SURA YA KWANZA : FASIHI KWA UJUMLA

Utangulizi

Katika sura hii utajifunza juu ya mitazamo ya fasihi, dhana ya sanaa, usanaa wa fasihi, aina, dhima na Chimbuko la fasihi. Vilevile, utajifunza kuhusu maendeleo ya fasihi katika mifumo ya maisha ya jamii, uhuru wa mtunzi wa kaziza kifasihi, dhana ya udhamini, aina, sababu na athari za udhamini. Aidha, utajifunzajuu ya uandishi wa kazi za kifasihi.


Mitazamo ya fasihi

Dhana ya fasihi ni pana. Dhana hii imejadiliwa na wataalamu mbalimbali kupitia mitazamo mbalimbali. Tunaweza kuigawa mijadala hiyo katika mitazamo mitano kama ifuatavyo:

Mtazamo wa kwanza unadai kuwa fasihi ni j umla ya maandishi yote katika lugha fulani. Mtazamo huu umeelezewa na Wellek na Warren (1986) wakisema kuwa njia mojawapo ya kuielezea fasihi ni kuichuku.lia kuwa ni jumla ya machapisho yote.

Changamoto ya mtazamo huu ni kuupanua mno uwanja wa fasihi na kujumuisha dhana ambazo si za kifasihi. Kwa mtazamo huu, maandishi yoyote, yakiwamo matangazo ya biashara, mafunzo ya historia, jiografia ama sayansi, yanaweza kujumuishwa humo- Aidha, mtazamo huu unabagua fasihi simulizi ambayo kimsingi haipo katika maandishi.

Mtazamo wa pili 'unadai kuwa fasihi ni hisi ambazo zinajifafanua kwa njia ya lugha. Wafuasi wa mtazamo huu ni John Ramadhani (1973), May Balisidya, (1973) Tigiti Sengo na Saifu Kiango (1973). Hawa wanadai kuwa lazima pawe na mguso ndipo mwanafasihi aweze kuandika au kueleza jambo kifasihi.

Wataalamu hao wanasema kuwa, hisi ni kama kuhisi njaa, baridi, joto, uchovu au kuumwa. Wataalamu kama vile Mugyabuso Mulokozi (2017) wanaeleza kuwas mtazamo huu unachanganya mambo matatu ambayo ni fasihi yenyewe, mambo yaelezwayo na fasihi, na mtindo wa kifasihi.

Changamoto ya mtazamo huu nikwamba, fasihi inaweza kuelezea hisi, kupitia mtindo wa fasihi, lakini fasihi yenyewe si hisi. Aidha, fasihi huweza kuelezea mgpenzi lakini fasihi yenyewe si mapenzi.

Mtazamo wa tatu 'unaitazama fasihi kama sanaa ya lugha yenye ubunifu bila ya kujali kama imeandikwa au la. Mtazamo huu unaafikiwa na Peter Kirumbi (1975), Aldin Mutembei (2006) na F.E.M.K Senkoro (2011). Kwa mujibu wa mtazamo huu, hata nyimbo na masimuli.zi ya kisanaa ni fasihi, ijapokuwa hayakuandikwa. Kwa mfano, Kirumbi anasema kuwa fasihi ni taaluma ya sanaa inayowasilishwa kwa njia ya lugha katika muundo wa maandishi au matamshi. Mtazamo huu ndio unaotawala katika taaluma ya fasihi. Inadaiwa kuwa neno fasihi limetokana na neno "fasuh" la Kiarabu lenye maana ya ufasaha au uzuri wa lugha. Hivyo, istilahi "fasihi" katika taaluma ya Kiswahili inatofautiana na istilahi ya "literature" inayotumika katika Kiingereza. Kwa sababu hii, neno fasihihalihusiani na maandishi wala vitabu, bali linahusiana na ufasaha wakauli. Hivyo, dhana hii katika Kiswahili inazingatia aina zote za fasihi, yaani fasihi simulizi na andishi. Mtazamo huu umehusisha fasihi na sanaa itumiayo lugha ya maandishi au mazungumzo. Hata hivyo, tatizo lake ni kutokuonesha uhusiano wa fasihi na jamii.

Mtazamo wa nne unadai kuwa fasihini maandiko bora ya kisanaa yenye manufaa ya kudumu. Akizungumzia mtazamo huu, Hollis Summers (1989) anasema kuwa fasihi ni sanaa inayojumuisha zaidi maneno yaliyoandikwa. Mtazamo huu unaupa uzito ufundi wa kubuni lakini unafinya mawanda ya fasihi kwa kuhusisha mawazo yaliyo bora tu.

Mtazamo wa tano unaona kuwa fasihi ni tokeo la matumizi ya lugha kwa njia isiyo ya kawaida ili kuleta athari maalumu. Kwa mujibu waMugyabuso Mulokozi (2017), waasisi wa mtazamo huu ni Roman Jakobson, Boris Tomashevsky na Viktor Shklovsky. Kwa maelezo ya wataalamu hawa, fasihi hukiuka taratibu za kawaida za matumizi ya lugha katika sarufi, maana na sauti ili kumvutia na kumuathiri msikilizaji au msomaji.

Changamoto ya mtazamo huu ni kuwa humfanya msomaji aitafakari lugha yenyewe badala ya kuutakafari ujumbe unaowasilishwa na lugha hiyo. Vilevile, fasihi inaonekana kuelemea zaidi upande wa fani na kupuuza maudhui, maana na muktadha wa kazi za fasihi.

Kwa ujumla, mijadala hii inaonesha kuwa kila mtazamo una ubora na udhaifu wake. Mitazamo hiyo inaeleza kwamba fasihi ni sanaa itumiayo lugha kufikisha ujumbe kwa jamii iliyokusudiwa. Zaidi, inaonesha kwamba kuna aina mbili za fasihi kutokana na namna ya uwasilishaji. Aina hizo ni fasihi simulizi na fasihi andishi. Kimsingi, fasili hizi zote zinahusisha fasihi, maisha na jamii. Kwa hiyo, tunaweza kusema kuwa fasihi ni sanaa inayotumia lugha kiufundi kuwasilishia masuala mbalimbali yanayomhusu mwanadamu na maisha yake. Tunaposema "lugha" hatuna maana ya usemaji wa kutumia sauti tu, bali hata mawasiliano ya kutumia ishara na vitendo. Kwa kuwa neno sanaa limejitokeza katika fasili za fasihi, ni vyema tukajua maana ya sanaa.

Dhana ya sanaa

Sanaa ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa, umbo ambalo msanii hulitumia katika kuelezea hisia zinazomgusa kwa kutoa kielelezo au vielelezo vyenye dhana maalumu. Sanaa ni matokeo ya kazi za mikono na akili ya mtu, nayo, aghalabu, huwa na umbo dhahiri lenye maana au dhana maalumu. Sanaa huweza kutokana na mwigo ambao hujengwa na kanuni au mbinu za uzuri na hata ubaya. Sanaa hujitokeza katika maumbo tofautitofauti kama inavyoonekana katika kielelezo kifuatacho:


Kielelezo Na. 1.1 Maumbo Ya Sanaa

Maumbo haya ya sanaa yanaweza kuwekwa katika makundi makuu matatu ambayo ni sanaa za uonesho, sanaa zaghibu na sanaaza vitendo (Penina Muhando na May Balisidya, 1976). Ufuatao ni ufafanuzi mfupi wa makundi hayo:

(a) Sanaa za uonesho: 

Ni sanaa ambazo uzuri wake hujitokeza katika umbo la kudumu, umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa na uzuri wake ukaoneshwa muda wowote. Sanaa hizi ni kama vile ufinyanzi, uchoraji, utarizi, ususi, uchongaji na ufumaji.

(b) Sanaa za ghibu: 

Nisanaa ambazo uzuri wake umo katika ufundi wa kutumia lugha kiasi cha kugusa hisia za mtu. Uzuri wa uimbaji au upigaji muziki na usimuliaji au usomaji wa fasihi umo katika hisia, Kwa mfano, msikilizaji anaposikia sauti tamu za wimbo, shairi au muziki, au kusoma kazi ya kisanaa hupata hisia au msisimko utakaomwezesha kupata yale yaliyokusudiwa na msanii. Aina hii ya sanaa hujumuisha kazi zote za fasihi, kama vile ngano, riwaya, ushairi na tamthiliya.

(c) Sanaa za vitendo: 

Nisanaa ambazo uzuri wake umo katika matendo. Msanii hana budi kuonesha matendo ya jambo alilokusudia au analokusudia mbele ya hadhira yake. Pia, hadhira sharti iwepo ili kushuhudia uzuri wa sanaa husika. Ili sanaa nyingi za aina hii zikamilike, huhitaji dhana inayotendeka, jukwaa, hadhira na wahusika.

Kwa mantiki hiyo, kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya sanaa za uonesho, za ghibu na za vitendo. Sanaa zote zina dhima mbalimbali katika maisha ya mwanadamu. Mifano ya dhima hizo ni kuburudisha, kuelimisha, kukosoa na kuadibu.ViIevile, kumsaidia mwanadamu huyo kupambana na mazingira yake kwa njia ya ubunifu.

Usanaa wa fasihi

Usanaa wa fasihi hujitokeza katika vipengele vifuatavyo:

(a) Mtindo

Katika fasihi, sanaa hujionesha katika namna ya kueleza jambo. Jambo linaweza kuelezwa kwa mkato. Aghalabu, methali nyingi hutolewa kwa lugha ya mkato, Kwa mfano, "MIa ni mlaleo, mla jana kala nini? /alileni?" Ali/eni ni alikula nini? Methali hii imefupisha taarifa ambayo ingeweza kutolewa hivi, mtu anayekula leo ndiye mlaji wa kweli, aliyekula jana hajulikani. Methali .hii hutumiwa kutukumbusha kwamba mtu mwenye uwezo au mali leo ndiye atakayeheshimiwa wala si yule aliyekuwa na uwezo au mali jana.

(b) Muundo

Kazi ya fasihi hupangiliwa katika muundo maalumu ili iweze kuwasilishwa vyema kwa jamii husika. Kila utanzu wa fasihi una muundo wake. Kwa mfano, shairi la kimapokeo huundwa na vipande, mishororo, beti, urari wa Vina na mizani. Aidha, utanzu kama Vile methali huundwa na pande mbili; upande wa kwanza huanzisha kauli na upande wa pili hukamilisha kauli hiyo. Pande hizi hutegemeana na kukamilishana. Muundo ndio unaotoa umbo au sura ya kazi husika.

(c) Matumizi ya lugha

Kazi za fasihi huwasilishwa kwa lugha ya kisanaa. Lugha ya kisanaa ni ile ambayo husheheni vipengele kama Vile nahau, misemo, methali, tamathali za semi, taswira na picha mbalimbali. Lugha ndio msingi wa fasihi; bila lugha hakuna fasihi. Hii yatokana na ukweli kuwa lugha hutumika kiufundi kuunda vipengele vingine vya kazi ya fasihi kama Vile wahusika, _mandhari, dhamira na matukio. Matumizi ya lugha ya kisanaa huibua hisia za hadhira. Hivyo, lugha inatakiwakutumika ipasa vyo katikakaziza fasihi ili kufanikisha dhima hii ya kuwa kiungo muhimu.

(d) Wahusika

Katika fasihi, wahusika ni Vitus watu au viumbe wengine waliokusudiwa kuwasilisha dhana, mawazo au tabia za watu. Usawiri wa wahusika na majukumu ya uhusika wao hufanywa katika namna inayoleta mvuto wa kisanaa. Kwa mfano, wahusika wasio binadamu kama Vile mti au sungura wanapopewa uwezo wa kuongea huleta mvuto wa namna fulani.

(e) Mandhari

Mandhari ni dhana inayorej elea mahali na wakati kazi ya fasihi inapotendeka. Hiki ni kipengele cha kisanaa kwa sababu kinadokeza muktadha wa utokeaji au ufendekaji wa tukio la kifasihi. Uteuzi na uumbaji wa mandhari hufanywa kwa ufundi; hivyos, kutoa mchango mkubwa katika kujenga mvuto wa kazi. Kazi za fasihi huweza kutumia mandhari halisi au za kubuni. Kwa mfano, riwaya za Rosa Mistika (Euphrase Kezilahabi, 1971), Utubora Mkulima (Shaaban Robert, 1968) zimetumia mandhari halisi; ilhali riwaya za Kufikirika (Shaaban Robert, 1967) na Ziraili na Zirani (William Mkufya, 1999) zimetumia mandhari ya kubuni.

(f) Uwasilishaji

Uwasilishaji wa kazi za fasihi hufanywa kwa njia ya mdomo, vitendo au maandishi. Uwasilishaji huo hufanywa kwa kutumia mbinu mbalimbali kama vile mpangilio wa matukio, ucheshi, na taharuki ili kuleta mvuto katika kazi husika. Mbinu nyingine katika fasihi simulizi huhusisha namna ya u tamkaj i wamaneno na sentensi, uchezaji, matumizi ya viungo vya mwili, matumizi ya ala mbalimbali, matumizi ya maleba, uigizaji, kubadili muundo wa simulizi, pamoja na uhusishaji wa kazi husika na miktadha iliyo karibu na ufahamu wa hadhira. Katika kazi za fasihi andishi, ufundi wa uwasilishaji hufanywa kwa kutumia mbinu kama vile uumbaji wa wahusika, matumizi ya lugha na uumbaji wa mandhari.

Aina za fasihi

Fasihi simulizi

Hii ni aina ya fasihi ambayo huwasilishwa kwa njia ya mdomo. Fasihi simulizi ma umbo maalumu, kwa wakati maalumu, kwa kuzingatia misingi mbalimbali ya tanzu .ziundazo aina hii ya fasihi. Aidha, ni tukio ambalo huambatana na mwingiliano wa mambo manne ambayo ni dhana, muktadha, watu na mahali. Mambo haya ndiyo yanayoamua fani ya fasihi simulizi ichukue umbo lipiiwasilishwe vipi, kwa hadhira gani, kwa wakati na mahali gani. Kwa mfano, hadithi inaweza kugeuzwa wimbo na utendi unaweza kuwa hadithi, kutegemea dhana inayowasilishwa katika muktadha, watu na mahali. Maelezo zaidi kuhusu fasihi simulizi yatatolewa katika sura ya pili katika mada ya maendeleo ya fasihi simulizi.

Fasihi andishi

Fasihi andishi ni aina ya fasihi inayowasilishwa kwa njia ya maandishi. Msingi mkuu wa fasihi andishi ni mwandishi kwani ndiye anayetunga na kuandika kiubunifu kazi ya fasihi. Maelezo zaidi kuhusu fasihi andishi yatatolewa Sura ya Tatu katika mada ya maendeleo ya fasihi andishi.

Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi

Fasihi simulizi na fasihi andishi huingiliana na kutofautiana katika vipengele mbalimbali. Wakati mwingine fasihi andishi huweza kutendwa kama fasihi simulizi, kwa mfano tamthiliya na mashairi. Tofauti ya fasihi simulizi na fasihi andishi huweza kuoneshwa kwa kutumia vigezo vifuatavyo kama vinavyooneshwa katikajedwali lifuatalo:

Jedwali Tofauti kati va fasihi simulizi na fasihi andishi

Na. Kigezo Fasihi Simulizi Fasihi Andishi

1.

Utunzi

Huweza kutungwa mapema na kukaririwa kabla ya uwasilishaji. Huweza pia kutungwa papo kwa papo wakati wa utendaji.

Hutungwa kwa kipindi kirefu kabla ya kuwasilishwa kwa hadhira.

2.

Uwasilishaji

Huwasilishwa kwa njia ya mdomo, ishara na vitendo. Uwasilishaji huo hutumia viambato kama vile maleba, miondoko na sauti.

Huwasilishwa kwa njia ya maandishi.


3.

Umri

Ni kongwe kwa sababu ilianza kabla ya ugunduzi wa maandishi.

Ilianza baada ya mwanadamu kugundua maandishi.

4.

Umiliki

Tanzu nyingi za fasihi simulizi ni mali ya jamii nzima.

Ni mali ya mtunzi na mdhamini wake.

5.

Uhifadhi

Huhifadhiwa kiehwani na kuendelezwa kwa njia ya kupokezana, ijapokuwa kutokana na maendeleo ya teknolojia, huweza kuhifadhiwa katika vinasa sauti, kompyuta na hata maandishi

Huhifadhiwa katika nyaraka au kwa njia za kidijiti.

6.

Tanzu na vipera

Idadi ya tanzu na vipera vya fasihi simulizi ni kubwa kuliko ilivyo katika fasihi andishi. Aidha, huwa na mwingiliano mkubwa wa vipera.

Idadi ya tanzu na vipera vya fasihi andishi ni ndogo. Aidha, vipera vyake havina mwingiliano mkubwa.

7.

Mabadiliko

Hubadilika kwa haraka kutegemeana na mahitaji ya hadhira, tukio la kijamii na wakati.

Haibadiliki kwa haraka kwa sababu ipo katika hali ya kudumu.

8.

Hadhira

Hadhira hai ambayo hushiriki katika utendaji kama kuitikia, kupiga vigelegele na makofi).

Ni wasomaji; hivyo hawashiriki katika utendaji, isipokuwa katika tanzu chache zinazowasilishwa kiutendaji kama vile


mashairi na tamthiliya.

9.

Wahusika

Hutumia wahusika mchanganyiko (kwa mfano binadamu, wanyama, mimea na vitu visivyo na uhai).

Hutumia zaidi wahusika binadamu. Wahusika wasio binadamu hutumika mara chache.

10.

Muundo

Huwa na muundo wa moja kwa moja aghalabu bila utata.

Huweza kuwa na muundo wa moja kwa moja au changamani kutegemeana na utanzu.

Dhima za fasihi

Fasihi ina dhima mbalimbali kama ifuatavyo:

(a) Kuelimisha jamii

Kazi kubwa ya fasihi ni kuelimisha jamii. Fasihi huufumbua macho umma na kupiga vita mazingira ya njaa, maradhi, umaskini na matatizo mengine. Aidha, fasihi huipa jamii maarifa na stadi za kukabiliana na mazingira ambamo j amii inaishi. Kwa mfano, wimbo wa "Kachiri" humfundisha mtoto wakike kustahimili shida wakati mumewe anaposafiri:

Kachiri

Kachiri kachiri - saga

Mume wangu kasafiri - saga

Kaniaehia ukili - saga

Upatao pima mbili - saga

Na kipande cha hariri - saga

Kachiri - saga

kachiri - saga

(b) Kuburudisha jamii

Dhima nyingine ya fasihi ni kuburudisha jamii. Katika kutimiza jukumu hili, fasihi hustarehesha, huliwaza na kutuliza mwili na akili ya hadhira. Kwa mfano, watu wanapotazama vichekesho na maigizo ya "Mizengwe" (katika ITV Tanzania) hufurahia vituko, kejeli na mizaha inayoigizwa.

(c) Kuadibu na kunasihi jamii

Mara nyingi, kazi za fasihi hutumika katika kuasa na kuadibu kuhusu mambo mbalimbali yanayojitokeza katikajamii. Kwa mfano, tamthiliya yaNgoswe Penzi Kitovu cha Uzembe (Edwin Semzaba, 1988) inawaadibu na kuwaasa watu kufanya kazi kwa nidhamu. Kwa ufupi, tamthiliya hiyo inatoa funzo kwamba mtaka yote kwa pupa, hukosa yote. Katika fasihi simulizi, nyimbo hutumika kukamilisha jukumu hili. Kwa mfano, wimbo wa bongo fleva wa Naseeb Abdul (maarufu kama Diamond) uitwao ''Nitarejea." Ifuatayo ni sehemu ya wimbo huo:

Aah vipi mizigo umeweka tayari? ii ihii,

Nisije chelewa nikaachwa na gari, aa ahaa,

Basijikaze usil_ie mpenzi, aahaaa,

Mimi nitarudi niombee kwa Mwenyezi, aahaa,

Zile taabu na njaa msimu mzima mavuno hakuna,

Huwa nakosa raha mkikosa cha kutafuna,

Roho yangu inauma sana, sema nitafanya nini fedha Sina aaahaa, 

Nakuonea huruma, bora niende mjini kusaka chuma aaahaa.

Kiitikio:

Kama mtoto akinililia, mwambie kesho nitarejea x2 

Wadanganye na vibagia, waambie pipi nitawaletea, 

Na usichoke kuvumilia, na kila siku kuniombea.

Katika wimbo huu, mume anamnasihi mkewe avumilie na awalee watoto vizuri wakati yeye (mume) akiwa katika pilikapilika za kusaka maisha.

(d) Kutia hamasa jamii

Fasihi hutia hamasa kuhusiana na mambo mbalimbali yanayotendeka katika jamii. Mathalani, riwaya ya Pepo ya Mahwege (Harrison Mwakyembe, 1980) inatia hamasa kwa vijana, kusimamia kile wanachokiamini. Mhusika Kalenga alisimama kidete kufichua uozo uliomo kwenyejamiina, hatimaye, alipandishwa cheo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya. Vilevile, kazi nyingine za fasihi kama nyimbo zimekuwazikitumika kutia hamasa. Wimbo wa "Gezaulole" ulioimbwa na bendi ya Urafiki Jazz ulikuwa unahamasisha wanajamii waishio mijini bila kazi kuhamia vijijini ili kujishughulisha na kilimo. Katika kipindi cha miaka ya 1970 kilimo kilionekana kuwa ndio uti wa mgongo wa maisha na kwamba kila mtu anaweza kulima.

(e) Kukomboa jamii

Dhima nyingine ya fasihi ni kupiga vita mambo mbalimbali yanayokwamisha maendeleo ya jamii kama vile ujinga, maradhi na umaskini. Tamthiliya ya Hawalaya Fedha (Amandina Lihamba, 1985), kwa mfano, inaeleza mambo yanayosababisha umasikini ambayo ni ujinga na uvivu. Aidha, wakati wa harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika, bendi za muziki zilipiga nyimbo za kuwaunganisha watu kwa ajili ya ukombozi. Wimbo mmojawapo ni "Mwenyekiti Mwalimu Nyerere" ulioimbwa na bendi ya Urafiki Jazz miaka ya 1970. Ufuatao ni wimbo huo:

Mwenyekiti wa nchi tano zilizo mstari wa mbele,

Tunakuomba uzidishe mapambano ya Kusini mwa Afrika,

Kwani, maadui wa Afrikaaa wanalisumbua sana bara Ietu hili Ia Afrika, 

Rais Kaunda na Samora wa Msumbiji, Seretse Khama, na Neto wa Angola, tunawaambia aluta continua.

Kiitikio:

Mwenyekiti, Mwalimu Nyerere Baba, imarisha ukombozi wa .4frika x2

Uhuru wetu hauwezi kuwa safi mpaka Afrika yote imekuwa huru, Mwalimu eeh!

Kiitikio:

Mwenyekiti, Mwalimu Nyerere Baba, imarisha ukombozi wa Orika x2

Maadui wa bara Ia Afrika wameanza kuwahujumu viongozi, Mwal imu eeh!

Kiitikio:

Mwenyekiti, Mwalimu Nyerere Baba, imarisha ukombozi wa Afrika x2


Murtala Mohammed wa Nigeria na Marien Nguabi wa Kongo wamepotea, Mwalimu eeh!

Kiitikio:

Mwenyekiti, Mwalimu Nyerere Baba, imarisha ukombo:i wa 4/i•ika x2.

Uhuru wetu hauwezi kuwa safi nypaka Afrika yote imekuwa hurus

Mwalimu eeh!

(f) Kuhilhdhi na kurithisha amali za jamii

Fasihi husaidia kutunza amali na kumbukumbu nyingine za jamii. Mifano ya amali hizo za kijamii ni mila, desturi, historia na sanaa. Tamthiliya za Kiswahili kama Vile Kinjekitile (Ebrahim Hussein, 1969) na Ngoma ya Ng'wanamalundi (Emmanuel Mbogo, 1988) zimebeba vyema jukumu hili la kuhifadhi na kurithisha amali za jamii. Pia, zinafafanua masuala ya kijadi kama Vile imani, uganga na uchawi.

(g) Kukosoa jamii

Fasihi ina dhima ya kukosoa jamii katika mambo mbalimbali ya maisha, Kwa mfano, katika riwaya ya Kg/ikirika (Shaaban Robert, 1967) mwandishi anakosoa tabaka tawala linalotumia rasilimali nyingi kwa manufaa ya watu wachache ilihali wanajamii wengine wanateseka. Hali kadhalika, methali katika fasihi hutumika kukosoa au kuonya jamii. Methali kama Vile "Mkataa pema, pabaya panamwita" inakosoa mtu anayekataa wosia mzuri kwani kuna madhara yanaweza kumpata. Aidha, methali kama "Tamaa mbele, mauti nyuma" imekusudiwa kuwaonya wanajamii kuwa mtu mwenye tamaa anaweza kukabiliwa na madhara.(h) Dhima ya kifalsafa

Falsafa ni mwelekeo wa kimawazo ambao unadhihirika katika kazi ya kifasihi. Kwa hiyo, falsafa ni busara ya kimawazo iliyofikiwa baada ya mtu au watu kutafakari kwa kina kuhusu maisha na masuala ya kiulimwengu. Mathalani, falsafa huuliza maswali kama ifuatavyo: Kwa nini tupo duniani? Kwa nini tunakufa? Hatima ya maisha ni nini? Ulimwengu ulitoka wapi na hatima yake ni nini? Je, kuna Mungu? Kwa jicho la kifalsafa, fasihi huwachochea wasomaji au wasikilizaji kuyatafakari masuala hayo kwa umakini zaidi. Katika fasihi ya Kiswahili, baadhi ya kazi za kifalsafa ni Nagona (1990) na Mzingile (1991) zote za Euphrase Kezilahabi na BinAdamu (Kyallo Wamitila, 2002).

(i) Kukuza na kuhifadhi lugha

Kutokana na ukweli kwamba fasihi hutumia lugha, lugha haiwezi kudumaa kwa sababu inakuwa kwenye matumizi. Mwanafasihi hutumia maneno kuibua na kueleza dhana mbalimbali katika utunzi wa kazi zake. Uandishi wa kazi za fasihi huibua misemo mipya mara kwa mara; kwa njia hii lugha huweza kukua. Kwa mfano, katika riwaya ya Kusadikika (Shaaban Robert, 195 1) kuna uibuaji wa msamiati kama vile 'ali ali' (tukufu) 'azali' (asili au kiini) 'kitali' (mapigano) na 'mlizamu' (chemchem).

Ingawa fasihi ina dhima hizi chanya tulizozieleza, huweza kuwa na dhima hasi kwa baadhi ya watu na nyakati. Hii ni kwa kuwa fasihi ni zao la harakati na mivutano ya kijamii. Aidha, huweza kutumiwa na dola au kundi moja kukandamiza au kudhalilisha kundijingine. Kwa mfano, fasihi ya wakoloni iliyofasiriwa kwa Kiswahili ilikuwa inahalalisha ukoloni kwa kumkweza Mzungu na kumtweza Mwafrika. .Mifano ya kazi hizo ni Mashimo ya Mfalme Sulemani (Ridder Haggard, 1929) na Allan Quartermain (Ridder Haggard, 1934). Zipo pia kazi za fasihi zinazosifia na kutukuza wauaji na madikteta badala ya kuwakemea.

Chimbuko la fasihi

Kuna mitazamo miwili inayohusu chimbuko [a fasihi: mtazamo wa kidhanifu na mtazamo wa kiyakinifu.

(a) Mtazamo wa kidhanifu

Msingi wa mtazamo huu ni mawazo ya kudhani yasiyotokana na uhalisi. Waasisi wa mtazamo huu ni wanafalsafa wa Kiyunani wakiwamo Plato na Sokrate. Waasisi wa mtazamo huu wanaamini kuwa fasihi na sanaa vimetoka kwa Mungu. Hivyo, mwanafasihi huipokea sanaa ikiwa tayari imeivishwa na Mungu. Wachambuzi wengine wenye mtazamo wa kidhanifu ni Felician Nkwera na John Ramadhani.

Katika insha yake kuhusu fasihi, Felician Nkwera (1976) anasema "Fasihi ni sanaa ambayo huanzia kwa Muumba, humfikia mtu katika vipengele mbalimbali... (ni) hekima ambayo mtu ameshirikishwa apate kumtambua

Muumba wake". Akiunga mkono mtazamo huu, Ramadhani (1975) anadai kwamba, ingawa fasihi ni hisi, kitendo chamtu kuibuni kazi ya sanaa ni uigaji wa Mungu ambaye ndiye mfalme wa sanaa zote. Mawazo ya wanafalsafa wa mtazamo huu hayana uthibitisho wowote zaidi ya kumtenga msanii na jamii yake kwa kumkweza na kuonekana yuko karibu na Mungu kuliko wanajarmi wengine. Aidha, waumini wa mtazamo huu wanaamini kuwa mwanafasihi hawezi kubuni kitu chochote zaidi ya kuiga sanaa ambayo tayari Mungu ameitengeneza.

(b) Mtazamo wa kiyakinifu

Wafuasi wa mtazamo huu wanadai kuwa chimbuko la sanaa na fasihi ni mazingira halisi ya jamii, hususani sanaa ya mwanzo iliyofungamana na kazi za uzalishaji mali. Hii inamaanisha kwamba binadamu (jamii) na mazingira yake ndio chanzo cha fasihi na sanaa. Katika harakati za kukabili mazingira yake, ilimlazimu binadamu kufanya kazi. Binadamu wa mwanzo waliishi katika mazingira yasiyo rafiki. Hivyo, iliwalazimu kutumia silaha ili wapambane na mazingira hayo. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kutafuta njia za kurekebisha silahazao (mawebutu) kwa kuyaehonga ili yawe na ncha kali.Uchongaji huo ndio ulikuwa sanaa yenyewe. Kwa hiyo, hisia za kisanaa zimefungamana na maendeleo ya mtu katika kupambana na mazingira yake na katika kufanya kazi. Mtazamo huu una mwelekeo zaidi kwani unakubaliana na fikra kuwa, wanadamu walianza mawasiliano kupitia kazi zao. Kwa mantiki hiyo, chimbuko la sanaa ni kazi.

Kadiri binadamu alivyozidi kuendelea, alikuwa na mahitaji mengme zaidi ya mahitaji ya msingi. Mahitaji hayo yaliamsha hisia za kuchora vielelezo vya shughuli zake za kujikimu. Michoro ya mapangoni iliyopo Kondoa (Tanzania) ni mifano mizuri ya vielelezo hivyo. Kuzuka kwa lugha kuliongeza aina nyingine ya sanaa ambayo ni fasihi. Fasihi hii haikutoka kwa Mungu wala haikutokana na hisi tu.

Fasihi, kama zilivyo sanaa nyingine, ilitokana na kazi alizofanya binadamu katika kupambana na mazingira yake. Fasihi ilianzia katika wimbo wa kazi. Baadaye, tanzu nyingine za fasihi zilitungwa na kusimuliwa kwa madhumuni ya kufunza, kukosoa, kuadibu, kuchokoza fikra na kuliwaza jamii baada ya kazi. Kadiri maendeleo ya uzalishaji mali yalivyoongezeka, binadamu akapata muda wa kupumzika na kustarehe kwa njia ya sanaa, fasihi ilianza kutengana na kazi za uzalishaji. Fasihi ikawa shughuli maalumu ya jamii katika matukio mbalimbali, kama vile sherehe na ibada. Fasihi na sanaa nyingine zilirithishwa kizazi hadi kizazi kwa njia ya masimulizi mpaka maandishi yalipogundulika.

Maendeleo ya fasihi katika mifumo ya maisha ya jamii

Fasihi hubadilika kulingana na mabadiliko ya mwanadamu. Kadiri binadamu anavyobadili mifumo yake ya maisha ndivyo fasihi inavyobadilika. Hii inajidhihirisha kupitia rmfumo mbalimbali ya uzalishaji mali aliyoipiti a binadamu ambayo ni ujima, utumwa, ukabaila, ubepari na ujamaa kama ifuatavyo:

(a) Mfumo wa ujima

Mfumo wa awali kabisa wa jamii ya binadamu baada ya kutoka katika usokwe ulikuwa ni ujima. Katika mfumo huo watu waliishi katika makundi kwa usawa, wakimiliki kila kitu kwa pamoja, na wakishirikiana kupambana na mazingira kama vile ukame na wanyama wakali. Kila walichokipata waligawana.

Fasihi ya kipindi hiki ilihusu uzalishaji mali na uwindaji. Fasihi hii ilifungamana na haja ya kukidhi mahitaji ya lazima. Ilitumika kama chombo cha kazi. Binadamu wa kipindi hicho alitumia nyimbo katika shughuli zake za kilimo kwa lengo la kufanya kazi kwa muda mrefu pasipo kuchoka. Pia, fasihi ya wakati huo ilikuwa na lengo la kuwaunganisha watu pamoja kwa lengo la kufanya kazi, hasa kilimo. Vilevile, binadamu alitumia fasihi simulizi kama chombo cha kusifu na kupongeza watemi au mashuj aa waliokuwa wanajitokeza katika jamii zao. Mashujaa hao walitungiwa nyimbo za kuwasifu au walijitungia nyimbo za kujisifu mbele yajamii zao. Kimsingi, fasihi ya kipindi hiki haikuwa ya kitabaka kwa sababu jamii ilikuwa haijagawanyika katika matabaka mbalimbali. Kwa hiyo, fasihi iliwanufaisha watu wengi katika jamii.

(b) Mfumo wa utumwa

Mfumo huu haukuenea sana hapaAfrika bali ulitamalaki zaidi huko Ulaya na Asia. Katika mfumo huu, matajiri walimiliki ardhi, migodi na watumwa, na kuwatumia watumwa hao kuzalisha mali. Kwa minajili hii, iliibuka fasihi ya tabaka tawala ya kutukuza wamiliki wa watumwa na mali zao na kuwatweza watumwa. Fasihi ya watumwa iliyopinga mfumo huo ilienezwa kwa siri; watunzi hao walipogunduliwa waliadhibiwa vikali. Pamoja na masaibu yote hayo, baadhi ya watumwa hawakuacha kutumia fasihi katika kujitetea au kuelezea ubaya wa mfumo huo kwa lengo la kujikomboa.


(c) Mfumo wa ukabaila

Katika mfumo huu, mtaji mkubwa wa uzalishaji ulikuwa ardhi. Uhusiano wa utwana na ubwana ulifikia hatua mpya ambapo tabaka tawala lilitawala njia zote za kiuchumi na kiutamaduni. Mbinu mojawapo ya kutawala uchumi ni kukodisha mashamba. Kabaila hukodisha (ma) shamba, ambapo mtwana hutoa fungu kubwa kwa mwinyi wakati wa mavuno, Fasihi ilitawaliwa na falsafa zilizohalalisha uhusiano wa mabwana (makabaila) na watwana (waishio kwa jasho Iao). Mfumo huu ulikuwa na uozo mwingi. Uozo mmojawapo uliojitokeza katika mfumo huu ni kusisitiza starehe na mapambo yasiyo na maana. Pia, kazi za fasihi ziliathiriwa na uozo huu na .zilisisitiza mapambo. Kazi za fasihi kama zile za Al-Inkishgfi (Sayyid Abdallah binAli bin Nasir, 1800) na Utenzi wa Mwanakupona (Mwanakupona bint Mshamu; 1858) ni mifano mizuri ya kazi za wakati huo.

Kazi .za fasihi katika mfumo huu ziliathiri sana nafasi ya mwanamke katika jamii. Mwanamke alisawiriwa kama pambo la mwanamume kama inavyodhihirika katika beti zifuatazo:

Nawe ipambe libasi,

Ukae kama arusi,

Maguu tia kugesi,

Na mikononi makoa.

Na kidani na kifungo,

Sitoe katika shingo, 

Muili siwate mwengo, Kwa marashi nadalia.

Nyumba yako inadhifu,

Mumeo umsharifu, Wakutanapo sufufu, Msifu na kumtaya.

Mume wako mtukuze,

Sifa zake zieneze,

Wala simsharutize,

Asichoweza kutom

Beti za hapo juu zinasisitiza umuhimu wa mapambo kwa wanawake. Mwanakupona anamuusia binti yake akubali kuwa pambo kwa mume wake. Fasihi katika mfumo huu ilitumiwa kumuasa mwanamke aelekeze akili yake katika kumsifu, kumfurahisha na kumhudumia mumewe.

(d) Mfumo wa kibepari

Baada ya mfumo wa kikabaila kuanguka, uliibuka mfumo wa kibepari. Msingi mkuu wa mfumo wa kibepari ni mtaji. Kila jambo huamuliwa kwa nguvu ya fedha. Katika mfumo huu kila kitu kinachofaa kuwa bidhaahufanywa kuwa bidhaa. Kwa hiyo, fasihi pendwa ndiyo inayouzika zaidi kuliko fasihi dhati. Fasihi katika mfumo huu huegemea zaidi katika kuburudisha kuliko kuwafanya watu wafikirie maisha halisi. Watunzi wa kazi za fasihi hutumia vipaji vyao ili kujipatia fedha. Aidha, katika mfumo wa kibepari, mara nyingi fasihi husawiri maisha ya mtu mmoja mmoja badala ya jamii nzima. Mfano mzuri wa kazi za fasihi za mfumo huu ni riwaya za Mzimu wa Watu wa Kale (Mohammed Said Abdulla, 1957) na Simu ya Kijö (Faraji Katalambula, 1965); hizi ni riwaya za kipelelezi ambazo zimejishughulisha na matatizo ya watu binafsi badala ya matatizo yanayoikumba jamii nzima.

(e) Mfumo wa kijamaa

Mfumo mwingine unaoakisi maendeleo ya fasihi ni mfumo wa kijamaa. Huu ni mfumo wenye kujali usawa na utu wa mtu. Ni mfumo ambao kila mtu anatakiwa kufanya kazi na kufaidi matunda ya j asho lake kwa kugawana kulingana na kazi aliyoifanya. Nchini Tanzania, mfumo huu ulishadidiwa na Azimio la Arusha lililoanzishwa mwaka 1967 kwa lengo la kuondoa ubepari na kujenga ujamaa. Baadhi ya kazi za fasihi zenye kuakisi mfumo huuni Ufunguo Wenye Hazina (Paul Ugula, 1969), Ngonjera za UKUTA (Mathias Mnyampala, 1970) Shida (May Balisidya, 1975) Ndotoya Ndaria

(John Ngomoi, 1976), Mtu ni Utu (George Mhina, 1977), Gamba la Nyoka (Euphrase Kezilahabi, 1978), Lina Ubani (Penina Mhando, 1984), Kaptula la Marx (Euphrase Kezilahabi, 1999), Mashairi yaAzimio la Arusha kilicho haririwa na Farouk Topan na Kamenju (Longman 1971) na kwa upande mwingine, kulikuwa na kazi nyingine za fasihi zilizokosoa ama kuhakiki mfumo huu.

Zoezi 01

(i) Elezadhana ya fasihi kama ilivyojadiliwa na wanafasihi mbalimbali.

(ii) Eleza tofauti kati ya fasihi na vipengele vingine vya sanaa.

(iii) Jådili mitazamo kuhusu chimbuko la fasihi kwa kuzingatia ubora na udhaifu wa kila mtazamo.

(iv) Fasihi ina umuhimu gani katika maisha ya mwanadamu?

(v) Kwakutumia mifano,jadilikaulikwamba"Fasihihubadilika kulingana na jamii inavyobadilika."


Shughuli ya kufanya

landaliwe ngonjera fupi kuhusu "utumwa," miongoni mwa wahusika wakuu wa ngonjera hiyo wawe "mtumwa" na "bwana". Kisha ighanwe darasani.

Uhuru wa mtunzi wa kazi za kifasihi

Mtunzi wa kazi za fasihi ni mtu anayetunga kazi kama vile nyimbo, mashairi, ngonjera, riwaya au tamthiliya. Mtunzi anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

(i) Awe mbunifu ili aweze kutoa kazi ya kifasihi yenye mvuto;

(ii) Ajue vizuri utamaduni wa jamii anayoitungia kazi ya fasihi. Pia, ajue mabadiliko yanayotokea katika mifumo mbalimba[i ikiwamo ya kisiasa na ki uchumi;

(iii) Awe na ujuzi wa lugha anayotumia kutunga kazi yake ili aweze kuteua msamiati, nahau; misemo na methali ambazo zinaendana na kile anachokitunga;

(iv) Awe na ujuzi wa utanzu husika. Mathalani, kama anatunga shairi, ni lazima ajue kanuni na mbinu za utunzi wa mashairi. Kwa hiyo, ni muhimu mtunzi asome kazi mbalimbali zinazohusu utanzu husika ili kuongeza ujuzi na kubaini mambo ambayo hayajaandikiwa. Kama ni mtunzi simulizi ajue kanum za utunzi simulizi wa fani inayohusika; na

(v) Awena uwezo wakupangamatukiokwa sababu mpangiliomzuri wa matukio hufanya kazi ya fasihi ivutie

Fasili ya uhuru wa mtunzi wa kazi za kifasihi

Ili mtunzi aweze kufanya kazi yake barabara, sharti awe na uhuru. Uhuru wa mtunzi wa kazi za kifasihi ni dhana pana sana. Inajitokeza ndani na nje ya nafsi ya mtunzi. Kwa mujibu wa Euphrase Kezilahabi (1993) uhuru wa mwandishi uko katika mambo manne yafuatayo:

(i) Utashi ambao humfanyamtunzi kufanya mambo yake bila kuyumbishwa na mtu au kikundi cha watu.

(ii) Falsafa inayoendananamaishahalisi yajamiihusika. Hatahivyo,mwandishi anaweza kuwa na falsafa yake mwenyewe inayopingana na falsafa ya watu w engine.

(iii) Kuimudu lugha anayoitumia ili aweze kujieleza vizuri kwa hadhira yake na kutoa kazi zinazokubalika katika jamii.

(iv) Kuitawala kazi anayoishughulikia; kwani mtunzi anayejua vema misingi na taratibu za sanaa anayoishughulikia, mara nyingi, hutoa kazi ambazo huvutia hadhira yake kifani na kimaudhui.

Kutokana na maelezo hayo, tunaweza kusema kuwa uhuru wa mtunzi wa kazi za kifasihi ni hali inayomfanya mtunzi kufanya kazi yake pasipo kuingiliwa na mtu, kikundi cha watu, au taasisi yenye nguvu.

Tathmini ya uhuru wa mtunzi wa kazi za kifasihi

Wataalamu wa fasihi wanasema kuwa ili mtunzi awe na uhuru katikajamii yoyote; inatakiwa iwepo demokrasia ya kweli itakayomfanya mtunzi atoe mawazo yake bila kubanwabanwa kwa njia ya sanaa. Vilevile, anatakiwa kuwa na uwezo fulani wa kiuchumi kwani kutokuwa na fedha kunamfanya mtunzi kuyumbishwa na wenye fedha kiasi cha kumfanya kikaragosi Chao. Hali kadhalikas uhuru wa mtunzi unahitaji kuwapo machapisho mbalimbali ya kusoma. Kwa hiyo, studio na maktaba vinatakiwa kuwapo ili kumwezesha mtunzi kupata maehapisho na sidii mbalimbali zenye kumjengea uwezo wa kutunga kazi "bora.

Hata hivyo, jambo la kujiuliza ni kuwa je, kuna uhuru wa mtunzi nchini Tanzania? Kimsingi, swali hili linahitaji majibu makini kutokana na ukweli kuwa mtunzi ni mwanajamii na jamii ina miiko na mipaka yake. Hivyo, mtunzi anapokiuka mipaka hiyo, anakumbana na matatizo. Hali hii inapotokea, huibua hisia za kutokuwapo kwa uhuru wa mtunzi. Mjadala wa uhuru wa mtunzi si kwa Tanzania tu bali unajitokeza hata nchi nyingine duniani. F.E.M.K Senkoro (1984:18) akimnukuu Karl Marx (1899) anasema: "Sheria inaruhusu kuandika Iakini kwa sharti moja kuwa niandike kwa mtindo usio wangu. Ninayo haki ya kuonesha undani wa mambo, Iakini nalazimishwa niuoneshe undani huo kwa kupitia katika kauli isiyo yangu. Mimi ni mcheshi, lakini sheria inaniamrisha niandike bila mzaha wowote; mimi hupenda kusema mambo bila kuficha, lakini sheria hainitaki niandike hivyo."

Kaulihii ya Marx inaonesha walakini kuhusu dhana ya uhuru wa mtunzi wa kazi za fasihi. Uhuru wa mwandishi umebanwa na sheria zilizowekwa na watu wenye mamlaka ambazo mtunzi hatakiwi kuzikiuka. Katika kipindi cha utumwa na ukabaila hali haikuwa tofauti. Tunaambiwa kuwa katika kipindi cha utumwa, baadhi ya wasanii walioonekana kuwatetea wenzao kwa kulaani mfumo huo kwa kutumia nyimbo, walitenganishwa na wenzao au walikatwa ndimm zao au kuuawa. Lengo lilikuwa ni kuwanyima wasanii uhuru wa kujieleza kuhusu dhambi za mfumo husika ili wasije wakawapa wenzao maarifa ya kuepukana na mfumo huo.

Katika kipindi cha ukoloni, vitabu vilivyotukuza uzungu kama vile Mashimo ya Mfalme Sulemani na Allan Quatermain (Richard Haggard 1948), ndivyo vilivyochaguliwa kutumika shuleni.

Waandishi wa Kiafrika waliojiiokeza kuulaani na kuupinga ukoloni, waliandika kazi zao kwa kificho sana. Mfano wa waandishi hao ni Shaaban Robert aliyeandika riwaya za Kusadikika (1951 ) na Kt!fikirika (1967).

Baada ya kupata uhuru, baadhi ya serikali za Kiafrika ziliendeleza tabia ya kuwafunga midomo watunzi, Kazi zote za kifasihi zilizoonekana kwenda kinyume na mwelekeo wa kisiasa na kijamii zilipigwa marufuku. Mfano mzuri ni riwaya yaRosa Mistika (Euphrase Kezilahabi, 1971) ambayo inasawiri maovu yaliyomo ndani ya jamii ambapo watu wazima wenye dhamana ya kuwalinda watoto wa kike wako mstari wa mbele kuwaharibu. Kazi yake ny ingine iliyowahi kufungiwa ni Kaptula la Marx ( 1999) iliyokosoa mienendo ya baadhi ya viongozi wa serikali. Kwa upande wa fasihi simulizi, mfano wa nyimbo zilizofungiwa ni "Wapo" (Elibariki maarufu kama 'Ney wa Mitego',. 2018). "Wapo" ulifunguliwa kwa idhini ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano baada ya kuona maudhui yake hayajakiuka maadili yajamii.

Mbali na serikali, pia udhibiti wa watunzi wa kazi za fasihi umekuwa ukifanywa na wafadhili, mashirika ya uchapishaji, taasisi za elimu na mashirika mbalimbali ya kidini. Wasanii wamekuwa wakidhibitiwa kwa kutumia nguvu za kimamlaka au fedha ili waandike yale yanayotakiwa na vyombo hivyo.

Hata hivyo, kazi mbalimbali za fasihi zimekuwa zikitolewa mara kwa mara. Hali hii inaweza kuwa kiashiria kwamba watunzi wa kazi za fasihi hapa nchini wana uhuru wa kutosha. Jambo muhimu la kujiuliza ni je, hizi kazi za watunzi zinazotolewa mara kwa mara zinaakisi mawazo ya watunzi pasipo kuingiliwa na watu wengine? Inawezekana, watunzi wengi wa kazi za fasihi hapa nchini wamekuwa wakitoa kazi pendwa ndio maana kazi hizo hazifungiwi.

Ikumbukwe kuwa kunapokuwa na uhuru wa mtunzi wa kazi za kifasihi, kuna ukosoaji wa jamii au tabaka Iolote lile linaloenda kinyume cha sheria na taratibu zilizopo kama vile wala rushwa, wanyonyaji, wezis wakwepa kodi na wahujumu uchumi. Hali kadhalika, uhuru wa mtunzi wa kazi za kifasihi utasaidia kuikomboa jamii kisiasa, kiudhumi na kiutamaduni kupitia fasihi. Pia, utasaidia kutokomeza mawazo ya kikasuku yaliyomo vichwani mwa baadhi ya watu. Vilevile, utasaidia kutoa elimu kama mwongozo wa maendeleo ya jamii. Msanii atakuwa huru kutoa elimu kuhusu mambo mbalimbali katika jamii yake ili iwe ya kisasa na ya kimaendeleo. Zaidi ya hayo, utasaidia kuchochea jamii iondokane na matatizo yanayoikumba, ikiwa ni pamoja na mtu kuwa na msimamo unaoeleweka katika kutetea jamii yake. Kwa hiyo, ni muhimu wasanii kuzingatia maadili na utamaduni wa jamii husika.

Zoezi 02

(i) Kwa kutumia mifano, fafanua jinsi uhuru wa mtunzi unavyoweza kuhusishwa na utamaduni wajamii.

(ii) ''Uhuru wa mwandishi ni wa kitabaka zaidi kuliko wa mtu binafsi." Jadili.

Udhamini

Udhamini ni moja ya dhana muhimu zinazoj itokeza katika kazi za fasihi. Katika fasihi, udhamini ni hali ya mtu, kundi, shirika au asasi fulani kutoa fedha, mali au huduma kwa ajili ya kugharamia kazi ya fasihi. Mdhamini hutoa mali zake kwa malengo maalumu ambayo huyapa kipaumbele. Kwa ujumla, lengo la mdhamini ni kuona udhamini huo unamsaidia kupata faida au matokeo aliyokusudia. Athari za udhamini huo huweza kuwa hasi au chanya.

Aina za udhamini

Kuna udhamini wa aina kuu nne wa kazi za fasihi. Aina hizo ni udhamini wa jamii, udhamini wa ushawishi, udhamini wa nguvu na udhamini wa mtunzi m wenyewe.

(a) Udhamini wa jamii

Udhamini mkubwa kuliko wote ni ule wajamii. Walengwa wa kazi ya sanaa, ikiwemo fasihi ni wanajamii. Wao ndio wasomaji wa mashairi, riwaya au tamthiliya na ndio wanunuzi wa kazi za sanaa. Mwandishi na msanii hujitahidi kuwaridhisha wanajamii ili waipende na kuinunua kazi yake.

(b) Udhamini wa ushawishi

Katika udhamini huu mdhamini hutumia fedha, mali na uzoefu wake katika fasihi kwa lengo la kuwavuta wasanii mbalimbali. Udhamini wa tuna hii umejikita zaidi katika fedha au mali aliyo nayo mdhamini. Mdhamini hutumia vitu vyenye kuwavuta wasanii kwa lengo la kukamilisha mahitaji yake.

Mdhamini anaweza kumshawishi msanii kwa kumpa fedha za kuzalisha na kusambaza kazi zake. Wamiliki wa vyombo vya habari kama vile runinga na redio hurusha kazi za wasanii mara kwa mara ili kuwatumia katika matamasha makubwa kwa gharama ndogo. Pia, udhamini wa aina hii hutumiwa na mashirika ya uchapishaji vitabu na baadhi ya asasi za serikali na zisizo za serikali hasa kupitia mashindano mbalimbali ya utungaji wa kazi za kifasihi.

Kupitia umaarufu wa mdhamini, msanii anaweza kulazimika kupitiakwenye mgongo wa mdhamini huyo ili aweze kufanikiwa katika kazi zake za kisanii. Hii ni kwa sababu msanii anakuwa na imani na mdhamini au anakosa uwezo wa kujidhamini yeye mwenyewe.

(c) Udhamini wa nguvu

Udhamini wa aina hii hutegemea zaidi mamlaka aliyo nayo mdhamini dhidi ya mdhaminiwa au msanii. Mara nyingi, udhamini wa aina hii hufanywa na vyombo vya tabaka tawala kama vile serikali inayomiliki vyombo vyote vya dola. Serikali, kwa mfano, inaweza kuwatumia wasanii katika shughuli za maadhimisho ya sherehe za kitaifa, Hapa, msanii hulazimika kuandika au kutunga kazi ya kisanaa kwa kufuata matakwa ya chombo chenye mamlaka. Msanii huwa kama kasuku; hana sauti katika kile anachokiandika au kukitunga.

(d) Udhamini wa mtunzi mwenyewe

Mtunzi wa kazi za kifasihi anaweza kujidhamini yeye mwenyewe wakati wa uchapishaji wa kazi zake. Wakati mwingine hutumia fedha zake katika kuhakikisha kuwa kazi yake inazalishwa kupitia usimamizi wake. Wakati mwingine, anaweza kusambaza kazi zake yeye mwenyewe au kupitia kwa wasambazaji mbalimbali ambao wanakuwa kama mawakala wake. Katika udhamini huu mtunzi huandika au kutunga kazi za fasihi zenye ujumbe anaoutaka yeye mwenyewe kwa sababu hafuati matakwa ya mtu mwingine. Msanii anayeweza kujidhamini ana uwezo wa kutetea tabaka lolote analolitaka.

Sababu za udhamini katika kazi za fasihi

Kuna sababu mbalimbali za udhamini katika kazi za fasihi. Sababu hizo ni pamoja na:

l. Kutojiamini: Baadhi ya wasanii ni waoga na hawajiamini katika kufanya kazi zao. Wanafikiri kuwa bila mtu fulani hawawezi kufanikiwa kisanaa. Kwa hiyo, huwalazimu kutafuta mdhamini ili wafanikiwe.

2. Uhaba wa fedha: Baadhi ya watunzi wa kazi za fasihi hawana fedha za kutosha kuendesha shughuli zao za sanaa. Hali hii huwafanya watafute wadhamini.

3. Tamaa ya kupata fedha za harakaharaka: Baadhi ya wasanii hudhaminiwa na wadhamini wanotaka kupata fedha za harakaharaka. Hii hutokana na umaarufu wa mdhamini katika 'uwanja wa fasihi. Wasanii wa aina hii hulazimika kutunga yale anayoyataka mdhamini hata kama hayana mchango katika maendeleo ya jamii.

4. Kujipendekeza kwa baadhi ya wasanii kwa wadhamini: Baadhi ya wasanii wana tabia ya kujipendekeza kwa wadhamini ili kulinda na kutetea maslahi yao na ya wadhamini wao mbele yajamii.

5. Kulazimishwa: Hii inatokea pale ambapo tabaka moja katika jamii lina nguvu za kisiasa na kiuchumi kiasi cha kuwa na nguvu juu ya matabaka mengine. Katika hali hii, msanii apende asipende atadhaminiwa na tabaka lenye nguvu. Iwapo msanii atakataa kudhaminiwa na tabaka hilo, kazi zake zinaweza kupigwa marufuku au kudhibitiwa.

6. Kutafuta umaarufu: Baadhi ya wasanii hudhaminiwa kwa lengo la kuwafanya wajulikane kwa watu. Wasanii wa aina hii wanapenda kutumia umaarufu wa mtu au shirika fulani ili na wao wajulikane angalau hata robo ya mdhamini wao. Wanaona ufahari kujulikana bila kujali athari mbaya wazipatazo au izipatazo jamii.

7. Mgawanyo wa kazi: Jamii imegawanyika katika "makundi kazi" mbalimbali yakiwamo ya wasanii na wadhamini. [li makundi haya yaendelee kuwapos, hayana budi kutegemeana na kuendelezana hata kama kuna athari zake.

Athari za udhamini

Udhamini una faida na hasara katika kazi za kifasihi. Zifuatazo ni faida na hasara hizo.

Faida za udhamini

1. Husaidia baadhi ya wasanii kufanya tafiti za masuala mbalimbali yanayohusu jamii. Baada ya tafiti hizo, wasanii huwasilisha masuala hayo kwa njia ya sanaa.

2 Husaidia jamii kupata kazi mbalimbali za fasihi, hasa fasihi andishi ambayo inahitaji fedha nyingi ili ikamilike. Kupitia msaada wa wadhamini, mwandishi hapati shida ya kuzalisha na kusambaza kazi yake kwa umma. Kazi hizi zote hufanywa na wadhamini na, hivyo, kuwafikia walengwa kiurahisi.

3. Udhamini husaidia kuibua na kuendeleza vipaji, hasa vya wasanii chipukizi ambao hawana fedha za kutosha ili kukamilisha kazi zao na kuonesha vipaji vyao kwa jamii. Kwa mfano, mashindano ya uandishi wa kazi za fasihi kwa Shule za sekondari yaliyodhaminiwa na Umoja wa Waandishi wa Vitabu Tanzania (UWAVITA) miaka ya 1970 yalisaidia kuibua na kuendeleza vipaji vya waandishi chipukizi ikiwa ni pamoja na kuchapisha kazi zao. Kadhalika, mashindano ya ushairi ya "Tuzo ya Ebrahim Hussein" yamesaidia kuibua vipaji vya washairi chipukizi. Pia, Bongo Star Search ya TBCI na Tanzania House ofTa1ents (THT) ambayo ipo chini ya Clouds Media Group hudhamini wanamuziki wachanga. Wadhamini hawa huweza kuibua na kuendeleza vipaji vya washiriki

4. Baadhi ya wasanii hujipatia fedha kutokana na kudhaminiwa. Hii inatokana na mgao (mrabaha) wanaoupata baada ya kazi zao kuuzwau Vilevile, wasanii hutajirisha wadhamini kutokana na mauzo ya kazi zao.

5. Udhamini husaidia kuleta ushindani wa ubora wa kazi katika soko la kazi za fasihi. Kuwapo kwa wadhamini wengi husababisha kuwapo kwa wasanii wengi na, hivyo, kuwa na kazi za kutosha. Matokeo yake huleta ushindani wa bei katika soko. Hili pia husaidia kuinua kiwango cha ubora wa kazi husika kwani kazi duni hukosa wanunuzi hata kama zitauzwa kwa bei ya chini.

Hasara za udhamini


I. Humtenga msanii na jamii yake; kwani msanii hutunga kazi zenye maudhui yanyotakiwa na mdhamini au mamlaka zilizopo hata kama yamepotoka.

2 Udhamini humnyima msanii uhuru. Kazi za fasihi hutawaliwa na mwelekeo wa mdhamini kifani na kimaudhui. Hivyo, msanii hukosa uhumu wa kutunga kazi yenye maudhui ayatakayo;

3. Mara nyingi, kazi ya sanaa huwa mali ya mdhamini ambaye huwa na mamlaka kuliko msanii, hasa kama msanii huyo hana hakimiliki.

4. Udhamini husababisha utegemezi miongoni mwa wasanii. Hata kama msanii anajitosheleza kifedha, bado atahitaji mkono wa mdhamini ili kazi yake ikamil ike.

5. Udhamini husababisha wasanii wengi kupenda fedha kuliko wajibu wao wa kuelimisha jamii. Kutokana na kupenda fedha, wasanii hutunga kazi pendwa ambazo baadhi haziusawiri vizuri uhalisi.

6. Udhamini hukuza utabaka kati ya mdhamini na mdhaminiwa.

7. Udhamini huifanya sanaa kuwa na mwelekeo wa aina moja; na hivyo, huwafanya wasanii kushindwa kueleza hali halisi. Hii inatokana na ukweli kuwa kazi za fasihi hazina budi kuendana na itikadi ya mdhamini.

Zoezi 03

(i) Fafanua dhana ya udhamini wa kazi za fasihi.

(ii) "Udhamini wa ushawishi ni sawana udhamini wa nguvu." Jådili.

(iii) Fafanua athari za udhamini wakazi za fasihi kwajamii.

(iv) Eleza ni kwa namna gani jamii nzima ni mdhamini wa kazi ya fasihi. Toa mifano muafaka.

Uandishi wa kazi za kifasihi

Uandishi wa kazi za fasihi ni mchakato wa kiubunifu unaotumiwa na mtunzi wa kazi za fasihi katika kutunga kazi yake. Katika kuandika kazi za fasihi, msanii anatakiwa kujiuliza maswali kadha wa kadha. Baadhi ya maswali hayo ni: Anaandika kuhusu nini? Anamwandikia nani? Anaandika kwa kutumia mandhari ipi? Lengo lake ni nini? na, anaandika kwa namna gani? hii inatokana na ukweli kuwa mwandishi huandika kazi yake ili isomwe na watu wengine. Hivyo, mwandishi hana budi kuzingatia mahitaji na mitazamo ya wasomaji wake ili awevze kuwapeleka anakotaka huku wakiendelea kufurahia kusoma kazi husika.

Waandishi wa fasihi huandika kazi zao kwa malengo tofautitofauti. Miongoni mwa malengo hayo ni kusawiri uhalisi wa kijamii kwa lengo la kuurekebisha au hata kuubadili ikibidi. Hii ina maana kuwa mwandishi sharti aibuke na vitu vipya ambavyo vitawavutia wasomaji katika kuwahabarisha yale yanayotokea katika jamii yao. Vilevile, waandishi wa kazi za fasihi huandika kazi zao kwa lengo la kuelezea hisia zao ambazo wanaamini kuwa zitawavutia wasomaji wao ili wayaone maisha kama wanavyoyaona wao. Pia, waandishi wanaandika kazi zao ili kuwaburudisha wasomaji wao. Hii inatokana na ukweli kuwa katika mchakato wa usomaji, msomaji hupata maarifa na burudani. Hali kadhalika, waandishi huandika kazi zao ili kuwashawishi wasomaji wao wakubali ukweli na namna ya kutafsiri mambo mbalimbali kama wanavyofanya wao. Mbali na hayo, waandishi huandika kazi zao kwa lengo la kuonesha na kuendeleza vipaji vyao ambapo hujipatia fedha kutokanana mauzo ya kazi hizo ikiwa ni pamoja na kutambuliwa na jamii zao.

Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa kazi za kifasihi

Kazi za kifasihi huwa na mtiririko wa hoja, mawazo na msuko wa visa kisanaa. Kazi hizi huweza kuwasilishwa katika maumbo manne ambayo ni hadithi fupi, riwaya, tamthiliyana ushairi. Yafuatayo ni mambo ya msingi ya kuzingatia katika kuandika kazi za kifasihi.

Wazo au dhamira

Mwandishi hufikiria masuala na athari ambazo zinafaa kuifikia hadhira yake. Mawazo ya mwandishi hutokana na uzoefu wake katika maisha kwani mwandishi huwa haandiki vitu kutoka hewani. Kwa hiyo, dhamira hutokana na uhalisi wa maisha ya binadamu. Mwandishi huchagua dhamira zinazoigusa zaidi jamii na kuandika kazi yake ili kufikisha ujumbe kwajamii. Mifano ya mambo yanayoigusa jamii ambayo mwandishi anaweza kuyatungia kazi ya fasihi ni ukombozi wa mwanamke, ajira kwa watoto, mapenzi, umaskini na upelelezi wa matukio ya kisiasa na kiuchumi. Mtunzi huchagua utanzu wa kutolea kazi yake. Utanzu huu huweza kuwa ushairi, hadithi fupi, riwaya na tamthiliya. Mtunzi mwenye wazo la kuonesha kuwapo kwa matabaka katika jamii anaweza kuwasilisha wazo lake kwa njia ya ushairi kama ifuatavyo:

Watoto wawili

l. Mtoto wa tajiri akilia hupewa mkate,

Mtoto wa tajiri akilia hupewa picha kuehezea, 

Mtoto wa tajiri akilia huletewa kigari akapanda,

Akiendelea kulia hupanda mgongo wa yaya,

Akikataa kunyamaza ulimwengu mzima hulaumiwa.

2. Mtoto wa masikini akilia hula mchanga,

Mtoto wa masikini akilia hupewa mti kuchezea,

Akilia mtoto wa masikini huvutwa kashani,

Akiendelea kulia hupanda mgongo wa mama ulio uchi, 

Akikataa kunyamaza wazazi husikitika kimya kimya.


Hapa mtunzi ametumia mbinu ya usawiri sambamba ili kumfanya msomaj i ajione mwenyewe na kulinganisha tofauti za kitabaka baina ya watoto hao wawili.Wazo hili linaweza kuelezwa katika umbo la riwaya au tamthiliya Pia.

Wahusika

Wahusika ni viumbe wenye kubeba maudhui yanayotokana na jamii husika. Wahusika hupewa vitendo na lugha kwa ajili yakuwasilisha ujumbe kwa hadhira. Mwandishi huwapa wahusika sifa na tabia ambazo hadhira huziona kama za watu wanaoishi katika jamii zao. Wahusika hawa hupewa majukumu mbal imbali ambayo huwapambanua kama wahusika wakuu au wahusika wadogo.

Wahusika wakuu sharti wapewe nafasi kubwa katika kazi ya fasihi husika kwa kuwa wanawåkilisha wazo kuu la mwandishi. Mwandishi anaweza kumfanya mhusika mkuu kuwa mwenye akili, nguvu, huruma na mbunifil.

Wahusika wadogo hupewa nafasi ndogo na hubeba mawazo madogo kwenye kazi ya fasihi. Hata hivyos, wahusika hawa wote sharti wajengwe katika migogoro inayoibua dhamira na hatimaye, ujumbe. Wahusika hawa sharti waakisi waziwazi au kimafumbo uhalisi wa maisha ya kila siku ya jamii. Matumizi ya wahusika lazima yazingatie muktadha, mwonekano, sifa na uwezo wa mhusika. [dadi ya wahusika hutegemea urefu wa kisa na idadi ya Visa vidogo vidogo ndani ya kisa kimoja. Mara nyingi, wahusika wa namna hii ni wahusika wa riwaya na tamthiliya. Katika ushairi, si kila mara mwandishi huonesha mhusika mkuu isipokuwa kama ataehanganya mtindo wa riwaya au tamthiliya katika utungo wake. Matumizi mazuri ya wahusika huifanya kazi ya kifasihi kuwa nzuri.

Matumizi ya lugha ya kisanaa

Lugha ya kisanaa ndiyo msingi wa kazi yoyote ya fasihi kwa sababu huitofautisha kazi ya kifasihi na kazi nyingine zisizokuwa za kifasihi. Hivyo, mwandishi wa kazi za fasihi anatakiwa kutumia lugha yenye kumvutia msomaji. Lugha ya kisanaa hujumuisha, pamoja na vipengele vingine tamathali za semi, taswira, methali na nahau kulingana na maudhui husika ili kuvuta hisia za wasomaji.

Kwa upande wa ushairi, mwandishi anatakiwa kuzingatia uteuzi wa msamiati wenye mnato, ambao unaweza kujenga picha na taswira. Aidha, anapaswa kujua kwamba hafungwi na kanuni za kisarufi, hivyo anaruhusiwa kutumia maneno ya mkato na hata kubadili mpangilio wa sentensi.

Muundo

Muundo ni umbile au mpangilio wa visa na matukio katika kazi ya fasihi. Mwandishi anaweza kuandika kazi yake kwa kutumia muundo wa moja kwa moja, ambapo kisa cha kwanza hufuatwa na cha pili hadi cha mwisho. Pia, mwandishi anaweza kuandika kazi yake kwa kutumia muundo rejeshi au changamani, ambapo visa namatukio huchangamana au hurejeleana. Mathalani, mtunzi wa riwaya anaweza kujenga muundo wa hadithi kwa kutumia sehemu au sura mbalimbali. Ndani ya sura au sehemu hizo kunatakiwa kuwe na msuko wa matukio ambao unaleta mgogoro miongoni mwa wahusika. Kwa maneno mengine, kazi za kifasihi hujengwa na migogoro baina ya wahusika. Aidha, upangaji wa kazi za fasihi katika sura hurahisisha usomaji.

Mtunzi wa hadithi fupi anatakiwa kuwa na visa vichache na kutumia wahusika wachache. Kwa kawaida, hadithi fupi huwa na kisa kikuu kimoja, na wahusika wakuu wawili wanaokinzana. Wahusika hao wanaweza kuwa na wafuasi wao wachache wasiokuwa watendaji wakuu. Mgogoro wa hadithi fupi huwa mkali, na unaposuluhishwa hadithi humalizika. Hadithi fupi haipaswi kuwa na mawanda mgpana ya kiwakati na kijiografia.

Mtunzi wa tamthiliya anatakiwa kujenga kazi yake kwa kutumia, Vitendo, Sehemu au Maonesho, na kutoa maelezo ya jukwaa kwa hadhira yake. Maelezo ya jukwaa husaidia kufafanua mandhari, vifaa na matendo ya wahusika.

Mtunzi wa ushairi azingatie idadi ya mishororo katika ubeti, na urari wa vina na mizani katika kila ubeti, hasa kama ni mwanamapokeo. Mathalani, anaweza kutunga shairi lenye muundo wa mishororo minne au mitano kadiri atakavyoona inakidhi kanuni za utungaji wa mashairi ya kimapokeo. Kwa upande wa wana usasa, uteuzi wa muundo haufungwi na sheria bali huongozwa na maudhui, lengo la mtunzi na mbinu za uwasilishaji.

Mtindo

Mtindo ni namna ambavyo msanii hutunga kazi yake na kuipa upekee tofauti na kazi nyingine. Kwa vile mtindo huonesha upekee wa mwandishi, ni vema mwandishi akachagua mtindo utakaowavutia wasomaji. Mitindo ya uandishi wa kazi za kifasihi ni mingi kwa mfano katika hadithi, ushairi na tamthiliya zilichota vipengele kutoka katika fasihi simulizi. Ni jukumu la mwandishi kuhakikisha kuwa kazi yake inakuwa katika ubora na upekee ili kuifikishia hadhira yake yale aliyoyakusudia kwa njia ya kuvutia.

Mandhari

Mandhari ni mahali ambapo Visa na matukio ya ndani ya kaziya fasihi hufanyika. Aidha, mandhari hujumuisha wakati na muktadha ambao Visa na matukio hutendeka. Mandhari huweza kuwa ya kubuni au halisi. Mwandishi ni lazima atumie mandhari inayoakisi matukio na Visa vya kazi husika. Iwapo, kwa mfano kazi ya fasihi inahusu maisha ya kijijini, mtunzi atumie mandhari ya kijiji ili kuijengea hadhira dhana inayoelezwa kwa urahisi. Mathalani, mtunzi hawezi akawa anaeleza kisa cha kijijini halafu akasema: "Wahusika walipokuwa ofisini ghorofa ya Saba, lifti ikagoma kufanya kazi." Vljiji vyetu vingi havina mandhari ya namna hiyo.

Mandhari iliyobuniwa vizuri husaidia kufikisha ujumbe na kuaminika kwa masimulizi. Uhalisi wa matukio na Visa, katika kazi za kifasihi, hutegemea zaidi mandhari na muktadha wake.

Hadhira

Mwandishi huandika kazi yake ili iweze kusomwa na watu wengine. Kwa hiyO, hana budi kujua aina ya watu anaowaandikia kazi husika. Mwandishi anatakiwa kujua mahitaji ya wasomaji Wake, ikiwa ni pamoja na mitazamo yao kuhusu kile anachokiandika. Kwa mfano, kama mwandishi anawaandikia watoto, anatakiwa kuandika hadithi fupi yenye lugha nyepesi ili watoto waweze kuvutiwa kusoma na kuelewa maudhui ya hadithi hiyo kwa urahisi. Aidha, anaweza kuweka picha au michoro yenye rangi mbalimbali ili kuwavutia watoto na kuwajengea kumbukumbu.

Ujumbe

Ujumbe ni taarifa au funzo linalotokana na kazi ya fasihi. Kazi moja inaweza kuwa na ujumbe zaidi ya mmoja. Mathalani, kazi ya kifasihi inaweza ikawa inatoa ujumbe kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii, kujikinga na maradhi, kuepuka tamaa, uaminifu na utii.

Zoezi la 04

(i) Kwa nini mtunzi wa kazi za kifasihi hutakiwa kuzingatia mandhari?

(ii) Linganisha vipengele vya muundo wa shairi la kimapokeo na muundo wa riwaya, 

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256