FORM TWO KISWAHILI NECTA 2004

KISWAHILI 2004

SEHEMU A

UFAHAMU NA UFUPISHO

1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali.

"Musa, unamuona yule kijana, yulee. . . . . . . .  ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Angani.Yeye ni wa tabia chafu, anajihusisha sana na vitendo vya ngono. Hata hivyo, cha ajabu bado anad_unda" Samweli alimweleza Musa na huku akimnyooshea kidole kijana aliyekuwa akipita.

"Huwezi kumtambua mtu mwenye Ukimwi kwa kumwangalia tu. Mtu mwenye siha nzuri, mnene na mtanashati anaweza kuwa na virusi vya ukimwi, na mwingine mwenye kuonekana dhaifu na afya isiyoridhisha akawa hana virusi vya Ukimwi, na mwingine mwenye kuonekana dhaifu na afya isiyoridhisha akawa hana virusi vya Ukimwi. Hivyo umbile au muonekano wa nje wa mtu hauwezi kukuhakikishia kuwa mtu huyo hana virusi vya Ukimwi, wala kukuhakikishia wewe usalama wako dhidi ya maambukizi ya virusi endapo utakuwa na mahusiano naye ya kimapenzi yasiyo salama.

Kumbuka kwamba mtu anaweza kuwa na virusi vya ukimwi kwa miaka mingi sana bila kuonesha dalili hata moja ya kuwa na maambukizi ya virusi hivyo, achilia mbali dalili za kuwa na Ukimwi. Hebu fikiria katika kipindi hicho, anaweza kuwa ameambukiza wangapi endapo atakuwa na mahusiano ya kimapenzi yasiyo salama, hasa kwa mtu kama huyo kijana unayesema ni mwingi", alijibu.

Njia pekee ya kutambua kama mtu ana virusi vya Ukimwi au la ni kupima. Kwa maneno mengine, njia pekee ya kujihakikishia usalama na kuepukana na maambukizi ya virusi vya ukimwi ni ile ya kutoona soo, kuambizana ukweli juu ya kupima damu. Baada ya kupima, ni kuhakikisha kuwa mnazingatia ushauri mnaopewa, kwani mtu anapopimwa anapewa ushauri nasaha wa namna ya kuishi salama.

Baadhi ya vijana wanasikika wakisema eti wana mpenzi mmoja tu, naye ni mwaminifu, hivyo hawawezi kuambukizana virusi vya Ukimwi. Hakika huko ni kujipotosha na kujitafutia maangamizi kwani uaminifu huo hauthibitiki bali ni wa kufikiria tu. Wangapi wanavunja uaminifu katika ndoa, sembuse wapenzi tu. Kwa vijana ni vyema ni wasione soo wasubiri wawe waaminifu au watumiç kondomu. Vijana husema kuwa wataweza wapi kupima? Eti leo uende ukapime na Mwanjiti, kesho na Sikudhani, kesho kutwa na Mwanjaa. Tahadhari kubwa ni lazima wawe nayo katika kujilinda, kujikinga na kujiepusha na vitendo vya ngono.

Ikumbul«ve kuwa vijana ni Taifa la kesho, ndiyo nguvu kazi na jamii inayotegemewa. Bila vijana, kesho hapatakuwa na Taifa. Rais wa kesho atatokana na vijana, Daktari wa kesho yu miongoni mwao, vile vile mwalimu, mhandisi, kasisi, shelthe, mwanasayansi, karani na wengine wote watatokana na kizazi kipya. Kesho inategemea vijana waliopo leo. Kutokana na hilo, ni lazima ?a?a vijana watambue nafasi yao, wajibu wao na majukumu yao kisha wabadili tabia na mienendo isiyofaa. "Kijana uko shuleni bado unahangaikia nini? Kumbuka, mshika mawili jamani msione soo!

MASWALI

(a) (i) Andika kichwa cha habari uliyosoma, kisichozidi maneno matano (5).

View Ans


(ii) Kwa nini huwezi kumtambua mtu mwenye virusi vya ukimwi kwa kumwangalia tu?

View Ans


(iii)Eleza maana ya maneno yaliyopigiwa mstari kama yalivyotumika kwenye habari uliyoisoma.

  • Mwingi . . . . . .
  • Anadunda . . . . . 
View Ans


(iv)Faida za kupima virusi vya ukimwi ni

View Ans


(v) Unafikiri kuwa na mpenzi mmoja ni kinga tosha ya maambukizi ya ukimwi? Kwa nini?

View Ans


(vi) Ni njia ipi kuu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi?

View Ans


(vii) Njia bora zaidi kwa vijana ya kujikinga na UKIMWI ni

View Ans


(viii) Unafikiri ni kwanini mwandishi amependekeza njia hiyo? 

View Ans


(ix) Ni athari zipi zitakazolikumba Taifa endapo vijana wengi wataathirika na Ukimwi?

View Ans


(x) Nini maana ya msemo "usione soo"?

View Ans


(b) Andika ufupisho wa habari hii usiozidi maneno themanini (80),

View Ans


2. (a) Soma swali lifuatalo kisha andika herufi ya jibus 'hi.

Kati ya kauli zifuatazo, ipi ni fasili ya lugha?

  1. Lugha ni maneno
  2. Lugha ni sauti zinazotumika katika mawasiliano ya watu
  3. Lugha ni mfumo wa mawasiliano uliokubalika na kutumiwa katika jamii.
  4. Lugha ni mfumo wa sauti za binadamu za nasibu zenye mpangilio maalumu wenye kuleta maana zilizokubalika na jamii kwa ajili ya mawasiliano.
Choose Answer :


(b) Taja mazingira ambayo sentensi zifuatazo zinaweza kutumika:

(i) Nimemuanzishia dozi ya dripu. .

(ii) Utusamehe sisi wakosefu ee Mungu!

(iii) Zuia babu! Vichwa vitatu hivyo vinakuja. ..

(iv) Chapa barua mbili niletee nizisaini ili ziondoke hapa.

(v) Napenda kujibu swali Ia nyongeza Ia mheshimiwa kama ifuatavyo. ............

View Ans


(c) Andika sentensi zifuatazo kwa usahihi:

(i) Mwenyekiti aliwakilisha taarifa ya mapato na matumizi katika kikao.

(ii) Naibeba nafasi hii kumkaribisha mgeni rasmi.

(iii) Yule kijana huwaga hapendagi fujo.

(iii) Sisi wote tutaondoka kesho jioni. 

(iv) Chai imengia sisimizi.

View Ans


SEHEMU C

SARUFI

3. (a) Sarufi ni . . . . . . .

View Ans


(b) Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo 

(i) Wanafunzi wale wamechelewa darasani.

(ii) Uvuvi una madhara yake.

(iii) Ambao ni washiriki watapewa zawadi.

(iv) Nilimwandikia barua lal<ini hakuipata.

(v) Mchezo wa mpira wa kikapu unapendwa na vijana

View Ans


(c) Nyambua maneno yafuatayo katika hali ya kutendeka, kutendwa na kutendeana,


Kutendeka

Rutendwa

Kutendeana

(i) Lima



(ii) Oga


(iii) Fua



View Ans


(d) Bainisha dhima za mofimu zilizopigiwa mstari katika maneno yafuatayo:

(i) Si kukuona . . . . . . . .

(ii) Walioadhibiwa . . . . . . . . 

View Ans


4. Soma simu ifuatayo kwa makini, kisha jibu swali linalofuata.

AMANi JALÍA SLP 74 IRINGA BABA NI MGONJWA AMÉLAZWA HOSPÍTALV MKOA NJOO HARARA SANA WARIDI

Swali: Kutokana na simu hiyo hapo juu, jifanye unasoma Shule ya Sekondari Mwalize, S.L.P 280, Iringa. Andika barua kwa Mkuu wa Shule umuombe ruhusa ya siku saba kwenda kumwona mgonjwa huyo.

Choose Answer :


5. (a) Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kuchagua jibu sahihi kutoka kwenye orodha uliyopewa.

(i) Chimbuko la fasihi simulizi ni ............

(ii) Fasihi simulizi ni sanaa inayowasilishwa kwa njia ya ..

(iii) Ili kuikamilisha katika kuwasilisha ni lazima pawepo na

ORODHA

  • Mazungumzo na masimulizi ya watu
  • Usanii katika fikra za binadamu
  • Mifumo ya maisha ya jamii katika siasa, uchumi na utamaduni Mchoro
  • Ufumaji
  • Kuandika
  • Kuzungumza/kusimulia kwa mdomo
  • Hadhira
  • Wachezaji
  • Fanani na hadhira
View Ans


(b) (i) Taja vipengele vitano (5) vya fani ya fasihi simulizi.

(ii) Masimulizi ya hadithi yanawasaidia watoto na vijana? Taja faida Sita (6) za hadithi kwa watoto na vijana.

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256