OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI
MTIHANI WA UTAMIRIFU KIDATO CHA PILI
021 KISWAHILI
Jumatano 29 Juni 2022 Muda : Saa 2:20
MAELEKEZO:
1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10)
2. Jibu maswali yote kutoka katika kila sehemu
3. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi zilizoachwa wazi.
4. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi
5. Vifaa vyote vya mawasiliano havitakiwi katika chumba cha upimaji.
6. Andika Namba yako ya mtihani katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.
SEHEMU A: UFAHAMU (ALAMA 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika kisanduku ulichopewa.
i. Ipi ni seti sahihi ya vipera vya semi?
ii. Dhima kuu ya misimu katika lugha ni ipi?
iii. Njia ipi ya uhifadhi wa fasihi simulizi inayoweza kupokea mabadiliko kwa haraka kati ya hizi?
iv. Mashairi ya majibizano baina ya watu wawili au zaidi:
v. Barua rasmi mara nyingi zinakuwa na anuani ngapi?
vi. Mzizi wa neno anakula ni
vii. Majibizano baina ya watu wawili au zaidi wanapozungumza ni
viii. Katika lugha ya Kiswahili kuna aina ngapi za vielezi
ix. Katika sababu zifuatazo ni ipi si sahihi kuhusu matumizi ya kamusi?
x. Tarihi ni?
i | Ii | iii | iv | v | vi | vii | viii | ix | x |
| | | | | | | | | |
2. Oanisha maelezo yaliyopo fungu A na dhana zilizopo funguB kwa kuandika herufi ya jibu sahihi ili kukamilisha maana.
FUNGU A | FUNGU B | |
i. Mitindo tofauti ya lugha katika miktadha mbalimbali ii. Upekee wa kundi la watu na shughuli inayofanyika iii. Kupamba lugha kuficha ujumbe, kukuza lugha iv. Kutwa mara tatu v. Mheshimiwa hakimu |
|
Fungu A | i | ii | iii | | iv | V |
Fungu B | | | | | | |
SEHEMU B: (ALAMA 70) SARUFI,
MAWASILIANO NA FASIHI
3. Eleza maana ya maneno yafuatayo:
a)Mzizi wa neno
b) Mofimu
c) Mnyambuliko
d) Kamusi
e)Kidahizo
4. Kwa ufupi eleza mambo yanayotofautisha lugha ya mazungumzo na maandishi.
Mazungumzo | Maandishi |
i. | |
ii. | |
iii. | |
iv. | |
v. | |
5. Tungo zifuatazo zina maana zaidi ya moja. Toa maana mbili tu kwa kila tungo.
6. a) Amempigia nini.
b) Nimenunua mbuzi
c) Eda ameshinda shuleni.
d) Ukija njoo na nyanya
e) Nyumbani kwao kuna tembo.
7. Bainisha dhima za rejesta katika lugha ya Kiswahili
8. Fafanua vipera vya fasihi simulizi vifuatavyo:
a.Ngano
b. Vigano
c. Soga
d. Tarihi
e. Visasili
8. Toa maana ya semi zifuatazo:
a. Kujitia kitanzi
b. Kuwa kinyonga
c. Kumpaka mtu matope
d. Mla mbuzi hulipa ng’ombe
e. Ulimi wa pilipili
9. Tegua vitendawili vifuatavyo:
a. Nasuka mkeka lakini nalala chini
b. Kila aendapo huacha alama
c. Nikimpiga mwanangu watu hucheza
d. Anatembea na nyumba yake
e. Nyumba yangu ina nguzo moja
SEHEMU C: (ALAMA 15)
UANDISHI WA INSHA/ UTUNGAJI
10. Wewe ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Tegemeo, S.L.P. 130 DODOMA, una matatizo ya kiafya, hivyo unahitaji kwenda kutibiwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Andika barua kwa Mkuu wako wa Shule kuomba ruhusa ya siku mbili. Jina lako liwe Juhudi Sabuni.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM TWO KISWAHILI REGIONAL SERIES-20 YEAR-2022
NAMBA YA MTAHINIWA . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
JMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA
MTIHANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA PILI
021 KISWAHILI
MUDA: MASAA 2:00 06, Juni, 2022
MAELEKEZO
1. Mtihani huu unasehemu A,B na C zenye jumla ya maswali kumi (10)
2. Jibu maswali yote
3. Andika jina lako katika kila ukurasa wa karatasi yako ya kujibia
4. .Majibu yote yaandikwe kwa usafi na kwa uwekevu.
KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU | ||
NAMBA YA SWALI | ALAMA | SAINI YA MTAHINI |
1 |
|
|
2 |
|
|
3 |
|
|
4 |
|
|
5 |
|
|
6 |
|
|
7 |
|
|
8 |
|
|
9 |
|
|
10 |
|
|
JUMLA |
|
|
SEHEMU A (Alama 15)
1.Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi za kujibia ulizopewa
i. ”Siri ya mtungi aijuaye kata” huu ni usemi ambao umeundwa na tamathali ya semi ambayo huvipa uwezo wa kibinadamu vitu ambavyo si viumbe hai. Je tamathari hiyo ni ipi kati ya hizi.
ii. Kipanya alipoulizwa swali la kutaja dhima tano za viambishi awali, alitoa hoja nne zilizo zahihi na hoja moja haikuwa shihi. Ibainishe hoja ya Kipanya ambayo haikuwa sahihi miongoni mwa hizi
iii. Haule alichezesha vitamkwa vya neno LIMA likawa MALI, LAMI na IMLA. Je Haule alitumia maarifa ya tawi gani la sarufi kufanikisha mchezo huo?
iv. Mwanafunzi mwenyewe hapendi kujisomea mara kwa mara ndio sababu kuu inayomfanya asiazime vitabu. Neno mwenyewe linapatikana kwenye aina gani ya kivumishi kati ya hizi;
v. “Samata amempigia mpira mwanae” kuna ukweli usiopingwa kwamba tungo iliyotajwa ina uvulivuli ndani yake. Je uvuluvuli huo umetokana na matumizi ya kauli gani miongoni mwa zifuatazo;
vi. Baada ya mjadala mrefu kuhusu matawi manne ya sarufi, wanafunzi wa mkiu walisahau kisawe cha sintakisia . wasaidie kukibaini hapo chini.
vii. Kila changamoto hutatuliwa kulingana na uzito wake kwa kuipatia suluhu inayofaa. Je ipi ni suluhu ya utatata uliopo kwenye tungo isemayo “Baba amenunua mbuzi”
viii. Chukulia umeokota kikapu kimejaa vikaratasi vilivyoandikwa vipengere vya maudhui, na kuna kikaratasi kimoja tu, kimeandikwa kipengere cha fani. Je unadhani kikaatasi chenye kipengere cha fani kitakuwa na neno gani miongoni mwa haya yafuatayo;
ix. Mzee Hashimu ni mvuvi maarufu ambaye hupenda kuimba nyimbo tamu za kujiliwaza awapo katika shughuli zake za uvuvi. Je nyimbo za mzee Hashimu kifasihi hufahamika kwa jina gani?
x. “Mshua anaupiga mwingi” katika tungo hii neno anaupiga mwingi lililozuka hivi karibuni likimaannisha kitendo cha kufanya jambo vizuri zaidi linaweza kuingizwa kwenye aina gani ya misimu kati ya zifuatazo;
i. | ii. | iii. | iv. | v. | vi. | vii. | viii. | ix. | x. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
2 .Oanisha dhana za maneno kutoka fungu A na maneno yaliyopo katika fungu B kwakuandika herufi ya jibu sahihi katika visanduku.
FUNGU A (VIPINDI MBALIMBALI) | FUNGU B ( MISIMU ILIYOZUKA) |
i. Kipindi cha azimio la Arusha 1967 ii. Kipindi cha njaa kali ya mwaka 1974 - 1975 iii. Kipindi cha kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi 1992 - 1995 iv Kipindi cha vita ya Kagera 1978 - 1979 v Kipindi cha ugumu wa maisha baada ya vita ya Kagera |
|
FUNGU A | i | ii | iii | iv | v |
FUNGU B |
SEHEMU B (Alama 70)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
3. A,Tumia taaluma ya unyambuaji wa maneno ya Kiswahili kunominisha maneno yafuatayo (i) Iga ………………..
(ii) Tubu …………………
(iii) Refu …………………
(iv) Agiza …………………
(v) Lea …………………
B. Kamilisha jedwali lifuatalo kulingana na maelekezo uliyopewa .
MIFANO WA NOMINO | AINA YA NOMINO |
i. Uraia | |
ii. Kabati | |
iii. Kucheza | |
iv. Wizara | |
v. Agosti | |
4. Unda vifupisho vya sesntensi zifuatazo kwa kuchunguza aina za maaneno yaliyotumika kukamilisha sentensi hizo. Tungo namba (i) imetolewa kama Mfano;
(i) Mtoto mchanga amelazwa kitandani = N+V+T+E
…………………………………………………………………………………………………………….
(ii) Wao walikuwa wanataka kusafiri leo =
…………………………………………………………………………………………………………….
(iii) Tai na mwewe si ndege wazuri =
……………………………………………………………………………………………………………
(iv) Babu anatembea polele =
…………………………………………………………………………………………………………….
(v) Aiseee! Mchezaji wetu hodari ameumia mguu. =
……………………………………………………………………………………………………………..
(vi) Njiwa ametua juu ya muembe =
……………………………………………………………………………………………………………
5.Ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha pili unayejianda kufanya mtihani wa Taifa mwaka huu, Onesha umahiri wako wa lugha kwa kufafanua dhana za istilahi zifuatazo na utoe mifano kuntu kwa kila dhana.
(i) Mawasiliano
…………………………………………………………………………………………………………............
............................................................................................................................................................................
(ii) Kidatu ………………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………………
(iii) Lafudhi
………………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………………
(iv) Kiimbo
………………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………………
(v) Mkazo ………………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………………
6. Ngoswe ni mwanafunzi mzembe aliyeshindwa kutaja dhima tano za rejesta katika lugha, ukiwa kama mwanafunzi hodari wa Kiswahili msaidie Ngoswe kwa kutoa hoja tano zenye mifano dhahiri.
(i)………………………………………………………………………………………………………………
(ii)……………………………………………………………………………………………………………
(iii)……………………………………………………………………………………………………………
(iv)……………………………………………………………………………………………………………
(v)………………………………………………………………………………………………………………
7. Mzee Fasihi ni mzazi mwenye watoto wawili, ambao ni Simulizi na Andishi.Mzee Fasihi ana wajukuu wanne kutoka kwa mwanae Simulizi ,ambao ni Hadithi,Semi,Ushairi na Maigizo. Fafanua vitukuu vitano vya Mzee Fasihi kutoka kwa mjukuu wake Hadithi.
(i) ……………………………………………………………………………………………………………
(ii) ……………………………………………………………………………………………………………
(iii)
……………………………………………………………………………………………………………
(iv)
…………………………………………………………………………………………………………….
(v) ……………………………………………………………………………………………………………
8.Fasihi simulizi ni sawa na mtoto mchanga anayebebwa kwa kutumia mbereko za aina mbalimbali,zikiwemo za kizamani na za kisasa, na kila mbereko huwa na utamu na ukakasi wake. Fafanua utamu na ukakasi kwa kila mbareko iliyotajwa hapo chini.
i. VINASA SAUTI
Utamu…………………………………………………………………………………………………
Ukakasi………………………………………………………………………………………………
ii. KANDA ZA VIDEO
Utamu…………………………………………………………………………………………………
Ukakasi………………………………………………………………………………………………
iii. KICHWA
Utamu…………………………………………………………………………………………………
Ukakasi………………………………………………………………………………………………
iv. MAANDISHI
Utamu…………………………………………………………………………………………………
Ukakasi………………………………………………………………………………………………
v. MTANDAO
Utamu…………………………………………………………………………………………………
Ukakasi………………………………………………………………………………………………
9 Tumia ujuzi ulioupata shuleni na uzoefu wa maisha ulionao, kuandika methali moja yenye maudhui yanayofaa kurejelea mazingira yaliyoelezwa hapo chini
(i) Wanafunzi walipuuza agizo la mwalimu kuhusu kushona vitabu vyote vyenye dariri za kuchanika majarada na hatimaye vitabu vyote vilichakaa vibaya kwa muda mfupi, na jana mwalimu amewaambia wanafuzi wote wenye vitabu chakavu wanunue vitabu vipya
……………………………………………………………………………………………………..
(ii) Watu walimcheka bwana Sanga alipokuwa akitembea kwa miguu akiuza viatu vichache mitaani, na sasa wanashangaa kumuona bwana Sanga akimiliki duka kubwa la viatu mjini
……………………………………………………………………………………………………..
(iii) Watoto wa mzee Sengo walifurahi kuwaona kuku wao wakipigana na kuumizana vibaya kwasababu waliamini kuku atakayezidiwa atachinjwa na kuwa kitoweo siku ile .
……………………………………………………………………………………………………..
(iv) Hamis aliposhindwa katika shindano la kuandika insha lililofanyika Njombe mjini, alijitetetea kwa wenzake kwamba ameshindwa kuandika vizuri kwasababu msimamizi wa shindano aliwalazimisha kuandikia peni za speedo ambazo yeye huwa hazipendi na hawezi kuandikia.
……………………………………………………………………………………………………..
(v) Mfalme Simba aliwaita wanyamapori wote na kuwasihi wasipendele kuiba nafaka za binadamu wakati wa mchana. Nyani hakuzingatia ushauri wa mfalme samba na akaendelea kuvunja mahindi ya binanadamu wakati wa mchana, mwishowe akapigwa risasi na mzee Matola.
…………………………………………………………………………………………………......
SEHEMU C (Alama 15)
10. Chukulia wewe ni nguli wa kutunga mashairi kutoka shule ya sekondari Mapambano S.L.P 54 59418 LUDEWA-NJOMBE, Umechaguliwa kwenda kushiriki kwenye shindano la utunzi wa mashairi yahusuyo sensa litakalofanyika mwezi Julai jijini Dodoma. Mwandikie barua baba yako ambaye ni mkuu wa shule kumuomba ruhusa ya siku saba kwaajili ya kwenda kushiriki shindano hilo. Jina lako liwe Imani Majaliwa
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM TWO KISWAHILI REGIONAL SERIES-3 YEAR-2022
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
BARAZA LA WAKUU WA SHULE ZA KIISLAMU TANZANIA
MTIHANI WA UTAMILIFU WA SHULE ZA KIISLAMU KIDATO II
021 KISWAHILI
MUDA: SAA 2:30 Alhamisi, 23 Septemba 2021 Mchana
Maelekezo
1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E.
2. Jibu maswali yote.
3. Fuata maelekezo ya kila swali.
4. Majibu yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa.
5. Majibu yote yaandikwe kwa wino wa bluu au mweusi
6. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.
7. Andika Namba yako ya Mtihani upande wa juu kulia wa kila ukurasa wa karatasi yako.
KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU | ||
NAMBA YA SWALI | ALAMA | SAINI YA MTAHINI |
1 | | |
2 | | |
3 | | |
4 | | |
5 | | |
6 | | |
7 | | |
8 | | |
9 | | |
10 | | |
JUMLA | | |
SAINI YA MHAKIKI | |
SEHEMU A: (Alama 15) UFAHAMU
1. Soma kwa makini shairi lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata:
Shime basi waungwana, Umoja kutekeleza,
Mabibi hadi Mabwana, harambe nguvu kukoza,
Mpaka wetu vijana, tusije tukalegeza,
Nchi inayopendeza, ni watu kusikilizana.
Watu wakishikamana, hata amani huwepo,
Mambo kukubaliana, ndipo waendeleapo,
Viongozi pia kutuna, kazi yao inyookapo,
Nchi inayopendeza, ni watu kusikilizana.
Kaditama kwelezana, hapo basi nanyamaza,
La zaidi sina tena, ni hayo niloeleza,
Basi shime kuungana, usawa kutekeleza,
Nchi inayopendeza, ni watu kusikilizana.
Maswali:
(i) Pendekeza kichwa cha habari kisichozidi maneno matano.
(ii) Shairi hili linahusu nini?
(iii) Waungwana ni watu wa aina gani.
(iv) Nini maana ya kaditama?
(v) Kiitikio cha shiri hili ni kipi?
2. Fupisha shairi ulilosoma kwa maneno yasiyozidi arobaini (40).
SEHEMU B: (Alama 20)
SARUFI
3.(a) Tumia mzizi wa kitenzi – IMB – Kunyumbulisha maneno katika hali zifuatazo kwa kupigia mstari kinyumbulishi hicho kinachoonesha kazi (hali) hiyo.
(i) Hali ya urejeshi
(ii) Njeo
(iii) Hali ya ukanushi nafsi ya tatu umoja
(iv) Hali ya kutendwa
(v) Hali ya kutendeka
(b) Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo:
(i) Samia anasoma vizuri ____________________________________________
(ii) Vizuri vinaliwa na matajiri _______________________________________
(iii) Vyombo vizuri vimenunuliwa ______________________________________
(iv) Huyu ni mkorofi. _______________________________________________
(v) Baba na mama wanapendana sana ___________________________________
4. (a) (i) Nini maana ya mofimu?
(ii) Ubainishaji wa mofimu huzingatia mambo kadhaa. Taja mambo manne (4) yanayomwezesha mtumiaji wa lugha kubainisha mofimu.
(b) Mzee Kimbo alinunua kamusi na kumpatia binti yake aitwaye Fatma. Binti yule alipoifungua ndani ile Kamusi aliona picha na michoro mingi katika sehemu mbalimbali ya ile Kamusi. Akamuuliza baba yake, ‘Kwani hizi picha na michoro ina kazi gani? Mbona kama zinajaza tu nafasi na kuifanya Kamusi iwe kubwa na nzito? Inanipa kazi kuibeba!! Msaidie Mzee Kimbo kujibu swali hilo kwa kutoa hoja tano za kumuelewesha binti yake.
SEHEMU C: (Alama 20)
MAWASILIANO NA MATUMIZI YA LUGHA
5. (a) Nini maana ya lugha fasaha?
(b) Onesha madhara manne (04) yanayoweza kutokea endapo mtumiaji wa lugha hatatumia lugha fasaha.
6. Baini makosa katika sentensi zifuatazo kwa kupigia mstari, kisha ziandike vizuri kuepuka makosa hayo.
(a) Duka la madawa limefungwa.
(b) Chai imeingia nzi.
(c) Sisi wote tulikusanyika uwanjani.
(d) Nyinyi mnapenda kula matunda?
(e) Hakuna mtu yoyote aliyechelewa kufika.
SEHEMU D: (Alama 30)
FASIHI KWA UJUMLA
7. Tungo zifuatazo zinafanana vipera mbalimbali vya tanzu za fasihi simulizi. Baini vipera hivyo katika kila tungo zifuatazo:
(a) Kuku wangu katagia mibani _____________________________________________
(b) Aso hili ana lile _______________________________________________________
(c) Nitasikiliza nikusikie kukusikia nitasikia kwa kusikia sauti yako ____________________________________________
(d) Mchuma janga hula na wa kwao __________________________________________________
(e) Papai limevia nyumbani lakini siwezi kulila ________________________________
8. Baadhi ya watu hudai kuwa utungaji wa majigambo ni mgumu sana lakini kutunga majigambo si jambo gumu asilani.
Thibitisha kauli hii kwa kuandika kanuni tano (5) za kuzingatia katika uandishi wa majigambo.
9. Wewe ni mwanafunzi wa Kidato cha Pili ambaye una rafiki wa Kidato cha kwanza. Rafiki yako amekuomba umfafanulie maana ya maneno yafuatayo ili aweze kuelewa zaidi, kwani darasani hakuelewa vizuri. Msaidie rafiki yako kwa kumfafanulia maneno yafuatayo:
(i) Vichekesho
(ii) Mtindo
(iii) Lakabu
(iv)Soga
(v) Dhamira
SEHEMU E: (Alama 15)
UANDISHI/UTUNGAJI
10. Wewe ni mwanafunzi wa kidato cha Pili, ukiwa likizo kijijini kwenu Mafyati kilichopo Wilaya ya Nachingwea S.L.P. 99 Nachingwea, serikali ya kijiji imeandaa sherehe ya makaribisho ya mwenge. Katika sherehe hiyo miongoni mwa wanaotarajiwa kualikwa ni pamoja na Mkuu wa Mkoa. Kwa niaba ya serikali ya kijiji, Andika barua ya kumualika kiongozi huyo katika sherehe hiyo. Anuani ya Mkuu wa Mkoa ni S.L.P. 602, Lindi. Jina lako liwe HALIM SAID au HALIMA SAID.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM TWO KISWAHILI REGIONAL SERIES-10 YEAR-2021