THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION
121/1 KISWAHILI 1
(Kwa Watahiniwa Walioko Shuleni tuu)
Muda: Saa 3 Jumatano, 07 Februari 2011 asubuhi
Maelekezo 1. Karatasi hii ina maswali kumi na tatu (13) katika sehemu A, B, C, D na E.
2. Jibu maswali tano (5) kwa kuchagua swali moja kutoka kila sehemu.
3. Kila sehemu ina alama ishirini (20).
4. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.
5. Vikokotozi haviruhusiwi ndani ya chumba cha mtihani.
6. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.
SEHEMU A
HISTORIA
1."Ingawa wazungu ndio watu wa kwanza kukisanifisha Kiswahili lakini kwa upande mwingine wanastahili kulaumiwa na wazalendo wa lugha hii. "Toa hoja nne (4) kutetea madai hayo.
View Ans
2.Kwa kutoa mifano hai minne (4) eleza jinsi Kiswahili kama ilivyo kwa lugha yoyote kinavyokwenda na wakati.
View Ans
3."Shughuli zilizofanywa na Waarabu katika nchi za Afrika Mashariki zilikuza na kudumaza lugha ya Kiswahili". Toa hoja nne (4) kuthibitisha dai hilo.
View Ans
SEHEMU B
SARUFI 4. Fafanua dhana ya uwakilishi katika sentensi kwa kutoa mifano minne (4) kudhihirisha maelezo yako.
View Ans
5. Viambishi vijenzi katika lugha ni viambishi ambatishi na viambishi nyambuaji. Kwa kutumia mifano mitatu (3) kwa kila kiambishi eleza tofauti iliopo kati ya viambishi hivyo.
View Ans
6. Ainisha sentensi zifuatazo na eleza sababu za mwainisho wako:
(a) Ugonjwa wa UKIMWI hautibiki na wala kukingika.
(b) Ulifika na paka wako pwani ili paka wako anyooshe mwili wake na kupunga hewa safi.
(c) Lisemwalo lipo.
(d) Akiniamkia nitamwitikia. (e) Kalamu haina wino.
View Ans
SEHEMU C
MATUMIZI YA LUGHA 7."Lugha ya mazungumzo hutawaliwa na mada ya mazungumzo, wahusika katika mazungumzo hayo, na mahali.” Thibitisha usemi huo kwa kutumia mifano sita (6), yaani mifano miwili kwa kila kipengele.
View Ans
8.”Mjuzi wa lugha zaidi ya moja, ujuzi wake hauwezi kuwa wa kiwango sawa.” Fafanua sababu zinazoleta utofauti huo.
View Ans
9. Kwa kutumia mifano eleza maana, chanzo, aina na matumizi ya misimu katika Kiswahili.
View Ans
SEHEMU D
UTUNGAJI 10. Andika barua kwa Mhariri wa gazeti la Nipashe Ijumaa ya tarehe 18 Februari 2011, kumsifu mpokeaji simu wa Maktaba ya Taifa kwa huduma yake nzuri kwa wasomaji.
View Ans
11. Andika insha ya maneno yasiyozidi mia nne (400) na yasiyopungua mia tatu (300) juu ya wanafunzi wengi kushindwa somo la Hisabati.
View Ans
12. Kwa niaba ya wanafunzi wenzako wa Kidato cha Sita andika hotuba yenye maneno yasiyopungua mia tatu (300) ambayo itasomwa mbele ya mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Siku ya mahafali yenu.
View Ans
SEHEMU E
UFAHAMU 13. Soma habari hii kisha jibu maswali yanayofuata.
Siku ya pili Mzee Tindo hakuwa kama kawaidayake. Hakuwasemesha wenzake kwa bashasha kama ilivyo desturi yake. Alizungumza nao kikazi tu, na baada ya kumaliza aliondoka peke yake. Waliagana wakutane usiku Mlandege kwa safari ya kwa Morarji.
Wakati ulipofika wote walikutana pale walipoagana na walianza safari yao. Walilikuta lango kubwa la nyumba ya Morarji hapo Hurumzi liko wazi. Ukumbi wa jumba hilo ulikuwa uking'ara kwa mataa ya umeme yaliyoko katika kila ukuta wa kuta nne za ukumbi huo.
Morarji na mwenzake mmoja wa Kibaniani walikuwa wamekaa hapo ukumbini. Walikuwa wamekaa juu ya jukwaa lililotandikwa kwa mito iliyovishwa foronya nyeupe. Wote walikuwa juu ya mito hiyo ambayo ilikuwa Iaini kabisa. Walivaa mashati marefu ya bafta yaliyokuwa na vifungo mpaka kooni. Walivaa pia windanyembamba ambazo hazikuweza kuwasitiri vizuri.
Mbele yake Morarji palikuwa na sanduku zuri la mscüi. Morarji na mwenzake walikuwa wanazungumza Kibaniani. Mzee Tindo na wenzake walipofika mbele ya lango la nyumba hiyo walipata hofu kuingia ndani, lakini Rashidi bila ya kujali kitu chochote ndiye aliyekuwa wa mwanzo &1Lkiuka kizingiti cha lango hilo na kuingia ndani. Iliwabidi wenzake, yaani Farjalla na Mzee Tindo wamfuate, na wote kwa umoja waliingia ndani, na kukabiliana na Morarji uso kwa uso.
"Min nataka hapa" Morarji aliwauliza kwa sauti ya kijeuri. Mukki! Si umesema tuje kukuona leo usiku?" Mzee Tindo alijibu huku hofu imemjaa. Morarji hata hakujali, aliendelea kuzungumza Kibaniani na wenzake. Walizungumza kwa muda mrefu huku akina Rashidi na wenzake wakiwa wamesimama hapo mlangoni.
"Sasa nan nasema pesa hapana tosha? Wewe, wewe ...". Morarji aliuliza baada ya kuacha mazungumzo yake huku akimnyooshea kidole Rashidi na Farjalla ili kutaka kujua ni yupi hasa aliyesababisha matata. Farjalla kama hayupo, kimya kabisa, lakini Rashidi alijibu.
"Ndiyo Mukki pesa kidogo, hazitoshi". "Nani mwingine nasema pesa hapana tosha?" Morarji aliuliza tena.
Wote walinyamaza kimya wamenywea kama waliotiwa maji. Rashidimabega yalimpwaya alipohisi wenzake wamemtupa mkono.
"Basi kama wewe nasema pesa haitoshi kwenda tafuta kazi pahali ingine iko pesa mingi!". Morarji alimwambia Rashidi kwa fedhuli, kisha alimgeukia Mzee Tindo na kumwambia, "Tindo, hapana chukua yeye kazini tena, haya Jao!" Wote waliondoka na kuelekea makwao.
"Kujua kwingi huko, sasa unaona faida yake? Mzee Tindo alisema huku akimfanyia tashtiti Rashidi. Rashidi hakujibu kitu alinyamaza kimya na kufuata njia yake moja kwa moja mpaka kwao.
MASWALI
(a) Toa maana ya maneno yaliyopigiwa mstari katika habari hii.
(b) Mwandishi anatoa ujumbe gani kwa hadhira yake?
(c) Unafikiri ni kwanini Mzee Tindo hakuwa na bashasha kama ilivyokuwa desturi yake?
(d) Mwandishi anaposema "Wote walinyamaza kimya kama waliotiwa maji" unapata taswira gani katika usemi huo?
(e) Kwa maoni yako unakionaje kitendo cha Rashidi kukaa kimya na kuelekea kwao baada ya kufanyiwa tashtiti na Mzee Tindo?
View Ans