FORM TWO HISTORIA NECTA 2025

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI

060 HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI

(MKONDO WA AMALI)

(Kwa wanafunzi Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

Muda: Saa 2:30 Mwaka: 2025

Maelekezo

  1. Upimaji huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote kwenye nafasi ulizopewa.
  3. Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B sabini (70) na sehemu C ina alama kumi na tano (15).
  4. Andika majibu yote kwa kutumia kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  5. Vifaa vyote vya mawasiliano na vitu vingine visivyonuhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.
  6. Andika Namba yako ya Upimaji katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.
KWA MATUMIZI YA MPIMAJI TU
NAMBA YA SWALI ALAMA SAHIHI YA MPIMAJI
1.

2.

3.

4.

5.

6.

7.

8.

9.

10.

JUMLA

SAHIHI YA MHAKIKI

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Katika kipengele (i) – (x), chagua jibu sahihi kutoka kwenye machaguo uliyopewa na kuandika herufi yake katika kisanduku ulichopewa.

(i) Wakati wa somo la Historia ya Tanzania na Maadili mwalimu aliwaonesha wanafunzi picha za majengo ya kale na sanaa za jadi. Vitu hivyo hutambulika kama:

  1. maeneo muhimu kwa ajili ya utalii.
  2. historia na utambulisho.
  3. urithi wa kihistoria na kiutamaduni.
  4. visaidizi vya kuelewa historia yetu.
Choose Answer :


(ii) Kabla ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964, Zanzibar ilikuwa imepata uhuru uliojulikana kama “Uhuru wa bendera”. Uhuru huo ulipatikana mwaka gani?

  1. 1957
  2. 1963
  3. 1961
  4. 1962
Choose Answer :


(iii) Serikali ya Tanganyika iliongozwa na kiongozi gani kabla ya kuwa Jamhuri mwaka 1962?

  1. Gavana Mkuu
  2. Waziri Mkuu
  3. Rais
  4. Malkia
Choose Answer :


(iv) Ni ipi kati ya orodha zifuatazo inabainisha nguzo ya kujenga maadili katika mfumo wa elimu ya jadi?

  1. Mila na desturi za jamii, ujuzi wa kazi, lugha, jando na unyago
  2. Jando na unyago, mavazi na mafunzo ya kusaidia vijana
  3. Vyakula, mila na desturi, ujuzi wa kazi za jamii na umoja
  4. Mila na desturi za jamii, lugha, muziki na vyakula vya jamii
Choose Answer :


(v) Ni kwa namna gani unaweza kumaliza mgogoro kati ya wanafunzi wawili wanaopigana darasani kwa kutumia maarifa ya mifumo ya haki ya jadi?

  1. Kumuadhibu aliyesababisha ugomvi
  2. Kuwatenganisha wasichdelee kupigana
  3. Kuwapatanisha na kumaliza ugomvi kati yao
  4. Kuwashitaki kwa mujibu wa sheria za shule
Choose Answer :


(vi) Wanafunzi wa shule yako walipata fursa ya kutembelea mbuga za wanyama za Serengeti na Ngorongoro. Yapi kati ya maelezo yafuatayo yanatoa maana sahihi ya shughuli hiyo?

  1. Kusafiri na kukaa nje ya shule kwa muda
  2. Kwenda nje ya shule kwa ajili ya burudani
  3. Kutoka shuleni kwenda mbugani kwa wanyama
  4. Kutoka nje ya shule yako kwa lengo la kujifunza
Choose Answer :


(vii) Ni mbinu ipi ilitumiwa na wakoloni kudhoofisha matumizi ya tiba za jadi?

  1. Kuziondoa kwenye maala wa shule zao
  2. Kutowazajiri wakunga na matabibu wa jadi
  3. Kutowapa mafunzo ya kisasa waganga wa jadi
  4. Kuzihusianisha na uchawi na ushirikina
Choose Answer :


(viii) Maelezo yapi yanathibitisha ukweli kuhusu jamii zilizoamua kuungana na wavamizi wa kikoloni ili kuweza kuwashinda maadui zao wa muda mrefu?

  1. Zilitawaliwa kirahisi na wakoloni
  2. Ziliimarika kisiasa na kiuongozi
  3. Zilifanikiwa kiuchumi na kiusalama
  4. Zilipata misaada ya silaha za kivita
Choose Answer :


(ix) Ni kwa namna gani udhibiti wa rasilimali kwa watu binafsi na vikundi katika mfumo wa kikabaila ulikuza siasa za jamii husika?

  1. Ulisababisha kufutwa kwa mfumo wa koo
  2. Ulipunguza vitendo vya rushwa katika jamii
  3. Ulichangia kuendesha uchaguzi huru na haki
  4. Uliwapa watu nguvu na ushawishi mkubwa katika jamii
Choose Answer :


(x) Ni kwa namna gani matumizi ya lugha ya Kiswahili katika utengenezaji wa filamu za Kitanzania yanaweza kusaidia kukuza uchumi na ushirikiano wa kimataifa?

  1. Kufikia watazamaji wengi zaidi Afrika Mashariki
  2. Kuifanya iwe lugha ya kufundishia ili kuongeza wataalamu
  3. Kurahisisha mawasiliano katika biashara na sanaa
  4. Kuzuia matumizi ya lugha nyingine nchini
Choose Answer :


2. Oanisha maelezo kuhusu uhusika wa viongozi wa makabila ya jamii za Kitanzania katika harakati za kuupinga uvamizi wa kikoloni katika Orodha A na majina ya viongozi husika katika Orodha B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika jedwali ulilopewa.

Orodha A  Orodha B

(i) Kiongozi wa kabila la Wahehe aliyepambana na Wajerumani. 

(ii) Kiongozi aliyeungana na Wajerumani kupigana dhidi ya Wahehe.

(iii) Kiongozi aliyeshirikiana na Wajerumani kuuangusha utawala wa Wakibosho.

(iv) Kiongozi wa Wanyamwezi aliyepinga kuenea kwa ukoloni wa Kijerumani Tanganyika.

(v) Kiongozi wa Wayao aliyekataa kusaini mikataba ya kilaghai ya Wajerumani.

  1. Chifu Merere
  2. Chifu Machemba
  3. Mangi Mandara
  4. Mangi Mashingia
  5. Chifu Mkwawa
  6. Chifu Fundikira
  7. Chifu Mirambo
  8. Chifu Mangungo
View Ans


SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Bainisha umuhimu wa kuhifadhi urithi wa asili na kiutamaduni. Toa hoja tano.

View Ans


4. "Maadili yana mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi." Fafanua usemi huu kwa kutumia hoja tano.

View Ans


5. Kwa kutumia hoja tano, eleza jinsi maarifa ya mifumo ya kisiasa na kiuchumi kabla ya ukoloni yanavyoweza kutumika kuimarisha uwajibikaji katika jamii za sasa.

View Ans


6. Chambua hatua tano za kisiasa zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania kujenga taifa baada ya uhuru.

View Ans


7. Tumia hoja tano kuchambua mchango wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika upatikanaji wa Uhuru wa Tanganyika.

View Ans


8. Kwa kutumia hoja tano, tofautisha elimu ya jadi na elimu ya sasa.

View Ans


9. Changanua vigezo vitano vya kiteknolojia vinavyotofautisha zana za mawe na zana za chuma.

View Ans


SEHEMU C (Alama 15)

Jibu swali la kumi (10).

10. Eleza mabadiliko matano ya kisiasa yaliyoletwa na utawala wa Waingereza katika jamii za Kitanzania.

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256