FORM TWO KISWAHILI NECTA 2009

KISWAHILI 2009

SEHEMU A

UFAHAMU

1. Soma barua ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata,

Ndugu Mhariri,

Naomba unipe nafasi katika gazeti lako la "SAUTI YA MSOMAJI" ili niweze kutoa dukuduku langu kwa jamii ya Watanzania. Tanzania kama nchi nyingine zinazoendelea imekumbwa na wimbi kubwa Ia mabadiliko ya jamii kutokana na athari za utandawazi. Wimbi kubwa Ia vijana limekuwa likitoka vijijini kukimbilia mijini kama vile nzige wavamiavyo shamba. Leo hii si Dar es Salaam, Arusha wala Mwanza, miji yote imefurika vijana wanaotafuta ajira, wengi ni vijana waliohitimu elimu ya msingi na elimu ya sekondari. Kila mwaka lipo ongezeko kubwa; athari ya ongezeko hili ni kuibuka kwa vitendo vya uhalifu wa kutumia nguvu, vitendo vya ukahaba, utumiaji wa madawa ya kulevya ubakaji, ushoga na kubwa zaidi ni kuongezeka kwa kasi ya maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI.

Tatizo Ia UKIMWI limesababisha ukiwa katika familia nyingi. Kumekuwa na idadi kubwa ya wajane na watoto wa mitaani. Wote hawa wamekuwa wakizurura ovyo mijini, wengine wakijiingiza kwenye kundi Ia ombaomba na wengine kwenye madanguro. Shida kubwa zaidi naiona kwa watoto wa mitaani. Hawa wamekuwa huru kama kondoo asiyekuwa na mchungaji au niseme mbuzi waliolishwa kago ambao hawafai kwa supu wala kufuga; kila mmoja anawapisha wapite. Hakuna anayejali watakula nini, wanalala wapi au wanaishi vipi! Nionavyo mimi hii ni dosari katika jamii, tena ni dhambi. Hawa ni binadamu sio mbuzi. Uchungu wa mwana aujuae ni mzazi, lakini kama watoto hawa ni yatima nani anawajibika nao? Hawana wajomba! Hawana shangazi, Hawana baba wadogo au mama wadogo! Kama hao wote hawapo je hakuna majirani? Mbona tunaingia makanisani na misikitini ambako tunafundishwa kutenda mema. "Mpende jirani yako kama nafsi yako" Upendo uko wapi katika jamii yetu? Waumini na viongozi wa dini wanayo changamoto kubwa; na pengine niseme wajiandae kujibu swali " Wamefanya nini" kwa ajili ya wajane, yatima na watoto hawa wa mitaani mbele ya Mwenyezi Mungu wakati ule wa hukumu ya mwisho.

Kwa upande mwingine niulize serikali: Je, inafanya nini kudhibiti au Iqopunguza jeshi hili kubwa la watoto wasio na ajira wala mtaji zaidi yci roho zao? Je, haioni yanayotokea nchi za wenzetu wa jirani ambao wo tu waovu wamewakusanya watoto hawa masikini na kuwatumia Ionna askari wa kupigania matakwa ya nafsi zao wenyewe?

Ni vizuri serikali kuchukua tahadhari mapema maana ni heri kuziba lik

Nayapongeza mashirika binafsi yanayochukua dhamana ya Iquwatafuta, kuwakusanya na kuwahudumia watoto hawa; ingawa yapo machache ambayo yamewageuza watoto hawa kama chambo cha kujipatia misaada toka nje kwa ajili ya kujitajirisha badala ya kuwahudumia wahanga hawa.

Ili kupunguza au kuondoa tatizo la kuenea kwa maambukizi mapya UKIMWI, utumiaji wa madawa ya kulevya, mimba za utotoni, ajira mbaya ya watoto ni lazima serikali iweke mikakati ya muda mfupi na mrefu kukabiliana na tatizo hili. Chelea chelea unaweza Iqukuta mwana si wako. Ujinga, umasikini na maradhi vitaendelea kwa kasi katika taifa hili kama hali ya kuendelea kukua kwa kundi hili haitadhibitiwa.

Mtendawema Mtuwangu, 

S.L.P 6700,

Dar - es - Salaam.

MASWALI

(a) Andika kichwa cha habari uliyoisoma kwa maneno yasiyozidi matano

View Ans


(b) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika: 

(i) Ukiwa

(ii) Madanguro

(iii) Heri kuziba ufa kuliko kujenga ukuta

(iv) Wahanga

View Ans


(c) Eleza athari za kuendelea kuwepo kwa tatizo la watoto wo mtaani katika jamii. (Taja tatu)

View Ans


(d) Fikiria kwamba wewe ni mtangazaji wa Redio "SAUTI YANGU" umesoma, barua hiyo ya msomaji kwenye gazeti la "SAUTI YA MSOMAJI" iandike habari uliyoisoma kwa maneno kati ya 50 na 80 ili iweze kusomwa kwenye kipindi cha "Magazetini leo".

View Ans


SEHEMU B

UTUMIZI WA LUGHA NA USAHIHI WA MAANDISHI

2. (a) Soma dayolojia ifuatayo kisha onesha makosa ya kisarufi yaliyojitokeza na uziandike sentensi zenye makosa kwa usahihi.

Jirani: Unazania utampata?

Mzee Dumba: Wewe ndiye mwisi wangu au vipi?

Jirani: siyo hivyo

Mzee Dumba: Ngo'mbe ile ina samani kubwa, haiwesi kwenda hivi hivi, afadhali ingechukua mbusi

Jirani: Mlinzi alikuwa wapi wakati ngo'mbe anaibiwa?

Mzee Dumba: Juma Jana ilikuwa ina ugonjwa wa Malaria, ilikwenda hospitali, lakini sijui ilikuwa na nani.

View Ans


(b) Onesha muktadha wa utokeaji wa rejesta zifuatazo:

(i) "Ukuti ukuti wa mnazi wa mnazi ukija upepo! Wapepea!" Muktadha wa

(ii) Haya wote tusimame ni wakati wa kusifu sasa.

Muktadha wa

(iii) Jamaa alichukua mvua tatu; du! Tutamsahau kabisa. Muktadha wa .

(iv) Mheshimiwa; kwa idhini yako naomba kuwasilisha vielelezo vifuatavyo mbele yako.

Muktadha wa

(v) Funga goli! Mwanga yuko mbele, tutapigwa bao.

Muktadha wa

View Ans


SEHEMU C

SARUFI

3. (a) Onesha mfuatano wa maneno yafuatayo katika mpangilio wa alfabeti ndani ya kamusi. Andika jibu Kwa tumia herufi A - E 

  1. Tafrani = A
  2. Takabali =B
  3. Tafadhali = C
  4. Tashtiti = D
  5. Tazama = E
View Ans


(b) Unda maneno mawili ya Kiswahili lcwa Eila mzizi uliopewa hapo chini:

  1. -pamb- 
  2. -it-
  3. -on-
  4. -la-
  5. -chek-
View Ans


SEHEMU D FASINI SIMULIZI 4. (a) Taja methali moja ambayo ungeweza kuitumia kuonya au kuadilisha kulingana na tukio Iililoelezwa hapa chini. Mfano: Mtoto alilelewa vibaya na hatimaye akawa jambazi. Methali: Samaki mkunje angali mbichi. (i) Ndege alijenga kiota kwa kuchukua jani moja moja na hatimaye baada ya siku tatu kiota kilikamilika kujengwa. Methali: . . . . . . . . . . . (ii) Wastara alikuwa masikini, akajibidisha sana kufanya kazi usiku kucha hatimaye akafanikiwa kupata utajiri na kuishi maisha yenye hadhi. Methali . . . . . . . . . . . . . (iii) Simba alivamia zizi Ia Mzee Mahende na kukamata ngo'mbe mmoja, alipotoka na mkuki kumkabili, alishindwa akarudi nyuma kwa hofu; kisha alipiga yowe. Wanakijijji walikusanyika, wakiwa na mikuki na mapanga, na marungu wakampiga wakamuua. Methali: . . . . . . . . . (iv) Dereva aliendesha gari kwa kasi na kusababisha ajali mbaya. Methali: . . . . . . . . . . (v) Baba alipofiwa na mtoto wake alilia sana hadi akazimia. Methali: . . . . . . . . . . .View Ans


(b) Soma maelezo yafuatayo kisha jaza jedwali kwa neno moja lenye dhana inayoelezwa, herufi moja kila chumba kwenda kulia au chini.

  • Sherehe au ibada za kienyeji zifanywazo katika makabila zikiambatana na utoaji wa makafara kwa lengo Ia kuabudu mizimu, miungu au mapepo ili kuomba jambo Fulani. (i)
  • Tungo za maneno yenye maadili kwa jamii ambazo hutolewa katika mtindo wa uwili wenye ukinzani husemwa aghalabu katika kuonya au kufunda. (ii)
  • Jina Ia mhusika mnyama au ndege katika fasihi simulizi anayeweza kutumika katika simulizi za visasili. (iii)
  • Ni Manju au Mtambaji wa kazi za fasihi. (iv)
  • Kiishilizo cha kifungu cha maneno yenye ujumbe fulani katika mtindo wa ushairi. (v)
JEDWALI
View Ans


(c) Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali.

Wanangu mwanishangaza, hivyo ninavyowaona,

Nashindwa mate kumeza, mavazi mnayoshona,

Ni kiooyaangaza, nguo za ndani twaona, 

Hii ni tabia gani, mavazi mnayovaa?


Bintiyangu nakueleza, wengijua wakuona, 

Uache kujitembeza, nusu uchi kila kona,

Aibu watakubeza, watafutani we mwana?

Hii ni tabia gani, mwana kwenda tuputupu?


Manyonyoyanatokeza, makalio suguana,

Wadhani unapendeza, nguo zinavyokubana 

Waume wawachokoza, na ungali Shule mwana 

Hii ni tabia gani, nini hasa unauza?


Na kakio ashangaza, akili ni kama hana,

Vidonge anapomeza, tendojema mwana hana, 

Suruali analegeza, makalio kuyaona,

Hii ni tabia gani, wana kama sikuzaa?


Suruali aidebweza, nyani dume kufanana, 

Itwa shoga wa kupoza, eti "mpira wa kona.

" Wanja ameukoleza, avuta marijuana,

Hii ni tabia gani, mbona mwaniaibisha.


Utu mwaupoteza, utamaduni kukana,

Kuiga sitokaza, ila igayano mana, 

Kuiga bila uliza, ni kama akili huna, 

Sipo sikia wakuu, tende litakuotea.


Soma acheni kucheza, mwili hauna dhamana,

Afya ikikuteleza, ripea hakuna tena,

Tabaki kuomboleza, thamani takuwa huna, 

Tabia hiyo si njema, naonya wanangu acha.

MASWALI

(i) Nini dhamira ya Fanani?

(ii) Je, Fanani ana msimamo/mtazamo gani katika shairi hili?

(iii) Je, ni mgogoro gani umejitokeza baina ya wahusika?

(iv) Nini imani au falsafa ya Fanani kuhusu mgogoro huo?

(v) Je, umejifunza nini kutokana na shairi hili?

View Ans


SEHEMU E

UANDISHI WA INSHA/UTUNGAJI

5. Umepokea barua ifuatayo; soma kisha andika kadi ya mwaliko kwa kufuata maelekezo ya barua hiyo.

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256