FORM THREE KISWAHILI EXAMS SERIES

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

KISWAHILI KIDATO CHA TATU

MUDA: SAA 3:00        MAY  2022

 

MAELEKEZO

 1.                Karatasi hii ina sehemu A, B, na C, zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12)
 2.                Jibu maswali yote kama ilivyoelekezwa katika kila sehemu. A na B maswali matatu kutoka sehemu C
 3.                Sehemu A ina alama kumi natano (15), sehemu B alama arobaini (40) na sehemu C ina alama arobaini na tano (45)
 4.                Zingatia mwandiko mzuri, Mpangilio na usahihi wa majibu yako.
 5.                Majibu yote yaandikwe kwenye karatasi za kujibia.

 

 

SEHEMU A

Jibu maswali yote katika sehemu hii

 1.                Chagua herufi ya jibu sahihi katika kipengtele cha (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi ya kujibia
 1. Lugha huweza kuchukua maneno kutoka katika lugha za asili, baini maneno hayo katika orodha ifuatayo;
 1.              Bendera na meza
 2.               Bunge na shule
 3.               Hela na mtutu
 4.              Godoro na sharubati
 5.               Kitivo na ngeli
 1. Ipi ni aina ya tungo ambayo muudo wake una kitenzi ndani yake? Kitenzi hiko huweza kutoa taarifa kamili au isiyo kamili.
 1.              Kishazi
 2.               Kirai
 3.               Shamirisho
 4.              Yambwa
 5.               Sentensi
 1. Katika neon wanaimba, kuna viambishi vingapi?
 1.              4
 2.               8
 3.               3
 4.              5
 5.               6
 1. Ni mchakato wa uundaji wa maneno kwa kupachika viambishi kabla na baada ya mzizi wa neno.
 1.              Utohoaji
 2.               Uambishaji
 3.               Mnyambuliko
 4.              Uambatishaji
 5.               Urudufishaji
 1. Kitomeo huweza kuwa na taarifa kadha wa kadha. Je ipi kati ya zifuatazo si taarifa sahihi inayopatikana katika kitomeo?
 1.              Wingi wa neon
 2.               Aina ya neno
 3.               Mfano wa matumizi
 4.              Asili ya neno
 5.               Mnyumbuliko wa maneno
 1. Katika maneno choka na chako ni mbinu gani imetumika katika kuunda maneni hayo?
 1.              Uradidi
 2.               Uambishaji
 3.               Uhulutishaji
 4.              Mpangilio tofauti wa vitamkwa
 5.               unyumbulishaji
 1. Vipashio vya lugha hupangwa kidarajia kuanzia kidogo kwenda kikubwa katika mpangilio huo ni kipashio kipi kikubwa cha lugha?
 1.              Kirai
 2.               Neno
 3.               Sentensi
 4.              Kishazi
 5.               Sauti
 1. Kutokana na kigezo cha tabia muhusika JOTI ni aina gani ya mhusika?
 1.              Mhusika shida
 2.               Mhusika bapa
 3.               Mhusika foili
 4.              Mhusika mkuu
 5.               Mhusika duara
 1. Waingereza wanakumbukwa kwa mchango wao mkubwa kwa kufanya jambo moja la pekee tofauti na Waarabu na Waingereza katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili enzi za utawala wao, jambo gani hilo.
 1.              Kutoa elimu kwa lugha ya Kiswahili
 2.               Kusafirisha manamba kutoka sehemu mbalimbali na kuwa fundisha Kiswahili
 3.               Kuteua lahaja ya kiunguja na kuisanifisha
 4.              kuhimizA matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ofisi zao
 5.               kuchapisha kamusi mbalimbali za lugha ya kiswahili
 1. Ipi ni maana ya nahau “Uso mkavu”
 1.              Uso usio na mafuta
 2.               Uso usio na nuru
 3.               Uso usio na haya
 4.              Uso usio na shukurani
 5.               Uso wenye mabaka mabaka
 1.                Oanisha maana ya dhana zilizo katika ORODHA A kwa kuchangua herufi ya dhana husika katika ORODHA B

ORODHA A

ORODHA B

 1.                  Ngeli
 2.                Sentensi
 3.             Nomino za pekee
 4.              Neno lenye mofimu nne
 5.                Kiambishi cha nafsi ya pili wingi
 1.              Pangani, Asha, Usingizi na John
 2.               Anayesinzia ni mvivu
 3.               Chaki
 4.              PAMUKU
 5.               Wanaimba
 6.                Mnaimba
 7.              Mtoto
 8.              Chai
 9.                 Kariakoo, Tanga, Iringa na Ali
 10.                 Wewe ni mvivu

 

SEHEMU B (Alama 40)

Jibu maswali yote ya sehemu hii kwa kuzingatia maelekezo ya kila swali.

 

 1.                Taja mambo manne (4) yakuzingatia katika uandishi wa kumbukumbu za mikutano
 2.                Badili vishazi tegemezi vifuatavyo kuwa vishazi huru
 1.                  Mtoto aliyelia jana usiku
 2.                Kazi zinazofanywa
 3.             Jambo litakalomsumbua
 4.              Kitabu kinachosomwa
 1.                Kwa mwanafunzi anayeijua vizuri sarufi ya lugha ya Kiswahili ni rahisi kutambua makossa yanayotokea katika lugha. Kwa hoja nne (4) na mifano fafanua makossa ya kisarifi yanayojitokeza katika utumiaji wa lugha kwa mwanafunzi wa kitanzania.
 2.                Ainisha sentensi zifuatazo, kisha toa sababu moja (1) yaa uainishaji huo kwa kila sentensi.
 1.                  Mkate uliotupatia umeharibika
 2.                Sanga alikuwa amelala
 3.             Aliadhibiwa kwa kuwa alifanya makossa
 4.              Mwalimu akirudi tutaendelea na somo
 1.                “Licha ya lugha ya Kiswahili kuteuliwa kuwa lugha ya Taifa la Tanzania, bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali kwa sasa” Onesha ukweli wa kauli hiyo kwa hoja nne (4)
 2.                Vifuatavyo ni vipera vya tanzu za fasi simulizi. Onesha tofauti iliyopo baina ya jozi za vipera hivyo
 1.                  Visakale na visasili
 2.                Ngonjera na majingambo
 3.             Mizungu na misemo
 4.              Wimbo na utenzi

 

SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali matatu (3) kutoka sehemu hii

 

 1.                Anna ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kibo. Alikutwa na simu licha ya katazo la serekali na shule kuwa hairuhusiwi mwanafunzi kumiliki simu akiwa shuleni. Baada ya kukutwa na simu hiyo alihojiwa na mwalimu wa nidhamu. Kwa kutumia ukurasa mmoja na nusu (11/2) andika namna mazungumzo yao yalivyokuwa. 

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 90

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

KIDATO CHA TATU 2021

MSIMBO: 021 KISWAHILI

MUDA: SAA 3:00                                                             AUG 2021

 

MAELEKEZO

 1.                Karatasi hii ina sehemu A, B and C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12)
 2.                Jibu maswali yote katika sehmu A na B na maswali matatu (03) kutoka sehemu C
 3.                Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali
 4.                Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa karatasi

SEHEMU A {Alama 15 }

Jibu maswali yote

 1.                Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu hilo katika karatasi yako ya kujibia.
 1. Tuimbe sote ni


 1.                 Wingi nafsi ya kwanza
 2.                Wingi nafsi ya pili
 3.                 Umoja nafsi ya kwanza
 4.                Umoja nafsi ya pili
 5.                 Wing nafsi ya tatu


 

 1. Kusoma kwake kwa bidii kumempatia mafanikio, Neno lililopigiwa mstari ni:


 1.                 Kitenzi
 2.                Kitenzzi kisaidizi
 3.                 Kitenzi jina
 4.                Kitenzi kikurupushi
 5.                 Nomino


 

 1. Jozi ipi ina vipengele sahihi vinavyounda umbo la ndani la kazi ya fasihi simulizi
 1.                 Falsafa, muundo, ujumbe, wahusika
 2.                Mandhari, msimamo, ujumbe, dhamira
 3.                 Ujumbe, mtizamo, migogoro, dhamira
 4.                Ujumbe, msimamo, dhamira, wahusika
 5.                 Lugha, migogoro, falsafa, mtindo

 

 1. Mpangilio sahihi wa vipashio vinavyounda lugha ya kiswahili ni upi
 1.                 Mofimu, kishazi, kirai, neno na sentensi
 2.                Mofimu, neno, kirai, sentensi na kishazi
 3.                 Neno, kirai, kishazi,  sentensi na mofimu
 4.                Neno, mofimu, kirai, kishazi na sentensi
 5.                 Mofimu, neno, kirai, kishazi na sentensi
 1. Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi Fulani ya kifasihi


 1.                 Muundo wa kazi husika
 2.                Wahusika wa kazi husika
 3.                 Jina la kazi husika
 4.                Jina la mtunzi husika
 5.                 Mtindo wa kazi husika


 1. Ipi ni sehemu Ndogo sana ya lugha?


 1.                 Mofimu
 2.                Neno
 3.                 Herufi
 4.                Silabi
 5.                 Mofoloji


 

 1. Ni taratibu zipi zinazofuatwa na lugha fasaha:
 1.                 Kimaana, kimatamshi, kilafudhi, kimuundo
 2.                Kimatamshi, kimofolojia, kiufundi, kimaana
 3.                 Kimatamshi, kimaana, kimuundo, kimantiki
 4.                Kimantiki, kifonolojia, kimaana, kilafudhi
 5.                 Kilafudhi, kimuundo, kiufundi, kimaana

 

 1. Kwa nini lugha ni sauti za nasibu____________
 1.                 Kwa sababu inatumia ishara
 2.                Kwa sababu intumia sauti
 3.                 Kwa sababu inabeba maana
 4.                Kwa sababu inatumiwa na wanyama
 5.                 Kwa sababu inatumiwa na binadamu

 

 1. Ni sifa ipi hutofautisha fasihi simulizi na fasihi andishi?


 1.                 Ukubwa
 2.                Ueneaji
 3.                 Uwasilishaji
 4.                Uhifadhi
 5.                 Utamkaji


 

 1. Mhakiki wa kwanza katika kazi ya fasihi simulizi mfano wa igizo ni:


 1.                 Mtunzi
 2.                Mtazamaji
 3.                 Msomaji
 4.                Mwigizaji
 5.                 Mfasili


 

 

 1.                Oanisha maana za dhana za uandishi zilizo katika orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana husika katika Orodha B, Kisha andika herufi husika katika karatasi yako ya kujibia:

ORODHA A

ORODHA B

 1. Irabu
 2. Sarufi
 3. Sentensi sahili
 4. Kidahizo
 5. Chagizo
 1.              Kiwakilishi cha a – unganifu
 2.               Tanzu ya lugha
 3.               Maana ya msingi
 4.              Inaotamkwa huwa hakuna kizuizi chochote kwenye mkondo wa hewa
 5.               Ina hadhi ya kishazi huru
 6.                Kitomeo na taarifa zake
 7.              Ni maneno yanayotokea baada ya kitenzi na kufanya kazi kama kielezi.

 

 

 

SEHEMU B (Alama 40)

 

 1.                Kwa kutumia mifano dhabiti fafanua dhana zifuatazo
 1.                 Urudufishaji
 2.                Uambishaji
 3.                 Kutohoa maneno
 4.                Ngeli

 

 1.                Maneno huweza kubadilika kutoka aina moja na kuwa aina nyingine “Dhihirisha kaulli hii kwa kubadili maneno yafuatayo kwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika mabano
 1.                 Kwenda (Badili kuwa nomino)
 2.                Ogopa (Badili kuwa kivumishi)
 3.                 Mzazi (Badili kuwa kitenzi)
 4.                Linda (Badili kuwa nomino)
 5.                 Bisha (Badili kuwa kivumishi)
 6.                 Bora (Badili kuwa kitenzi)
 7.                Refu (Badili kuwa kitenzi
 8.                Kabati (Badili kuwa kielezi)

 

 1.                Kwa kutumia mifano kuntu fafanua tabia zisizopungau nne (4) za vitenzi vya kiswahili

 

 1.                Wewe na msaidizi wako mmehudhruria kikao cha kupanga mahafali ya kidato cha nne.  Andika kumbukumbu ya kikao kilichofanyika katika shule yenu.

 

 1.                Baada ya kiswahili kuteuliwa kuwa lugha ya Taifa vyombo mbalimbali viliundwa kwa lengo la kukuza na kueneza kiswahili dhibitisha dai hilo kwa kutumia asasi tatu (03)

 

 1.                Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata

 

 1.                Korona ugonjwa gani umezua taharuki;

Chanjo haipatikani Ulaya hakukaliki,

Tiba haijulikani, Dunia haifurukutu,

Korona ni maafa kujikinga lazima,

 

 1.                Hofu kubwa imetanda, wakubwa kwa wadogo;

Mafua, homa kupanda utaona uki”gugo”,

China mpaka mpanda, korona haina vigo,

Korona ina maafa kujikinga lazima

 

 1.                Walakini juu ya yote, mapenzi yameoteshwa,

Karantini kwa wotee, makapera wameoa,

Mabinti wasiopenzini, huu msimu wa ndoa

Korona ina maafa kujinginga lazima

 

 

 

 1.                Hakika baniani mbaya Kiatu chake dawa,

Wanandoa walishane penzi bila taabu,

Nao wapenzi wachanga, wasubiri janga lipite

Korona ina maafa kujikinga lazima

 

 1.                Mungu atasaidia Korona itaisha,

Elimu tazingatia Wizara wanakumbushia,

Tunawe yetu mikono, epuka msongamano

Koroana ina maafa kujikinga lazima

MASWALI

 1.                 Pendekeza kichwa cha habari kisichozidi maneno matatu
 2.                Unafikiri kwa nini mshairi anatuasa kuwa Korona ina maafa kujikinga lazima?
 3.                 Mashairi wa shairi hili anawashauri nini wanafunzi kuhusiana na suala la mapenzi?
 4.                Kutokana na shairi ulilosoma eleza njia tano unazozijua utakazotumia kuepukana na ugonjwa wa Korona

 

SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii

 1.                Fasihi simulizi ndio fashihi ya awali iliyoanza wakati binadamu alipoanza kutumia lugha mara kwa mara inapowasilishwa kwa hadhira huchukua sifa muhimu ambazo sirahisi kuziona katika fasihi Andishi.  Dhibitisha ukweli huu kwa kutumia hoja tano.

 

 1.            Nyimbo ni mbinu ya kifasihi ambayo wasanii wengi hutumia ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira.  Dhibitisha usemi huu kwa kutumia waandishi wawili wa riwaya ulizosoma.

 

 1.            Taswira ni kibebeo cha ujumbe wa mwandishi katika jamii.  Jadili kauli hii kwa kutumia thamthiliya mbili ulizosoma.

 

 1.            “Mshairi siku zote hukemea uonevu katika jamii “dhibitisha kauli hii wa kutoa hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya Diwani mbili (2) ulizosoma.

 

ORODHA YA VITABU

USHAURI

Wasakatonge    - M.s Khatibu (DUP)

Malenga wapya  - Takiluki (DUP)

Mashairi ya chekacheka - T. A Mvungi (EP & D. LTD)

RIWAYA

Takadini   - Benj. Hanson (MBS)

Watoto wa mama ntiliye - E. Mbogo (H.P)

Joka la mdimu   - A.J Safari  (H.P)

TAMTHILIYA

Orodha Steven Reynolds (MA)

Ngoswe penzi kitovu cha uzembe -E. semzaba

Kilio chetu     -Medical Aid foundation 

Page 1 of 4

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 65

  OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA KWANZA

KIDATO CHA TATU

021KISWAHILI

(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

MUDA: SAA 3 MEI 2021


Maelekezo

1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).

2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A, Bna chagua maswali matatu (03)kutoka sehemu C.

3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali.

4.Andika kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au nyeusi

5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa haziruhusiwikatika chumba cha mtihani.

6. Andika namba yako ya mtihani katika kila karatasi yako ya kujibia.

 1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele i-x kisha andika herufi ya jibu sahih katika kisanduku.
 1.  Ni neno lipi linalotoa taarifa kuhusu Nomino?

A: Kitenzi  B: Kielezi  C: Kivumishi

D: Kiwakilishi  E: Kiunganishi

(ii) Katika lugha ya Kiswahili kuna aina ngapi za Vitenzi.

 A: Mbili  B: Tano  C: Sita

 D: Tatu  E: Nne

(iii) Maneno yapi kati ya haya yafuatayo yametokana na lugha ya Kibantu.

  A: Kitindamimba ba bendera   B: Hela za mtoto

  C: Kitivo na ngeli    D: Godoro na sharubati

  E: Bunge na Shule

(iv) Ni mambo gani muhimu ya kuzingatia katika kuteua maneno na miundo 

    ya tungo wakati wa mazungumzo.

   A: Mada, muktadhia wa mazungumzo ya aina kwa nia

    B: Mada, mazungumzo na uhusiano wa wazungumzaji

   C: Mada, mzungumzaji na muktadha wa mazungumzo 

   D: Mada, mzungumzaji na uhusiano wa wazungumzaji

   E: Mada, muktadha na uhusiano wa wazungumzaji.

(v)  Bainisha kauli unayoonyesha dhima muhimu za vitendawili katika jamii za 

    vitendawili katika jamii.

     A. Kuhimiza umoja na mshikamano.

    B. Kupanga watu katika marika yao.

    C. Kuchochea udadisi wa mambo

  D. Kuchochea uwongo wa mambo.

  E. Kukosoa wadadisi wa mambo.

(vi) Njia mojawapo ya kuzuia utata katika lugha ya mazungumzo ni ipi kati ya zifuatazo?

 A. Kuepuka makosa ya kisarufi na kimantiki

 B. Kutumia neno lenye maana zaidi ya moja 

 C. Kutumia kiwakilishi kiambata katika neno 

 D. Kuweka msisitizo au ufafanuzi zaidi

 E. Kutumia misimu sahihi za wakati.

(vii) ‘’Wanafasihi hutumia wahusika wenye mienendo hiyo’’ katika tamthiliya ulizosoma, ni wahusika wapi kati ya wafuatao wana mienendo isiyokubalika?

 A. Joti, Ngoswe na Mama Furaha

 B. Padri James, Ngoswe na Baba Anna.

 C. Mazoea, Mama Furaha na Joti

 D. Ngoswe, Baba Anna na Suzi

 E. Ngoswe, Joti na Padri Jamaes

(viii) Kati ya sababu zifuatazo ni ipi si sahihi kuhusu matumizi ya Kamusi?

 A. Kujifunza Lugha ya Kigeni

 B. Kusanifisha maneno mapya

 C. Kubaini kategoria ya neno

 D. Kujua maana za maneno

 E. Kujua tahajia za maneno.

(ix) Ni methali ipi inayokinzana na methali ‘’Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.’’

 A. Manahodha wengi, chombo huenda mrama.

 B. Palipo na wengi, hapaharibiki neno

 C. Haba na haba, hujaza kibaba.

 D. Kidole kimoja, hakivunji chawa

 E. Fimbo ya mnyonge, ni umoja 

(x) Upachikaji wa Viambishi katika mzizi wa neno huitwaje?

 A. Mnyambuliko  B. Utohoaji  C. Uambishaji

 D. Viambishi   E. Kukopa maneno  

 1. Oanisha maana za maneno kutoka orodha A kwa kubainisha dhama zilizoko katika

Orodha B na uandike herufi ya jibu sahihi pembeni na swali.

ORODHAA

ORODHAB

(i) Tungo shurutia ukwasi

A. Rejesta ya Tanga

(ii) Kimtang’ata

B. Angeliniita ningeitika

(iii) Malaika, Shetani, Mzimu

C. Lahaja ya Kiswahili

(iv) Juzi asubuhi

D. Nomino za mguso


E. Njeo ya ya wakati wa mazoea


F. Nomino za dhahania


G. Kirai kielezi


H. Utajiri

SEHEMU B: (ALAMA 40)

Jibu maswali yote kutoka sehemu hii

 1. Bainisha mzizi asilia kwa kila neno katika maneno yafuatayo.

(a) Anawaandikisha

(b) Mkimbizi

(c) Mlaji

(d) Muumbaji

(e) Nisingelipenda

(f) Kuburudika

(g) Sadifu

(h) Aliokota

(i) Walichopoka

(j) Kipambanuliwe.

 1. Bainisha matumizi mbalimbali ya ‘’KWA’’ katika sentensi zifuatazo

(a) Amejificha kwa kuwa hapendi anione

(b) Kukataa kwa Mwajuma kumesababisha matatizo mengi.

(c) Amelima shamba kwa jembe

(d) Ameenda kwa Mwalimu

(e) Amesafiri kwa ndege

 1. Kwa kutumia mfano taja njia tano za uundaji wa maneno.
 2. Toa maana mbili katika tungo tata zifuatazo?

(a) Pili alimwandikia barua Asha

(b) Wizi wa Silaha umeongezeka

(c) Mwalimu ameijia fedha yake

(d) Mtoto amelalia uji

(e) Mama amenuena Mbuzi

 1. Taja mambo matano ya kuzingatia wakati wa utunzi wa Insha na ueleze umuhimu wa kila jambo.
 2. Eleza tofauti za msingi tano, zilizopo baina ya varua ya kikazi na barua za kindugu.

SEHEMU C: (ALAMA 45)

Jibu maswali matatu tu toka sehemu hii

 1. Eleza sababu tano zilizosaidia kuenezza Kiswahili wakati wa utawala wa Wajerumani.
 2. Fasihi ni Chuo chenye kufundisha kila mwanajamii husika. Thibitisha hoja hiyo kwa kutumia vitabu viwili vya riwaya ulivyosoma. Toa hoja tatu kwa kila Kitabu.
 3. Mashairi huburudisha na kuliwaza pale yanapoimbwa au kusomwa lakini nayatoa mafunzo mazuri sana kwa jamii husika. Jadili kauli hii kwa kutumia Diwani mbili ulizosoma. Toa hoja nne kutoka kila diwani.
 4. Siku zote katika jamii, migogoro ndiyo inayoibua dhamira mbalimbali. Thibitisha dai hili kwa kutumia tamthiliya mbili ulizozisoma ukitoa hoja tano kwa kila kitabu.

1

LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 55

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA 2020

021KISWAHILI

(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

MUDA: SAA 3 DECEMBER 2020


Maelekezo

1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).

2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A, B na chagua maswali matatu (03) kutoka sehemu C.

3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali.

4Andika kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au nyeusi

5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

6. Andika namba yako ya mtihani katika kila karatasi yako ya kujibia.

SEHEMU A, (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika karatasi yako ya kujibia.

(i) Ni kanuni, sheria na taratibu zipi zinazozingatiwa na wazungumzaji wa lugha fulani?

A Mofimu, Neno, Kirai, Kishazi na Sentensi

B Herufi, Sauti, Mofimu,Silabi na neno.

C Sarufi Maana, Sarufi Miundo, Sarufi Maumbo na Sarufi Matamshi.

 Sarufi maana, Mofimu, Neno na Kirai

E Silabi, Neno, Kirai na Sentensi.

(ii)………………. Ni sauti zinazotamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti.

 A Sauti B Herufi

 C irabu D  Silabi

 E Konsonanti

(iii)  Zipi ni nyenzo za lugha yoyote duniani?

A Sarufi na Fasihi B Irabu na Konsonanti

C Sarufi, Irabu na KonsonantiD Fasihi, Irabu na Konsonanti

E Sarufi, Fasihi, Irabu na Konsonanti

(iv) Mpangilio sahihi wa ngeli za kisintaksia ni upi?

A YU/A-WA, I-ZI,LI-YA,U-I,KI-VI,U-ZI,U-YA, KU,PA-MU-KU

B U-ZI, I-ZI,LI-YA,U-I, KU, YU/A-WA,U-YA, KI-VI, PA-MU-KU

C YU/A-WA, I-ZI, LI-YA,U-YA, KI-VI,U-ZI,U-I, KU,PA-MU-KU

D YU/A-WA,I-ZI, LI-YA,U-I,KI-VI, U-ZI,U-YA, PA-MU-KU, KU

E YU/A-WA, I-ZI,LI-YA, U-I, KI-VI,U-ZI, U-YA,KU, PA-MU-KU

(v)  Ni upi mpangilio sahihi wa mjengo wa Tungo?

A Kirai, Neno, Sentensi na Kishazi

B Neno, Kirai, Kishazi na Sentensi

 Kishazi, Kirai, Sentensi na Neno

E Sentensi, Neno. Kishazi na Kirai

(vi)  Ni lugha mseto ya muda inayozuka pindi makundi mawili yenye lugha mbili tofauti yakutanapo.

 Lugha ya vizalia B Pijini

C Kibantu D Kiswahili

E Kiunguja

(vii)Mambo muhimu yanayopatikana katika maana ya lugha ni kama yafuatayo, isipokuwa;

A Ni sauti za nasibu B Ni mfumo

C Lugha hufurahisha na kufundisha D Lugha inamuhusu binadamu

E Lugha ni chombo cha mawasiliano

(viii)  Ni sentensi ipi sio sentensi huru?

A Juma anacheza mpira B Anaimba vizuri

C Mtoto aliyepotea jana amepatikana. D Asha ni mtoto mzuri

EYule alikuwa anataka kucheza mpira.

(ix)  ……………. Ni kipashio kidogo kabisa cha lugha chenye maana. Maana hiyo yaweza kuwa ya kisarufi au kileksika;

 Isimu B Shina

C Mzizi D Kiimbo

E Mofimu

(x) Ni seti ipi inawakilisha kikamilifu wahusika wa fasihi simulizi?

A Vitu, mahali, wanyama, binadamu, fanani na maleba.

B Hadhira, wanyama, maleba, binadamu na fanani.

C Fanani, vitu, mahali, binadamu, maleba na wanyama.

 Wanyama, manju, binadamu, vitu, mahali na maleba

E Hadhira, binadamu, wanyama, vitu, mahali na fanani.

2. Oanisha maelezo yaliyo katika orodha ‘’A’’ ambayo ni aina ya tungo na orodha ‘’B’’ ambazo ni aina za maneno yanayounda tungo hizo kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.

ORODHA “A”

ORODHA “B”

i.Wale waliamini maneno yangu

 ii. Salama alikuwa mwanafunzi wangu

 iii. Walikuwa wanataka kwenda kulima

 iv.Alikuwa anajisomea darasani polepole

 v. Loo! Yule anapenda ugomvi

A. N + t +N +V

B. H + w +T + N

C. W + T + N + V

D. Ts + T + E +E

E. Ts + Ts + Ts + T

F. N + V + t +E

G. N + U+ N+ T

SEHEMU B (Alama 40)

Jibu maswaliyote katika sehemu hii

3.Tunga sentensi moja kwa kila alama kuonesha matumizi ya alama zifuatazo.F4

i. Mkato

ii. Mabano

iii. Alama za mtajo

iv. Nukta pacha

4.Andika maana ya methali zifuatazo;

 1. Kikulacho ki nguoni mwako.
 2. Mtaka cha uvunguni sharti ainame.
 3. Mchumia juani hulia kivulini.

5.(a) Tenga kiima na kiarifu katika sentensi zifuatazo. Tumia alama ya mkwaju (/) na kuweka herufi “K” juu ya kiima na herufi “A” juu ya kiarifu.

i. Mdogo wangu anaongea sana

ii. Yule kijana aliyekuja hapa juzi amefariki dunia

iii. Frank ni kijana mpole sana

iv. Mama amelala sakafuni

(b) Changanua sentensi zifuatazo kwa njia yamatawi kwa kutumia mkabala wa kimapokeo

i. Fisi mkubwa ameuawa kichakani jana alfajiri.

ii. Mtoto aliyekuwa anacheza uwanjani amevunjika mguu.

6.(a) Kwa kutumia mifano miwili kwa kila kipengele, fafanua kwa ufupi jinsi vipengele vifuatavyo vinavyoonesha kuwa vitenzi vya Kiswahili na lugha za kibantu vina asili moja.

 1. Mpangilio wa viambishi katika vitenzi
 2. Kiambishi tamati katika vitenzi

b) Eleza kwa ufupi juu ya nadharia zifuatazo kwa jinsi zinavyoelezea asili ya Kiswahili

a)Kiswahili ni pijini au krioli

b)Kiswahili ni kiarabu

7. Kwa kutumia mifano, fafanua dhana zifuatazo kama zinavyotumika katika fasihi

a)Tashibiha

b)Takriri

c)Sitiari

d)Tashihisi

e)Mubaalagha

8. Soma kifungu cha habari kifuatacho, kisha jibu maswali yanayofuata;

Wanangu, toka zamani bara letu la Afrika lilikuwa na mambo yaliyohitilafiana na haya tunayoyaona sasa. Hadithi, vitimbi, na visa vilivyotokea zamani katika bara letu vinatofautiana sana na mabara yoyote mengine. Vyetu ni vitamu na bora kuliko vyote vile vilivyotokea katika mabara hayo.

Miujiza ya mambo yaliyotokea ina mizizi ambayo viini vyake hubenua waziwazi mila na desturi za asili tangu zamani, hivyo, hadithi hizo zina tija ya makumbusho ya daima milele. Kwa hiyo, katika hali yoyote yatupasa kuhifadhi hazina za mila zetu. Mila zetu zidumishwe; kwa mfano watu kuzunguka moto huku kizee kikongwe au ajuza akisimulia hadithi za mambo ya kale liwe ni jambo la kawaida kabisa. Katika dunia ya leo simulizi hizo za ujasirina uzalendo zimeenea kutoka vizazi hadi vizazi. Mambo mengi yamebadilika kutoka mitindo aina aina, hivyo mabadiliko hayo yasitufanye sisi kusahau simulizi zetu katika mitindo yetu. Ni wajibu utupasao kuendeleza tabia hizi ili tubenue mbinu za masimulizi hata kwa vitabu.

Maswali

 1. Pendekeza kichwa cha habari hii kisichozidi maneno matatu.
 2. Bara la Afrika lina mambo gani mawili mazuri.
 3. Mwandishi anatuhimiza tudumishe mila ipi?
 4. Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua 50 na yasiyozidi 60.

SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali matatu(3) kutoka katika sehemu hii.

9.Wewe kama afisa Manunuzi wa kiwanda cha mbao cha Mshikamao S. L. P 100 Chamwino, andika barua kwa mfanyabiashara yeyote mashuhuri wilayani kwenu kuhusu agizo la vifaa vifuatavyo; Misumeno 5, gundi ya mbao lita 20, misumari ya nchi sita Kg 25, na kofia ngumu 40. Jina lako liwe Shukrani Kazamoyo.

10. Kwa kutumia diwani mbili ulizosoma, eleza jinsi taswira tatu kutoka kila diwani zilivyotumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe kwa jamii.

11. “Kazi ya fasihi ina radha kwa sababu inamzungumzia pia mwanamke kwa namna tofautitofauti” Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu katika riwaya mbili ulizosoma.

12. Chagua wahusika wawili katika tamthiliya teule mbili ulizosoma na uoneshe ujumbe unaowasilishwa na waandishi kupitia matendo yao.

ORODHA YA VITABU 

USHAIRI

Wasakatonge ---------------------------- M. S Khatibu (DUP)

Malenga wapya-------------------------- TAKILUKI (DUPU)

Mashairi ya Chekacheka---------------- T. A. Mvungi (EPdD.LTD)

RIWAYA

Takadini ----------------------------------- Ben J. Hanson (MBS)

Watoto wa Mama Ntilie ----------------- E. Mbogo (H.P)

Joka la Mdimu ---------------------------- A. J. Safari ( H.P)

TAMTHILIYA

Orodha ------------------------------------ Steve Reynolds ( M. A)

Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe ----- E. Semzaba (ESC)

Kilio Chetu --------------------------------- Medical Aid Foundation (TPH)

LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 37

THE PRESIDENT'S OFFICE

MINISTRY OF REGIONAL GOVERNMENT AND LOCAL GOVERNMENT

AUGUST-SEPTEMBER   EXAMINATION SERIES

KISWAHILI  FORM-3

2020

TIME: 2:30 HRS

Maelekezo

 1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
 2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C.
 3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.
 4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
 5. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu chako cha kujibia.

(i) Neno lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza mtenda au mtendwa?

 1. Kiunganishi   
 2. Kivumishi
 3. Kihisishi 
 4. Kiwakilishi 
 5. Kielezi

(ii) Shamba letu li kubwa neno “Li” ni aina gani ya neno? 

 1. Kiwakilishi 
 2. Kielezi 
 3. Kivumishi 
 4. Kiunganishi 
 5. Kitenzi kishirikishi

   (iii) Lugha fasaha hufuata taratibu za lugha, taratibu hizo ni pamoja na 

A       fonolojia, mofolojia, semantiki na sintaksia

B        maana, matamshi, muundo na maumbo

C        maana, matamshi, muundo na mantiki

D        kiimbo, shada, mkazo na toni

E.       fonolojia, mkazo, shada na semantiki

(iv) Kamati ya lugha ya Afrika ya Mashariki (the interteritorial Swahili language committee) iliteua lahaja moja na kuisanifisha, lahaja hiyo ilikuwa ni

A         kimvita             

 B       kiunguja

C         kimtang’ata       

D        kisiu

E         kivumba

(v). Watoto hawa wanacheza vizuri neno “Vizuri” ni aina gani ya neno? 

 1. Kivumishi 
 2. Kielezi 
 3. Kiwakilishi 
 4. Kivumishi cha sifa 
 5. Kihisishi 

 

(vi) Kiswahili ni kibantu kwa kuwa:- 

 1. Kinaongewa na wabantu wengi 
 2. Ni lugha ya Taifa 
 3. Kina maneno mengi ya kibantu 
 4. Kimethibitishwa kiisimu na kihistoria 
 5. Wasomi wengi wamethibitisha hivyo.  


(vii) Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi fulani ya kifasihi? 

 1. Muundo 
 2. Mtindo 
 3. Wahusika 
 4. Jina la mtunzi  
 5. Jina la kazi husika 


(vii) Ipi ni fasili sahihi kuhusu tungo? 

 1. Maneno yanayoonesha uhusiano baina ya neno moja na jingine. 
 2. Kipashio kidogo katika lugha kinachotumika kama dhana ya kuchambulia lugha Fulani. 
 3. Matokeo ya kuweka na kupanga pamoja vipashio sahili ili kujenga vipashio vikubwa zaidi. 
 4. Kipashi cha kimuundo chenye neno moja na kuendelea 
 5. Maneno yenye kutoa maana kamili


(viii) Nini maana ya sentensi sahili. 

 1. Ni sentensi yenye kishazi kuu kimoja au zaidi pamoja na kishazi tegemezi.
 2. Ni sentensi yenye kishazi huru 
 3. Ni sentensi yenye kuonesha masharti 
 4. Ni sentensi yenye maana nyingi 
 5. Ni sentensi yenye vishazi vingi 


(ix) Zifuatazo ni sifa za pijini isipokuwa 

A.      Pijini huwa na maneno kutoka lugha mbili au zaidi

B.      Pijini hutokea kurahisisha mawasiliano baina ya watu ambao kila mmoja 

         ana lugha yake

C.      Miundo ya maneno na tungo katika pijini imerahisishwa ili kukidhi 

         mawasiliano

   D.     Pijini haina msamiati mwa kutosha, hivyo wazungumzaji hutumia sana 

        ishara

  E.    Pijini ina watu ambao kwao hiyo ni lugha yao ya kwanza


2. Katika kila sentensi uliyopewa, orodhesha vishazi huru katika Safu A na vishazi tegemezi katika safu B.
(a) Ngoma hailii vizuri kwa kuwa imepasuka.
(b) Watoto walioandikishwa watakuja kesho.
(c) Kiongozi atakayefunga mkutano amepelekewa taarifa.
(d) Mtawatambua walio wasikivu.
 (e)       Kitabu ulichopewa kina kurasa nyingi. 

 

3. Taja aina za sentensi zifuatazo kisha eleza muundo ujengao kila sentensi.

 1. Maisha ni safari ndefu.
 2. Ukisoma kwa bidii utafaulu kwa kiwango cha juu.
 3. Mtoto aliyelazwa hospitalini ameruhusiwa kwenda nyumbani.
 4. Nitakuja leo ingawa nitachelewa sana.
 5. Alinunua madaftari lakini kitabu cha Kiswahili alipewa na mwalimu.

4. Andika maneno matano ambayo yameundwa kutokana na kufananisha sauti. Kwa kila neno tunga sentensi moja.

5. Eleza dhima za mofimu "li" kama ilivyotumika katika sentensi zifuatazo:

 1. Shamba letu li kubwa sana.
 2. Wlishelewa kurudi.
 3. Tunalifuatilia.
 4. Limeharibika.
 5. Shikilia.

6. Andika sentensi zifuatazo katika hali ya ukanushi:

 1. Ameshiba sana.
 2. Watoto wengi wanaogelea.
 3. Mvua ilinyesha kwa wingi sana.
 4. Kijana anakula chakula kingi.
 5. Mimi nasoma polepole.

7. Bainisha mzizi wa asili kwa kila neno katika maneno yafuatayo:

 1. Anawaandikisha
 2. Mkimbizi
 3. Mlaji
 4. Muumbaji
 5. Nisingelipenda
 6. Kuburudika
 7. Sadifu
 8. Aliokota
 9. Walichopoka
 10. Kipambanuliwe

1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

Karibu masikio ya watu wa mahali pengi yalijaa habari za Karama na mashtaka yake. Umaarufu wake wa ghafla ulizungumzwa karibu na mbali. Mtu yeyote wa desturi anapozuka katika umaarufu, huyavuta masikio na macho ya watu wengi kwa sababu jambo kama hili hutokea nadra sana kwa watu ambao bahati mbaya imeshughulika kuwaweka nyuma. Kwa hiyo, siku ya tatu ya baraza ilihudhuriwa na mfalme, watu wenye vyeo mbalimbali, pamoja na nusu moja ya umati mkubwa wa Kusadikika. Fikra zilizochanganyika ziliushika umati huu. Baadhi ya watu walimwajabia Karama wakamhesabu kama mtu bora wa karne yao. Hawa walitumaini ataokoka lakini wengine waliwaza kuwa Karama alikuwa kama mjinga aliyekuwa akicheza na hatari kubwa iliyofunua taya mbele yake.

Waliokuwa wakimtazamia kuokoka walikuwa na wasiwasi wao; na wale waliokuwa wakimtazamia kuanguka walikuwa na fadhaa yao. Walakini hapana mtu hata mmoja aliyepata kulisema wazo lake.

Bila ya kujua alivyoajabiwa Karama aliendelea kusema mbele ya baraza, “Watu wanaoteswa ndio wanaoyajua mateso yao.” Kusadikika ilikuwa chini ya mateso makubwa sana. Maisha yao yalizungukwa na maradhi na mauti, uadui usiokwisha, nchi iliyokaribia kugeuka jangwa na mwamba na madhila mengine mazito yaliyowakabili watu. Wanakusadikika walitaka faraja katika mateso haya. Kila jitihada ilijaribiwa ili kuirekebisha saa ya maendeleo ya nchi, lakini mara kwa mara majira yake yalirudishwa nyuma. Kama hili lilifanywa kwa makosa ama kwa makusudi ni siri iliyo ng’ambo ya fahamu zangu hata sasa. Lakini kama siri njema hufichika, ile iliyo mbaya haifichiki hata kidogo. Uchaguzi wa wajumbe ulikuwako lakini hathibitisho ya matokeo ya ujumbe hayakupatikana.

Kusadikika iliishi kuona mjumbe baada ya mjumbe kuadhiriwa na kuadhibiwa vibaya. Kama washauri hawakudhuriwa na hili lakini watu wengine walidhuriwa sana. Kazi njema za wajumbe wawili zilipotea bure. Manung’uniko ya lawama hii yalikuwa katika hewa yote ya Kusadikika.

Hili lilipotokea serikali iliombwa ima faima kufanya ujumbe mwingine. Basi mjumbe wa tatu alitakikana ajitolee mwenyewe kwa ujumbe wa Kusini. Wito wa mjumbe wa tatu uliitikiwa na Kabuli; mtu mwenye busara, haya na mcheshi. Yeye alipatikana upesi kabisa kuliko ilivyokuwa kwa mara ya pili na ya kwanza. Misiba ya Buruhani na Fadhili ilikuwa mikubwa ya kutosha kuikongoa mioyo ya bidii katika bawaba zake. Kabuli aliyajua haya yote lakini alikuwa mtu wa moyo wa namna nyingine kabisa. Alikuwa na bidii kubwa kama ile ya siafu athubutiye kukivuka kijito kwa daraja iliyofanywa kwa maiti ya siafu wengine walioelea majini huko na huko. Maji yalijulikana kuwa na asili ya rutuba, mvuke na umeme. Nguvu nyingine za namna mbalimbali zipo pia katika maji. Kama siafu mdudu mdogo na kipofu wakati mwingine haogopi kuzikabili nguvu hizo pamoja na hatari zake kwa sababu njema, basi ni dhahiri kuwa viongozi wa wanadamu wanapoteswa bure bidii za wafuasi wao hutanuka ajabu.

Hapana tishio liwezalo kuukomesha mwendo huu. Kwa hakika utafululiza kuwako duniani mpaka mateso yakome kabisa, na labda wakati huo dunia hii itakuwa njema kama itamaniwavyo kuwa.

Buruhani na Fadhili walitoa sadaka zao bora ili kuyahimiza majilio ya wakati uliotakikana sana. Kabuli aliwaona watu wawili hawa kama wafadhili wakubwa wa ulimwengu. Alitaka kuwa mshirika wao kwa thamani yoyote ya maisha yake.

Kama ilijulikanavyo, Kusini na upande wa dunia yatokako matufani makubwa na baridi kali sana. Kabuli aliyakabili mashaka haya bila ya kigeugeu. Naam, alikuwa kama mtu aliyekuwa akinywa uchungu bila ya kigegezi. Mara mbili alikamatwa akafanywa mahabusu.

Maswali

(a) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu cha habari:

 1. Fadhaa
 2. Madhila
 3. Kuadhiriwa
 4. Ima faima
 5. Kigeugeu
 6.  Kigegezi.

(b) Eleza mchanganyiko wa fikira walizonazo wana wa Kusadikika kuhusu Karama.

(c) Kwanini bidii ya mjumbe wa Kusini imelinganishwa na bidii ya siafu? Toa sababu mbili.

(d) Ujumbe wa mwandishi wa kifungu hiki unahusu nini?

SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii.

8. Andika insha isiyozidi maneno mia tatu (300) na isiyopungua mia mbili na hamsini (250) kuhusu faida za televisheni kwa jamii.

ORODHA YA VITABU USHAIRI

Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)

Malenga   Wapya - TAKILUKI (DUP)

Mashairi   ya   Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D.LTD)

RIWAYA

Takadini - Ben J. Hanson (MBS)

Watoto   wa   Maman’tilie - E. Mbogo (H.P)

Joka   la   Mdimu - A.J. Safari (H.P)

TAMTHILIYA

Orodha - Steve Reynolds (MA)

Ngoswe Penzi Kitovu   cha   Uzembe - E. Semzaba (ESC)

Kilio   Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

10. "Fasihi ya Kiswahili imemweka mwanamke katika hadhi tofauti tofauti." Thibitisha usemi huu kwa kutumia hoja tatu kwa kila riwaya kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.

11. (a) Vigano ni nini?

(b) Tunga vigano kwa kutumia methali isemayo "Umdhaniaye siye kumbe ndiye!"

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 28

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256