FORM TWO KISWAHILI NECTA 2021

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI

021 KISWAHILI

Muda: 2:30 Mwaka: 2021

Maelekezo

l . Karatasi hii ina sehemu A. B. C. D na E zenye jumla ya maswali kumi (10).

2. Jibu maswali yote.

3. Sehemu A na E zina alama kumi na tano (15) kila moja. sehemu B na C zina alama ishirini (20) kila moja na sehemu D ina alama thelathini (30).

4. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa.

5. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.

6. Vifaa vyote vya mawasiiiano visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.

7. Andika Namba yako ya Upimaji katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kuiia.

KWA MATUMIZI YA MPIMAJI TU

NAMBA YA SWALI

ALAMA

SAHIHI YA MPIMAJI

1



2



3



4



5



6



7



8



9



10



JUMLA



SAHIHI YA MHAKIKI


SEHEMU A (Alama 15)

UFAHAMU

1. Soma kifungu cha maneno kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

UKIMWI ni kifupi cha Upungufu wa Kinga Mwilini. Upungufu huo wa kinga mwilini husababishwa na aina ya virusi vinavyoshambulia chembechembe hai nyeupe zilizomo ndani ya damu. Chembechembe hizo nyeupe za damu ndizo zinazojenga kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Uharibifu wa chembechembe hizo baadaye hufikia kiwango ambacho huufanya mwili upoteze kinga yake dhidi ya maradhi.

Virusi hivyo vinavyoshambulia chembechembe nyeupe ndani ya damu vimepewa jina la virusi vya UKIMWI kwa kifupi (V V U). Katika mwili wa binadamu virusi hivi huishi katika damu na majimaji ya mwilini.


Virusi vya UKIMWI sio UKIMWI. kuna tofauti kubwa kati ya mtu mwenye V VU na mgonjwa wa UKIMWI. Kama ilivyoelezwa VVU ni virusi ambavyo hushambulia chembechembe hai nyeupe zinazojenga na kulinda kinga ya mwili, lakini UKIMWI ni ile hali ya mtu kukosa kinga ya mwili kiasi kwamba akipata ugonjwa wowote ule unamshambulia sana na haponi kwa haraka.

Baada ya kuambukizwa mtu anaweza kuishi na VVU hata kwa miaka kumi bila kuonesha dalili yoyote ya ugonjwa wa UKIMWI. Hivyo. huwezi kujua kama mtu ana virusi vya

UKIMWI kwa kumwangalia kwa macho tu.

Maswali

(a) Andika kichwa cha habari kisichozidi maneno matano kinachofaa kwa habari uliyosoma.

(b) Andika kirefu cha UKIMWI.

(c) Virusi vya UKIMWI vina madhara gani mwilini mwa binadamu?


(d) (i) Kuna tofauti gani kati ya mtu mwenye Virusi vya UKIMWI na mgonjwa wa UKIMWI?

(ii) Fafanua kazi ya chembechembe nyeupe za damu katika mwili wa binadamu.

View Ans


2. Fupisha habari uliyoisoma kwa maneno yasiyopungua hamsini (50) na yasiyozidi sitini (60).

View Ans


SEHEMU B (Alama 20)

SARUFI

3. Eleza maana ya maneno yafuatayo:

(a) Mzizi wa neno

(b) Mofimu

(c) Mnyambuliko

(d) Kamusi

(e) Kidahizo

View Ans


4. (a) Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ya kutendesha.

(i) Imba

(ii) Lima

(iii) Zoa

(iv) Piga

(v) Soma

(b) Onesha kivumishi katika tungo zifuatazo kisha bainisha ni aina gani ya kivumishi.

(i) Mti mkavu umekatwa.

Kivumishi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Aina . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .  . . . . . . . . . . . . . . . . 

(ii) Watoto wanne wameondoka.

Kivumishi   . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Aina  . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 


(iii) Mtu yule ni mwizi.

Kivumishi   . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Aina   . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

(iv) Banda ta kuku limejengwa vizuri.

Kivumishi   . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Aina   . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

(v) Wanafunzi wangu wamefaulu mtihani.

Kivumishi  . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Aina   . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

View Ans


SEHEMU C (Alama 20) 

MAWASILIANO NA UTUMIZI WA LUGHA

5. Tungo zifuatazo Zina maana zaidi ya moja. Toa maana mbili tu kwa kila tungo.

(a) Amempigia nini.

(b) Nimenunua mbuzi.

(c) Eda ameshinda shuleni.

(d) Ukija njoo na nyanya.

(e) Nyumbani kwao kuna tembo

View Ans


6. Onesha kosa katika sentensi zifuatazo kisha andika sentensi hizo kwa usahihi. Sentensi ya kwanza imetumika kama mfano.

(a) Kiranja Mkuu alimwasilisha Mkuu wa Shule katika mkutano huo.

(i) alimwasilisha

(ii) Kiranja Mkuu alimwakilisha Mkuu wa Shule katika mkutano huo.

(b) Sisi hatuna nyumba tumepangisha kwa mzee Juma.

(c) Diwani alihutubia kwa muda wa masaa Sita.


(d) Amenunua dazani mbili za sufuria.

(e) Sisi wote tu abiria, kelele za nini?

(f) Mwalimu alisahihisha daftari za wanafunzi wake.

View Ans


SEHEMU D (Alama 30)

FAS?H? KWA UJUMLA

7. Fafanua vipera vya fasihi simulizi vifuatavyo:

(a) Ngano

(b) Vigano

(c) Tarihi

(d) Tarihi

(e) Visasili

View Ans


8. Toa maana ya semi zifuatazo: 

(a) Kujitia kitanzi

(b) Kuwa kinyonga

(c) Kumpaka mtu matope......

(d) Mla mbuzi hulipa ng'ombe...........

 (e) Ulimi wa pilipili

View Ans


9. Tegua vitendawili vifuatavyo:

(a) Nasuka mkeka lakini nalala chini . . . . . . . .

(b) Kila aendapo huacha alama . . . . . . . . . . .

(c) Nikimpiga mwanangu watu hucheza. . . . . . . .

(d) Anatembea na nyun?ba . . . . . . . . . . .

(e) Nyumba yangu ina nguzo moja. . . . . . . . . .

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256