OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MKOA WA KILIMANJARO
MTIHANI WA UTAMIRIFU KIDATO CHA NNE
MSIMBO 0021 KISWAHILI
MUDA: 3:00 27/06/2022
MAELEKEZO
l. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenyej umla ya maswali kumi nambili (12)
2. Jibu maswali yote katika sehemuAna B na maswali matatu (3)kutoka sehemu C
3. SehemuA ina alama kumi na tano(15) sehemu B ina alama arobaini (40) na sehemu C ina alama arobaini na tano (45)
4. Zingatİa maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali
5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoıuhusiwa havitakiwi katikachumba cha mtihani
6. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa karatasi za kujibia
SEHEMU A (ALAMA 15)
1. Chaguaherufi yajibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kishaandikaherufi yajibu hilo katika karatasi ya kujibia.
i. Maneno yapi kati ya yafuatayo yanatokana na lugha za kibantu
ii. Ni neno lipi linalotoa taarifa kuhusu nomino?
iii. Nj ia mojawapo ya kuzuia utata katika lugha ya mazungumzo ni ipi kati ya zifuatazo?
iv. Neno lipi kati ya haya ni mofimu huru?
v. Ni semi zinazoonesha upinzani wa fikra.
vi. Ni hatua inayofuata baadayakipengele chamwisho wa baruakatika uandishi wa barua rasmi.
vii. Nisifaipi haitofautishi fasihi simulizinafasihi andishi?
viii. Ni maneno yapi kati ya haya yafuatayo yametokana na njia ya kuambatanisha maneno?
ix Tarihini mojawapo kati ya viperavyahadithiarnbavyo huelezeakuhusu.
x. Moja kati ya zifuatazo Sio tabia ya Vitenzi halisi?
2. Oanishamaananadhanakatika Orodha A kwakuchaguaherufiyadhanahusikakatika Orodha B kasha andika herufi husika
SAFU A | SAFU B |
i. Ng'ombe zangu wanatoamaziwa mengi ii. Huandikwakwa lugha mbili iii. Ni kanuni,sheria na taratibu zinazowabana wazungumzaj iwa lugha wapate kuelewana iv. Manenoyasiyo sanifuyanayozungumzwanakikundi kidogo cha watu v. Misemo yapicha ambayo huletamaana iliyofichika. |
|
SEHEMU B (ALAMA 40)
(Jibu maswali yote katika sehemu hii)
3. Kwakila sentensi onesha kiima na kiarifu kwa kutenga na kistarina kuandika "K" kwa kiimana "A" kwa kiarifu
i. Mwanasiasa alikuwa anahutubia wanakij iji wote leo
ii. Mbuzi wangu mkubwa amekula majani yote.
iii.Ng'ombe wetu amekunywa maji machafu mno.
iv. Walifika asubuhi walimu wetu.
v. Mwalimu alikuj a kufundisha Kiswahili asubuhi.
4. Tungozifuatazo zinamaanazaidiyamoja. Toamaanambili tukwakilatungo.
A.Nimenunua mbuzi
B. Eda ameshinda shuleni
C. Ukija njoo na nyanya
D.Nyumbani kwao kuna tembo.
5. a) Soma kwa makini sentensi (i) hadi (iv) kasha fafanua kwa pamoja vipengele vinne (4) vinavyodhihirisha uhusiano baina ya Kiswahili na lugha za kibantu kisayansi
i. Mtoto amelala(kiswahili)
ii. Mwana agonile(kingoni)
iii. Mwana yogonile(kigogo)
iv. Omwana yanagile(kihaya)
b) Kwa kutumia mifano na kutoa hoja mbili kwa kila hoja moja, eleza kwa utupl mafanikio ya lughayaKiswahili enzi za waarabu katika.
i) Dini
ii) Biashara.
6. Kwa kutumia mifano kutoka katika tamthiliya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe E. Semzaba (ESC). Eleza kwa kifupi madhara manne yanayoweza kutokea katikajamii iwapo zoezi la uhesabuji watu (Sensa) litakumbwa na Uzembe.
7. Fikiria kuwa umekutana na mtu ambaye ameteuliwa kutoa hotuba kwenye mkutano wa kijiji kinachoendekeza mila potofu ya unyanyasaji wa walemavu wa ngozi lakini hajawahi kutoa hotuba tangu azaliwe. Wewe kamamwanafunzi wa kidato cha nne eleza kwa ufupi mambo makuu matano (05) atakayopaswa kuzingatia wakati wa utoaji wa hotuba hiyo ili ujumbe uliokusudiwa uweze kuwafikia walengwa.
8. Soma beti zifuatazo za shairi la kimapokeo,
Kishajibu maswali yanayofuata.
Tuitafute elimu, vitabu vyote vyasema,
Nikitu lilo muhimu, kwa maisha yako mema
Tuipate na idumu, ijenge yalo hekima.
Elimu dira sahihi, Ongoza yetu maisha
Elimu kwetu ni mali, uishike ninasema,
Haitaki ukatili,yakutaka uwe mwema,
Maisha kuyakabili, kuyafanya yawe mema
Elimu dira sahihi, Ongoza yetu maisha
Maswali
a) Bainisha ukwapi na utao wamstari watatu wa ubeti wapili
b) Tajatamathali mbilizasemi kwamifanokutokakatikashairi ulilosoma.
c) Mwandishiwashairi hili anÜungumzianafsi ipi? Thibitishajibulakokwamifanomiwili kutoka katika shairi ulilosoma.
d) Elimu humpatiamtu fedha kwani atalipwa kuendananataalumaaliyonayo lakini kuna watu wana fedha nyingi ila hawana elimu. Kwa muj ibu wa shairi hili unadhani watu hao wanakosa kitu gani cha msingi? Eleza kwa hoja moja.
SEHEMU (Alama 45)
Jibu maswali matatu katika sehemu hii
9. Jifanye umepata baruayamwaliko washereheyasikuyakuzaliwakwarafikiyakoaitwaye Dadakiboga Stella itakayofanyika tarehe 12/08/2022 lakini kwa bahati mbaya Siku tano kablaya sherehe umepata safari ya kikazi kuelekea mkoani Mwanza. Andika barua kumtaarifu rafiki yako Dadakiboga Stella wa sanduku la barua 110 Soweto kuwa hutaweza kuhudhuria sherehe hiyo Jina lako liwe Makoti Msweta, Sanduku la posta 212 Arusha.
ORODHAYAVITABU KWASWALI LA 10-12
USHAIRI
RIWAYA
TAMTHILIYA
10. "Mshairi ni mjuzi wa kubuni na kuandaa taaswira itakayo mvuta msomaji katika kazi ya ushairi ” Kwa kutumia diwani mbili kati ya tatu ulizosoma, Elezajinsi mwandishi alivyotumia taaswiratatu kutoka katika kila diwani zilivyotumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe kwaj amii.
1l. Watanzania wa leo wangefaidika sana na tamthiliya kama wangekuwa na utamaduni wakusoma tamthiliya. Thibitisha kauli hii kwa kutumia vitabu viwili kati ya hivyo vilivyotaj wa hapojuu.
12. "Waandishi wa kazi za Fasihi huibua migogoro mbalimbali nakupendekeza masuluhisho ili kuelimisha jamii husika Thibitisha kauli hiyo kwa kutoa hoj a tatu kutoka katika Riwaya mbili kati ya riwaya tatu ulizosoma.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI REGIONAL SERIES-35 YEAR-2022
OFSI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA MUUNGANO WA WAKUU WA SHULE ZISIZO ZA SERIKALI(OHONGSS)
MTIHANI WA UTIMILIFU KIDATO CHA NNE 2022
KISWAHILI
MASAA : 3 JUNI 2022
MAELEKEZO
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Chagua herefi ya jibu sahihi kisha andika jibu lako kwenye kijitabu cha kujibia.
(i) Mhazili ni;
(ii) ‘Pigia mstari.’ Msemo huu una maana ya;
(iii) Amechomwa na mwiba. Neno lililokolezwa wino ni;
(iv) Mwanzilishi wa mashairi ya mtindo kujibizana ni;
(v) Neno ‘mbakaji’ limeundwa kwa njia ya;
(vi) Maneno yapi yametokana na mbinu ya ukopaji?
(vii) Kipande cha pili katika mshororo wa shairi huitwa;
(viii) Utokeaji wa misimu katika jamii hutegemea……………
(ix) Neno lipi kati ya yafuatayo linaweza kudokeza mtenda au mtendwa?
(x) Kati ya sababu zifuatazo ni ipi si sahihi kuhusu matumizi ya kamusi?
2. Oanisha maelezo ya kifungu A na maneno katika kifungu B
KIFUNGU A | KIFUNGU B |
|
|
SEHEMU A (Alama 40)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
3. Bainisha mizizi ya maneno yafuatayo:
4. Eleza miundo minne ya kishazi tegemezi.
5. (a) Bainisha kwa mifano njia nne za uundaji wa misimu.
(b) Eleza mambo manne ya kuzingatia unapofanya mazungumzo.
6. Kiswahili ni kibantu. Thibitisha dai hili kwa kutumia hoja nne.
7. Bainisha taswira mbili kwa kila diwani za Wasakatonge na Malenga Wapya.
8. Chukulia kuwa wewe ni mwalimu Haule Ndomba wa shule ya sekondari Nyika. Mwandikie barua pepe mkuu wako wa shule ukimtaarifu kuwa hutaweza kufika kazini kwa kuwa hujihisi vizuri kiafya.
SEHEMU C (Alama 45)
Jibu maswali matatu tu katika sehemu hii.
9. Tunga utenzi wenye beti tano kuhusu Sensa ya watu na makazi 2022.
10. Tumia diwani mbili, hoja tatu kwa kila moja, kuonesha ni kwa namna gani waandishi wa kazi za fasihi hutumia kazi zao kuelimisha jamii.
11. Uteuzi mzuri wa wahusika ndio husaidia kuibua dhamira mbalimbali katika kazi za fasihi. Jadili kauli hii kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma. (Hoja 6)
12. Dhihirisha utokeaji wa migogoro katika jamii kwa kutumia riwaya mbili ulizosoma. (Hoja 6)
ORODHA YA VITABU
USHAIRI
Wasakatonge - M. S. Khatibu (DUP)
Mashairi ya Cheka Cheka - T. Mvungi (DUP)
Malenga Wapya - TUKI
RIWAYA
Watoto wa Mama N’tilie - E. Mbogo
Joka la Mdimu - A. J. Safari (HP)
Takadini -
TAMTHILIYA
Kilio Chetu - Steve Raynolds (MA)
Orodha - Medical Aid Foundation
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - Edwin Semzaba
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI REGIONAL SERIES-30 YEAR-2022
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOSA UMOJA WA KITAALUMA KANDA YA MIKUMI
MTIHANI WA KIDATO CHA NNE WA KUJIANDAA NA UTAMILIFU
021 KISWAHILI
(Kwa watahiniwa walioko shule tu)
Muda: Saa 3 Alhamisi Machi 18, 2021
MAELEKEZO:
1. Mtihani huu una sehemu A, B, na C zenye jumla maswali 12.
2. Jibu maswali yote katila sebemu A na B kisha maswali matatu (3) kutoka sebemu C.
3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali.
4. Hauruhusiwi kuingia na simu wala nakala yoyote inayohusiana na somo la Kiswahili.
5. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu Chako cha kujibia.
SEHEMU A (ALAMA 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
l. Katika kipengele cha i-x chagua jibu sahihi kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu Chako cha kujibia
i.Sentensi ipi kati ya zifuatazo ina kiambishi cha mtendwa nafsi ya pili umoja?
ii.________________ ni mabadiliko ambayo yamesababisha uhitaji wa neno nywila
iii. Zifuatazo ni nomino za kawaida isipokuwa
iv. Sentensi "Waziri wa fedha atawakilisha bajeti ya mwaka wa fedha 2010/2011" ina kosa gani la kisarufi?
v. Maneno, nahau au sentensi ambatano hutumiwa na wasanii wafasihi ili kutia nguvu katika maana, mtindo na sauti katika maandishi ama kusoma huitwa
vi. Vifuatavyo ni vigezo vya kiisimu vinavyothibitisha ubantu wa Kiswahili isipokuwa
vii. Ni seti ipi haina tawi la sanaa?
viii. Zifuatazo ni dhima za uundaji wa maneno mapya katika lugha isipokuwa
ix. Viambishi vya 0-rejeshi ya nomino "gari" ni vipi kati ya vi fuatawo?
x.Taja seti iliyosahihi katika mambo yanayounda fasili ya lugha.
2. Oanisha maana ya dhana ya vifungu vya maneno vilivyo katika orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana husika katika orodha B, kisha andika herufi husika katika kijitabu chako cha kujibia.
ORODHA A | ORODHA B |
(i) Simo (ii) Tungo shurutia (iii) Kamusi wahidiya (iv) Ngeli (v) Kiambishi cha nafsi ya pili wingi |
|
SEHEMU B (ALAMA 40)
Jibu maswali yote kutoka schemu hii
3. Kwa mifano dhahiri, unadhani watanzania watakumbwa na matatizo gani endapo watatumia lugha isiyofaha katika mawasiliano yao ya kila siku, Tao hoja nne.
4. Kwa kawaída fasihi simulízi huweza kukumbwa na matatizo katika vipengele vyake vikubwa vinne. Vitaje
5. (a) Nini maana ya Msamiati?
(b) Moja ya tabia ya lugha ni kujizalisha ili kupata msamiati mpya utakaokidhi haja ya mawasiliano. Kwa kifupi, eleza mbinu tano ambazo lugha ya Kiswahili inaweza kuzitumia ili kujizalishia maneno mapya.
6.(a) Toa mfano wa neno linaloonesha dhima ya kiambishi ulichopewa kulingana na maelezo yake na ukipigie mstari.
(i) "Li" - kuonesha urejeshi wa mtendwa
(ii) "Kwa" — kuonesha sababu na kuulizia sababu
(iii) ‘Tu’ kuonesha nafsi
(iv)"Ku" kuonesha wakati uliopita
(b). Kwa maelezo mafupi tofautisha istilahi zifuatazo.
(i) Sarufi na Fasihi
7. Waarabu, Wajerumani na Waingereza kwa nyakati tofauti waliitawala Tanganyika, eleza kwa ufupi mambo matano (5) yaliyofanywa na Waingereza katika kuikuza na kuineza lugha ya kiswahili.
8. Soma shairi lifuatalo kishajibu maswali yatakayofuata
l. Mtu wa fikra njema na kwa watu huacha jina.
Kwa kujua dunia nzima, likawa kubwa hazina
Kwa kujua jambo jema, lisilokuwa na shari,
Na watu wajao nyuma, wakapenda kulisoma.
2. Mvuka nguo chutama, wendapo wajihadhari, Na busara ni kutenda, tendo ambalo ni jema, Viumbe wakalipenda, ukapata na heshima, Tabasuri na hekima, ni muhimu maishani.
3. Maisha daima yenda, utaacha nini nyuma?
Ni roho yenye hekima, usambe ni santuri,
Ambayo huweza sema, maneno kwa kukariri, Hali haina uzima, ufahamu ni tafakuri.
4. Kama akili hunena, tungeshindwa na vinanda,
Vya sauti nzuri sana,visivyoweza kutenda,
Matendo yenye maana, ambayo mtu hutenda,
Fikra ni fani bora, katika fani za watu,
5. Weledi wenye busara, na maarifa ya vitu,
Wafahamu kwa sura, ulimwengu wetu wote,
Hekima na busara ya mtu, hupimwa kwa matendo mema, Ayatendayo yenye utu, na wala si maneno mengi kinywani.
(a) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
(b) Neno jina lina maana gani katika shairi?
(c) Mtu mwenye akili ni mtu wa namna gani?
(d)Eleza maana ya maneno yaliyokolezwa wino kama yalivyotumiwa kwenye shairi hili.
(e) Kwa nini hekima na busara ya mtu humpimwa kwa matendo na siyo maneno?
SEHEMU C (ALAMA 45)
Jibu maswali matatu (3) tu kutoka schemu hii
9. Andika insha ya hoja isiyopungua maneno mia mbili (200) na isiyozidi maneno mia mbili na hamsini (250) kuhusu madhara ya kuchafua mazingira.
ORODHA YA VITABU KWA SWALI LA 10-12
USHAIRI
RIWAYA
TAMTHILIYA
10. ‘Mshairi siku zote hukemea uonevu katika jamii.’ Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tano kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizosoma
11."Waandishi wa kazi za fasihi ni walimu wa jamii", Wewe kama mwanajamii, eleza namna ulivyonufaíka na ualimu wa waandishi wawili wa riwaya ulizosoma. Toa hoja tatu kila kitabu.
12. Vijana ndio nguvu kazi ya Taifa lakini mara nyingi vijana hao huliangusha taifa kwa kutenda matendo yasíyofaa. Kwa kutumia tamthilíya mbili ulizosoma, fafanua matendo yasiyofaa yanayotendwa na vijana. Toa hoja tatu kila kitabu
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI REGIONAL SERIES-50 YEAR-2021
Namba ya Mwanafunzi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA UTIMIRIFU MKOA WA ARUSHA MEI 2021
KIDATO CHA NNE
KISWAHILI
MAELEKEZO
SEHEMU A (ALAMA 15)
1.Jibu maswali yote Katika sehemu hii,
(i) Ni aina ya wahusika ambao hawabadiliki na wamepewa majina ambayo humfanya msomaji aelewe tabia na matendo yao;
(ii) Vishazi tegemezi vimegawanyika katika aina kuu mbili ambazo ni;
(iii) Anatoa ufafanuzi juu ya ubantu wa Kiswahili kwa kuelezea wakazi wa mwambao waliojulikana kama "Wazanji" na watawala wao waliojulikana kama "Wakilimi"
(iv) Ni lahaja zinazopatikana Mombasa;-
(v) Mofimu ku iliyopigiwa mstari imebeba dhima gani katika kitenzi sikukukumbuka
(vii) Sehemu ya mzizi asilia iliyoambikwa kiambishi "a" mwishoni
(viii) Ni tamathali ya semi ambayo Jina la mtu hutumiwa kwa watu wengine wenye tabia, mienendo, hulka au kazi sawa na mtu huyo
(ix) Neno SHADARA limepatikana Iwa kutumia njia gani ya uundaji wa maneno?
(x) Chama cha kukuza na kueneza Kiswahili "TAKILUKI" kilianzishwa mwaka
(xi) Aina ya hadithi za ngano zenye wahusika wanyama tu hujulikana kama,
2. Chagua kifungu cha maneno kutoka orodha B kinachotoa maelezo sahihi ya maneno neno katika orodha A.
ORODHA A | ORADHA B |
|
|
SEHEMU B ( Alama 40)
3. Bainisha aina ya kauli katika vitenzi vilivyopigiwa mstari, huku ukifafanua kiambishi kinachojenga kauli hiyo katika tungo zifuatazo.
(i) Matukio ya ubakaji yanaogofya
Waoga wanafahamika
(iii) Nyumba itajengwa na wazazİ
(iv) Dawa za kienyeji zilimlevya sana
4. Huku ukuota mifano. Fafanua dhima nne za mofimu "M" katika lugha ya Kiswahili.
5. Fafanua kwa hoja nne, mambo yanayothibitisha kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni pwani ya Afrika ya Mashariki,
6. Methali hutawaliwa na vipengele mbalimbali vya lugha, onesha vipengele vya lugha vilivyotumika katika utunzi wa methali zifuatazo.
(i) Kibuzi na kibuzi hununa jahazi
(ii) Akili ni mali
(iii) Farasi hamuwawezi, tembo mtawalishani?
(iv) Baniani mbaya kiatu chakc dawa.
(v) Avumayc 'baharini papa, kumbe wengine wapo
7. Soma shairi lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata Mtu wa fikra njema, kwa watu umcacha jina
Chuma chetu imara, Afrika na dunia nzima,
Mikakati imara lojenga, Tanzania nuru kuangaza
Jiwe Ietu limeondoka takuenzi daima
Katika yote dunia, Jinalo lilivema
Misimamo yenye mashiko, ndiyo yako şifa njema
Nia kubwa kujenga, boma, ndiyo ndoto yako imara
Chuma chetu kimelala, hakika umeacha alama
'Umoja uliujenga, utengano likemea
Uchapakazi ulihimiza, nani alibaki nyuma?
Macndeleo kuyajcnga, Elimu hukuacha nyuma.
Nguzo yetu imeinama, nyoyo zetu zimechutama
Wangu wosia naweka, aloacha kuyaenzi
Uzalendo tuudumishe, Ufisadi tuupinge
Vizazi vijavyo tupate hadilhia, mazuri ya mwamba wetu.
Takuombea daima, lalc kwa ushindi shujaa.
Maswali
(a) (i) Shairi hili limejegwa kwa kutumia muundo gani?
(ii)Fafanua mambo ya msingi yakuzingatia wakati wa uchambuzi wa muundo katika ushairi (Hoja Nne)
(b) Onesha upekee wa mıvandishi katika shairi hili (Hoja Nne)
(c) Mwandishi ana maana gani anaposema jiwe, mwamba chuma na nguzo?
(d) Andika kichwa cha habari cha shairi hili.
(e) Mwandishi anahimiza nini katika kumuenzi shujaa.
8. Kijiji chenu cha Kiloza kimeanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji. Wewe kama afisa manunuzi, andika barua katika kampuni ya Olotu inayojihusisha na uuzaji pembejeo za kilimo kuangiza bidhaa zitakazotumika katika kuendesha mradi. Jina lako ni Ombeni Mtapewa.
SEHEMU C (Alama 45)
Jibu maswali matatu kutoka katika sehemu hii.
9. Ni kweli kwamba lugha ya Kiswahili imevuka mipaka na kuenea katika maeneo mbalimbali duniani. Thibitisha ukweli wa dai hili (Hoja - 5)
TAMTHILYA
Orodha - Steve Reynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe -E. Semzaba (ESC)
Kilio chetu - Medical Aid Foundation
RIWAYA
Takadini - Ben Hnson (MBs)
Mamantilie - Emanuel Mbogo
Joka la mndimu - A. J. Safari (HP)
USHAIRI
Cheka cheka - T. Muungi
Malenga wapya - Takiluki
Wasaka tonge - Mohamed Seif Khatibu
10. Washairi ni wataalamu wazuri na waliobobea katika kutumia jazanda zinazotoa ujumbe kwajamii. Tumia jazanda tatu kwa kila diwani mbili uliyosoma.
11. Lugha ni kipengele cha msingi katika ujenzi wa kazi ya fasihi ambayo husaidia katika kufikisha wazo la msanii kwa jamii. Kwa kutumia riwaya teule mbili (2) ulizozisoma. Jadili jinsi wasanii wa riwaya hizo walivyotumia kipengele cha tamathali za semi hoja Sita (6)
12. Mwandishi ni Mjenzi wa jamii. Thibitisha ukweli wa dai hili kwa kutoa hoja tatu kutoka katikaTamthilia mbili ulizozisoma
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI REGIONAL SERIES-27 YEAR-2021
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA UTAMILIFU MKOA WA DODOMA 2020
021 KISWAHILI
(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)
MUDA: SAA 3 Alhamisi, 6 Agosti 2020 mchana
Maelekezo
1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A, B na chagua maswali matatu (03) kutoka sehemu C.
3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali.
4. Andika kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au nyeusi
5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.
6. Andika namba yako ya mtihani katika kila karatasi yako ya kujibia.
SEHEMU A, (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika karatasi yako ya kujibia.
(i) Ni kanuni, sheria na taratibu zipi zinazozingatiwa na wazungumzaji wa lugha fulani?
(ii) ………………. Ni sauti zinazotamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti.
(iii) Zipi ni nyenzo za lugha yoyote duniani?
(iv) Mpangilio sahihi wa ngeli za kisintaksia ni upi?
(v) Ni upi mpangilio sahihi wa mjengo wa Tungo?
A Kirai, Neno, Sentensi na Kishazi
B Neno, Kirai, Kishazi na Sentensi
C Kishazi, Kirai, Sentensi na Neno
E Sentensi, Neno. Kishazi na Kirai
(vi) Ni lugha mseto ya muda inayozuka pindi makundi mawili yenye lugha mbili tofauti yakutanapo.
(vii) Mambo muhimu yanayopatikana katika maana ya lugha ni kama yafuatayo, isipokuwa;
(viii) Ni sentensi ipi sio sentensi huru?
(ix) ……………. Ni kipashio kidogo kabisa cha lugha chenye maana. Maana hiyo yaweza kuwa ya kisarufi au kileksika;
(x) Ni seti ipi inawakilisha kikamilifu wahusika wa fasihi simulizi?
2. Oanisha maelezo yaliyo katika orodha ‘’A’’ ambayo ni aina ya tungo na orodha ‘’B’’ ambazo ni aina za maneno yanayounda tungo hizo kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.
ORODHA “A” | ORODHA “B” |
i. Wale waliamini maneno yangu ii. Salama alikuwa mwanafunzi wangu iii. Walikuwa wanataka kwenda kulima iv. Alikuwa anajisomea darasani polepole v. Loo! Yule anapenda ugomvi | A. N + t +N +V B. H + w +T + N C. W + T + N + V D. Ts + T + E +E E. Ts + Ts + Ts + T F. N + V + t +E G. N + U+ N+ T |
SEHEMU B (Alama 40)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
3. Tunga sentensi moja kwa kila alama kuonesha matumizi ya alama zifuatazo.
i. Mkato
ii. Mabano
iii. Alama za mtajo
iv. Nukta pacha
4. Andika maana ya methali zifuatazo;
5. (a) Tenga kiima na kiarifu katika sentensi zifuatazo. Tumia alama ya mkwaju (/) na kuweka herufi “K” juu ya kiima na herufi “A” juu ya kiarifu.
i. Mdogo wangu anaongea sana
ii. Yule kijana aliyekuja hapa juzi amefariki dunia
iii. Frank ni kijana mpole sana
iv. Mama amelala sakafuni
(b) Changanua sentensi zifuatazo kwa njia ya matawi kwa kutumia mkabala wa kimapokeo
i. Fisi mkubwa ameuawa kichakani jana alfajiri.
ii. Mtoto aliyekuwa anacheza uwanjani amevunjika mguu.
6.(a) Kwa kutumia mifano miwili kwa kila kipengele, fafanua kwa ufupi jinsi vipengele vifuatavyo vinavyoonesha kuwa vitenzi vya Kiswahili na lugha za kibantu vina asili moja.
b) Eleza kwa ufupi juu ya nadharia zifuatazo kwa jinsi zinavyoelezea asili ya Kiswahili
7. Kwa kutumia mifano, fafanua dhana zifuatazo kama zinavyotumika katika fasihi
8. Soma kifungu cha habari kifuatacho, kisha jibu maswali yanayofuata;
Wanangu, toka zamani bara letu la Afrika lilikuwa na mambo yaliyohitilafiana na haya tunayoyaona sasa. Hadithi, vitimbi, na visa vilivyotokea zamani katika bara letu vinatofautiana sana na mabara yoyote mengine. Vyetu ni vitamu na bora kuliko vyote vile vilivyotokea katika mabara hayo.
Miujiza ya mambo yaliyotokea ina mizizi ambayo viini vyake hubenua waziwazi mila na desturi za asili tangu zamani, hivyo, hadithi hizo zina tija ya makumbusho ya daima milele. Kwa hiyo, katika hali yoyote yatupasa kuhifadhi hazina za mila zetu. Mila zetu zidumishwe; kwa mfano watu kuzunguka moto huku kizee kikongwe au ajuza akisimulia hadithi za mambo ya kale liwe ni jambo la kawaida kabisa. Katika dunia ya leo simulizi hizo za ujasiri na uzalendo zimeenea kutoka vizazi hadi vizazi. Mambo mengi yamebadilika kutoka mitindo aina aina, hivyo mabadiliko hayo yasitufanye sisi kusahau simulizi zetu katika mitindo yetu. Ni wajibu utupasao kuendeleza tabia hizi ili tubenue mbinu za masimulizi hata kwa vitabu.
Maswali
SEHEMU C (Alama 45)
Jibu maswali matatu(3) kutoka katika sehemu hii.
9. Wewe kama afisa Manunuzi wa kiwanda cha mbao cha Mshikamao S. L. P 100 Chamwino, andika barua kwa mfanyabiashara yeyote mashuhuri wilayani kwenu kuhusu agizo la vifaa vifuatavyo; Misumeno 5, gundi ya mbao lita 20, misumari ya nchi sita Kg 25, na kofia ngumu 40. Jina lako liwe Shukrani Kazamoyo.
10. Kwa kutumia diwani mbili ulizosoma, eleza jinsi taswira tatu kutoka kila diwani zilivyotumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe kwa jamii.
11. “Kazi ya fasihi ina radha kwa sababu inamzungumzia pia mwanamke kwa namna tofautitofauti” Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu katika riwaya mbili ulizosoma.
12. Chagua wahusika wawili katika tamthiliya teule mbili ulizosoma na uoneshe ujumbe unaowasilishwa na waandishi kupitia matendo yao.
ORODHA YA VITABU
USHAIRI
Wasakatonge ---------------------------- M. S Khatibu (DUP)
Malenga wapya-------------------------- TAKILUKI (DUPU)
Mashairi ya Chekacheka---------------- T. A. Mvungi (EPdD.LTD)
RIWAYA
Takadini ----------------------------------- Ben J. Hanson (MBS)
Watoto wa Mama Ntilie ----------------- E. Mbogo (H.P)
Joka la Mdimu ---------------------------- A. J. Safari ( H.P)
TAMTHILIYA
Orodha ------------------------------------ Steve Reynolds ( M. A)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe ----- E. Semzaba (ESC)
Kilio Chetu --------------------------------- Medical Aid Foundation (TPH)
LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM FOUR KISWAHILI REGIONAL SERIES-11 YEAR-2020