K1SWAHILI - 2010
SEHEMU A UFAHAMIJ
1. Wewe ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika kilili chetu, umechaguliwa kusoma risala kwa Mgeni Rasmi. Soma risala hiyo kisha jibu maswali yanayofuata.
Ndugu Mgeni Rasmi,
Mustakabali wa taifa letu na raia wake upo katika hati hat] iwapo half iliyopo sasa miongoni mwa viongozi wetu tuliowapa dhamana kubwa ya kuliongoza taifa hill haitadhibitiwa. Ubinafsi uliokithiri, rushwa, ufisadi ubadhirifu wa mall ya umma, uhujumu uchumi, jambazi, dhuluma, utapeli, mauaji ya imani za kishirikina na uovu wa kila aina umekuwa ndio sera yao. Dhamira njema ya ukombozi wa wananchi kufikia maisha bora kwa kila Mtanzania itakuwa ndoto za alinacha tu kama hautakuwepo utashi wa dhati wa kisiasa wa kupambana na hall hiyo.
Ndugu Mgeni Rasmi,
jambo la kuSikitisha ni kuendelea kukua kwa kasi pengo lililopo baina ya wenye nacho na wasionacho; yaani matajiri na maskini katika jamii inayoamini katika misingi ya usawa wa binadamu. Katika jamii hii ya tabaka la wakulima na wafanyakazi; wapo watu wenye fedha nyingi wanaishi maisha ya kifahari sana na kuwaacha wengine wengi ambao hata kupata mlo kamili wa siku ni shida. Wengi hawana ajira za kuaminika wala mitaji au elimu ya ujasiriamali, wakijaribu kukopa mikopo midogo midogo wafanye biashara ill kujikwamua kiuchumi, Lakin' wapi! Wametumbukia katika la umaskini uliokithiri.
Maisha yamekuwa ya samaki baharini. Samaki mkubwa kumla mdogo!
Ndugu Mgeni Rasmi,
Vita juu maadui wakubwa wa jamii yetu, ujinga, umaskini na maradhi imekuwa ni nadharia tu. Vifo vya wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano vimeongezeka. Kipato cha Mtanzania kinazidi kushuka na thamani ya fedha yetu halikadhalika. Utandawazi ulikusudiwa kutupatia wajomba kwa jina maarufu "wawekezaji" iii waje kutukwamua kiuchumi. Wote tuliweka matumaini ya kukua kwa uchumi na kuongezeka kwa nafasi za ajira katika viwanda, migodi, mashamba, mabenki, mashirika na makampuni katika sekta binafsi. Hata hivyo hall si ya kuridhisha; wajomba wengi "wanatula visogo", Wanakula vyetu huku wanatung'ong'a. Wanawasainisha waheshimiwa wetu ya ulaghai, na wanatumia udhaifu uliomo ndani ya mikataba hiyo kuhamisha utajiri wetu kwenda kwao. Madini, mbao hata wanyama! Maskini, wajinga ndio waliwao. Usimwamshe aliyelala usije ukalala wewe.
Ndugu Mgcni
Leo hii kumeanza kuzuka migogoro ya kugombea ardhi; baina ya wakulima na wafugaji, wawekezaji na wanavipp na viongozi na raia. Mahali pengine kama vile kule Kilosa damu ilimwagika. Hii si dalili nzuri kwa mustakabali wa taifa letu, amani yetu tuliyojivunia kwa kitambo sasa Ltilaiwvka rehani. Ukiona vyaelea vimeundwal.
Ndugu ivigeni Rasmi,
Hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha. Dalili ya mvua ni mawingu. Dalili za kuzinduka kutoka katika usingizini mzito zinaanza kuonekana. Tumeanza kufuta matongotongo. Hoja za kuhoji na hatimaye kukubali kuirejea baadhi ya mikataba tuliyoingia kichwa kichwa inayoonesha kila dalili za kiwingu cha rushwa ni hatua ya kujivunia. Mapambano dhidi ya ufisadi na uimarishaji wa demokrasia na miundo mbinu ya nchi ni hatua ya mafanikio. Wabunge bila shaka mtaendelea kuisaidia serikali na sekta binafsi kuboresha mazingira yaliyopo iii kusaidia kuinua uchumi wa nchi yetu na mtu mmoja mmoja. Changamoto kubwa mliyonayo ni kubaini nafasi za ajira na kuongeza mitaji kwa makundi ya kijamii. Mnapoomba kura zetu zingatieni hayo.
MASWALI
(a) Andika kichwa cha habari uliyosoma kwa maneno yasiyozidi matano.
(b) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika
- Mustakabali
- Hatihati
- Lindi la umaskini
- Mikataba
- Weka rehani
(c) (i) Jambo gani linalomsikitisha mwandishi wa risala hii?
(ii) Je Mgeni Rasmi katika hafla hii ni nani? Mtaje kwa wadhifa wake.
(d) Andika ufupisho wa habari hii kwa maneno yasiyopungua 50 na yasiyozidi 80.
View Ans
2. (a) Kwa kila kauli hapo chini andika kwa kauli ambayo ni sahihi na kwa kauli ambayo si sahihi mbele yake.
- Fani na maudhui ni nyanja kuu mbili za lugha.
- Mawasiliano ya binadamu hutumia zaidi vyombo vya habari na simu za mikononi.
- Utumizi wa lugha hubadilika kutokana na muktadha, mada, wahusika na kusudi la mazungumzo.
- Lugha ni sauti za nasibu zenye kubeba maana iii kuwasilisha ujumbe kwa hadhira husika. ....... .....
- Umbo, sauti, mpangilio na maana ni tanzu nne za lugha.
View Ans
(b) Lugha ina dhima nyingi katika jamii. Taja dhima tano tu.
View Ans
(c) Rekebisha sentensi zifuatazo na uziandike upya kwa kuzingatia pia usanifu wa lugha.
- Siku zote tunaendaga kumsalimia.
- Kikao kiliadhimia kukupandisha cheo.
- Tasavali usiniache peke yangu.
- Ni budi kila mtu abebe mzingo wake.
- Kikao kimehairishwa hadi kesho.
View Ans
3. (a) Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.
Juu ya mti alikwea mkwezi; sikumtambua, ulikuwa mrefu, naye aliangua nazi. Zilidondoka kwa shindo moja baada ya nyingine Pu! Pu! Pu! Nilipoangalia juu ya kuti, hamadi! Joka la kijani. Nilipiga yowe uwii shuka! Shuka haraka kuna nyoka! Yule kijana aliruka toka juu Nadi chini. Sikuweza kumtazama, niliogopa.
- Bainisha vitenzi vikuu vitano katika kifungu hicho cha habari.
- Kwa kila kitenzi kikuu ulichobainisha onesha kiini cha neno.
View Ans
(b) Jedwali lifuatalo lina istilahi zenye fasili zilizotolewa hapo chini. Tafuta maneno hayo na uyaandike mbele ya maelezo yaliyo sahihi.
(i) ........ ni kitabu cha marejeo chenye msamiati uliokusanywa
kutoka kwa watumiaji wa lugha fulani. Maneno hupangwa kwa utaratibu wa kialfabeti, hutoa maana na ufafanuzi wa utumizi wa maneno na jinsi yanavyotamkwa.
(ii) ........... ni maneno yaliyoingizwa katika Kamusi na kuandikwa kwa
wino mzito na kupewa ufafanuzi.
(iii] ...... ni neno pamoja na ufafanuzi wake katika kamusi. Kwa mfano: Baba - Mzazi wa jinsi ya kiume.
- ...... ni neno au sehemu ya neno iliyo ndogo kabisa yenye maana kisarufi na ambayo haiwezi kugawanyika zaidi bila kubadili maana ya neno.
- ni vipande vya maneno vinavyopachikwa kabla na baada ya
mzizi wa neno katika vitenzi.
View Ans
SEH EMU D: FASIHI SIMULIZI
4. (a) Soma maelezo yafuatayo kisha onesha yanatoa fasili ya istilahi gani kati ya hizo ulizopewa kwenye kisanduku cha majibu.
(i) Kauli yenye picha za mafumbo na inayoonesha ukinzani wa fikra au tukio.
(ii) Ni maigizo yenye visa virefu vinavyoakisi maisha ya jamii Fulani.
(iii) Utungo ambao mtunzi hujitukuza na kujifanya shujaa mwenye uwezo wa kutenda matendo makuu kinyume na uwezo kwa kawaida wa binadamu.
(iv) Tungo za fasihi simulizi zitumiazo lugha ya nathari kufikisha ujumbe kwa hadhira.
(v) Ufundi wa kuwasilisha ujumbe kwa hadhira husika kwa kutumia lugha au Vitu halisi kama vile picha au vinyago.
Namba | Jibu |
| Majigambo |
| Sanaa |
| Ushauri
|
| Methali |
| Sanaa za maonyesho |
View Ans
(b) Soma utungo ufuatao kisha hakiki maudhui yake.
Mtini lilichanua,
Jua linakotokea,
harufu yoke murua,
Ua langu.
Kucha kutwa nalilea,
gharama kubwa kutoa,
maji nalimwagilia,
Ua langu.
Udongo kutifulia,
na mbolea kumwagia,
siachi kuzungukia,
Ua langu.
Jana lipotembelea,
kituko kimetokea,
nyuki kanyemelea,
Ua langu.
Ndani Bwana kaingia,
ala sivyogharamia,
maskini mi-nalia,
Ua langu.
Napita naulizia,
nataka hasa kujua,
sababu nichukulia,
Ua langu.
Kwani kwingine situa,
Ukaja kwangu kutua,
Kwa ubabe kuchukua,
Ua langu?
Wai-lahi nakuapia,
Hata kama kwa jambia,
Lazima utaachia,
Ua langu.
MASWALI
- Nini dhamira ya mtunzi wa utungo huu?
- Je, kuna mgogoro gani unaomkabili mtunzi?
- "Kizuri kina gharama". Je, ni kwa namna gani mtunzi wa utungo huu anathibitisha usemi huo?
- Ungekuwa wewe ni mtunzi; ungechukua hatua gani dhidi ya aliyechukua Ua lako?
- Taja fundisho ulilopata kutokana na tukio lililomtokea mtunzi wa utungo huu.
View Ans
5. Umepokea kadi hiyo hapo chini ya mwaliko wa harusi ya rafiki yako aliyehitimu kozi ya Ualimu. Amekuagiza uisome kisha umwandikie barua rasmi Mkuu wa shule ya Sekondari Jitegemee kumwomba ahudhurie sherehe hizo kwani alitoa mchango mkubwa uliomsaidia kufaulu Kidato cha Sita.
Familia ya Bw. na Bi, Sikudhani Sikumoja Ingekuwa hivyo wa Mtoni Kijichi Dar es Salaam wanayo furaha kukualika/kuwaalika dw./Bi./Bibi/Dic./ Proi./iVich./Mv, Mkubwa Kubwa kwenye sherehe ya harusi ya kijana wao mpendwa Msomi anayetarajia kufunga ndoa na Bi. Tunu kwenye kanisa la Mtakatifu Bwana la Mtoni Kijichi siku ya Jumamosi tarehe 05/12/2010 saa 9.00 alasiri na baadaye kwenye tafrija maalumu itakayofanyika ukumbi wa Mtoni Kijichi kuanzia saa 12.00 jioni.
Tafadhali fika na kadi hii iii kuepuka usumbufu.
Majibu kwa wasiofika piga simu namba 0656000011 au 025100001
View Ans