KISWAHILI FORM SIX REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

image

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MKOA WA NJOMBE

MTIHANI KABLA YA MTIHANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA SITA

CODE: 121/2                                                               KISWAHILI 2

MUDA: SAA 3                              JUMATANO, 23 Agosti 2023, Mchana

image

MAELEKEZO

1.       Mtihani huu una sehemu kuu mbili A na B zenye jumla ya maswali nane (08).

2.       Jibu maswali yote katika sehemu A na maswali matatu (03) katika sehemu B, swali la sita (06) ni la lazima.

3.       Sehemu A ina alama arobaini (40) na sehemu B ina alama sitini (60).

4.       Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.

5.       Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani. 

6.       Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa karatasi zako za kujibia. 

NAMBA YA SWALI

WEKA VEMA(V)

WATAHINI TU

ALAMA

SAINI

1

 

 

 

2

 

 

 

3

 

 

 

4

 

 

 

5

 

 

 

6

 

 

 

7

 

 

 

8

 

 

 

JUMLA

 

 

 

SEHEMU A: ALAMA AROBAINI (40).

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1.      Mjengo wa ushairi wa Kiswahili hutegemea utaalamu wa mjenzi wa ushairi huo. Thibitisha kauli hiyo kwa mifano kwa kueleza vijenzi vitano (05) vya ushairi wa Kiswahili.

 

2.      Michezo ya Watoto ni muhimu sana kulingana na utamaduni waw a jamii husika.Thibitisha kwa mifano kwa kueleza ubaya wa michezo ya Watoto.(Toa hoja tano)

 

3.      “Usanii wa kifasihi ni zaidi ya usanii wa muziki”. Taja na kueleza kwa mifano mambo matano (5) yanayofanya usanii wa kifasihi kuwa tofauti na usanii wa sanaa nyingine. 

 

4.      Soma habari ifuatayo kisha bainisha vipengele vya fani vilivyotumika.

 

Uhasama kati ya Boaz na Jeta sasa ulidhihirika. Baada ya tukio la fumanizi Nimoni hakutakuwa na kuongea na Boaz tena badala yake kila alipokuwa bwaloni aliongea na Jeta. Tena wakati huo kuna kila dalili kuwa walihusiana kimapenzi. 

Boaz alijigonga kwa Nimoni na kumtaka radhi. Lakini sijui maombi yake yangesikilizwa vipi wakati hakuweza hata kumsogelea Nimoni mwenyewe. Hata akiwa karibu naye alishona mdomo kwa uzi wa shaba na kuchomelea kwa risasi. 

Nimoni nisamehe nimekosa Boaz aliomba radhi. Nilifanya makosa kukuficha habari za Anita. Hayo yamekwisha, tutazame mengine, maneno hayo yalizidi kumchengua Nimoni. Badala yake mrembo huyo alimfuata Jeta huku akimwita hadharani “mpenzi Jeta una mpango gani wa

Jumapili hii?”.

Jeta alikuwa mwenye soni sana. Hakujibu mbele ya watu akijua waziwazi Boaz alikuwa karibu. Lakini kulimridhisha Nimoni, zaidi na kumchukia Boaz. Boaz aliona kuwa ni majivuno. Nimoni alimsogelea Jeta na kumgusa begani na kuacha mkono wake utulie pale huku akimwangalia Jeta machoni kwa uchokozi.

Ama kweli mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu. Haya yalimuumiza Boaz. Akiwa mnyonge aliyawaza mengi. Alitamani hata kukimbia kambi kama mwasi, lakini hilo lisingekuwa na faida kwake kwani ulikuwa umebaki mwezi mmoja tu wamalize awamu ya kwanza ya miezi sita, halafu watawanywe kwenye makambi mengine. Ndipo alipoamua kumwandikia barua Nimoni sehemu ya barua yake nzito ilisomeka hivi.

 

Mpenzi Nimoni

Salaamu, waama baada ya salamu usishangae kuwa nakuandikia barua ya kukuona wakati tupo wote hapa kambini, nimejitahidi kila namna nikueleze binafsi dukuduku langu lakini kila mara kunipiga changa la moyo.

Mpenzi Nimoni binadamu hukosea kwa hili hueleweka hata binadamu waligombana hupatanishwa isitoshe wewe au mimi kwa hali yoyote ile tunategemea msamaha toka kwa Mungu.  Tafadhali sana tusahau yaliyopita, kama ungekuwa rafiki tu tungeachia ngazi swala hapa ni uchumba maana lengo langu hasa ni kuoana na wewe.

Pia ni vipi upoteze wakati na huyo hohehahe Jeta? Au tuseme hiyo ndiyo maana ya kunikomoa? Jambo hili halivumiliki kwangu maana linanitia kichefuchefu, uchungu na aibu pia. 

Mpenzi nimeona ufikiri tena na utazame tulikotoka wewe nami. 

Wasalamu

Ndimi, Boaz

Sehemu hiyo ya barua ndiyo hasa iliyomgusa Nimoni. Mtoto wa watu hakawii kushikwa na hisia za mtu. Jumapili iliyofuata Nimoni na Jeta walikutana mafichoni kama kawaida yao, hapo ndipo Nimoni alipomsimulia Jeta juu ya Anita. 

Jeta hasa akajiona aliyebahatika kupendwa hakuwa na wivu zaidi alimshauri Nimoni. “Mpenzi” Jeta alisema kama Boaz ana nia njema nawe yafaa aheshimu hilo. Lakini ajue kama tutaendelea na hila hizi hasa kumuonyesha unyama, huenda akawa na chuki kali dhidi yangu. 

“Potelea mbali” Nimoni alisema ujue mapenzi kama mmea, ni mbegu tu inayokujakuchipua, kisha mmea unakua na kuzaa matunda. Siku moja ukinyauka na kufa siyo ajabu. Ingawa Jeta hakuridhika na majibu hayo hakuacha kujiuliza. Lakini kuchagua kupo, bado sijachelewa. Huyu Nimoni ana sababu zake za kunichagua hohehahe kama mimi. Kwanini sasa nisitamke ukweli?

Nimoni ingawa alikuwa na uhakika wa penzi la Jeta aligundua kuwa kulikuwa na mabadiliko. Mbona unaonekana kuwa mbali na hapa? Nimoni aliuliza kuna jambo gani unaliwaza? “sikiliza ewe mwana kung’ara”. Jeta alisema. Tumezoeana kiasi cha kutosha, kwanini tusiweke ahadi ya kuoana. Hakika ukiwa mchumba wangu nitafurahi sana. 

Hata mimi Nimoni alisema, najua tutapata kozi baada ya hapa na mwisho wa ajira. Tukiajiriwa tunaweza kuishi pamoja.  

SEHEMU B (ALAMA 60).

Jibu maswali matatu katika sehemu hii, swali la sita (6) ni lalazima.

 

ORODHA YA VITABU USHAIRI.

        Kimbunga             – Haji Gora.

Mapenzi Bora                   – Shaabani Robert Chungu Tamu                    – Theobald Mvungi.

Fungate ya Uhuru  – Mohamed Khatibu. 

 

RIWAYA.

Usiku Utakapokwisha       - Mbunda Msokile  Kufikirika         – Shaabani Robert.

        Mfadhili                 – Hussein Tuwa 

        Vuta N’kuvute                    – Shafi Adamu Shafi.

TAMTHILIYA.

Kwenye ukingo wa Thim   – Ebrahim Hussein.

        Morani                               – Emmanuel Mbogo

        Kivuli Kinaishi                 – Said Mohamed

        Nguzo Mama                    – Penina Muhando.

 

 

5.      Tathmini umuhimu wa dhamira zilizojadiliwa na wasanii wa diwani mbili ulizosoma kwa kutoa hoja nne (04) kutoka kila diwani. 

 

6.      “Mtindo ni mtu na muundo ni kipengele kinachohusu umbo au mwonekano wa kazi ya sanaa”. Kwa hoja nne (04) kutoka katika diwani mbili ulizosoma onesha namna kazi za wasanii zilivyoumbwa. 

7.      Kwa kutumia riwaya mbili ulizosoma eleza namna migogoro mingi katika jamii inayosababishwa na tamaa. Hoja tatu (03) kutoka katika kila kitabu. 

8.      “Rushwa ni adui wa haki” Jadili athari za rushwa kama mpokeaji na mtoaji hawatakomeshwa katika jamii, kwa hoja tatu (03) kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma. 

 

FORM SIX KISWAHILI EXAM SERIES 84  

FORM SIX KISWAHILI EXAM SERIES 84  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

image

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MKOA WA NJOMBE

MTIHANI KABLA YA MTIHANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA SITA

CODE: 121/1                                                                              KISWAHILI 1

MUDA: SAA 3                                         JUMATATU, 21 Agosti 2023, Asubuhi

image

MAELEKEZO

1. Karatasi hii inasehemu A na B yenye jumla ya maswali 8.

2. Jibu maswali yote katika sehemu A na maswali matatu (3) kutoka sehemu B swali la nane (8)    ni la lazima.

3. Soma maelekezo ya kila swali kwa umakini.

4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.

5. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

NAMBA YA

SWALI

WEKA VEMA(V)

WATAHINI TU

ALAMA

SAINI

1

 

 

 

2

 

 

 

3

 

 

 

4

 

 

 

5

 

 

 

6

 

 

 

7

 

 

 

8

 

 

 

JUMLA

 

 

SEHEMU A (Alama 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kwa makini kisha jibu kwa usahihi maswali yafuatayo:

Shafi alikuwa ni kijana mwenye ndoto nyingi za maisha ,kiasi kwamba  lau zingefanikiwa basi bila ya tone la shaka angeliishi maisha ya kifahari sana hata hivyo maisha yaliendelea nae akihangaika huku na kule, mchana na usiku akitafuta kazi nzuri ya kufanya lakini hakuambulia usumbufu na lugha ya kukatisha tamaa kila mahali alipokwenda kuomba kazi kwani hakua akikidhi vigezo vilivyokuwa vikiainishwa katika matangazo mbalimbali ya wanaohitajika.

Siku moja aliamka akiwaza sana juu ya haya maisha, anajiuliza kwanini maskini wanaendelea kuwa maskini na matajiri wanabaki na utajiri wao,akiiangalia familia yake haoni isipokuawa madhila tu yanayowaandama kwani kila mwezi lazima wasumbuliwe na mama mwenye nyumba kudai kodi yake na mara nyingine huwatishia hata kuwatimua na virago vyao na hapo ndio utabaini kuwa dunia haina huruma kwani majirani hukaa vibarazani wakifurahia yanayowatokea wengine ilihali wakijua wazi kuwa “shida ina miguu”.

Mara nyingi mtoto wa Shafi alililia vitu ovyovyo watoto wengine kwani naye alitamani avipate ila wapi, chakula tu kilikua cha kubahatisha ilimradi siku ipite,alipokua akimdai baba yake  basi alisema kesho nitakuletea zawadi nzuri kumbe ni danganya toto tu, kipato chake kilikua cha chini sana na hakikuweza kukidhi mahitaji hata yale ya msingi tu sembuse kununua midoli  ya kuchezea au chakula cha kujenga Afya mwilini.kweli wahenga hawakukosea waliposema   tamaa mbaya” kuna kipindi alitafuta njia ya mkato kwa kujihusisha na vikundi vya uporaji na ukabaji ili kujipatia kipato cha haraka kumbe alikua anajidanganya kwani alijikuta mikononi mwa polisi na kuiongezea mzigo familia yake kwa kulipa faini za mahakama . Alielewa kuwa anahitajika kufanya jitihada za taratibu katika kujikwamua katika umaskini alionao.

 

Hatimae aliamua maamuzi magumu kwa kujiunga kwenye ujasiriamali kwa kuuza mbogamboga, na hali ya maisha ilianza kubadilika kidogokidogo , bidii kubwa aliilekeza kwenye kupambana na maisha na sasa ameona mwanzo mpya , ama kweli Mungu hamtupi mja wake sasa anasadiki maneno yale aliyosoma kwenye kitabu cha “usiku utakapokwisha”, tabu na mashaka nayo yote yanaweza kuondoka moja baada ya jingine. Aliamini kua kama kijana mwenye nguvu ni lazima kupambana yeye mwenyewe na sio kuhangaika kutafuta kazi za maofisini tu, kuvaa suti kali, kiatu kizuri miguuni nakadhalika lakini jitihada za kuyafikia maisha hayo zinapogonga mwamba basi angalia namna ya kujikwamua pale ulipo, ni mfano wa kuigwa kwani sasa maisha yameanza kuwa mepesi na mazuri,akijikimu kwa chakula na mavazi mazuri. Ndoto zake zinaweza kuwa za kweli kama jitihada zake zitaendelea kuwa thabiti.

 

MASWALI

(a)  Andika kichwa cha habari uliyosoma kwa maneno yasiyozidi matatu.

(b)  Eleza maana ya maneno yaliyokolezwa wino kama yalivyojitokeza katika Habari        uliyosoma:

i.     Hakuambulia

ii.   Virago

iii.  Kipato

iv.  Tamaa.

v.   Anasadiki

vi.   Jitihada

(c)  Mwandishi ana maana gani anposema “shida ina miguu”

(d)  Eleza kwa ufupi dhana  ya “ Usiku utakapokwisha” kama habari inavyojieleza

2.      (a)Tumia O-rejeshi kuandika upya sentensi zifuatazo;

(i)       Aliingia mahali mna chatu

(ii)    Alighani shairi zuri sana

(iii)  Alinunua kiti kibovu

(iv)   Alivunja nazi mbovu

(v)     Alipata ugonjwa ambao haujulikani

 (b)Weka nomino zifuatazo katika ngeli husika kwa kigezo cha kisintaksia.

(i)       Mahali.

(ii)    Shairi.

(iii)  kiti.

(iv)   Nazi.

(v)     Ugonjwa.

3.      Badili vitenzi vifuatavyo viwe katika kauli iliyopo kwenye mabano mbele ya kitenzi husika na   uoneshe kiambishi cha kauli hiyo:

(i)       Fua (Utendea).

(ii)    Chukua (Utendwa).

(iii)  Pasua (Utendana)

(iv)   Hesabu (Utendeka).

(v)     Soma (Utendesha)

4.      Kwanini ni muhimu kuzingatia uhusiano baina ya wahusika wakati wa kutumia lugha? Eleza      kwa kifupi hoja tano (5) kwa mifano dhahiri.

SEHEMU B (ALAMA 60)

Jibu maswali matatu (3) kutoka sehemu hii swali la nane (8) ni lazima.

5.      Wewe ni mwanafunzi wa kidato cha tano Bondeni sekondari S.L. P 123 Geita, jina lako ni

Kiya Jumanne.Mwandikie barua mjomba wako wa S.L. P 343 Tabora kua unapenda kuhamia     Uchama sekondari S.L. P 550 Tabora.Andika barua kwa kuzingatia taratibu za uandishi wa      aina hiyo ya barua.

 

6.      “Matumizi ya lugha ya kwanza hua ni kufanikisha nia ya mawasiliano kabla mtu(mtoto)       hajajifunza lugha nyingine”. Eleza hoja tano (5) kwa mifano ni kwanini ni rahisi kwa mtu        (mtoto) kujifunza lugha ya kwanza ukilinganisha na lugha ya pili?

 

7.      “Mbali na BAKITA kuwa na mchango mkubwa sana katika ukuzaji na uendelezaji wa Lugha  ya kiswahili kupitia majukumu yake.chombo hiki kilianzisha idara mbalimbali za        taaluma”. Fafanua idara tano(5) kwa mifano anuai.

              

8.      Kazi nyingi za tafsiri za kifasihi zilishika kasi kuanzia karne ya 19, na karne ya 20 ilijulikana       kama karne ya tafsiri kutokana na wimbi la tafsiri ingawa tafsiri hiyo imekumbwa na       changamoto nyingi” Eleza kwa mifano changamoto tano(5) zinazojitokeza katika kufasiri        matini za kifasihi.

     

 

FORM SIX KISWAHILI EXAM SERIES 83  

FORM SIX KISWAHILI EXAM SERIES 83  

BARAZA LA WAKUU WA SHULE ZA KIISLAMU TANZANIA

MTIHANI WA UTAMILIFU WA SHULE ZA KIISLAMU KIDATO VI

KISWAHILI 1

121/1                         (Kwa Watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

 

MUDA: SAA 3                              Jumatatu Machi 06, 2023 mchana

image

                                                                                     

MAELEKEZO  

1.      Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali nane (8).

2.      Jibu maswali yote kutoka sehemu A na maswali matatu (3) kutoka sehemu B.

Swali la tano (5) ni la lazima.

3.      Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.

4.      Simu za mkononi na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.

5.      Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa Kijitabu chako cha Kujibia.

 

SEHEMU A (Alama 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata:

Niliota kwa yakini, niliota ndoto tatu.

Nalala usingizini, niliota mara tatu.

Ni kweli nawambieni, niliota siku tatu. Niliota ndoto tatu, maana yake ni nini?

 

Maana yake nini, kuota ndoto tatu.

Awezae kubaini, anieleze kiutu.

Na niliota kwanini, mfululizo siku tatu.

Niliota ndoto tatu, maana yake ni nini?

 

Nilipita darajani, njia ipitayo watu.

Hilo daraja kwa ndani, lina maji metu metu.

Na humo ndani majini, mna mzoga wa chatu.

Niliota ndoto tatu, maana yake ni nini?

 

Pili niliota baharani, mfano bahari yetu.

Zimo samaki majini, zaidi ya laki tatu.

Zina vichwa mkiani, si mfano wa za kwetu.

Niliota ndoto tatu, maana yake ni nini?

 

Tena zina vya kichwani, mfano kama za kwetu.

Kichwani na mkiani, vichwa viwili ni kitu.

Ni kitu kweli yakini, kushangaza vichwa vyetu.

Niliota ndoto tatu, maana yake ni nini?

 

Tatu naota nyumbani, nilikozaliwa kwetu.

Naota nyumba zamani, ya rahamu baba yetu.

Yaongezwa kwa hisani, juu kwa tofali tatu.

Niliota ndoto tatu, maana yake ni nini?

 

 

Nimesahau baini, ndoto ya pili si tatu.

Kwa ndoto ya baharini, nimemsahau mtu.

Alopita baharini, kwa baiskeli si yetu.

Niliota ndoto tatu, maana yake ni nini?

 

Anapopita majini, ajabu yake mwenzetu.

Nyuma yake mgogoni, kuna kauka kukutu.

Wanachuoni nipeni, ajabu ya ndoto tatu.

Niliota ndoto tatu, maana yake ni nini?

 

Hili si fumbo katani, ninaapa baraatu.

Siku moja na yakini, huziota ndoto tatu.

Na ndoto hizo amini, nimeota siku tatu.

Niliota ndoto tatu, maana yake ni nini?

 

Kaditama taabani, jibuni mambo kwa utu.

Msione hayawani, kwa kuwa za jambo butu.

Mnitoe ujingani, siniache zumbukuku.

Niliota ndoto tatu, maana yake ni nini?

 

Maswali

(a)   Pendekeza kichwa cha shairi kisichozidi maneno matano.

(b)   Bainisha makosa ya kisarufi yaliyojitokeza katika ubeti wa nne wa shairi.

(c)   Mwandishi wa shairi hili ametumia nafsi ya ngapi katika kituo bahari chake?

(d)   Toa maana za maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa na mshairi:

(i)                 Zumbukuku

(ii)              Kukutu

(iii)            Metumetu

(iv)             Butu

(v)               Rahamu

 

2.      Mwanaume mmoja anaweza kuoa mke zaidi ya mmoja kama ilivyo kwenye maneno ya Kiswahili neno moja huweza kuwa na maana zaidi ya moja. Tunga sentensi tano kwa kutumia neno “Panda”.

3.      Pesa huweza kubadilika jina kulingana na matumizi yake, ukiolea itaitwa mahari na ukilipia masomo itaitwa ada, na ukilipia huduma ya usafiri itaitwa nauli, sawa na maneno ya Kiswahili huweza kubadilika kutoka kategoria moja kwenda nyingine. Kwa kutumia sentensi badili maneno yafuatayo: (i) Mkulima (nomino kuwa kitenzi)

(ii)              Paa (kitenzi kuwa nomino)

(iii)            Mzuri (kiwakilishi kuwa kivumishi)

(iv)             Shambani (kielezi kuwa nomino) (v)     Piga (kitenzi kuwa kitenzi jina)

 

4.      Kirai ni aina ya tungo yenye neno moja au zaidi ambayo uhusiano wake umekitwa katika neno kuu. Kwa kutumia mifano jadili dhima tano (5) za tungo hiyo.

 

SEHEMU A (ALAMA 60)

5.      “Uteuzi wa lahaja ya Kiunguja kuwa lugha rasmi umepitia mchakato mrefu wa jasho na damu kwa watu wa Afrika Mashariki. Jadili ukweli wa kauli hii kwa kutumia hoja tano (5).

 

6.      “Taasisi na vyombo mbalimbali vilivyoundwa nchini Tanzania ili kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili ni sawa na mvuvi aliye baharini kwenye upepo mkali na mawimbi.” Thibitisha kauli hii kwa kutoa changamoto tano (5).

 

7.      Wewe ni mkazi wa Manga Mpakani wilayani Chalinze mkoani Pwani. Andika barua katika gazeti la Mwananchi kuhusu kero ya ubovu wa barabara kutoka Mbwewe hadi Manga Mpakani. Jina lako liwe Mdangirwa Kisakeni, anuani yako ni 8016.

 

8.      “Taaluma ya tafsiri na Ukalimani ni sawa na pande mbili za shilingi.” Thibitisha kauli hii kwa kutumia hoja sita (6).

 

 

 

FORM SIX KISWAHILI EXAM SERIES 57  

FORM SIX KISWAHILI EXAM SERIES 57  

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

OFISI YA MKUU WA MKOA KILIMANJARO

MTIHANI WA UTAMIRIFU KIDATO CHA SITA

KISWAHILI 2

MAELEKEZO

  1.   Karatasi hii ina sehemu mbili A na B zenye jumla ya maswali nane (8)
  2.   Jibu maswali yote sehemu A na maswali matatu (3) kutoka sehemu B
  3.   Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali
  4.   Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  5.   Andika namba yako ya mtihani katika kila kurasa ya karatasi utakayojibia.

 

SEHEMU A (ALAMA 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

  1.   Mhakiki wa kazi za fasihi simulizi ni mnyonyaji wa kazi asilia. Jadili kauli hii kwa kutoa hoja tano(5) zenye mashiko.
  2.   Fasihi ya Kiswahili ni ya muda mrefu tofauti na fasihi ya waswahili pamoja na fasihi kwa Kiswahili. Jadili changamoto mbalimbali zinazoifanya fasihi ya Kiswahili kukua, toa hoja tano(05)
  3.   Eleza sababu tano (05) za ufaraguzi wa fanani katika uwasilishaji wa kazi za fasihi simulizi.
  4.   Fafanua kwa kutoa mifano Dhahiri vipengele vya kisanaa vilivyo tumika katika shairi lifuatalo.

Hao miungu waliosimama,

Wambie waka echini warefu,

Kaeni chini wengi nyuma hatuoni,

Hatutaki venu vichafu, visogo kuona,

Ndugu kaeni chini kaeni chini ndiyo amri,

Achene kelele! Kelele zajaza tumbo,

Kaeni chini tulio nyuma yatuchoma moyo,

Twataka chagua watu! Watu! Watu hasa!

Ulipewa uongozi ukawapaka rangi nyingi,

Na madaraka madaraka yakawalevya,

Sasa yavueni wapisheni wenye nia.

Au hamjaona hasira ikifura ya wengi watu?

Ulizeni saidi aliyechomewa sokoni,

Na Abdala aliye mgonga maskini,

Miungu nanyi ndugu chini bwetekene

Tukanyage mpite mbele tujisukume 

Sisi twauza bidhaa ninyi mwauza maneno,

Tuko sawa haikai mdomoni.

 

Kateni yote misitu, fimbo tuenee,

Na vinyago tuwachongee watoto wachezee,

Kausheni yote maziwa, maji tuwalowanishe,

Kukipambazuka wasiweze ruka angani,

Kokeni moto, mashujaa wa uoneve tuwabanike,

Kamwe hapata kuwa kilio, wala matanga,

Bali hoi za ushindi na madaraka kwa umma.

 

SEHEMU B(Alama 60)

Jibu maswali matatu (03) katika sehemu hii, swali la tano ni lazima.

 

ORODHA YA VITABU

 

USHAIRI:

KIMBUNGA    - HAJI G HAJI

FUNGATE YA UHURU  - M.S.KHATIBU

MAPENZI BORA   - SHAABAN ROBERT 

CHUNGU TAMU    - T.A MVUNGI

 

RIWAYA:

KUFIKIRIKA    - SHABANI ROBART 

USIKU UTAKAPOKWISHA - MBUNDA MSOKILE

VUTA”NKUVUTE   - SHAFI A.SHAFI

MFADHILI    - HUSSEINI TUWA

 

TAMTHILIA:

NGUZO MAMA   - PENINA MHANDO

KIVULI KINAISHI   - SAID A. MOHAMED

KWENYE UKINGO WA THIM - E. HUSSEIN

MORAN    - EMANUEL MBOGO

 

  1.   Fasihi Andishi ya Kiswahili ni kapu kubwa lililosheni semi mbalimbali” Thibitisha usemi huu kwa kutumia Hoja tatu (03) kutoka katika kila Diwani mbili ulizosoma.
  2.   Ushairi ni dawa ya kutibu majeraha mbalimbali katika jamii” Tumia Diwani mbili katika ya ulizosoma darasani kuthibitisha usemi huu. Toa hoja tatu kwa kila Diwani.
  3.   Vijana si watu wazuri’ Thibitisha kauli hii kutoa hoja tatu(03) kwa kila Riwaya kutoka katika riwa mbili ulizosomo.
  4.   “Wahusika huweza kuanishwa kwa kutumia vigezo viwili, yaani majukumu yao na tabia zao, kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma fafanua aina ya wahusika kwa kigezo cha tabia. Toa hoja tatu (03) kwa kila tamthiliya.

FORM SIX KISWAHILI EXAM SERIES 44  

FORM SIX KISWAHILI EXAM SERIES 44  

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

OFISI YA MKUU WA MKOA KILIMANJARO

MTIHANI WA UTAMIRIFU KIDATO CHA SITA

KISWAHILI 1

MAELEKEZO

  1.                Karatasi hii ina sehemu mbili A na B zenye jumla ya maswali nane (8)
  2.                Jibu maswali yote sehemu A na maswali matatu (3) sehemu B
  3.                Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali
  4.                Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  5.                Andika namba yako ya mtihani katika kila kurasa ya karatasi utakayojibia.

 

SEHEMU A (ALAMA 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

  1.                Soma kifungu cha habari kifuatacho kwa makini kisha jibu kwa usahihi maswali yanayofuata.

 

Nilianza katika dimbwi la mawazo kiasi cha kuhama nlipokua ooh! Maskini kwanini hakusikiliza ushauri? Ama kweli asiyesikia la mkuu huvunja guu, “mkataa pema pabaya panamwita”. Dimbwi hili la mawazo liliwahusu Gobosi na Simosa, vijana walikua maarufu katika kijiji chetu. Gobosi alikuwa mvulana rijali jamaa wa miaka 19 na Simosa alikuwa msichana mrembo wa miaka 20. Vijana hao walikuwa viongozi wa wanafunzi katika shule ya sekondari Jitambueni.

 

Baada ya kuhitimu kidato cha sita. Simosa alifaulu na hivyo alijiunga katika chuo kikuu cha kilimo Sokoine kilichopo Morogoro, yeye alipenda kilimo na ufugaji. Gobosi alichaguliwa kujiunga katika chuo kikuu cha Mzumbe kusomea shahada ya uongozi. Wanakijiji tulifurahi sana tulikuwa na matarajio makubwa kwa wasomi haw.

 

Siku moja ya asubuhi nilipata fununu iliokuwa ikisambaa kijijini kumhusu Gobosi. Moyo ulienda mbio na macho ya wengi yalibaki yakitiririka machozi na kuondolewa. Ooh! Maskini Gobosi! Mzee mmoja alisikika. Kumbe alipofika Mzumbe alijiunga na makundi ya vijana wa mtaani wanaotumia dawa za kulevya. Ni mwaka mmoja sasa umepita tangu alipojiunga na chuo kikuu. Saa akili zimeruka na amekua teja! Hawezi tena kusoma wazazi wake walimpeleka Hospital ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu lakini bado hali haikuwa nzuri. Baada ya kuanza dawa za kulevya alianza kuwa mgomvi.

 

Siku moja alipigana na mwenzake ambaye alimpiga jiwe kichwani na kuharibu sehemu ya ubongo wake. Ndoto zake zote zimepotea. Wazazi na jamii tumepoteza nguvu kazi ya Taifa. Alishauriwa sana aachane na vikundi hivyo lakini hakusikia, hakika mkaidi hafaidi mpaka siku ya Idd. Ghafla nilianza kusinzia kwa huzuni ya moyo na kutokomea katika ulimwengu wa njozi.

 

MASWALI

  1.                Andika kichwa cha habari uliyosoma kisichozidi maneno (5)
  2.               Eleza maana ya maneno au vifungu vya maneno ka ilivyotumika katika habari uliyosoma
  1. Dimbwi la mawazo
  2. Ulimwengu wa njozi
  3. Fununu
  4. Tokomea
  5. Teja
  1.                Methali “Asiyesikia la mkuu huvunjiaka guu” inasaidia vipi katika habari uliyosoma? Toa hoja tatu.
  2.               Kutokana na habari uliyosoma, mada ya ufahamu ina manufaa gani kwako? Eleza manufaa gani kwako matatu.
  1.                Katika kila tungo zifuatazo taja kielezi na fafanua aina ya kielezi hicho.
  1.                Amekaa juu ya nyumba
  2.               Anapigana kishujaa
  3.                Hospital imefungwa kwa mara ya tatu.
  4.               Nitaondoka asubuhi na mapema.
  5.                Ameelekea upande wa kulia
  1.                Umbo la O-rejeshi lina majukumu mbalimbali katika tungo. Bainisha majukumu matano (05) ya umbo hilo kwa mifano
  2.                Wewe kama mtu unayemudu v izuri lugha ya Kiswahili, unafikiri ni mambo gani yanaweza kupoteza uwezo wako wa kuimudu lugha hiyo? Toa hoja tano (05)

 

SEHEMU B (ALAMA 60)

Jibu maswali matatu (03) katika sehemu hii. Swali la nane (08) ni lazima

  1.                Wewe ni Afisa Habari wa shirika la ndege Tanzania, andika kwa tangazo kwa abiria kuhusu katizo la usafiri wa ndege NAMBA JET 343 iliyokuwa ifanye safari yake toka Songea kwenda Zanzibar siku ya Ijumaa tarehe 25/12/2022 saa 12 asubuhi, kuwa safari hiyo itafanyika siku ya Jumapili ya tarehe 27/12/2022 saa 8 Mchana. Mabadiliko haya yanatokana na kuchafuka kwa hali ya hewa angani. Jina la mtoa tangazo ni Kudura Riziki.
  2.                “Kushuka kwa hadhi ya Kiswahili toka uhuru hadi leo kunasababishwa na watanzania wenyewe” Thibitisha dai hili kwa hoja tano (5) na mifano Dhahiri.
  3.                Kamati ya usanifishaji wa lugha ya Kiswahili. The Inter-territorial Language Swahili Committee ilipoundwa mwaka 1930 ilikabidhiwa majukumu mbalimbali. Eliza majukumu sita (6) ya kamati hiyo
  4.                (a)Fafanua dhima na udhaifu wa Tafsiri ya Kisemantiki na Tafsiri ya Kimawasiliano.

(b) ‘Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, dhana ya Ukalimani inahitajika katika shughuli mbalimbali za kila siku’ Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja nne(04)

FORM SIX KISWAHILI EXAM SERIES 43  

FORM SIX KISWAHILI EXAM SERIES 43  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

(TAMISEMI)

MTIHANI WA UTIMILIFU KANDA YA KUSINI

(LINDI NA MTWARA)

121/2                                                         KISWAHILI 2

(Kwa watahiniwa walioko na wasiokuwa shuleni)

Muda: Saa 3                                                                                      04-02-2022 Ijumaa Asubuhi.

image

Maelekezo kwa Watahiniwa

1.    Mtihani huu una sehemu A na B zenye jumla ya maswali nane (8).

2.    Jibu maswali yote sehemu A na sehemu B jibu maswali matatu (3) swali la tano (5) ni la lazima.

3.    Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.

4.    Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.


SEHEMU A (ALAMA 40)

Jibu maswali yote kutoka sehemu hii.

1.    Kwa kutumia mifano, elezea kwa sababu gani vitendo vya wahusika katika fasihi simulizi ni vya muhimu. (Toa hoja tano)

2.    Eleza matatizo ya usambaaji wa sanaa za maonesho nchini Tanzania kwa kutoa hoja tano (5).

3.    Mwandishi yeyote wa kazi ya fasihi anahitaji kile kinachoitwa uhuru wa mwandishi na ili uhuru wa mwandishi uthibitike kuwa upo, mambo kadhaa ni lazima yadhihirike kwa mwandishi husika. Eleza kwa mifano.

4.    Soma makala ifuatayo kisha chambua mbinu za kifani zilizotumika.

Uwapi uzuri wako, haupo umepotea

Ya wapi malingo yako, na hashuo za dunia

Leo upo peke yako, sote tumekukimbia

Sasa ni chano cha maji, watu wajichanyatia Umekwisha ujuaji, haya zimekupotea yale usiyotarajia, kwako yamekuhamia

Bao la mkahawani, kila mtu akalia

Juhaha huna usoni, na wala sitara pia

Wenyeji wote mjini, wamekwisha kupitia

Sasa jamvi la wageni, wajapo huwapokea

Imekutoka thamani, Mtu duni mebakia

Hata mbwa wa mjini, kikuona hukimbia.

SEHEMU B (ALAMA 60)

Jibu maswali matatu (3) kutoka sehemu hii swali la tano (5) ni la lazima.

ORODHA YA VITABU

(A) USHAIRI

Kimbunga

-

Haji G. Haji

Mapenzi Bora

-

Shaban Robert

Chungu tamu

-

Theobald Mvungi

Fungate ya Uhuru

(B) RIWAYA

-

Mohamed S. Khatibu

Usiku utakapokwisha

-

Mbunda Msokile

Kufikirika

-

Shaban Robert

Mfadhili

-

Hussein Tuwa

Vuta N’kuvute

(C) TAMTHILIYA

-

Shafi Adam Shafi

Kwenye Ukingo wa Thim

-

Ibrahim Hussein

Morani

-

Emmanuel Mbogo

Kivuli kinaishi

-

Said Mohamed

Nguzo Mama

-

Penina Muhando

5.    “Juhudi za kimaendeleo za wanajamii zinakwamishwa na vitendo vya viongozi wao vinavyosababishwa na matendo yao maovu dhidi yao” Jadili kauli hii kwa kukubali au kukataa. Tumia diwani mbili ulizosoma kwa kutoa hoja nne kutoka kila diwani.

6.    “Lugha ni uti wa mgongo wa kazi za fasihi pasi na kuwepo matumizi ya lugha kazi ya fasihi haitajengeka na hakuna fasihi” Kwa kutumia kauli hiyo juu ya umuhimu wa lugha, eleza matumizi ya Tamathali za semi katika diwani mbili ulizosoma.

7.    “Taifa litajengwa na watu wenye moyo”. Fafanua usemi huu kama ulivyotumika katika riwaya mbili ulizosoma kwa kutoa hoja nne kwa kila kitabu, kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.

8.    “Mwandishi Mwanamke-kwani mwanamke nani? Kila cha maana hubebwa na mwanaume, kazi ya mwanamke ni kuzaa, kupika na kumtumikia mume” Kwa kutumia kauli hii batilisha nafasi ya mwanamke kama alivyotukuzwa na waandishi wa tamthiliya mbili ulizosoma. Toa hoja nne kutoka kila tamthiliya.

FORM SIX KISWAHILI EXAM SERIES 23  

FORM SIX KISWAHILI EXAM SERIES 23  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

(TAMISEMI)

MTIHANI WA UTIMILIFU KANDA YA KUSINI

( LINDI NA MTWARA)

121/1KISWAHILI 1

(Kwa watahiniwa walioko na wasiokuwa shuleni)

Muda: Saa 301-02-2022 Jumanne Asubuhi.

Maelekezo kwa Watahiniwa

1.Mtihani huu una sehemu A na B zenye jumla ya maswali nane (8).

2.Jibu maswali yote sehemu A na sehemu B jibu maswali matatu (3) swali la nane (8) ni la lazima.

3.Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.

4.Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (ALAMA 40)

Jibu maswali yote kutoka sehemu hii.

1. Soma habari ifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.

Ilikuwa jioni mishale ya saa kumi ilipotimia ndipo niliposikia tangazo kutoka kwa waziri mkuu kuwa yule mgeni tuliyemsikia siku nyingi zilizopita amewasili nyumbani kwetu. Tangu muda huo sote tuliingiwa na huzuni nyingi na mfadhaiko mkubwa sana, tukanyong’onyea kama puto lililotolewa upepo. Baada ya tangazo la waziri mkuu kuisha, mkuu wa shule alimwambia kiranja mkuu agonge kengele. Sote tulikusanyika uwanja wa matangazo mithili ya ng’ombe walioko machinjioni wakisubiri kuchinjwa. Mkuu wa shule akagonga msumari kwenye kidonda ambacho kilikuwa bado kibichi kwa kutangaza kuwa kila mwanafunzi anatakiwa kurudi kwa wazazi wake kama tangazo la waziri mkuu lilivyoelekeza. Nikajisemea moyoni mwangu “Mbuzi wa maskini hazai na hata akizaa huzaa dume.”

Siku iliyofuata sote tulirejea kwa wazazi wetu. Mimi nilifurahi kuonana na wazazi wangu, ndugu, jamaa na marafiki. Tuliendelea kuishi kwa pamoja kwa upendo huku tukisikiliza taarifa na maelekezo kutoka kwa viongozi wetu kuhusiana na mgeni aliyeingia ndani mwetu. Mengi yalisemwa kuhusiana na mgeni huyu. Baadhi ya yaliyosemwa ni kuwa mgeni huyu ni hatari, akikualika hudhofisha mfumo wa upumuaji, hubana kifua , hukwaruza koo, husababisha kikohozi, homa na mambo mengine kibao.

Ili tumuepuke mgeni huyo tuliambiwa tunawe mikono mara kwa mara, tusikumbatiane, tukoholee kwenye kiwiko cha mkono na tusisafiri pasipo na ulazima. Tulikaa nyumbani hadi tukachoka, tukakumbuka shule maana hata vituo vya masomo ya ziada vilifungwa na wazazi wangu walikuwa hawataki hata nisogelee mlango wa geti.

Siku moja mama alinituma sokoni. Nikapitia kwa mpenzi wangu aliyekuwa anafanya kazi katika kampuni ya kitalii. Alihamdulilah! Nikamkuta na nilivyokuwa nimemkumbuka laazizi Mahabuba wangu nikamrukia mithili ya paka arukiaye panya akiwa na njaa. Naye bila ya hiyana akanipokea kwenye uwanja wa sita kwa sita. kilichoendelea hata sielewi maana nilipozinduka nilijikuta nimevaa suti ya asili. Nikavaa nguo zangu juu ya suti ya asili nikarudi nyumbani. shule zilipofunguliwa nilirudi shuleni wiki moja baadae tukapimwa afya. Yeleuwi! nilibainika kuwa nimejaa uzito, nikarudishwa kwa wazazi wangu. hapo ndipo ndoto za kuwa rubani zimepotea maana wazazi ni hohehahe.

Amakweli majuto ni mjukuu na mtaka yote kwa pupa hukosa yote.

Maswali:

(i)Andika kichwa cha habari uliyosoma kwa maneno yasiyozidi matatu.

(ii)Neno “Mgeni” lina maana gani?

(iii)Akagonga msumari kwenye kidonda kibichi, msemo huu una maana gani?

(iv)Kwanini msimuliaji anarudishwa kwa wazazi wake baada ya shule kufungwa.

(v)Fupisha habari uliyosoma kwa maneno sitini (60).

2.(a) Mofu ni nini?

(b) Kwa mifano dhahiri eleza aina tano (5) za mofu.

3.Toa maana ya Istilahi zifuatazo kama zilivyotumika katika lugha ya kiswahili.

(i)Ngeli za nomino

(ii)Kirai

(iii)Sentensi

(iv)Alofoni

(v)Mofimu

4.Fafanua mambo matano (5)yanayomwongoza mtumiaji wa lugha ya kiswahili katika uteuzi wa rejesta.

SEHEMU B (ALAMA 60)

Jibu maswali matatu (3) kutoka sehemu hii swali la nane (8) ni la lazima.

5.Wewe ni mwenyekiti wa kijiji cha Amani mtaa wa Miembe 7 jina lako bwana Ayubu Mkoni. Andika ripoti ya taarifa kwa polisi kuhusu tukio la ajali ya moto lililotokea mtaani kwako saa 8:00 usiku wa tarehe 02/09/2021.

6.Fafanua michango mitatu (3) ya kila taasisi zifuatazo katika kusimamia lugha ya kiswahili.

(i)Taasisi ya Elimu Tanzania (T.E.T)

(ii)Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (T.E.W.W)

7.“Utawala wa mwingereza nchini Kenya ni chanzo cha mweneo mdogo wa kudidimia kwa kiswahili nchini humo”. Fafanua dai hilo kwa hoja sita (6).

8.Kwa kutumia mifano, fafanua kauli inayosema “Mfasiri ni mhaini”. Toa hoja tano.

FORM SIX KISWAHILI EXAM SERIES 19  

FORM SIX KISWAHILI EXAM SERIES 19  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256