitinda mimba B. Kilembwe C. Mwanambee D. Mziwanda
iii. Mzee Umbe alirudi mapema nyumbani mara baada ya kumwaga unga kazini kwake. Je, nahau mwaga unga ina maana gani? A. Kuwahi kazini B. Kumaliza kazi mapema C. Kufukuzwa kazi D. Ajiriwa
iv. Lipi kati ya haya yafuatayo ni jibu la kitendawili hiki” Gari moshi relini? A. Treni B. Zipu C. Msitu D. Reli
v. Liwali amekonda sana lakini hana dawa. Je, jibu la kitendawili hiki ni lipi? A. Sisimizi B. Siafu C. Sindano D. Pini
vi. Mzee Jamali alisema loo! nalipa faini kosa lisijui. Ndipo tulipokumbuka jibu la kitendawili hiki ni A. Usingizi B. Kutereza C. Kujikwaa D. Kuanguka
vii. Tulipofika stesheni tulikuta treni la abiria likianza safari, ghafla rafiki yangu aliniambia gari moshi relini. Ndipo nilipojua anataka jibu la kitendawili hicho. A. Dereva B. Sisimizi C. Siafu D. Zipu
viii. Tulipofungwa karata na baba nililalamika sana ndipo mama aliposema “Asiyekubali kushindwa A. Hawezi B. Hathaminiki C. Hatashinda D. Si msindani
ix. Maige huuza bidha kwa bei ya rejareja kwa kuzunguka nazo mtaani. Je Maige ni nani? A. Dalali B. Machinga C. Muuzaji D. Mhandisi
x. Mama Jamila hapendi watoto wamwage chakula pindi wanapo shiba. Hupenda kuwaambia wakifunike na kukihifadhi kwa matumizi ya baadae. Je, ni methali gani itatumika kusisitiza maelezo hayo. A. Haba na haba hujaza kibaba C. Chovya chovya humaliza buyu la asali B. Chembe na chembe mkate hua D. Akiba haiozi
4. Tumia maneno yaliyopo kwenye mabano ili kujaza sehemu zilizoachwa wazi
Muda, Mvua, Mbayuwayu, Vitoweo, Hasira, Kunepa, Ujumbe, Kiongozi, Kucheza, kumbukumbu
i. Alijiweka mbele kila wakati ili achaguliwe kuwa................................ wao.
ii. Tawi lilianza............................. baada ya kutua ndege wengi.
iii. Alipotuamuru tuondoke tulijawa na ...............................................
iv. Hatukuona ndege yoyote isipokuwa .............................................tu wakila kumbikumbi.
v. Tulipopata .....................................wa kuuguliwa kwake sote tulikwenda kumsalimia.
SEHEMU D: UTUNGAJI
5. Panga sentensi zifuatazo katika mtiririko maalumu kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E
i. Baada ya kusubiri kwa nusu saa basi liliwasili na nikapanda basi hilo kwenda Bunda.
ii. Abilia wote walishuka kwenye basi.
iii. Liliwasili mjini Mwanza, gari moshi lilisimama taratibu na kutangaza kuwa hapo ndipo mwisho wa basi.
iv. Nami nilishuka na kwenda moja kwa moja kwenye kituo cha basi.
v. Mimi na abiria wenzangu tulisafiri kwa Amani na kufika Bunda salama jioni.
SEHEMU E: UFAHAMU
6. Soma habari ifuatayo kwa usahihi kisha jibu maswali utakayoulizwa.
Hapo zamani za kale kulitokea mgogoro mkubwa sana kati ya ndege na wanyama. Juhudi za kumaliza mgogoro huu zilionekana kugonga mwamba na hatimaye vita ilianza. Wakati majeshi hayo mawili ya wanyama na ndege yakijiandaa kupigana, popo alisita kuchagua upande wa kujiunga na kivita. Jeshi la ndege lilifika nyumbani kwa popo na kumwambia. “Twende vitani ewe popo ndege mwezetu”. Popo alikataa na kusema “mimi ni mnyama na si ndege kama ninyi”. Baadaye jeshi la wanyama lilifika nyumbani kwa popo na kumwambia ni ndege na wala si mnyama kama ninyi”. Basi kukawa na ngurumo za kutisha za wanyama shupavu kama vile simba, duma na tembo, na ndege shupavu kama vile tai na mbuni. Majike wenye ndama na majike wenye makinda walihisi kiama chao kimefika.
Kwa bahati nzuri sana, katika dakika za mwisho kuelekea vita, muafaka ulifikiwa kati ya pande zote mbili na vita ikaepukikwa. Kukawa na Amani badala ya mapigano. Makundi yote mawili yakawa na shamrashamra za kusheherekea kuepukana na mgogoro. Kuona hivyo, popo naye alitamani kuwa sehemu ya shamrashamra hizo. Alikwenda kwa ndege akitaka kujiunga nao lakini ndege walimfukuza. Baadaye akaenda kwenye kundi la wanyama nao walimfukuza. Popo akabaki kuwa njia panda kwani hakuruhusiwa kujiunga na kundi la ndege au kundi la wanyama.
MASWALI
i. Mwandishi ameeleza katika habari kuwa kulikuwa na mgogoro. Je, mgogoro uliotokea hapo zamani uliwahusu kina nani?
ii. Mwandishi amesema juhudi zote ziligonga mwamba. Je, maneno yaliyopigiwa mstari yana maanisha nini?
iii. Katika hadithi uliyoisoma wametumia neno “kiama” Je neno kiama lina maana gani?
iv. Kutokana na hadithi uliyosoma nani alibaki njia panda?
v. Kutokana na habari uliyosoma hadithi hii inahusu nini?
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 96
OFISI YA RAISI
WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI UNAOPIMA UMAHIRI
MTIHANI WA MAANDALIZI-OCTOBA-2023
KISWAHILI – DARASA LA NNE
MUDA 1:30 MASAA
JINA .................................................................. SHULE ...................................
MAELEZO
SEHEMU A
IMLA
SEHEMU B
MSAMIATI NA SARUFI
SEHEMU C
LUGHA YA KIFASIHI
Methali, Nahau na vitendawili
(amekula chumvi nyingi, ana mkono mrefu, ana mkono wa birika, ana inda)
(kuwa mkweli, kuwa kigeugeu, kuwa mpole, kuwa muungwana)
(Kisongo, kope, macho, uso)
(Masikini, tajiri, mgonjwa, mdhaifu)
SEHEMU D
UTUNGAJI
Ukwasi dalali bidhaa mavazi makazi
Baraka ni (i) …………. Katika soko la Miembeni. Ukifika sokoni hapo utamkuta Baraka akinadi (ii) ….. mbalimbali kama vile (iii) ……. Shughuli hii imemletea Baraka (iv) …… katika maisha yake. Baraka alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga na sasa amehamia katika (v) ……. Yake.
SEHEMU E
UFAHAMU
Madini ni maliasili inayotupatia fedha nyingi. Tunayo machimbo ya almasi na dhahabu. Vilevile kuna machimbo ya ulanga, bati, rubi na tanzanite. Dhahabu hutumika kutengeneza mapambo kama vile bangili, herein, mikufu na pete.
Ni muhimu kila mtu aelewe faida ya kutunza kila maliasili tuliyonayo. Wanyama wakitunzwa vizuri huzaliana vizuri, miti ikitunzwa vizuri hukua haraka. Tukitunza misitu itatutunza. Misitu inatupatia mvua ya kutosha, hewa safi na miti ya mbao.
Maswali
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 88
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA NUSU MUHULA WA PILI
KISWAHILI DARASA LA NE
AGOSTI-2023
SEHEMU A
IMLA
SEHEMU B
MSAMIATI NA SARUFI
SEHEMU C
LUGHA YA KIFASIHI
Methali, Nahau na vitendawili
(amekula chumvi nyingi, ana mkono mrefu, ana mkono wa birika, ana inda)
(kuwa mkweli, kuwa kigeugeu, kuwa mpole, kuwa muungwana)
(Kisongo, kope, macho, uso)
(Masikini, tajiri, mgonjwa, mdhaifu)
SEHEMU D
UTUNGAJI
Ukwasi dalali bidhaa mavazi makazi
Baraka ni (i) …………. Katika soko la Miembeni. Ukifika sokoni hapo utamkuta Baraka akinadi (ii) ….. mbalimbali kama vile (iii) ……. Shughuli hii imemletea Baraka (iv) …… katika maisha yake. Baraka alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga na sasa amehamia katika (v) ……. Yake.
SEHEMU E
UFAHAMU
Madini ni maliasili inayotupatia fedha nyingi. Tunayo machimbo ya almasi na dhahabu. Vilevile kuna machimbo ya ulanga, bati, rubi na tanzanite. Dhahabu hutumika kutengeneza mapambo kama vile bangili, herein, mikufu na pete.
Ni muhimu kila mtu aelewe faida ya kutunza kila maliasili tuliyonayo. Wanyama wakitunzwa vizuri huzaliana vizuri, miti ikitunzwa vizuri hukua haraka. Tukitunza misitu itatutunza. Misitu inatupatia mvua ya kutosha, hewa safi na miti ya mbao.
Maswali
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 83
OFISI YA RAISI
WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MITIHANI YA KUJIPIMA MSINGI
MTIHANI WA MUHULA WA KWANZA –MEI 2023
KISWAHILI – DARASA LA NNE
MUDA 1:30 MASAA
JINA .................................................................. SHULE ...................................
MAELEZO
SEHEMU A
IMLA
SEHEMU B
SEHEMU C
ORODHA A | ORODHA B |
|
|
SEHEMU D
SEHEMU E
SHAIRI
Baba ninakulaumu, shule hukunipeleka ,
Ningekuwa hakimu, jela ningekupeleka,
Ingekufaa hukumu, nyumbani ukaondoka,
Shule hukunipeleka, baba ninakulaumu
Na mimi ningalisoma, hadi mbali nikafika,
Barua ningalisoma, na pia kuziandika,
Lakini nimeshakwama, elimu imeponyoka,
Shule hukunipeleka, baba ninakulaumu
Maswali:
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 74
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MITIHANI YA MAZOEZI DARASA LA NNE
KISWAHILI
ANNUAL FOR 2022
JIBU MASWALI YOTE
SEHEMU A
IMLA
SEHEMU B
MSAMIATI NA SARUFI
SEHEMU C
LUGHA YA KIFASIHI
Methali, Nahau na vitendawili
SEHEMU D
UTUNGAJI
Hatimaye wanafunzi mvua
Manyunyu ukungu baridi
Siku moja nilikuwa naelekea shuleni. Hali ya hewa ilibadilika kukawa na (i) …….. ambayo yalisababisha mimi nihisi (ii) ……….. (iii) ……… ulitanda kila mahali. Kengele iligongwa na (iv) …….. wote tuliingia darasani. (v) ……… mwalimu wa Kiswahili aliingia darasani.
SEHEMU E
UFAHAMU
Juma na Ally ni watoto pacha. Asubuhi huenda shuleni na wanaporejea nyumbani jioni huwasaidia wazazi wao kufanya shughuli mbalimbali. Juma ni fundi katika mapishi, hivyo humsaidia mama kupika. Ally hupenda mifugo, hivyo humsaidia baba kuchunga na kukamua maziwa. Hufanya kazi zao kwa bidi. Walimu wao huwapenda sana kwa kuwa hufanya vizuri katika masomo yao ya darasa la nne.
Maswali
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 68
OFISI YA RAIS,
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA.
MTIHANI WA KUJIPIMA.
SOMO LA KISWAHILI: DRS IV -SEPT 2022.
Muda 1: 30
JINA LA MTAHINIWA ………………………………………………….Shule…..………….………………
1. SEHEMU A. IMLA
2. SEHEMU B. Chagua herufi ya jibu sahihi.
3. SEHEMU C. Chagua neno ambalo halifanani na mengine na kisha liandike kwenye nafasi iliyowazi.
Andika knyume cha maneno yafuatayo.
iv. Adui …………………………………………………………
v. Huzuni …………………………………………………………
4. SEHEMU D. AndikaUmoja ama wingi kwa maneno yafuatayo.
UMOJA WINGI
Badili sentensi zifuatazo kuwa katika wakati ujao.
v. Anaimba vizuri …………………………………………………………………………….
5. SEHEMU E, Methali, Nahau na Vitendawili.
Toa maana ya nahau zifuatazo.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 65
MTIHANI WA KISWAHILI DRS IV
SEHEMU A:IMLA
1__________________________________________________
2__________________________________________________
3__________________________________________________
4__________________________________________________
5__________________________________________________
SEHEMU B:CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI NA
UANDIKE HERUFI YAKE
SEHEMU C:METHALI ,NAHAU NA VITENDAWILI
(KITENDAWILI)
SEHEMU D:ANDIKA NENO MOJA BADALA YA KIFUNGU CHA HABARI ULICHOPEWA
UFAHAMU
SOMA HABARI KISHA JIBU MASWALI YAFUATAYO.
Mwalimu alisema wanafunzi wanaweza kujieleza kupitia sanduku la maoni na mikutano ya shule. Alisema hivi karibuni, kutakuwa na baraza la shule, hata hivyo mwalimu alitahadharisha kwamba uhuru wa kujieleza una mipaka yake. Haturuhusiwi kutoa maneno ya kashfa kuhusu wengine kwani ni haki ya kila mtu kuheshimiwa.
MASWALI
21. Mwalimu alitahadharisha kwamba uhuru wa kujieleza una __ (A)maoni yake (B) mipaka (C) masharti yake (D) faida zake
22. Mwalimu alieleza ni_______kila mtu kuheshimiwa .
(A) haki (B) halali (C) lazima (D) faida
23.Wanafunzi wanaweza kujieleza kupitia__________
(A) mikutano tu (B)kwenye runinga (C) kisanduku cha maoni na mikutano ya shule (D)kisanduku tu
24.Tunapojieleza kuhusu wengine haturuhusiwi kutoa maneno ya ______(A)kufurahisha (B)uwongo (C)kuumiza (D)kashfa
25.Neno tahadhari kama lilivyotumika katika kifungu hiki cha habari lina maana gani? (A )Kuwa makini (B)kuwa tayari (C)kuonya (D) B na C ni majibu
MAJIBU
IMLA
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 64
OFISI YA RAIS,
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA.
MTIHANI WA KUJIPIMA.
SOMO LA KISWAHILI: DRS IV - APRIL 2022.
Muda 1: 30
JINA LA MTAHINIWA ………………………………………………….Shule…..………….………………
1. SEHEMU A. IMLA
2. SEHEMU B. Chagua herufi ya jibu sahihi.
3. SEHEMU C. Chagua neno ambalo halifanani na mengine na kisha liandike kwenye nafasi iliyowazi.
Andika knyume cha maneno yafuatayo.
iv. Adui …………………………………………………………
v. Huzuni …………………………………………………………
4. SEHEMU D. AndikaUmoja ama wingi kwa maneno yafuatayo.
UMOJA WINGI
Badili sentensi zifuatazo kuwa katika wakati ujao.
v. Anaimba vizuri …………………………………………………………………………….
5. SEHEMU E, Methali, Nahau na Vitendawili.
Toa maana ya nahau zifuatazo.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 62
MTIHANI WA KISWAHILI DRS IV
SEHEMU A:IMLA
1__________________________________________________
2__________________________________________________
3__________________________________________________
4__________________________________________________
5__________________________________________________
SEHEMU B:CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI NA
UANDIKE HERUFI YAKE
SEHEMU C:METHALI ,NAHAU NA VITENDAWILI
(KITENDAWILI)
SEHEMU D:ANDIKA NENO MOJA BADALA YA KIFUNGU CHA HABARI ULICHOPEWA
UFAHAMU
SOMA HABARI KISHA JIBU MASWALI YAFUATAYO.
Mwalimu alisema wanafunzi wanaweza kujieleza kupitia sanduku la maoni na mikutano ya shule. Alisema hivi karibuni, kutakuwa na baraza la shule, hata hivyo mwalimu alitahadharisha kwamba uhuru wa kujieleza una mipaka yake. Haturuhusiwi kutoa maneno ya kashfa kuhusu wengine kwani ni haki ya kila mtu kuheshimiwa.
MASWALI
21. Mwalimu alitahadharisha kwamba uhuru wa kujieleza una __ (A)maoni yake (B) mipaka (C) masharti yake (D) faida zake
22. Mwalimu alieleza ni_______kila mtu kuheshimiwa .
(A) haki (B) halali (C) lazima (D) faida
23.Wanafunzi wanaweza kujieleza kupitia__________
(A) mikutano tu (B)kwenye runinga (C) kisanduku cha maoni na mikutano ya shule (D)kisanduku tu
24.Tunapojieleza kuhusu wengine haturuhusiwi kutoa maneno ya ______(A)kufurahisha (B)uwongo (C)kuumiza (D)kashfa
25.Neno tahadhari kama lilivyotumika katika kifungu hiki cha habari lina maana gani? (A )Kuwa makini (B)kuwa tayari (C)kuonya (D) B na C ni majibu
MAJIBU
IMLA
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 61
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA DARASA LA NNE
KISWAHILI
MUDA:1: 30
JINA_____________________________________SHULE__________________
SEHEMU A.
1. Sikiliza kwa makini kisha andika Sentensi Kwa Usahihi
SEHEMU B. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA
SEHEMU C. LUGHA YA KIFASIHI
SEHEMU D. UTUNGAJI
4. Panga sentensi zifuatazo katika mtiririko unaofaa ili kupata habari iliyokamilika kisha uzipe herufi A,B,C, D na E.
SEHEMU E. UFAHAMU
5. Soma kifungu kifuatacho kisha jibu maswali
Madini ni maliasili inayotupatia fedha nyingi. Tunayo machimbo ya dhahabu na almasi. Pia kuna ulanga na bati. Dhahabu hutumika kutengeneza mapambo kama vile bangili, hereni, mikufu na pete. Ni vizuri kila mtu aelewe faida ya kutunza kila maliasili tuliyo nayo. Wanyama wakitunzwa huzaliana vizuri. Miti ikitunzwa vizuri hukua haraka. Tukitunza misitu nayo itatutunza. Itatupatia mvua ya kutosha, hewa safi na miti ya mbao na ya kujengea. Tunatakiwa tusubiri muda mrefu vitu vizaliane. Mvumilivu hula mbivu. Tukazane kupanda miti karibu na nyumba zetu ili kuzuia upepo usiharibu mapaa ya nyumba.Amani anaishi na nani?................................
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 56
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA
MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA DARASA LA NNE
KISWAHILI
MUDA:1: 30
JINA_____________________________________SHULE__________________
SEHEMU A.
1. Sikiliza kwa makini kisha andika Sentensi Kwa Usahihi
SEHEMU B. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA
2. Chagua jibu lililosahihi na uandike herufi yake katika kisanduku
i. Kuku, bata, njiwa, kunguru na mwewe kwa jina moja huitwaje?____________
ii. Ugonjwa ulienea kwa kasi. Badili sentensi hii katika wingi.
iii. Wanakijiji wengi.................. mkutano ule.
iv. Amosi si mwanafunzi mtiifu. Yakinisha sentensi hii.
v. Neno lipi ukidondosha Herufi moja linabakiza neno UJUZI?
SEHEMU C. METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
Tumia maneno yaliyo kwenye kisanduku kujibu maswali haya.
SEHEMU D. UTUNGAJI.
Weka alama za uandishi katika sentensi hizi
SEHEMU E. UFAHAMU
5. Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali kwa usahihi.
Amina na Ali ni pacha. Wanaishi katika kgiji cha Kamachumu. Wote ni wanafunzi katika shule ya Msingi Izigo. Kila siku huamka mapema na kujiandaa kwenda shuleni. Kabla ya kwenda shuleni, huwasalimia wazazi wao. Baada ya hapo, huagana nao na kuelekea shuleni. Wafikapo shuleni, huungana na wenzao kufanya usafi. Kisha huingia darasani na kuanza masomo. Watoto hawa wanapendwa na walimu wao kwa sababu ni watiifu.
Maswali
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 43
WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
MTIHANI WA KUJIPIMA
DARASA LA NNE
NUSU MUHULA WA PILI, SEPT 2021
SEHEMU A: IMLA
Sikiliza kwa makini sentensi zifuatazo kisha uziandike kwa usahihi.
SEHEMU B: SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA.
6…………….ili wekewa mbolea ili istawi.
7……………..inanyesha.
8.Ali alifunga…………..yote.
9……………anataga mayai.
10. Mtoto wa kuku anaitwa…………
SEHEMU C: VITENDAWILI, METHALI NA NAHAU.
Jaza nafasi zilizoachwa wazi.
11.Subira huvuta………..
12. Ukiyastaajabu ya musa…………
13. Mkono mtupu…………
14. Mwamba ngoma…………..
15. Mkuki kwa nguruwe,…………..
16. Nahau “kuandaa meza” ina maana gani?...............
17. Kitendawili kisemacho “kaa hapa nikae pale tumfinye mchawi” jibu lake ni lipi?............
18.Kitendawili kisemacho “Watoto wa mfalme ni wepesi sana kujificha” jibu lake ni lipi?................
19.Nahau “kugonga mwamba” maana yake ni ipi?..............
20.Mjomba hataki tuonane” jibu la kitendawili hiki ni?..................
SEHEMU D: UFAHAMU
Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali kwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi.
Dada, kaka na mimi tulisafiri kwenda Manda. Tuliondoka Dodoma kwa gari hadi Kyela kwa kupitia Morogoro na Iringa.
Kyela ipo katika mkoa wa Mbeya. Tulipofika Kyela tulilala na asubuhi yake tulikwenda Itungi. Huko ndiko tulikopanda meli na kuelekea Manda. Kabla ya kufika Manda tulipitia Lupingu. Tulianza safari ya melini saa moja asubuhi na ilichukua muda was aa nane kufika hadi Manda.
Maswali
21.Ndugu ………….walikuwa wanasafiri kwenda Manda.
22.Ndugu hao walisafiri kwa…………..kutoka Itungi.
23.Kyela ipo katika mko wa…………..
24. Safari ya kutoka Itungi hadi Manda ilichukua saa………….
25. Safari yetu kwa meli ilianza bandari ya………..
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 38
OFISI YA RAIS
WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MITIHANI YA KUJIPIMA MSINGI
MTIHANI WA NUSU MUHULA WA KWANZA -MACHI 2021
KISWAHILI – DARASA LA NNE
FOMATI MPYA
MUDA 1:30 MASAA MACHI 2021
JINA …………………………... SHULE ………………………...
MAELEZO
Jibu maswali yote
IMLA
MATUMIZI YA LUGHA
(i) Mwombeki alikuja na Kyoma.Sentensi hii katika wakati ujao itakuwaje?______________ [ ]
(ii) Kanusha sentensi hii.Mjuni hufuga samaki bwawani_____ [ ]
(iii) Nomino SOMO ikibadilishwa kuwa tendo tutapata nini?_[ ]
(iv) Wananchi wengi__________mkutano ule [ ]
(v) Ni neno lipi tunalipata tukidondosha herufi moja ya neno KABATI
A. Kaba B. kabari C.kaati D. bakati [ ]
METHALI,NAHAU NA VITENDAWILI
Kamilisha methali,nahau,na vitendawili vifuatavyo kwa kuchagua jibu sahihi kutoka kwenye mabano.
UTUNGAJI
Zipange sentensi zifuatazo katika mtiririko unaoleta maana.Anza na ya kwanza kwa kuzipa herufi A hadi ya mwisho herufi E
UFAHAMU
Ilikuwa siku ya Jumamosi nilipohudhuria harusi ya dada yangu Sinta. Siku hiyo watu wengi walifika katika ukumbi uliopo Sakina wakiwemo majirani wetu. Rafiki yangu Hassani hakuweza kufika kwa sababu alikuwa mgonjwa. Ugonjwa wa Malaria ulikuwa unamsumbua mara kwa mara. Hata hivyo wazazi wake walishiriki katika sherehe hiyo. Watu walikula na kunywa kwa furaha. Sherehe ilimalizika usiku.
Jibu maswali haya;
a) Ugonjwa wa malaria b) Ufahamu [ ]
c) Jibu maswali haya d) Harusi ya Sinta
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 29
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA
MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA DARASA LA NNE
KISWAHILI
MUDA:1:30
JINA_____________________________________SHULE_________________________
SEHEMU A: IMLA(ALAMA 10)1.Sikiliza kwa makini sentensi utakazo somewa na mwalimu kisha uandike kwa usahihi
i.______________________________________________
ii. _____________________________________________
iii. ____________________________________________
iv. ____________________________________________
v. _____________________________________________
SEHEMU B: MSAMIATI, SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA10)2.Chagua jibu kwa kuandika heruf iya jibu sahihi katika mabano
i.Tulishuhudia _______ ikimiminika juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro
A. theluji
B. theruji
C. dheluji
D. dheruji
ii. _________ ni vifaa tunavyo tumia majumbani
A. samani
B. thamani
C. zamani
D. dhamani
iii. “Wanafunzi waliosoma“ sentensi hii ipo katika wakati gani?
A. ujao
B. timilifu
C. uliopo
D. uliopita
iv. Mtoto aliyezaliwa bila pua huitwa _____________
A. toinyo
B. kigego
C. kiziwi
D. bubu
v. Neno“ nadra‘ lina jumla ya konsonati ngapi?
A. tano
B. mbili
C. sifa
D. tatu
SEHEMU C: LUGHA YA KIFASIHI (ALAMA 10)3. Kamilisha methali, vitendawili na nahau zifuatazoi.
i. Kuku mgeni ___________________________________________________________
ii. Viti vyote nimekalia isipikuwa hicho ________________________________________
iii. Mgaagaa na upwa _____________________________________________________
iv. Nyumba yangu inanguzo moja ___________________________________________
v. John amevaa chupa maneno“amevaachupa“yana maana gani? _________________________________________________________________
SEHMU D: UTUNGAJI (ALAMA 10)4.Panga sentensi zifuatazo katika mtiririrko uliosahihi kwa kuzipa herufi A, B, C, na E.
i. Alizaliwa mjini namtumbo( )
ii.Alijiunga na jeshi la Wananchi mara baada ya kumaliza shule()
iii. Amina ni mtoto pekee wa bwana na bibi Kazimoto ()
iv. Alisoma shule ya msingi kawekamo jijini Mwanza ()
v. Kwasasa ni mwanajeshi wa jamhuri ya muunganowa Tanzania ()
SEHEMU E: UFAHAMU (ALAMA 10)Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata
Dunia imesimama,Huzuni imetawala.
Korona nihimahima, Hakuna hata kulala,Sadiki sioukoma, Hakuna hata kulala
Tahadhari chukueni, korona epukeni
MASWALI
i.Taja vina vyakati na mwisho katika shairi ulilosoma _______________
ii. Neno “ Sadiki” kamali livyotumika katika shairi lina maana gani ______________
iii. Shairi lina mizani mingapi ___________________
iv. Andika kituo cha shairi ulilosoma ____________________
v. Shairi lina mishororo mingapi ___________________
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 22
THE PRESIDENT’S OFFICE
MINISTRY OF EDUCATION, LOCAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT
KISWAHILI- AUGUST-SEPTEMBER
STD FIVE
TIME: 1.30 HRS 2020
NAME:_______________________________________CLASS:___________
MAELEZO
1.Mtihani huu una sehemu A,B,C,D na E yenye jumla ya maswali 45.
2.Jibu maswali yote.
3.Huruhusiwi kuingia na simu au matini yoyote kwenye chumba cha mtihani. 4.Zingatia usafi katika kazi yako.
SEHEMU A: SARUFI
Katika swali la 1-20, weka kivuli katika herufi ya jibed lililo sahihi katika karatasi yako ya kujibia.
1.Sweta langu limeshonwa na fundi mzoefu. “Mzoefu” ni aina gani ya neno?
A. Kielezi
B. Kivumishi
C. Kiunganishi
D. Nomino
E. Kitenzi
2.“Ningejua ukweli wa mambo kabla ____ hapa bure saa hizi”. Neno gani linakamilisha sentensi hiyo?
A. nisingalikuja
B. ningekuja
C. singelikuja
D. nisingelikua
E. nisingekuja
3.“UKIWMI unaua!” Mbunge alisema. Ipi ni kauli taarifa ya sentensi hiyo kati ya hizi zifuatazo:-
A.Mbunge aliwaambia UKIMWI unaua
B.Mbunge alisema UKIMWI unaua.
C.UKIMWI unaua, mbunge alisema.
D.Mbunge alisema kwamba UKIMWI unaua.
E.Mbunge alieleza UKIMWI unaua.
4.“Anna anatembea polepole ______ twiga” Kifungu kipi cha maneno kina kamilisha sentensi hiyo?
A. mithili ya
B. mathalani ya
C. mahadhi ya
D. mathiri ya
E. madhali ya
5.Neno lipi halilandani na maneno mengine miongoni mwa haya yafuatayo?
A. Msonge
B. Tembe
C. Daraja
D. Kibanda
E. Ghorofa
6.Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo ni kauli ya kutendea?
A. Watoto wanacheza mpira.
B. Mpira unachezwa na watoto
C. Watoto wanachezeana mpira
D. Watoto wanachezea mpira
E. Mpira unachezeshwa na watoto
7.“Tumejifunza ____ kujikinga na VVU na UKIMWI.” Kifungu kipi cha maneno kati ya vifungu vifuatavyo kinakamilisha sentensi hiyo?
A. ibara ya
B. jinsi ya
C. jinsia ya
D. hali ya
E. aina ya
8.Neno “Mazingaombwe” lina silabi ngapi?
A. sita B. Saba C. tano D. nne E. Tatu
9.Kisawe cha neno “dhiki” ni kipi kati ya maneno yafuatayo:-
A. karabu B. raha C. shida D. adha E. faraja
10.Watafunga shule mwezi ujao. Mtenda katika sentensi hii ni. A. Sisi B. Mimi C. Yeye D. Wao E. Yule
11.“Yeye ndiye mwizi aliyepigwa jana jioni.” Sentensi hii ni aiana gani?
A. Sahihi B. changamano C. Ambatano D. Shurutia E. Tegemezi
12.Hotuba ya Mwenyekiti iliwatia moyo wanakijiji “Kutia moyo” maana yake ni:-
A. kutia hamasa
B. kuhuzunisha
C. kukasirisha
D.kuchochea moto
E. kuchangamsha
13.“Bwana Jitihada alijenga ua mkubwa kuzunguka nyumba nzima. “Wingi wa neno ua ni:-
A. Ua
B. nyua
C. Maua
D. Viua
E. Uani
14.Nimenunua pete yenye ____ kubwa.
A. Zamani
B. dhamani
C.thamani
D. samani
E. bei
15.Katika neno “tutakuja” kiambishi cha wakati ni____
A. Tu B. –ku- C. –ja- D. –u- E. –ta-
16.Katika sentensi zifuatazo ipi ni sahihi?
A.Kuku yangu ametaga mayai B.Kuku zangu zimetaga mayai
C. Kuku wangu wametaga mayai
D. Kuku wangu hutaga miyai
E. Kuku zangu ametaga mayai
17.Mwalimu wetu wa somo la Kiswahili ni muungwana sana. Neno “ni” limetumika kama aina ipi ya kitenzi?
A. kitenzi kisaidizi
B. kitenzi kikuu
C. kitenzi kishirikishi
D. kitenzi kitegemezi
E. kitenzi tegemezi
18.Kikombe kimevunjika. Sentensi hii iko katika kundi lipi la ngeli za nomino? A. ki-vi, B. u-zi C. li-ya D. zi E. a-wa
19.Asha anakula kwa kijiko. Neno “kwa” katika sentensi hiyo limetumika kama:-
A. kivumishi
B. kielezi
C. kihusishi
D. kitenzi kisaidizi
E. kitenzi kishirikishi
20.Wingi wa neno cherehani ni upi kati ya maneno yafuatayo?
A.Vyelehani
B. vyerehani
C. vyerahani
D. vyelahani
E. cherehani
SEHEMU B: LUGHA ZA KIFASIHI
Chagua herufi ya jibu sahihi kasha weka kivuli herufi hiyo mbele namba ya swali katika karatasi ya kujibia.
21.Usiache mbachao kwa mswala upitao. Methali ambayo inauhusiano nahii ni ipi?
A. Ufalme kama mvua hupiga na kupita.
B. Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha.
C. Ukiwanalako, usitazame la mwenzio.
D. Ujananitembo la nazi, halikuwahikupita.
E. Usishindane na kari, kari ni mjawa Mungu.
22.Maana ya nahau isemayo “Vunjika moyo” inafananishwa na:-
A.Kupata ugonjwa wa moyo
B. Kupasuka moyo
C. Kukereketwa moyo
D. Kusinyaa moyo
E. Kata tamaa
23.Kukubali kwa ulimi ni msemo wenye maana ipi?
A. Kukubali kwa dhati
B. Kukubali bila kusema neno
C. Kukubali kimoyomoyo
D.Kukubali kwa moyo mmoja
E. Kukubali kwa maneno.
24.Tegua kitendawili hiki. “Uzi mwembamba umefunga dume kubwa.” A. Usingizi B. Mawingu C. Ndoto D. Mvua E. Ugonjwa
25.Neno lipi linakamilisha methali isemayo “_____Janga hula na wakwao”
A. Mchuma B. Mpata C. Muona D. Mpewa E. Mnunua
26.“Maneno mengi hula vitendo. “Kati ya tafsiri zifuatazo ipi inayotoa maana sahihi ya msmo huo?
A.Ukifanya kazi bila kuhusisha jambo jingine itakamilika kwa wakati.
B. Fanya kazi kwa bidii
C. Dalili ya mvua ni mawingu
D. Kutoa ni moyo sio utajiri
E. Ukifanya kazi kwa bidii utapata faida kubwa
27.Ukitaka kuruka agana na nyonga. Methali hii ina toa funzo gani?
A. fikiri kwanza kabla ya kutenda jambo lolote
B. asiye na nyonga haruki angani
C. huruhusiwi kuruka kabla ya kuuliza nyonga
D. pima nyonga zako kwanza kabla ya kuruka
E. tusikubali kuruka kabla ya kuuliza
28.Methali “kidole kimoja hakivunji chawa” inafanana na ipi kati ya zifuatazo? A.Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
B.Haraka haraka haina Baraka
C.Penye miti hakuna wajenzi
D.Usiache mbachao kwa msala upitao
29.Methali isemayo “chanda chema huvikwa pete” inakinzana na methali ipi kati ya zifuatazo?
A. asiye kujua hakuthamini
B. mchumia juani hulia kivulini
C. samaki mkunje angali mbichi
D. aisifuye mvua imemnyea
E. bandu bandu humaliza gogo
30.Ukumbuu wa babu mrefu. Jibu la kitendawili hiki ni lipi?
A. njaa B. kisogo C. shingo D. ugonjwa E. ulimi
SEHEMU C: USHAIRI
Soma shairi lifuatalo kisha jibu swali la 31-36 kwa kusiliba alama yenye jibu sahihi mbele ya namba ya swali kwenye karatasi ya kujibia. I.Si mali wala elimu, hadhi ya mtu matendo, Kifuku hata msimu, enenda mwema menendo, Wanaopenda kaumu, nao wakupe mapendo, Hadhi ya mtu matendo, si mali wala elimu. II.Matendo yaliyotimu, yasiyomapindopindo, Yanufaisha elimu, Katika wao mkondo, Ukitenda kiwazimu, mavuno yake uvundo, Hadhi ya mtu matendo, si mali wala elimu.
Maswali
31.Vina vya kati na vya mwisho vya shairi hili ni ......A. Ndo na mu B. mu na mu C. mu na ndo D. Hadhi na elimu E. u na o
32.Mshairi anaeleza kwamba, ukitenda mambo kiwazimu matendo yako yatakua A. Elimu B. Isimu C. Uhondo D. Kidogo E. Uozo
33.Neno hadhi kama lilivyotumika katika shairi lina maana ya .... A. mali B. heshima C. Upendo D. amani E. mapindopindo
34.Mstari mmoja wa shairi huitwa ..... A. Mzani B. Mshororo C. Kituo D. KinaE. Kituo bahari
35.Kichwa cha shairi hili kinafa kiwe....... A. Matendo ya watu B. Elimu C. Kupata elimu D. Kupata mali
36.Kiitikio katika shairi hili ni ..........A.Matendo yaliyotimu, yasiyomapindopindo B.Yanufaisha elimu, Katika wao mkono C.Ukitenda kiwazimu, mavuno yake uvundo D.Hadhi ya mtu matendo, si mali wala elimu E.Hadhi ya mtu matendo, matendo yaliyotimu
SEHEMU D: UTUNGAJI/UANDISHI WA HABARI NA BARUA
Panga sentensi zifuatazo katika mtiririko mzuri wa mawazo kwa kuzipa herufi A,B,C na D na kusiliba herufi hizo mbele ya namba ya swali husika kwenye karatasi yako ya kujibia.
37.Alizaliwa Mkoani Mara mwaka 1922.
38.Taifa halitamsahau kwani amejenga misingi imara ya amani na utulivu 39.Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndiye Baba wa Taifa.
40.Alisoma nchini elimu ya msingi na sekondari na baadaye alipata shahada ya uchumi na historia huko Uingereza.
SEHEMU E: UFAHAMU
Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali yafuatayo kwa kumalizia sehemu iliyoachwa wazi.
Kwa namna moja au nyingine binadamu hupenda burudani. Burudani zipo za aina nyingi mathalani uogeleaji, kutazama televisheni na michezo kadhaa na kadha. Pamoja na burudani zilizokwishaainishwa, muziki ni burudani ambayo hukonga nyoyo za binadamu na hata wanyama. Muziki huweza kumtoa nyoka pangoni na kumtuliza panya kwenye utambaa panya. Muziki ni zaidi ya burudani kwani humsheheneza binadamu hisia mbalimbali za jana, leo na kesho. Muziki huleta furaha, muziki huleta karaha, muziki ...... Wewe acha tu hata kichanga mja hutikisa kichwa.
MASWALI
41.Kuogelea, michezo, kutazama televishen ni aina mbalimbali za ......
42.Neno gani limetumika kumaanisha mtoto aliyezaliwa hivi karibuni?..............................................................................................
43.Andika neno moja linalomaanisha aina ya burudani inayozungumziwa katika habari hii ........................................
44.Andika neno lenye maana sawa na neno “mathalani” kama ilivyotumika katika habari hii ...............................................
45.Muziki huleta furaha na vilevile huleta ....................................
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 20
OFISI YA RAIS
WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
KISWAHILI- AUGUST-SEPTEMBER EXAM
DARASA LA NNE
MUDA : Saa 1 na NUSU
JINA LA MWANAFUNZI___________________________________
JINA LA SHULE___________________________________________
MKOA_________________________________________________________
WILAYA_________________________________________________
MAELEZO
SEHEMU A: IMLA
1.Sikiliza kwa makini sentensi zinazosomwa na msimamizi wa mtihani kisha uziandike kwa usahihi.
i.______________________________________________________________
ii._______________________________________________________________
iii._______________________________________________________________
iv._______________________________________________________________
v.______________________________________________________________
SEHEMU B: MSAMIATI, SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA
2.Chagua jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye kisanduku:i.Neno Mchwalinaundwa na silabi zipi?
(a). M, c,h,w,a
(b). M,chwa
(c). M, ch, w, a
(d). M, ch,wa
ii.Neno HESHIMA lina irabu ngapi?
(a). Sita
(b). Tatu
(c). Mbili
(d). Tano
iii. Neno lipi kati ya linaweza kuundwa kwa kudondosha silabi moja katika neno MWALIMU?
(a).Elimu
(b). Wali
(c). Walimu
(d). Mwali
iv.Lipi kati ya maneno yafuatayo halifanani na mengine?
(a). Mbuni
(b). Kunguru
(c). Bundi
(d). Nzige
v.Yakinisha sentensi hii: “Elimu haina mwisho”
(a). Elimu siyo mwisho
(b). Kusoma kuna mwisho
(c). Elimu nimwisho
(d). Elimu ina mwisho
SEHEMU C: METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
3.(a). Kamilisha methali zifuatazo
.i.Umoja ni nguvu_____________________________________
ii.____________________________________ yasiyokuwa na mbu.
(b).Tegua vitendawili vifuatavyo
(iii). Fuu funika fuu funua_________________________________
(iv). Baba kafa kaniachia pete ______________
(c). Nahau kata shauri ina maana gani? ______________
SEHEMU D: UTUNGAJI
4.Weka alama za uandishi katika sehemu zilizoachwa wazi
Mfano: Unaitwa nani?
i.Mimi ni mwanafunzi ______
ii.Je, unasoma wapi_______
iii.Juma _____Anita na Jenifa wanasoma darasa la nne.
iv. Loooh_______ maji yamemwagika.
v.“Acheni kupika kelele_______Mwalimu alisema
SEHEMU E: UFAHAMU
5.Soma kwa makini hadithi ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuataHapo zamani za kale kulitokea mgogoro mkubwa sana kati ya ndege na wanyama. Juhudi zote za kumaliza mgogoro huu zilionekana kugonga mwambana hatimaye vita ilianza. Wakati majeshi hayo mawili ya wanyama na ndege yakijiandaa kupigana, popo alisita kuchagua upande wa kujiunga nao kivita. Jeshi la ndege lilifika nyumbani kwa popo na kumwambia “ Twende vitani ewe popo ndege mwenzetu”Popo alikataa na kusema “ Mimi ni mnyama na si ndege kama ninyi”. Baadaye jeshi la wanyama nalo lilifika nyumbani kwa popo na kumwambia “ Twende vitani ewe popo mnyama mwenzetu”. Popo alikataa tena na kujibu “ Mimi ni ndege na wala si mnyama kama ninyi”. Basi kukawa na ngurumo za kutishaza wanyama shupavukama vile simba, duma na tembo, na ndege shupavu kama vile tai na mbuni. Majike wenye ndama na majike wenye makinda walihisi kiama chao kimefika. Kwa bahati nzuri sana, katika dakika za mwisho kuelekea vita, muafakaulifikiwakati ya pande hizo mbili na vita ikaepukwa. Kukawa na amani badala ya mapigano. Makundi yote mawili yakawa na shamrashamraza kusherehekea kuepukana na mgogoro. Kuona hivyo, popo naye alitamani kuwa sehemu ya shamrashamra hizo. Alikwenda kwa ndege akitakakujiunga nao lakini ndege walimfukuza. Baadayae akaenda kwenye kundi la wanyama nao walimfukuza. Popo akabaki kuwa njia panda kwani hakuruhusiwa kujiunga na kundi la ndege au kundi la wanyama.
MASWALI
i.Mgogoro uliotokea hapo zamani uliwahusu akina nani?__________________________________________________
ii.Nini maana ya nahau kugonga mwambakama ilivyotumika katika hadithihapo juu?________________________________________
iii.Neno kiamakatikahadithi hapo juu lina maana gani?_____________________________________________________
iv.Neno lipi katika hadithi uliyosoma hapo juu lina maana sawa na neno shangwe?__________________________________________
v.Nani alibaki njia panda?______________________________________Kwanini?_______________
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 15
OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA MWISHO MWAKA-KISWAHILI
DARASA LA NNE
MUDA: 1.30 2020
JINA:_______________________________MKONDO:___________
MAELEKEZO
SEHEMU A:
IMLA:
Sikiliza kwa makini sentensi utakazosomewa kisha uziandike kwa usahihi
SEHEMU B: MATUMIZI YA LUGHA
Chagua herufi ya jibu sahihi
6. Neno lipi halilandani na mengine
7. Ni neno lipi haliwezi kutokana na jina mwanchi?
8. Yupi kati ya hawa ni lazima awe mwanamke?
9. Tukitaka kufaulu mtihani yetu_________________ kusoma kwa bidii
10. Wamekuja wote_______________ Munira ambaye anaumwa
SEHEMU C: LUGHA YA KIFASIHI
11. Malizia methali hii, Ukitaka kuruka _________________
12. Japo kuna maktaba nyumbani kwao lakini Joni hapendi kukaa na kujisomea, mara nyingi Juma huenda kwa akina Joni kuomba muda japo kidogo apate kusoma vitabu. Juma anatamani mno kuwe na maktaba nyumbani kwao lakini wazazi wake hawana uwezo huo. Methali ipi inafaa kwa maelezo haya
13. Mwenyekiti ameahirisha kikao baada ya wajumbe kuja wamevaa miwani,
nahau vaa miwani ina maana gani?
14. Andika nahau iliyo kinyume na ile isemayo tia moyo____________
SEHEMU D: UTUNGAJI
Weka alama za uandishi katika sentensi zifuatazo kwa kuandika alama sahihi katika nafasi iliyoachwa wazi
15. Utamaliza kazi yako saa ngapi ______________
16. Ebo amemaliza ugali wote ule………………..
17. Juma Sharifu na Ayubu wamegombana…………..
18. Shangazi amekwenda kumpokea baba___________
19. Watoto wataletwa na nani………….
SEHEMU E: UFAHAMU
Soma habari ifuatayo kwa makini kisha jibu maswali yafuatayo
Tulianza safari alfajiri ya saa kumi na moja.Ulikuwa ni umbali wa kilomita
sitini kutoka pwani hadi kwenye mazalia ya samaki. Baada ya kufika mjengi alitushauri tutege nyavu chache tu kwani hali ya hewa haikuridhisha. Baada ya kutega tulianza safari ya kurudi pwani . Ghafla tulipigwa na dhoruba . Jahazi
lilianza kuyumba na tanga letu likararuka. Haraka mimi na Mwekwa tulitweka tanga la akiba na kulifunga chapuchapu. Msengi na Hongoa walichukua buli na kuanza kutoa maji yaliyokuwa yanaingia jahazini. Tulipata shida mno, baada ya siku mbili majini tuliwasili salama pwani. Tuliponea chupuchupu, tulikata tamaa na kusubiri miujiza ya Maulana ili tubaki hai.
MASWALI
20. Msimuliaji wa habari hii na wenzake wanafanya kazi gani? __________
21. Kulikuwa na watu wangapi katika jahazi ?__________
22. Kitambaa maalumu kinachofungwa katika jahazi ili kulisaidia kutembea kinaitwaje?_________
23. Andika nahau moja iliyotumika katika habari hii _________
24. Taja kisawe cha neno Maulana kama lilivyotumika katika habari hii
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 9
OFISI YA RAISI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA KUJIPIMA DARASA LA NINE
APRILI-2020 MUDA:SAA 1:30
KISWAHILI
MAELEZO KWA MTAHINIWA
SOMA HABARI IFUATAYO KISHA UJIBU MASWALI.
Hapo zamani palikuwa na watu waishio katika kijiji kimoja kiitwacho shukajeni. Siku moja kijiji hicho kilipatwa na kipindi cha njaa ambapo hawakuwa na chakula cha kula ilikupata nguvu ya kuwinda wanyama. Ikatokea mvulana mmoja ambaye alikuwa shujaa katika kijiji kingine ambacho kilikuwa jirani na Shukajeni . Alipo ingia katika shukajeni alisali na kuomba dua hadi kijiji hicho kikapata chakula cha kula na kupata nguvu.
Kisha mvulana huyo shujaa akafanywa kuwa kiongozi wa kijiji hicho.
JIBU MASWALI YAFUATAYO.
1.Katika kijiji hicho kazi yao ilikuwa nini? …
2.Kipindi gani kilizuka katika kijiji hicho? … … … … … … ..
3.Kwa nini mvulana aliye kuja katika kijiji cha Shukajeni aliteuliwa kuwa kiongozi? … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … .
4.Umejifunza nini kutokana na habari uliyoisoma? … … … … … … … … … … … … .....
5.Jiji lao lilikuwa laitwaje? … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … .
TUNGA SENTENSI KWA KUTUMI A MANENO YAFUATAYO.
6. shujaa … … … … … … … … … … … … … … … … ..
7. kuwinda … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … …
8.njaa … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … …
9. kula … ....................................... ............... ....................... .............. ......
10. nguvu … … .
ANDIKA MANENO MANNE YANAYOWAKILISHWA NA NENO LA JUMLA
11. Vyombo
12. wanyama
13. vinywaji
14. kamusi
15. wachezaji
UTUNGAJI
16. Simulia sherehe uliyowahi kuhudhuria.
ZINGATIA YAFUATAYO:-
1. kichwa cha habari.
2. walioshiriki katika sherehe.
3. kitu kilicho kufurahisha
4. kitu kilicho kuchukiza
KANUSHA MANENO YAFUATAYO.
17. Sisi tunapenda nyama ya swala. … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … …
18. Mpoki alipanda mabasi ya mwendokasi. … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … .
19. Baba atarina asali yetu wiki ijayo. … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … .
20. Wote walishangaa kwa kifo chake. … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … .
21. Wazazi watawanunulia watoto wao sare za shule. … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … .
ANDIKA VITENDAWILI VYENYE MAJIBU YAFUATAYO.
22. Jogoo … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … …
23. ugali … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … …
24. macho … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … …
25. mlango … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … …
26. uyoga … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … .
27. utelezi … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … ....
OANISHA SEHEMU A’’ na B’’ kwa kuandika jibu sahihi.
28.unga mkono | A] kuwa mwangalifu |
29.kuwa macho | B]futwa kazi |
30.bega kwa bega | C]kushirikiana |
31.pigwa kalamu | D]fariki |
32.kata roho | E]kubaliana |
Swali | 28. | 29. | 30. | 31. | 32. |
Jibu |
LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD FOUR EXAM SERIES 2