JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MTIHANI LA TANZANIA
MTIHANI WA UPIMAJI WA KIDATO CHA PILI
021 KISWAHILI
Muda: 2:30 2019
 MAELEKEZO:Â
- Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E zenye jumla ya maswali kumi (10).
- Jibu maswali yote.
- Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa.
- Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
- Vifaa vyote vya mawasiliano visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
- Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.
SEHEMU A (Alama 15)
UFAHAMU
1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kicha jibu maswali yanayofuata.
Katika miji mikubwa nchini Tanzania wimbi la ongezeko la watu bado ni kubwa. Ongezeko hilo la watu limesababisha kukuza kwa matatizo makubwa maeneo ya mijini ikiwemo msongamano mkubwa wa magari na watu. Hali hii imesababish wafanyakazi kuchelewa kazini, wanafunzi kuchelewa shuleni na hata wagonjwa kuchelewa kufikishwa katika vituo vya kutolea huduma za matibabu.
Hebu tujiulize, kwa nini watu wengi wanaondoka vijijini na kukimbilia mijini? Majibu yanaweza kuwa mengi, lakini miongoni mwa majibu hayo inaweza ikawa huduma zisizokidhi mahitaji ya kijamii. Jamii inatarajia kupata huduma bora za maji, umeme, barabara, matibabu, ajira na mawasiliano. Jamii inaposhindwa kupata huduma hizo katika maskani yao, lazima itafute huduma hizo nje. Na njia pekee ne kikimbilia mijini ambako huduma hizo zinapatikana.
Anasa pia ni sababu mojawapo. Ikumbukwe kuwa kundi kubwa la watu wanaokimbilia mijini ni vijana. Kundi hili ni la watu wanaopenda starehe, hawataki kujituma na kujikwamua kimaisha, wanapenda kupata mafanikio ya haraka. Vijana wengi wanakimbilia mijini jambo ambalo linaleta wasiwasi wa hali ya maisha katika maeneo hayo ikilinganishwa na rasilimali zilizopo. Wengi wao hujiingiza katka vitendo vya uhalifu kama wizi na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Ongezeko la watu mijini husababisha makazi duni, uchafuzi wa mazingira na uhalifu wa kila aina. Ongezeko la watu katika maeneo ya miji linakwenda sambamba na ongezeko la magari, hivyo tatizo la miundombinu isiyokidhi pia hujitokeza. Hali hii ikiachwa iendelee uharibifu wa mazingira utaongezeka kwa kiasi kikubwa kwa sababu watu watatafuta njia mbadala ili kuzitatua changamoto zinazowakabili.
Maswali:Â
(a) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu hiki cha habari.
- Msongamano
- Maskani
- Miundombinu
- Changamoto
(b) (i) Kulingana na kifungu cha habari ulichosoma ni kundi gani la watu hukimbilia mjini?
(ii) Taja sababu mbili muhimu zinazowafanya watu wakimbilie mjini
(c) Ongezeko la watu mijini lisipodhibitiwa litasababisha nini?
(d) Pendekeza kichwa cha habari kinachofaa kwa kifungu cha habari ulichosoma kisichozidi maneno matano.
View Ans
2. Andika ufupicho wa kifungu cha habari ulichosoma kwa maneno yasiyopungua hamsini (50) na yasiyozidi sitini (60).
View Ans
SEHEMU B (Alama 20)
SARUFI
3. Bainisha mzizi wa asili wa kila kitenzi katika sentensi zifuatazo.
- Mtoto anacheza mpira
- Wanafunzi wanapigana darasani
- Sisi hatupendani
- Watoto walifungiana milango
- Vifaa feki viliharibiwa.
- Mwalimu alitambulisha wanafunzi wageni
- Jana hatukusomeana
- Mama alimwonyesha baba daftari langu
- Mamia ya wachezani wa Taifa Stars walipokelewa kwa shange.
- Wakorofi walitowa darasani
View Ans
4. (a) Eleza maana ya maneno yafuatayo:
- Kidahizo
- Kitomeo
- Alifabeti
- Kamusi
- Kitenzi
View Ans
(b) Bainisha aina ya nomino zifuatazo:
Mfano: Maji – nomino ya jumla/wingi.
- Papai
- Mungu
- Arusha
- Upepo
- Jumamosi
View Ans
SEHEMU C (Alama 20)
MAWASILIANO NA UTUMIZI WA LUGHA
5. Onesha rejesta zifuatazo hutumika katika mazingira gani.
(i) Mimi kuku ugali moja, huyu wali maharage na wale pale Ng’ombe.
(ii) Zuia babu, kula hivyo vichwa vitatu.
(iii) Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa kama ifuatavyo.
(iv) Ndugu Madongo Kuinuka unatuhumiwa kwa kosa la jinai la kuiba mali ya umma.
(v) Jipatie mahitaji ya jikoni, nyanya, vitunguu, karoti, hoho, pilipili na ndimu vyote vipo.
View Ans
6. Fafanua sifa tano za lugha ya kimazungumzo.
View Ans
SEHEMU D (Alama 30)
FASIHI KWA UJUMLA
7. Eleza kwa ufupi dhima kuu tano za fasihi.
View Ans
8. Fafanua methali zufuatazo:
- Hakuna masika
- Mchanga mwiko
- Chanda chema
- Asiyefunzwa na mamaye
- Dalili ya mvua
View Ans
9. “Ngonjera ni maigizo na pia ni mashairi”. Toa sababu tatu za kuthibitisha usemi huo.
(i) Ngonjera ni maigizo kwa sababu:
(ii) Ngonjera ni mashairi kwa sababu:
View Ans
SEHEMU E (Alama 15)
UANDISHI WA INSHA /UTUNGAJI
10. Kwa kuzingatia hoja nne. Andika insha isiyopungua maneno mia moja na hamsini (150) na isiyozidi maneno mia mbili (200) kuhusu Umuhimu wa Lugha ya Kiswahili.
View Ans