OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MKOA NA SERIKALI ZA MTAA
MTIHANI WA NUSU MUHULA WA PILI
SEPTEMBA-2022
KISWAHILI KIDATO CHA NNE
MAELEKEZO
SEHEMU A
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
ORODHA A | ORODHA B |
|
|
SEHEMU B (Alama 40)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
(b)Msimu huwa na sifa za kuendana na wakati, taja misimu mine iliyozuka kipindi cha serikali ya awamu ya tano nchini Tanzania
Amani. Amani!
Amani huyu ndio wimbo unaohitajika kusikika masikioni mwa vizazi vyetu vilivyopo lakini na vijavyo. Huu ndo ulikuwa wosia alikuwa akiutoa mzee mmoja aitwae Majanga kwa watoto wake. Lakini pia kwa wajukuu zake. Baada ya maneno hayo mjukuu mmoja alimuuliza babu yake, kwa nini unapenda tuimbe Amani siku zote? Mzee Majanga alisema yafuatayo : Amani ndio kila kitu Amani huleta umoja na mshikamano, Amani huleta maendeleo, Amani hufanya watu kulipa hata maduhuli ya serikali, Amani hufanya watu kutunza na kulinda miundombinu mbalimbali, Amani huwafanya watu kulala fofofo, Amani huwafanya watu kujenga majumba ya kifahari, Amani huwafanya watu kula chakula na kushiba, Amani inawafanya watu kuongeza familia. Amani ni kila kitu mjukuu wangu.
Baada ya maelezo hayo yote mjukuu wa pili wa mzee Majanga alimuuliza babu yake swali tena. Kwani babu Amani kutoweka inasababishwa na nini? Mzee majanga alimueleza mjukuu wake yafuatayo. Kuna vitu na mambo mengi yanayoweza kufanya Amani ipotee miongoni mwao ni pamoja na ufisadi wa viongozi, uongozi mbaya, ukosefu wa haki miongoni mwa watu, matumizi. Matumizi mabaya ya rasimali za nchi, ukabila, vifo vya watu na hudumu mbovu kwa wananchi. Punde si punde mjukuu wa tatu aliuliza swali kwa babu yake kuwa kwani Amani ikipotea kunatokea madhara gani? Babu alimjibu mjukuu wake kwa kusema kuwa, kwanza usiombe Amani hata ya familia ikipotea maana madhara yake huwezi kuyamudu hata siku moja.
Kwanza watu hugeuka na kuwa watumwa nchini mwao. Pili vifo kuongezeka, uharibifu wa miundombinu mfano barabara, reli n.k njaa kali, nchi kumwaga damu, maandamano yasiyoisha, hudumu zote za kijamii kuzorota kwa ujumla na hakuna awezaye kufanya lolote lenye tija sehemu ambayo haina Amani. Babu alihitimisha wosia wake kwa kuwakumbusha wajukuu zake kuwa wawe mstari wa mbele kuziunga mkono juhudi za mfalme wao anazozifanya ikiwa ni pamoja na kupiga vita rushwa na ufisadi, kujenga uchumi, kujenga aina zote za miundombinu, kuboresha usafiri wa angani na majini lakini kikubwa zaidi kutumia fursa ya elimu bila malipo
Kabla babu hajakataa roho aliwambai wajukuu zake kuwa “Amani ikipotea huwezi kuirudisha kwa urahisi ni bora njaa ya tumbo kuliko njaa ya akili.”
Maswali
(ii) Je unahisi Amani ikipotea madhara yake huwa ni makubwa sana? Taja mawili tu.
SEHEMU C (Alama 45)
Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii.
ORODHA YA VITABU TEULE KWA SWALI LA 10 – 12
USHAIRI
Wasakatonge - M.S Khatibu (DUP)
Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP)
Mashari ya Chekacheka - T.A Mvungi (EP & D.LTD)
RIWAYA
Takadini - Ben J. Hanson (MBS)
Watoto wa Mama Ntilie - E. Mbogo (H.P)
Joka la Mdimu - A.J.Safari (HP)
TAMTHILIYA
Orodha - Steve Raynolds (MA)
Ngoswe Penzi kitovu cha Uzembe - E.Semzaba (ESC)
Kilio chetu - Medical Aid Foundation
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 123
Namba ya Mwanafunzi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
JULAI 2022
KISWAHILI KIDATO CHA NNE
MAELEKEZO
SEHEMU A (ALAMA 15)
1.Jibu maswali yote Katika sehemu hii,
(i) Ni aina ya wahusika ambao hawabadiliki na wamepewa majina ambayo humfanya msomaji aelewe tabia na matendo yao;
(ii) Vishazi tegemezi vimegawanyika katika aina kuu mbili ambazo ni;
(iii) Anatoa ufafanuzi juu ya ubantu wa Kiswahili kwa kuelezea wakazi wa mwambao waliojulikana kama "Wazanji" na watawala wao waliojulikana kama "Wakilimi"
(iv) Ni lahaja zinazopatikana Mombasa;-
(v) Mofimu ku iliyopigiwa mstari imebeba dhima gani katika kitenzi sikukukumbuka
(vii) Sehemu ya mzizi asilia iliyoambikwa kiambishi "a" mwishoni
(viii) Ni tamathali ya semi ambayo Jina la mtu hutumiwa kwa watu wengine wenye tabia, mienendo, hulka au kazi sawa na mtu huyo
(ix) Neno SHADARA limepatikana Iwa kutumia njia gani ya uundaji wa maneno?
(x) Chama cha kukuza na kueneza Kiswahili "TAKILUKI" kilianzishwa mwaka
(xi) Aina ya hadithi za ngano zenye wahusika wanyama tu hujulikana kama,
2. Chagua kifungu cha maneno kutoka orodha B kinachotoa maelezo sahihi ya maneno neno katika orodha A.
ORODHA A | ORADHA B |
|
|
SEHEMU B ( Alama 40)
3. Bainisha aina ya kauli katika vitenzi vilivyopigiwa mstari, huku ukifafanua kiambishi kinachojenga kauli hiyo katika tungo zifuatazo.
(i) Matukio ya ubakaji yanaogofya
Waoga wanafahamika
(iii) Nyumba itajengwa na wazazİ
(iv) Dawa za kienyeji zilimlevya sana
4. Huku ukuota mifano. Fafanua dhima nne za mofimu "M" katika lugha ya Kiswahili.
5. Fafanua kwa hoja nne, mambo yanayothibitisha kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni pwani ya Afrika ya Mashariki,
6. Methali hutawaliwa na vipengele mbalimbali vya lugha, onesha vipengele vya lugha vilivyotumika katika utunzi wa methali zifuatazo.
(i) Kibuzi na kibuzi hununa jahazi
(ii) Akili ni mali
(iii) Farasi hamuwawezi, tembo mtawalishani?
(iv) Baniani mbaya kiatu chakc dawa.
(v) Avumayc 'baharini papa, kumbe wengine wapo
7. Soma shairi lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata Mtu wa fikra njema, kwa watu umcacha jina
Chuma chetu imara, Afrika na dunia nzima,
Mikakati imara lojenga, Tanzania nuru kuangaza
Jiwe Ietu limeondoka takuenzi daima
Katika yote dunia, Jinalo lilivema
Misimamo yenye mashiko, ndiyo yako şifa njema
Nia kubwa kujenga, boma, ndiyo ndoto yako imara
Chuma chetu kimelala, hakika umeacha alama
'Umoja uliujenga, utengano likemea
Uchapakazi ulihimiza, nani alibaki nyuma?
Macndeleo kuyajcnga, Elimu hukuacha nyuma.
Nguzo yetu imeinama, nyoyo zetu zimechutama
Wangu wosia naweka, aloacha kuyaenzi
Uzalendo tuudumishe, Ufisadi tuupinge
Vizazi vijavyo tupate hadilhia, mazuri ya mwamba wetu.
Takuombea daima, lalc kwa ushindi shujaa.
Maswali
(a) (i) Shairi hili limejegwa kwa kutumia muundo gani?
(ii)Fafanua mambo ya msingi yakuzingatia wakati wa uchambuzi wa muundo katika ushairi (Hoja Nne)
(b) Onesha upekee wa mıvandishi katika shairi hili (Hoja Nne)
(c) Mwandishi ana maana gani anaposema jiwe, mwamba chuma na nguzo?
(d) Andika kichwa cha habari cha shairi hili.
(e) Mwandishi anahimiza nini katika kumuenzi shujaa.
8. Kijiji chenu cha Kiloza kimeanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji. Wewe kama afisa manunuzi, andika barua katika kampuni ya Olotu inayojihusisha na uuzaji pembejeo za kilimo kuangiza bidhaa zitakazotumika katika kuendesha mradi. Jina lako ni Ombeni Mtapewa.
SEHEMU C (Alama 45)
Jibu maswali matatu kutoka katika sehemu hii.
9. Ni kweli kwamba lugha ya Kiswahili imevuka mipaka na kuenea katika maeneo mbalimbali duniani. Thibitisha ukweli wa dai hili (Hoja - 5)
TAMTHILYA
Orodha - Steve Reynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe -E. Semzaba (ESC)
Kilio chetu - Medical Aid Foundation
RIWAYA
Takadini - Ben Hnson (MBs)
Mamantilie - Emanuel Mbogo
Joka la mndimu - A. J. Safari (HP)
USHAIRI
Cheka cheka - T. Muungi
Malenga wapya - Takiluki
Wasaka tonge - Mohamed Seif Khatibu
10. Washairi ni wataalamu wazuri na waliobobea katika kutumia jazanda zinazotoa ujumbe kwajamii. Tumia jazanda tatu kwa kila diwani mbili uliyosoma.
11. Lugha ni kipengele cha msingi katika ujenzi wa kazi ya fasihi ambayo husaidia katika kufikisha wazo la msanii kwa jamii. Kwa kutumia riwaya teule mbili (2) ulizozisoma. Jadili jinsi wasanii wa riwaya hizo walivyotumia kipengele cha tamathali za semi hoja Sita (6)
12. Mwandishi ni Mjenzi wa jamii. Thibitisha ukweli wa dai hili kwa kutoa hoja tatu kutoka katikaTamthilia mbili ulizozisoma
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 101
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
KISWAHILI KIDATO CHA NNE
MUDA: SAA 3:00 MAY 2022
MAELEKEZO
SEHEMU A
Jibu maswali yote katika sehemu hii
ORODHA A | ORODHA B |
|
|
SEHEMU B (Alama 40)
Jibu maswali yote ya sehemu hii kwa kuzingatia maelekezo ya kila swali.
SEHEMU C (Alama 45)
Jibu maswali matatu (3) kutoka sehemu hii
ORODHA YA VITABU
USHAIRI
Wasakatonge M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya chekecheka T.A. Mvungi (EP&D.LTD
RIWAYA
Takadini Ben J. Hanson (MBS)
Watoto wa Mama N’tilie E. Mbongo
Joka la mdimu A.J. Safari
TAMTHILIA
Orodha Steve Reynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe E. Semzaba (ESC)
Kilio Chetu Medical Aid Foundation (TPH)
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 97
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
PRESIDENT’S OFFICE REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT
FORM IV MOCK EXAMINATION 2022
012 HISTORY
TIME: 3:00 HOURS JULY, 2022
INTRUCTIONS
SECTION A (20 MARKS)
Answer all questions in this section.
LIST A | LIST B |
|
|
SECTION B (35 MARKS)
Answer all question in this section
B) Outline at least five features of colonial transport and communication networks during colonial rule.
SECTION C: (45MARKS)
ANSWER THREE (3) QUESTIONS FROM THIS SECTION
1
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 94
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
KIDATO CHA NNE
021KISWAHILI
MUDA: SAA 3:00 2021
MAELEKEZO
SEHEMU A (Alama 10)
SEHEMU B (Alama 5)
KIFUNGU A | KIFUNGU B |
|
|
KIFUNGU: A | | | | | |
KIFUNGU B |
|
|
|
|
|
SEHEMU C: ALAMA 40;
Jibu maswali yote katika sehemu hii
Utu wa binadamu, ni kama yai na kuku,
Utu niile nidhamu,mola aliyo kukhuluku,
Ubinadamu ni damu,ya utu wa kila siku,
Utu wowote wa mtu,ni kuwajali wenzake.
Yeyote mwanadamu, ana asili ya mtu,
Yaani kwenye yake damu, hakikosi hiki kitu,
Utu sifa maalum,ya mtu kuitwa mtu,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake.
Utu ni kiumbe hai, tunacho chaonekana,
Utu kamwe haudai, tabia ya kujivuna,
Utu ni ule uhai,ushikao uungwana.
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake
Utu unayo aibu, na tabia ya muhali,
Utu huenda na jibu,kila imani na ukweli,
Utuwe hauna tabu,tabia ya ujalili,
Utu wowote wa mtu,ni kuwajali wenzake.
MASWALI
SEHEMU D(Alama 45)
Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii swali la 9 ni lazima
9. Ukiwa kiongozi wa michezo katika shule ya Sekondari Kizota S L P 30 Dodoma, andika barua kwa mkuu wako wa shule kupitia kwa mwalimu wa michezo kuomba kuongezewa siku za michezo shuleni. jina lako liwe Sikunjema Afya.
10 “Msanii ni kinda la jamii husika anayoandika kuihusu jamii hiyo”. Jadili kauli hii kwa kutumia hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili zilizoorodheshwa.
11. “Wahusika katika kazi za fasihi ni mfano wa kuigwa na jamii kwa tabia na matendo yao”. Thibitisha kauli hii kwa kutumia hoja tatu kwa kila mhusika kutoka katika tamthilliya mbili zilizoorodheshwa.
12.Elimu ni ufunguo wa Maisha. Fafanua kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu kati ya vitabu viwili vya riwaya vilivyoorodheshwa.
ORODHA YA VITABU
USHAIRI
Wasakatonge M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka T.A.Mvungi (EP & D.LT.D)
RIWAYA
Takadini Ben J. Hanson (Mbs)
Watoto Wa Mama N’tilie E. Mbogo (H.P)
Joka La Mdimu A.J.Safari (H.P)
TAMTILIYA
Orodha Steve Reynolds (Ma)
Ngoswe Penzi Kitovu Cha Uzembe E.Semzaba (Esc)
Kilio Chetu Medical Aid Foundation(Tph)
1
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 91
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
021 KISWAHILI
MUDA: SAA 3:00 APRILI: 2022
MAELEKEZO
1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, na D
2. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali.
3. Majibu yote yaandikwe kwa wino wa bluu au mweusi.
4. Jibu maswali yote katika sehemu A, B, C na maswali matatu sehemu D, swali la tisa ni lazima.
SEHEMU A (Alama 10)
1.Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herefu ya jibu hilo.
i) Ni jambo gani linalodhihirisha umbo la nje ya kazi ya fasihi?
ii) Ni sehemu ya neno ambayo huweza kutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti.
iii) leta wali kuku.hii ni aina gani ya rejista?
A. Rejesta ya Hotolini
B. Rejesta ya Hospitalin
C. Rejesta ya Mtaani
D. Rejista ya Shambani
iv) Ipi maana inayoelekeana na methali hii? ‘chanda chema huvikwa pete’
v) ..........ni hadithi zinazozungumzia matukio ya kihistoriya.
vi) Mara nyingi fasihi simulizi huzingatia uwepo wa;
vii)Upi ni mzizi wa neno anakula?
viii)Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi Fulani ya kifasihi?
ix) Neno lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza mtenda au mtendwa?
x) Ni sifa ipi haitofautishi fasihi simulizi na fasihi andishi?
SEHEMU B (Alama 5)
2. Oanisha sentensi za kifungu A, kwa kuchagua jibu sahihi katika kifungu B, andika jibu lako kwa usahihi katika kisanduku ulichopewa hapo chini;
KIFUNGU A | KIFUNGU B |
|
|
KIFUNGU: A | I | II | III | IV | V |
KIFUNGU B |
|
|
|
|
|
SEHEMU C: ALAMA 40
Jibu maswali yote katika sehemu hii
3. Eleza maana ya kielezi kwa kutoa mfano wa sentensi moja.
4. Kwa kila tungo uliyopewa pigia mstari kielezi na kisha taja ni kielezi cha aina gani?
i) Darasani kuna utulivu mkubwa.
ii) Wanafunzi wanaimba kimasihara.
iii) Mwalimu amerudi tena.
iv) Nitaondoka wiki ijayo.
5. Toa maana tano (5) za neno “Kibao” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana ulitoa.
6.Taja njia nne (4) zitumikazo kuunda misamiati na utoe mfano kwa kila njia.
7. Taja aina mbili za Mashairi na maana zake.
8. Soma shairi lifuatalo kisha jibu sehemu hii.
Utu wa binadamu, ni kama yai na kuku,
Utu niile nidhamu, mola aliyo mtunuku,
Ubinadamu ni damu, ya utu wa kila siku,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake.
Yeyote mwanadamu, ana asili ya mtu,
Yaani kwenye yake damu, hakikosi hiki kitu,
Utu sifa maalum, ya mtu kuitwa mtu,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake.
Utu ni kiumbe hai, tunacho chaonekana,
Utu kamwe haudai, tabia ya kujivuna,
Utu ni ule uhai, ushikao uungwana.
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake
Utu unayo aibu, na tabia ya muhali,
Utu huenda na jibu, kila imani na ukweli,
Utuwe hauna tabu, tabia ya ujalili,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake.
MASWALI
SEHEMU D (Alama 45)
Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii swali la 9 ni lazima
9. Ukiwa kiongozi wa michezo katika shule ya Sekondari Kizota S L P 30 Dodoma, andika barua kwa mkuu wako wa shule kupitia kwa mwalimu wa michezo kuomba kuongezewa siku za michezo shuleni. jina lako liwe Siku njema Afya.
10 “Msanii ni kinda la jamii husika anayoandika kuihusu jamii hiyo”. Jadili kauli hii kwa kutumia hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili zilizoorodheshwa.
11. “Wahusika katika kazi za fasihi ni mfano wa kuigwa na jamii kwa tabia na matendo yao”. Thibitisha kauli hii kwa kutumia hoja tatu kwa kila mhusika kutoka katika tamthilliya mbili zilizoorodheshwa.
12.Elimu ni ufunguo wa maisha. Fafanua kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu kati ya vitabu viwili vya riwaya vilivyoorodheshwa.
ORODHA YA VITABU
USHAIRI
Wasakatonge M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka T.A.Mvungi (EP & D.LT.D)
RIWAYA
Takadini Ben J. Hanson (Mbs)
Watoto Wa Mama N’tilie E. Mbogo (H.P)
Joka La Mdimu A.J.Safari (H.P)
TAMTILIYA
Orodha Steve Reynolds (Ma)
Ngoswe Penzi Kitovu Cha Uzembe E.Semzaba (Esc)
Kilio Chetu Medical Aid Foundation (Tph)
1
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 80
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA KWANZA
KIDATO CHANNE
021KISWAHILI
(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)
MUDA: SAA 3MEI 2021
Maelekezo
1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A, Bna chagua maswali matatu (03)kutoka sehemu C.
3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali.
4.Andika kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au nyeusi
5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa haziruhusiwikatika chumba cha mtihani.
6. Andika namba yako ya mtihani katika kila karatasi yako ya kujibia.
UFAHAMU
SEHEMU A: ALAMA 15
(A) Anakimbia (B) Huyu (C) Alikuwa
(D) Nimesafiri (E) Mtoto.
(A) Miwili (B) Mitatu (C) Mnne
(D) Mmoja (E) Haina
(A) Kielezi (B) Kivumishi (C) Kitenzi
(D) Kiwakilishi (E) Nomino
(A) Kuonyesha nafsi (B) Wakati uliopita
(C) Urejeshi wa mtendwa (D) Hali ya masharti
(E) Wakati timilifu.
(A) Tatu (B) Moja (C) Nne
(D) Mbili (E) Tano
Sayansi?
(A) Njia ya kichwa (B) Njia ya maandishi
(C) Njia ya simu (D) Njia ya kanda za Sinema na Video (E) Njia ya magazeti.
(A) Binadamu (B) Wanyama
(C) Lugha (D) Vitu na mahali
(E) Hadhara.
(A) Sentensi (B) Konsonanti
(C) Mofimu (D) Irabu
(E) Silabi
(ix) Mtindo wa lugha unapatikana katika mada ya:
(A) Kamasi (B) Viambishi
(C) Musimu (D) Rejesta (E) Ngeli.
(x) Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi fulani ya kifasihi.
(A) Muundo wa kazi husika (B) Wahusika wa kazi za fasihi
(C) Jina la kazi husika (D) Jina la mtunzi wa kazi husika
(E) Mtindo wa kazi husika.
ORODHAA | ORODHAB |
(i) Sherehe/shughuli zinazofanywa na jamii katika kipindi maalumu cha mwaka. | A. Vichekesho |
(ii) Maigizo mafupi yaliyojaa ucheshi na mzaha. | B. Miviga |
(iii) Kitenzi kishirikishi kipi kinaonekana kukubali kuwepo kwa hali fulani | C. si |
(iv) Sehemu ya neno ambalo hutumika kuandika jina jipya. | D. ni |
(v) Tabia ya kuonyesha nafsi | E. Mizizi |
F. Shina | |
G. Kauli | |
H. Kitenzi |
SEHEMU B.
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
(i) Kile kimetiwa rangi nyeupe
(ii) Upi umeisha?
(iii) Vifaranga vya Juma vipo, vyako havipo.
(iv) Ambao wamefika hapa ni Wanasayansi
(v) Wangapi wamekula Mayai
(vi) Wale hawasomi kwa sababu hawana karo.
(vii) Watoto wako wamefika, wangu bado.
(viii) Ambaye anataka kujiunga na Jeshi afike Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
(ix) Nyinyi mlifanya uchaguzi vizuri
(x) Ile ya kijani si mali yake.
(b) Toa maana ya maneno yafuatayo:-
(i) Kiima (ii) Kiarifu (iii) Prediketi (iv) Shamirisho
(v) Chagizo.
(i) Paa (ii) Panga (iii) Kata
(iv) Mbuzi (v) Kaa
Kijinsia. Zingatia kanuni za kimapokeo.
(b) Onesha na uelezee kanuni zifuatazo kama zilivyojitokeza katika shairi
Uliliotunga. (i) vina (ii) mizani (iii) kipande
(iv) mshororo.
SEHEMU C (ALAMA 45)
Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii.
1
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 54
THE PRESIDENT'S OFFICE
MINISTRY OF REGIONAL GOVERNMENT AND LOCAL GOVERNMENT
PRE-NATIONAL EXAMINATION SERIES-1
KISWAHILI FORM-4
2020
TIME: 3:00 HRS
Maelekezo
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu chako cha kujibia.
(i) Neno lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza mtenda au mtendwa?
(ii) Ni sentensi ipi haina kitenzi kisaidizi?
(iii) Ni sentensi ipi inawakilisha kikamilifu wahusika wa fasihi simulizi?
(iv) Bainisha seti ya maneno inayofaa kuingizwa kwenye kamusi kwa kuzingatia mpangilio wa alfabeti.
(iv) Watoto hawa wanacheza vizuri neno “Vizuri” ni aina gani ya neno?
(v) Kiswahili ni kibantu kwa kuwa:-
(vi) Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi fulani ya kifasihi?
(vii) Ipi ni fasili sahihi kuhusu tungo?
(viii) Nini maana ya sentensi sahili.
(ix) Zifuatazo ni sifa za pijini isipokuwa
A. Pijini huwa na maneno kutoka lugha mbili au zaidi
B. Pijini hutokea kurahisisha mawasiliano baina ya watu ambao kila mmoja
ana lugha yake
C. Miundo ya maneno na tungo katika pijini imerahisishwa ili kukidhi
mawasiliano
D. Pijini haina msamiati mwa kutosha, hivyo wazungumzaji hutumia sana
ishara
E. Pijini ina watu ambao kwao hiyo ni lugha yao ya kwanza
2. Oanisha maana za dhana za uandishi zilizo katika orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana husika katika orodha B kisha andika herufi husika katika orodha B kisha andika herufi husika katika karatasi ya kujibia.
Orodha A | Orodha B |
|
|
3. (a) Eleza maana ya kielezi kwa kutoa mfano wa sentensi moja.
(b) Kwa kila tungo uliyopewa pigia mstari kielezi na kisha taja ni cha aina gani.
(i) Darasani kuna utulivu mkubwa
(ii) Wanafunzi wanaimba kimasihara.
(iii) Mwalimu amerudi tena.
(iv) Nitaondoka wiki inayokuja.
4. Moja ya faida ya misimu ni kuhifadhi historia ya jamii. Toa mfano mmoja wa misimu zagao iliyovuma Tanzania katika vipindi vifuatavyo:
(a) Muda mfupi baada ya kupata uhuru.
(b) Miaka ya Azimio la Arusha.
(c) Njaa ya mwaka 1974/1975.
(d) Miaka ya vita vya Kagera.
(e) Kipindi cha hali ngumu ya maisha baada ya vita vya Kagera.
5. Taja aina za sentensi zifuatazo kisha eleza muundo ujengao kila sentensi.
6. (a) Eleza maana ya Kiambishi.
(b) Bainisha viambishi vilivyopo katika vitenzi vifuatavyo:
7. Katika kila sentensi andika neno moja lenye maana sawa na maelezo ya sentensi husika.
1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.
Ustaarabu ni jambo jema ambalo hupendwa na kila jamii yenye utashi hapa duniani. Kila jamii yenye ustaarabu mambo yake huendeshwa kwa kuzingatia kanuni na taratibu zinazoeleweka. Maamuzi na mafanikio mbalimbali miongoni mwa wanajamii hutolewa bila hamaki wala kukurupuka. Kanuni na taratibu hizo huiongoza jamii kufikia upeo wake kimaendeleo kuanzia ngazi za chini kabisa ambayo ni familia mpaka ngazi ya juu kabisa ambayo ni taifa. Taratibu na kanuni hizo huwekwa katika chombo kimoja maalumu kinachoitwa katiba.
Katiba ni jumla ya sheria, kanuni na taratibu fulani zilizokubaliwa kuwekwa na jamii au taifa fulani kama dira ya maisha ya kila siku ya jamii au taifa hilo. Taifa bila katiba ni sawa na behewa la garimoshi bila injini. Hivyo katiba ina umuhimu wa kipekee katika taifa lolote lile.
Katika nchi zenye utamaduni wa kidemokrasia, katiba huundwa kutokana na maoni ya wananchi wake kwa utaratibu maalumu uliowekwa na serikali. Aghalbu, maoni na mawazo yaliyotolewa na wananchi huwa ni chimbuko la katiba hiyo. Wananchi hujiona ni sehemu ya utawala. Kwa upande wa pili wa sarafu, nchi zenye utaratibu wa kiimla, katiba hutayarishwa na watawala kwa maslahi yao binafsi. Katiba hutumiwa kama sera kwa maslahi ya watawala. Maoni na mawazo ya wananchi hayazingatiwi katika kuunda katiba.
Umuhimu wa katiba huonekana na kujidhihirisha waziwazi katika maisha ya kila siku ya nchi yoyote ile. Kwanza, katiba huelekeza wajibu wa ila mwanajamii kwa taifa lake na wajibu wa viongozi walio madarakani kwa wananchi au raia. Pili, katiba huonesha na kuainisha haki ambazo kila raia anastahili kupata na pia taratibu za kufuata katia kudai au dupewa haki hizo. Mbali na hayo, katiba hutoa utaratibu wa jinsi ya kuwapata viongozi wetu katika ngazi mabalimbali za kisiasa na kijamii. Pia uhuru wa mtu binafsi hulindwa na katiba. Hivyo, katika nchi ambayo ina katiba inayokidhi matarajio ya wananchi wote mambo huwa mazuri na kamwe chombo hakiwezi kwenda mrama.
Aidha, wananchi hawana budi kuelewa maana ya katiba ili waweze kutoa maoni na mapendekezo ya kuunda katiba mpya au kuimarisha iliyopo. Ni muhali kwa mtu asiyejua maana ya katiba kutoa maoni kuhusu katiba. Wananchi hupaswa kuelimishwa kupita semina, warsha na makongamano mbalimbali ili kujua katiba zao na kutoa maoni kuhusu uundaji wa katibu mpya.
Hata hivyo, wananchi wengi hasa vijana hawajitumi katika kuzijua katiba za nchi zao au kutoa maoni ya uundaji wa katiba mpya. Athari zake ni kutojua haki zao za msingi na kuburutwa kama mkokoteni na watawala katika mambo mbalimbali. Vilevile hulalamikia mambo ambayo hawakuchangia mawazo.
Hivyo basi, ni vizuri kwa wananchi kutambua, kuthamini na kuheshimu uwepo wa katiba kama kiongozi kizuri katika kuonesha njia muafaka ya kujiletea maendeleo kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kwa nchi husika.
Maswali
(a) Toa maana ya maneno yote yaliyokolezwa wino kama yalivyotumika katika habari uliyosoma.
(b) Kwa mujibu wa habari uliyosoma, taja mambo mazuri mawili yatokanayo na uwepo wa katiba katika nchi.
(c) Kwanini mwandishi anasema katiba hutumiwa kama sera kwa maslahi ya watawala?
(d) Je, ni hofu gani aliyonayo mwandishi dhidi ya vijana kuhusu katiba?
(e) Andika kichwa cha habari uliyosoma kisichozidi maneno matano (5).
SEHEMU C (Alama 45)
Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii.
9. Andika insha ya hoja isiyopungua maneno mia mbili na hamsini (250) na isiyozidi maneno mia tatu (300) kuhusu ‘Madhara ya Madawa ya Kulevya nchini Tanzania’.
ORODHA YA VITABU KWA SWALI LA 10-12
USHAIRI
Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D. LTD)
RIWAYA
Takadini - Ben J. Hanson (MBS)
Watoto wa Mama Ntilie - E. Mbogo (H.P)
Joka la Mdimu - A.J .Safari (H.P.)
TAMTHILIYA
Orodha - Steve Reynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)
Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)
10. "Fasihi ya Kiswahili imemweka mwanamke katika hadhi tofauti tofauti." Thibitisha usemi huu kwa kutumia hoja tatu kwa kila riwaya kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.
11. “Ustadi wa msanii hudhihirishwa na fani”. Dhihirisha kauli hiyo kwa kutumia vipengele vitatu vya lugha kwa kila diwani kutoka katika diwani mbili ulizosoma.
12. Kwa kutumia diwani mbili ulizosoma eleza jinsi taswira tatu kutoka katika kila diwani zilivyotumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe kwa jamii.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 27
OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA MWIGO WA KISWAHILI
KIDATO CHA NNE
MUDA 3:00 JUNI 2020
Maelekezo
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu chako cha kujibia.
(i) Neno lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza mtenda au mtendwa?
(ii) Ni sentensi ipi haina kitenzi kisaidizi?
(iii) Ni sentensi ipi inawakilisha kikamilifu wahusika wa fasihi simulizi?
(iv) Bainisha seti ya maneno inayofaa kuingizwa kwenye kamusi kwa kuzingatia mpangilio wa alfabeti.
(v) Ni sifa ipi haitofautishi fasihi simulizi na fasihi andishi?
(vi) Jozi ipi ina vipengele sahihi vinavyounda umbo la ndani la kazi ya fasihi simulizi?
(vii) "Ngombe zangu wanatoa maziwa mengi." Kosa lililojitokeza katika tungo hii ni lipi kati ya haya?
(viii) "Serikali imeweka mikakati kabambe ili kupunguza umasikini."Neno "ili" katika sentensi hii ni aina gani ya neno?
(ix) Mpangilio sahihi wa vipashio vinavyounda lugha ya Kiswahili ni upi?
(x) Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi fulani ya kifasihi?
2. Oanisha istilahi za fasihi simulizi katika orodha A na maana zake katika Orodha B.
Orodha A | Orodha B |
|
|
SEHEMU B (Alama 40)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
3. Taja njia zilizotumika kuunda maneno yafuatayo:
4.Andika nahau yenye maana sawa na tungo zifuatazo:
5.(a). Kwa kila tungo uliyopewa pigia mstari kielezi na kisha taja ni cha aina gani.
(i) Darasani kuna utulivu mkubwa
(ii) Wanafunzi wanaimba kimasihara.
(iii) Mwalimu amerudi tena.
(iv) Nitaondoka wiki inayokuja.
(b) Toa maana tano tofauti za neno “kibao” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana uliyotoa.
6.(a) Taja aina za sentensi zifuatazo kisha eleza muundo ujengao kila sentensi.
b. Eleza dhima za mofimu "li" kama ilivyotumika katika sentensi zifuatazo:
7. Andika sentensi zifuatazo katika hali ya ukanushi:
8. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.
Nchi yetu ya Tanzania imejulikana sana kutokana na mazingira yake yanayowavutia watalii. Hali yake ya hewa ni nzuri na yenye kutamanika. Mvua yake si nyingi na haichukizi bali ni ya rasharasha na tena ni ya hapa na pale. Majira yenyewe ya masika ni mafupi sana na hayana baridi kama huko ulaya.
Kitu hasa kinachowavutia watalii kutembelea nchi yetu ni pwani zetu ambazo zina mchanga mweupe na laini. Mchanga wenyewe hauna matope wala uchafu wowote. Kandokando ya pwani hizo kuna vichaka vyenye miti yenye rangi chanikiwiti na maua ya sampuli nyingi ya kutamanisha. Maua hayo yapo ya rangi nyekundu na vilevile hunukia vizuri, ama huweza kuwa na rangi ya manjano na kisha yakawa mviringo.
Kando kidogo unaweza kuona mawe makubwa yenye mapango makubwa mweusi ambamo wanyama wakubwa na wakali kama chui huishi. Pengine hata wanyama wa kuchekesha na hata watundu kama tumbili na kima huonekana humo.
Pembezoni, ambapo ni nje ya pwani zetu, kuna mashamba yenye mimea ya rangi ya kijani ikinawiri hasa wakati wa masika. Kipindi hiki wakulima nao huwa wanajishughulisha na matayarisho pamoja na maendeleo ya kazi zao za kila siku. Baadhi yao hupenda kufanya kazi huku wamevaa majoho marefu meupe au pengine shuka za kaniki zilizochakaa. Aidha, wengine hawajishughulishi kamwe na mambo ya mavazi kwani wao huvaa vikoi vikuukuu na vilivyokwajuka, bila kujali wapita njia.
Zaidi ya pwani zetu, watalii huvutiwa sana na mbuga zetu za wanyama wa porini. Wengi wa wanyama katika mbuga zetu huwa na gozi zenye madoa ya rangi za kuvutia. Pengine hata maungo yao huwa ya kutisha na yasiyokuwa ya kawaida. Mathalani ukimwona kifaru unadhani amekasirika na kwamba anataka kukurarua vipande vipande. Simba naye anajulikana kwa makucha yake marefu ya kutisha. Kiboko kwa upande wake, anajulikana kwa unene wake. Tumbo lake ni kubwa la kuchekesha kwani kila umwonapo utadhani matumbo yataporomoka dakika yoyote.
Basi mambo kama hayo na mengine mengi, ndiyo yanayowavutia watalii kuja kwetu. Watalii hawa ambao wengine kati yao ni warefu na pia wachangamfu lakini wapo walio wembamba na wepesi katika kuipanda milima yetu. Hata hivyo, wapo pia wazee vikongwe wenye ari na nguvu katika kuipanda milima hiyo. Wote hawa wanakuwa na hamu ya kutembelea vivutio vyetu. Baada ya kutembelea sehemu mbalimbali, hurudi kwao na furaha isiyo kipimo huku wakituachia fedha nyingi za kigeni.
(a) Andika kichwa cha habari hii kisichozidi maneno manne.
(b) Taja dhamira kuu inayotokana na habari hii
(c) Mwandishi anatoa ushahidi gani kuthibitisha kuwa nchi yetu ina vivutio vingi vya utalii?
(d) “Wenyeji wa nchi yetu ya Tanzania nao ni sehemu ya vivutio vya utali” Thibitisha kauli hii kwa mujibu wa habari uliyosoma
(e) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kufungu cha habari
SEHEMU C (Alama 45)
Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii.
9. Umechaguliwa kutoa risala kwa niaba ya wanakijiji wa kijiji cha Kisombogho, wanaotaka kutoa shukrani zao kwa Mkuu wa Wilaya aliyewachimbia kisima cha maji kijijini hapo. Andika risala utakayoisoma siku ya kikao.
ORODHA YA VITABU KWA SWALI LA 10-12
USHAIRI
Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D. LTD)
RIWAYA
Takadini - Ben J. Hanson (MBS)
Watoto wa Mama Ntilie - E. Mbogo (H.P)
Joka la Mdimu - A.J .Safari (H.P.)
TAMTHILIYA
Orodha - Steve Reynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)
Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)
10.Fasihi simulizi ikihifadhiwa katika maandishi hupoteza uhai na uhalisia wake. Fafanua changamoto nne zinazoweza kujitokeza kwa kuhifadhi fasihi simulizi katika maandishi.
11. "Mshairi ni mwalimu wa viongozi wa nchi." Jadili kauli hii kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizosoma.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 24
OFISI YA RAIS
WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA NUSU MUHULU- MACHI-2020
KISWAHILI
SEHEMU A (Alama 10)
UFAHAMU
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata;
Nchi yetu ya Tanzania imejulikana sana kutokana na mazingira yake yanayowavutia watalii. Hali yake ya hewa ni nzuri na yenye kutamanika. Mvua yake si nyingi na haichukizi bali ni ya rasharasha na tena ni ya hapa na pale. Majira yenyewe ya masika ni mafupi sana na hayana baridi kama huko ulaya.
Kitu hasa kinachowavutia watalii kutembelea nchi yetu ni pwani zetu ambazo zina mchanga mweupe na laini. Mchanga wenyewe hauna matope wala uchafu wowote. Kandokando ya pwani hizo kuna vichaka vyenye miti yenye rangi ya chanikiwiti na maua ya sampuli nyingi ya kutamanisha. Maua hayo yapo ya rangi nyekundu na vilevile hunukia vizuri, ama huweza kuwa na rangi ya manjano na kisha yakawa mviringo.
Kando kidogo unaweza kuona mawe makubwa yenye mapango makubwa meusi ambamo wanyama wakubwa na wakali kama chui huishi. Pengine hata wanyama wa kuchekesha na hata watundu kama tumbili na kima huonekana humo.
Pembezoni, ambapo ni nje ya pwani zetu, kuna mashamba yenye mimea ya rangi ya kijani ikinawiri hasa wakati wa masika. Kipindi hiki wakulima nao huwa wanajishughulisha na matayarisho pamoja na maendeleo ya kazi zao za kila siku. Baadhi yao hupenda kufanya kazi huku wamevaa majoho marefu meupe au pengine shuka za kaniki zilizochakaa. Aidha, wengine hawajishughulishi kamwe na mambo ya mavazi kwani wao huvaa vikoi vikuukuu na vilivyokwajuka, bila kujali wapita njia.
Zaidi ya pwani zetu, watalii huvutiwa sana na mbuga zetu za wanyama wa porini. Wengi wa wanyama katika mbuga zetu huwa na ngozi zenye madoa ya rangi za kuvutia. Pengine hata maungo yao huwa ya kutisha na yasiyokuwa ya kawaida. Mathalani ukimwona kifaru, utadhani amekasirika na kwamba anataka kukurarua vipande vipande. Simba naye anajulikana kwa makucha yake marefu ya kutisha. Kiboko kwa upande wake, anajulikana kwa unene wake. Tumbo lake ni kubwa la kuchekesha kwani kila umwonapo utadhani matumbo yataporomoka dakika yoyote.
Basi mambo kama hayo na mengine mengi, ndiyo yanayowavutia watalii kuja kwetu. Watalii hawa ambao wengine kati yao ni warefu na pia wachangamfu lakini wapo walio wembamba na wepesi katika kuipanda milima yetu. Hata hivyo, wapo pia wazee vikongwe wenye ari na nguvu katika kuipanda milima hiyo. Wote hawa wanakuwa na hamu ya kutembelea vivutio vyetu. Baada ya kutembelea sehemu mbalimbali, hurudi kwao na furaha isiyo kipimo huku wakituachia fedha nyingi za kigeni.
Maswali
2. Fupisha habari ulioisoma kwa maneno yasiozidi arobaini (40)
SEHEMU B (Alama 25)
SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
3. (a) Eleza maana ya utohoaji.
(b) Maneno yafuatayo yametoholewa kutoka lugha gani.
4. Taja aina za sentensi zifuatazo kisha eleza muundo ujengao kila sentensi.
5. (a) Eleza maana ya urejeshi katika kitenzi.
(b) Tunga sentensi tatu zinazoonesha urejeshi wa:
6. Bainisha tabia za maumbo yaliyokolezwa wino katika vitenzi ulivyopewa.
7. (a) Eleza maana na dhima ya kiunganishi katika sentensi.
(b) Tunga sentensi mbili kwa kila kiunganishi kifuatacho;
8. Jifanye kuwa mfanyabiashara wa mchele na unataka kuitangaza biashara yako nje na ndani ya nchi. Andika tangazo kuhusu biashara hiyo na jina lako liwe Pera Mlavi.
SEHEMU C. (Alama 45)
FASIHI KWA UJUMLA
Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii.
ORODHA YA VITABU:
USHAIRI
Wasakatonge - M.S. Khatiby (DUP)
Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya ChekaCheka - T.A. Mvungi (EP & D. LTD)
RIWAYA
Takadini - Ben J. Hanson (MBS)
Watoto wa Mama N’tilie - E. Mbogo (H.P)
Joka la Mdimu - A.J. Safari (H.P)
TAMTHILIYA
Orodha - Steve Reynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)
Kilio chetu - Medical Aid Foundation (TPH)
9. “Waandishi wa tamthiliya wameshindwa kufikisha ujumbe kwa jamii iliyokusudiwa.” Kanusha kauli hii kwa kutumia hoja tatu kwa kila kitabu kotoka katika tamthiliya mbili ulizosoma.
10. “Mshairi ni mwalimu wa viongozi wa nchi.” Jadili kauli hii kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ilizosoma.
11. Kwa kutumia hoja tatu kwa kila tamthiliya kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma, jadili kufaulu kwa waandishi katika kipengele cha utumizi wa tamathali za semi.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 4