THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL
ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION
EXAMINATION
121/1 KISWAHILI 1
(Kwa Watahiniwa Walioko Shuleni na Wasiokuwa Shuleni)
Muda: Saa 3Jumatatu, 04 Mei 2015 asubuhi
Maelekezo
1. Karatasi hii ina maswali kumi (10) katika sehemu A, B, C, D na E.
2. Jibu maswali saba (7) kwa kuzingatia maelekezo kutoka katika kila sehemu.
3. Kila sehemu ina alama ishirini (20).
4. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.
5. Vikokotozi haviruhusiwi ndani ya chumba cha mtihani.
6. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.
SEHEMU A (Alama 20)
UFAHAMU
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Tunaarifiwa kwamba punde si punde baada ya mapinduzi, mambo yalibadilika hapo shambani. Mabadiliko hayo yalianza na maziwa kutoweka. Baadaye ilibainika kwamba maziwa hayo yalitengwa kwa matumizi ya nguruwe peke yao, na umuhimu wa matumizi hayo ukasisitizwa na nguruwe wote, hadi wanyama wengine wakakubali.
Baadaye nguruwe walijitengea vya tunu vyote, palipo na tufaha, hadi shayiri na pombe. Mambo yalipozidi kunoga upande wa nguruwe na kuzorota upande wa wanyama wengine, iliamuliwa ya kuwa ardhi iliyotengewa wanyama wazee-wastaafu ilimwe iii ipandwe shayiri za kutengenezea pombe, ulevi ulioruhusiwa kwa nguruwe peke yao. Mayai pia yaliliwa na nguruwe, na mengi kuuzwa kwa manufaa ya hao nguruwe.
Wanyama walionewa vya kutosha. Kuna baadhi ya wanyama waliohitaji chakula maalumu. Chakula hicho walikuwa wakipewa hata na dhalimu mchoyo, Mtiki. Kwa mfano, kuku walizoea kutiliwa maziwa katika chakula chao. Haya yote yalibadilishwa na viongozi wapya. Vyakula hivi ambavyo vilikuwa ni haki ya wanyama wote, sasa vililiwa na nguruwe tu. Wanyama wengine wote walianza kuisahau ladha ya maziwa, tufaha na tunu nyinginezo. Ladha ya pombe na mayai hawakuijua kamwe, kwa sababu hata enzi ya Mtiki, hakuna mnyama aliyeruhusiwa kuonja vitu hivi. Kinywaji hiki, pombe, kilikuwa ni cha tunu mno. Binadamu peke yao ndio walioionja.Walipogundua uhondo wake, nguruwe walifuata mtindo huohuo wa binadamu, wa kuwanyima wanyama wenzao cha tunu hicho. Tofauti hapa ni kwamba wakati wa Mtiki, wanyama hawakutoa jasho lao kupanda shayiri za kutengenezea pombe. Mtiki alipata pombe yake yote kutaa masoko ya nje ya shamba lake. Enzi ya utawala wa nguruwe, kwa upande mwingine, wanyama walifanya kazi ya kulima shayiri, lakini hawakuonjeshwa pombe hata tone moja. Waliondokea kuisikia harufu yake nzuri tu. Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu.
Tabia hii ya nguruwe ya lufwanyanyasa wanyama wengine ilipopevuka ikiambatana na takabari, wanyama wengine walizidi kunyimwa haki nyinginezo. Kwa mfano, mahali ambapo walikuwa wameshazoea kufanya kazi kulingana na uwezo wao, na kutarajia kupata chakula kulingana na mahitaji yao, hali ilibadilika sana hadi mwishowe ikawa ya kwamba wanyama wote, isipokuwa nguruwe na mbwa, walifanyishwa kazi hadi kifo. Aidha, walipunguziwa chakula chao mara nyingi hadi ikafikia kiwango cha kuwa wanafanya kazi nyingi ya sulubu huku wakiwa wamebanwa na njaa. Na mahali ambapo, hapo mwanzo walikuwa hawafanyi kazi Jumapili, mambo yalipozidi walitakikana wajitolee na kujihimu kila Jumapili; wote ambao hawakujitolea, posho yao ilipunguzwa zaidi. Haya yote yalitendeka mahali ambapo, mwanzo wa mapinduzi, waliahidiwa mapunziko, na si hivyo tu, walikuwa na faragha nyingi sana, faragha ambazo walikuwa hawakuzoeshwa enzi ya Mtiki.
Maswali
(a) Andika kichwa cha habari hii uliyosoma kwa maneno yasiyozidi matatu.
(b) Taja mabadiliko manne muhimu yaliyoelezwa katika habari uliyosoma yaliyotokea baada ya mapinduzi ukilinganisha na hali halisi katika nchi zinazoendelea.
(c) Toa maana za maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika habari uliyosoma.
(i) Tunu
(ii) Tufaha
(iii) Takabari
(iv) Kujihimu
(d) Taja matabaka mawili yaliyojidhihirisha katika utawala wa aina mbili aliouelezea mwandishi wa habari uliyosoma na jinsi tabaka moja lilivyonufaika dhidi ya tabaka jingine.
View Ans
2. Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua mia moja na hamsini.
View Ans
SEHEMU B (Alama 20)
MATUMIZI YA SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA
Jibu maswali mawili (2) kutoka sehemu hii.
3. Nini maana ya sentensi sahili na sentensi ambatano. Kwa kutumia mifano, onesha miundo minne kwa kila moja.
View Ans
4. Taja dhima tano za mofimu U kwa kutunga sentensi mbili kwa kila dhima.
View Ans
5. "Japokuwa Kiswahili kimefikia hadhi ya Kimataifa, kimatumizi bado hakijapata ridhaa ya kuwa lugha ya kufundishia mtaala wa elimu ya juu nchini Tanzania." Jadili kauli hii ukitoa hoja nne za msingi za kuzingatiwa iii lugha hii itumike kufundishia elimu ya juu.
View Ans
6. Fafanua dhana ya vivumishi vionyeshi na viwakilishi vionyeshi kisha kwa kutumia mifano, taja aina mbili za vionyeshi ukizingatia mashina yake.
View Ans
SEHEMU C (Alama 20)
UTUNGAJI
Jibu swali la saba (7)
7. Andika insha ya maneno yasiyopungua mia tatu na yasiyozidi mia nne kuhusu kauli isemayo "Kilimo Kwanza."
View Ans
SEHEMU D (Alama 20)
MAENDELEO YA KISWAHILI
Jibu swali moja (1) kutoka sehemu hii.
8. "Asili ya wabantu ni Afrika ya Magharibi." Thibitisha kauli hii kwa kuelezea hatua nne za kusambaa kwa wabantu kutoka Afrika ya Magharibi hadi Pwani ya Afrika ya Mashariki.
View Ans
9. "Utawala wa Mwingereza nchini Kenya ni chanzo cha mweneo mdogo na kudidimia kwa Kiswahili nchini humo." Fafanua dai hilo kwa kutumia hoja tano.
View Ans
SEHEMU E (Alama 20)
TAFSIRI
Jibu swali la kumi (10)
10. Kwa kutumia mifano, eleza faida tano zinazotokana na ukalimani kwa jamii ya Tanzania.
View Ans