FORM TWO EDK NECTA 2024

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI

015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU

Muda: saa 2:30   Mwaka: 2024

Maelekezo 

  1. Hati hii ina sehemu A B na C zenye jumla ya maswali kumi 10.
  2. Jibu maswali yote.
  3. Sehemu A ina alama 15 sehemu B ina alama 70 na sehemu C ina alama 15.
  4. Maandishi yote lazima yawe kwa wino mweusi au bluu na michoro lazima iwe kwa penseli.
  5. Simu za mkononi na vitu visivyoruhusiwa havitaruhusiwa ndani ya chumba cha mtihani
 FOR EXAMINER’S USE ONLY
 QUESTION NUMBER  SCORE  EXAMINER’S INITIIALS
1

2

3

4

5

6

7

8

9

10

 TOTAL

 CHECKER’S INITIALS

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Katika kipengele (i) - (x) chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake katika kisanduku.

(i) Kwa kuzingatia mtazamo wa Uislamu juu ya dhana ya elimu ni kipengele gani kina bainisha mgawanyo sahihi wa elimu?

  1. Elimu dunia na elimu akhera
  2. Elimu ya mwongozo na elimu ya Qur'an
  3. Elimu ya mazingira na elimu ya shule
  4. Elimu ya mwongozo na elimu ya mazingira
Choose Answer :


(ii) Bainisha hoja inayoeleza kazi kuu ya Dini katika maisha kwa mujibu wa Uislamu.

  1. Kuweka njia ya mahusiano baina ya watu
  2. Kuwanusuru watu katika namna zote za uonevu
  3. Kufafanua asili ya wanadamu na malengo yao
  4. Kukamilisha hitajio la mtu kiroho na kiitikadi
Choose Answer :


(iii) Ukipewa nafasi ya kwenda kuhiji Makka kwa kigezo cha kuzingatia aina ya Hijja iliyo nafuu kwa mtu anayetoka mbali utachagua aina gani?

  1. Tamattu
  2. Qiraan
  3. Umrah
  4. Ifraad
Choose Answer :


(iv) Ni kafara gani anayetekeleza mtu aliyevunja kiapo halali kwa mujibu wa Uislamu?

  1. Kufunga miezi mitatu bila kuacha
  2. Kufunga siku saba mfululizo
  3. Kufunga siku tatu mfululizo
  4. Kufunga miezi miwili
Choose Answer :


(v) Mzee Faki ni baba mwenye mke mmoja ambaye ni mjamzito na wana watoto wanne mmoja kati yao ni wa kulea ambaye si Muislamu. Ni kiasi gani cha nafaka anapaswa kutoa kwa ajili ya Zakatul-Fitr?

  1. Kg. 10
  2. Kg. 12.5
  3. Kg. 15
  4. Kg. 17.5
Choose Answer :


(vi) Katika mchakato wa kuhifadhiwa Qur'an hapo mwanzo Mtume (S.A.W) aliwaamrisha maswahaba wake kukusanya na kuiandika Qur'an mafungu mangapi?

  1. Saba
  2. Mawili
  3. Matatu
  4. Thelathini
Choose Answer :


(vii) Hoja gani inabainisha umuhimu wa kushuka Qur'an kidogo kidogo kwa muda wa miaka 23?

  1. Kutoa nafasi ya maandalizi ya kuihifadhi kimaandishi
  2. Kurahisisha mchakato wa usomaji na uandishi wake
  3. Kutoa nafasi kwa Masahaba kufanya shughuli zingine
  4. Kutoa nafasi kwa waumini kuihifadhi na kuitekeleza
Choose Answer :


(viii) Hadithi kamilifu inahakikiwa katika vipengele gani muhimu?

  1. Isnad Rawi na Mutawatir
  2. Isnad Matin na Rawi
  3. Isnad Matin na Mutawatir
  4. Isnad Mutawatir na Riwaya
Choose Answer :


(ix) Bainisha hoja iliyoibua na kuonesha umuhimu wa sayansi ya Hadithi.

  1. Kutambua vigezo vya uchujaji wa Hadithi
  2. Kutambua historia ya waandishi wa Hadithi
  3. Kutambua Hadithi sahihi na zisizo sahihi
  4. Kutambua historia ya wapokezi wa Hadithi
Choose Answer :


(x) Kwa nini katika karne ya 6 A.D ulimwengu unatajwa kuwa katika kipindi cha Jahiliyyah?

  1. Hapakuwa na mafundisho yoyote ya dini
  2. Maisha yalikuwa katika zama za mawe
  3. Watu hawakuwa na maarifa
  4. Maovu ya aina mbalimbali yalienea
Choose Answer :


2. Oanisha maelezo ya makundi ya wanaostahiki kupewa Zaka katika Orodha A na majina ya makundi hayo katika Orodha B kisha Andika herufi ya jibu sahihi katika sehemu ya kuandiikia majibu uliyopewa.

Orodha A

Orodha B

  1. Wasioweza kumudu mahitaji yao ya kila siku mpaka wasaidiwe 
  2. Walioharibikiwa njiani kwa kuibiwa au kuishiwa matumizi yao muhimu
  3. Wanaofanya shughuli za kuhuisha
  4. Dini ya Uislamu
  5. Walotezwa nguvu au kumilikiwa Waliopungukiwa na Mahitaji yao ya kila siku.
  1. ibnu Sabiil
  2. Fi sabilillah
  3. Watumwa.
  4. Fukara
  5. Masikini
  6. waliosilimu
  7. Al aamilina Alayha.
View Ans


SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. bainisha njia tano, zinazomwezesha mwanadamu kutambua uwepo wa Mola wake katika maisha.

View Ans


4. ‘’Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu’’ Qur’an (51: 56). Kwa mujibu wa aya hiyo; 

  1. Fafanua dhana ya ibada kisheria
  2. Bainisha mahusiano yaliyopo kati ya ibada maalumu na maisha ya Muislamu ya kila siku.
  3. Bainisha sababu ya kuwepo kwa maumbile yote yaliyomzunguka mwanadamu.
View Ans


5. (a) Bainisha mambo sita muhimu anayopaswa kufanyiwa mtu anayekaribia kufariki,

View Ans


(b) Bainisha mambo manne ya faradhi anayostahiki kufanyiwa maiti wa Kiislamu.

View Ans


6. Panga historia ya kushuka Qur'an kwa Mtume (S.A.W) katika mtiririko sahihi kwa kuandika namba 1-5 katika sehemu ya kuandikia majibu uliyopewa.

  1. Kutoka humo ikamfikia Mtume (S.A.W) kwa hatua kupitia Malaika Jibril (A.S) kwa miaka 23.
  2. Mwanzo wa kushuka kwake Mtume (S.A.W) alipokea Aya tano za Surah Alaq.
  3. Kabla ya Qur'an Mtume (S.A.W) alikuwa akipata wahyi kwa ndoto.
  4. Qur'an ilishushwa kutoka Lawh al Mahfudh mpaka mbingu ya kwanza.
  5. Qur'an yote kwa jumla ilihifadhiwa katika ubao mtukufu kwa Allah (S.W) katika Arshi yake.
View Ans


7. Bainisha vigezo vitano vinavyotumika kutambua Hadithi isiyo sahihi kwa kuzingatia matini.

View Ans


8. Utambuzi binafsi na mwelekeo wa mwanadamu unategemea tafsiri aliyonayo juu ya mambo matatu ya akihistoria. Fafanua mambo hayo kwa mujibu wa Uislamu.

  1. Asili ya mwanadamu.
  2. Lengo la mwanadamu
  3. Hadhi na wajibu wa mwanadamu
View Ans


9. Taja vipengele vitano vinavyoonesha kuandaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) ki-ilhamu.

View Ans


SEHEMU C (Alama 15)

Jibu swali la kumi (10)

10. Eleza mambo Matano yanayobatilisha ibada ya funga.

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256