Namba ya upimaji ya Mwanafunzi. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
Bismillaahir rahmaanir rahiim
OFISI YA RAIS OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUFIJI
MTIHANI WA UMAHIRI KIDATO CHA PILI
015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
MUDA: SAA 2:30 MWAKA: 2025
Maelekezo
KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU | ||
NAMBA YA MASWALI | ALAMA | SAHIHI YA MSAHIHISHAJI |
1. | ||
2. | ||
3. | ||
4. | ||
5. | ||
6. | ||
7. | ||
8. | ||
9. | ||
10. | ||
TOTAL | ||
SAHIHI YA MHAKIKI |
SEHEMU ‘A’ (Alama 15 %)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
1. Katika kipengele (i) – (x) Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake katika sehemu iliyowazi.
(i) Je utawezaje kumtambua muislamu aliyeelimika?
(ii) Wana wa chuoni wanatuambia Tawhid maana yake ni kumpwekesha Allh (sw). ni Tawhid ipi inaohusika na kumpwekesha Allah katika uungu wake?
(iii) Muandaaji wa Sanda anapaswa kuzingatia mambo gani katika uandaaji wa Sanda ya Mwanamke?
(iv) Pamoja na kutoonekana Allah wala kudirikika katika milango mikuu ya fahamu ila huwasiliana na waja wake kupitia njia zifuatazo:
(v) Fafanua sunnah katika elimu ya hadithi lina maana gani?
(vi) Jozi ipi klati yua zifuatazo inawakilisha nguzo za funga?
(vii) Kwa mujibu wa uislamu kuna aina kuu mbili za Dini “dini ya Allah na Dini za watu, fafanua aina tatu za Dini za watu.
(viii) Changanua mkanganyiko ufuatao;
(ix) Allah (sw) alishawahi kuangamiza baadhi ya familia za mitume wake, ni mtume gani aliyeangamiziwa mke na mtoto wake.
(x) Mambo ya lazima kufanyiwa maiti wa kiislam bainisha ni katika faradhi gani?
2. Oanisha maneno kutoka orodha “B” na sentensi kutoka orodha “A” kisha jaza herufi yake kwenye jedwali hapo chini.
A | B |
(i) Huswaliwa qabla na baada ya swala za faradhi. (ii) Huswaliwa kwaajili ya kuomba mvua. (iii) Huswaliwa muda wowote mara tu uingiapo msikitini. (iv) Huswaliwa pindi lipatwapo jua au mwezi. (v) Huswaliwa rakaa mbilimbili hadi nane usiku wa manane. |
|
i | I | iii | iv | V |
. |
SEHEMU “B” (ALAMA 70)
Jibu maswali yote kwa ufupi katika sehemu hii
3. Fafanua njia kuu tano zinazomuwezesha mwanadamu kumtambua Mola wake
4. Makafiri hawaamini kama kuna maisha baada ya kufa. Fafanua hatua tano(5) anazopitia mwanaadamu kuyaendea maisha hayo.
5. a) Waislamu wengi na hata wasiokuwa waislamu(makafiri) hawaelewi maana halisi ya neno dini, wewe ukiwa kama mjuzi katika masuala haya, toa maana yake halisi kwa mitazamo yote miwili.
5 b) Ainisha sababu tatu za kwanini mwanadamu hawezi kusibi bila ya Dini.
6. (a) Waislamu wangi wanadhani kuwa Ibada ni kuswali, kufunga, kutoa zaka na kuhiji, wakati si sahihi. Wewe ukiwa mwana wa zuoni ifafanulie jamii maana yake halisi kilugha na kisheria;
(i) Kilugha
(ii) Kisheria
(b) Kuna mlevi mmoja maeneo ya Tandale alikuwa akiropoka kuwa hakuna lengo lolote la kuumbwa mwanaadamu ulimwenguni na vilivyomo. Wewe kama muislamu unayejitambua hebu fafanua lengo la kuumbwa kila kimoja
7. (a) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo katiba ya kuendeshea nchi, na uislamu una sheria zake. Ni ipi misingi inayotumika kuendeshea sheria mbalimbali za kiislamu
(b) Kuna mkanganyiko mkubwa kati ya Sharia na Fiq-hi, toa maelezo yatakayoondoa mkanganyiko huo.
8. Mtume (saw) na maswahaba wake walitumia njia madhubuti na makini katika kuilinda na kuihifadhi Qur-an, na ndio maana makafiri wanajaribu kuikejeli na kuichafua lakini wanashindwa, toa njia tano (5) zilizotumika kuilinda na kuihifadhi Qur-an.
9. Kuna waislamu wanadai kuwa sunnah hazina umuhimu na nafasi yoyote katika uislamu, kwa kutumia nukta tano (5), fafanua umuhimu na nafasi yake katika uislamu.
SEHEMU “C” (ALAMA 15)
Jibu swali lifuatalo katika mfumo wa insha.
10. Wanafunzi wa kidato cha kwanza hawana elimu juu ya mambo ambayo wakiyafanya swaumu zao zitakuwa zimeharibika. Wewe kama mjuzi wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu waelimishe wanafunzi hao juu ya mambo yanayobatilisha funga (Hoja tano)
FORM TWO EDK EXAM SERIES 128
FORM TWO EDK EXAM SERIES 128