JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA, MTIHANI WA KUHITMU KIDATO CHA NNE
021 KISWAHILI
(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)
Muda: Saa 3 Mwaka 2021
Maelekezo
Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C.
Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B alama arobaini (40) na sehemu C ina alama arobaini na tano (45).
Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x). kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye kijitabu chako cha kujibia.
(i) İpi ni seti sahihi ya vipera vya semi?
Methali, mizungu na maghani
Soga, nyimbo na nahau
Misemo, mafumbo na vigano
Mafumbo, soga na maghani
Nahau, vitendawili na mizungu
Choose Answer :
(ii) Dhima kuu ya misimu katika lugha ni ipi?
Kuunda mizizi ya maneno.
Kuficha jambo kwa wasiohusika.
Kuongeza ukali wa maneno.
Kutambulisha aina za maneno.
Kupatanisha maneno.
Choose Answer :
(iii) Bainisha sentensi yenye muundo wa kiwakilishi + kirai vumishi + kitenzi kikuu + kirai nomino:
Sisi sote tulicheza vizuri sana.
Mimi na yeye hatuelewani hata kidogo.
Wao hawataki tuimbe nyimbo zetu.
Wale wote wanapenda muziki.
Ninyi nyote tunawapenda sana.
Choose Answer :
(iv) Njia ipi ya uhifadhi wa fasihi simulizi inayowcza kupokea mabadiliko kwa haraka kati ya hizi?
Maandishi
Kichwa
Vinasa sauti
Kanda za video
Kompyuta
Choose Answer :
(v) "Ni budi nisome kwa bidii ili nifaulu mtihani wangu.” Yapi ni masahihisho sahihi ya sentensi hii?
Nina budi kusoma kwa bidii ili nifaulu mtihani wangu.
Sio budi kusoma kwa bidii ili nifaulu mtihani wangu.
Sina budi kusoma kwa bidii ili nifaulu mtihani wangu.
Sitakiwi kusoma kwa bidii ili nifaulu mtihani
Sio lazima kusoma kwa bidii ili nifaulu mtihani wangu.
Choose Answer :
(vi) "Kutwa mara tatu; asubuhi, mchana na jioni." Dhima ya muundo wa mazungumzo haya ni ipi?
Kupunguza ukali v„ra mazungumzo.
Kufupisha urefu wa mazungumzo.
Kupamba lugha ya mazungumzo.
Kuonesha msisitizo wa mazungumzo.
Kukidhi haja ya mazungumzo.
Choose Answer :
(vii) "Juma anaendesha baiskeli yake polepole." Kiarifu cha sentensi hii kimejengwa na mfuatano upi wa viambajengo?
Kiima, chagizo na shamirisho
Kitenzi kishirikishi, shamirisho na chagizo
Kiarifu, kiima na chagizo
Shamirisho, chagizo na kitenzi kikuu
Kitenzi kikuu, shamirisho na chagizo
Choose Answer :
(viii) Fungu la sauti zinazotokea katikati au mwishoni mwa kila mstari wa ushairi huitwaje?
Vina
Vituo
Mizani
Silabi
Mistari
Choose Answer :
(ix) Mambo muhimu ya kuzingatiwa katika uandishi wa tangazo la biashara ni yapi kati ya haya?
Aina ya bidhaa na idadi ya wateja.
Kichwa cha tangazo na bei ya kila bidhaa.
Aina na kichwa cha tangazo la bidhaa.
Aina ya bidhaa na bei ya kila moja.
Kichwa cha tangazo na lengo lake.
Choose Answer :
(x) Ni kauli ipi iliyotumika katika uundaji wa neno "nitamfitinia"?
kutenda
kutendana
kutendea
kutendeana
kutendewa
Choose Answer :
2. Oanisha maana za dhana za uundaji wa maneno katika Orodha A na dhana husika katika Orodha B, kisha andika herufi yajibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.
Orodha A
Orodha B
Kuchukua maneno katika lugha nyingine ili kukuza lugha.
Kuchukua mofimu au sehemu ya neno ili kuunda neno jipya.
Kuzalisha kauli mbalimbali.
Kuunganisha maneno zaidi ya moja ili kupata neno jipya.
7. Soma beti zifuatazo za wimbo wa taifa, kisha jibu maswali yanayofuata:
Mungu ibariki Afrika, Wabariki viongozi wake, Hekima, umoja na amani, Hizi ni ngao zetu, Afrika na watu wake, Ibariki, Afrika x 2 Tubariki, watoto wa Afrika.
Mungu ibariki Tanzania, Dumisha uhuru na umoja, Wake kwa waume na watoto, Mungu ibariki,
Tanzania na watu wake, Ibariki, Tanzania x 2 Tubariki, watoto wa Tanzania.
Maswali
(a) Wimbo huu una umuhimu gani kwa jamii ya Tanzania? Toja hoja mbili.
(b) Wahusika wawili wanaodhihirika katika wimbo huu ni wepi? Toa sababu moja ya uhusika wa kila mmoja.
(c) Onesha bayana vina viwili vilivyotumika katika mishororo ya ubeti wa pili.
(d) (i) Kwa kutumia mifano, bainisha tamathali za semi mbili zilizotumika katika wimbo huu.
(ii) Eleza sababu ya mtunzi wa wimbo huu kutumia tamathali za semi ulizobaini katika kipengele (d) (i).
8. Andika barua kwa Mkuu wa Chuo cha Uuguzi Peramiho S.L.P 133 Songea, kuomba nafasi ya kujiunga na mafunzo ya uuguzi. Jina lako liwe Nakiete Kajiru wa S.L.P 502 Malolo Ndanda. Barua yako ipitie kwa Afisa Mtendaji wa kata unayoishi.
9. Baada ya kuhitimu elimu ya Sekondari, umeitwa kwenye usaili wa nafasi ya kazi katika Baraza la Sanaa la Taifa. Katika usaili umetakiwa kuthibitisha iwapo fasihi ina umuhimu wowote katika jamii. Kwa kutumia hoja tano na mifano ya kazi mbalimbali za kifasihi thibitisha hoja hiyo ili kukidhi haja ya usaili wako.
11. Waandishi wa riwaya za Watoto wa mama Ntilie na Joka la Mdimu wameonesha kuwa rushwa ni miongoni mwa malatizo yanayozikabili jamii nyingi. Kwa kutumia mifano, eleza mambo matatu yaliyopendekezwa na waandishi kwa kila riwaya yenye lengo la kuzuia rushwa katika jamii.
12. Eleza jinsi uteuzi wa mandhari ulivyoibua dhana ya mapenzi machungu kwa wahusika kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma.