JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
MTIHANI WA KUHITIMU KIDATO CHA INNE
021 KISWAHILI
(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)
Muda: Saa 3 Alhamisi 07 Novemba 2019 mchana
Maelekezo
Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C.
Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.
Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu chako cha kujibia.
(i)Neno lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza mtenda au mtendwa?
Kiunganishi
Kivumishi
Kihisishi
Kiwakilishi
Kielezi
Choose Answer :
(ii) Ni sentensi ipi haina kitenzi kisaidizi?
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa mtiifu.
Watoto wanatakiwa kulala mapema ili wawahi shuleni.
Paka alikuwa anataka kula chakula cha mbwa.
Juma alikuwa anasoma kitabu cha hadithi za mapenzi.
Robert Kelly anataka kuja kutumbuiza mwezi Desemba.
Choose Answer :
(iii)Ni sentensi ipi inawakilisha kikamilifu wahusika wa fasihi simulizi?
Vitu, mahali, wanyama, binadamu, fanani na maleba.
Hadhira, wanyama, maleba, binadamu na fanani.
Hadhira, binadamu, wanyama, vitu, mahali na fanani.
Fanani, vitu, mahali, binadamu, maleba na wanyama.
Wanyama, manju, binadamu, vitu, mahali na maleba.
Choose Answer :
(iv)Bainisha seti ya maneno inayofaa kuingizwa kwenye kamusi kwa kuzingatia mpangilio wa alfabeti.
Jabali, jadhibika, jabiri, jadi, jalada
Jabali, jabiri, jadhibika, jadi, jalada
Jabali, jadi, jadhibika, jalada, jabiri
Jabiri, jabali, jalada, jadi, jadhibika
Jabali, jalada, jabiri, jadhibika, jadi
Choose Answer :
(v)Ni sifa ipi haitofautishi fasihi simulizi na fasihi andishi?
Ukubwa
Uhifadhi
Uwasilishaji
Ukuaji
Ueneaji
Choose Answer :
(vi) Jozi ipi ina vipengele sahihi vinavyounda umbo la ndani la kazi ya fasihi simulizi?
Falsafa, muundo, ujumbe, wahusika
Mandhari, msimamo, ujumbe, dhamira
Ujumbe, mtazamo, migogoro, dhamira
Ujumbe, msimamo, dhamira, wahusika
Lugha, mgogoro, falsafa, mtindo
Choose Answer :
(vii)"Ngombe zangu wanatoa maziwa mengi." Kosa lililojitokeza katika tungo hii ni lipi kati ya haya?
Unyumbuaji wa maneno
Udondoshaji wa herufi
Unyumbuaji wa maneno
Upatanisho wa kisarufi
Uongezaji wa kiambishi
Choose Answer :
(viii) "Serikali imeweka mikakati kabambe ili kupunguza umasikini."Neno "ili" katika sentensi hii ni aina gani ya neno?
Kielezi
Kiunganishi
Kiwakilishi
Kihisishi
Kivumishi
Choose Answer :
(ix)Mpangilio sahihi wa vipashio vinavyounda lugha ya Kiswahili ni upi?
Mofimu, kishazi, kirai, neno na sentensi.
Mofimu, neno, kirai, sentensi na kishazi.
Neno, kirai, Kishazi, sentensi na mofimu.
Neno, mofimu, kirai, kishazi na sentensi.
Mofimu, neno, kirai, kishazi na sentensi.
Choose Answer :
(x) Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi fulani ya kifasihi?
Muundo wa kazi husika.
Wahusika wa kazi husika.
Jina la kazi husika.
Jina la mtunzi wa kazi husika.
Mtindo wa kazi husika.
Choose Answer :
2. Oanisha maana za dhana za uandishi zilizo katika Orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana husika katika Orodha B, kisha andika herufi husika katika kijitabu chako cha kujibia.
ORODHA A
ORODHA B
Kujieleza kwa lugha fasaha, mpangilio mzuri wa mawazo na kutumia misamiati.
Kujenga fikra fulani katika kifungu cha maneno.
Mpangilio mzuri wa mawazo unaoeleweka kwa mwandishi na msomaji.
Kifungu cha maneno chenye kuelezea wazo maalumu, au sehemu ya wazo lililo katika mtiririko.
Alama ya uandishi inayotenga maneno yaliyo katika orodha fulani.
6.(a) Soma kwa makini sentensi (i) hadi (iv), kisha fafanua kwa pamoja vipengele vinne vinavyodhihirisha uhusiano baina ya Kiswahili na lugha za Kibantu.
7.Kwa kutumia mifano kutoka katika riwaya ya Takadini na Watoto wa Mama Ntilie, eleza kwa kifupi mambo manne ya kufanana kati ya wahusika Sekai na Mama Ntilie kuhusu wasifu wao wa ndani.
8.Soma kifungu cha habari kifuatacho, kishajibu maswali yanayofuata:
Soni aliamka usingizini na kuendelea na safari yake. Awali alishtushwa na mitikisiko iliyotokea karibu na mbuyu. Hakujua yuko wapi lakini hakuchelewa kukumbuka nia ya safari yake. Aliukamata mkuki wake vizuri na ngao yake pia. Alipiga goti moja na kusimama hali akiuangalia mbuyu. Punde, aliwaona nyani wawili wakikimbilia nyasini. Wakasimama na kumtazama Soni. Naye alipoona hakuna hatari ya wanyama wakali, aliendelea na safari yake. Muda huo wa mchana ulikuwa salama kwani wanyama wakubwa walikuwa mapangoni mwao. Zaidi zilisikika sauti za panzi, nyenje na ndege tu waliojibizana kwa zamu.
Soni alipumzika kidogo kwa mara nyingine ili kumnyonyesha mtoto. Hata hivyo, vivuli virefu vilimkumbusha kuwa usiku ulikaribia. Lakini hakusikia wala kuona dalili yoyote ile iliyoonesha kuwa binadamu waliishi katika eneo hili. Bado hakuelewa ni wapi alipokuwa. Ni kosa gani alilofanya? Je, mwanawe hakuwa binadamu? Ni-kwewtofauti yake .ni_rangi-tu2 Hakuwa na vidole vya mikono na miguu vilivyomzidi baba yake. Macho yake na masikio pia yalikuwa sawa, aliyahesabu yote. Pale kila kitu kilipowekwa pamoja, mtoto alikuwa karibu sawa na wengine kuliko tofauti yake ya rangi tu. Sasa nvbona wanataka kumuua?
Soni alianza kukimbia kwa kasi kwani kama hangefika kijiji jirani, basi kutoroka kwake kungekuwa kazi bure. Punde si punde alishtushwa na mlio wa vipande vya miti vilivyovunjika. Soni alisimama akabana pumzi zake akisubiri sauti ile isikike tena. Huyo hakuwa mnyama mkali bali mtu aliyekusanya kuni. Upesi Soni aliharakisha upande ilikotoka sauti. Ghafla akamwona mzee mmoja akikusanya kuni. Alisogea kiasi ambacho kungetokea hatari angekimbia. Alimsalimia mzee yule. "Tafadhali kuwa mwema ili umsaidie mwanao aliyepotea," alisubiri atakavyojibiwa. Kwa sauti ile yule mzee alizunguka na kuinua shoka lake kama ishara ya kutisha. Punde alipogundua kuwa aliyeongea alikuwa ni mwanamke, alipata ahueni na kulishusha shoka lake chini. Wakati ule Soni alisita na kuamua kusimama. Tumaini alizinduka usingizini. Huenda alihisi shaka iliyomkumba mama yake, akaanza kulia.
Punde si punde, yule mzee alijiandaa kwa mashambulizi. Aliwaza kuna mtu nyuma ya yule mama. Iweje mwanamke mwenye mtoto mchanga aranderande msituni bila ya kuwa na mlinzi? Huenda anatumiwa na kijana imara aliyetaka kumuua. Wakati huo angefanyaje? Alikusanya kuni chache alizozipasua, akageuka ili aondoke. "Tafadhali usinitupe niliwe na wanyama wa usiku. Nisaidie! La, huwezi kunisaidia binti yako, basi msaidie mwanangu. Hajaonja maisha bado, na si vyema kufa sasa. Kilio mfululizo cha yule mtoto na maneno ya Soni vilimgusa yule mzee. Ingawa alisita, lakini hatimaye aligeuka nyuma. Kutokana na kauli yake, alihisi Soni alikuwa mgeni katika eneo hilo. Akaamua hata kama iweje, angemsaidia. Kwa hadhari kubwa aliwasogelea mama na mtoto wake. "Njoo mwanangu, tutakwenda kibandani kwangu."
Maswali
Pendekeza kichwa cha habari hii kisichozidi maneno matatu.
9.Wewe ni mshiriki wa shindano la uandishi wa insha lililoandaliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa. Kaulimbiu ya shindano ni "Watoto zingatieni daima maonyo ya wazazi wenu". Kwa kutumia kauli mbiu hii, andika insha ya kisanaa isiyopungua maneno mia mbili (200) na isiyozidi maneno mia mbili hamsini (250), yenye kuishia na methali "Asiyesikia la mkuu huvunjika guu".
1l . "Waandishi wa kazi za fasihi huibua migogoro mbalimbali na kupendekeza masuluhisho ili kuelimisha jamii husika". Thibitisha kauli hiyo kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.
12. Kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma, fafanua madhara yanayotokana na kukosekana kwa elimu ya jinsia kwa vijana kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila kitabu.