FORM TWO KISWAHILI NECTA 2008

KIISWAHILI 2008

SEHEMU A

UFAHAMU

1. Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata. 

Bismilah rahmani, wanangu natabaruki, 

Mlio Bara na Pwani, salamu mwastahiki, 

Nataka niwaambieni,ya kale kizazi hiki,

Mambo sivyo yavyokuwa, zamani na siku hizi.


Wananguyafahamuni, mambo bado msojua,

Siku hizo za zamani, nyumba tulimokulia,

Tope nyasi ezekoni, bati katu halikua,

Zamani na siku hizi, mambo sivyoyavyokuwa.


Leo mpo ghorofani, mwavenea ka' chiriku,

Na lami barabarani, gari tele huku na huku,

Wamama wana sukani, waendesha kwa kupiku, 

Mambo sivyoyavyokuwa, zamani na siku hizi.


Tulopeleka Bungeni, wamegeuka nyang'au,

Mafisadi karna nini, baladhuli mabahau,

Wanauvutúa mpini. konde wamelisahau,

Zamani na siku hizi, mambo sivyo, zamani na siku hizi.


Uwe na mia ganjani, siku zile wewe mtu,

Tajaza kapu sokoni, na taksi hadi Kisutu,

Bado za bia mezani, za kumhonga bi Tatu, 

Mambo sivyoyavyokuwa, zamani na siku hizi.


Leo pesa si thamani, huwezijenga kwa laki,

Bei za vitu pomoni, za panda bila haki,

Mnyonge arudi chini, tajiri ndo atamalaki,

Zamani na siku hizi, mambo sivyoyavyokuwa.


Ingia mahakamani, rupia usipenyeze,

Jua chamtemakuni, ni haki haki iteleze,

Hakimu hana utani, unani akubembeleze, 

Mambo sivyo yavyokuwa, zamani na siku hizi.


Nako huko mashuleni, tumelishwa mahirizi,

Ametugawa shetani, mafungu kamaya ndizi, 

Hawa Sta Albani, wengine kule Chamazi,

Zamani na siku hizi, mambo sivyoyavyokuwa.


Mungu hako mioyoni, mtu hana woga tena,

Aua maalbini, ajuza na mwana wana,

Vichanga nao jamani, wakatwa shingo mchana, 

Mambo sivyoyavyokuwa, zamani na siku hizi.


Ukiuliza kwanini, mamboyotejibu pesa,

Wauzwa ughaibuni, mabinti vigoli hasa,

Na wengine kokeini, waipeleka Mombasa, 

Zamani na siku hizi, mambo yamebadilika.

MASWALI

(a) (i) Andika kichwa cha shairi hilo kwa maneno yasiyozidi matano (5).

View Ans


(ii) Fikiria kwamba wewe ni kiranja mkuu umepewa nafasi ya kuwaeleza wanafunzi wenzako kuhusu shairi hili, kwa kutumia maneno kati ya 50 na 100.

View Ans


(iii) Andika maelezo yako ukizingatia mambo muhimu tu.

View Ans


(b) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika. 

(i)wanauvunja mpini

(ii) kumhonga

(iii) pomoni

(iv) chamtemakuni

(v) ughaibuni

View Ans


SEHEMU B

UTUMIZI WA LUGHA NA USAHIHI WA MAANDISHI

2. (a) Kwa kuzingatia matumizi ya Kiswahili sanifu sentensi zifuatazo zina makosa. Ziandike upya kwa ufasaha.

Mfano: Kiti mkubwa amevunjika.

Jibu : Kiti kikubwa kimevunjika.

(i) Chai imeingia inzi.

(ii) Anakwenda baba kesho safari.

(iii) Humwambiaga lakini hanielewi!

(iv) Ngo'mbe zangu zimeibiwa.

(v) Daktari nina kifua sijalala usiku kucha.

View Ans


(b) Kama lugha isingekuwepo katika jamii ya binadamu, unafikiri ni matatizo gani manne ambayo yangetokea?

View Ans


(c) Oanisha orodha A na B ili kujenga dhana sahihi. Onesha majibu yako kwa kisanduku kama hiki.

Orodha A Orodha B

(i) Kuonesha mpangilio wa maneno ya lugha kialfabeti, jinsi yanavyoandikwa, kutamkwa na maana zake.

(ii) Lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi.

(iii) Maneno yasiyo sanifu yanayozungumzwa na kikundi kidogo cha watu.

(iv) Taaluma inayoshughulikia maumbo au mjengo wa maneno katika tungo.

(v) Ni mtindo wa lugha inayozungumzwa kulingana na muktadha na kusudi maalumu.


  1. Tanzu za lugha
  2. Rejesta
  3. Simo
  4. Sarufi maumbo
  5. Misemo 
  6. Mofimu
  7. Nomino
  8. Kamusi


Orodha A

(i)

(ii)

(iii)

(iv)

(v)

Orodha B






View Ans


SEHEMU C

3. (a) Majina yafuatayo katika Daftari la mahudhurio ya wanafunzi yamepangwa vibaya. Kwa kuzingatia matumizi ya kamusi yapange majina kwa mpangilio sahihi. 

(i) Roza

(ii) Sakina

(iii) Zena

(iv) Zakaria

(v) Yolanda

View Ans


(b) Tafakari matumizi ya mofimu katilca sentensi kwenye Orodha A kisha onesha matumizi sahihi kwa kuchagua kifungu cha maelezo yanayo oana toka Orodha B. Onesha majibu yako Kwa kutumia kisanduku kama hiki:

Orodha A Orodha B

(i) Ukimwona atakueleza ukweli

(ii) Anakipenda hikihiki cheusi

(iii) Kikombe kimevunjika

(iv) Kijidudu chenyewe kidogo

(v) Amepigana kiume


  1. Kuonesha udunishi
  2. Kuonesha ukaribu na msisitizo
  3. Kuonesha nafsi
  4. Kuonesha nafsi na njeo ya wakati ujao
  5. Kuonesha sifa ya juu/ushujaa 
  6. Kuonesha upatanisho wa kisarufi 
  7. Kuonesha kitu kilivyoathirika


Orodha A (i) (ii) (iii) (iv) (v)
Orodha B




View Ans


(c) Soma kifungu cha habari ifuatayo kisha ainisha maneno yaliyopigiwa mstari kwa kuandika ufupisho wa aina ya neno chini yake: (N, V, W, T, E, H au U)

”Bandubandu humaliza gogo. M?o?o alianza udokozi kidogokidogo. Mara kadokoa nyama jikoni, mara pipi dukani, mara daftari shuleni, mara  . . . . . Mama yake ukimwambia anakujia juu, mkali kama pilipili! Ukome! Mwache mwanangu, wizi umemfundisha wewe! Leo kabambwa mchana kweupe. Lo! Aibu. Mama analia kama mbwa koko; wale aliotuona adui zake ndio anatufuata tumsaidie. Polisi waitwe waje wachukue watu wao, mama na mtoto wote wapelekwe kituoni”.

View Ans


SEHEMU D

FASIHI SIMULIZI

4. (a) Kutoka katika kisanduku cha majibu chagua jibu lililo sahihi na kuliandika mbele ya namba ya maelezo yanayoelezea dhana hiyo.

Miv?ga, Ngano, Maghani, Vitendawili, Misimu, Nahau, ?ambiko, Ngonjera, Visasili, Methali, Fani, Maudhui

Namba moja imeshajibiwa kama mfano.

Mfano:

(i) Jumla ya mawazo au dhamira, migogoro, mtazamo/ msimamo, falsafa na ujumbe katika kazi ya fasihi.

Jibu: Maudhui.

(ii) Semi za muda na mahali maalumu ambazo huzuka na kutoweka kutegemea na mazingira na mahitaji ya janjii husika.

(iii) Misemo yenye kueleza wazo lililofichika maelezo yake huwa na ukinzani wa pande mbili.

(iv) Majibizano, mjadala au malumbano ya watu wawili au zaidi katika mtindo wa kishairi.

(v) Hadithi zinazosimulia matukio ya kihistoria na kuhusisha mambo yanayosadikiwa na jamii ya watu.

(vi) Hadithi zinazoelezea vyanzo au chimbuko la maumbileya binadamu, wanyama, miti au vitu visivyo na uhai. 

View Ans


(b) Chagua herufi ya jibu sahihi katika maswali yafuatayo:

(i) Ana "mkono mrefu" Maana yake:

  1. Urefu wa mkono wake umezidi kawaida
  2. Mlemavu wa mkono ndio sababu ni mrefu
  3.  Ana tabia mbaya
  4. Mdokozi au mwizi
Choose Answer :


(ii) Ipi ni maana sahihi ya kitendawili "kulia kwake ni kicheko kwetu".

  1. Machozi
  2. Maji
  3. Mvua
  4. Utomvu wa mpapai
Choose Answer :


(iii) Walikutwa darasani "wakipiga domo" badala ya kusoma. Kupiga domo ni kufanya nini?

  1. Kupayuka
  2. Kuteta watu
  3. Kusimulia hadithi
  4. Kusogoa
Choose Answer :


(iv) Simba mwendapole ndiye mla nyama” Methali hii ni sawa na: .........

  1. Mwenye kisu kikali ndiye awezaye kula nyama
  2.  Kawia ufike
  3.  Usiache mbachao kwa msala upitao 
  4. Bura yangu sibadili kwa rehani
Choose Answer :


(v) Pita huku nami nipite huku tukutane kwa mjomba”. Fumbua kitendawili hiki.

  1. Barabara
  2. Mkanda
  3. Ukili
  4. Mnyororo
Choose Answer :


(c) Soma wimbo ufuatao kwa makini kisha hakiki vipengele vya maudhui: Dhamira, mtazamo, falsafa, migogoro na ujumbe wa mwandishi.

"Siwema usinipe ugonjwa wa moyo

Nilidhani nimepata mpenzi wa kweli

Kumbe nimepatikana na mambo ya ajabu.


Wema wangu kumbe kwako ni bure

Fadhila zote kumbe kwako ni bure 

Nimejifunza kutokana na makosa 

Siwema dada mama.


Nimezunguka Tanzania bara

Unguja na Pemba kote nimefika

Nimewaona warembo wenye sifa

Wenye kujipamba na kupambika 

Kwa hiyo nielewe dada 

Sibabaiki na sura.


Napenda tabia njema

Tabia njema ndio silaha kwako

Sibabaiki na sura

Napenda tabia njema ....”


MASWALI

(i) Nini dhamira ya Fanani?

(ii) Je, Fanani ana mtazamo/msimamo gani kuhusu mapenzi?

(iii) Je, ni mgogoro gani umejitokeza baina ya wahusika?

(iv) Nini imani/FaIsafa ya Fanani kuhusu mgogoro huo? 

(v) Je, umejifunza nini kutokana na wimbo huu?

View Ans


SEHEMU E

UANDISHI WA INSHA/UTUNGAJI

5. Wewe ni mzazi wa Mwanafunzi Masumbuko Mtata aliyehitimu Elimu ya Msingi shule ya Juhudi, S.L.P 69, Mwanza. Umeona tangazo la nafasi ya masomo ya Kidato cha Kwanza kwenye gazeti la "Nipashe" la tarehe 02/11/2008. Andika barua kuomba nafasi kwa ajili ya mwanao. Tumia maneno kati ya 80 na 120.

TANGAZO

Mkuu wa Shule ya Sekondari Umoja ana Watangazia wazazi/walezi nafasi ya masomo ya kidato cha 1-4 katika shule mpya kabisa. Shule ni mchepuo  wa Sayan?i. Shule ipo jijini Dar-es-SaIaam çneo la Mbezi Beach, ni ya wa?içhana na wavulana. Ina nafasi za majengo na vifaa vya kutosha vya kufundishia ma kujifunzia. lna walimu wa kutosha, Masomo yote yatafundishwa, Ada ni rahisi huduma zote za jamii zinapatikana. Shule  itafunguliwa tarehe 6/1/2009. Tuma maombi yaka kwa: Mkuu Wa Shule S. L. P 3043 au Piga simu 0796-865708. Fomu za maombi ni sh. 10,000/= tu, zinapatikaiiâ  shuleni, Wahi mapema.

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256