FORM TWO KISWAHILI NECTA 2016

2016 - KISWAHILI

SEHEMU A

1.  Soma hadithi ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata:

Katika nchi ya ughaibuni kulikuwa na mfalme mwenye dharau na maringo sana, aliwaona wananchi wake kama wajinga. Watu wake waliishi bila amani na walichukia vitendo vya mfalme wao. Mfalme huyo alikuwa anajigamba kuwa yeye ni tajiri kuliko wafalme wote katika nchi za jirani. Kwa ujumla mfalme huyo alikuwa mnyanyasaji na mwenyekebehi nyingi.

Mfalme alikuwa mwenye kufuru sana, hata alidiriki kutamka kwenye mkutano wa hadhara kuwa hajawahi kuona njaa. Mzee mmoja mwenye busara aitwaye Bwana Adili alimwambia mfalme kuwa asihofu atampeleka mahali njaa inakopatikana. Bwana Adili kwa kukubaliana na mfalme walipanga siku ya safari ya kwenda kumwonesha mahali ilipo njaa. Safari hiyo ilikuwa na masharti kuwa hakuna kula chochote asubuhi na hakuna kubeba masurufu yoyote yakiwemo maji, ingawa Bwana Adili kwa ujanja wake alibeba.

Safari ilianza asubuhi mapema huku mfalme akiwa na furaha kubwa ya kwenda kuona njaa. Walitembea mwendo wa saa zisizopungua ?ita, mfalme akawa amechoka sana akamwomba Bwana Adili wapumzike. Uchovu huo ulitokana na ukweli kwamba mfalme hakuwahi kwenda mwendo mrefu kwa miguu. Wakati wa mapumziko mfalme alimwomba Bwana Adili maji na mkate lakini Bwana Adili alimnyima, walipumzika kwa muda wa saa moja na safari ikaendelea. Ilipofika jioni mfalme alikuwa amechoka kabisa kwani mwendo ulikuwa mrefu na njaa ilimuuma mno. Walipumzika chini ya mti, mfalme alimuuliza Bwana Adili, mbona hatufiki safari yetu? Bwana Adili hakumjibu chochote bali alichukua mkate akala na kunywa maji, mfalme alihisi njaa kali, alimwomba Bwana Adili mkate na maji lakini alimnyima.

Hali ya mfalme ilizidi kuwa mbaya sana, ndipo Bwana Adili akamwambia nitakupa maji na mkate ule lakini uahidi kwa maandishi kuwa utaacha dharau na majivuno kwa watu. Mfalme alipiga magoti mbele ya Bwana Adili na kuchukua karatasi na kalamu aliyopewa na Bwana Adili na kuahidi kwa maandishi kuwa ataacha kabisa tabia ya dharau na majivuno. Bwana Adili alipokea maelezo ya mfalme na akampa mkate na maji. Mfalme alipomaliza kula alimshukuru sana, ndipo Bwana Adili alipomgeukia mfalme na kumweleza kuwa hakuna maskani ya njaa bali hali aliyokuwa nayo mtu asipokula chakula. Waliporudi mfalme aliitisha mkutano wa hadhara. aliwaomba radhi wananchi wake na tangu siku hiyo mfalme aliishi kwa upendo na wananchi wote.

Maswali

(a)(i)     Bwana Adili alitoa masharti gani ya safari?.........................................

(ii)    Kwa nini Bwana Adili alitoa masharti uliyoeleza katika kipengele

(b)     Toa methali moja inayolingana na fundisho linalopatikana katika hadithi uliyosoma.

(c)     Toa maana za maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika hadithi uliyosoma:

(i)Anajigamba ..................

(ii)Kebehi .....................

(iii) Kufuru ..................

(iv)Masurufu . .......................

 (v) Maskani....................

(d)     Andika ufupisho wa habari uliyosoma kwa maneno 60.

View Ans


SEHEMU B

MATUMIZI YA LUCHA NA USAHIHI WA MAANDISHI

2. (a) Andika kwa usahihi maneno yaliyokolezwa wino kama yalivyotumka katika tungo zifuatazo:

(i) Mashirikiano ni muhimu kwetu .................

(ii) Mimi ni mwanainji wa Tanzania ...............

(iii)Mama anakaaga jikoni anapopika ............

(iv) Hakuna mapungufu yaliyojitokeza ........

(v) Hajafika mwanafunzi yoyote leo ..................

(vi) Huyu ni rafiki angu.................................

(b)     Eleza maana mbili kwa kila tungo.

(i) Mama anaota.

(ii)Tafathali nipe sahani ya kulia.

(iii)Vijakazi wanalima barabara.

(iv)Amekanyaga mtoto.

(v) Shangazi anawachezea wanangu.

(c)     AndikaKWELI kama sentensi ni sahihi au SIO KWELI kama sentensi si sahii
(i) Tafadhali mpikie ugali. Hii ni tungo tata .........

(ii) Kifaa kinachotumika kulia chakula kiitwacho uma wingi wake ni uma ... ... ...

(iii) Rejesta ni misimu ya Kiswahili . 

(iv) Amekula chumvi nyingi. Hii ni nahau 

(v) Mbili kutwa mara tatu. Ni rejesta ya kujifunza hesabu ........

View Ans


SEHEMU C

SARUFI

3. (a) Bainisha aina za maneno yaliyopigiwa mstari katika tungo zifuatazo: Mfano: Sisi tunacheza mpira uwanjani.

Jibu: Kiwakilishi ... .... ..... ......

(i)Kukuy_u bandani . .............

(ii)Maskini! Ameumia! ...............

(iii)Wako hatakiwi hapa .................

(iv)Dagaavva Kigoma ni watamu ................

(v)Mtoto alikuwa anacheza mpira . ..................

(b) Unda vitenzi kutokana na nomino zifuatazo:

(i) Kiumbe                                                

(ii) Pigo  

(iii)Mteule  

(iv)Mlinzi    

(v)Kiongozi

(vi) Mchezo 

(vii) Adhabu

(viii) Muundo  

(ix) Chakula

(x)  Mtego 

(c) Tunga sentensi kwa kutumia aina za maneno zifuatazo:

Mfano: Jana usiku litumike kama kielezi

Wote wawili waliondoka jana usiku  

(i) Mimi litumike kama kiwakilishi . ................

(ii) Letu litumike kama kivumishi . ...............

(iii) Tutaendelea litumike kama kitenzi kisaidizi .................. 

(iv) Na litumike kama kiunganishi . ..........................

(v) Upendo litumike kama nomino dhahania ..................

View Ans


SEHEMU D

FASIHI SIMULIZI

4.    (a) Kamilisha methali zifuatazo:

(i)Kuishi kwingi ......................

(ii)Mchuma janga ....................

(iii)Chanda chema ...................

(iv) Asiyekubali kushindwa ....................

(v) Jambo usilolijua ............................

(b)     Bainisha tofauti tano zilizopo kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi.

(c)     Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata:

Mada iliyo moyoni, hii ninawaletea,

Watoto wa mitaani, mada nimeshafungua, 

Wanapata mitihani, katika hit dunia,

Nawaonea huruma, imewatupa dunia.

Wanashinda jalalani, hayo ndiyo mazoea,

Umkute kituoni, anaomba abiria

Ni njaa mwake tumboni, ndiyo inasumbua,

 Ataomba kwa imani, huku anakulilia.

Wapo pia maaluni, vibaya wamezoea,

Hawaombi wala nini, kaziyao kukwapua,

Husimama vituoni, abiria kuvizia,

Abiria wanalia, kila kitu kimekombwa.

Twajenga taifa gani, watoto kuachilia? 

Wazurure mitaani, na Sisi twachekelea,

Tunadhania utani, na mwishowe tutalia,

Kwani mzaha mzaha, hutumbukia usaha.

Maswali

(i)Bainisha muundo na mtindo wa shairi hili.

  • Muundo wa shairi hili ni . ...  
  • Mtindo wa shairi hili ni .. ....

(ii) Eleza dhamira ya mtunzi katika ubeti wa Pili.

(iii) Eleza ujumbe wa shairi hili.

(iv) Toa methali nyingine moja yenye maana sawa na methali iliyopo katika ubeti wa nne.

Andika kichwa cha habari cha shairi kisichozidi maneno matano na kisichopungua maneno matatu.

View Ans


SEHEMU E

UANDISHI WA INSHA/UTUNGAJI

5. Wewe ni mwanafunzi wa Kidato cha Pili katika Shule ya Sekondari Tegemeo,  S.L.P 130, Dodoma, una matatizo ya kiafya, hivyo unahitaji kwenda kutibiwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Andika barua kwa Mkuu wako wa Shule kuomba ruhusa ya siku mbili (02). Jina lako liwe Juhudi Sabuni.

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256