JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA NUTIHANI LA TANZANIA
MTIHANI WA KUHITIMU KIDATO CHA NNE
021 KISWAHILI
(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)
Muda: Saa 3 Mwaka: 2020
Maelekezo
l . Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
2.Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C.
3.Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B alama arobaini (40) na sehemu C ina alama arobaini na tano (45).
4.Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
5.Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
6.Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi yajibu hilo katika kijitabu chako cha kujibia.
(i) Ni neno lipi linalotoa taarifa kuhusu nomino?
Kitenzi
Kielezi
Kivumishi
Kiwakilishi
Kiunganishi
Choose Answer :
(ii)Katika lugha ya Kiswahili kuna aina ngapi za vitenzi?
mbili
tano
Sita
tatu
nne
Choose Answer :
(iii)Maneno yepi kati ya yafuatayo yametokana na lugha za Kibantu?
Kitindamimba na bendera
Hela na mtutu
Kitivo na ngeli
Godoro na sharubati
Bunge na shule
Choose Answer :
(iv)Ni mambo gani muhimu ya kuzingatia katika kuteua maneno na miundo ya tungo wakati wa mazungumzo?
Mada, muktadha na mazungumzo ya ana kwa ana.
Mada, mazungumzo na uhusiano wa wazungumzaji.
Mada, mzungumzaji na muktadha wa mazungumzo.
Mada, mzungumzaji na uhusiano wa wazungumzaji.
Mada, muktadha na uhusiano wa wazungumzaji.
Choose Answer :
(v)Bainisha kauli inayoonesha dhima muhimu za vitendawili katika jamii:
Kuhimiza umoja na ushirikiano.
Kupanga watu katika marika yao.
Kuchochea udadisi wa mambo.
Kuchochea uwongo wa mambo.
Kukosoa wadadisi wa mambo.
Choose Answer :
(vi)Njia mojawapo ya kuzuia utata katika lugha ya mazungumzo ni ipi kati ya zifuatazo?
Kuepuka makosa ya kisarufi na kimantiki.
Kutumia neno lenye maana zaidi ya moja.
Kutumia kiwakilishi kiambata katika neno.
Kuweka msisitizo au ufafanuzi zaidi.
Kutumia mofimu sahihi za wakati.
Choose Answer :
(vii)”Waandishi wa fasihi huzungumzia watu wenye mienendo isiyokubalika katika jamii ili kukemea mienendo hiyo.” Katika tamthiliya ulizosoma, ni wahusika wepi kati ya wafuatao wana mienendo isiyokubalika?
Joti, Ngoswe na Mama Furaha.
Padri James, Ngoswe na Baba Anna.
Mazoea, Mama Furaha na Joti.
Ngoswe, Baba Anna na Suzi.
Ngoswe, Joti na Padri James.
Choose Answer :
(viii)Kati ya sababu zifuatazo ni ipi si sahihi kuhusu matumizi ya kamusi?
Kujifunza lugha ya kigeni.
Kusanifisha maneno mapya.
Kubaini kategoria ya neno.
Kujua maana za maneno.
Kujua tahajia za maneno.
Choose Answer :
(ix)Ni methali ipi inayokinzana na methali ''Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu?”
Manahodha wengi, chombo huenda mrama.
Palipo na wengi, hapaharibiki neno.
Haba na haba, hujaza kibaba.
Kidole kimoja, hakivunji chawa.
Fimbo ya mnyonge, ni umoja.
Choose Answer :
(x)Bainisha sentensi ambatano yenye muundo wa sentensi changamano mbili kati ya sentensi zifuatazo:
Gari lililomteka tumeliona na dereva aliyetekwa ameonekana.
Mtoto aliyeumia jana amelazwa na mtoto mwingine hajitambui.
Mpe haki yake yote ili nae akupe haki yako yote.
Uchunguzi uliofanyika juzi umezaa matunda.
Baba anataka kujenga nyumba lakini mama hataki kabisa.
Choose Answer :
2.Oanisha maana za vipera vya Fasihi Simulizi katika Safu A na dhana za Fasihi Simulizi zilizo katika Safu B; kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.
Safu A
Safu B
(i)Sherehe au shughuli zinazofanywa na jamii katika kipindi maalumu cha mwaka.
(ii)Masimulizi ya mambo ya kishujaa ambayo mtu amewahi kuyafanya maishani mwake.
(iii)Maigizo mafupi yaliyojaa ucheshi na mzaha.
(iv)Sadaka itolewayo kwa miungu au mahoka.
(v)Masihara wanayofanyiana wanajamii wakati wa shida na raha.
6.Kwa kutumia mifano kutoka katika riwaya ya Takadini iliyoandikwa na Ben J. Hanson (MBS), eleza kwa kifupi madhara manne yanayoweza kutokea katika jamii iwapo itaendekeza mila potofu ya kuwabagua walemavu wa ngozi.
10. Kauli za washairi ni nyenzo muhimu katika ujenzi wa jamii bora. Thibitisha usemi huu kwa kutumia hoja tatu kwa kila kitabu kutoka katika diwani mbili ulizozisoma.
I I . "Jamii ya kitanzania inakabili'.va na matatizo mbalimbali ya kijamii yanayokwamisha maendeleo.” Thibitisha kauli hii k',va kutoa hoja tatu kwa kila riwaya kati ya riwaya mbili ulizosoma.
12. "Waandishi wa kazi ya fasihi hulenga kulcta mabadiliko katika yale wanayoyaandika.” Kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma, tetea kauli hii kwa kutumia hoja tatu kutoka katika kila kitabu.