SURA YA 01 : MATUMIZI YA LUGHA
UTANGULIZI Sura hii inahusu matumizi ya lugha. Kwa hiyo, utajifunza dhana ya lugha (maana, sifa, na tabia), dhana ya pijini, krioli, lugha ya kwanza, lugha ya pili, lugha ya taifa, lugha ya kimataifa, na lugha rasmi. Vilevile, utajifunza dhana ya rejesta katika lugha, mambo ya kuzingatia katika kutumia lugha, misimu, umahiri wa lugha, na utata katika matumizi ya lugha. Lengo la kujifunza mada hizi ni kukuwezesha kutambua na kutumia mitindo anuwai ya lugha katika kuzungumza na kuandika. Baada ya kujifunza sura hii, utapata maarifa na ujuzi wa kuzungumza na kuandika kwa Kiswahili sanifu katika miktadha mbalimbali. |
Dhana ya lugha
Wataalamu mbalimbali wamefasili dhana ya lugha kwa mitazamo tofauti. Mathalani, TUKI (1990:35) wanasema kuwa lugha ni “mfumo wa sauti nasibu zinazotumiwa na watu wa jamii fulani wenye utamaduni unaofanana ili kuwasiliana.” Naye Crystal (1992) anaifasili lugha kuwa ni “mfumo wa sauti nasibu, ishara au maandishi kwa ajili ya mawasiliano na kujielezea katika jamii ya watu.” Aidha, Massamba (2004:45) anasema kuwa lugha ni “mfumo wa sauti nasibu ambazo zimebuniwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao.” Hivyo basi, kwa kuangalia fasili hizo tunaona kwamba, wataalamu hawa wanaonekana kukubaliana kwamba lugha ni mfumo wa sauti nasibu pamoja na mfumo wa ishara (alama), ambazo hutumiwa na jamii ya watu kwa madhumuni ya mawasiliano baina yao. Kwa ujumla, fasili hizi zinahusisha mambo ya msingi yafuatayo:
1. Mfumo
Lugha yoyote ile huundwa kwa mfuatano wa sauti ambazo huungana kuunda silabi. Silabi hizo huungana kuunda neno ambapo maneno nayo huwekwa pamoja kwa utaratibu maalumu ili kuunda sentensi zenye maana. Vilevile, sentensi hizo zikiunganishwa huunda kifungu cha habari. Mifumo ya miundo hii ndiyo hutofautisha lugha moja na nyingine na ndiyo huunda mfumo mzima wa lugha. Hata hivyo, kuna baadhi ya vipengele vya miundo hiyo ambavyo ni vya jumla, yaani vinapatikana katika lugha zote duniani.
2. Unasibu
Sauti za lugha ni sauti ambazo uteuzi wake haufanywi kwa kufuata utaratibu maalumu, bali unatokana na makubaliano ya kimazoea tu ya watumiaji wa lugha inayohusika. Kwa hiyo, hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kitaja na kitajwa. Hii inamaanisha kuwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya dhana au kitu kinachorejelewa (kitajwa) na neno linalotaja (kitaja). Kwa mfano, kitaja meza hakina uhusiano wa moja kwa moja na kitu kilichotengenezwa kwa mbao, chuma, madini, au kioo chenye uvungu na ubapa juu, kinachotumiwa kulia chakula, kuandikia, au kwa ajili ya michezo.
3 . Sauti
Sauti ndiyo msingi wa lugha. Kila lugha huunganisha sauti ili kuunda silabi na silabi kuunda neno na maneno kuunda tungo kubwa zaidi. Sauti hizo huunganishwa pamoja kwa utaratibu maalumu kulingana na lugha inayohusika.
4. Jamii ya wanadamu
Lugha ni chombo cha mawasiliano baina ya jamii ya wanadamu. Hii ina maana kuwa binadamu tu ndio wanaotumia lugha. Binadamu huteua na kuyapa maneno maana wanazozitaka kulingana na mazingira na tamaduni zao. Kwa msingi huu, tunaona kuwa mifumo ya mawasiliano ya viumbe wengine wasio binadamu haina sifa ya kuitwa lugha.
5. Mawasiiano
Lugha ni chombo cha mawasiliano miongoni mwa wanajamii. Kwa maana hiyo, lugha huwawezesha wanajamii fulani kuwasiliana baina yao na kuwasiliana na jamii nyingine. Kwa hiyo, lugha ni kiungo muhimu kati ya mtu na mtu, mtu na jamii, au taifa na taifa lingine.
Tabia za lugha
Lugha ya binadamu huwa na tabia zifuatazo:
1. Hukua
Lugha ya binadamu ina tabia ya kukua kadiri inavyotumiwa na jamii. Kukua kwa lugha hujumuisha kuongezeka kwa msamiati, na kupanuka kwa maana za maneno. Kukua huko kunatokana na mahitaji na mabadiliko ya jamii. Mathalani, maendeleo ya sayansi na teknolojia na uvumbuzi wa vitu na mambo mapya husababisha kukua kwa lugha. Vitu vinavyovumbuliwa hupewa majina na kusababisha kuongezeka kwa msamiati katika lugha. Kwa mfano, katika lugha ya Kiswahili, msamiati ambao umetokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia ni kama vile runinga, king’amuzi, tovuti, simufifi, na simumtelezo.
2. Kuathiriana
Lugha ya binadamu ina tabia ya kuathiri au kuathiriwa na lugha nyingine. Lugha mbili au zaidi zinapokaribiana huweza kuathiriana katika vipengele mbalimbali kama vile msamiati, muundo, au maana. Kwa mfano, lugha ya Kiswahili imeathiriwa na Kiarabu, Kiingereza, Kijerumani, Kireno, Kifaransa na Kiajemi, hususani katika kipengele cha msamiati. Vilevile, lugha ya Kiswahili imeathiri lugha nyingine za Kibantu zilizopo Tanzania katika msamiati.
3. Ubora wa lugha
Lugha yoyote ile ya binadamu inajitosheleza katika matumizi yake. Hujitosheleza kulingana na mahitaji ya jamii inamotumika katika kipindi husika. Lugha huwawezesha watumiaji wa jamii inayohusika kuwasiliana na kushiriki katika majukumu mbalimbali. Kwa hiyo, tunaweza kusema kuwa hakuna lugha bora kuliko nyingine. Kila lugha ni bora katika muktadha wa matumizi yake.
4. Kitambulisho cha utamaduni
Kila lugha huwa ni kitambulisho cha utamaduni wa jamii fulani inayotumia lugha hiyo. Lugha hubeba dhana za shughuli, majina ya watu na vitu vilivyopo katika jamii inayohusika. Dhana hizi hubeba utamaduni wa jamii hiyo. Kwa mfano, majina ya Kiswahili kama vile Uhuru, Azimio, Amani, Chausiku, Chiriku, au Mwanaheri yanadokeza dhana zinazobeba matukio fulani katika jamii ya Waswahili.
6 Lugha hufa
Lugha huwa na tabia ya kufa. Lugha yoyote duniani isipotumiwa kwa muda mrefu hufa. Hali hii inajitokeza pale ambapo wazungumzaji wa lugha inayohusika watatoweka au kuacha kuitumia lugha hiyo na kuanza kutumia lugha nyingine. Uhai wa lugha hutokana na kutumiwa katika nyanja mbalimbali za kijamii. Kwa mfano, baadhi ya lugha za Kibantu, mathalani Kividunda (Morogoro) na Kikahe (Moshi), zinasemekana kuwa ziko hatarini kutoweka kwa sababu ya kupungua kwa wazungumzaji wake.
Istilahi za lugha
Kuna istilahi mbalimbali ambazo zinatumika katika kujifunza na kuelezea dhana mbalimbali kuhusu lugha. Dhana hizo ni pijini, krioli, lugha ya kwanza (L1), lugha ya pili (L2), lugha ya taifa, lugha ya kimataifa na lugha rasmi.
1. Pijini
Pijini ni lugha ya mawasiliano inayozaliwa kutokana na makundi mawili ya watu wanaotumia lugha tofauti kukutana na kushirikiana katika shughuli za kijamii au kiuchumi. Kwa kuwa watu wanaokutana huwa hawana lugha moja inayowaunganisha kimawasiliano katika shughuli mbalimbali, huamua kuunda lugha moja itakayokidhi mawasiliano yao kwa kipindi fulani. Pijini huwa ina tabia ambazo ni tofauti na lugha zinazozungumzwa na makundi yanayohusika.
Sifa za pijini
Pijini ina sifa zifuatazo:
2. Krioli
Krioli ni pijini iliyokomaa. Hivyo, krioli huzaliwa kutokana na pijini. Watu wanaozungumza pijini wanapooana na kuzaa watoto, watoto hao huzungumza lugha ambayo si ya mama wala ya baba, bali huzungumza lugha hiyo mpya ambayo ndiyo huitwa krioli. Lugha hii inaweza kuwa na msamiati mwingi zaidi kutoka lugha moja, au msamiati sawa kutoka lugha zinazotumiwa na wazazi wa watoto hao.
Sifa za krioli
Krioli ni lugha yenye sifa zifuatazo:
3 Lugha ya kwanza (L)1
Hii ni lugha ambayo mtu huiamili kwa mara ya kwanza kutoka kwa wazazi au walezi au jamii inayomzunguka baada ya kuzaliwa. Mtu huamili lugha ya kwanza kwa urahisi na kuwa mahiri kutokana na kukulia katika jamii inayotumia lugha hiyo. Lugha ya kwanza hujulikana pia kama lugha mama kwa sababu ni lugha ambayo hutumika katika kumlea na kumkuza mtu hadi pale anapopata ufahamu wa kuamili au kujifunza lugha nyingine. Lugha ya kwanza ina sifa zifuatazo:
Lugha ya kwanza hutumika katika kufanikisha mawasiliano kati ya mtoto na wazazi na jamii inayomzunguka. Kwa mfano, katika mazingira ya Tanzania, wale waliozaliwa vijijini hujikuta wakiamili lugha za jamii zao kama lugha ya kwanza. Kwa upande wa wale waliozaliwa mijini huwa na nafasi kubwa ya kuamili Kiswahili kama lugha yao ya kwanza.
4. Lugha ya pili (L)2
Hii ni lugha ambayo mtu hujifunza baada ya kuamili lugha ya kwanza. Kwa mfano, Kiswahili katika jamii ya Watanzania ni lugha ya pili kwa baadhi ya watu, hususani waliokulia vijijini. Aidha, watu wengi waliozaliwa mijini hujifunza lugha ya Kiingereza kama lugha ya pili. Mtu hujifunza lugha ya pili akiwa na malengo ya kufanya jambo fulani kama vile kufanya mawasiliano na watu wa jamii nyingine katika shughuli za kijamii, kibiashara, kielimu, na kadhalika. Lugha ya pili ina sifa zifuatazo:
Lugha ya pili hutumika katika kuwaunganisha watu wenye lugha tofauti. Vilevile, lugha hii hutumika kama nyenzo ya kufundishia na kujifunzia. Kwa mfano, nchini Tanzania lugha ya Kiswahili, ambayo ni lugha ya pili kwa baadhi ya Watanzania, hutumika kufundishia katika elimu ya msingi, hususani katika shule za serikali.
5. Lugh a ya taifa
Hii ni lugha ambayo huteuliwa na taifa fulani kuwa utambulisho wa taifa hilo, na kutumika katika mawasiliano baina ya watu wake. Kwa upande wa Tanzania, lugha ya Kiswahili ndiyo lugha ya taifa tangu mwaka 1963. Aidha, lugha ya Kiswahili ni lugha ya taifa katika nchi za Kenya, Uganda na Rwanda. Hivyo, Kiswahili ni utambulisho wa utamaduni wa jamiilugha ya Waswahili mbele ya jamii nyingine duniani. Lugha ya taifa ina sifa zifuatazo:
Hata hivyo, ifahamike kwamba lugha ya taifa huweza kuwa zaidi ya moja. Kwa mfano, lugha za taifa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (JKK) ni nne; Kituba, Chiluba, Lingala, na Kiswahili.
6. Lugha ya kimataifa
Lugha ya kimataifa ni lugha inayotumiwa na idadi kubwa ya watu katika mataifa mbalimbali. Hii ni lugha ambayo matumizi yake yamevuka mipaka ya taifa moja; yaani hutumika katika mataifa zaidi ya moja. Husaidia katika kukidhi mahitaji ya mawasiliano ya watu wenye lugha tofauti tofauti kutoka mataifa mbalimbali. Mifano ya lugha za kimataifa ni kama vile Kiswahili, Kiingereza, na Kifaransa. Lugha ya kimataifa huwa na sifa zifuatazo:
7. Lugha rasm i
Lugha rasmi ni lugha ambayo huteuliwa na serikali ili itumike katika shughuli za kiserikali. Lugha ya Kiswahili ni lugha rasmi nchini Tanzania, na inatumika katika nchi za kigeni. Pia, inaweza kuwa zaidi ya moja kama ilivyo nchini Tanzania ambapo lugha rasmi ni Kiswahili na Kiingereza. Lugha hizi ziliteuliwa kuwa lugha rasmi mwaka 1963. Kimsingi, lugha rasmi hutumika katika mawasiliano, hususani katika shughuli rasmi za kijamii, ofisini, shuleni na katika mihimili ya serikali kama vile bunge, mahakama na katika baraza la mawaziri. Lugha rasmi ina sifa zifuatazo:
Tofauti na ilivyo katika nchi ya Tanzania ambapo Kiswahili kina hadhi ya kuwa lugha ya taifa na lugha rasmi, lugha rasmi na lugha ya taifa zinaweza kuwa lugha mbili tofauti katika nchi moja.
Rejesta
Lugha hutumika katika mazingira mbalimbali ambako kuna watu wanaofanya shughuli tofauti tofauti. Kutokana na kuwa na mazingira yanayotofautiana kishughuli, kimahusiano na kiutamaduni, matumizi ya lugha moja hutofautiana. Mitindo ya matumizi ya lugha fulani katika mazingira mahususi ndiyo huitwa rejesta. Kwa mfano, lugha inayotumika katika makundi ya wavuvi, wawindaji, wafanyabiashara, na wanamichezo inatofautiana kwa kiasi fulani.
Mambo yanayosababisha kuzuka kwa rejesta
Rejesta huzuka kutokana na mambo mbalimbali. Miongoni mwa mambo hayo ni haya yafuatayo:
1. Upekee
Hii ni hali waliyonayo kikundi fulani cha watu katika namna ya kusoma au kuzungumza. Hali hii hutofautisha kikundi kimoja na kingine katika utumiaji wa lugha. Upekee huu huweza kujitokeza katika matamshi na msamiati. Hivyo, watu wanakuwa na mtindo wao wa kuzungumza ambao haubadiliki kila wanapozungumza katika muktadha mahususi.
2. Shughuli iliyopo
Shughuli inayotendeka katika mazingira mahususi hutupatia rejesta za mahali kama vile, kanisani au msikitini, sehemu za biashara, mahakamani na bandarini. Kwa mfano, katika shughuli ya harusi kuna rejesta yake inayoweza kuoneshwa na maneno kama vile, hongera kwa kupata jiko, anameremeta, tumpambe maua, na kadhalika.
3 . Mahitaji ya kuficha jambo
Matumizi ya lugha kwa lengo la kuficha mambo husababisha kuzuka kwa rejesta miongoni mwa wazungumzaji wa lugha moja. Kwa mfano, vijana wakiwa vijiweni wanaweza kutumia mtindo wa lugha ambao watu wenye umri tofauti wanaweza wasielewe kinachosemwa. Wanapotumia maneno kama vile oya mwanangu, tujikate wakimaanisha tuondoke, mtu wa rika lingine anaweza asielewe.
Dhima za rejesta
Rejesta zina dhima zifuatazo katika matumizi ya lugha:
Mambo ya kuzingatia katika kutumia lugha
Matumizi ya lugha yoyote hutawaliwa na mazingira ya watumiaji wa lugha hiyo. Kwa hiyo, watumiaji wa lugha huongozwa na mambo ya msingi yafuatayo katika mitindo mbalimbali ya lugha wanayotumia.
1. Uhusiano wa wazungu m zaji
Uhusiano wa wazungumzaji huamua aina ya lugha ya kutumia, uteuzi wa maneno, na utamkaji. Kwa mfano, mtu mwenye cheo cha chini ataonesha tofauti ya jinsi atakavyotumia lugha anapoongea na mkuu wake wa kazi tofauti na anapoongea na mtu mwenye cheo kama chake. Uhusiano huu unaweza kuwa wa rika, madaraka, au familia. Chunguza mazungumzo yafuatayo ya marafiki wawili:
Mazungumzo 1
Kibude: Oya wangu, vipi mambo?
Kwezu: Poa mwanangu. Inakuwaje?
Kibude: Baridi mshikaji. Mambo leo siyo shwari wangu!
Kwezu: Vipi, maji shingoni siyo! Usikonde. Kuna ishu ikienda poa basi ...
Kibude: Basi taim, taim ... nistue. Nipo maskani.
Kwezu: Poa!
Mazungumzo 2
Nduke: Vipi mshikaji, mbona unamisi skuli siku hizi? Niaje?
Ndosi: Ah! Si yule ticha Mbwetu ... ananimaindi saana!
Nduke: Niaje kwani?
Ndosi: Si juzi kati dogo, nilikuwa viwanja kwenye anga zangu basi ndo ...
Nduke: (Anamuona baba yake anakuja). Kausha basi dogo, dingi huyooo.
Ndosi: Haina mbaya braza. Samtaim basi, tujikate mshikaji.
(Wanatawanyika kila mmoja anaelekea upande wake)
Mazungumzo haya yanaonesha jinsi kuzoeana kwa vijana kunavyowapa uhuru wa kutumia maneno. Unaposoma mazungumzo haya unaona jinsi vijana hawa wa rika moja wanavyozungumza lugha ya Kiswahili ambapo si rahisi kwa mzungumzaji wa Kiswahili wa rika lingine kuelewa kwa urahisi kile kinachozungumzwa.
2. Mada inayozungu m ziwa
Mada inawafanya wanaozungumza kuchagua maneno yanayohusiana na jambo linalozungumziwa na kuhakikisha kuwa maneno hayo yanawasilisha dhana na ujumbe uliokusudiwa. Hii inawafanya wazungumzaji kuelekeza fikira zao kwenye jambo linalozungumziwa. Kwa mfano, wazungumzaji wanaozungumzia mambo ya ufundi wa magari watatumia maneno kama vile injini, giaboksi, breki padi, rejeta, na klachi. Wazungumzaji wa mambo ya utabibu wa hospitalini watatumia maneno kama vile vipimo vya malaria, vidonge na sindano. Iwapo tiba hiyo inahusiana na uganga wa kijadi, wazungumzaji watatumia maneno kama vile tunguli, ramli, mavumba, ubani, kifungua mkoba, na kadhalika.
3 . Muktadha
Muktadha ni mazingira au mahali ambapo tukio au jambo hutendeka. Muktadha ni kitu cha kuzingatia katika matumizi ya lugha kwa sababu humsaidia mtumiaji wa lugha kutumia lugha inayotakiwa katika mazingira ya tukio linalohusika. Lugha inayotumika katika miktadha mbalimbali hujibainisha kwa shughuli za mazingira ambamo lugha hiyo inatumika. Mazingira yanaweza kuwa ya kidini, kisheria, kisiasa, kibiashara, au yale ya migodini, bandarini, hotelini, sokoni, ofisini, na kadhalika. Katika matumizi ya lugha, mazingira kama hayo ndiyo yanayowafanya wazungumzaji kuibua maneno maalumu yanayotumika katika mazungumzo yao. Chunguza mazungumzo yafuatayo:
Hakimu: Ninakuuliza, jaribio la kuvunja nyumba kwa kutumia silaha na kukusudia kuiba lilitendeka?
Mbiche: Hapana mheshimiwa hakimu. Mimi sikuwa na kusudio hilo bali nilipopita na kuusogelea mlango sikujitambua kwani nilikuwa nimelewa.
Hakimu: Ulikuwa na silaha gani ulipousogelea mlango?
Mbiche: Sikuwa na silaha yoyote, bali kulikuwa na shoka nje ya nyumba ambalo lilisahaulika wakati wenye nyumba walipokwenda kulala.
Hakimu: Umewezaje kukumbuka shoka uliloliona usiku, ilhali wewe ulikuwa umelewa kiasi cha kukosa kujitambua?
Mbiche: Kwa neema tu mheshimiwa hakimu.
Hakimu: Shauri lako linaahirishwa hadi tarehe 03.04.2016 litakaposomwa tena. Dhamana yako imekataliwa na utarudi tena rumande.
Mazungumzo haya ni mazungumzo ya mahakamani kwa sababu kuna msamiati wa mahakamani kama vile hakimu, shauri, dhamana, na rumande, pamoja na matumizi ya lugha rasmi. Mara nyingi mahojiano katika mahakama hayaendi haraka haraka. Kwa mfano, kila mtu anayehusika hususani hakimu, mwendesha mashtaka, wakili, mshtakiwa, na shahidi hujieleza kwa uwazi bila kujali urefu wa maelezo yake. Hivyo, tunaweza kusema kuwa hii ni rejesta ya mahakamani.
Kwa upande mwingine, rejesta ya mahakamani ni tofauti na rejesta ya hotelini, mahali ambapo watu hupata huduma ya chakula. Lugha ya hotelini ina mtindo wake ambao, katika hali ya kawaida, huenda isieleweke kwa mtu asiyehusika katika mazungumzo hayo. Chunguza mazungumzo yafuatayo:
Mhudumu: Nani mbuzi?
Mteja: Mimi!
Mhudumu: Kuku?
Mteja: Hapa!
Mhudumu: Biriani?
Mteja: Mimi!
Mzungumzaji anapouliza, “Nani mbuzi?” haimaanishi kuwa anamuulizia mtu anayeitwa Mbuzi, bali anaulizia mteja aliyeagiza nyama ya mbuzi. Pia, anaposema kuku anamaanisha mteja aliyeagiza kuku. Aidha, anaposema biriani hakuna mteja anayeitwa biriani, bali mteja aliitikia akiwa na maana angehitaji kula biriani.
4. Lengo la mazungumzo
Lengo la mazungumzo humwezesha mtumiaji wa lugha kuteua mtindo wa lugha ya kutumia. Mtu mwenye lengo la kuomba hela atatumia lugha ya unyenyekevu na upole. Mtu huyo huyo akiwa na lengo la kuelimisha kuhusu athari za matumizi ya simu, atatumia lugha ya kuonya, kusisitiza, na kushauri.
Mitindo ya matumizi ya lugha
Dhana ya mitindo ya lugha inakwenda sambamba na dhana ya rejesta katika lugha. Mitindo ya lugha, katika mazungumzo au maandishi, hurejelea namna au jinsi lugha inavyotumika katika mazingira na shughuli maalumu. Kwa hiyo, mitindo ya lugha husaidia pia kubaini aina za rejesta. Kuna mitindo mbalimbali ya lugha ambayo inaweza kuwa katika makundi yafuatayo:
1. Mtindo wa lugha ya kiofisi
Mtindo huu hutumika katika mawasiliano rasmi ambayo hufanyika katika ofisi au mahali popote pa kazi. Mtindo huu huweza pia kujulikana kama mtindo wa lugha ya kikazi. Mtindo huu hutumika katika mikataba, sera, kanuni za kazi, matini za kisheria, matangazo ya vikao, ripoti za mikutano, na kadhalika.
Sifa za mtindo wa lugha ya kiofisi
Chunguza mfano wa lugha yenye mtindo wa kiofisi:
|
2. Mtindo wa lugha ya kitaaluma
Huu ni mtindo unaopatikana katika vitabu na majarida ya kitaaluma na katika utoaji wa mafunzo yanayohusu elimu. Mtindo huu hutumika shuleni, vyuoni, kwenye semina, warsha, makongamano, na ripoti mbalimbali za kitaaluma.
Sifa za mtindo wa lugha ya kitaaluma
3. M tindo wa luia ya magazetini
Mtindo huu hutumika katika uandishi wa habari katika magazeti.
Sifa za mtindo wa lugha ya magazetini
Chunguza mfano ufuatao wa uandishi wa magazetini.
Taifa Stars Yairarua Malawi : Samatta atupia mawili Msuva akihitimisha karamu ya magoli matatu Kielelezo 1.1 Mtindo wa lugha ya gazetini Dar es Salam. Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli matatu kwa sifuri katika pambano la kukata na shoka dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi. Katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa. Mshambuliaji hatari wa Tanzania na timu ya Genk, Mbwana Samatta alifunga magoli mawili kabla Simon Msuva hajapigilia msumari wa mwisho katika dakika ya 89. Mchezo huo ulishuhudiwa pia na Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.. (Chanzo: Gazeti la Mtanzania 7/10/2017) |
4. Mtindo wa lugha ya mazungumzo na maandishi ya kawaida
Haya ni maongezi au maandishi ya kawaida yanayotumika kila siku nyumbani, katika sehemu za starehe, kwenye misiba, na mahali pengine popote pasipohusika na shughuli za kiofisi, kikazi, au kitaaluma.
Sifa za mtindo wa lugha ya mazungumzo na maandishi ya kawaida
Zoezi la 1.1
|
Misimu
BAKITA (2015) wanafasili msimu (simo) kuwa ni neno au maneno yanayozuka na kutumiwa na watu kwa muda fulani na baadaye kupotea. Aidha, misimu inaweza kufasiliwa kama maneno yasiyo sanifu ambayo huzushwa na kikundi cha watu wenye utamaduni mmoja ili kuelezea uhusiano wao. Hata hivyo, kuna baadhi ya misimu ambayo huweza kudumu na hata kusanifishwa kuwa msamiati sanifu kama vile kasheshe, vuvuzela, na chakachua.
Aina za misimu
Kwa kuzingatia muktadha wa utumiaji wa misimu, tunaweza kupanga misimu katika makundi makuu matatu kama ifuatavyo:
1. Misimu ya pekee
Hii ni misimu ambayo hueleza uhusiano wa jamii yenye utamaduni mmoja, yaani kundi dogo la watu. Eneo la matumizi ya misimu hii ni dogo ukilinganisha na makundi mengine na huwa haijulikani kwa watu wengi. Makundi hayo huweza kuwa ya wanafunzi, wafanyabiashara au wafanyakazi wa ofisi moja na kadhalika. Kwa mfano, msimu bumu (pesa za kujikimu) hutumika katika vyuo vikuu nchini Tanzania na haujulikani katika jamii nyingine.
2. Misimu ya kieneo
Hii ni misimu ambayo inatumika katika eneo kubwa au pana kidogo kimatumizi. Misimu ya aina hii inaweza kupatikana kwenye kata, tarafa, au wilaya. Mifano ya misimu hii ni pamoja na sekido (pikipiki ya abiria - Bukoba), toyo (pikipiki ya abiria - Kanda ya Kaskazini mwa Tanzania).
3. Misimu zagao
Hii ni misimu ambayo inatumika katika eneo kubwa kimatumizi. Ni misimu ambayo inafahamika kwa watu wengi katika nchi na huweza kuvuka hata mipaka ya nchi. Misimu ya aina hii hutumika katika magazeti, vitabu, na vipindi vya redio. Aghalabu, misimu hii huweza kuota mizizi na kusanifiwa kisha kutumika kama msamiati sanifu. Mifano ya misimu hii ni kama vile bodaboda (pikipiki inayosafirisha abiria), chakachua (kuharibu ubora au uhalisi wa kitu) daladala (mabasi madogo yanayosafirisha abiria mijini) na kadhalika. Misimu hii imezagaa na inaeleweka katika nchi nzima ya Tanzania. Aidha, imedumu katika matumizi kiasi kwamba imefikia hatua ya kusanifishwa na kuingizwa katika kamusi.
Sifa za misimu
Misimu ina sifa mbalimbali. Baadhi ya sifa hizo ni kama zifuatazo:
Umuhimu wa misimu
Changamoto za kutumia misimu katika lugha
Misimu ina changamoto mbalimbali katika matumizi ya lugha endapo haitatumika vizuri. Zifuatazo ni changamoto zinazoweza kujitokeza katika kutumia misimu:
Zoezi la 1.2
|
Umahiri wa lugha
Umahiri wa lugha ni uwezo wa mtu kumudu stadi nne za lugha, ambazo ni: kusikiliza, kuzungumza, kuandika, na kusoma, katika mawasiliano yake ya kila siku pamoja na kuuelewa utamaduni wa lugha inayohusika. Umahiri katika stadi hizo unatokana na kumudu vizuri vipengele vya lugha kama vile msamiati, miundo, matamshi, maana, na mbinu za utumiaji wa lugha katika miktadha mbalimbali. Watumiaji wa lugha ambao bado hawajamudu stadi hizo za lugha huwa si mahiri wa lugha. Mambo yanayomwezesha mtu kuwa mahiri wa lugha Yafuatayo ni mambo ya msingi yanayoweza kumsaidia mtumiaji wa lugha kupata umahiri wa lugha:
1 . Matumizi ya lugha katika shughuli mbalimbali
Shughuli mbalimbali anazofanya mzungumzaji wa lugha humwezesha kumudu stadi za lugha hiyo. Kwa mfano, shughuli zinazohusiana na elimu, kusoma vitabu na magazeti, kusikiliza redio na televisheni, kuhudhuria mikutano mbalimbali, kuhudhuria na kushiriki katika shughuli mbalimbali katika maeneo kama vile mahakamani, kanisani, misikitini, na kadhalika. Kadiri mtu anavyozidi kushiriki katika shughuli kama hizi ndivyo anavyozidi kukuza umahiri wake wa lugha.
2 . Kusomea lugha kwa kiwango cha juu
Umahiri pia hupatikana kwa kujifunza lugha inayohusika kwa kiwango cha juu. Jambo hili humpa mtu uwezo wa kubainisha na kutumia mitindo mbalimbali ya lugha katika mazingira mbalimbali. Kwa mfano, kuna wataalamu mbalimbali wa lugha ya Kiswahili ambao wamesomea lugha
3 . Kuwa karibu na watumiaji mahiri wa lugha
Kuwa karibu na wazungumzaji wa lugha inayohusika husaidia kuongeza kiwango cha umahiri. Kwa mfano, mtu akikaa karibu na wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili humwezesha kumudu zaidi lugha hiyo kwa kusikiliza na kujirekebisha, au kurekebishwa na watumiaji hao mahiri. hiyo katika ngazi mbalimbali za elimu kama vile, stashahada, shahada ya kwanza, shahada ya umahiri, na shahada ya uzamivu. Umahiri wa lugha kwa watu hawa ni mkubwa. Wengine wamekuwa mahiri kwa kuwa wamekuwa wakiitumia lugha hiyo katika miktadha na taaluma mbalimbali.
Athari za utovu wa umahiri wa lugha zaidi ya moja
Utovu wa umahiri wa lugha zaidi ya moja unaweza kusababisha athari mbalimbali zifuatazo:
1. Athari katika matamshi
Mtumiaji wa lugha zaidi ya moja asipokuwa makini anaweza kuathiri utamkaji wa maneno katika lugha ya pili. Kwa mfano, Mkurya hutamka neno chakura badala ya kusema chakula. Hii inatokana na athari ya lugha yake ya kwanza ambayo ni Kikurya.
2. Athari katika msamiati
Utovu wa umahiri wa lugha zaidi ya moja husababisha mzungumzaji kuchanganya maneno ya lugha mbili wakati wa mazungumzo. Kwa mfano, mzungumzaji anaweza kuchanganya lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa kusema nitakuinform badala ya kusema nitakujulisha.
3. Athari za kimuundo
Muundo wa tungo huweza kutofautiana kati ya lugha moja na nyingine. Tofauti hizo huweza kujitokeza katika mpangilio wa maneno au upatanisho wa kisarufi katika tungo. Mathalani, mzungumzaji wa kabila la Kihehe hutumia wingi anapozungumza na mtu ambaye anamheshimu. Kwa mfano, anapozungumza Kiswahili kama lugha ya pili anaweza kuuliza Baba mmekuja? Akimaanisha Baba umekuja? Hii hutokana na athari ya lugha ya Kihehe katika kipengele cha upatanisho wa kisarufi.
4. Athari katika maana
Hii hujitokeza wakati kunapokuwa na maneno ya lugha mbili yanayoeleza dhana moja. Neno la lugha moja linaweza kuwa na maana pana zaidi kuliko lugha nyingine. Kwa mfano, maneno katika tungo, Wash your hand yanaweza kufasiliwa kama Osha mikono yako wakati kiuhalisia katika Kiswahili tunasema Nawa mikono yako.
Mambo yanayopoteza umahiri wa lugha
Kuendelea kuwa na umahiri wa lugha hutegemea ni kwa kiasi gani mtu anaendelea
kutumia lugha hiyo. Umahiri wa lugha unaweza kuathiriwa na mambo yafuatayo:
1. Matumizi madogo ya lugha inayohusika
Umahiri wa lugha kwa mzungumzaji hudumaa ikiwa mzungumzaji haitumii lugha hiyo mara kwa mara. Kwa hiyo, kadiri mtumiaji anavyoendelea kuitumia lugha, ndivyo anavyokuza umahiri wake katika lugha hiyo lakini asipoitumia, hudumaza umahiri wake.
2. Kupungu za kusoma machapisho na kusikiliza vyom bo vya habari Mtumiaji wa lugha anapopunguza kusoma machapisho kama vile vitabu, majarida, magazeti, vipeperushi, na kusikiliza vipindi mbalimbali vya redio na televisheni huweza kufifisha umahiri wake katika lugha inayohusika. Kufanya hivyo kunasaidia kuongeza msamiati na kuzidi kujua miundo na mitindo mbalimbali ya lugha na matumizi yake katika miktadha sahihi.
3. Kuishi katika jamii isiyotumia lugha inayohusika
Umahiri wa lugha hukuzwa iwapo mtumiaji wa lugha ataishi katika jamii inayotumia lugha hiyo. Iwapo ataishi katika jamii ambayo haitumii kabisa lugha hiyo, basi umahiri wake unaweza kupungua.
4. Kuchanganya lugha katika matumizi
Kuchanganya lugha mbili au zaidi katika matumizi hufifisha umahiri wa lugha. Kila lugha ina muundo na mtindo wake kimatumizi. Kuchanganya lugha mbili au zaidi katika matumizi kunaharibu sarufi na utaratibu wote wa matumizi ya lugha inayohusika. Kwa mfano, baadhi ya watu waliosoma, hasa nchini Tanzania, huchanganya lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Tabia hii hupoteza umahiri katika lugha zote mbili.
5. Kukosa ari na umuhimu wa kutumia lugha inayohusika
Baadhi ya watu hukosa ari ya kutumia lugha yao kwa sababu mbalimbali kama vile kuinasibisha na jamii fulani, uduni, kundi fulani la kisiasa, au kundi la dini fulani. Hali hii hupunguza umahiri wao katika lugha hiyo.
6. Kubadili mfumo wa maisha
Wakati mwingine mtumiaji wa lugha anapobadili mfumo wa maisha hupunguza au hupoteza umahiri wa lugha. Kwa mfano, mtu anapoingia na kuishi katika jamii ambamo kiwango na ujuzi wa lugha alionao hauhitajiki sana hujikuta akitumia kiwango cha chini cha lugha; jambo ambalo hupunguza umahiri wake katika lugha.
Zoezi 1.3
|
Utata katika matumizi ya lugha
Utata ni hali ya tungo kuwa na maana zaidi ya moja. Kiswahili, kama zilivyo lugha nyingine, kina sentensi na maneno yenye maana zaidi ya moja. Chunguza mifano ifuatayo:
Tungo hii inaweza kutoa maana hizi: Kombo anaruka juu (anaelekea angani) au Kombo anatoa magamba ya samaki.
Tungo hii inaweza kuwa na maana zifuatazo: Kimindi amenunua mnyama anayefugwa au Kimindi amenunua kifaa cha kukunia nazi.
Tungo hii itakuwa na maana zifuatazo: Baba amemshauri mtu fulani au baba na mtu mwingine wameshauriwa.
Neno kata katika muktadha wa sentesi hii, linaweza kuibua maana hizi: Ana amenunua chombo kinachotengenezwa kwa kutumia kibuyu, au kifuu cha nazi kwa ajili ya kutekea maji, au kunywea mvinyo au Ana amenunua kitambaa, au pamba inayofunika jeraha linalotoa damu.
Neno ua linaweza kuwa na maana ya uzio uliojengwa kwa mabua, tofali, au matete kuzunguka nyumba au sehemu ya mmea inayochanua.
Chanzo cha utata katika lugha
Utata katika lugha husababishwa na mambo anuwai yafuatayo:
(a) Neno kuwa na maana zaidi ya moja. Kwa kawaida, katika kila lugha kuna maneno yenye maana zaidi ya moja. Kwa mfano, neno paa lina maana zifuatazo:
Kuondoa utata katika matumizi ya lugha
Mawasiliano ni muhimu sana katika jamii. Ili mawasiliano yaweze kufanikiwa ni lazima lugha iwe fasaha bila ya kuwa na utata wowote. Kuna njia mbalimbali za kuondoa utata katika matumizi ya lugha. Njia hizo ni pamoja na:
Zoezi la 1.4
|
Tamrini