1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali.
Miti ina faida nyingi sana kwa binadam . Nchi i?iyo na miti ni sawa na mtu ambaye amevuliwa nguo.
Kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya Watu na kutokuwepo nishati mbadala hasa sehemu za vijijini kama vile gesi, umeme nafuu kwa sehemu za mjini kumepelekea kuwepo na matumizi lukuki ya kuni na mkaa katika maisha ya kila siku ya binadamu. Hali hii imesababisha baadhi ya sehemu za nchi yetu kuanza kugeuka jangwa kutokana na watu kuzidi kukat miti ovyo; kama waswahili wasemavyo "usipoziba ufa utajengau ta".
Nchi yetu iliona„tatizo hilo na imeanzisha kampeni mbalimbali za kuwahamasisha wananchi kupanda miti kupitia katika vyombo vya habari kama vile redio, magazeti na lunjnga.
Vilevile imeanza misemo mbalimbali ama vile "kata mti panda miti", "Panda mti wa "millennium” na ia imeweka siku maalumu ya kitaifa ya kupanda miti. Kutokana na Kampeni hizo, upandaji wa miti nchini umeongezeka kufikia iti 120 milioni mwaka huu. Juhudi za Taifa letu katika kampeni hiz zinatokana na ukweli kuwa miti au misitu ni roho ya Taifa. Binadamu hufaidika na mambo mengi yanayotokana na miti.
Kutokana na miti, watu hujenga nyumba za kila namna. Wengine hupasua miti mikubwa minene na ku?ata mbao na boriti kwa ajili ya kuezekea nyumba. Fito zikifungwa na kamba nzuri na ngumu, tunapata nyumba imara.
Miti pia hupasuliwa ili kupata mbao za kutengenezea masanduku, kabati, meza na madawati, pia hutumiwa kutengenezea nyumba ambazo si ghali kama nyumba za matdfali ya saruji. Mashua na meli pia hutumia mbao na boriti wakati wa kuundwa. Miti huchongwa na uwa mitumbwi, fimbo, vinu, vinyago, mipini na sanaa mbalimbali. Kuni zinatumika kwa kupikia, kuchemsha maji na mkaa unatufaa kwa kazi nyingi.
Nchi i?iyo na miti haipati mvua, kwani miti hasa misitu husaidia kuvuta mvua. Zaidi ya hayo mizizi ya miti husaidia kushikamanisha udongo hivyo huzuia kumomonyoka kwa udongo. Chemçhem za maji pia zinapatikana ikiwa kuna miti ya kutosha na msitu.
Magome ya miti, majani na mizizi hutufaa kwa dawa mbalimbali zinazoponya magonjwa mbalimbali. Pengine hututia nguvu miili ama hutukinga kwa maadui kama nyoka.
Miti hutupa matunda ambayo ni matamu na ambayo ni mazuri kwa afya ya miili yetu. Machungwa, mapapai, maembe ni baadhi tu ya matunda ambayo tunayatumia kama chakula. Ni jukumu la kila mtu kuihifadhi miti na misitu yetu.
MASWALI
(a) (i) Andika kichwa cha habari uliyosoma kisichozidi maneno matano (5).
(b) Andika kweli kama uainishaji wa neno lililopigiwa mstari katika sentensi ni sahihi na andika si kweli kama uainishaji wa neno lililopigiwa mstari katika sentensi si sahihi
5. (a) Orodha A ina tanzu za fasihi simulizi na orodha B ina vipera vyake. Oanisha orodha A na orodha B kwa kujanza nafasi zilizoachwa wazi katika jedwali la orodha A.