KISWAHILI NECTA EXAMINATIONS
YEAR : 2018  SUBJECT : KISWAHILI

JAMHURI VA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA KUHITIMU KIDATO CHA NNE

021      KISWAHILI

(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

Muda: Saa 3:00           Jumatatu, 05 Novemba 2018 asubuhi 

Maelekezo

  1.  Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E zenye jumla ya maswali kumi na tano (15).
  2.  Jibu maswali vote katika sehemu A, B na D, swali moja (1) kutoka sehemu C na maswali matatu (3) kutoka sehemu E. Swali la 15 ni la lazima.
  3.  Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.
  4.  Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.

SEHEMU A (Alama 10)

UFAHAMU

Jibu tnaswali yote katika sehemu hii.

1.Soma kwa umakini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.

Ingawa utaona kuwa haya nitakayoyasimulia hayakuhusu ndewe wala sikio, kwa vile mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi, lakini kumbuka, mwenzio akinyolewa na wewe tia maji maana yaliyompata beku na ungo yatampata.

Ukiona yale yanayomsibu Mwanaheri hivi sasa ni dhahiri utakubaliana na mimi kuwa ujana ni kama maua. Kwa matatizo anayoyapata Mwanaheri ni kuntu kuwa upigao ndio ufunzao. Ingawa kwake ni sawa na maji yaliyomwagika hayazoleki, na ninaamini kuwa kwa wengine hill ni fundisho kwa kuwa watu husema, kama hujui kufa tazama kaburi.

Uzee unaomkabili Mwanaheri sasa unahitaji msaada mkubwa wa mtoto wake haidhuru mjukuu wake. Lakini maskini, hakupenda watu hao kuwa nao tangu awali ya maisha yake. Ingawa hivi sasa anao watoto wa ndugu zake, lakini hawana msaada wowote kwake. Ndiyo maana watu hawakukosea kusema ndugu akizaa na wewe uzae maana changu si chetu. Hata wale mashoga zake waliokuwa wakishirikiana naye‘katika kukata mitaa, wamemtupa Kigoma mwisho wa refi.

Kwa uzuri, alhamdulillah, aliumbika, maana alikuwa chuma hasa wala si masihara. Enzi zake Mwanaheri, alikuwa Mwanaheri kweli. Alikuwa hapitwi na mwanamume. Mbali ya kuwa na kidevu cha mfuto chenye kidimbwi kwa mbali, macho yake ya gololi yalimvuta mwanamume yeyote hata muumini wa dini.

Miguu iliumbwa kadri ya mwili wake. Ukimwangalia kwa nyuma umbo lake ni sawa na umbo la namba nane. Ingawa alikuwa na nywele za kipilipili, lakini alizitengeneza zikawa kama za singa. Uzuri wote huo aliotunukiwa kama hedaya yake papa duniani, umeathiriwa na mwenendo tu. Mwenendo huu ulimpa jina baya la kuitwa jamvi la wageni.

Mwenendo huu ulikuwa sadfa ya ambacho kimekamilisha ule usemi wa wahenga kuwa uzuri wa kuyu ndani imeoza au uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti. Alipokuwa kijana alikuwa hapendi wachumba, wala watoto kwa kuchelea kutibua starehe zake. Kwa jinsi alivyokuwa anadanganyika na ujana pamoja na rangi za dunia akifikiri atakuwa kijana mpaka kufa kwake. Alijididimiza katika wimbi la starehe hadi akazama kiasi kwamba akalowana chapa. Naam! aliyetota hajui kutota. Mbali na kutosikia la baba wala la mama, pia hakusikia la viongozi wa dini. Maisha yalikuwa dunia na yeye na dunia. Ingawa alikuwa na wenzake katika shughuli hizo, lakini ni yale yale, yetu yetu, yakikupata yako peke yako, lakini wenzako walikuwa wakifanya hayo na akili zao. Yeye hakukumbuka kwamba nahodha mtweka chombo si mjinga wa bahari kwani mtu hufanya jambo kwa akili take, lakini Mwanaheri mwenzangu na miye hakuwa na hill wala lile. Venzake hao sasa wana watoto wao ambao wanawasaidia kwa moja au kwa jingine. wakati yeye anaumbuka. Kidagaa kimemwozea. Mbali ya kuwa na ubao mara kwa mara, pa kuweka ubavu pia alipasikia kwenye bomba. Kwa intu aliyeuona ujana wa Mwanaheri, hawezi kuamini kuwa ni htiyu anayeadhirika sasa hi vi. Naam! Asiyesikia la mkuu huvunjika gnu, kama wanenavyo waneni, asiyefunzwa na mama hufunzwa na ulimwengu.

Majuto ni mjukuu, na hivi sasa nina imani kuwa Mwanaheri anajuta kwa kuuchezea ujana wake. Hakujua ujana ni hazina kubwa ya maisha ya baadaye. Hivi sasa ninahisi angalipenda arudie hall ile ile ya juzi na jana iii apate mume yeyote yule, hata angalikuwa kabwela kupindukia, mbali ya wale wa maana aliokuwa akiwapiga mateke. Hata hivyo, yote haya ni kutaka kupata mtoto, hata liwe toto jinga, maana jinga ni lako, kwani tikiti baya lipo shambani kwako. Lakini hilo ni jambo ambalo haliwezekani hata afanye ibada usiku na mchana. Hata hivyo, afae hakosi mzishi, kwani ingawa watu wengi wamekata mguu, kuja kumliwaza, bado ndugu wachache hufika kumhudumia, angalau kwa kujitoa kimasomaso. Watu husema, damu nzito kuliko maji.

Maswali

  1.  Kwa mujibu wa habari uliyosoma eleza kitu kilichoathiri uzuri wa Mwanaheri.
  2.  Andika nahau mbili zinazopatikana katika kifungu cha habari ulichokisoma.
  3.  Fafanua methali zifuatazo kwa kutoa mifano halisi kutoka katika simulizi uliyosoma:     (1) Maji yakimwagika hayazoleki.       (ii) Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
  4. Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma.

2. Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua mia moja (100).

SEHEMU B (Mama 25)

SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA 

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Fafanua dhana zifuatazo na kisha toa mfano mmoja kwa kila dhana uliyofafanua.

  1. N e n o
  2.  Kirai
  3.  K i s h a z i
  4.  Sentensi
  5.  K a m u s i

4.  Nyambua maneno yafuatayo iii kupata maneno mawili zaidi kwa kila neno;

  1. b e b a
  2. p o k e a
  3.  r u d i
  4.  s o m a
  5.  shughuli 
  6.  sema
  7.  p e n d a
  8. .heshimu
  9.  p i g o
  10.  p i k a

5   Bainisha tabia za maumbo yaliyokolezwa wino katika vitenzi ulivyopewa. 

  1.  Futa ubao.
  2.  Hutafaulu mtihani.
  3.  Ametualika.
  4.  Mtoto hulia mara nyingi.
  5.  Yeye ni mwalimu.
  6.  Mgonjwa amejilaza chini.
  7.  Wanavisoma vitabu vyao. 
  8. Paka amepigwa.
  9.  Mti umekatika.

6. (a) Eteza maana na dhima ya kiunganishi katika sentensi.

(b) Tunga sentensi mbili kwa kila kiunganishi kifuatacho;

  1.  kwa sababu
  2.  k a m a
  3.  i n g a w a
  4.  l a k i n i

7."Kuambatanisha maneno ni namna mojawapo ya kuzalisha maneno mapya katika lugha ya Kiswahili." Bainisha njia tatu za kuambatanisha maneno kisha toa mifano miwili kwa kila njia uliyobainisha.

SEHEMU C (Mama 10) UANDISHI

Jibu swali moja (1) kutoka katika sehemu hii.

8. Tofautisha muundo wa barua rasmi na barua za kindugu/kirafiki.

9. Jifanye kuwa mfanyabiashara wa mchele na unataka kuitangaza biashara yako nje na ndani ya nchi. Andika tangazo kuhusu biashara hiyo na jina lako liwe Pera Mlavi.

SEHEMU D (Alama 10)

MAENDELEO YA KISWAHILI

Jibu swali la kumi (10) .

10 "Sifa ya lugha ni kuwa na uwezo wa kupokea msamiati kutoka lugha za kigeni." Kwa kutumia mifano, eleza sababu nne zilizokifanya Kiswahili kuwa na maneno mengi ya Kiarabu kuliko kutoka lugha nyingine za kigeni.

SEHEMU E (Mama 45)

FASIHI KWA UJUMLA

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii. Swali la 15 ni la lazima.

ORODHA YA VITABU

USHAIRI

Wasakatonge                  - M.S. Khatibu (DUP)

Malenga Wapya TAKILUKI (DUP) 

Mashairi ya Chekacheka T.A. Mvungi (EP & D. LTD)

RIWAYA

Takadini                      Ben J. Hanson (MBS)

Watoto wa Mama Ntilie         E. Mbogo (H.P)

 Joka la Mdimu             AJ.Safari (H.P.)

TAMTHILIYA

 Orodha                         Steve Reynolds (MA)

 Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe           E. Semzaba (ESC)

Kilio Chetu                Medical Aide Foundation (TPH)

Eleza maana na matumizi ya methali zifuatazo:

(a) Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua. 

(b) Mchimba kisima huingia rnwenyewe.

(c) Ukiona zinduna ambari iko nyuma.

(d)Waarabu wa pemba wanajuana kwa vilemba.  

 (e)     Mbaazi ukikosa maua husingizia jua.

"Washairi hutumia mashairi yao kuelimisha jamii kuhusu mambo yanayoikabili." Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kutumia hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizosoma.

 "Mwanamke ni mtu mwenye huruma na fadhila." Thibitisha hoja hiyo kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu kutoka katika vitabu viwili vya riwaya kati ya vilivyoorodheshwa.

"Waandishi wa tamthiliya wameshindwa kufikisha ujumbe kwa jamii iliyokusudiwa." Kanusha  kauli hii kwa kutumia hoja tatu kwa kila kitabu kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma. Tunga • utenzi wenye beti nne (4) juu ya "Umuhimu wa Katiba Mpya Tanzania."

YEAR : 2017  SUBJECT : KISWAHILI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL

CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION

021             KISWAHILI

(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

Muda: Saa 3:00                                      Jumanne, 31 Oktoba 2017 mchana

Maelekezo

  1.  Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E zenye jumla ya maswali kumi na tano (15).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A, B na D, swali moja (1)      kutoka sehemu C na maswali    matatu (3) kutoka sehemu E. Swali la 15 ni lazima.
  3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.
  4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.
  5. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 10) UFAHAMU

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1.    Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.

Mipango ya elimu katika nchi mbalimbali duniani siku zote inahitilafiana, kimuundo na elimu itolewayo. Mipango hiyo huhitilafiana kwa sababu nchi zenyewe zinazotoa elimu huhitalifiana, kwa sababu elimu yoyote iwe ya darasani au si ya darasani, ina shababa yake. Shabaha yenyewe ni kurithishana maarifa na mila za taifa kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine na kuwaandaa vijana wawe tayari kuchukua nafasi zao katika kulitumikia na kuliendeleza taifa. Hivi ndivyo ilivyo katika nchi zote yaani nchi za kikabaila za Magharibi, nchi za kikomunist za Mashariki na hata zilivyokuwa nchi za kiafrika kabla ya ukoloni.

Kwa hiyo, sio kweli kusema kwamba kabla ya ukoloni waafirka hawakuwa na elimu, eti kwa sababu tu hawakuwa na shule, na kwamba makabila machache yalitoa mafunzo kwa muda mfupi tu kambini. Watoto na vijana walijifunza kwa kuishi na kutenda. Nyumbani au shambani walijifunza ufundi wa kazi zilizopaswa kufanywa, pamoja na tabia wanayopaswa kuwa nayo watu wa jamii ile. Vile vile walifijunza aina za majani na mizizi ya miti ya porini, na kazi zake; walijifunza namna ya kushughulikia mavuno na jinsi ya kuangalia mifungo. Haya yote waliyafanya kwa kushirikiana na wale waliowazidi umri au wakubwa kuliko wao.

HIvyo jamii zilijifunza historia za makabila yao, na uhusiano baina ya kabila moja na makabila mengine, uhusiano baina ya makabila yao na mizimu kwa kusikiliza tu hadithi zilizokuwa zikitolewa na wazee. Kwa njia hii na kwa desturi za kushirikiana walizofunzwa vijana, tamaduni za nchi ziliendelezwa. Kwa hiyo elimu waliyopata haikuwa y kukosekana kwa madarasa hakumaanishi kwamba hakukuwako elimu, wala hakukupunguza umuhimu wa elimu katika Taifa. Kwa msingi hiyo inawezekana kabisa kwamba elimu aliyokuwa akiipata kijana wa enzi zile ilikuwa elimu inayomfaa kuishi katika jamii yake.

Huko Ulaya elimu ya darasani ilianza siku nyingi. Lengo la elimu hiyo ya Ulaya ilikuwa sawa na ile iliyotolewa kwa mtindo wa asili wa Kiafrika, yaani, kwa kuishi na kutenda. Madhumuni makubwa yalikuwa ni kuimarisha mila zilizokuwa zikitumika katika nchi, na kuwanadaa awatoto na vijana kutimiza wajibu wao katika nchi hiyo. Na hivyo ndivyo ilivyo katika nchi za kikomunisti siku hizi. mafunzo yanayotolewa ni tofauti na yale yanayotolewa katika nchi za Magharibi, lakini lengo likiwa ni moja; kuwaandaa vijana kuishi katika taifa na kulitumikia taifa hilo, na kuendeleza busara, ujuzi na mila za taifa katika kizazi kijacho. Mahali popote ambapo elimu inashindwa kutimiza malengo hayo, basi maendeleo ya nchi hiyo yatalegalega, vinginevyo kutatokeo malalamiko watu watakapogundua kwamba elimu yao imewaandalia kuishi maisha ambayo kwa kweli hayapo.

 Maswali

  1. Eleza sababu mbili zinazosababisha nchi mbali mbali kuhitilafiana katika muundo wake wa elimu.
  2.  (i)      Fafanua namna jamii za kiafrika zilivyokuwa zinatoa elimu kwa watu wake.

     (ii)    Ni nami waliohusika kutoa elimu katika jamii za kiafrika?

  3. Elimu iliyotolewa katika jamii za kiafrika na ile iliyotolewa huko Ulaya zilikuwa na malengo gani?
  4. Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma.
2. Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasipungua mia moja (100) na yasiyozidi mia moja na arobaini (140).

SEHEMU B (Alama 25) SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA
Jibu maswali yote katika sehemu hii.


3. Katika kila sentensi uliyopewa, orodhesha vishazi huru katika Safu A na vishazi tegemezi katika safu B.
(a)       Ngoma hailii vizuri kwa kuwa imepasuka.
(b)       Watoto walioandikishwa watakuja kesho.
(c)       Kiongozi atakayefunga mkutano amepelekewa taarifa.
(d)       Mtawatambua walio wasikivu.
(e)       Kitabu ulichopewa kina kurasa nyingi.

4.   (a) Eleza maana ya kielezi kwa kutoa mfano wa sentensi moja.
(b) Kwa kila tungo uliyopewa pigia mstari kielezi na kisha taja ni cha aina gani.
(i) Darasani kuna utulivu mkubwa 
(ii) Wanafunzi wanaimba kimasihara.
(iii)  Mwalimu amerudi tena.
(iv)  Nitaondoka wiki inayokuja.

5.  Toa maana tano tofauti za neno “kibao” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana uliyotoa.

6. Moja ya faida ya misimu ni kuhifadhi historia ya jamii. Toa mfano mmoja wa misimu zagao iliyovuma Tanzania katika vipindi vifuatavyo:
(a) Muda mfupi baada ya kupata uhuru.
(b)  Miaka ya Azimio la Arusha.
(c)  Njaa ya mwaka 1974/1975.
(d)  Miaka ya vita vya Kagera.
(e)   Kipindi cha hali ngumu ya maisha baada ya vita vya Kagera.

7.   (a) Eleza maana ya kiarifu.
      (b) Kwa kutumia mifano, taja miundo minne ya kiarifu.

SEHEMU C (Alama 10) UANDISHI
Jibu swali moja (1) kutoka sehemu hii.

8.Andika barua kwa rafiki yako kuhusu mipango yako ya baadaye utakapoaliza Kidato cha Nne. Jina la rifiki yako liwe Dito Jito wa S.L.P 300 Longido na jina lako liwe Kijito Bahari wa Shule ya Sekondari Mtaweza, S.L.P 200 Dar-es-Salaam.

9.   Andika insha ya hoja isiyopungua maneno mia mbili na hamsini (250) na isiyozidi maneno mia tatu (300) kuhusu ‘Madhara ya Madawa ya Kulevya nchini Tanzania’.
SEHEMU D (Alama 10) MAENDELEO YA KISWAHILI
Jibu swali la kumi (10)

10. “Lugha ya Kiswahili imetokana na lahaja za Kibantu.” Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja mbili kuelezea chanzo cha lahaja na hoja tatu kuhusu matumizi ya lahaja katika Kiswahili sanifu.

SEHEMU E (Alama 45) FASIHI KWA UJUMLA
Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii. Swali la 15 ni la lazima.

ORODHA YA VITABU

USHAIRI
Wasakatonge                                              - M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya                                         - TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka                          - T.A. Mvungi (EP & D.LTD)

RIWAYA
Takadini                                                       - Ben J. Hanson (MBS)
Watoto wa Maman’tilie                              - E. Mbogo (H.P)
Joka la Mdimu                                             - A.J. Safari (H.P)

TAMTHILIYA
Orodha                                                        - Steve Reynolds (MA)
          Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe              - E. Semzaba (ESC)
Kilio Chetu                                         - Medical Aid Foundation (TPH)

11.Fasihi simulizi ikihifadhiwa katika maandishi hupoteza uhai na uhalisia wake. Fafanua changamoto nne zinazoweza kujitokeza kwa kuhifadhi fasihi simulizi katika maandishi.

12.“Msanii ni kinda la jamii husika hivyo anayoandika huihusu jamii hiyo.” Jadili kauli hii kwa kutumia hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizosoma.

13. “Elimu ni ufunguo wa maisha.” Fafanua kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu kati ya vitabu viwili vya riwaya vilivyoorodheshwa.

14. “Wahusika katika kazi za fasihi ni mfano wa kuigwa na jamii kwa tabia na matendo yao.” Thibitisha kauli hii kwa kutumia hoja tatu kwa kila mhusika kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma.

15.Tunga shairi la kimapokeo lenye beti nne kuhusu “Rafiki yako anayechamia shule nyingine.”

YEAR : 2016  SUBJECT : KISWAHILI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL

CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION

021 KISWAHILI

(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

Muda: Saa 3 Jumanne, 01 Novemba 2016 mchana

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E.

  1. Jibu maswali yote katika sehemu A, B na D, swali moja   (1)  kutoka sehemu C na maswali matatu (3) kutoka sehemu E. Swali la 15 ni lazima.

  1. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila   swali.

  1. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

  1. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 10) UFAHAMU

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.

Nchi yetu ya Tanzania imejulikana sana kutokana na mazingira yake yanayowavutia watalii. Hali yake ya hewa ni nzuri na yenye kutamanika. Mvua yake si nyingi na haichukizi bali ni ya rasharasha na tena ni ya hapa na pale. Majira yenyewe ya masika ni mafupi sana na hayana baridi kama huko ulaya.

Kitu hasa kinachowavutia watalii kutembelea nchi yetu ni pwani zetu ambazo zina mchanga mweupe na laini. Mchanga wenyewe hauna matope wala uchafu wowote. Kandokando ya pwani hizo kuna vichaka vyenye miti yenye rangi chanikiwiti na maua ya sampuli nyingi ya kutamanisha. Maua hayo yapo ya rangi nyekundu na vilevile hunukia vizuri, ama huweza kuwa na rangi ya manjano na kisha yakawa mviringo.

Kando kidogo unaweza kuona mawe makubwa yenye mapango makubwa mweusi ambamo wanyama wakubwa na wakali kama chui huishi. Pengine hata wanyama wa kuchekesha na hata watundu kama tumbili na kima huonekana humo.

Pembezoni, ambapo ni nje ya pwani zetu, kuna mashamba yenye mimea ya rangi ya kijani ikinawiri hasa wakati wa masika. Kipindi hiki wakulima nao huwa wanajishughulisha na matayarisho pamoja na maendeleo ya kazi zao za kila siku. Baadhi yao hupenda kufanya kazi huku wamevaa majoho marefu meupe au pengine shuka za kaniki zilizochakaa. Aidha, wengine hawajishughulishi kamwe na mambo ya mavazi kwani wao huvaa vikoi vikuukuu na vilivyokwajuka, bila kujali wapita njia.

Zaidi ya pwani zetu, watalii huvutiwa sana na mbuga zetu za wanyama wa porini. Wengi wa wanyama katika mbuga zetu huwa na gozi zenye madoa ya rangi za kuvutia. Pengine hata maungo yao huwa ya kutisha na yasiyokuwa ya kawaida. Mathalani ukimwona kifaru unadhani amekasirika na kwamba anataka kukurarua vipande vipande. Simba naye anajulikana kwa makucha yake marefu ya kutisha. Kiboko kwa upande wake, anajulikana kwa unene wake. Tumbo lake ni kubwa la kuchekesha kwani kila umwonapo utadhani matumbo yataporomoka dakika yoyote.

Basi mambo kama hayo na mengine mengi, ndiyo yanayowavutia watalii kuja kwetu. Watalii hawa ambao wengine kati yao ni warefu na pia wachangamfu lakini wapo walio wembamba na wepesi katika kuipanda milima yetu. Hata hivyo, wapo pia wazee vikongwe wenye ari na nguvu katika kuipanda milima hiyo. Wote hawa wanakuwa na hamu ya kutembelea vivutio vyetu. Baada ya kutembelea sehemu mbalimbali, hurudi kwao na furaha isiyo kipimo huku wakituachia fedha nyingi za kigeni.

Maswali

(a) Andika kichwa cha habari hii kisichozidi maneno manne.

(b)  Taja dhamira kuu inayotokana na habari hii

(c)  Mwandishi anatoa ushahidi gani kuthibitisha kuwa nchi yetu ina vivutio vingi vya utalii?

(d) “Wenyeji wa nchi yetu ya Tanzania nao ni sehemu ya vivutio vya utali” Thibitisha kauli hii kwa mujibu wa habari uliyosoma

(e)  Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kufungu cha habari

  1. Chanikiwiti

  2. Vilivyokwajuka

2. Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyozidi arobaini (40).

SEHEMU B (Alama 25) SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. (a) Eleza maana ya utohoaji.

(b) Maneno yafuatayo yametoholewa kutoka lugha gani?

  1. Picha 

  2.  Duka 

  3.  Shule

  4. Rehema  

  5. Shati

  6. Trekta 

  7.  Ikulu 

  8.  Bunge

  9.  Achali

4. Taja aina za sentensi zifuatazo kisha eleza muundo ujengao kila sentensi.

  1. Maisha ni safari ndefu.

  2. Ukisoma kwa bidii utafaulu kwa kiwango cha juu.

  3. Mtoto aliyelazwa hospitalini ameruhusiwa kwenda nyumbani.

  4. Nitakuja leo ingawa nitachelewa sana.

  5. Alinunua madaftari lakini kitabu cha Kiswahili alipewa na mwalimu.

5. (a) Eleza maana ya urejeshi katika kitenzi.

 (b) Tunga sentensi tatu zinazoonesha urejeshi wa:

  1. Mtenda nafsi ya tatu umoja.

  2. Mtendwa (idadi - wingi).

  3. Mtenda (kitu).

6. Andika maneno matano ambayo yameundwa kutokana na kufananisha sauti. Kwa kila neno tunga sentensi moja.

7. (a) Eleza maana ya Kiambishi.

(b) Bainisha viambishi vilivyopo katika vitenzi vifuatavyo:

  1. Tunalima.

  2. Wanatembea.

  3. Godoro.

SEHEMU C (Alama 10) UANDISHI

Jibu swali moja (1) kutoka sehemu hii.

8. Andika insha isiyozidi maneno mia tatu (300) na isiyopungua mia mbili na hamsini (250) kuhusu faida za televisheni kwa jamii.

9. Umechaguliwa kutoa risala kwa niaba ya wanakijiji wa kijiji cha Kisombogho, wanaotaka kutoa shukrani zao kwa Mkuu wa Wilaya aliyewachimbia kisima cha maji kijijini hapo. Andika risala utakayoisoma siku ya kikao.

SEHEMU D (Alama 10) MAENDELEO YA KISWAHILI

Jibu swali la kumi (10)

10. Taasisi ya Elimu (TET) na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) ni miongoni mwa asasi zilizoanza mara tu baada ya uhuru. Fafanua kazi tatu kwa kila moja katika kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Tanzania.

SEHEMU E (Alama 45) FASIHI KWA UJUMLA

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii. Swali la 15 ni la lazima.

ORODHA YA VITABU USHAIRI

Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)

Malenga   Wapya - TAKILUKI (DUP)

Mashairi   ya   Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D.LTD)

RIWAYA

Takadini - Ben J. Hanson (MBS)

Watoto   wa   Maman’tilie - E. Mbogo (H.P)

Joka   la   Mdimu - A.J. Safari (H.P)

TAMTHILIYA

Orodha - Steve Reynolds (MA)

Ngoswe Penzi Kitovu   cha   Uzembe - E. Semzaba (ESC)

Kilio   Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

11. (a) Kwa kutumia mifano dhahiri, jadili muundo wa vitendawili kwa kutoa hoja muhimu nne.

(b) Fafanua dhima tatu za vitendawili kwa jamii.

12. "Mshairi ni mwalimu wa viongozi wa nchi." Jadili kauli hii kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizosoma.

13. "Fasihi ya Kiswahili imemweka mwanamke katika hadhi tofauti tofauti." Thibitisha usemi huu kwa kutumia hoja tatu kwa kila riwaya kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.

14. Kwa kutumia hoja tatu kwa kila tamthiliya kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma, jadili kufaulu kwa waandishi katika kipengele cha utumizi wa tamthali za semi.

15. (a) Visasili ni nini?

(b) Tungakisasili kimoja kuhusu "Mnyama unayempenda."

YEAR : 2015  SUBJECT : KISWAHILI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL

CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION

021 KISWAHILI

(Kwa Watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

Muda: Saa 3:00 Jumatatu, 02 Novemba 2015 asubuhi

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E.

  1. Jibu maswali yote katika sehemu A, B na D, swali moja (1) kutoka sehemu C na maswali matatu (3) kutoka sehemu E. Swali la 15 ni lazima.

  1. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila   swali.

  1. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

  1. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 10) UFAHAMU

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.

Ustaarabu ni jambo jema ambalo hupendwa na kila jamii yenye utashi hapa duniani. Kila jamii yenye ustaarabu mambo yake huendeshwa kwa kuzingatia kanuni na taratibu zinazoeleweka. Maamuzi na mafanikio mbalimbali miongoni mwa wanajamii hutolewa bila hamaki wala kukurupuka. Kanuni na taratibu hizo huiongoza jamii kufikia upeo wake kimaendeleo kuanzia ngazi za chini kabisa ambayo ni familia mpaka ngazi ya juu kabisa ambayo ni taifa. Taratibu na kanuni hizo huwekwa katika chombo kimoja maalumu kinachoitwa katiba.

Katiba ni jumla ya sheria, kanuni na taratibu fulani zilizokubaliwa kuwekwa na jamii au taifa fulani kama dira ya maisha ya kila siku ya jamii au taifa hilo. Taifa bila katiba ni sawa na behewa la garimoshi bila injini. Hivyo katiba ina umuhimu wa kipekee katika taifa lolote lile.

Katika nchi zenye utamaduni wa kidemokrasia, katiba huundwa kutokana na maoni ya wananchi wake kwa utaratibu maalumu uliowekwa na serikali. Aghalbu, maoni na mawazo yaliyotolewa na wananchi huwa ni chimbuko la katiba hiyo. Wananchi hujiona ni sehemu ya utawala. Kwa upande wa pili wa sarafu, nchi zenye utaratibu wa kiimla, katiba hutayarishwa na watawala kwa maslahi yao binafsi. Katiba hutumiwa kama sera kwa maslahi ya watawala. Maoni na mawazo ya wananchi hayazingatiwi katika kuunda katiba.

Umuhimu wa katiba huonekana na kujidhihirisha waziwazi katika maisha ya kila siku ya nchi yoyote ile. Kwanza, katiba huelekeza wajibu wa ila mwanajamii kwa taifa lake na wajibu wa viongozi walio madarakani kwa wananchi au raia. Pili, katiba huonesha na kuainisha haki ambazo kila raia anastahili kupata na pia taratibu za kufuata katia kudai au dupewa haki hizo. Mbali na hayo, katiba hutoa utaratibu wa jinsi ya kuwapata viongozi wetu katika ngazi mabalimbali za kisiasa na kijamii. Pia uhuru wa mtu binafsi hulindwa na katiba. Hivyo, katika nchi ambayo ina katiba inayokidhi matarajio ya wananchi wote mambo huwa mazuri na kamwe chombo hakiwezi kwenda mrama.

Aidha, wananchi hawana budi kuelewa maana ya katiba ili waweze kutoa maoni na mapendekezo ya kuunda katiba mpya au kuimarisha iliyopo. Ni muhali kwa mtu asiyejua maana ya katiba kutoa maoni kuhusu katiba. Wananchi hupaswa kuelimishwa kupita semina, warsha na makongamano mbalimbali ili kujua katiba zao na kutoa maoni kuhusu uundaji wa katibu mpya.

Hata hivyo, wananchi wengi hasa vijana hawajitumi katika kuzijua katiba za nchi zao au kutoa maoni ya uundaji wa katiba mpya. Athari zake ni kutojua haki zao za msingi na kuburutwa kama mkokoteni na watawala katika mambo mbalimbali. Vilevile hulalamikia mambo ambayo hawakuchangia mawazo.

Hivyo basi, ni vizuri kwa wananchi kutambua, kuthamini na kuheshimu uwepo wa katiba kama kiongozi kizuri katika kuonesha njia muafaka ya kujiletea maendeleo kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kwa nchi husika.

Maswali

(a)  Toa maana ya maneno yote yaliyokolezwa wino kama yalivyotumika katika habari uliyosoma.

(b) Kwa mujibu wa habari uliyosoma, taja mambo mazuri mawili yatokanayo na uwepo wa katiba katika nchi.

(c)  Kwanini mwandishi anasema katiba hutumiwa kama sera kwa maslahi ya watawala?

(d) Je, ni hofu gani aliyonayo mwandishi dhidi ya vijana kuhusu katiba?

(e) Andika kichwa cha habari uliyosoma kisichozidi maneno matano (5).

2. Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua mia moja (100).

SEHEMU B (Alama 25) SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Watumiaji wa lugha ya Kiswahili hufanya makosa mengi bila ya kudhamiria. Taja aina mbili za makosa hayo kwa kutoa mfano wa sentensi mbili kwa kila kosa.

4. (a) Eleza maana ya rejesta.

(b) Kwa kutoa mifano, taja mambo muhimu matatu yanayomwongoza mtumiaji wa lugha katika uteuzi wa rejesta.

5. Katika kila sentensi andika neno moja lenye maana sawa na maelezo ya sentensi husika.

  1. Mtu anayechunguza uhalifu.

  2. Ng’ombe dume aliyehasiwa.

  3. Chombo cha usafiri kinachopita juu ya vyuma.

  4. Mti unaozaa matunda yanayotengenezwa kinywaji cha kahawa.

  5. Sehemu ndogo ya nchi iliyochongoka na kuzungukwa na bahari katika sehemu zake tatu.

6. Eleza dhima za mofimu "li" kama ilivyotumika katika sentensi zifuatazo:

  1. Shamba letu li kubwa sana.

  2. Wlishelewa kurudi.

  3. Tunalifuatilia.

  4. Limeharibika.

  5. Shikilia.

7. Andika sentensi zifuatazo katika hali ya ukanushi:

  1. Ameshiba sana.

  2. Watoto wengi wanaogelea.

  3. Mvua ilinyesha kwa wingi sana.

  4. Kijana anakula chakula kingi.

  5. Mimi nasoma polepole.

SEHEMU C (Alama 10) UANDISHI

Jibu swali moja (1) kutoka sehemu hii.

8. Jifanye wewe ni Gudhah Mukish anayeishi mtaa wa Tandamti - Gerezani Kariakoo na unataka kuuza gari yako aina ya TOTYOTA CARINA. Andika tangazo kwenye gazeti la Mwananchi.

9. Andaa kadi ya mwaliko kwa rafiki zako ili washiriki katika mahafali ya kumaliza Kidato cha Nne yatakayofanyika shuleni kwako siku ya Jumamosi tarehe 21/11/2015, kisha kufuatiwa na tafrija fupi itakayoandaliwa na wazazi wako katika ukumbi wa Kijiji mnamo saa 10.00 jioni. Jina lako liwe Sili Silali wa SHule ya Sekondari Kiriche.

SEHEMU D (Alama 10) MAENDELEO YA KISWAHILI

Jibu swali la kumi (10)

10. Chama cha Kiswahili cha Afrika (CHAKA) ni miongoni mwa taasisi zilizojitahidi katika kukuza na kueneza Kiswahili Barani Afrika. Eleza majukumu matano ya chama hiki katika kufanikisha azma hiyo.

SEHEMU E (Alama 45) FASIHI KWA UJUMLA

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii. Swali la 15 ni la lazima.

ORODHA YA VITABU

Ushairi

Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)

Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP)

Mashairi   ya   Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D.LTD)

Riwaya

Takadini - Ben J. Hanson (MBS)

Watoto   wa   Maman’tilie - E. Mbogo (H.P)

Joka la Mdimu - A.J. Safari (H.P.)

Tamthiliya

Orodha - Steve Reynolds (MA) Ngoswe Penzi Kitovu   cha   Uzembe - E. Semzaba (ESC) Kilio Chetu - Medical Aid Founda

11. Kwa kutumia mifano, fafanua kanuni muhimu nne za utunzi wa mashairi ya kimapokeo.

12. "Kazi za fasihi hufichua mivutano iliyopo katika jamii." Kwa kutumia hoja tatu kwa kila diwani fafanua mivutano hiyo kutoka katika diwani mbili ulizosoma.

13. "Mandhari iketeuliwa vizuri humsaidia mwandishi katika kufikisha yale aliyokusudia kwa jamii yake" Thibitisha hoja hiyo kwa kutoa mifano mitatu toka katika kila kitabu kati ya riwaya mbili zilizoorodheshwa.

14. Kwa kutumia tamthiliya mbili miongoni mwa zilizoorodheshwa eleza jinsi waandishi walivyoonesha athari za utamaduni wa kigeni katika maadili ya jamii ya kiafrika.

15. (a) Vigano ni nini?

(b) Tunga vigano kwa kutumia methali isemayo "Umdhaniaye siye kumbe ndiye!"

YEAR : 2014  SUBJECT : KISWAHILI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL

CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION

021 KISWAHILI

(Kwa Watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

Muda: Saa 3 Jumanne, 04 Novemba 2014 mchana

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E.

  2. Jibu maswali yote katika sehemu A, B na D, swali moja   (1)  kutoka sehemu C na maswali matatu (3) kutoka sehemu E. Swali la 15 ni lazima.

  3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila   swali.

  4. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

  5. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 10)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

UFAHAMU

1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

Karibu masikio ya watu wa mahali pengi yalijaa habari za Karama na mashtaka yake. Umaarufu wake wa ghafla ulizungumzwa karibu na mbali. Mtu yeyote wa desturi anapozuka katika umaarufu, huyavuta masikio na macho ya watu wengi kwa sababu jambo kama hili hutokea nadra sana kwa watu ambao bahati mbaya imeshughulika kuwaweka nyuma. Kwa hiyo, siku ya tatu ya baraza ilihudhuriwa na mfalme, watu wenye vyeo mbalimbali, pamoja na nusu moja ya umati mkubwa wa Kusadikika. Fikra zilizochanganyika ziliushika umati huu. Baadhi ya watu walimwajabia Karama wakamhesabu kama mtu bora wa karne yao. Hawa walitumaini ataokoka lakini wengine waliwaza kuwa Karama alikuwa kama mjinga aliyekuwa akicheza na hatari kubwa iliyofunua taya mbele yake.

Waliokuwa wakimtazamia kuokoka walikuwa na wasiwasi wao; na wale waliokuwa wakimtazamia kuanguka walikuwa na fadhaa yao. Walakini hapana mtu hata mmoja aliyepata kulisema wazo lake.

Bila ya kujua alivyoajabiwa Karama aliendelea kusema mbele ya baraza, “Watu wanaoteswa ndio wanaoyajua mateso yao.” Kusadikika ilikuwa chini ya mateso makubwa sana. Maisha yao yalizungukwa na maradhi na mauti, uadui usiokwisha, nchi iliyokaribia kugeuka jangwa na mwamba na madhila mengine mazito yaliyowakabili watu. Wanakusadikika walitaka faraja katika mateso haya. Kila jitihada ilijaribiwa ili kuirekebisha saa ya maendeleo ya nchi, lakini mara kwa mara majira yake yalirudishwa nyuma. Kama hili lilifanywa kwa makosa ama kwa makusudi ni siri iliyo ng’ambo ya fahamu zangu hata sasa. Lakini kama siri njema hufichika, ile iliyo mbaya haifichiki hata kidogo. Uchaguzi wa wajumbe ulikuwako lakini hathibitisho ya matokeo ya ujumbe hayakupatikana.

Kusadikika iliishi kuona mjumbe baada ya mjumbe kuadhiriwa na kuadhibiwa vibaya. Kama washauri hawakudhuriwa na hili lakini watu wengine walidhuriwa sana. Kazi njema za wajumbe wawili zilipotea bure. Manung’uniko ya lawama hii yalikuwa katika hewa yote ya Kusadikika.

Hili lilipotokea serikali iliombwa ima faima kufanya ujumbe mwingine. Basi mjumbe wa tatu alitakikana ajitolee mwenyewe kwa ujumbe wa Kusini. Wito wa mjumbe wa tatu uliitikiwa na Kabuli; mtu mwenye busara, haya na mcheshi. Yeye alipatikana upesi kabisa kuliko ilivyokuwa kwa mara ya pili na ya kwanza. Misiba ya Buruhani na Fadhili ilikuwa mikubwa ya kutosha kuikongoa mioyo ya bidii katika bawaba zake. Kabuli aliyajua haya yote lakini alikuwa mtu wa moyo wa namna nyingine kabisa. Alikuwa na bidii kubwa kama ile ya siafu athubutiye kukivuka kijito kwa daraja iliyofanywa kwa maiti ya siafu wengine walioelea majini huko na huko. Maji yalijulikana kuwa na asili ya rutuba, mvuke na umeme. Nguvu nyingine za namna mbalimbali zipo pia katika maji. Kama siafu mdudu mdogo na kipofu wakati mwingine haogopi kuzikabili nguvu hizo pamoja na hatari zake kwa sababu njema, basi ni dhahiri kuwa viongozi wa wanadamu wanapoteswa bure bidii za wafuasi wao hutanuka ajabu.

Hapana tishio liwezalo kuukomesha mwendo huu. Kwa hakika utafululiza kuwako duniani mpaka mateso yakome kabisa, na labda wakati huo dunia hii itakuwa njema kama itamaniwavyo kuwa.

Buruhani na Fadhili walitoa sadaka zao bora ili kuyahimiza majilio ya wakati uliotakikana sana. Kabuli aliwaona watu wawili hawa kama wafadhili wakubwa wa ulimwengu. Alitaka kuwa mshirika wao kwa thamani yoyote ya maisha yake.

Kama ilijulikanavyo, Kusini na upande wa dunia yatokako matufani makubwa na baridi kali sana. Kabuli aliyakabili mashaka haya bila ya kigeugeu. Naam, alikuwa kama mtu aliyekuwa akinywa uchungu bila ya kigegezi. Mara mbili alikamatwa akafanywa mahabusu.

Maswali

(a) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu cha habari:

  1. Fadhaa

  1. Madhila

  1. Kuadhiriwa

  2. Ima faima
  3. Kigeugeu
  4.  Kigegezi.

(b) Eleza mchanganyiko wa fikira walizonazo wana wa Kusadikika kuhusu Karama.

(c) Kwanini bidii ya mjumbe wa Kusini imelinganishwa na bidii ya siafu? Toa sababu mbili.

(d) Ujumbe wa mwandishi wa kifungu hiki unahusu nini?

2. Fupisha habari uliyosoma katika swali la kwanza kwa maneno yasiyopungua mia moja na hamsini (150) na yasiozidi mia mbili (200).

SEHEMU B (Alama 25) SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Fafanua utata uliopo katika sentensi zifuatazo:

  1. Mama anafurahia pango.

  2. Mwalimu analima barabara.

  3. Alimpigia ngoma.

  4. Kijana amepata fomu.

  5. Baba anaunda.

4. Tumia neno “Paa” katika sentensi kuunda dhana zifuatazo:

  1. Nomino

  2. Kitenzi

  3. Kielezi

  4. Kivumishi

  5. Shamirisho

5. Bainisha mzizi wa asili kwa kila neno katika maneno yafuatayo:

  1. Anawaandikisha

  2. Mkimbizi

  3. Mlaji

  4. Muumbaji

  5. Nisingelipenda

  6. Kuburudika

  7. Sadifu

  8. Aliokota

  9. Walichopoka

  10. Kipambanuliwe

6. Vibadilishe vitenzi vifuatavyo viwe katika kauli ya kutendeka:

  1. Badili

  2. Kata

  3. Komboa

  4. Zuia

  5. Fika

  6. Zoa

  7. Jenga

  8. Remba

  9. Tumia

  10. Lima

7. Fafanua maana ya neno “chenga” kwa kutumia sentensi tano tofauti.

SEHEMU C (Alama 10) UANDISHI

Jibu swali moja (1) kutoka sehemu hii.

8. Andika insha yenye maneno yasiopungua mia mbili (200) na yasiozidi mia tatu (300) kuhusu methali isemayo “Samaki Mkunje angali mbichi”.

9. Wewe ni mwenyekiti wa mtaa ambao umekumbwa na mafuriko lakini wananchi wako wanakataa kuhamia makazi mapya. Andaa hotuba utakayoitoa kwa wananchi wa mtaa wako ili kuwashawishi kuondoka katika sehemu hiyo. Jina la mtaa ni Kwamachombo na eneo la makazi mapya linaitwa Kitivo.

SEHEMU D (Alama 10) MAENDELEO YA KISWAHILI

Jibu swali la kumi (10)

  1. Kwa kutumia hoja tano, fafanua jinsi utawala wa Waingereza ulivyoimarisha Kiswahili nchini Tanzania kwa kupitia mfumo wa elimu.

SEHEMU E (Alama 45) FASIHI KWA UJUMLA

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii. Swali la 15 ni la lazima.

11. Kutokana na mabadiliko yanayoikumba jamii, baadhi ya methali zimepitwa na wakati. Thibitisha hoja hiyo kwa kutumia methali sita.

12. “Ustadi wa msanii hudhihirishwa na fani”. Dhihirisha kauli hiyo kwa kutumia vipengele vitatu vya lugha kwa kila diwani kutoka katika diwani mbili ulizosoma.

13. Jadili kukubalika kwa wahusika wawili kama kielelezo halisi cha wanajamii kati ya Takadini, Maman’tilie na Brown Kwacha kutoka katika riwaya mbili ulizosoma. Toa hoja tatu kwa kila mhusika.

14. “Kujenga jamii bora ni dhima ya mwandishi.” Thibitisha kauli hii kwa kutumia hoja tatu toka katika kila tamhtiliya kati ya tamthiliya mbili ulizosoma.

15. Tunga tamthiliya fupi kuhusu umuhimu wa elimu kwa vijana wa Tanzania ya leo. Tamthiliya hiyo isipungue maneno mia tatu (300).

ORODHA YA VITABU

Ushairi

Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)

Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP)

Mashairi ya Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D.LTD)

Riwaya

Takadini - Ben J. Hanson (MBS)

Watoto wa Maman’tilie - E. Mbogo (H.P)

Joka la Mdimu - A.J.Safari (H.P.)

Tamthiliya

Orodha - Steve Reynolds (MA) Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)

Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

YEAR : 2013  SUBJECT : KISWAHILI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL

CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION

021 KISWAHILI

(Kwa Watahiniwa Walioko Shuleni tu)

Muda: Saa 3 Jumanne, 05 Novemba 2013 mchana

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E.

  2. Jibu maswali yote katika sehemu A, B na D, swali moja (1) kutoka sehemu C na maswali matatu (3) kutoka sehemu E. Swali la 15 ni la lazima.

  3. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila   swali.

  4. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

  5. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 10) UFAHAMU

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

Baba alikuwa na wajibu maalum wa kuhakikisha usalama wa familia yake. Ilimbidi awe na nyumba watakamoishi mke na watoto. Nyumba zilijengwa kwa mitindo tofauti katika sehemu mbalimbali hapa nchini. Wanyakyusa walikuwa na ujenzi wao ambao ni tofauti na ule wa Wahaya. Wote wakijenga kwa ufundi wa kuvutia sana. Serikali yetu imehifadhi kwa njia ya makumbusho nyumba zilizojengwa na wakazi wa sehemu mbalimbali hapa nchini wakitumia mitindo yao ya asili. Nyumba hizi zipo katika kijiji cha makumbusho kilichopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Baba akishirikiana na mama walikuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa jamii yao ilipata chakula cha kutosha. Mapema watoto nao walishiriki katika shughuli za kutafuta na kuandaa chakula.

Jamii nyingine hapa nchini zilikuwa zikishughulika na ufugaji tu. Maisha na utajiri wa jamii hizi ulitegemea wanyama. Tangu utoto wao, mafunzo makuu yalihusu ufugaji. Kwa mfano, mtoto wa kimasai alijifunza kuchunga na kulinda wanyama wake tangu utotoni. Ilimbidi awe askari hodari, aweze kupambana na maadui waliotaka kuteka wanyama wao. Alitakiwa aweze kupigana na wanyama wakali porini wenye kuishambulia mifugo. Kumuua simba ilikuwa ni ishara kubwa ya uhodari wa kijana wa kimasai. Mafunzo ya kumwandaa kijana huyo, tangu utoto wake kwa kazi zitakazomkabili katika maisha, yalichukua sehemu kubwa ya malezi.

Kijana wa Kihaya alikabiliwa na mazingira tofauti sana na yale mwenzie wa kimasai. Wahaya ni wakulima, ufugaji ulichukua sehemu ndogo tu katika shughuli zao za kiuchumi. Wahaya hulima mazao ya kudumu kama vile migomba, mashamba yao yalihitaji ulinzi na utunzaji mzuri. Hivyo serikali imara yenye kuhakikisha amani katika nchi ili raia waweze kuendelea na kazi za kilimo kwa amani, ilihitajika. Pia Wahaya walihitaji nyumba za kudumu; maana hali ya maisha yao haikuruhusu uhamaji wa mara kwa mara kama vile Wamasai. Kwa hiyo mafunzo kamili yalihitajika ili kuwaandaa watoto kwa maisha ya namna hiyo.

Maisha katika sehemu mbalimbali katika nchi yalilazimu ziwepo njia maalum za kuwalea, kuwafundisha na kuwaandaa kwa yale yatakayowakabili katika siku za usoni.

Maswali

  1. Eleza faida mbili zinazoweza kupatikana kwa kuhifadhi mitindo ya nyumba za asili katika kijiji cha makumbusho.

  2. Unafikiri ni sababu gani iliifanya jamii ya Kimasai kuhamahama?

  3. Kwa mujibu wa habari uliyoisoma vijana walikuwa na jukumu gani katika jamii zao?

  4. Andika kichwa cha habari kisichozidi maneno matano kinachofaa kwa habari uliyoisoma.

  5. Andika methali ya Kiswahili inayoendana na aya ya mwisho ya habari uliyoisoma.

2. Fupisha habari uliyoisoma kwa maneno yasiyozidi mia moja (100).

SEHEMU B (Alama 25) SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Onesha nomino katika tungo zifuatazo kisha bainisha ni aina gani ya nomino:

  1. Hatuna budi kumshukuru Mola.

  2. Mazao yamestawi shambani.

  3. Uzalendo usisitizwe shuleni.

  4. Mpeleke mtoto ndani.

  5. Nimechoshwa na upweke.

4. Andika tungo zifuatazo kwa usahihi:

  1. Mwenyekiti alihairisha kikao.

  2. Mtoto amedumbukia shimoni.

  3. Kila mwanafunzi anatakiwa kuchangia deksi.

  4. Mama amenunua dazani ya sufuria.

  5. Mwanafunzi msafi amepewa zawadi.

5. Tambulisha viambishi vyenye dhima zilizowekwa kwenye mabano katika maneno yafuatayo:

  1. Hakukumbuka (njeo ya wakati uliopita)

  2. Wamekamatana (kauli ya kutendana)

  3. Akisema (hali ya masharti)

  4. Ananiona (kurejesha mtendwa)

  5. Tuliwashangilia (kurejesha watenda)

  6. Huimba (hali ya mazoea)

  7. Wamelima (wakati uliopita hali timilifu)

  8. Wanatucheka (urejeshi wa watendwa)

  9. Hawakusoma (ukanushi)

  10. Amenipigisha (kauli ya kutendesha)

6. Onesha maana tano za neno “kata” na kwa kila maana tunga sentensi moja.

7. “Upatanisho wa kisarufi ni kigezo kimojawapo kati ya vigezo vya kuunda ngeli za nomino.” Thibitisha dai hilo kwa kutunga sentensi ukitumia ngeli zifuatazo:

  1. U-I

  2. LI-YA

  3. U-ZI

  4. I-ZI

  5. U-YA

SEHEMU C (Alama 10) UANDISHI

Jibu swali moja (1) kutoka sehemu hii.

8. Wewe ni mfanyabiashara mashuhuri mjini Dodoma. Andika barua ya kutuma bidhaa kwa mteja wako aitwaye Dunia Msimbo anayeishi Lindi. Jina lako liwe Nyila Sasisha.

9. Andika tangazo kwenye gazeti la Rai ukitoa taarifa kuhusu kupotea kwa mwanao aitwaye Raha Karaha, jina lako liwe Furaha Machupa.

SEHEMU D (Alama 10) MAENDELEO YA KISWAHILI

Jibu swali la kumi (10)

10. Kwa kutumia hoja tano, onesha juhudi za Wajerumani katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili nchini wakati wa utawala wao.

SEHEMU E (Alama 45) FASIHI KWA UJUMLA

Jibu maswali matatu (3) kutoka sehemu hii. Swali la 15 ni la lazima.

11. Fafanua matatizo matano ya kuhifadhi kazi za fasihi simulizi kwenye kanda za kunasa sauti.

12. “Mshairi siku zote hukemea uonevu katika jamii.” Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizosoma.

13. “Fasihi ni chuo cha kufundisha maisha kwa jamii husika. “Jadili ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila riwaya kati ya riwaya mbili ulizosoma.

14 Chagua wahusika watatu wa kike, kutoka katika kila tamthiliya kati ya tamthiliya mbili ulizosoma, kisha onesha kukubalika kwao kama kielelezo cha maisha katika jamii.

15. Tunga tenzi yenye beti tano kuhusu ongezeko la watoto wa mitaani.

ORODHA YA VITABU

Ushairi

Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)

Malenga wapya - TAKILUKI (DUP)

Mashairi ya Chekacheka - T.A Mvungi (EP& D.LTD)

Riwaya

Takadini - Ben Hanson (MBS)

Watoto wa mama N’tilie - E. Mbogo (H.P)

Joka la Mdimu - A.J. Safari (H.P.)

Tamthiliya

Orodha - Steve Reynolds (MA) Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)

Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

YEAR : 2012  SUBJECT : KISWAHILI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL

CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION

021 KISWAHILI

(Kwa Watahiniwa Walioko Shuleni tu)

Muda: Saa 3 Jumanne, 9 Oktoba 2012 mchana

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E.

  2. Jibu maswali yote  katika sehemu A, B na D, swali moja   (1)  kutoka sehemu C na maswali matatu (3) kutoka sehemu E. Swali la 15 ni la lazima.

  3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila   swali.

  4. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

  5. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 10) UFAHAMU

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

Mtu hutembea njiani akajikwaa, ukucha ukang’oka au pengine hata kubwagwa chini vibaya na kisiki, kisha mtu huyu hugeuka na akakiangalia kisiki hicho, ambacho pengine huwa hata hakitazamiki.

Kama kisiki kimkwazavyo mtu atembeaye, pia mikasa mbalimbali, midogo kwa mikubwa, huwakwaza na pengine hata kuwabwaga chini binadamu katika maisha yao. Jinsi baadhi ya mikasa hii ilivyo adhimu, mtu anapokumbuka huweza kulia. Kwa upande mwingine mtu hujionea fahari alivyopambana na mikasa hiyo kwa ujasiri hadi akaishinda au kuikwepa. Tukio kama hili hufanya shajara la mambo bora ya kukumbukwa maishani.

Maisha ya shule ni mazuri, lakini mara nyingi huwa magumu na hasa lile wingu jeusi la mitihani likaribiapo. Wanafunzi hupuuza sheria kama vile kwenda madarasani, michezoni na pengine hata kula, wakajibanza mahali pa faragha wakajisomea. Nyakati zipendwazo ni usiku wa manane, kwa kujua kuwa kila mtu amelala na kuwa hayupo mwalimu wa zamu awezayo kuzuru shule wakati huo. Wanafunzi wenye bahati hunufaika sana kwa mpango huo wala hawagunduliwi. Wengine mara hugunduliwa wakapewa adhabu ambayo huridhika kuifanya kwani nzi kufa kwenye kidonda si hasara.

Siku hiyo ilikuwa Jumapili, nami nikajiunga katika ngoma ya kusoma na wenzangu wanne, wawili wao walikuwa viranja wa madarasa. Ilipata saa nane za usiku nasi tukaingia katika chumba cha kuoneshea picha, tukafunga mlango kwa funguo na komeo. Baada ya kuhakikisha kuwa hapana hata mwonzi mdogo wa taa uliotambaa nje, tulitoa ala zetu, kila mtu akashughulika na hamsini zake.

Hapakupita saa moja, mara tunasikia mlango unabishwa hodi, “fungua mlango! tokeni sasa hivi.” Sauti hiyo ilikuwa ya mmoja wa wanafunzi wa shule yetu. Mwanafunzi huyu aliandamana na mtu ambaye tulimtambua kwa sauti kuwa alikuwa Tatu, dada mkuu wa shule. Mioyo ilianza kutudunda kwa hofu, damu zetu zikawa karibu kuganda. Mara nilipata fahamu nikazima taa, lakini kwa bahati mbaya chumba hicho hakikuwa na madirisha ambayo kwayo tungeliweza kutoka. Kumbe mwanafunzi huyo naye alipata maarifa, alipanga viti kimoja juu ya kingine, akapanda juu na kuchungulia ndani katika mwanya uliokuwa karibu na dari. Kumulika ndani akamtambua Dora. Dora! Dora! fungueni mlango na tokeni sasa hivi!” akang’aka, lakini tukapiga kimya humo ndani.

Mwanafunzi huyo alipoona ameshindwa kututoa, alifanya hila ya kumwita mwalimu mkuu. Naam, sauti ya simba huweza kumdondosha chini panya aliyejificha darini. “Dora fungua mlango sasa hivi!” alinguruma, sote tulibaki tumeduwaa. Dora akafungua mlango, “ ushikwapo shikamana” wahenga walisema, mlango ulipofunguliwa mimi nilibana nyuma yake bila mtu kufahamu. Mwalimu mkuu aliwasha taa akachungulia ndani. Kuona hakuna mtu alizima taa akaondoka zake kwenda kuwadadisi wenzangu. Moyo ulishuka pwaa! nikatoka huku nagwaya mwili mzima, nikakimbia kwa mashaka makubwa hadi benini kwangu. Kwa vyovyote vile nilijua nilikuwa ndani.

Hazikupita hata datika tano tokea nijitupe kitandani nikashtukia taa zinawashwa mabwenini. Kumbe mwalimu mkuu, mwalimu wa zamu na Tatu, wakisaidiana na akina dada kadhaa walikata shari wafanye uchunguzi wa shule nzima, ili kuona iwapo wanafunzi wote walikuwepo. Ama kweli “ siku za mwizi arobaini,” wanafunzi wapatao kumi na watano walikuwa mjini ambako kulipigwa muziki na bendi mashuhuri kutoka Dar es Salaam. Asubuhi niliamka kichwa kizito nikauhisi mwili sio wangu. Masomo kuanza tu likapitishwa tangazo likiwaita wale wenzangu niliokuwa nao usiku na wale waliotoroka. Ilipofika saa nne, tukakuta wote wanafunga virago, nikaanza kuwa na matumaini kuwa ama kweli niliponea chupuchupu.

Maswali

(a) Fafanua maana za misemo ifuatayo kama ilivyotumika katika habari uliyosoma:

  1. Nzi kufa kwenye kidonda si hasara.

  2. Kila mtu akashughulika na hamsini zake.

  3. Ushikwapo shikamana.

  4. Siku za mwizi arobaini.

(b) Unafikiri kwanini uongozi wa shule aliyokuwa anasoma mwandishi ilipiga vita tabia ya wanafunzi kusoma wakati wa usiku wa manane.

(c) Una mawazo gani kuhusu kitendo cha Tatu kufuatilia mienendo ya wanafunzi wenzake hasa kwa usiku ule wa manane.

(d) Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma kisichozidi maneno matano (5).

2. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha andika ufupisho wa maneno arobaini (40).

Kamati imeundwa ikihusisha kikundi maalum cha wataalamu ambao watavalia miwani na kuandika upya historia ya Bara la Afrika. Mpango huu ni mahususi na tunaunga mkono wananchi wote. Ni mpango wa jinsi hii ambao utatokomeza maandishi yaliyoandikwa na wakoloni, waliopotosha ukweli wa maisha, mila na utamaduni wetu.

Vitabu vingi vya historia ya bara letu vinavyotumiwa na vijana shuleni, viliandikwa na watu waliokuja kutawala na kujitafutia mali. Katika maandishi yao walidiriki kutufanya tuamini kwamba lugha zao, lia na maisha yao vilikuwa na vitu azizi kuliko vyetu. Mpaka leo hii ni watu wachache wanaoamini kuwa tunao ustaarabu na utamaduni ulio imara tangu zama za wahenga. Tunaamini kuwa miaka michache ijayo upeo utageuka kabisa katika nadharia zilizo vichwani mwa watu wengi waliolishwa kasumba ya ukoloni.

SEHEMU B (Alama 25) SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Kwa kutumia mifano dhahiri, fafanua dhana zifuatazo:

  1. Kiima

  2. Chagizo

  3. Shamirisho

  4. Utohoaji

  5. Urudufishaji

4. “Maneno huweza kubadilika kutoka aina moja na kuwa aina nyingine.” Dhihirisha kauli hii kwa kubadili maneno yafuatayo kwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika mabano.

(a) Mkono (badili kuwa kielezi)

(b) Kwenda (badili kuwa nomino)

(c) Bora (badili kuwa kitenzi)

(d) Ogopa (badili kuwa kivumishi)

(e) Mzazi (badili kuwa kitenzi)

(f) Bisha (badili kuwa kivumishi)

(g) Refu (badili kuwa kitenzi)

(h) Linda (badili kuwa nomino)

(i) Kabati (badili kuwa kielezi)

(j) Uguza (badili kuwa nomino)

5. Kamusi ni muhimu kwa mtumiaji yeyote wa lugha. Taja hoja tano zinazothibitisha umuhimu huo.

6. Kwa kutumia mifano ya lugha ya Kiswahili, taja sababu tano za utata katika mawasiliano.

7. Kwa kutumia mifano, taja miundo mitano ya kirai nomino.

SEHEMU C (Alama 10) UANDISHI

Jibu swali moja (1) kutoka sehemu hii.

8. Jifanye kuwa umepata barua ya mwaliko wa sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa rafiki yako aitwaye Faraja Matata, itakayofanyika siku ya tarehe 10/10/2012. Kwa bahati mbaya siku tatu kabla ya sherehe umepata safari ya kikazi kuelekea mkoani Singida. Andika barua kumtaarifu rafiki yako kuwa hutaweza kuhudhuria sherehe hiyo. Jina lako liwe Tumaini Baraka.

9. Andika insha yenye maneno yasiyopungua mia mbili na hamsini (250) na yasiyozidi mia tatu (300) kuhusu umuhimu wa huduma za simu ya mkononi.

SEHEMU D (Alama 10) MAENDELEO YA KISWAHILI

Jibu swali la kumi (10)

10. Kwa kutumia mifano, onesha jinsi shughuli za dini, utawala, biashara na elimu zinavyokuza na kueneza lugha ya Kiswahili nchini Tanzania.

SEHEMU E (Alama 45) FASIHI KWA UJUMLA

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii. Swali la 15 ni la lazima.

11. “Maana ya methali inafungamana na muktadha, hivyo ikitumiwa vibaya inaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii.” Dhihirisha dai hilo kwa kutumia methali sita za Kiswahili.

12. “Washairi ni wataalamu wazuri na waliobobea katika kutumia taswira zinazotoa ujumbe kwa jamii.” Tumia taswira tatu kwa kila diwani kati ya diwani mbili zilizoorodheshwa kuthibitisha kauli hiyo.

13. Tumia vitabu viwili vya riwaya kati ya vilivyoorodheshwa, kutoa hoja tatu kwa kila kitabu, zinazothibitisha dai kuwa mwanaume ni kikwazo cha mafanikio katika jamii.

14. Tumia vitabu viwili vya tamthiliya kati ya vilivyoorodheshwa, kujadili madhara ya ukosefu wa elimu katika jamii. Toa hoja tatu kwa kila tamthiliya.

15. Umeteuliwa kuwa mmoja kati ya waandaaji wa shindano la sanaa za maonesho litakalofanyika wakati wa kusherehekea siku ya walimu duniani mwaka 2013. Andika majigambo yenye beti nne ya mhusika ambaye ni mwalimu.

ORODHA YA VITABU

Ushairi

Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)

Malenga wapya - TAKILUKI (DUP)

Mashairi ya Chekacheka - T.A Mvungi (EP& D.LTD)

Riwaya

Takadini - Ben Hanson (MBS)

Watoto wa Maman’tilie - E. Mbogo (H.P)

Joka la Mdimu - A.J. Safari (H.P)

Tamthiliya

Orodha - Steve Raynolds (MA) Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)

Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

YEAR : 2011  SUBJECT : KISWAHILI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL

CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION

021 KISWAHILI

(Kwa Watahiniwa Walioko Shuleni tu)

Muda: Saa 3 Jumanne, 4 Oktoba 2011 mchana

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E

  2. Jibu maswali yote katika sehemu A, B na D, swali moja (1) kutoka sehemu C na maswali matatu (3) kutoka sehemu E. Swali la 15 ni la lazima.

  3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.

  4. Vitokotozi haviruhusiwi katika chumba cha mtihani.

  5. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

  6. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 10) UFAHAMU

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

Misitu ya nchi ni mingi sana hata wakati mwingine tunadanganyika kuwa haitakwisha kamwe. Tunaamini kwamba tunaweza kuendelea kuitumia miti yake na kuikata kwa ajili ya kupata mashamba na malisho ya wanyama wetu bila kujishughulisha kupanda au kuhifadhi mingine kwa ajili ya siku za mbele. Fikiria tulivyo na mawazo potofu. Fikira mbaya kama hizo wanazo watu wengi nchini mwetu. Kwa hiyo imenilazimu kuwaonesheni kuwa misitu ni lazima ilindwe na haitalindwa kwa manufaa ya kizazi chetu cha sasa tu, bali pia kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo.

Basi mjue kuwa kama misitu yote itakatwa patakuwa na upungufu mkubwa wa mbao na pia upungufu wa maji ambao ni mbaya zaidi. Ubaya kama huu hautakiwi utokee katika Taifa letu linalosonga mbele. Hatuwezi kuruhusu uharibifu wa misitu yetu uendelee kufanyika kwa sababu unarudisha nyuma hali ya maisha yetu na unazuia ustawi wa nchi yetu. Hebu fikiria kwanza maisha yetu yatakuwaje iwapo miti itakosekana - taabu ya kupika, gharama ya kujenga kwa chuma, mawe au udongo ulaya badala ya miti. Gharama ya viti, vitanda na meza ikiwa vitatengenezwa kwa chuma tu. Halafu fikiria kama maji yote yakikauka, ninyi nyote mwajua shida zitakazotokea, kwa hiyo hatutaki kabisa shida kutokea.

Kwa nini tuwe na shida ya kukosa maji katika sehemu ambazo zina maji ya kutosha? Basi inatupasa kuona kwamba kuna ulazima wa kuhifadhi misitu kwa ajili ya matumizi ya leo na kesho.

Bila shaka sasa utajiuliza mwenyewe. Je, siwezi kukata kabisa misitu ili niweze kulima? Jibu ni kwamba unaweza kabisa, lakini ni katika sehemu zile ambazo hazikuhifadhiwa. Tena ifahamike kwamba sehemu ambazo zimehifadhiwa ni chache sana ukilinganisha na mapori makubwa yaliyobaki wazi kwa ajili ya kilimo.

Sasa nataka kusisitiza hasa juu ya misitu iliyohifadhiwa. Hizi ndizo sehemu za misitu ambazo ni za lazima sana, na inatakiwa zihifadhiwe daima kwa matumizi ya faida ya Taifa. Misitu iliyohifadhiwa ni misitu inayotazamiwa kudumu daima nchini. Inatunzwa ili itumiwe kwa utaratibu ulio bora kwa kizazi hata kizazi. Kwa wakati ujao misitu hiyo itatoa mbao za kujenga nyumba, shule, hospitali na majengo mengine, pia kutengeneza viti, meza, makabati, milango, madirisha na masanduku. Hata sasa, mbao nyingi zitumikazo hutokana na miti iliyoota katika misitu iliyohifadhiwa. Lakini kwa sababu ardhi yenye misitu ya aina hiyo inahitajiwa sana kwa kilimo, itatubidi kuanza kuotesha misitu mipya kwa ajili ya mahitaji yetu. Basi ni lazima niwakumbushe wananchi kuwa miti iliyomo katika misitu iliyohifadhiwa haitatosha kufanyia kazi zetu zote ili kuinua maisha ya watu na kuinua uchumi wa nchi. Misitu iliyohifadhiwa lazima iongezwe kwa kupanda miti mingine, kwa mfano hivi sasa Idara ya misitu inapanda miti kati ya eka elfu nne na tano kila mwaka na pia inaangalia miti ya asili katika sehemu kubwa kabisa ya nchi hii.

Maswali

  1. Kwa mujibu wa habari uliyosoma watu wengi hufikiria nini juu ya misitu?

  2. Mwandishi wa habari hii anasema ni jambo gani huleta uharibifu wa misitu?

  3. Mwandishi anashauri misitu ikatwe katika sehemu gani?

  4. Je, ni madhara gani yatatokea endapo misitu itatoweka kabisa?

  5. Je, ni sahihi kusema kuwa kwa vile kuna misitu iliyohifadhiwa hakuna haja ya kushughulika na kupanda miti nchini? Kwa nini?

2. Fupisha aya tatu (3) za mwisho za habari uliyosoma kwa maneno themanini (80).

SEHEMU B (Alama 25) SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Tumia kiambishi “KA” kuonesha matukio kumi (10).

4. “Kila lugha ina tabia ya kuchukua maneno kutoka lugha nyingine ili kukidhi mahitaji yake kimsamiati.” Fafanua kauli hii ukitumia maneno kumi (10) ya Kiswahili.

5. Yapange maneno yafuatayo kama yanavyoonekana katika kamusi, kisha eleza maana ya kila neno kwa kutoa mfano mmoja (1) wa sentensi.

(a)

Falsafa

(b) Barizi

(c) Anuwai

(d) Barubaru

(e)

Kinda

(f) Ajuza

(g) Fanusi

(h) Ghaibu

(i)

Goigoi

(j) Kinanda




6. Eleza maana ya upatanisho wa kisarufi. Fafanua jibu lako kwa kutoa mifano minne.

7. “Misemo mingi hutumika kwa madhumuni ya kulinda heshima na kuvuta makini ya watu.” Fafanua usemi huu kwa kutumia misemo mitano (5).

SEHEMU C (Alama 10) UANDISHI

Jibu swali moja (1) kutoka sehemu hii.

8. Andika insha isiyo ya kisanaa yenye maneno mia mbili na hamsini (250) kuhusu mandhari ya shule yenu.

9. Andika kumbukumbu za kikao cha wanafunzi kuhusu sherehe ya kumuaga mkuu wenu wa shule aliyepata wadhifa wa kuwa Afisa Elimu wa Mkoa.

SEHEMU D (Alama 10) MAENDELEO YA KISWAHILI

Jibu swali la kumi (10)

10. Fafanua athari ya Waarabu katika lugha ya Kiswahili kwa kutoa hoja nne (4).

SEHEMU E (Alama 45) FASIHI KWA UJUMLA

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii. Swali la 15 ni la lazima.

11. Sifa muhimu mojawapo ya methali ni kujenga picha au taswira ambazo huchotwa katika mazingira yanayoizunguka jamii.” Thibitisha hoja hii kwa kutumia methali tano (5).

12. “Maelekezo yanayotolewa na msanii wa fasihi hukidhi matarajio ya jamii yake.” Kwa kutoa hoja tatu (3) kwa kila mchairi, jadili kauli hii kwa kuwatumia washairi wawili (2) kati ya walioorodheshwa.

13. “Nyimbo ni mbinu ya kifani ambayo wasanii wengi huitumia ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira.” Thibitisha usemi huu kwa kutumia waandishi wawili (2) wa riwaya kati ya waliorodheshwa.

14. Jadili jinsi wasanii wawili (2) wa tamthiliya mbili (2) ulizosoma walivyotumia mbinu ya kicheko kutoa ujumbe walioukusudia kwa jamii.

15. Eleza muundo wa soga. Tunga soga ya kusisimua kuhusu kisa cha kubuni.

ORODHA YA VITABU

Ushairi

Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)

Malenga wapya - TAKILUKI (DUP)

Mashairi ya Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D. LTD)

Riwaya

Takadini - Ben Hanson (MBS)

Watoto wa Mama N’tilie - E. Mbogo (H.P)

Joka la Mdimu - A.J. Safari (H.P)

Tamthiliya

Orodha - Steve Raynolds (MA) Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)

Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

YEAR : 2010  SUBJECT : KISWAHILI

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL

CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION

021 KISWAHILI

(Kwa Watahiniwa walioko Shuleni tu)

Muda: Saa 3 Jumanne, 5 Oktoba 2010 mchana

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E.

  2. Jibu maswali yote katika sehemu A, B na D, swali moja (1) kutoka sehemu C na maswali matatu (3) kutoka sehemu E. Swali la 15 ni la lazima.

  3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.

  4. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

  5. Vikokotozi haviruhusiwi ndani ya chumba cha mtihani.

  6. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 10) UFAHAMU

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

  1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yatakayofuata:

Sikukuu ya kusherehekea uvunaji wa viazi vipya ilikuwa inakaribia na Umuofia ilikuwa katika hali ya matayarisho. Hii ilikuwa ndiyo siku ambayo watu walitoa kafara kwa Ani, Mungu wa rutuba ya ardhi na mwamuzi wa mwenendo na uadilifu wa watu wote. Alikuwa Mungu aliyehusika sana na maisha ya watu na mababu wa Umuofia waliozikwa katika ardhi yake.

Kwa sababu hii, sikukuu ilifanywa kila mwaka kabla mavuno hayajaanza. Hakuna mtu ambaye angeweza kula viazi vipya kabla havijatolewa sadaka kwa Ani au Mahoka wa mababu wa Umuofia.

Watu wote waliifurahia siku hii na kuingoja kwa uchu mkubwa kwa sababu yalikaribia majira ya vyakula maridhawa mwaka mpya. Watu wote waliokuwa na viazi vya mwaka uliopita ilibidi wavitupilie mbali kabla ya sikukuu hii haijaanza. Mwaka mpya ulitakiwa kuanzwa na vyakula vipya vilivyo vinono. Haikuwa heshima wala jambo la faraja kuendelea na vile vilivyokauka kutoka mwaka jana. Hata vyombo vya kupikia na vya kulia vilioshwa barabara. Kinu kile ambamo viazi vipya vilitwangwa kililazimu kusuguliwa sana.

Sikukuu ya viazi lilikuwa tukio la nderemo Umuofia nzima. Yeyote aliyekuwa na mkono wenye nguvu kama wazee wasemavyo alitegemea kualika wageni wengi kutoka karibu na mbali. Okonkwo aliwaalika ndugu wa wake zake na kwa sababu alikuwa na wake watatu, wageni hao walikuwa wengi wa kutosha.

Lakini ingawa hivyo, Okonkwo hakuwa mtu wa kufurahia sikukuu za aina yoyote. Ni kweli kwamba yeye aliweza kula sana, hata alipokunywa tembo alimaliza vibuyu vikubwa lakini kule kukaa bure bila kazi ndiko kulikomfanya asiwe na furaha. Furaha yake ilikuwa katika kazi ya shamba.

Sasa sikukuu ilikuwa imekaribia na wake zake Okonkwo walisugua kuta za vibanda vyao kwa udongo wa aina mbalimbali. Wao wenyewe walijipamba kwa kuchorachora matumbo yao na migongo. Wageni wengi walikuwa wamealikwa hata Ikemefuna alikuwa katika shamrashamra hiyo. Kwao pia kulikuwa na sikukuu kama hii lakini hapa ilionekana kubwa na ya kufana zaidi. Na kwao sasa kilikuwa kitu kilichoanza kupotea katika dunia ya kumbukumbu yake.

Maswali

  1. Eleza sababu mbili (2) zilizowafanya wananchi wa Umuofia waisubiri kwa uchu mkubwa siku iliyoelezewa kwenye kifungu cha habari.

  2. Kwa mujibu wa kifungu cha habari, eleza sifa moja (1) iliyomtofautisha Okonkwo na watu wengine wa Umuofia.

  3. Eleza maana ya maneno au kifungu cha maneno kilichokolezwa wino.

  4. Unafikiri ni sababu ipi kubwa iliyosababisha kutupwa kwa viazi vyote vya zamani na vyombo vyote kuoshwa?

  5. Andika kichwa cha habari kisichozidi maneno matano (5) kinachofaa kwa habari uliyosoma.

2. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha andika ufupisho wa maneno sitini (60) kuhusu habari hiyo.

Kwa miaka mingi baadhi ya mila na desturi zetu zimetufunga hadi kutufikisha mahali ambapo imekuwa ni vigumu kwetu kubaini ukweli kuhusu mambo muhimu yanayotuzunguka, yakiwa ni yale yanayohusu sisi na miili yetu na yale yaliyonje ya miili hii.

Kwa mfamo hadi leo kuna watoto wa umri mkubwa kufikia miaka saba ambao hawajui majina ya baba au mama zao. Lakini pia kuna vijana wa umri wa kuvunja ungo au balehe ambao hawajui ni kwa vipi mtoto anapatikana hasa maeneo ya vijijini. Kuna watu wazima ambao hadi leo mjadala kuhusu kifo ukiingizwa kenye mazungumzo huwa hawako tayari kusikiliza wakiamini kuwa huo ni mwiko na uchoro mkubwa. Hali hii kwa sehemu kubwa inatokana na desturi na mila zetu ambazo zimepogoka na zinahitaji kutazamwa upya kama zina faida kwa jamii. Baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakichukuliwa kama mwiko mkubwa kuyajadili hadharani au hata kati ya watu zaidi ya mmoja ni yale yanayohusu mbegu za kiume, yai la mwanamke na upatikanaji wa mimba.

Siyo jambo la siri kwamba mada zenye kuhusu mambo haya ni nadra sana kujadiliwa katika jamii zetu na wengi ni maamuma kabisa kuhusiana na masuala haya. Inawezekana ikawashangaza wengi pale mtu atakaposema kuwa mwanamume anaweza kumpa mimba mwanamke bila mwanamume huyo kukutana kimwili na mwanamke anayehusika.

SEHEMU B (Alama 25) SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Eleza tofauti za msingi mbili (2) zilizopo kati ya kirai na kishazi. Toa mifano miwili kwa kila tofauti.

4. Ni kigezo kipi kinachotumika katika kuunda ngeli za kimapokeo? Dhihirisha utumiaji wa kigezo hicho kwa kutunga sentensi tano (5) za ngeli tofauti.

5. Kwa kutoa mifano, taja matumizi matano (5) tofauti ya kiunganishi “Kwa”.

6. Eleza tofauti kati ya viambishi awali na viambishi tamati. Toa maoni yako kuhusu dhana ya viambishi “kati” katika Kiswahili.

7. “Mofimu huru zina hadhi ya neno.” Fafanua usemi huu kwa kutumia sentensi tano (5) tofauti.

SEHEMU C (Alama 10) UANDISHI

Jibu swali moja (1) kutoka sehemu hii.

8. Eleza tofauti iliyopo kati ya hotuba na risala. Andika hotuba kuhusu “Maji ni Uhai.”

9. Wewe kama afisa ununuzi, andika barua kwa mfanyabiashara mashuhuri wilayani kwenu kuhusu agizo la bidhaa.

SEHEMU D (Alama 10) MAENDELEO YA KISWAHILI

Jibu swali la kumi (10)

10. Kwa kutumia mifano, thibitisha ubantu wa Kiswahili kwa hoja madhubuti nne (4).

SEHEMU E (Alama 45) FASIHI KWA UJUMLA

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii. Swali la 15 ni la lazima.

11. Fafanua misemo ifuatayo:

  1. Mungu si Athumani

  2. Kata mzizi wa fitina

  3. Mtu kidole

  4. Kondoo si mali

  5. Kuiba kauli

12. “Kiongozi katika jamii ni nahodha ambaye hutakiwa aongoze chombo kisiende mrama.” Kwa kutumia hoja tatu (3) kutoka katika kila diwani jadili kauli hii ukitumia wasanii wawili uliowasoma.

13. Jadili jinsi fani ilivyotumika kukamilisha kazi za waandishi wawili (2) wa riwaya ulizosoma, ukizingatia mtindo na mandhari.

14. Waandishi wa tamthiliya wamemchora mwanamke katika sura tofauti. Thibitisha kauli hii kwa kutumia waandishi wawili (2) wa tamthiliya mbili (2) ulizosoma.

15. Tunga shairi la kimapokeo lenye beti nne (4) kuhusu unyanyasaji wa kijinsia.

ORODHA YA VITABU

Ushairi

Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)

Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP)

Mashairi ya Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D. LTD)

Riwaya

Takadini - Ben Hanson (MBS)

Watoto wa Mama N’tilie - E. Mbogo (H.P)

Joka la Mdimu - A.J. Safari (H.P)

Tamthiliya

Orodha - Steve Raynolds (MA) Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)

Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

   Click Here To Access You Scheme(ONLY IF YOU A HAVE CODE)