OFISI YA RAIS, WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MITIHANI YA KUJIPIMA MSINGI
MTIHANI WA NUSU MUHULA WA KWANZA -MACHI 2021
URAIA NA MAADILI – DARASA LA TATU
FOMATI MPYA
MUDA1:30 MASAA MACHI 2021
JINA …………………………...SHULE ………………………...
MAELEZO
- Mtihani huu una sehemu Mbili A na B na jumla ya maswali matano
- Sehemu ya A ina alama 26 na sehemu B ina alama 24
- Jibu maswali yote kulingana na maelezo ya kila swali
- Mtihani wote una alama 50
SEHEMU A. ALAMA 26
Jibu maswali yote
1. Chagua jibu sahii kutoka chaguzi ulizo pewa
- Kuonyesha tabia nzuri kwa wengine kwa maneno na vitendo huitwa
- Kuongea
- Tabia mbaya
- Lugha ya adabu
- Lugha ya kihuni
- Kitu ambacho unatakiwa kukifanya au kukitekeleza kinaitwa
- Haki
- Jukumu
- Malengo
- Wajibu
- Kitu ambacho kila mtu anastahili huitwa?
- Jukumu
- Haki
- Upendeleo
- Ustaarabu
- Ipi kati ya hizi ni haki yam toto
- Kufanyizwa kazi
- Kupata elimu
- Kuchapwa
- Kutumikishwa
- Vitu venye dhamana zinazopatikana kwenye mazingira huitwa?
- Utajiri
- Fedha
- Rasilimali
- Mali
2. Umepewa jedwali A na Jedwali B. Chagua jibu sahihi kutoka jedwali B ambalo linaendana na maelezo katika jedwali A.
Jedwali A | Jedwali B |
- Lugha ya Taifa ya Tanzania
- Inaonyesha ustawi na uhuru
- Utamaduni
- Rangi ya kijani katika bendera yetu
| - Mwenge wa uhuru
- Kiswahili
- Ujumla wa Maisha ya watu
- Uoto wa asili
|
- Tumia maneno yaliyo kwenye kisanduku kujaza nafasi zilizowazi
Majukumu, Uvumilivu, Ustamilivu, Uaminifu |
- Kuwa mkweli na muwazi
- Vitu ambavyo mtu anastahili na anapaswa kupewa
- Uwezo wa kuishi na watu hata kama mnatofautiana kimawazo
- Uwezo wa kuvumilia au kujikwamua katika hali ngumu
SEHEMU YA B. ALAMA 24
JIBU MASWALI YOTE
3. Kamilisha jedwali lifuatalo kwa kujaza maana ya rangi za bendera ya Taifa
Rangi ya Bendera | Maana yake |
Kijani |
|
Manjano |
|
Samawati |
|
Nyeusi |
|
- Angalia mchoro hufuatao kwa makini kisha jibu maswali yafuatayo

- Taja alama ya Taifa ambayo imeonyeshwa hapo juu
- To umuhimu wa alama hii
- Alama hii utaipata wapi mara nyingi?
- Taja alama nyingine mbili za Taifa ambazo unaziona hapo juu
- Soma kifungu kifuatacho kisha jibu maswali yafuatayo.
Ni muhimu sana kutunza mwili wako, akili, na nafsi kila siku na sio tu wakati unaumwa. Hili linawezekana kwa kula vyema, kufanya mazoezi, kupunguza mawazo, na kwenda mapumuziko mwili unapohitaji. Mambo haya yatakufanya ukae mwenye furaha, mwenye afya na mstahilimilivu.
- Kifungu hiki kinahusu nini?
- Taja njia tatu za kutunza miili yetu
- Taja vitu vitatu tunapaswa kuzingatia hili kuwa na afya
- Unafikiria ni nini kitatokea kama tutashindwa kutunza miili yetu.