FORM TWO KISWAHILI NECTA 2018

2018- KISWAHILI

SEHEMU A

      1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.

Siku zote madereva hupambana na hatari mbalimbali wanapoendesha magari yao barabarani. Hatari hizo husababishwa na obuvu wa magari, uzembe wa waenda kwa miguu na hali ya barabara yenyewe. Kusudio la Taifa siku zote ni kuwa na dereva wa kujihami, ambaye atahakikisha usalama barabarani wakati wote.

Dereva bora lazima awe na utaalamu wa kutosha katika kazi yake, awe na mbinu kadhaa za kutumia katika kukwepa ajali na kujiokoa yeye, gari lake na watumiaji wengine wa barabara. Lazima uwezo wake wa kuhisi na kutambua hatari uwe mkubwa. Asiendeshe kwa kudhani au kubahatisha, bali awe na uhakika. Angamue hatari mapema na aamue kukwepa hatari na vikwazo vya barabarani.

Si hivyo tu, bali pia ajitahidi kuepuka hatari na kuzuia janga kutokea. Ajifunze na atumie mbinu mbalimbali wakati ufaao. Aendeshe kwa kufikiri mbele zaidi na akihisi tatizo atekeleze maamuzi mara moja. Asingojee yatokee, aepushe shari, asiwaze kuwa dereva mwenzake ndiye atasimama bali asimame yeye.

Wanafunzi wanaokwenda shuleni na wazee wamo hatarini zaidi kuliko watu wazima. Hivyo, ni muhimu watu hao walindwe na wafundishwe juu ya usalama barabarani. Kwa hiyo waendesha vyombo vya moto, wahakikishe ubora wa afya zao kabla ya kuendesha. Aidha, magari yakaguliwe mara kwa mara ili yasisababishe ajali za barabarani. Tukizingatia hayo ajali za barabarani zitapungua kama siyo kuisha kabisa.

MASWALI

(a)     "Dereva bora ni yule anayejihami." Usemi huo una maana gani?

(b)     (i) Usalama barabarani unamhusu nani hasa?

(ii) Taja watumiaji wawili wa barabara ambao wapo hatarini zaidi wawapo barabarani kulingana na habari uliyosoma.

(c)     Orodhesha hatari tatu anazokumbana nazo dereva anapokuwa barabarani.

(d) Pendekeza kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma kisichozidi maneno matano.

View Ans


     2.  Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua sitini (60).

View Ans


SEHEMU B

SARUFI

3.Taja kazi tano za kamusi.

View Ans


4.Eleza kazi moja ya mofimu tegemezi iliyopigiwa mstari katika maneno yafuatayo. (i) Alicheza

(ii)Tunasoma

(iii)Hawachezi

(iv)Anayepika

(v)Huandika

View Ans


SEHEMU C

MAWASILIANO NA UTUMIZI WA LUGHA,

5.Eleza maana ya lugha fasaha kisha onesha madhara manne (4) yanayoweza kutokea endapo mtumiaji wa lugha hatatumia lugha fasaha.

View Ans


6.Eleza tofauti za msingi tano (5) kati ya lugha ya maandishi na lugha ya mazungumzo.

View Ans


SEHEMU D

FASIHI KWA UJUMLA

7.(a) Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata.

Haya shime tuitane, sote tushirikiane,

Wala tusitegeane, kwa pamoja tushikane, Aliye mwoga anene, kabisa tusigombane, Tutie jembe mpini tuteremke shambani.

Njaa ikituvamia, sote tutaangamia,

Hakuna cha kungojea, lazima kuizuia, Si kitu cha kuchezea, mbona itatuumbua?

Tutie jembe mpini, tuteremke shambani.

MASWALI

(i)Shairi hili lina beti ngapi?

(ii)Kila mshororo wa kila ubeti una mizani ngapi?

(iii)Kina cha kati cha ubeti wa pili ni kipi?

(iv)Kibwagizo cha shairi hili ni kipi?

(v)Shairi hili lipo katika kundi gani la mashairi?

(b)     Baioisha tanzu ya kila kipera kwa vipera vya fasihi simulizi vifuatavyo:

Ci) Utani (ii) Miviga

(iii)Tenzi

(iv)Kisasili

(v)Ngano

View Ans


8.Eleza sifa kuu tano za fasihi simulizi.

View Ans


9.(a) Taja sehemu kuu tatu za kitendawili.

(b)     Taja wahusika wawili wa kitendawili.

(c)      Mbali na fasihi, taja aina nyigine tano za sanaa.

View Ans


SEHEMU E

UANDISHI WA INSHA/UTUNGAJI

10. Wewe ni mwanafunzi wa Kidato cha Pili katika Shule ya Sekondari Uhuru, S.L.P 120, Newala. Mwandikie barua baba yako anayefanya kazi katika Kiwanda cha Mbao, Sanduku la Posta 599 Mtwara, kisha mfahamishe kuwa umeanza kufanya Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili na umejiandaa vizuri kwa upimaji huo.

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256