JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
MTIHANI WA KUHITIMU KIDATO CHA NNE
021 KISWAHILI
(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)
Muda: Saa 3 Mwaka : 2022
Maelekezo
Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C.
Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B alama arobaini (40) na sehemu C ina alama arobaini na tano (45).
Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye kijitabu chako cha kujibia.
(i) "Kushindana na mtu aliyekuzidi kwa kila hali si busara." Methali zifuatazo zinazashabihisha kauli hii isipokuwa:
Mwenye pesa si mwenzio
Nazi haishindani na jiwe
Chanda chema, huvikwa pete
Mwenye nguvu mpishe
Maji yakija kasi yapishe
Choose Answer :
Sababu: Methali "Chanda chema, huvikwa pete" haionyeshi uzito wa kuepuka kushindana na mtu mwenye uwezo mkubwa, bali inasisitiza kuthamini vitu vyenye thamani.
(ii) Neno linaloingizwa katika kamusi kwa wino uliokolezwa, fasili, matamshi na aina ya neno hilo kwa pamoja huitwaje?
Kidahizo
Kategoria
Fasili
Istilahi
Kitemoeo
Choose Answer :
(iii) Kikundi cha maneno kinachoonyesha jambo lililotendwa na mtenda katika sentensi hujulikana je?
Chagizo
Kitenzi
Kivumishi
Shamrisho
Nomino
Choose Answer :
(iv) Bainisha sentensi yenye vielezi zaidi ya kimoja katika sentensi zifuatazo:
Vitabu vyangu vyote vimeibwa na watoto wako.
Mbuzi aliyepotea jana ameonekana leo asubuhi.
Shule yetu inazawaza kushiriki mashindano?
Wengi walikuwa wanataka kwenda msomoni.
Wanajiji hawa wamefanya uchaguzi kwa amani.
Choose Answer :
(v) Pande mbili zinazohusika katika lugha ya mawasiliano ni zipi?
Mwandishi na msikilizaji
Msimulizi na msomaji
Mwandishi na mzungumzaji
Msomaji na msimuliji
Msomaji na mwandishi
Choose Answer :
Sababu: Mawasiliano katika maandishi yanahusisha msomaji anayepokea ujumbe kutoka kwa mwandishi.
(vi) Dhima ya vielegelele katika utendaji wa sanaa za maonesho ni ipi?
Kuishirikisha na kuiondoa hadhira udhia wa kumsikiliza mtu mmoja.
Hadhira kukata shauri juu ya mwendo wa kazi ya sanaa za maonesho.
Kuweka alama za mapigo ya kimuziki katika kazi ya sanaa za maonesho.
Kuonesha upeo wa furaha na burudani ya kazi ya sanaa za maonesho.
Kuonesha mbwembwe katika kazi ya sanaa za maonesho.
Choose Answer :
(vii) Njia ipi huhifadhi sauti pamoja na vidokezo vyake katika kuhifadhi kazi ya fasihi simulizi kati ya hizi?
Maandishi
Mikanda ya filamu
Mitandao
Kinasa sauti
Masimulizi
Choose Answer :
(viii) Jambo gani muhimu huzingatiwa na mtunzi wa insha ya hoja?
Lugha yenye ukinzani
Lugha isiyo na mvuto
Lugha ya kisanaa
Lugha ya kufikirisha
Lugha inayosifia
Choose Answer :
(ix) Zifuatazo ni kazi za alama ya uandishi nukta mkato (,) isipokuwa:
Kuonesha kwamba vitu vinavyofuata viko katika orodha.
Kuunga mawazo mawili tofauti katika sentensi.
Kuonesha kwamba kinachofuata ni ufafanuzi zaidi.
Kuunga mawazo mawili au zaidi katika sentensi.
Kutenga vifungu vya sentensi ambavyo ni ndefu.
Choose Answer :
(x) Kipi ni kipengele kinachohusu muundo wa kazi za fasihi?
Mitindo
Muundo
Mandhari
Wahusika
Lugha
Choose Answer :
2. Oanisha maana za tamathali za semi zilizotoka katika Orodha A na tamathali husika kutoka Orodha B, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.
Orodha A
Orodha B
(i) Ushangaji wa jambo fulani, aghalabu huambatana na alama ya mshangao.
(ii) Upangiliaji wa maneno katika namna ya kupingana ili kusisitiza mawazo fulani.
(iii) Ulinganishaji wa vitu viwili au zaidi vyenye sifa tofauti kwa kutumia viunganishi.
(iv) Uhusishaji wa kitu kisicho binadamu kupewa uwezo wa kutenda kama binadamu.
(v) Urudiaji wa neno, herufi au silabi ili kusisitiza jambo.
6. Wanafunzi wengi wa Kidato cha Kwanza huchanganya maana za tanzu na vipera vya fasihi simulizi. Ili kuwaondolea mkanganyiko huo, onesha tofauti iliyopo kwa kila seti (a) – (d) kwa kutoa maelezo mafupi na mfano kwa kila moja.
7. Ukiwa kama Afisa Utalii katika eneo lako, pendekeza namna utakavyokuzwa na kueneza lugha ya Kiswahili kwa wageni katika vipengele (i) hadi (iv) na kutoa mfano kwa kila moja.
8. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibe maswali yanayofuata:
Teknolojia ya Habari na Mawasiiiano (TEKNOHAMA) hutumiwa kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi: kuimarisha ufundishaji; uwazi na kuongeza ufanisi. TEKNOHAMA imetambuliwa na wataalamu wa elimu kuwa ni muhimu katika shughuli za ufundishaji na ujifunzaji. Lengo is kutumia TEKNOHAMA ni kurahisisha ufundishaji kwa sababu hudhihirishwa katika hall halisi kwa kutumia aina mbalimbali za TEKNOHAMA.
Dunia ya sasa imebadilika; na mambo ya kijamii na kiuchumi yanategemea sana mitandao ya kompyuta. Katika kipindi cha miongo mitano iliyopita mpaka sasa, matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano yamezidi kuenea katika elimu kote ulimwenguni.
Ili kufanikisha ufundishaji wa mada mbalimbali, mwalimu anahitaji kutumia TEKNOHAMA kwa ajili ya kupata taarifa na habari kutoka vyanzo mbalimbali, kuendeleza ujifunzaji unaompa mwanafunzi nafasi ya kati na kumpa mwalimu jukumu la kuwa mlezi na mwenezi badala ya We wa mjua vyote. Mwalimu wa karne hii anaweza kujihusisha na matumizi ya TEKNOHAMA katika ufundishaji wake darasani, hall inayoweza kumpa ahueni katika kazi yake.
Hata hivyo, katika nchi zinazoendelea walimu wengi hawatumii TEKNOHAMA katika ufundishaji. Hii inatokana na teknolojia hii kuhitaji muda, fedha na maarifa ya ziada kwa watumiaji. Hayo kwa jumla yanakwamisha utumiaji wa teknolojia hiyo katika elimu. Hivyo. hatuna budi kuhakikisha tunakabiliana na mambo hayo ili kuhakikisha teknolojia hiyo inatumika katika elimu ili kurahisisha mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji.
Maswali
(a) Bainisha matumizi manne ya TEKNOHAMA katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji kulingana na habari uliyosoma.
(b) Fupisha habari hiyo kwa maneno yasiyopungua 60 na yasiyozidi 70.
Mashairi ya Chekacheka - T. A. Mvungi (EP & D. LTD)
RIWAYA
Takadini - Ben J. Hanson (MBS)
Watoto wa Mama N'tilie - E. Mbogo (H. P)
Joka la Mdimu - A. J. Safari (H. P.)
TAMTHILIYA
Orodha - Steve Reynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)
Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)
9. Chama cha Waandishi wa Vitabu Tanzania kimeanzisha shindano la uandishi wa insha kuhusu Manufaa ya Sayansi na Teknolojia kwa Maendeleo ya Kiswahili. Ukiwa mmoja wa wanafunzi, andika insha isiyopungua maneno mia mbili (200) na isiyozidi maneno mia mbili hamsini (250) kuhusu shindano hilo.
10. Umeagizwa na mwalimu wako wa somo la Kiswahili kutunga shairi moja utakaloghani siku ya mahafali yenu ya kuhitimu Kidato cha Nne. Lengo la shairi hilo ni kuwasaidia wahitimu kuboresha maisha yao ya baadaye. Chagua mashairi matatu kwa kila diwani kutoka katika diwani mbili ulizosoma kisha eleza mafunzo utakayoyajumuisha katika shairi lako.
12. "Ujinga ni chanzo cha maendeleo duni katika jamii.". Kwa kutumia wahusika watatu kwa kila tamthiliya, onyesha jinsi ujinga wao ulivyozorotesha maendeleo katika jamii zao kupitia tamthiliya mbili ulizosoma.