KISWAHILI FORM TWO REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA PRESIDENT’S OFFICE, REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT

KALIUA DISTRICT COUNCIL

FORM TWO PRE – MOCK DISTRICT JOINT EXAMINATION - MAY 2024

021 KISWAHILI

Muda: Saa 2:30

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B, na C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa.
  3. Sehemu A na C zina alama kumi na tano (15) kila moja, na sehemu B ina alama sabini(70).
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
  5.  Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  6.  Vifaa vyote vya mawasiliano visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  7. Andika Namba yako ya Upimaji wa Kiutimilifu katika kila ukurasa sehemu ya juu upandewa kulia

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Katika vipengele (i) hadi (x), chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika kisanduku cha kujibia.

(i) Sauti za lugha ambazo hutamkwa bila kuwepo kwa kizuizi chochote kwenye mkondo wa hewa ujulikana kama:

  1. Sauti
  2. Herufi
  3. Irabu
  4. konsonanti

(ii) Lipi si jibu sahihi kati ya yafuatayo kuhusu ufahamu wa kusoma kwa sauti?

  1. Kutamka maneno inavyotakiwa
  2. Kuzingatia alama za uandishi
  3.  Kusoma bila kutoa sauti
  4.  Kuzingatia nguvu ya utamkaji wa neno

(iii) Chunguza taarifa ifuatayo, kisha jibu swali linalofuata.

Shule ya Sekondari Migungani,

S.L.P 104507, Mto wa Mbu.

20/04/2024.

Taarifa hiyo ina vipengele vingapi?

  1.  Kimoja: anwani ya mwandishi.
  2. Viwili: anwani ya mwandishi na tarehe.
  3. Viwili: anwani ya mwandishi na alama za uandishi.
  4. Vitatu: anwani ya mwandishi, mji aliopo mwandishi na tarehe.

(iv) Mawazo makuu ya mtunzi wa kazi ya fasihi simulizi humfikia mlengwa kwa njia ipi kati ya hizi?

  1. Fani
  2.  Falsafa
  3.  Migogoro
  4. Dhamira

(v) Neno lipi kati ya haya ni mofu huru?

  1.  Uji
  2.  Uzuri
  3.  Uchache
  4.  Ufa

(vi) Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo haina maana zaidi ya moja?

  1. Mjomba amefua nguo
  2.  Nipe sahani ya kulia
  3. Maeda amenunua mbuzi
  4. Mwalimu amenunua kanga

(vii) “Mtangazaji wa televisheni huhakikisha watazamaji wanapata habari sahihi kwa wakati.” Katika fasihi, kazi hiyo hufanywa na nani kati ya hawa wafuatao?

  1. Wasikilizaji
  2.  Hadhira
  3.  Fanani
  4.  Wasomaji

(viii) Aina ya neno inayofafanua zaidi kuhusu nomino au viwakilishi huitwaje?

  1.  Kielezi
  2. Kivumishi
  3. Kihusishi
  4. Kibainishi

(ix) Aina ya kamusi ambayo huandikwa kwa kutumia lugha zaidi ya mbili huitwaje?

  1. Kamusi wahidiya
  2. Kamusi thaniya
  3. Kamusi mahuluti
  4. Kamusi mchanganyiko

(x) Kauli mbalimbali za kitenzi ni dhima ya:

  1. Mofu
  2. Mofimu
  3. Mofu tegemezi
  4. Mzizi


2. Oanisha maelezo yaliyopo katika Orodha A na dhana za kikamusi zilizopo katika Orodha B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika jedwali lililopo hapo chini.

Orodha A Orodha B
  1. Neno lililoorodheshwa katika kamusi kwa chapa iliyokozwa au kwa kuwekwa rangi kwa lengo la kutofautishwa na maneno mengine ili lifafanuliwe.
  2. Kidahizo pamoja na maelezo yake
  3. Asili ya neno
  4. Kamusi ya lugha mbili
  5. Jinsi au namna neno linavyoandikwa
  1. Etimolojia
  2. Kidahizo
  3. Tahajia
  4. Mahuluti
  5. Thaniya
  6.  Wahidiya
  7. Kitomeo
  8. Alfabeti

SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

Kwa neno zima uzalendo ni mapenzi ya nchi. Mapenzi haya hayafanyiki kwa njia za kubuniwa na watu lakini yamekwisha tangulia katika mioyo yetu. Uzalendo ni tabia ya maumbile, nasi tunayo toka wakati wa kuzaliwa. Tunafikiri habari za nchi yetu kama tufikiriavyo habari za baba na mama zetu; kwa hivi kila mtu anajali sana mahali alipozaliwa. Baadhi ya watu hawakubali nao wako tayari siku zote kupinga pishi ya hoja zako kwa ukufi wa hoja zao. Wao hufikiri kwamba uzalendo ni maono ya ushupavu na dalili ya uchache wa ustaarabu wa moyo. Kwao uzalendo ni imani ya kishenzi, kwa sababu hutenga kando nchi nyingine.

Wanadai kwamba mtu ni lazima apende ulimwengu mzima na watu wa ulimwengu hufanya kila mtu kuwa raia wa dunia si wa mahali pake padogo pajulikanapo kama nchi yake. Lazima niseme kweli kwamba wazo la udugu wa ulimwengu ni bora kwa makisio lakini kwa matumizi haliwezekani. Bora katika watu ni yule apendaye nchi yake kwanza. Kuna mashaka makubwa kama mtu anaweza kuamini katika mapenzi ya undugu wa ulimwengu bila kupenda nchi yake; ikiwa hivyo, uzalendo huthibitisha ubora wa kupenda sehemu ya ulimwengu ambayo ndani yake tumezaliwa.

Mapenzi ya mtu kwa nchi yake hayaoneshi chuki kwa nchi nyingine za ulimwengu. Uzalendo wa uwongo ndio utufanyao kuchukia nchi nyingine. Aidha, lazima tupende nchi zetu kwa sababu ya nchi zenyewe. Pasiwe na kusudi baya au la choyo nyuma yake. Kuna uzalendo wa uwongo vilevile ambao ni hila tufanyayo kwa makusudi yetu wenyewe ya choyo kwa sababu ya nia mbaya za kujitajirisha. Uzalendo wa kweli hutokana na mapenzi yasiyo na choyo ya nchi zetu na heshima yetu ya historia na malezi. Uzalendo usitufanye kujiona kwamba sisi ni watu azizi ulimwenguni na makabila yote si kitu.

Mpenzi ya nchi yetu huonekana kama maono bora lakini hayana maana kama hayachukuani na matendo. Uzalendo wa matendo tu ndio wenye thamani nchini iwapo katika hatari ya shambulio la adui. Mapenzi ya mtu kwa nchi yasiyo na matendo yanaweza kuwa mema katika nyakati za amani, lakini nyakati za vita uzalendo huthibitisha unyofu wake katika kitali. Uzalendo hutaka sadaka za maisha, jamaa, mali, na kila kitu cha mtu. Watu wanaotoa sadaka za maisha yao kwa sababu ya nchi zao ni mashahidi.

Maswali

  1. Mwandishi ana msimamo gani kuhusu uzalendo?
  2. Mwandishi anatoa angalizo gani kuhusu uzalendo?
  3. “Kupinga pishi ya hoja zako kwa ukufi wa hoja zao.” Usemi huu una maana gani kulingana na habari uliyosoma?
  4.  Andikwa kichwa cha habari kinachofaa kwa kifungu cha habari ulichosoma.

4. Andika sentensi zenye vipashio vifuatavyo:

(a) N + Ts + T + N + E

(b) N + V + T + E

(c) W + t + N + V

(d) Ts + T

(e) W + V + Ts + T + H + N

5. Kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya kujifunza lugha ya Kiswahili kwa sababu baadhi ya watu hawaoni umuhimu wake. Kwa hoja tano (5) wafafanulie umuhimu wa kujifunza lugha hii.

6. Ni taarifa gani za muhimu zinazoingizwa kwenye kamusi anazozihitaji mtumiaji wa kamusi?(taja tano)

7. a). Sentensi zifuatazo zinamakosa uziandike kwa usahihi.

  1. Wanafunzi watoro wataazibiwa
  2. Kuku zangu zinakunywa maji
  3. Mbuzi wangu ni mjamzito
  4. Nilimkuta hayupo
  5. Gari yangu imeharibika

b). Eleza dhima za viambishi vilivyokolezwa wino.

  1. anasoma
  2. Wamempikia
  3. Atakusubiri
  4. Atakulilia
  5. Unakula

8. Methali ni kipera cha semi chenye kubeba hekima na busara. Matumizi mabaya ya methali huweza kusababisha upotoshaji kwa jamii. Thibitisha kauli hii kupitia methali zifuatazo.

(a) Haraka haraka haina baraka.

(b) Tamaa mbele mauti nyuma.

(c) Mficha uchi hazai.

(d) Si kila king’aacho ni dhahabu.

(e) Ajali haina kinga

9.Kazi za fasihi simulizi huweza huhifadhiwa kwa njia mbalimbali ili zisipotee. Fafanua faida tano (5) za kuhifadhi fasihi kwa njia ya vinasa sauti.

SEHEMU C (Alama 15)

Jibu swali la kumi (10).

10. Chukulia kuwa wewe ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Maendeleo, iliyoko wilayani Tandahimba. Andika barua kwa mkuu wa shule yako ukiomba ruhusa ya kuhudhuria semina ya Uelimishaji Rika itakayofanyika katika shule ya Sekondari Songambele iliyoko Songea-Ruvuma kuanzia tarehe 15/07/2023 hadi tarehe 22/07/2023. Barua yako ipitie kwa mwalimu wa darasa lako. Anwani ya shule yako ni S.L.P 10023, Tandahimba na jina lako liwe Bahati Msomi.

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 105  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 105  

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (OR TAMISEMI)

HALMASHAURI YA WILAYA YA RUFIJI

MTIHANI WA KUPIMA UJUZI NA MAARIFA KIDATO CHA PILI – 2024

021 KISWAHILI

MUDA: SAA 2:30 Alhamisi121, Machi, 2024 Mchana

MAELEKEZO

  1.  Mtihani huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali 10.
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A, B, na C.
  3. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali
  4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  5. Andika Namba yako ya mtihani kwa usahihi katika kila ukurasa.

SEHEMU A (ALAMA 15 )

JIBU MASWALI YOTE KATIKA SEHEMU HII

1. Katika kipengele (i) hadi (x), chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika kisanduku ulichopewa

i. Mzizi wa neno “ watakapokunywa” ni

  1. Kuny
  2. ku 
  3.  nyw
  4.  ny 
  5. wata.

ii. Mwalimu aliwaagiza wanafunzi wawili wajibizane kishairi mbele ya wenzao darasani ni kipera kipi kinawakilisha walicho fanya wanafunzi hao?

  1. Ngonjera 
  2.  majigambo 
  3. kichekesho
  4.   igizo 
  5. tenzi.

iii. Sauti ya lugha inayotamkwa bila kuwapo na kizuizi chochote kwenye mkondo wa hewa huitwaje?

  1. Silabi 
  2.  irabu 
  3.  konsonanti
  4.  mkazo
  5.  kiimbo.

iv. Rais Ally Hassani Mwinyi alikuwa mtiifu neno lililopigiwa mstari katika sentensi hii ni aina gani ya neno

  1. Kivumishi 
  2.  kitenzi kikuu 
  3.  kitenzi kishirikishi 
  4. kitenzi kisaidizi
  5. kieuzi cha namna au jinsi.

v. Unyambulishaji katika lugha ya Kiswahili huhusisha upachikaji wa viambishi:

  1.  Kabla ya mzizi 
  2. Baada ya mzizi 
  3. kabla na baada ya mzizi
  4.  katikati ya mzizi 
  5. kabla, kati kati, na baada ya mzizi

vi. Utata hutokea pale maneno au sentensi zinapokuwa na maana zaidi ya moja je, utata huo huwa wa aina gani?

  1. Kisarufi na kimantiki 
  2. kisarufi na kiliksika 
  3. kimtindo na kimatamshi 
  4. kimsamiati na kimuundo 
  5. kimantiki na kileksika.

vii. Pita huku nami nipite huku tukutane kwa mjomba” fumbua kitendawili hiki

  1.  Barabara 
  2. mkanda 
  3. ukili 
  4. mnyororo
  5.  kamba.

viii. Neno lipi kati ya haya yafuatayo halitokani na utohoaji

  1. Posta
  2.  kompyuta 
  3. polisi 
  4. boksi 
  5. achali.

ix. Mtangazaji wa televisheni huhakikisha watazamaji wanapata habari sahihi kwa wakati” katika fasihi , kazi hiyo hufanywa na nani kati ya hawa wafuatao

  1. Wasikilizaji 
  2. hadhira 
  3. canani
  4. wasomaji
  5.  wazungumzaji.

x. Moja wapo ya alama ya uandishi ni nukta, kazi ya alama hiyo ni ipi katika sentensi

  1. Kukariri au kurudia maneno yaliyosemwa
  2. Kuonesha sentensi imefika mwisho na imekamilika
  3. Kubadilisha sehemu mbili za sentensi zilizo kinyume
  4. Kuashiria maneno yaliyo kwenye orodha
  5. Hutumika kuonesha kituo kidogo ndani ya sentensi .

2. Oanisha kifungu cha maneno kutoka Orodha B ambacho kinatoa maelezo sahihi ya neno maneno yaliyopo kwenye orodha A kisha andika herufi ya jibu sahihi

ORODHA A ORODHA B
  1. Utani
  2. Majigambo
  3. Mandhari
  4. Ngano, visasili,tarihi
  5. Michezo ya watoto
  1. Hadithi fupi zinazosimulia asili ya watu ivitu na hata wanyama
  2. Mtambaji wa kazi za fasihi simalizi
  3.  Mafumboyanayohitaji kufumbuliwa
  4.  Vipera vya tanzu za hadithi
  5.  Mbinu anazozitumia msanii ili kufikisha ujumbe kwa hadhira
  6. Kujisifu kunako ambatana na matendo
  7. . Vipera vya tanzu za semi
  8. Maneno ya mzaha pasipo kuchukia
  9. IAina ya sanaa inayotumia lugha inapowasilishwa kwa hadhira
  10.  Mazingira /mahali inapofanyika kazi ya fasihi
  11. Shughuli zinazo fanywa na watoto kwa lengo la kijiburudisha
  12. Watazamaji wa kazi ya fasihi

SEHEMU B (ALAMA 70)

JIBU MASWALI YOTE KATIKA SEHEMU HII

3. Soma kifungu cha habari kifuatacho, kisha jibu maswali

Naomba mia , naomba hela ya kula, shikamoo/ mzazi leo nimelala nihesa mapaa na mitambaa panya. Naomba msaada nisadieee .. . . . . . . . .hayo ndiyo maneno yanayotawala kundi ambalo linaendelea kuwa kubwa la kizazi chao kundi hilo limesahaulika kana kwamba jamii haioni . . . . . . . . . . ni lugha inayosikika na inayoendelea kuenea katika miji mikubwa kwa midogo ina sehemu mbalimbali zenye mkusanyiko wa wate ukitaka kujua nani wanaotoa kilio hicho kila kukicha, basi siku moja ubahatike kukutana na watoto mmoja wapo kati ya kundi la watoto wa mitaani utayaamini hayo yanayosemwa. Hali hii walionayo si kwamba wameitaka iwasibu lahasha imewapata kutokana na mlolongo wa mambo yanayochangia hali hiyo kutokea, kuyaeleza yote mengine nitayatia chumvi lakini umasikini kutamalaki katika familia zetu ni moja wapo, Aidha uzazi usiotarajiwa, na pengine katika umri mdogo, ukosefu wa elimu kuvunjika kwa ndoa na kubwa zaidi gonjwa la ukimwi lilotapakaa nalo limeongezea tatizo hili kuwa kubwa. Kilio cha kundi hilo kingesikilizwa, kIngekuwa na ahueni, lakini wapi, Watoto hao wanaambulia kubakwa na kulawitiwa tiba zenyewe hawapati, na kuhusu elimukwao inakuwa ni njozi na ni vigumu kutekelezwa hatimaye, kundi hilo linapokosa matumaini, basi madawa ya kulevya, pombe, na wizi vinakuwa ndilo kimbilio lao Kila mwananchi wewe na mimi tunapowaona wahusika hao tuna mtupia fulani mpira huo,kwamba ndiye mwenye uwezo na wajibu wa kumiliki tatizo hilo. kasumba hiyo haiwezi  kumaliza janga hilo hatuna budi wote tuliokusanyika kwenye konatuone kama kila mmoja wetu anawajibika kuiondoa hatari hii. Kukaa pembeni na kubaki kuoneshea kidole na kukandia wengine taatifulani ndiye mwenye jukumu la kutunza kundi hilo, sisahihi hivi ndivyo tusemavyo eti, serikali ndiyo yenye jukumu hilo lakini serikali ni pamoja na sisi sote, waswahili husema, mcheka mwana kulia mwishoni utawa wewe”

Maswali

i. Andika kichwa cha habari kisichozidi maneno matatu

ii. Mwandishi anasema ukitaka kuamini yanayosemwa ufanye nini

iii. Taja jambo kubwa moja ambalo limeonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa tatizo analolizungumzia mwandishi

iv. Ni maeneo gani ambayo kundi la watu hao huonekana .

v. Watoto hao wa mitaani walishakata tamaa ya maisha na kukimbilia kwenye nini

vi. Mwandishianamaana gani anaposema, “kukaapembeni na kuoneshea kidole na kukandia wengine”

vii. Eleza maana za maneno yafuatayo jinsi yalivyotumiwa katika habari hii

  • Ahueni
  • Njozi
  • Mpira ..
  • Wajibu .
  • Chumvi

viii. Taja funzo moja unalolipata kutokana na habari hii

ix. Andika ufupisho wa habari hii usiozidi maneno sitini (60).

4. Chunguza sentensi zifuatazo, kisha bainisha vivumishi vilivyo tumika kwa kufafanua ni aina gani ya kivumishi

Mfano: wezi wale wamekamatwa usiku huu

Wale ni kivum ishi cha kuonesha

  1. Kinu chake kimepotea ___________
  2. Mti upi umeangushwa na upepo ____________
  3.  Kitabu cha mwanafunzi kimepatikana ________________
  4.  Nyumba nzuri hujengwa kwa gharama kubwa ___________
  5.  Hiki kidogo kimearibika ___________________

5. Asha alibishana na Amina kuwa mochoro na picha katika Kamusi haina maanani kumaliza karatasi tu wewe kama mwanafunzi mtetee Amina kwa hoja tano (5)

6. (a)Kwa kutumia mifano eleza dhima tano (5) za viambishi

(b)Chunguza jedwali lifuatalo kwa makini kisha jaza sehemu zilizo achwa wazi

Neno  Mzizi  Kauli ya kutendeana  Kauli ya kutendwa
i. Kusema ____________ ______________ ______________
ii. _________ _____________ Kupigana _______________
iii. Kuomba ________________ Kuombana _______________
iv. __________ Andik ______________ Kuandikwa

7. Baisha tofauti tano zilizopo kati ya lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo

  1. Uwasilishaji ________________________________________________________________
  2.  Chanzo na kikomo ___________________________________________________________
  3. Wahusika ___________________________________________________________________
  4. Uhifadhi ____________________________________________________________________
  5. Uhusiano na hadhira __________________________________________________________

8. Mzee fasihi ni mwenyekiti wa mtaa wa mgomba alioa wake wawili mke wa kwanza ni Simulizi na mkwe wa pili ni andishi mke wa kwanza ana watoto wanne na wajukuu kwa kutumia mchoro onesha majina ya watoto hao na uoneshe wajukuu angalau watatu kwa kila mtoto.

9. (a)Tunga sentensi moja kuonesha rejesta inayoweza kutumika katika maneno yafuatayo:-

  1. Sokoni
  2. Mgahawani
  3.  Shuleni
  4.  Kwenye kituo cha afya

(b) Mama yake tina alimuuliza mwanae, mbona umefeli mtihani wa muhula huu ? Tina alimjibu si unajua bi mkubwa Yule ticha ni noma, yaani anapendelea kinoma, nome langu analichuma kutokana na taarifa hiyo toa sifa tano zilizotokana na aina hiyo ya msimu alioutumia tina

SEHEMU C (ALAMA 15)

10. Jifanye wewe ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari chemchem, S.L.P. 45, Rufiji unamatatizo ya kiafya, hivyo unahitaji kwenda kutibiwa hospitali ya mkoa. Andika barua kwa baba yako kuomba fedha ya kwenda hospitali kwa ajili ya matibabu jina lako uwe majaliwa rindamali

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 95  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 95  

Namba ya Mtahiniwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA

UPIMAJI WA PAMOJA KIDATO CHA PILI –AWAMU YA 1

021 KISWAHILI

MUDA: MASAA 2:30 MACHI 2024

MAELEKEZO:

  1.  Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10)
  2. Jibu maswali yote
  3. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa
  4. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu ya wino wa bluu au mweusi
  5. Vifaa vyote vya mawasiliano haviruhusiwi katika chumba cha mtihani


SEHEMU A (ALAMA 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu hilo katika karatasi ya kujibia.

i. Sauti za lugha ambazo hutamkwa bila kuwepo kwa kizuizi chochote kwenye mkondo kwa hujulikana kama: -

  1. sauti 
  2.  Herufi 
  3. Irabu
  4. Konsonanti

ii. Silabi zinazotokea katikati au mwishoni mwa kila mstari wa shairi huitwa .

  1. Vina
  2.  Mizani 
  3. Sitiari 
  4.  Vituo

iii. Kiimbo hufasiliwaje katika mazungumzo?

  1.  Kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti
  2. kuzungumza na kuongea kwa sauti
  3. kuzungumza kwa kupandisha mawimbi ya sauti
  4. kuzungumza kwa kushusha mawimbi ya sauti

iv. Dhana ipi kati ya hizi zifuatazo haina maana Zaidi ya moja?

  1.  Kaka amefua nguo
  2. Nipe sahani ya kulia
  3.  Eva amenunua kanga
  4. ohn amempigia mpira

v. Mkisi ameenda Dodoma. Neno Dodoma limetumika kama

  1. Kihisishi 
  2. Nomino 
  3. Kiwakilishi 
  4. Kielezi

vi. Mawazo makuu ya mtunzi wa kazi ya fasihi humfikia mlengwa kwa njia ipi kati ya hizi zifuatazo.

  1.  Fani
  2.  Falsafa
  3.  Migogoro 
  4. Dhamira

vii. Ipi ni tofauti ya msingi kati ya mashairi na ngonjera?

  1. . Mpangilio wa vina na mizani
  2. Idadi ya mizani na mishororo
  3. Majibizano baina ya watu wawili au Zaidi
  4. Mpangilio wa silabi na lugha ya mkato.

viii. ‘Bosi samahani kuna barua yako hapa’ Mtindo huu wa mazungumzo unatumika wapi?

  1. Ofisini
  2.  Kiwandani 
  3. Shambani 
  4. Kanisani

ix. Sababu zifuatazo husababisha kutokea kwa utata katika tungo isipokuwa

  1.  Neno kuwa na maana Zaidi ya moja
  2. Kuzingatia taratibu za uandishi
  3. Kutumia maneno yenye maana ya picha
  4.   Kutotamka neno ulilokusudia kwa usahihi

x. Seti ipi ni sahihi kuhusu vipengele vya fani katika fasihi simulizi?

  1. Dhamira, migogoro, mtindo na mafunzo
  2. Ujumbe, matumizi ya lugha, wahusika, mtindo na muundo
  3. Wahusika, matumizi ya lugha, muundo, mtindo na mandhari
  4. Migogoro, Ujumbe, wahusika, mafunzo na mtindo.

2. Oanisha dhima za nyimbo za fasihi simulizi zilizo katika orodha A na aina za nyimbo kutoka orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kisanduku ulichopewa.

Orodha A  Orodha B
  1. Husimuliwa kama mifano ya kuadiri watu
  2. Husimulia chimbuko la asili ya kitu Fulani
  3.  Husimulia kwa nia ya kuchekesha na kukejeli
  4. Husimulia kwa lengo la kuwaasa watoto
  5. Husimuliwa kuhusu matukio ya kihistoria
  1.  Soga
  2.  Tarihi
  3.  Vigano
  4.  Visasili
  5.  Hadithi
  6. Mizungu
  7. ngano

SEHEMU B (ALAMA 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.

Mazingira yaliyotunzwa huleta raha kwa viumbe na mazingira yaliyoharibiwa ni Karaha kubwa si tu kwa binadamu bali hata kwa viumbe vingine vyote. Aidha utunzaji wa mazingira ni wajibu wa kila mtu na kila raia wa Tanzania na ulimwenguni kote kwa ujumla. Hata hivyo wapo wananchi wanaokiuka wajibu huo muhimu na kusababisha uharibifu mkubwa sana.

Katika nchi zilizoendelea uharibifu wa mazingira husababishwa na shughuli za viwanda ambapo mitambo mbalimbali iungurumapo hutoa moshi kwa wingi ambao huenea angani na kusababisha madhara makubwa kwa mimea na wanyama.

Hali hii ni tofauti kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Katika nchi kama hizo mazingira yanaharibika kutokana na shughuli za kibinadamu kama vile kilimo, ujenzi, pamoja na uchimbaji wa mchanga na kokoto.

Kilimo kinachohusishwa na uharibifu wa mazingira ni kile kinachojumuisha ukataji wa miti bila huruma, uchomaji moto misitu na kulima kwenye miteremko mikali.

Hali hiyo husababisha mmomonyoko wa udongo kwani upepo mkali na maji vinafanya kazi bila kizuizi chochote. Ili kunusuru hali hii yafaa kupanda miti kwa bidii, kusimamia sheria zilizowekwa za utunzaji wa mazingira na kuelimisha raia wote juu ya utunzaji wa mazingira.

MASWALI

(a) Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma kisichozidi maneno matano.

(b) Kwa mujibu wa habari uliyoisoma eleza kwa kifupi ni kwa vipi kulima kwenye miteremko huweza kusababisha mmomonyoko wa udongo

(c) Taja shughuli mbili za kibinadamu zinazoweza kuharibu mazingira

(d) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu cha habari ulichosom

  1. Karaha
  2.  Kiukai
  3.  Nusuru
  4.  Bidii
  5. Iungurumapo

(e) Andika funzo ulilopata kutokana na habari hii

4. Ni taarifa gani zinazohusu neno ambazo huingizwa katika kamusi? (Taja tano)

5. Sentensi zifuatazo ni tata. Toa maana mbili kwa kila sentensi ili kudhibitisha utata huo

  1.  Masudi ameiba kanga
  2. Kaka amenunua tai
  3.  Daktari aliniunga mkono
  4.  Tausi amemwandikia mama yake barua
  5. Juma alimpigia mwanangu mpira

6. (a) Bainisha maana ya kihusishi

(b) Bainisha thamani ya maneno yaliyopigiwa mstari

  1. Nimemuona paka chini ya meza
  2. Nimemuona paka chini ya meza
  3. Nimemuona paka chini ya meza
  4. Nimemuona paka shume chini ya meza
  5. Nimemuona paka shume mnene sana chini ya meza

(c) Taja mambo makuu manne ambayo mzungumzaji huzingatia katika kuteua maneno na miundo ya tungo zake.

7. (a) Sentensi zifuatazo zina makosa, sahihisha

  1. Wanafunzi watoro wataazibiwa
  2.  Ng’ombe zangu zinakunywa maji
  3. Mbuzi wangu mjamzito
  4.  Nilimkuta hayupo
  5. Gari yangu imeharibika

(b) Eleza dhima za viambishi vilivyopigwa msitari

  1.  Anasoma
  2. Wamempikia
  3. Atakusubiri
  4. Atakulilia
  5.  Unakula

8. (a) Taja madhara Matano (5) ya kuhifadhi kazi za fasihi simulizi kwa njia ya Maandishi

(b) Taja aina tano (5) za wahusika wa fasihi simulizi

9. Taja methali moja ambayo ungeweza kuitumia au kubadilisha kulingana na tukio lililoelezwa hapo chini

(a) Ndege alijenga kiota kwa kuchukua jani mojamoja na hatimaye baada ya siku tatu kiota kilikamilika.

(b) Wastara alikuwa masikini akajibidisha sana kufanya kazi usiku na mchana hatimaye akafanikiwa kupata utajiri na kuishi maisha yenye hadhi.

(c) Simba alivamia zizi la mzee Mahende na kukamata ng’ombe mmoja, alipotoka na mkuki kumkabilialishindwa akarudi nyuma kwa hofu, kisha kapiga yowe wanakijiji walikusanyika wakiwa na mikuki namapanga na marungu wakampiga na kumuua simba huyo.

(d) Dereva aliendesha gari kwa kasi na kusababisha ajali mbaya

(e) Baba alipofiwa na mtoto wake alilia sana hadi akazimia

SEHEMU C (ALAMA 15)

10. Andika insha isiyopungua maneno 150 na isiyozidi maneno 200 kuhusiana na athari za ugonjwa wa UKIMWI.

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 87  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 87  

Namba ya Mtihani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

OFISI YA RAIS TAWALA - TAMISEMI TAHOSSA ROMBO DISTRICT EXAMINATION SYNDICATE

MTIHANI WA UPIMAJI WA UTAMIRIFU KIDATO CHA PILI

021 KISWAHILI

MUDA : SAA 2:30 Agusti, 2024

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii in sehemu A, B and C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A, B na C.
  3. Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B ina alama sabini (70) na sehemu C ina alama kumi na tano (15).
  4. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa.
  5. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  6. Vifaa vyote vya mawasiliano visivyoruhusiwa havitakiwi kwenye chumba cha upimaji.
  7. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.
KWA MATUMIZI YA MTIHANI TU
NAMBA YA SWALI  ALAMA  SAINI YA MTAHINIWA
1. 

2. 

3. 

4. 

5. 

6. 

7. 

8. 

9. 

10. 

JUMLA

SAINI YA MHAKIKI

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika kipengele cha (i-x), kisha jaza kwenye kisanduku.

i Katika neno “tumekopeshwa” silabi ya mwisho ina muundo gani wa silabi?

  1.  Irabu peke yake
  2. Konsonati, konsonati, kiyeyusho irabu
  3. Konsonati, konsonati, konsonati irabu
  4. Konsonati na irabu

ii Vitabu vipo darasani japokuwa havijapangwa.Je wewe kama mtaalamu wa sarufi maumbo neno lililopigiwa mstari linaingia katika ku ndi gani la maneno?

  1. Kivumishi
  2. Kihusishi
  3. Kielezi
  4. Kitenzi

iii Unyumbulishaji katika lugha ya Kiswahili huusisha upachikaji wa viambishi…..

  1. Kabla ya mzizi wa neno
  2. Katikati ya mzizi wa neno
  3. Baada ya mzizi wa neno
  4. Kabla na baada ya vitenzi

iv Ng’ombe zangu wanatoa maziwa mengi, kosa lililojitokeza katika tungo hii ni ipi kati ya haya?

  1. Unyumbuaji maneno
  2. Uambishaji wa maneno
  3. Upatanisho wa kisarufi
  4. Upunguzaji wa kitamkwa

v Katika lugha ya Kiswahili kuna maumbo tofauti tofauti ambayo huwakilisha mofimu moja. Maumbo hayo huitwa ………..

  1. Mofu
  2. Alomofu
  3. Mofimu
  4. Alofoni

vi Ili mpokeaji wa barua aweze kuishughulikia barua kwa haraka ni jambo lipi hulizingatia?

  1. Anwani ya mwandishi
  2. Tarehe
  3. Kichwa cha barua
  4. Jina la mwandishi

vii Mwalimu wa somo la Kiswahili aliwaambia wanafunzi watano watunge sentensi yenye kitenzi kishiriikishi ndani yake.Je ni sentensi ipi ya mwanafunzi ambayo haikuwa na kitenzi hicho.

  1. Mama ana nyumba nzuri
  2. Yeye ndiye mwizi
  3. Huyu alikuwa shimoni.
  4. Amekuja ingawa ameondoka

viii Mambo yanayojenga umbo la ndani la kazi ya fasihi ni ………

  1. Falsafa, mtazamo, wahusika, matumizi ya lugha na ujumbe.
  2. Dhamira, ujumbe,mtazamo, migogoro na falsafa
  3. Dhamira , ujumbe, wahusika, migogoro na mtazamo
  4. Mandhari,wahusika, matumizi ya lugha, jina la kazi husika ya fasihi na dhamira

ix Vipengele vifuatavyo hutumiwa katika uandishi wa barua rasmi isipokuwa …

A Anuani ya mwandishi na mwandikiwa
B Lengo
C Kichwa cha barua/ mada
D Saini na jina la mwandishi

x Watoto wa viumbe mbalimbali hitwa vizawa au vikembe, Mfano mtoto wa Ng’ombe huitwa Ndama, Je, mtoto wa Simba huitwaje?

  1. Kinyemere
  2. Nirigi / Nirihi
  3. Kibuli / Kimeme
  4. Shibli

2. Oanisha sentensi zifuatazo katika orodha A na mfuatano sahihi wa vipashio katika Orodha B kisha andika herufi husika katika karatasi ya majibu.

ORODHA A  ORODHA B
  1. Wale wapole ni wanafunzi
  2. Mtoto yule anatembea vibaya
  3. Ebooo! Walikuwa wanataka kucheza
  4. Liandeli si mtoto wake
  5. Seypalm na Leonidas wameondoka.
  1. H + Ts + Ts + T
  2. W + V + t + N
  3. N + U + N + T
  4. N + E + T + N
  5. N + t + N + V
  6. N + Ts + T + E
  7. N + V + T + E

MAJIBU

ORODHA A i ii iii iv v
ORODHA B




SEHEMU (ALAMA 70)

Jibu maswali yote

3 (a) Onesha viambishi awali, mzizi na viambishi tamati katika maneno yafuatayo:-

NENO
VIAMBISHI AWALI
KIINI
VIAMBISHI TAMATI
i. Amenyweshwa



ii. Wamekula



iii. Amekuja



iv. Salishana



v. Wamesomeana



(b) Onesha maana ya mofimu zilizopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo:-

I. Ndege itapaa juu sana …………………………………………………………

II. Jana tulimsafirisha mwanafunzi ………………………………………………

III. Machungwa hayajaiva …………………………………………………………

IV. Wanarukaruka kwa furaha ……………………………………………………

V. Juma atalilia nini? ………………………………………………………………

4 (a) Maneno katika lugha yana dhima mbalimbali, bainisha aina ya vivumishi katika tungo zifuatazo: -
i. Shamba la bibi limeota nyasi
_____________________________________________________________
_____________________________________________________________

ii. Gari lililoondoka limepata ajali
_____________________________________________________________
_____________________________________________________________

iii. Nyumba yetu ni nzuri sana
_____________________________________________________________
_____________________________________________________________

iv. Kiatu kile ni cha mtoto
_____________________________________________________________
_____________________________________________________________

v. Wanafunzi wangapi wanapenda mayai?
_____________________________________________________________
_____________________________________________________________

(b) vitenzi vifuatavyo kuwa nomino:

i. Andikiwa _____________________________________________________________

ii. Cheza _____________________________________________________________

iii. Pika _____________________________________________________________

iv. Kula _____________________________________________________________

v. Funga _____________________________________________________________

5.Unaelewa nini kuhusu istilahi zifuatazo?

(i) Lakabu ___________________________________________________________
_________________________________________________________________

(ii) Ufahamu _________________________________________________________
_________________________________________________________________

(iii) Miviga ___________________________________________________________
_________________________________________________________________

(iv) Kitenzi __________________________________________________________
_________________________________________________________________

(v) Ngonjera ________________________________________________________
_________________________________________________________________

6 (a) Juma alikuwa hajui sababu za fasihi simulizi kuwatumia wahusika wasio binadamu. Hivyo alimfuata rafiki yake aitwae Amina. Unadhani Amina alimtajia sababu zipi?
i. …………………………………………………………………………………………

ii. …………………………………………………………………………………………

iii. …………………………………………………………………………………………

iv. …………………………………………………………………………………………

v. …………………………………………………………………………………………

(b) Eleza maana ya nahau zifuatazo
i. Kujitia kitanzi
……………………………………………………….……………………………

ii. Ulimi wa upanga
……………………………………………………….…………………………..

iii. Kutia chumvi
……………………………………………….……………………………………

iv. Kuwa kinyonga
…………………………………………………………………………………….

v. Kuvimba kichwa
………………………………………………..……………………………………

7. (a) Fasihi simulizi inaweza kuhifadhiwa kwa njia mbalimbali. Zitaje tano na ueleze ubora na udhaifu wake

NJIA
UBORA
UDHAIFU
i.



ii.



iii.



iv.



v.



(b) Fafanua kwa mifano dhahili dhana zifuatazo:-

i. Mofu ………………………………………………………………………………….

……………………………………………………………………………………………

ii. Hekaya ……………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………

iii. Simo ………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………

iv. Miviga ………………………………………………………………………………..
……………………………………………………………………………………………

v. Ukwapi ……………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………

8. Sentensi zifuatazo zimekosewa. Bainisha kosa kwa kupigia mstari neno lililokosewa kisha ziandike kwa usahihi:
(i) Nyinyi nyote mnaitwa ofisini.
________________________________________________________________

(ii) Kifaranga changu amepotea.

________________________________________________________________

(iii) Baba alikasilika sana jana.

________________________________________________________________

(iv) Atutaenda kumuona bibi maana amekuja.

________________________________________________________________

(v) Thamani zote za darasa letu zimevunjwa.

________________________________________________________________

9. Andika neno moja sahihi kutokana na maelezo yafuatayo:-

i. Mahali maalumu ambapo matukio ya kazi ya kifasihi yanafanyika

……………………………
ii. Tungo za kifasihi simulizi zitumiazo lugha ya picha, tamathali za semi na ishara huitwa …………………………………….

iii. Hadithi fupi za kuchekesha na kukejeli huitwa?

……………………………………

iv. Silabi zinazofanana zinazounda mistari ya beti za mashairi huitwa

……………………………..…….

v. Mbinu ya kisanaa ambayo mhusika huuliza swali ambalo jibu analifahamu huitwa ………………..…………………………

vi. Semi zenye pande mbili zenye ukinzani …………………………………

vii. Mstari wa mwisho katika kila beti huitwa ……………………………………..

viii. Majibizano, mjadala au malumbano ya watu wawili au zaidi katika mtindo wa shairi ………………………………….

ix. Hadithi zinazoelezea vyanzo au chimbuko la maumbile ya binadamu, wanyama, miti au vitu visivyo na uhai ………………….……………………

x. Jumla ya mawazo, dhamira, migogoro, mitazamo, msimamo, falsafa na ujumbe katika kazi za fasihi ………………………………………….

SEHEMU C (ALAMA 15)

Jibu maswali yote

10. Kampuni ya SEYPALM imetangaza nafasi tatu za ajira katika idara ya Uafisa masoko kupitia gazeti la Majira la tarehe 20/03/2024. Watu wote wenye sifa stahiki wanatakiwa watume maombi yao kabla ya tarehe 20/04/2024 kwa mkurugenzi mkuu wa SEYPALM, S.L.P 65473 Dodoma Hivyo mwandikie barua rafiki yako ambaye ana vigezo vilivyoaninishwa ukimjuza kuhusiana na fursa hizo. Jina lako liwe, LIANDELI LEONIDAS LUKWARO.

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 84  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 84  

TUME YA KIKRISTO YA HUDUMA ZA JAMII (CSSC)

KANDA YA MAGHARIBI

image

MTIHANI WA UTIMILIFU KIDATO CHA PILI

KISWAHILI

CODE: 021

MUDA: 3: 00 MASAA   TAREHE: 29/08/2023

MAELEKEZO

  1. Katarasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10) 2. Jibu maswali yote.
  2. Sehemu A ina alama 16, sehemu B ina alama 54 na sehemu C ina alama 30.
  3. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali
  4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi kwenye chumba cha mtihani.
  5. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukrasa wa mtihani huu.
  6. Majibu yote yaandikwe katika nafasi ulizopewa kwa wino mweusi mweusi au bluu

SEHEMU A: ( alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele i-x, kisha andika jibu katika kisanduku ulichopewa

i. Uhakiki wa kazi yoyote ya fasihi huzingatia vipengele /maeneo makuu mawili ambayo ni :

  1. Falsafa na msimamo wa mwandishi
  2. Fani na dhamira ya mwandishi
  3. Umbo la nje la kazi na umbo la ndani 
  4. Umbo la kazi na husiano wa mambo

ii. Upi ni mzizi wa neno ANAKUNYWA?

  1. kunywa
  2. kunyw 
  3. nyw
  4. nywa

iii. Sehemu ya neno inayoundwa na sauti moja au zaidi inayotamkwa mara moja kama fungu moja la sauti

  1. Silabi
  2. Fonimu 
  3. Mofimu
  4. Neno

iv. Ni muundo upi wa ushairi wa fasihi simulizi huundwa na mstari/mishororo mitano?

  1. Sabilia
  2. Takhmisa 
  3. Tathilitha
  4. Tathimisa

v. Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo haina maana zaidi ya moja?

  1. Kaka amefua nguo
  2. Nipe sahani ya kulia
  3. Suedi amenunua mbuzi
  4. Asha amempigia mpira

vi. Kwanini kuna haja ya kutumia maneno katika miktadha mbalimbali?

  1. Ili kujenga heshima
  2. Ni chanzo cha rejesta na misimu
  3. Huonesha elimu tuliyonayo kwa watu wengine
  4. Kutafsiri maneno kutoka lugha moja kwenda nyingine

vii. Lugha ni sauti za nasibu kwasababu

  1. Binadamu hazaliwi na lugha
  2. Lugha ni muunganiko wa herufi
  3. Lugha huwa na maana maalumu
  4. Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye mpangilio

viii. Silaha yake haina risasi, kauli hiyo hujulikana kama:

  1. Hutokana na mazingira
  2. Hana uwezo wowote katika jamii
  3. Tafsida
  4. Matumizi ya misimu

ix. Pande zinazohusika katika lugha ya maandishi ni zipi?

  1. Mwandishi na mchapaji
  2. Msomaji na mwandishi
  3. Msomaji, mwandishi na msikilizaji
  4. Msomaji na msikilizaji

x. Nyimbo ni nyenzo muhimu katika kurahisisha kazi na kupunguza uchovu. Ni nyimbo zipi utashauri ziimbwe kwenye shughuli za kilimo?

  1. Wawe
  2. Kimai 
  3. Nyiso
  4. Mbolezi

Swali

i

ii

iii

iv

v

vi

vii

viii

ix

x

Jibu

2. Oanisha maana ya dhana zilizopo orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana husika katika orodha B, kisha andika herufi husika katika sehemu ya majibu uliyopewa

ORODHA A

ORODHA B

  1. Taniaba
  2. Mubaalagha
  3. Mjalizo
  4. Nidaa
  5. Sitiari
  1. Matumizi ya viunganishi katika maneno
  2. Kulinganisha maneno bila viunganishi
  3. Jina la mtu hutumiwa na mtu mwingine mwenye tabia kama ile
  4. Hali ya kuongeza maneno ya ziada
  5. Mfuatano wa maneno bila kutumia viunganishi mfano aliimba, alicheza, aliruka n.k
  6. Matumzi ya alama ya mshangao
  7. Mbinu ya kupunguza ukali wa maneno

SEHEMU B: (alama 70)

3. Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata:

Kwa kweli maisha ya vijana wa kisasa yanatofautiana sana na yale ya wazee wao. Sio katika mavazi, lugha, mienendo, mitazamo au mawazo tu bali pia katika mambo mengine mengi. Yote haya ni vielelezo vya jinsi kizazi cha leo kinavyoishi katika ulimwengu ambao ni kivuli tu cha vizazi vilivyotangulia. Baadhi ya watu wameieleza hali hii kuwa maisha sio jiwe. Kwao si ajabu katu kuwaona vijana wakiwa na mitindo mipya ya maisha yao. Kama vile, wakizungumza lugha yao ya kipekee au wakivaa nguo zinazobana ajabu na kudhihirisha bayana maungo yao badala ya kuyasitiri.

Watu wengi hufikiri kwamba maasi ya vijana wa leo yanayotokana na mambo lukuki, kama vile vishawishi, tamaa, kutaka maisha ya mkato na kupenda vitu vikubwa zaidi ya uwezo wao. Upande huu umetoa rai kwamba kizazi hiki kisingelipotoka kama tu kingezingatia na kustahi utamaduni wa wahenga wao ambao wazazi wao ndimo walimokulia. Wanazidi kufafanua kuwa nyendo hizi za miaka ya nyuma zilithamini sana amali kama uaminifu, heshima kwa wazee ama wakuu, kukinai, bidii, ushirikiano, ukarimu, unyenyekevu, hadhari katika kila jambo, utiifu na pia kujitegemea. Mambo haya yote yamesahaulika ama yamepuuzwa katika utamaduni wa kisasa.

Swali lililopo ni je tunapaswa kuwahukumu vijana wa leo kwa kutumia vigezo au masharti gani? Tuwapime kwa mujibu wa hali ya duniani ya leo ama kwa mujibu wa jinsi maisha ya baba na babu zao yalivyokuwa. Jibu la swali hili ni gumu na sharti lifafanuliwe kwa makini ili lisije likaegemea upande wowote.

Ni jambo lisilopingika kuwa maisha ni utaratibu unaoathirika na hivyo hubadilika daima. Kwa kweli maendeleo ya elimu, sayansi na hata mawasiliano yameyageuza maisha ya siku hizi. Mathalan leo inawezekana vijana wa barani Afrika wakaona na hata kuzungumza na wenzao kutoka Uropa, Asia na Marekani wakiwa nyumbani kwao. Athari za filamu, video, vitabu, magazeti au majarida haikadiriki. Mambo hayo kwa kiasi yamewafanya vijana hata kupevuka kabla ya wakati wao. Isitoshe yameweza kuwazuzua na kuwaaminisha kuwa yale wanayojifunza ni kweli. Matokeo yake yamekuwa ni wao kuudharau utamaduni wao wa asili na kuvutiwa na ule wa kigeni.

Hivyo wazazi wana wajibu mkubwa wa kuwaongoza na kuwasaidia vijana ili kuwa na uwezo wa kujitambua na kufanya maamuzi mwafaka katika maisha yao.

Maswali

a. Andika kichwa cha habari uliyoisoma, kisichozidi maneno matano

________________________________________________________________

b. Kwa nini kizazi cha leo kinadaiwa kuishi katika ulimwengu ambao ni kivuli tu cha vizazi vilivyotangulia?

________________________________________________________________________

______________________________________________________

c. Kulingana na mwandishi, kundi linalodai kuwa “maisha sio jiwe” lina maoni gani?

_______________________________________________________________________

______________________________________________________

d.  Bainisha jambo moja (1) linaloweza kusaidia kizazi cha vijana wa leo kisipotoke

________________________________________________________________________

________________________________________________________________________

e.  Toa mfano mmoja (1) unaoonesha namna maendeleo ya elimu, sayansi na mawasiliano yalivyoyageuza maisha ya vijana wa leo

__________________________________________________________________

__________________________________________________________________


4.(a) Toa mfano mmoja kwa kila kielezi cha namna kifuatacho

i. Kielezi cha namna kikariri__________________________________________

ii. Kielezi cha namna kiigizi ___________________________________________

(b) Ainisha maneno yanayounda tungo zifuatazo

i. Kaka Ali anacheza bao _____________________________________________

ii. Hapa si pazuri ____________________________________________________

(c) Bainisha hisia zilizomo katika vihisishi vifuatavyo:

i. La hasha! ___________________________________________________

ii. Oyee! _________________________________________________________

(d) Badilisha vitenzi vifuatavyo katika kauli ya kutendwa

i. Omba________________________________________

ii. Sahau ________________________________________

(e) Fafanua kwa kutumia mfano aina zifuatazo za unominishaji

i. Nomino kutokana na kivumishi_________________________________________________________

ii. Nomino kutokana na kitenzi __________________________________________________________________________________________________________________

5. Kwa kutumia mifano fafanua dhima zifuatazo za rejesta

i. Kuficha jambo kwa wasiohusika

ii. Rejesta husaidia kukuza lugha

iii. Rejesta hutumika kama kitambulisho cha jamii

iv. Rejesta hutumika kurahisisha mawasiliano

v. Rejesta hutumika kupamba lugha

6. Fafanua mambo matano ya kuzingatia wakati wa kutunga hadithi

a. ______________________________________________________________

b. _________________________________________________________________

c. __________________________________________________________________

d. __________________________________________________________________

e. __________________________________________________________________

7. Matumizi mabovu ya methali yanaweza kupotosha watu na kusababisha matatizo ndani ya jamii. Fafanua hoja hiyo kwa kutumia methali tano za Kiswahili

8. Mofimu tegemezi au viambishi huibua dhima mbalimbali kwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili kwa kutumia mfano mmoja toa hoja tano kuthibitisha kauli hiyo:

(b) Eleza maana ya istilahi zifuatazo

i. Maleba

ii. Fonimu

iii. Kongozi

iv. Mizungu

v. Kiimbo

9. Andika kifupisho kinachotumika katika kamusi ya Kiswahili sanifu kwa kila neno kati ya maneno yafuatayo: mfano: kwa mfano =k.m

i. Kemia ________________________________

ii. Kibaharia _____________________________

iii. Kiunganishi __________________________

iv. Fizikia ________________________________

(b) Taja aina za kamusi zinazowafaa watumiaji wafuatao:

i. Mtu anayetaka kujifunza misemo

______________________________________________________________

ii. Mtu anayetaka kujifunza fizikia, biolojia na isimu

_________________________________________________________

iii. Mtu anayetaka kujifunza maneno ya lugha moja yenye maana sawa

______________________________________________________________

iv. Mtu anayetaka kujifunza lugha zaidi ya mbili ______________________________________________________________

(c) Onesha mambo mawili yanayosababisha utata katika lugha

SEHEMU C: (alama 15)

10. Baba yako anafanya kazi kama mwalimu mkuu shule ya msingi Zimamoto S.L.P 3, Tukuyu mwandikie barua ukimuomba pesa ya matumizi binafsi uwapo shuleni. Jina lako liwe Akilimali Juma wa S.L.P 15 Unguja.

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 72  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 72  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

image 

SINGIDA MUNICIPAL COUNCIL

 021 KISWAHILI

Time: 2:30 Hours JULAI 2023 

MAELEKEZO: 

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10)
  2. Jibu maswali yote
  3. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa
  4. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu ya wino wa bluu au mweusi
  5. Vifaa vyote vya mawasiliano haviruhusiwi katika chumba cha mtihani

KWA MATUMIZI YA MTIHANI TU

NAMBA YA SWALI 

ALAMA 

SAHIHI YA MTAHINI

1

2

3

4

5

6

7

8

9

10

JUMLA 



SEHEMU A (ALAMA 15) 

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. i) Sauti za lugha ambazo hutamkwa bila kuwepo kwa kizuizi chochote kwenye mkondo kwa hujulikana kama:-

  1. sauti 
  2. Herufi 
  3. Irabu 
  4. Konsonanti

ii) Silabi zinazotokea katikati au mwishoni mwa kila mstari wa shairi huitwa . . .. 

  1. Vina 
  2. Mizani 
  3. Sitiari 
  4. Vituo

iii) Kiimbo hufasiliwaje katika mazungumzo?

  1. Kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti 
  2. kuzungumza na kuongea kwa sauti 
  3. kuzungumza kwa kupandisha mawimbi ya sauti 
  4. kuzungumza kwa kushusha mawimbi ya sauti

iv) Dhana ipi kati ya hizi zifuatazo haina maana Zaidi ya moja?

  1. Kaka amefua nguo 
  2. Nipe sahani ya kulia 
  3. Eva amenunua kanga 
  4. John amempigia mpira

v) Mkisi ameenda Dodoma. Neno Dodoma limetumika kama

  1. Kihisishi 
  2. Nomino 
  3. Kiwakilishi 
  4. Kielezi

vi) Mawazo makuu ya mtunzi wa kazi ya fasihi humfikia mlengwa kwa njia ipi kati ya hizi zifuatazo.

  1. Fani 
  2. Falsafa 
  3. Migogoro 
  4. Dhamira

vii) Ipi ni tofauti ya msingi kati ya mashairi na ngonjera?

  1. Mpangilio wa vina na mizani 
  2. Idadi ya mizani na mishororo 
  3. Majibizano baina ya watu wawili au Zaidi 
  4. Mpangilio wa silabi na lugha ya mkato.

viii) Bosi samahani kuna barua yako hapa “Mtindo huu wa mazungumzo unatumika wapi”? 

  1. Ofisini 
  2. Kiwandani 
  3. Shambani 
  4. Kanisani

ix) Sababu zifuatazo husababisha kutokea kwa utata katika tungo isipokuwa

  1. Neno kuwa na maana Zaidi ya moja 
  2. Kuzingatia taratibu za uandishi 
  3. Kutumia maneno yenye maana ya picha 
  4. Kutotamka neno ulilokusudia kwa usahihi

x) Seti ipi ni sahihi kuhusu vipengele vya fani katika fasihi simulizi?

  1. Dhamira, migogoro, mtindo na mafunzo 
  2. Ujumbe, matumizi ya lugha, wahusika, mtindo na muundo 
  3. Wahusika, matumizi ya lugha, muundo, mtindo na mandhari 
  4. Migogoro, Ujumbe, wahusika, mafunzo na mtindo.

i

Ii

iii

iv

V

vi

vii

viii

ix

X











2. Oanisha dhima za nyimbo za fasihi simulizi zilizo katika orodha A na aina za nyimbo kutoka orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kisanduku ulichopewa.

Orodha A

Orodha B

  1. Husimuliwa kama mifano ya kuadiri watu 
  2. Husimulia chimbuko la asili ya kitu fulani 
  3. Husimulia kwa nia ya kuchekesha na kukejeli
  4. Husimulia kwa lengo la kuwaasa watoto 
  5. Husimulia kuhusu matukio ya kihistotia
  1. Soga
  2. Tarihi
  3. Vigano
  4. Visasili
  5. Hadithi
  6. Mizungu
  7. ngano


Orodha A

i

ii

iii

iv

v

Orodha B






SEHEMU B (ALAMA 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.

Mazingira yaliyotunzwa huleta raha kwa viumbe na mazingira yaliyoharibiwa ni Karaha kubwa si tu kwa binadamu bali hata kwa viumbe vingine vyote. Aidha utunzaji wa mazingira ni wajibu wa kila mtu na kila raia wa Tanzania na ulimwenguni kote kwa ujumla. Hata hivyo wapo wananchi wanaokiuka wajibu huo muhimu na kusababisha uharibifu mkubwa sana.

Katika nchi zilizoendelea uharibifu wa mazingira husababishwa na shughuli za viwanda ambapo mitambo mbalimbali ingunemapo hutoa moshi kwa wingi ambao huenea angani na kusababisha madhara makubwa kwa mimea na wanyama.

Hali hii ni tofauti kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Katika nchi kama hizo mazingira yanaharibika kutokana na shughuli za kibinadamu kama vile kilimo, ujenzi, pamoja na uchimbaji wa mchanga na kokoto. Kilimo kinachohusishwa na uharibifu wa mazingira ni kile kinachojumuisha ukataji wa miti bila huruma, uchomaji moto misitu na kulima kwenye miteremko mikali.

Hali hiyo husababisha mmomonyoko wa udongo kwani upepo mkali na maji vinafanya kazi bila kizuizi chochote. Ili kunusuru hali hii yafaa kupanda miti kwa bidii, kusimamia sheria zilizowekwa za utunzaji wa mazingira na kuelimisha raia wote juu ya utunzaji wa mazingira.

MASWALI

a) Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma kisichozidi maneno matano.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

b) Kwa mujibu wa habari uliyoisoma eleza kwa kifupi ni kwa vipi kulima kwenye miteremko huweza kusababisha mmomonyoko wa udongo

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

c) Taja shughuli mbili za kibinadamu zinazoweza kuharibu mazingira

i) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .. 

ii) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

d) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu cha habari ulichosoma

i) Karaha . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

ii) Kiuka . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .. 

iii) Nusuru . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

iv) Bidii . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ....

v) Nguneno . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

e) Andika funzo ulilopata kutokana na habari hii

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .


4. Ni taarifa gani zinazohusu neno huingizwa katika kamusi? ( Taja tano )

i) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..... 

ii) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

iii) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

iv) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

v) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

5. Sentensi zifuatazo ni tata. Toa maana mbili kwa kila sentensi ili kudhibitisha utata huo

i) Masudi ameiba kanga

a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

ii) Kaka amenunua tai

a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

iii) Daktari aliniunga mkono

a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

iv) Tausi amemwandikia mama yake barua

a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

v) Juma alimpigia mwanangu mpira

a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

6. a)Eleza maana ya lugha ya mazungumzo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

b) Taja mambo manne yanayotakiwa kuzingatia wakati wa mazungumzo

i) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

ii) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

iii) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

iv) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

c) Eleza dhima tano za lugha

i. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .. 

ii. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

iii. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . iv. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . v. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

7. a) Sentensi zifuatazo zina makosa, sahihisha

i) Wanafunzi watoro wataazibiwa

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

ii) Ng’ombe zangu zinakunywa maji

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

iii) Mbuzi wangu mjamzito

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

iv) Nilimkuta hayupo

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

v) Gari yangu imeharibika

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

b) Eleza dhima za viambishi vilivyopigwa msitari

a)Anasoma

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .. 

b) Wamempikia

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

c) Atakusubiri . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

d) Atakulilia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .. 

e) Unakula . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

8. Toa tofauti tano (5) zilizo kati ya Lugha ya Mazungumzo na Lugha ya Maandishi.

LUGHA YA MAZUNGUMZO

LUGHA YA MAANDISHI 

i.


ii.


iii.


iv.


v.


9. Taja methali moja ambayo ungeweza kuitumia au kubadilisha kulingana na tukio lililoelezwa hapo chini

i) Ndege alijenga kiota kwa kuchukua jani mojamoja na hatimaye baada ya siku tatu kiota kilikamilika.

Methali . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

ii) Wastara alikuwa masikini akajibidisha sana kufanya kazi usiku na mchana hatimaye akafanikiwa kupata utajiri na kuishi maisha yenye hadhi.

Methali . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

iii) Simba alivamia zizi la mzee Mahende na kukamata ng’ombe mmoja, alipotoka na mkuki kumkabili alishindwa akarudi nyuma kwa hofu, kisha kapiga yowe wanakijiji walikusanyika wakiwa na mikuki na mapanga na marungu wakampiga na kumuua simba huyo.

Methali . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

iv) Dereva aliendesha gari kwa kasi na kusababisha ajali mbaya

Methali . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

v) Baba alipofiwa na mtoto wake alilia sana hadi akazimia

Methali . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

SEHEMU C (ALAMA 15)

10. Andika insha isiyopungua maneno 150 na isiyozidi maneno 200 kuhusiana na athari za ugonjwa wa UKIMWI.

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 67  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 67  

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

UPIMAJI KIDATO CHA PILI MKOA WA MOROGORO 

CODE: 021 KISWAHILI

MUDA: SAA 2:30   MWAKA: 2023

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10)
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A, B na Cimage
  3. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali
  4. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasl ulizopewa
  5. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1, Katika vipengele (i) hadi (x) chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika kisanduku ulichopewa.

  1. Msingi wa kujua lugha yoyote ni:
  1. Kujua kuongea lugha husika
  2. Kuifahamu ilikoanzia
  3. Kuifahamu sarufi yake
  4. Kuwa mjuvi wa kusomaimage
  5. Kuifahamu chimbuko lake

ii) Konsonanti na Irabu ni :-

  1. Herufi kuu 
  2. Fonimu 
  3. Tanzu za lugha
  4. Sauti
  5. Vitamkwa

iii) Janeti ni binti aliyekuwa anashindwa kutamka neno "Themanini". Unafikiri ni kwdnini alishindwa kutamka hasa herufi ya mwanzo?

  1. Kwa sababu alikuwa hana meno ya mbele
  2. Kwa sababu alikuwa hana uwqzo wa kutamka neno
  3. Kwa sababu alikuwa a kithembe, athari ya lugha mama
  4. Kwa sababu alikuwa a athari ya lugha ya kwanza aliyobobea.
  5. Kwa sababu alishind a kuelewa kirahisi maana ya neno "The"

iv) Kuunda maneno kwa kutumi mofimu mbalimbali hujulikana kama:-

  1. Uambishaji 
  2. Urudufishaji maneno
  3. Uhulutishaji 
  4. Uundaji wa
  5. Uundaji wa viambishi

v) Mzizi ni sehemu ya neno

  1. Kama shina 
  2. Yenye kuleta 
  3. Yenye kitenzi
  4. Kama silabi funge maana
  5. Isiyobadilika

vi) Kosa la kisarufi katika mawa iljano ni pamoja na

  1. Kosa la kimantiki 
  2. Kosa la kimuundo
  3. Kosa la kujitakia
  4. Kosa la kutofuata maelekezo 
  5. Kosa la kimawasiliano

vii) Vifuatavyo ni vivumishi vya -a-unganifu

  1. Juma na Rosa
  2. Kitabu chochote 
  3. Kitabu cha Anna
  4. Jino lolote
  5. Kibao chote

viii) Mzee Jumbe ana watoto wanne (04). Ally, Jesika, Selina na Ombeni. Mzee Jumbe ana wajukuu wengi sana ambao wamezaliwa na Ally ambaye ni;

  1. Hadithi 
  2. Nyimbo 
  3. Ngoma maonesho
  4. Jando na Unyago
  5. Sanaa na

ix) Unafikiri mzee Jumbe ni nani ukirejea hapo juu?

  1. Fasihi simulizi
  2. Tanzu za fasihi simulizi
  3. Babu wa wajukuu wengi
  4. Fasihi andishi
  5. Tanzu za fasihi andishi

x) Nukta pacha ni moja kati ya ......... katika uandishi

  1. Alama pacha
  2. alama za uandishi
  3. koma
  4. nukta
  5. alama ya mshangao

2. Oanisha dhana zilizo katika orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana husika katika orodha B kasha andika herufi husika katika karatasi ya kujibia.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Upekee wa kundi la watu na shughuli zinazofanyika.
  2. Mitindo tofauti tofauti ya lugha katika miktadha mbalimbali
  3. Mzizi
  4. Kupamba lugha, kuficha ujumbe, kukuza lugha
  5. Mofo huru
  1. Mkazo
  2. Rejesta
  3. Misimu
  4. Sasa
  5. –nyw-
  6. Chanzo cha rejesta
  7. Dhima za rejesta

SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata,

Zamani sana, watoto walichukuliwa kama chanzo cha mali. Mja aliyekuwa na wanawake wengi alihesfiimiwa sana na kuhesabiwa miongoni mwa walionacho. Halikuwa jambo la kushangaza kupata familia yenye wana ishirini,

Ingawa wazee wengi walikuwa na wake wengi waliowazalia wana chunqunzima watoto hawakuonekana kama mzigo. Kwa hakika walitumiwa kama nyenzo za kuzalisha mali katika mashamba na kuchunga ng'ombe. Sio ajabu basi kwamba zama hizo, vijana wengi walichelewa kuanza masomo ya shuleni kwa sababu ya kushughulika na harakati za nyumbani.

Kadri jamii ya binadamu ilivyozidi kukua na kupanuka, ndivyo maisha yalivyozidi kubadilika. Elimu ya kigeni ilianza kushika nguvu, mpaka sasa kuna mabadiliko na maendeleo ya hali ya juu.

MASWALI.

a) Andika kichwa kinachofaa katika habari uliyosoma.

b) Toa maana ya misamiati ifuatayo itokanayo na habari uliyosoma

i) Walionacho

ii) Wana

iii) Chungunzima

iv) Zama

c) Ni kwa nini watoto walichelewa kuanza shule

d) Fupisha habari uliyosoma kwa maneno kati ya 35-45 (aya 1).

4. Kwa kutumia mifano eleza maana ya dhana zifuatazo

a) Fonimu

i) maana............................

ii) mfano...........................

c) Sarufi miundo (sintaksia)

i) Maana..............................

ii) mfano..............................

d) Mofimu

i) Maana...............................

ii) Mfano.............................

e) Mtindo

i) Maana ..............................

ii) Mfano.............................

5. Taja miundo mitano (5) ya silabi huku ukionesha mifano hai,

a)..................................

Mfano

b....................................

Mfano..

c....................................

Mfano........

d.....................................

Mfano.................................

6, a) Kwa kutumia neno "alikuwa

i) Tunga sentenzi yenye kitenzi kisaidizi (TS)

ii) Tunga sentensi yenye kitenzi kishirikishi (t)

iii) N + TS + T + N + E (Tunga sentensi ya muundo huu).

b) Eleza maana ya dhana zifuatazo (Toa mifano).

i) Kielezi

Mfano

  1. Nomino

Mfano

  1. Mfano

c) Panga maneno yafuatayo katika kamusi

i) Zumat zama, zuwena, zayuna

ii) Baraka, Bayona, Bavana, Bakari

iii) Zawadi, Jeradi, Jeradina, Yoeli

7. a) Tunga ngonjera Takhmisa beti 2 kuhusu Mmomonyoko wa maadili kwa jamii ya sasa.

b) Chambua na uhakiki vipengele vifuatavyo kutoka kwenye ngonjera uliyotunga.

i) Wahusika (fani)

ii) Muundo (fani)

iii) Mtindo (fani)

iv) Dhamira kuu (maudhui)

v) Mgogoro (maudhui)

8. Onesha dhima tano (5) za viambishi (Toa mifano)

i) Mfano

ii) Mfano

iii) Mfano

iv) Mfano

v) Mfano

NAMBA YA MTAHINIWIA

9. Taja aina tano (5) za rejesta kutokana na miktadha mbalimbali (Tumia mifano kudadavua jibu lako). image

i) Mfano

ii) Mfano

  1. Mfano
  1. Mfano

v) Mfano

SEHEMU C (Alama 15)

Jibu swali la kumi (10)

10. Watu huwasiliana kwa njia mbalimbali. Barua ni njia mojawapo inayotumika. Ukiwa mwanafunzi unayetarajia kufanya mtihani wa taifa mwaka huu, andika barua kwa rafiki yako ukimjulisha namna ulivyojiandaa kwa mtihani huo.

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 63  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 63  

NAMBA YA MTAHINIWA . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

IMG_20230509_084505

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAOFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 

HALMASHAURI YA WILAYA YA MVOMERO 

NEMBO

MTIHANI WA UTIMILIFU KIDATO CHA PILI 

 021  KISWAHILI

MUDA: SAA 2:30 MEI 2023

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B and C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote.
  3. Sehem A ina alama kumi na tano (15), sehemu B ina alama sabini (70) na sehemu C ina alama kumi na tano (15).
  4. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa.
  5. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  6. Vifaa vyote vya mawasiliano visivyoruhusiwa havitakiwi kwenye chumba cha upimaji.
  7. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.

KWA MATUMIZI YA MPIMAJI TU

NAMBA YA SWALI

SAHIHI YA MPIMAJI

ALAMA

1
2
3
4
5
6
7
8
9
10

JUMLA

SAHIHI YA MHAKIKI

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika seheme hii.

1. Chagua jibu sahihi katika maswali yafuatayo:

i. Ni kiambishi kipi kinachodokeza ukanushi kati ya vifuatavyo:

  1. Wa-
  2. Sh-
  3. -a
  4. Si-
  5. Na-

ii. Neno lipi kati ya haya ni mofu huru?

  1. Uji
  2. Uzuri
  3. Uchache
  4. Ufa
  5. Upweke

iii. Unyumbulishaji katika lugha ya Kiswahili huhusisha uchapikaji wa viambishi.

  1. Kabla ya mzizi wa neno
  2. Katikati ya mzizi wa neno
  3. Baada ya mzizi wa neno
  4. Kabla na baada ya vitenzi
  5. Kabla, katikati na baada ya mzizi

iv. Ni kauli inayotumia maneno ya kawaida lakini hutoa maana tofauti kabisa na iliyopo kwenye maneno Yale.

  1. Mafumbo
  2. Nahau
  3. Misemo
  4. Semi
  5. Hadithi

v. Utokeji wa misimu katika jamii hutegemea na

  1. Uchaguzi wa viongozi
  2. Mabadiliko ya kijamii
  3. Shughuli itendekayo
  4. Utani uliopo miongoni mwa wanajamii
  5. Kutumika na kudumu kwa muda mrefu

vi. Nyenzo kuu za lugha ya mazungumzo ni

  1. Usimuliaji
  2. Mdomo
  3. Maandishi
  4. Vitendo
  5. Ishara
vii. Utoshelezi wa muwala ni vipengele vya
  1. Mtindo
  2. Matumizi ya lugha
  3. Muundo
  4. Ujumbe
  5. Falsafa

viii. Neno lipi kati ya haya yafuatayo halihusiani na ushahiri

  1. Mshororo
  2. Kipande
  3. Bahari
  4. Dayalojia
  5. Muwala
ix. Tamathali inayofanya kitu kisicho na uhai kutenda kama binadamu
  1. Sitiari
  2. Tashihisi
  3. Tashibiha
  4. Mubalaga
  5. Takriri

x. Ni uchunguzi au uchambuzi wa kina wa kazi ya fasihi kama vile tamthiliya,riwaya,na mashairi Kwa lengo la kufafanua

  1. Uhakiki
  2. Mhakiki
  3. Dhamira
  4. Hadhira
  5. Hadithi

2. Onesha dhana zilizopo fungu A na mifano iliyopo fungu B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi.

FUNGU A

FUNGU B

  1. Kiimbo
  2. Semi
  3. Vigano
  4. Miviga
  5. Masivina
  1. Sherehe zinazofanywa na jamii katika vipindi na mazingira mbalimbali
  2. Tungo fupi za kisanaa zitumiazo ishara na lugha ya picha .
  3. Mashairi yanayozingatia urari wa vina na mizani
  4. Mashairi yasiyozingatia urari wa vina na mizani
  5. Hadithi zitumiazo wahusika wa aina mbalimbali.
  6. Hadithi fupifupi zenye lugha ya ucheshi.
  7. Hadithi fupi zinazoelezea uovu wa watu
  8. Utaratibu wa kupanda na kushuka Kwa mawimbi ya sauti wakati wa utamkaji wa maneno.
  9. Ni kauli zitumiazo lugha ya picha na mafumbo kueleza vipengele vya Mila na desturi.

SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika seheme hii.

3. Tumia mofimu zifuatazo kuonesha thamani ilizopewa katika paradise Mfano Li- Kuonesha wakati uliopita (Aliondoka)
  1. ta - kuonesha wakati ujao   
  2. o - kuonesha mzizi wa neon -  
  3. ni - kuonesha kitenzi kishirikishi-  
  4. ku- kuonesha urejesho kwa mtendwa-  
  5. ki - kuonesha udurushaji -  
  6. me - kuonesha hali timilifu -  
  7. kwa - kuonesha mahali -  
  8. a - kuonesha nafsi -  
  9. ka - kuonesha kauli ya kutendeka -  
  10. ku - kuonesha wakati uliopita -  
4. (a) Maneno katika lugha yana dhima mbalimbali, bainisha aina ya vivumishi katika tungo zifuatazo: -
  1. Shamba la bibi limeota nyasi
  1. Gari dogo limepata ajali
  1. Nyumba yetu ni nzuri sana
  1. Kile kiatu ni cha mtoto
  1. Wanafunzi wangapi wanapenda mayai?
  1. Badilisha nomino zifuatazo kuwa vitenzi?
    1. Wimbo  
    2. Umbo   
    3. Kilio   
    4. Mtoro   
    5. Mlo   
5. Toa maana mbili kwa kila neno
  1. Mbuni
  2. Mto
  3. Ota
  4. Pepo
  5. Shuka
6. Sentensi zifuatazo zinabeba maana ya istilahi fulani. Zianishe istilahi hizo kwa kila sentensi. Mfano: Ni kipashio kidogo cha lugha chenye maana kisarufi “Mofimu
  1. Ni aya ndogo kwenye kamusi ambayo huhusisha kidahizo na maelezo yake yote
  2. Ni sauti ambazo hutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti
  3. Ni mtindo wa lugha wa watu Fulani katika kazi maalumu   
  4. Ni maneno ambayo huonesha hisia za mtenda au mtendwa   
  5. Kamusi huandikwa kwa lugha moja   

7. Kila mhusika ana kazi yake katika kazi ya fasihi. Taja kazi moja moja ya wahusika wafuatao.

  1. Fanani
  2. Hadhira
  3. Wanyama
  4. Binadamu
  5. Mahali

8. Katika kazi ya fasihi simulizi viungo vya mwili kama vile macho, mdomo, kichwa, miguu hata mikono husaidia kufanikisha kazi hiyo na kafikisha ujumbe kwa jamii. Taja na eleza kwa kifupi faida tano (5) za kutumia viungo hivyo vya mwili vilivyotajwa hapo juu katika kazi ya fasihi simulizi.

9. Zifuatazo ni njia zinazotumiwa kuhifadhi fasihi simulizi.Onesha faida Moja na hasara Moja Kwa Kila njia.

NJIA

FAIDA

HASARA

I). Kichwani

Ii). Maandishi

III).Vinasa sauti

iv).Sinema ( filamu)

v). Kompyuta ( mtandao)

SEHEMU C (Alama 15) 

10. Kwa hoja nne (4), fafanua hasara ambazo huweza kumkumba mtu yeyote asiyependa kushiriki mazoezi na michezo hasa kwa wanafunzi shuleni.

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 53  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 53  

BARAZA LA WAKUU WA SHULE ZA KIISLAMU TANZANIA

MTIHANI WA UTAMILIFU WA SHULE ZA KIISLAMU KIDATO II

021 KISWAHILI  

MUDA: SAA 2:30  Jumanne, 25 Julai 2023 Mchana

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A, B na C.
  3. Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B ina alama sabini (70) na sehemu C ina alama kumi na tano (15).
  4. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.
  5. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  6. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa.
  7. Vifaa vyote vya mawasiliano visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  8. Andika Namba yako ya upimaji katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kuli.

KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU

Namba ya swali

ALAMA

SAINI YA MTAHINI

1

2

3

4

5

6

7

8

9

10

JUMLA



SAINI YA MKAGUZI


SEHEMU A: (Alama 15)


Jibu maswaliyotekatika sehemu hii

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye kisanduku cha kujibia ulichopewa.

(i) Juma alinunua viatu vizuri, vizuri vyote vimehifadhiwa. Shinuna alivipanga vizuri. Katika mfuatano wa sentensi hizo neno “vizuri” limetumika kama:

  1. Kiwakilishi, kielezi na kivumishi
  2. Kiwakilishi, kivumishi na kielezi
  3. Kivumishi, kielezi na kiwakilishi
  4. Kivumishi, kiwakilishi na kielezi

(ii) Chunguza kwa makini taarifa ifuatayo kisha jibu swali linalofuata:

SHULE YA SEKONDARI ZIWANI,

S.L.P. 239,

MTWARA.

20/5/2023

Kwa mujibu wa taratibu za uandishi wa barua, taarifa hiyo ina vipengele vingapi?

  1. Viwili – Anuani na mahali
  2. Viwili – Anuani na tarehe
  3. Vitatu Anuani, mahali na tarehe
  4. Viwili – Anuani na shule

(iii) Mwalimu wako wa Kiswahili amekupa kazi ya kutunga shairi la kimapokeo lenye mishororo minne kila ubeti. Ni muundo gani utakaoutumia kutunga shairi hilo?

  1. Sabilia
  2. Tathilitha
  3. Tarbia
  4. Tathmina

(iv) Rauhiya ni mzaliwa wa Unguja na Rauhaina ni mzaliwa wa Mwanza na wote wanazungumza lugha ya Kiswahili. Dhana ipi kati ya zifuatazo huonesha utambulisho wa mazungumzo yao?

  1. Matamshi
  2. Sauti
  3. Lafudhi
  4. Silabi

(v) Walimu wa Kiswahili aghalabu husisitiza kutumia lugha kulingana na muktadha. Je, ipi kati ya zifuatazo ni sababu ya wao kututaka tutumie lugha kulingana na muktadha?

  1. Kuzuka kwa matukio mbalimbali
  2. Kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia
  3. Kumudu shughuli inayofanyika
  4. Kuwezesha mawasiliano

(vi) Shule yetu ipo mkabala na kituo cha polisi, aghalabu huwasikia polisi wakisema “Jambo afande.” Je, ni mtindo gani wa lugha ambao hutumiwa na polisi hao?

  1. Misimu
  2. Rejesta
  3. Utata
  4. Misemo

(vii) Mwalimu wetu wa michezo alitutembeza uwanjani haraka haraka. Katika sentensi hii neno lililopigiwa mstari ni aina gani ya neno?

  1. Kitenzi
  2. Kielezi
  3. Kivumishi
  4. Nomino

(viii) Majaliwa ni shuhuda wa ajali ya ndege iliyotokea Bukoba. Juzi alikuja shuleni kwetu akatusimulia tukio la ajali hiyo nasi tulimsikiliza kwa makini. Je, hii ni aina gani ya ufahamu?

  1. Ufahamu wa kusoma
  2. Ufahamu wa kusikiliza
  3. Ufahamu wa kuona
  4. Ufahamu wa kutafakari

(ix) Mwalimu wetu wa darasa ametupa simu za mkononi ili tuwasiliane na ndugu zetu mbalimbali. Je, ni jambo gani si muhimu kuzingatia wakati wa kuandika ujumbe wa simu za mkononi?

  1. Nambari ya simu ya mpokeaji ujumbe
  2. Jina na sura ya mpokeaji ujumbe
  3. Lengo la kuandika ujumbe
  4. Ujumbe uandikwe kwa kujitosheleza

(x) Milan ni Mturuki anayetaka kujua dhana ya ufahamu. Katika seti zifuatazo msaidie Milan kubaini fasili ya ufahamu iliyo sahihi.

  1. Kujua, kufikia na kuelewa jambo na vitu
  2. Kuona, kusikiliza na kutafakari
  3. Kujua, kuelewa na kuweza kufafanua jambo
  4. Kusoma, kusikiliza na kutafakari

2. Oanisha maana ya dhana za vipera vya fasihi simulizi katika orodha A na vipera husika kutoka orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kisanduku cha kujibia ulichopewa.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Ushairi unaotolewa kwa kutamka badala ya kuimba.
  2. Sadaka inayotolewa kwa miungu, mizimu au mahoka
  3. Hadithi zinazoelezea asili ya tabia, mambo na maumbile katika mazingira
  4. Sherehe au shughuli zinazofanywa na jamii katika mazingira mbalimbali na kwa kipindi maalum cha mwaka.
  5. Kauli yenye picha za mafumbo na inayoonesha ukinzani wa fikra au tukio
  1. Visasili
  2. Mizungu
  3. Tambiko
  4. Maghani
  5. Miviga
  6. Lakabu
  7. Nyimbo

Majibu:

Orodha A

(i)

(ii)

(iii)

(iv)

(v)

Orodha B






SEHEMU B(Alama70)

Jibu maswali YOTE

3. Hamisi ni mwanafunzi wa Kidato cha pili ambaye anaamini njia pekee ya kuepuka migogoro kwenye jamii ni kutotumia kabisa lugha. Mfafanulie Hamisi matatizo matano ambayo yanaweza kutokea kama lugha haitakuwepo katika jamii ya binadamu.

4. Rafiki yako amepewa kazi na mwalimu wake wa Kiswahili, akusanye kazi mbalimbali za fasihi simulizi kutoka jamii za Kitanzania lakini ameshindwa na kusema hajui namna ya kuzipata. Kwa kutumia ujuzi wako wa somo la Kiswahili muelezee rafiki yako njia tano (5) za kukusanya kazi za fasihi hiyo.

5. (a) Taja alama tano (5) za uakifishi na kisha utoe dhima moja kwa kila alama

(b) Kamilisha mchoro ufuatao wa vipera vya ushairi.

image

6. Rafiki yako hakuwepo darasani wakati Mwalimu wa Kiswahili alipokuwa anafundisha mada ya uandishi wa barua pepe. Mbainishie rafiki yako vipengele vitano (5) vya msingi anavyopaswa kuvizingatia wakati wa kuandika ujumbe wa barua pepe.

7. Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamefanya uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi uwe rahisi. Taja njia tano (5) za kisasa za kuhifadhi fasihi hiyo na kwa kila njia toa faida moja.

8. Mzee Kimwaga ni fanani mahiri ambaye kila jioni hukaa na wajukuu zake na kuwatolea vitendawili. Jana amewapa vitendawili vitano lakini hakuna aliyeweza kuvitegua. Tumia utaalamu wako ulioupata kwenye somo la fasihi kuvitegua.

(i) Yeye anatuona, sisi hatumuoni.

(ii) Popote niendapo ananifuata

(iii) Nyumba yangu haina mlango

(iv) Kitu kidogo kimemtoa Mfalme kitini.

(v) Mzazi ana miguu bali mzaliwa hanayo

9. Soma kifungu cha habari kisha jibu maswali yanayofuata:

“Wanangu chukueni vigoda mketi niwausie ya dunia, maana ya jana sio ya leo na ya leo sio ya kesho. Zama zetu hatukupata kumuona mwanamke akivaa kaptura wala bukta, pia hatukupata kumuona mwanaume katoga masikio wala kusuka nywele. Leo ni jambo la kawaida kuona hayo, tena hayo ni madogo kuna makubwa zaidi ya hayo.

Ukistajaabu ya Musa utaona ya Firauni. Binti yangu angalia sana mwanaume atakayekuoa. Unaweza kudhani umeolewa na mwanaume, kumbe ni mke mwenzio, kwako mumeo huko nje ni mke wa mtu.

Nawe kijana wangu sikuachi pakavu, kuwa makini na mwanamke utakayemuoa. Usije kuoa mwanamke ambaye ndani kwako ni mkeo lakini nje ni mume wa mtu.

MASWALI:

(i) Pendekeza kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyoisoma kisichozidi maneno matatu 

(ii) Toa maana ya maneno yafuatayo:

  1. Vigoda
  2. Kutoga 

(iii) Andika methali iliyotumika katika habari hii 

(iv) Mwandishi anazungumzia nini katika wosia wake?

(v) Mwandishi ana maana gani anaposema “Kwako mumeo huko nje ni mke wa mtu”.

SEHEMU C (Alama 15)

Jibu swali la kumi (10) katika sehemu hii

10. Barua ifuatayo ni rasmi lakini ina makosa kadhaa, isome kwa makini kisha jibu maswali yanayofuata:

Mkuu wa Shule,

Shule ya Sekondari Ulongoni,

S.L.P. 2935,

Kigamboni – Dar es Salaam

1/7/2023

Shule ya Sekondari Ulongoni,

S.L.P. 2935,

Kigamboni – Dar es Salaam.

Salaamu mkuu wangu wa shule, shikamoo

Yah: Kushindwa kufika shule juzi

Rejea salamu zangu kwako. Mkuu wa shule mimi naumwa sana yaani naumwa sana, hapa nilipo nimechomwa sindano nne. Siwezi kula chakula na hata kutembea nashindwa. Shule naitaka na naipenda sana lakini naumwa sana. Hata mjomba Juma nilimwambia juzi kuwa naumwa sijui kama alikupa taarifa? Ni hayo tu mkuu wangu wa shule, wasalimie wanafunzi wenzangu wa kidato cha pili, lakini nikija usinichape bakora.

(a) Taja makosa matano (5) yaliyojitokeza katika barua hiyo.

(b) Irekebishe barua hiyo na uiandike upya na kwa usahihi.

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 45  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 45  

Namba ya mtahiniwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA. 
 MKOA WA KILIMANJARO. 
 MTIHANI WA UTAM1RIFU WA KII)ATO CHA PILL MKOA.

MSIMBO:021 KISWAHILI

MUDA :SAA 2:30 MEI 2023

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina seheme A,B, na C zenye jumla ya maswali kumi (10)
  2. Jibu maswali yote kwa umakini na ufasaha katika kila sehemu
  3. Andika namba yako ya mtihani kila ukurasa wa karatasi ya kujibia.
  4. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi
  5. Simu za mkononi haziruhusiwi.

NAMBA YA SWALI

ALAMA

SAHIHI YA MTAHINI

1.

2.

3.

4.

5.

6.

7.

8.

9.

10.

JUMLA



1. Katika vipengele (i) hadi (x) ,chagua herufi ya jibu sahii kisha andika herufi ya jibu hilo katika kisanduku ulichopewa.

(i) Dhima ya vigelegele katika utendaji wa Sanaa za maonesho ni ipi katika ya hizi zifuatazo?

  1. Kuonesha mbwembwe katika kazi ya Sanaa.
  2. Kuweka alama za mapigo ya'kimuziki katika Sanaa.
  3. Hadhira kukata shauri juu ya mwenendo wa kazi za Sanaa.
  4. Kuonesha upeo wa furaha na burudani katika kazi ya Sanaa.

(ii)Tanzu za fasihi simulizi zina vipera tofauti ni seti ipi inaoanisha vipera vya ushairi.?

  1. Ngojera ,Tenzi, Shairi.
  2. Misemo, shairi, ngonjera.
  3. Maghani , nahau, tenzi .
  4. Mafumbo, vigano na shairi.

iii. Njia ipi ya uhifadhi wa fasihi simulizi inayoweza kupokea mabadiliko kwa haraka zaidi kati ya hizi?

  1. Maandishi
  2. Kichwani
  3. Vinasa sauti
  4. komputa.

iv. Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo haina maana zaidi ya moja.?

  1. Kaka amefua nguo
  2. Nipe sahani ya kulia
  3. Suedi amenunua mbuzi
  4. Asha amempigia mpira.

v. Mofimu tegemezi ina tabia ya kuwa na kazi mbalimbali, ipi kati ya hizi ni kazi ya mofimu tegemezi ?

  1. Kuonesha maana ya maneno
  2. Kuonesha lugha za kigeni
  3. Kuonesha hali mbalimbali
  4. Kuonesha idadi ya maneno.

vi. Asha na Ashura walizozana na kuanza kujihizana haina yao .Unatikiri kwa lugha ya Kiswahiii majibizano hayo huitwaje?

  1. Dayolojia
  2. mahubiri
  3. Riwaya
  4. Hadithi

(vii) Pande mbili zanazohusika katika lugha ya maandishi ni zipi?

  1. Mwandishi na msikilizaji
  2. Mwandishi na mzungumzaji
  3. Msomaji na mwandishi.
  4. Msomaji na msimuliaji.

viii. Misimu hutumia njia mbalimbali katika kuunda maneno . Neno mataputapu limeundwa kwa kutumia njia gani ?.

  1. Kufupisha maneno
  2. Kutohoa katika lugha za kigeni.
  3. Kutumia tanakali sauti.
  4. Kutumia sitiari.

ix ...................... .ni sauti zinazotamkwa bila ya kuwepo kwa kizuizi katika mkondo wa hewa kutoka mapafuni kwenda nje

  1. Irabu
  2. Konsonanti
  3. Silabi
  4. Fonimu.

x. Neno vizuri katika sentensi linaweza kusimama kama aina tofautitofauti ya neno. Katika sentensi hii "Vizuri vyote vimewekwa kabatini"Vizuri ni aina gani ya neno?

  1. Kielezi
  2. Kivumishi
  3. Kiwakilishi
  4. Nomino

Majibu.

i

ii

iii

iv

v

vi

vii

viii

ix

x











2. Oanisha maana ya vipera vya fasihi simulizi katika safu A na dhana za fasihi simulizi zilizopo katika safu B, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.

SAFU A SAFU B

I.Ni hadithi zinazoelezea makosa au uovu wa watu fulani na kueleza maadili yanayofaa.

II. Hizi ni tungo zenye mpangilio maalumu wa maneno na mahadhi ya kupanda na kushuka .

III. Hizi ni hadithi husimulia kuhusu matukio ya kihistoria .

IV. Ni semi fupifupi zenye kueleza kwa muhtasari fikra au mafumbo mazito yanayotokana na uzoefu wa kijamii.

V. Haya ni majina ya kupanga ambayo baadhi ya watu hupewa na kuj ipatia kutokana na sifa.

  1. Lakabu
  2. Methali.
  3. Vigano.
  4. Nyimbo
  5. Tarihi.
  6. Takiriri
  7. Mizungu

Majibu.

Safu A

i

ii

iii

iv

v

Safu B






SEHEMU B (Alama 70 )

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

Soma kwa makini Habari hii kisha Jibu maswali yafuatayo.

Miaka mingi iliyopita katika Kijiji cha Halingumu, waliishi watu wengi maskini. Nyumba zao zilikuwa za miti na ziliezekwa kwa nyasi. Miti yote katika Kijiji hiki ilikatwa kwa uhitaji wa kuni. Watu hawa waliishi katika nyakati mbalimbali, ikiwemo shida na vipindi vichache vya furaha. Mzee Mweta na Mkewe Bi Sikitiko walikuwa miongoni wakazi wa Kijiji hicho.

Sikumoja mchana, wingu zito lilitanda angani. Ndege wa kila aina waliruka juu wakiwa wenye furaha wakipiga kelele na kuimba nyimbo kuashiria kwanza kunyesha kwa mvua.

Baada ya muda kupita, sauti ya ndege waliokuwa wametanda angani zilikuwa zikififia na kutoweka. Matone makubwa ya mvua yalikuwa tayari yakiigusa ardhi iliyokuwa na kiu cha kipindi kirefu na kumezwa harakaharaka. Maskini Bi Sikitiko ndiyo kwanza alikuwa akipiga hatua kutoka kisimani akiwa na ndoo ya maji kichwani. Mzee Mweta yeye alikuwa akikaribia kufika ilipokuwa nyumba yake iliyokuwa imeezekwa kwa nyasi, akitokea Kijiji jirani kutafuta vibarua.

Baada ya mvua kunyesha kwa muda wa dakika arobaini, ilipungua kwa kiasi. Mzee Mweta aliishika njia kwa haraka iii kwenda kujua hatma ya nyumba yake. Alipofika upenuni pake aliunyanyua Uso wake kwa uzuni. Aliyatuma macho yake kuumulika ukuta uliokuwa ukimalizia safari yake ya kwenda chini. Nyumba yake ya udongo haikuhimili vishindo vya mvua hiyo na mirindimo ya radi. Tayari siri ya chumba ikawa imefichuliwa. Mijusi na panya waliokuwa wamefanya maskani yao katika jumba hilo la matope walishindikana kwa aibu kila mmoja na uelekeo wake. Jumba lote liliporomoka na kutoa sauti kubwa, puuu!

Mzee Mweta alibaki mkimya, hayaamini macho yake. Alijaribu kufikiri ni wapi angejisitiri kipindi hicho cha masika yasiyo na adabu. Mke wake aliposikia kishindo kikubwa alihisi mambo yalikuwa yameharibika. Aliukaza mguu wake kwa haraka akiwa na ndoo kichwani na galoni lake la maji mkononi. Naye alitupia macho yake kwenye jumba lao na kuona yaliyotokea. Alishikwa na fadhaa akatoa siahi kwa nguvu. Alijihisi kunyong'onyea. Galoni lilimponyoka na ndoo ikaanguka na kupasuka, pwaa! Fahamu ilimhama, akajua akiba ya fedha yake aliyokuwa kaificha katika nyufa imepotea.

Kutokana na hamaniko lililowakuta, Bi na mumewe walipoteza fahamu. Wote walichukuliwa na wasamaria hadi hospitalini ambako walilazwa kwa ajili ya matibabu. Baada ya fahamu kuwarudia, kila mmoja alisimlia chanzo cha hofu yake. Wahudumu wa hospitali na wanasihi walimshauri. Bi Sikitiko kuacha kutunza pesa yake kwenye nyufa za matofali bali angezipeleka benki kwa usalama na faida Zaidi.

Mzee Mweta, yeye alielezwa jinsi ya kujenga nyumba bora. Alifundishwa mbinu bora ya kuzuia upepo mkali kwenye nyumba yake. Wataalamu walisisitiza akijenga nyumba inampasa kupanda miti ili kuzuia majanga yasababishwayo na upepo.

Wote kwa Pamoja walipopata nafuu na ushauri walirejea kwao. Mzee Mweta alijenga nyumba ya kisasa wakati Bi Sikitiko alikuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wanawake kijijini pale kwa njia ya benki na mitandao ya simu. Hakika Kijiji cha halingumu kiligeuka na kuwa cha watu wenye Fuhara.

Maswali.

a) Pendekeza kichwa cha Habari hii kisichozidi maneno matatu.

b) Andika maana ya maneno haya:

  1. Nyumba ya biskuti
  2. Chutama
  3. Maskini
  4. Fadhaa

c) Bainisha tamathali za semi zilizo ndani ya Habari hii.

d) Baada ya kusoma Habari tunapata fundisho gani.

e) Taja wahusika wakuu katika Habari uliyosoma.

4. Fafanua kazi za mofimu KI zilizokolezwa wino katika sentensi zifuatazo .

  1. Ukimuona atakueleza kila kitu
  2. Amepigana kiume
  3. Kitabu kizuri kimechanika
  4. Kijumba chao ni kidogo
  5. Anakitaka hikihiki chekundu

5. Kama ungekuwa unashiriki moja kwa moja mazungumzo yafuatayo yanayojitokeza katika mukutadha tofauti tofauti. Andika rejesta ya kila sentensi mbele ya sentensi husika.

  1. Wapendwa inabidi tumjue Mungu sana maana mshahara wa dhambi ni mauti . . . . . . . . . . . . . .
  2. Mbili asubuhi ,mbili mchana ,na mbili jioni . . . . . . . . . . . . . . . . .
  3. Kimara Ubungo Mbagala wahi twende wenye haraka tuondoke. . . . . . . . . . . . . . . . . . .
  4. Boko, Boko anakwenda na mpira anapiga pasi ndefu pale goooooooo! ! ! . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
  5. Mkia chapati tia pilipili kidogo tafadhali usisahu limao. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

6. Utata husababishwa na mambo mengi. Toa maana mbili katika maneno yafuatayo na weka mfano mmoja kwa kila maana.

  1. Kanga
  2. Ua
  3. Pamba
  4. Mbuzi
  5. Kata

7. Kwa kila methali uliyopewa onesha fundisho lake katika maisha ya kila siku.

  1. Usiache mbachao kwa msala upitao
  2. Mgaagaa na upwa hall wali mkavu
  3. Mwenda tezi na omo marejeo ngamani.
  4. Mchelea mwana kulia hulia yeye
  5. Fadhila mfanyie mbuzi mwanadamu atakuudhi

8. Fasihi simulizi huwa na sifa zinazoitofautisha na fasihi andishi.Thibitisha usemi huu kwa hoja tano huku ukizingatia sifa za fasihi simulizi.


Fasihi simulizi

Fasihi andishi

i.



ii.



iii.



iv.



v.

.


9. Katika lugha ya Kiswahili kuna aina mbalimbali za maneno.Tunga sentensi kwa kutumia vipashio vifuatavyo.

  1. N+Ts+T +E
  2. V+N+T+N
  3. W+V+Ts+T+E
  4. W+t +N
  5. E+T+N

SEHEMU C (Alama 15)

10. Mwandikie baba yako barua ambaye ni mkuu wa shule ya sekondari Kivukoni SLP 20 Singida kumuomba hela ya safari ya kutembelea mbuga za Wanyama. Jina lako liwe Masumbuko Likoko SLP 345 Mbeya .

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 39  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 39  

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI

MTIHANI WA UTAMIRIFU KIDATO CHA PILI

021 KISWAHILI

Jumatano 29 Juni 2022 Muda : Saa 2:20

MAELEKEZO:

1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10)

2. Jibu maswali yote kutoka katika kila sehemu

3. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi zilizoachwa wazi.

4. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi

5. Vifaa vyote vya mawasiliano havitakiwi katika chumba cha upimaji.

6. Andika Namba yako ya mtihani katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.

SEHEMU A: UFAHAMU (ALAMA 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika kisanduku ulichopewa.

i. Ipi ni seti sahihi ya vipera vya semi?

  1. Methali, mizungu na maghani 
  2. Misemo, mafumbo na vigano
  3. Mafumbo, soga na maghani 
  4. Nahau, vitendawili na mizungu 

ii. Dhima kuu ya misimu katika lugha ni ipi?

  1. Kuficha jambo kwa wasiohusika
  2. Kuongeza ukali wa maneno
  3. Kutambulisha aina za maneno 
  4. Kupatanisha maneno

iii. Njia ipi ya uhifadhi wa fasihi simulizi inayoweza kupokea mabadiliko kwa haraka kati ya hizi?

  1. Maandishi 
  2. Kichwa 
  3. Vinasa sauti 
  4. Kompyuta 

iv. Mashairi ya majibizano baina ya watu wawili au zaidi:

  1. Nyimbo 
  2. Ngonjera 
  3. Tenzi 
  4. Semi

v. Barua rasmi mara nyingi zinakuwa na anuani ngapi? 

  1. 2
  2. 3
  3. B na C ni sahihi 

vi. Mzizi wa neno anakula ni 

  1. Kul 
  2. Ul 
  3.  L 
  4. Ku

vii. Majibizano baina ya watu wawili au zaidi wanapozungumza ni

  1. Dayolojia 
  2. Mahubiri 
  3. Hotuba 
  4. Risala 

viii. Katika lugha ya Kiswahili kuna aina ngapi za vielezi

  1. Moja 
  2. Tatu 
  3. Vinne 
  4. Zaidi ya nne 

ix. Katika sababu zifuatazo ni ipi si sahihi kuhusu matumizi ya kamusi?

  1. Kujifunza lugha ya kigeni. 
  2. Kusanifisha maneno mapya
  3. Kujua maana ya maneno 
  4. Kujua tahajia za maneno

x. Tarihi ni?

  1. Aina ya semi 
  2. Aina ya hadithi
  3. Aina ya sanaa ya maonyesho 
  4. Aina ya riwaya

i

Ii

iii

iv

v

vi

vii

viii

ix

x











2. Oanisha maelezo yaliyopo fungu A na dhana zilizopo funguB kwa kuandika herufi ya jibu sahihi ili kukamilisha maana.

FUNGU A

FUNGU B

i. Mitindo tofauti ya lugha katika miktadha mbalimbali

ii. Upekee wa kundi la watu na shughuli inayofanyika

iii. Kupamba lugha kuficha ujumbe, kukuza lugha

iv. Kutwa mara tatu

v. Mheshimiwa hakimu

  1. Lugha ya hospitalini
  2. Mkazo
  3. Dhima za rejesta
  4. Lugha ya mahakamani
  5. Chanzo cha rejesta
  6. Misimu
  7. Rejesta


Fungu A

i

ii

iii


iv

V

Fungu B







 SEHEMU B: (ALAMA 70) SARUFI,

MAWASILIANO NA FASIHI

3. Eleza maana ya maneno yafuatayo:

a)Mzizi wa neno

b) Mofimu

c) Mnyambuliko

d) Kamusi

e)Kidahizo

4. Kwa ufupi eleza mambo yanayotofautisha lugha ya mazungumzo na maandishi.

Mazungumzo

Maandishi

i.


ii.


iii.


iv.


v.


5. Tungo zifuatazo zina maana zaidi ya moja. Toa maana mbili tu kwa kila tungo.

6. a) Amempigia nini.

b) Nimenunua mbuzi

c) Eda ameshinda shuleni.

d) Ukija njoo na nyanya

e) Nyumbani kwao kuna tembo.

7. Bainisha dhima za rejesta katika lugha ya Kiswahili

8. Fafanua vipera vya fasihi simulizi vifuatavyo:

a.Ngano

b. Vigano

c. Soga

d. Tarihi

e. Visasili

8. Toa maana ya semi zifuatazo:

a. Kujitia kitanzi

b. Kuwa kinyonga

c. Kumpaka mtu matope

d. Mla mbuzi hulipa ng’ombe

e. Ulimi wa pilipili

9. Tegua vitendawili vifuatavyo:

a. Nasuka mkeka lakini nalala chini

b. Kila aendapo huacha alama

c. Nikimpiga mwanangu watu hucheza

d. Anatembea na nyumba yake

e. Nyumba yangu ina nguzo moja

SEHEMU C: (ALAMA 15)

UANDISHI WA INSHA/ UTUNGAJI

10. Wewe ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Tegemeo, S.L.P. 130 DODOMA, una matatizo ya kiafya, hivyo unahitaji kwenda kutibiwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Andika barua kwa Mkuu wako wa Shule kuomba ruhusa ya siku mbili. Jina lako liwe Juhudi Sabuni.

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 20  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 20  

NAMBA YA MTAHINIWA  . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

JMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA

MTIHANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA PILI

021 KISWAHILI 

MUDA: MASAA 2:00 06, Juni, 2022

MAELEKEZO

1. Mtihani huu unasehemu A,B na C zenye jumla ya maswali kumi (10)

2. Jibu maswali yote

3. Andika jina lako katika kila ukurasa wa karatasi yako ya kujibia

4. .Majibu yote yaandikwe kwa usafi na kwa uwekevu.

KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU

NAMBA YA SWALI

ALAMA

SAINI YA MTAHINI

1

 

 

2

 

 

3

 

 

4

 

 

5

 

 

6

 

 

7

 

 

8

 

 

9

 

 

10

 

 

JUMLA

 

 

SEHEMU A (Alama 15)

1.Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi za kujibia ulizopewa

i.  ”Siri ya mtungi aijuaye kata” huu ni usemi ambao umeundwa na tamathali ya semi ambayo huvipa uwezo wa kibinadamu vitu ambavyo si viumbe hai. Je tamathari hiyo ni ipi kati ya hizi.

  1. Sitiari 
  2. Tashibia 
  3. Tashihisi 
  4. Takriri

ii.  Kipanya alipoulizwa swali la kutaja dhima tano za viambishi awali, alitoa hoja nne zilizo zahihi na hoja moja haikuwa shihi. Ibainishe hoja ya Kipanya ambayo haikuwa sahihi miongoni mwa hizi

  1. Kudokeza njeo za vitenzi 
  2. Kudokeza kauli mbalimbali za vitenzi
  3. Kudokeza nafsi katika vitenzi 
  4. Kuonesha ukanushi
  5. Kudokeza umoja na uwingi

iii.  Haule alichezesha vitamkwa vya neno LIMA likawa MALI, LAMI na IMLA. Je Haule alitumia maarifa ya tawi gani la sarufi kufanikisha mchezo huo?

  1. MOFOLOJIA 
  2. SINTAKSIA 
  3. SEMANTIKI 
  4. FONOLOJIA

iv.  Mwanafunzi mwenyewe hapendi kujisomea mara kwa mara ndio sababu kuu inayomfanya asiazime vitabu. Neno mwenyewe linapatikana kwenye aina gani ya kivumishi kati ya hizi;

  1. kivumishi cha cha sifa 
  2. kivumishi cha jina kwa jina 
  3. kivumishi cha pekee 
  4. kivumishi cha A-unganifu.

v. Samata amempigia mpira mwanae” kuna ukweli usiopingwa kwamba tungo iliyotajwa ina uvulivuli ndani yake. Je uvuluvuli huo umetokana na matumizi ya kauli gani miongoni mwa zifuatazo;

  1. Tendwa 
  2. Tendewa 
  3. Tendeana 
  4. Tendea

vi.  Baada ya mjadala mrefu kuhusu matawi manne ya sarufi, wanafunzi wa mkiu walisahau kisawe cha sintakisia . wasaidie kukibaini hapo chini.

  1. Sarufi maumbo 
  2. Sarufi miundo
  3. Sarufi matamshi 
  4. Sarufi maana

vii.  Kila changamoto hutatuliwa kulingana na uzito wake kwa kuipatia suluhu inayofaa. Je ipi ni suluhu ya utatata uliopo kwenye tungo isemayo “Baba amenunua mbuzi”

  1. Kutokutumia maneno yenye maana zaisi ya moja
  2. Kuzingatia alama za uandishi mfano nukta na mkato
  3. Kuzingatia mkazo katika matamshi
  4. Maneno yenye maana zaidi ya moja yafafanuliwe yatumikapo

viii.  Chukulia umeokota kikapu kimejaa vikaratasi vilivyoandikwa vipengere vya maudhui, na kuna kikaratasi kimoja tu, kimeandikwa kipengere cha fani. Je unadhani kikaatasi chenye kipengere cha fani kitakuwa na neno gani miongoni mwa haya yafuatayo;

  1. Ujumbe 
  2. Mandhari 
  3. Dhamira 
  4. Msimamo

ix.  Mzee Hashimu ni mvuvi maarufu ambaye hupenda kuimba nyimbo tamu za kujiliwaza awapo katika shughuli zake za uvuvi. Je nyimbo za mzee Hashimu kifasihi hufahamika kwa jina gani?

  1. Kimai 
  2. Tendi 
  3. Wawe 
  4. Kongozi

x.  “Mshua anaupiga mwingi” katika tungo hii neno anaupiga mwingi lililozuka hivi karibuni likimaannisha kitendo cha kufanya jambo vizuri zaidi linaweza kuingizwa kwenye aina gani ya misimu kati ya zifuatazo;

  1. Misimu ya kitarafa 
  2. Misimu zagao 
  3. Misimu ya kihuni 
  4. Misimu ya pekee

i.  

ii.  

iii.  

iv.  

v.  

vi.  

vii.  

viii.  

ix.  

x.  

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

2 .Oanisha dhana za maneno kutoka fungu A na maneno yaliyopo katika fungu B kwakuandika herufi ya  jibu sahihi katika visanduku.

FUNGU A (VIPINDI MBALIMBALI)

FUNGU B ( MISIMU ILIYOZUKA)

i. Kipindi cha azimio la Arusha 1967

ii. Kipindi cha njaa kali ya mwaka 1974 - 1975

iii. Kipindi cha kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi 1992 - 1995

iv Kipindi cha vita ya Kagera 1978 - 1979

v Kipindi cha ugumu wa maisha baada ya vita ya Kagera

  1. Nduli
  2. Disco
  3. Mataputapu
  4. Ngangari
  5. Ulanguzi
  6. Malapa
  7. Mchumia tumbo
  8. Fegi
  9. Unga wa yanga

FUNGU A

i

ii

iii

iv

v

FUNGU B






 SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. A,Tumia taaluma ya unyambuaji wa maneno ya Kiswahili kunominisha maneno yafuatayo (i) Iga ………………..

(ii) Tubu …………………

(iii) Refu …………………

(iv) Agiza …………………

(v) Lea …………………

B. Kamilisha jedwali lifuatalo kulingana na maelekezo uliyopewa .

MIFANO WA NOMINO

AINA YA NOMINO

i. Uraia


ii. Kabati


iii. Kucheza


iv. Wizara


v. Agosti




4. Unda vifupisho vya sesntensi zifuatazo kwa kuchunguza aina za maaneno yaliyotumika kukamilisha sentensi hizo. Tungo namba (i) imetolewa kama Mfano;

(i) Mtoto mchanga amelazwa kitandani = N+V+T+E

…………………………………………………………………………………………………………….

(ii) Wao walikuwa wanataka kusafiri leo =

…………………………………………………………………………………………………………….

(iii) Tai na mwewe si ndege wazuri =

……………………………………………………………………………………………………………

(iv) Babu anatembea polele =

…………………………………………………………………………………………………………….

(v) Aiseee! Mchezaji wetu hodari ameumia mguu. =

……………………………………………………………………………………………………………..

(vi) Njiwa ametua juu ya muembe =

……………………………………………………………………………………………………………

5.Ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha pili unayejianda kufanya mtihani wa Taifa mwaka huu, Onesha umahiri wako wa lugha kwa kufafanua dhana za istilahi zifuatazo na utoe mifano kuntu kwa kila dhana.

(i) Mawasiliano

…………………………………………………………………………………………………………............

............................................................................................................................................................................

(ii) Kidatu ………………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………………

(iii) Lafudhi

………………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………………

(iv) Kiimbo

………………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………………

(v) Mkazo ………………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………………

6. Ngoswe ni mwanafunzi mzembe aliyeshindwa kutaja dhima tano za rejesta katika lugha, ukiwa kama mwanafunzi hodari wa Kiswahili msaidie Ngoswe kwa kutoa hoja tano zenye mifano dhahiri.

(i)………………………………………………………………………………………………………………

(ii)……………………………………………………………………………………………………………

(iii)……………………………………………………………………………………………………………

(iv)……………………………………………………………………………………………………………

(v)………………………………………………………………………………………………………………

7. Mzee Fasihi ni mzazi mwenye watoto wawili, ambao ni Simulizi na Andishi.Mzee Fasihi ana wajukuu wanne kutoka kwa mwanae Simulizi ,ambao ni Hadithi,Semi,Ushairi na Maigizo. Fafanua vitukuu vitano vya Mzee Fasihi kutoka kwa mjukuu wake Hadithi.

(i) ……………………………………………………………………………………………………………

(ii) ……………………………………………………………………………………………………………

(iii)

……………………………………………………………………………………………………………

(iv)

…………………………………………………………………………………………………………….

(v) ……………………………………………………………………………………………………………

8.Fasihi simulizi ni sawa na mtoto mchanga anayebebwa kwa kutumia mbereko za aina mbalimbali,zikiwemo za kizamani na za kisasa, na kila mbereko huwa na utamu na ukakasi wake. Fafanua utamu na ukakasi kwa kila mbareko iliyotajwa hapo chini.

i. VINASA SAUTI

Utamu…………………………………………………………………………………………………

Ukakasi………………………………………………………………………………………………

ii. KANDA ZA VIDEO

Utamu…………………………………………………………………………………………………

Ukakasi………………………………………………………………………………………………

iii. KICHWA

Utamu…………………………………………………………………………………………………

Ukakasi………………………………………………………………………………………………

iv. MAANDISHI

Utamu…………………………………………………………………………………………………

Ukakasi………………………………………………………………………………………………

v. MTANDAO

Utamu…………………………………………………………………………………………………

Ukakasi………………………………………………………………………………………………

9 Tumia ujuzi ulioupata shuleni na uzoefu wa maisha ulionao, kuandika methali moja yenye maudhui yanayofaa kurejelea mazingira yaliyoelezwa hapo chini

(i) Wanafunzi walipuuza agizo la mwalimu kuhusu kushona vitabu vyote vyenye dariri za kuchanika majarada na hatimaye vitabu vyote vilichakaa vibaya kwa muda mfupi, na jana mwalimu amewaambia wanafuzi wote wenye vitabu chakavu wanunue vitabu vipya

……………………………………………………………………………………………………..

(ii) Watu walimcheka bwana Sanga alipokuwa akitembea kwa miguu akiuza viatu vichache mitaani, na sasa wanashangaa kumuona bwana Sanga akimiliki duka kubwa la viatu mjini

……………………………………………………………………………………………………..

(iii) Watoto wa mzee Sengo walifurahi kuwaona kuku wao wakipigana na kuumizana vibaya kwasababu waliamini kuku atakayezidiwa atachinjwa na kuwa kitoweo siku ile .

……………………………………………………………………………………………………..

(iv) Hamis aliposhindwa katika shindano la kuandika insha lililofanyika Njombe mjini, alijitetetea kwa wenzake kwamba ameshindwa kuandika vizuri kwasababu msimamizi wa shindano aliwalazimisha kuandikia peni za speedo ambazo yeye huwa hazipendi na hawezi kuandikia.

……………………………………………………………………………………………………..

(v) Mfalme Simba aliwaita wanyamapori wote na kuwasihi wasipendele kuiba nafaka za binadamu wakati wa mchana. Nyani hakuzingatia ushauri wa mfalme samba na akaendelea kuvunja mahindi ya binanadamu wakati wa mchana, mwishowe akapigwa risasi na mzee Matola.

…………………………………………………………………………………………………......

SEHEMU C (Alama 15)

10. Chukulia wewe ni nguli wa kutunga mashairi kutoka shule ya sekondari Mapambano S.L.P 54 59418 LUDEWA-NJOMBE, Umechaguliwa kwenda kushiriki kwenye shindano la utunzi wa mashairi yahusuyo sensa litakalofanyika mwezi Julai jijini Dodoma. Mwandikie barua baba yako ambaye ni mkuu wa shule kumuomba ruhusa ya siku saba kwaajili ya kwenda kushiriki shindano hilo. Jina lako liwe Imani Majaliwa

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 3  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 3  

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

BARAZA LA WAKUU WA SHULE ZA KIISLAMU TANZANIA  

MTIHANI WA UTAMILIFU WA SHULE ZA KIISLAMU KIDATO II  

021 KISWAHILI

MUDA: SAA 2:30 Alhamisi, 23 Septemba 2021 Mchana

Maelekezo

1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E.

2. Jibu maswali yote.

3. Fuata maelekezo ya kila swali.

4. Majibu yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa.

5. Majibu yote yaandikwe kwa wino wa bluu au mweusi

6. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

7. Andika Namba yako ya Mtihani upande wa juu kulia wa kila ukurasa wa karatasi yako.

KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU

NAMBA YA SWALI

ALAMA

SAINI YA MTAHINI

1



2



3



4



5



6



7



8



9



10



JUMLA



SAINI YA MHAKIKI


SEHEMU A: (Alama 15) UFAHAMU

1. Soma kwa makini shairi lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata:

Shime basi waungwana, Umoja kutekeleza,

Mabibi hadi Mabwana, harambe nguvu kukoza,

Mpaka wetu vijana, tusije tukalegeza,

Nchi inayopendeza, ni watu kusikilizana.

Watu wakishikamana, hata amani huwepo,

Mambo kukubaliana, ndipo waendeleapo, 

Viongozi pia kutuna, kazi yao inyookapo, 

Nchi inayopendeza, ni watu kusikilizana.

Kaditama kwelezana, hapo basi nanyamaza,

La zaidi sina tena, ni hayo niloeleza, 

Basi shime kuungana, usawa kutekeleza,

Nchi inayopendeza, ni watu kusikilizana.

Maswali:

(i) Pendekeza kichwa cha habari kisichozidi maneno matano.

(ii) Shairi hili linahusu nini?

(iii) Waungwana ni watu wa aina gani.

(iv) Nini maana ya kaditama?

(v) Kiitikio cha shiri hili ni kipi?

2. Fupisha shairi ulilosoma kwa maneno yasiyozidi arobaini (40).

SEHEMU B: (Alama 20)

SARUFI

3.(a) Tumia mzizi wa kitenzi – IMB – Kunyumbulisha maneno katika hali zifuatazo kwa kupigia mstari kinyumbulishi hicho kinachoonesha kazi (hali) hiyo.

(i) Hali ya urejeshi

(ii) Njeo

(iii) Hali ya ukanushi nafsi ya tatu umoja

(iv) Hali ya kutendwa

(v) Hali ya kutendeka

(b) Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo:

(i) Samia anasoma vizuri ____________________________________________

(ii) Vizuri vinaliwa na matajiri _______________________________________

(iii) Vyombo vizuri vimenunuliwa ______________________________________

(iv) Huyu ni mkorofi. _______________________________________________

(v) Baba na mama wanapendana sana ___________________________________

4. (a) (i) Nini maana ya mofimu?

(ii) Ubainishaji wa mofimu huzingatia mambo kadhaa. Taja mambo manne (4) yanayomwezesha mtumiaji wa lugha kubainisha mofimu.

(b) Mzee Kimbo alinunua kamusi na kumpatia binti yake aitwaye Fatma. Binti yule alipoifungua ndani ile Kamusi aliona picha na michoro mingi katika sehemu mbalimbali ya ile Kamusi. Akamuuliza baba yake, ‘Kwani hizi picha na michoro ina kazi gani? Mbona kama zinajaza tu nafasi na kuifanya Kamusi iwe kubwa na nzito? Inanipa kazi kuibeba!! Msaidie Mzee Kimbo kujibu swali hilo kwa kutoa hoja tano za kumuelewesha binti yake.

SEHEMU C: (Alama 20)

MAWASILIANO NA MATUMIZI YA LUGHA

5. (a) Nini maana ya lugha fasaha?

(b) Onesha madhara manne (04) yanayoweza kutokea endapo mtumiaji wa lugha hatatumia lugha fasaha.

6. Baini makosa katika sentensi zifuatazo kwa kupigia mstari, kisha ziandike vizuri kuepuka makosa hayo.

(a) Duka la madawa limefungwa.

(b) Chai imeingia nzi.

(c) Sisi wote tulikusanyika uwanjani.

(d) Nyinyi mnapenda kula matunda?

(e) Hakuna mtu yoyote aliyechelewa kufika.

SEHEMU D: (Alama 30)

FASIHI KWA UJUMLA

7. Tungo zifuatazo zinafanana vipera mbalimbali vya tanzu za fasihi simulizi. Baini vipera hivyo katika kila tungo zifuatazo:

(a) Kuku wangu katagia mibani _____________________________________________

(b) Aso hili ana lile _______________________________________________________

(c) Nitasikiliza nikusikie kukusikia nitasikia kwa kusikia sauti yako ____________________________________________

(d) Mchuma janga hula na wa kwao __________________________________________________

(e) Papai limevia nyumbani lakini siwezi kulila ________________________________

8. Baadhi ya watu hudai kuwa utungaji wa majigambo ni mgumu sana lakini kutunga majigambo si jambo gumu asilani.

Thibitisha kauli hii kwa kuandika kanuni tano (5) za kuzingatia katika uandishi wa majigambo.

9. Wewe ni mwanafunzi wa Kidato cha Pili ambaye una rafiki wa Kidato cha kwanza. Rafiki yako amekuomba umfafanulie maana ya maneno yafuatayo ili aweze kuelewa zaidi, kwani darasani hakuelewa vizuri. Msaidie rafiki yako kwa kumfafanulia maneno yafuatayo:

(i) Vichekesho 

(ii) Mtindo

(iii) Lakabu

(iv)Soga

(v) Dhamira

SEHEMU E: (Alama 15) 

UANDISHI/UTUNGAJI

10. Wewe ni mwanafunzi wa kidato cha Pili, ukiwa likizo kijijini kwenu Mafyati kilichopo Wilaya ya Nachingwea S.L.P. 99 Nachingwea, serikali ya kijiji imeandaa sherehe ya makaribisho ya mwenge. Katika sherehe hiyo miongoni mwa wanaotarajiwa kualikwa ni pamoja na Mkuu wa Mkoa. Kwa niaba ya serikali ya kijiji, Andika barua ya kumualika kiongozi huyo katika sherehe hiyo. Anuani ya Mkuu wa Mkoa ni S.L.P. 602, Lindi. Jina lako liwe HALIM SAID au HALIMA SAID.

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 10  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 10  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256