FORM TWO KISWAHILI NECTA 2007

KISWAHILI 2007

SEHEMU A

UFAHAMU

1. Soma kifungu cha habari kifuatacho, kisha jibu maswali.

Miaka ya hivi karibuni kumetokea ajali nyingi hapa duniani. Wengi tumesikia taarifa za ajali mbalimbali kutoka katika vyombo vya habari na baadhi yetu tumeshuhudia kwa macho yetu ajali hizo. Kila aliyesikia au kuona ajali hizo alivaa uso wa huzuni; kwani nyingi zilikuwa za kutisha mno. Wapo watu waliokatika miguu, mikono, masikio na hata kunyofolewa macho na viungo vingine vya mwili. Ukiachilia mbali majeruhi na wale walionusurika, wapo ndugu na marafiki zetu waliopoteza maisha. Wengi tulipata machungu yaliyokithiri, tulilia, tulilaumu na kuwalaani wote tuliofikiria ndio waliosababisha ajali hizo.

Waliokufa katika ajali hizo ni watoto wadogo, watu wazima na hata vikongwe, wanawake kwa wanaume. Kama ilivyo desturi, kifo hakibagui na kwa kweli huvuna roho za watu wa umri na jinsia zote.

Wazazi wengi wanaofariki katika ajali hizi huacha watoto ambao hawamo katika utaratibu wa kuendelezwa kielimu. Badala yake, wanaingia katika kujitafutia riziki badala ya kujisomea. Watoto wengi hufanya kazi za kubeba mizigo, uvuvi, kuchimba madini migodini, vibarua mashambani, biashara ndogondogo na hata kazi za nyumbani.

Watoto hao walioachwa hukumbwa na matatizo mengi wafanyapo kazi katika sehemu hizo. Kwa kuwa wengi wao hawana upeo mkubwa wa mambo, hujikuta wakifanya kazi bila kufuata kanuni za kiafya. Hali hiyo huwasababishia magonjwa kama kifua kikuu na hata kupata ajali mbaya, wafanyapo kazi migodini, ambazo zinaweza kusababisha vifo au vilema vya maisha. Wengine huingizwa kwenye biashara za ukahaba na kupata mimba zisizotarajiwa, tena katika umri mdogo. Wengine huambukizwa magonjwa kama UKIMWI.

Pamoja na ukweli wa usemi kuwa "Ajali haina kinga," ajali nyingi zinazotokea zinatokana na makosa yetu wenyewe. Hizi tukiamua, tunaweza kuzizuia kwani penye nia pana njia. Hivyo hivyo, suala la kuwapatia elimu watoto walioathirika na ajali liwe la kufa na kupona. Kama Taifa, ni lazima tupige vita ajira kwa watoto, ikiwa kweli tunataka kwenda na wakati. Vinginevyo tutabaki nyuma.

MASWALI

(a) Kwa swali la (i) hadi (vi) andika herufi ya jibu sahihi kuliko yote.

(i) Mwandishi anafahamisha kuwa wanaokufa katika ajali mbalimbali ni:

  1. Watu wa aina zote.
  2. Watoto wadogo. 
  3. Watu wazima.
  4. Vikongwe, wanawake na wanaume.
Choose Answer :


(ii) Ipi si kweli kuhusu maeneo wanakoajiriwa watoto?

  1. Kwenye machimbo ya madini
  2. Kwenye biashara ndogondogo
  3. Kazi za nyumbani
  4. Kwenye ofisi za serikali
Choose Answer :


(iii) Ajira kwa watoto husababishwa na:

  1. Kutokuwepo kwa shule za kutosha
  2. Vifo vya wazazi na ugumu wa maisha
  3. Kampeni za vyama vya siasa
  4. Madeni ya nchi
Choose Answer :


(iv) Ili watoto waweze kufanikiwa katika maisha yao ya baadaye, lazima jamii:

  1. Ipige vita rushwa.
  2. Ifuate siasa ya ujamaa na kujitegemea.
  3. Iwape watoto elimu. 
  4. Ijenge barabara nzuri.
Choose Answer :


(v) Moja ya haya yafuatayo sio ajali ya kujitakia: 

  1. Gari kuanguka kutokana na mwendo wa Rasi.
  2. Kuzidisha uwezo wa uzito katika vyombo vya usafiri. 
  3. Kuendesha vyombo vya usafiri pasipo kuzingatia kanuni na sheria.
  4. Kuzuka kwa vimbunga vinavyoleta maafa makubwa.
Choose Answer :


(vi) Mwandishi anaamini kuwa tunaweza kuzuia ajali zisitokee kwa:

  1. Kumwomba Mungu atuepushe na ajali hata kama sheria na kanuni hazifuatwi.
  2. Kutoendesha magari katika barabara mbaya.
  3. Kuwa makini katika kuendesha vyombo vya usafiri.
  4. Kutowaruhusu wazazi wenye watoto kutumia vyombo vya usafiri.
Choose Answer :


(vii) Eleza maana ya misemo ifuatayo kama ilivyotumika katika habari uliyosoma.

  • Alivaa uso wa huzuni . . . . . . . .
  • Liwe la kufa na kupona . . . . . . .
  • Penye nia pana njia . . . . . . . . . .
View Ans


(viii) Andika kichwa cha habari hii kisichozidi maneno matatu.

View Ans


(b) Andika ufupisho wa habari hii usiozidi maneno sitini (60).

View Ans


SEHEMU B

LUGHA KWA UJUMLA NA UTUMIZI WAKE

2. (a) Kwa kila sentensi zifuatazo andika KWELI au SI KWELI katika nafasi zilizoachwa wazi.

(i)Lugha ni kitambulisho muhimu cha jamii.

(ii)Fani na maudhi ni nyanja kuu za lugha. .

(iii) Umbo, sauti, mpangilio na maana ni tanzu nne za lugha.

(iv) Mawasiliano ya binadamu hutumia zaidi vyombo vya habari na simu tu. ............

(v) Lugha hubadilika kutokana na muktadha.

View Ans


(b) Sentensi zifuatazo Zina utata. Kwa kila sentensi andika maana mbili ili kuondoa utata huo.

(i)) Nimekutana nao wamebeba paa.

(ii)Mzee Juma amepanga chumba.

(iii) Daktari huyu ndiye aliyeniunga mkono.

(iv) Utakapokuja, uje na nyanya.

(v) Hii si nyumba ya wageni.

View Ans


SEHEMU C

SARUFI

3.(a) Vifuatavyo ni vitenzi. Kwa kila kimoja unda nomino moja.

Cheza

Andika

Sema

Lima

Funga

View Ans


(b) Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo kwa kuandika ufupisho wa aina ya neno Chini ya neno lililopigiwa mstari.

Mfano: Mtoto yule anaimba na kucheza.

(i) Ubaya wake ni ubaya wao.

(ii) Ama kweli! kina cha maji katika Ziwa victoria kimepungua.

(iii) Ambao wameajiriwa watalipwa posho zao.

(iv) Bwalo la shule yetu limebomoka. (v) Wetu wamo zizini mwao.

View Ans


(c) Katika orodha ifuatayo, chagua mambo matano (5) ambayo yanapatikana kwenye kamusi, kwa kuweka alama ya vema (V) katika kisanduku.

(i) Asili ya neno

(ii) Mpangilio wa maneno kialfabeti

(iii) Viambishi

(iv) Matamshi ya neno

(v) Aina ya neno

(vi) Makosa ya kisarufi

(vii) Maana ya neno

(viii) Makosa ya kimantiki

(ix) Matumizi ya neno

View Ans


(d) Chini ya kila sentensi zifuatazo yapo maneno katika mabano, Chagua neno moja lililo sahihi zaidi na uliandike katika sehemu iliyoachwa wazi.

(i) Mwanahawa aliniita . . . . . . . . mtoto aliyekuwa akimsumbua kazini.

(nipigie, nimpige, nimpigize, nimpigie)

(ii) Ningejua ukweli wa mambo kabla ... ... ... hapa bure saa hizi.

(Nisifigalikuja, nisingekuja, singekuja, nisingelikuja)

(iii) Kama nikipata . . . . . . nitakuja ili tuzungumze.

(wasia, wasaa, saa, majira)

(iv) . . . . . yake ilikuwa kinyume kabisa na ukweli wa habari nzima.

(thana, zana, dhana, sana)

(v) Nyoka aliyetokea shimoni aliuawa baadaya .......... mafuta ya taa.

(Kumwagiliwa, kumwagiwa, kumwagilizia, kumwaga)

View Ans


SEHEMU D

UTUNGAJI

4. Kifuatacho ni kielelezo cha muundo wa barua rasmi/kikazi. Jaza vipengele husika.

View Ans


SEHEMU E

FASIHI SIMULIZI

5. (a) Kamilisha mchoro ufuatao.

View Ans


(b) Chagua kifungu cha maneno kutoka orodha B ambacho kinatoa maelezo sahihi ya neno/maneno yaliyoko kwenye orodha A. Andika herufi ya jibu sahihi katika nafasi iliyoachwa wazi.

ORODHA  A

(i) Utani

(ii) Fani

(iii) Michezo ya watoto

(iv) Methali, nahau, misemo

(v) Mandhari

(vi) Hadhira

(vii) Fanani

(viii)Ngano, visasili, tarihi

(ix) Maudhui

(x) Majigambo

ORODHA B

A. Hadithi fupi zinazosimulia asili ya watu, vitu na hata wanyama.

B. Mtambaji wa kazi ya fasihi simulizi.

C. Kujisifu kunakoambatana na matendo.

D. Shughuli zinazofanywa na watoto kwa lengo la kujiburudisha.

E. Mbinu anazotumia msanii ili kufikisha ujumbe kwa hadhira.

F. Wasikilizaji/watazamaji wa kazi ya fasihi.

G. Vipera vya utanzu wa semi.

H. Uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa.

Aina ya sanaa inayotumia lugha inapowasilishwa kwa hadhira.

Vipera vya utanzu wa hadithi.

K. Maneno ya mzaha pasipo kuchukia.

L. Ujumbe, dhamira, falsafa na ukweli tunaoupata kutoka kwa fanani.

M. Mazingira/mahali inapotendeka kazi ya fasihi. N. Mafumbo yanayohitaji kufumbuliwa.

View Ans


(c) Ni kwa vipi busara ya methali zifuatazo inaweza kwa upande mwingine kuleta hasara?

(i) Haraka haraka haina Baraka. 

(ii) Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.

(iii) Pole pole ndio mwendo.

(iv) Ajali haina kinga.

(v) Samaki mmoja akioza, wote wameoza.


View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256