Namba ya Upimaji ya Mwanafunzi . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI
021 KISWAHILI
Muda 2:30 Mwaka 2020
Maelekezo .
- Karatasi hii in sehemu A, B, C, D na E zenye jumla ya maswali kumi (10).
- Jibu maswali yote.
- Sehem A na E zina alama kumi na tano (15) kila moja, sehemu B na C zina alama ishirini (20) kila moja na sehemu D ina alma thelathini (30)
- Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa.
- Majibu yote yaandikwe kwa kaalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
- Vifaa vyote vya mawasiliano visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.
- Andika Namba yako ya Upimaji katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.
| KWA MATUMIZI YA MPIMAJI TUU
|
| NAMBA YA SWALI
| ALAMA | SAHIHI YA MPIMAJI
|
| 1. |
|
|
| 2. |
|
|
| 3. |
|
|
| 4. |
|
|
| 5. |
|
|
| 6. |
|
|
| 7. |
|
|
| 8. |
|
|
| 9. |
|
|
| 10. |
|
|
| JUMLA |
|
|
| SAHIHI YA MHAKIKI
|
|
SEHEMU A (Alama 15)
UFAHAMU
1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Jambo moja kubwa katika mambo ya huzuni kwa watu wote sasa lilitokea. Mke wangu mpenzi alishikwa na maradhi, na baada ya muda kidogo wa udhaifu na maumivu akafariki duniaUtengano huu kati yetu ulitokea baada ya miaka kumi ya kuishi pamoja kwa mapenzi, amani, raha na baraka. Tukio hili lilikuwa pigo kubwa sana kwangu na msiba mkubwa katika nyumba nzima. Marehemu huyu alikuwa tunu ya maisha yangu, tegemeo na mshauri mwema. Alinisaidia katika mambo mengi wakati wa maisha yetu pamoja ambayo yangalinishinda kuyatenda mimi peke yangu.
Sura yake ilikuwa jamali kwa kimo cha kadiri . , uso ulikuwa mviringo wa yai, nywele nyeusi za kushuka, paji pana, nyusi za upindi, macho mazuri yalikuwa na tazamo juu ya kila kitu kope za kutana, masikio ya kingo yasiyopitwa na sauti ndogo, meno ya mwanya yaliyojipanga vizuri mithili ya lulu katika chaza, ulimi wa fasaha na maneno ya kiada yaliyotawaliwa, midomo imara isiyokwisha tabasamu. Sauti pole na tamu kama wimbo, kiedevu cha mfuto katikati yake palikuwa na kidimbwi kidogo. Shingo kama mnara ambayo juu yake paliota kichwa cha mawazo mengi, chini ya shingo mabega yalikuwa kama matawi ya maua, kifua cha madaha, mikono ya mbinu, tumbo jembamba na miguu ya mvungu. Uzuri wake ulikuwa kamili. Kwa tabia alikuwa mwaminifu na mfano wa kuiga katika nyumba.
Wanawake ni wengi kama walivyo wanaume lakini wenye sura kama iliyoelezwa ni adimu sana kukutana nao duniani. Kabla ya kuoa nililitafuta umbo namna yake muda wa miaka kumi. Kitu nilichokuwa nikitafuta kwa muda wote mwisho nilikipata, lakini baada ya miaka kumi mingine kilikwenda safari ya watu wasikorudi na wito usiofika. Mauti yake ya mapema yalikuwa ni msiba na hasara kubwa sana kwangu. Nilishindwa kujizuia kama nilivyotaka, machozi yalinitoka mengi sana na yalikuwa hayazuiliki sababu ya pigo zito lililonijia.
Maswali
(a) Andika kichwa cha habari uliyosoma kwa maneno yasiyozidi matano.
(b) (i) Ni jambo gani kubwa liletalo huzuni kwa watu wote lililomtokea mwandishi wa habari hii?
(ii) Ni muda gani mwandishi wa habari hii aliishi na mkewe baada ya harusi yao?
(c) (i) Mke wa mwandishi wa habari hii alikuwa na tabia ya namna gani?
(ii) Katika aya ya pili mwandishi ana maana gani anaposema uzuri wake ulikuwa .kamili?
(d) Andika maana ya maneno au vifungu vya maneno kama vilivyotumika katika habari uliyosoma:
- (i) Tunu .
- (ii) Kimo cha kadiri .
- (iii) Adimu
- (vi) Safari ya watu wasikorudi
View Ans
2. Andika ufupisho wa habari uliyosoma kwa maneno sitini (60).
View Ans
SEHEMU B (Alama 20)
SARUFI
3(a) Nyambua maneno yafuatayo kwa kutumia kauli ya kutendeana.
- (i) Toa
- (ii) Fyeka
- (iii) Ondoa
- (iv) Piga
- (v) Lia
View Ans
(b) Unda nomino moja tu kutokana na vitenzi vifuatavyo:
- (i) Lea
- (ii) Nyoa
- (iii) Pika
- (iv) Cheza
- (v) Soma
View Ans
4. Bainisha nomino dhahania katika sentensi zifuatazo:
- (a) Ugonjwa uliotokea uliua watu wengi.
- (b) Shibe hulevya watu na wanyama.
- (c) Mwanadamu huangamia kwa kukosa maarifa.
- (d) Timu ya kijiji ilipata ushindi katika mechi ya jana.
- (e) Jumbe alishindwa mtihani kwa sababu ya starehe.
- (f) Gauni alilovaa limempendeza sana lakini uzuri nao unachangia.
- (g) Uvivu na janga la taifa.
- (h) Ukosefu wa mvua husababisha njaa.
- (i) Anasa huzorotesha maendeleo.
- (j) Mwanafunzi anapofaulu mtihani huwa na furaha kubwa.
View Ans
SEHEMU C (Alama 20)
MAWASILIANO NA UTUMIZI WA LUGHA
5. Eleza maana ya istilahi zifuatazo, toa mfano kwa kila maana ya istilahi.
(a) Mawasiliano
- (i) Maana ..... .
- (ii) Mfano.... .
(b) Silabi
- (i) Maana ..... .
- (ii) Mfano.... .
(c) Lugha
- (i) Maana ..... .
- (ii) Mfano.... .
(d) Irabu
- (i) Maana ..... .
- (ii) Mfano.... .
(e) Sentensi
- (i) Maana ..... .
- (ii) Mfano.... .
View Ans
6. Maneno yafuatayo yana maana zaidi ya moja. Tunga sentensi mbili kwa kila neno ukitofautisha maana hizo.
- (a) Kaa
- (b) Tai
- (c) Kata
- (a) Kanga
- (e) Ulezi
View Ans
SEHEMU D (Alama 30)
FASIHI KWA UJUMLA
7. Kamilisha methali zifuatazo:
- (i) Ukitaka kujua asili ya mwanga ..
- (ii) Ukitaka kujua raha ya mtu aliyesoma ...
- (iii) Jina jema .
- (iv) Haraka haraka .
- (v) Mjukuu si mwana ..
View Ans
8. Tegua vitendawili vifuatavyo:
- (a) Gari langu halitumii mafuta ..
- (b) Napigwa faini kosa silijui
- (c) Kamba yangu ndefu lakini haifungi kuni.
- (d) Ukiona njigi utadhani njege na ukiona njege utadhani njigi.
- (e) Nyumba yangu ndogo wapangaji wengi
View Ans
9. Fafanua mambo matano ya kuzingatia wakati wa kutunga hadithi.
View Ans
SEHEMU E (Alama 15)
UANDISHI WA INSHA/UTUNGAJI
10. Kwa maneno yasiyozidi kumi (10) mtumie simu ya maandishi dada yako Lulu Mwendokasi wa S.L.P 1012 Mwanza, kumfahamisha kuwa, mama yenu anaumwa. Jina lako liwe Mwasi Mwendokasi.
View Ans