KISWAHILI FORM FOUR TOPICAL EXAMINATIONS
TOPIC : 1  MAENDELEO YA KISWAHILI

MASWALI YA MADA, MADA YA 2.

MADA: MAENDELEO YA KISWAHILI:

KIDATO CHA NNE.

A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI.



  1. Wageni wa mwisho kuitawal Nchi ya Tanganyika na kuacha athari mbalimbali kutoka lugha ya Kiswahili ni:-

  1. Waarabu

  2. Waingereza

  3. Wareno.

  4. Wajerumani.

  1. Ni kwa vipi Waingereza walichangia kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili katika shughuli za kiutawala?

  1. Kuanzisha kamati ya lugha na kuanzisha kampuni ya uchapishaji wa vitabu.

  2. Kuwafukuza Waarabu wa Omani.

  3. Kuanzisha mafundisho ya elimu ya kutafsiri Biblia.

  4. Kuwafundisha wazungu wa kilowezi.

  1. Waingereza walisanifisha lugha ya Kiswahili ili:-

  1. Waweze kupata urahisi wa kufanya mawasiliano na watu wa Afrika Mashariki na kuimarish utawala wao.

  2. Kuwafukuza wakoloni wa Kijerumani.

  3. Kurahisisha utumiaji wa Kiswahili Ulaya.

  4. Kuwapa moyo Watanzania wa kujitawala.

  1. Kihistoria, lugha ya Kiswahili imeanzia katika;

  1. Visiwa vya Zanzibar na Pemba.

  2. Upwa wa Afrika ya Mashariki

  3. Nchini Mogadishu na Samalia.

  4. Pwani ya nchi ya Kenya.

  1. Moja ya taasisi zinazochangia kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania ni?

  1. UKUTA

  2. TFF

  3. UDASA.

  4. UKATA





SEHEMU B: JAZA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI:

  1. Mambo yaliyosaidia kukua na kueneza kwa lugha ya Kiswahili enzi za utawala wa Waingereza ni

  1. ______________________

  2. _____________________

  3. ____________________

  4. ___________________ na

  5. _____________________

  1. Ili kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili nchini Tanzania baada ya uhuru, Serikali iliunda Taasisi mbalimbali, moja ya Taasisi hizo ni Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI). Taja idara za TUKI.

  1. _____________________

  2. _______________________

  3. ______________________

  4. _____________________ na

  5. _______________________

  1. Bainisha sababu tatu zilizosaidia kukua na kuenea haraka kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania kuliko nchini Kenya na Uganda.

  1. ______________________

  2. ______________________ na

  3. _______________________



SEHEMU C: MAJIBU YA MAELEZO MAREFU

  1. Fafanua namna Taasisi ya elimu ya watu wazima inavyokuza na kueneza Kiswahili nchini Tanzania.

  2. Eleza jukumu la Wizara ya elimu na mafunzo ya Ufundi katika kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Tanzania.

  3. Eleza tathmini ya maendeleo ya Kiswahili nchini Tanzania wakati wa ukoloni.

  4. Eleza tathmini ya maendeleo ya Kiswahili nchini Tanzani baada ya Uhuru.

LEARNINGHUBTZ.CO.TZ Page 2


TOPIC : 2  UHAKIKI KAZI YA FASIHI ANDISHI

KISWAHILI KIDATO CHA NNE.

MASWALI YAMADA

MADA: UHAKIKI WA KAZI YA FASIHI ANDISHI.

SEHEMU A:

KUCHAGUA.

1. Chagua jibu lililo sahihi kutoka katika maneno uliyopewa.

  1. Moja ya vigezo vya uhakiki ni?

  1. Dhima ya uhakiki

  2. Ukweli wa mambo yanayoelezwa

  3. Fani na maudhui

  4. Maudhui na falsafa

(ii) Ufundi na uzuri wa kisanaa katika fasihi hujulikana kama?

  1. Fasihi

  1. Uhakiki

  1. Maudhui

  2. Fani

(iii) Vifuatavyo ni vipengele vya maudhui katika fasihi isipokuwa;

  1. Ujumbe

  1. Dhamira

  1. Wahusika

  2. Falsafa.

(iv) Zifuatazo ni tanzu za fasihi andishi isipokuwa?

  1. Hadithi

  1. Riwaya

  1. Tamthiliya

  2. Ushairi.

(v) Moja ya kigezo cha kufaulu kwa mtuzi wa kazi ya fasihi ni?

  1. Kubainisha matatizo yaliyomo kwenye jamii yake na kupendekeza njia sahihi ya kuyatatua.

  1. Kuandika kazi ya kufasihi ya kuvutia

  1. Kufuata ipasavyo vipengele vya uhakiki.

  2. Kubainisha wahusika wa kazi ya fasihi.










SEHEMU B:

2. Oanisha maneno yaliyo katika kifungu A ili yaendane nay ale ya kifungu B.

FUNGU: A

FUNGU: B

  1. Shughuli ya kupima ubora na dhaifu wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi.

  2. Maneno ya kawaida katika jamii yanayotumiwa na msanii kuibua dhana fulani.

  3. Hubainisha mambo yaliyomo pamoja na mafunzo katika kazi ya fasihi.

  4. Ni kipengele kinachotofautisha kazi ya fasihi na sanaa nyingine

  5. Utungo mrefu wa kimasimulizi wenye dhamira anuai.

  1. Wahusika

  2. Sanaa

  3. Lugha.

  4. Taswira.

  5. Fani.

  6. Dhamira

  7. Maudhui

  8. Uhakiki

  9. Uhakiki

  10. Fasihi.



SEHEMU C:

  • Jibu maswali yafuatayo kwa maelezo mafupi.

4. Fafanua vipengele vya fani na maudhui katika uhakiki wa kazi za fasihi .

5. Kwa kutumia mifano kutoka katika riwaya ya Watoto wa Mama N’tilie, eleza umuhimu wa kuhakiki vipengele hivi.

  1. Msimamo wa mwandishi

  2. Wahusika

  3. Falsafa ya mwandishi.

USHAIRI:

Malenga Wapya TAKILUKI

Mashairi ya ChekaCheka T.A. Mvungi

Wasakatonge M.S. Khatib.

6. Ushairi ni utanzu wa kifasihi ambao hauna mchango wowote kwa maendeleo na ustawi wa jamii. Jadili kauli hii kwa kutumia vitabu viwili ulivyosoma kati ya hivyo vilivyotajwa.

7. Jadili dhana ya matabaka inavyozorotesha ustawi wa jamii husika kwa kutumia diwani mbili ulizosoma kati ya hizo zilizotajwa.

8. Uhakiki wa kazi za ushairi na riwaya hutofautianaje katika vipengele hive?

  1. Muundo

  2. Mtindo

  3. Wahusika

  4. Picha na taswira.

9. Eleza kwa ufasaha dhana zifuatazo zitumikazo katika dhana ya uhakiki wa kazi ya kifasihi.

  1. Mhakiki

  2. Tahakiki

  3. Msanii

  4. Uhakiki.

SEHEMU D:

10. Andika NDIYO kwa kauli iliyo sahihi na HAPANA kwa kauli isiyo sahihi.

  1. Riwaya ya watoto wa Mama N’tilie imeaksi jamii ya Tanzania katika suala la umaskin na athari za ulevi____________

  2. Muundo katika ushairi hujumuisha idadi ya mistari katika ubeti____________

  3. Mkusanyiko wa mashairi na tenzi mbalimbali ndani ya kitabu kimoja huitwa diwani_________

  4. Falsafa ni wahusika ambao hujenga kazi ya fasihi_________

  5. Fani na maudhui katika kazi ya fasihi zinaweza kutenganishwa________

  6. Mhakiki ni msanii anayeiandika kazi ya fasihi kwa jamii yake iliyomlea na kumkuza_____

  7. Mashairi, nyimbo, ngonjera na maghani ni baadhi ya kazi za kifasihi zilizomo kwenye utanzu wa ushairi___________

  8. Uhakiki husaidia katika uboreshaji na uedelezaji wa kazi ya kifasihi___________

  9. Dhana ya mtindo husaidia katika ubainishaji wa kazi ya msanii mmoja na msanii mwingine___

  10. Migogoro na misuguano miongoni mwa wahusika wa kazi za fasihi husaidia katika uibuaji wa dhamira za msanii______

11. Soma beti mbili zifuatazo kutoka diwani ya WASAKATONGE kisha uhakiki vipengele vya fani na maudhui.

NAHODHA.

  1. Nahodha,

Wang’ang’nia sukani,

Mechafuka, bahari siyo shwari,

Si shwari, pepo zinatuathiri,

Zaathiri, na mawimbi ni hatari,

Ni hatari, tufani meshamiri,

Meshamiri na mvual zitiriri,

Zitiriri, radi nazo si kadri,

Nahodha tosa nanga!



  1. Nahodha,

Wang’ang’ania sukani,

Na jahazi, lenda mramamrama,

Mrama, na kupasuka matahima,

Mataruma, mkuku umeachama,

Meachama, tanga limo kudatama,

Kudatama, foromali yainama,

Yainama, chombo sasa kitazama.



12. Eleza kwa ufupi dhana ya mhakiki wa kazi ya fasihi.

13. Eleza umuhimu wa fasihi andishi katika jamii.

LEARNINGHUBTZ.CO.TZ Page 4


TOPIC : 3  UONGEZAJI MSAMIATI

MASWALI YA MADA. MADA YA KWANZA.

MADA: UONGEZAJI WA MSAMIATI:

KIDATO CHA NNE.

A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI.



  1. Neno “Kizibo” limeundwa kutokana na njia ya uundaji wa maneno iittwayo:-

  1. Kuambatanisha maneno

  2. Kubadili mpangilio wa maneno

  3. Kuangalia kazi ya kitu.

  4. Kubadili mpangilio wa neno.

  1. Ipi orodha ya maneno ambayo yameundwa kwa njia ya utohoaji wa maneno?

  1. Bendera, meza, beseni na pesa.

  2. Shuka, saa, doti na kigoda.

  3. Bajia, leso, waya na ikulu.

  4. Namba, elimu, papaya na ng’atuka.

  1. Ipi kati ya njia zifuatazo za uundaji wa maneno si njia sahihi ya uundaji wa maneno.:-

  1. Uambishaji.

  2. Kutohoa.

  3. Kuambatanisha maneno.

  4. Kutafsiri.

  1. Lipi kati ya maneno yafuatayo limeundwa kwa njia ya kufananisha sauti?

  1. Malapa.

  2. Redio

  3. Kikunio.

  4. Shati.

B: JAZA NAFASI ZILIZO WAZI:

  1. Neno “Kikunio” limeundwa kutokana na njia ya uundaji wa maneno iitwayo__________

  2. Mfano wa neno lililoundwa kwa njia ya uambishaji ni ________________

  3. Maneno motomot, mbalimbali, sawasawa, yameundwa kwa njia ya______________

  4. Neno “Kipanya” limeundwa kutokana na njia ipi?_________________

  5. Njia mbili za uundaji wa maneno ni __________________ na ________________

  6. Mfano wa neno lililoundwa kwa kufupisha maneno ni ________________





C: MAJIBU YA MAELEZO MAREFU:

  1. Eleza namna maneno yaliyoundwa katika miktadha ya:

  1. Maendeleo ya kiuchumi

  2. Maendeleo ya sayansi na teknolojia

  3. Mabadiliko yo mfumo wa siasa

  4. Maendeleo ya mfumo wa tiba

  5. Maendeleo ya kiutamaduni.

  1. Eleza umuhimu wa kuongeza msamiati katika lugha. Toa oja tano.

LEARNINGHUBTZ.CO.TZ Page 2


TOPIC : 4  UTUNGAJI KAZI YA FASIHI

KISWAHILI KIDATO CHA NNE.

MASWALI YAMADA

MADA: UTUNGAJI WA KAZI ZA FASIHI.

SEHEMU A:

KUCHAGUA.

1. Chagua jibu lililo sahihi kutoka katika maneno uliyopewa.

  1. Ipi si kweli kuhusu kanuni za utunzi wa mashairi ya kimapokeo?

  1. Vina

  2. Muundo

  3. Mizani

  4. Wahusika

(ii) Utunzi wa mashairi ya kwa kufuata muundo wa mistari mitatu kwa kila ubeti huitwa.

  1. Tathnia

  1. Tarbia

  1. Tathlitha

  2. Takhmisa

(iii) Zipo aina mbili za mashairi, nazo ni;

  1. Mashairi ya kimamboleo na kisasa

  1. Mashairi ya kimapokeo na kimamboleo

  1. Mashairi ya mtindo na muundo

  2. Mashairi ya kikasuku na kihakiki.

(iv) Vipera vya ushairi katika fasihi ni?

  1. Ngonjare, tenzi, nyimbo na mashairi

  1. Hadithi, Visasili, ngonjera an mashairi

  1. Muziki wa dansi, nyimbo, ngonjera na riwaya

  2. Nyimbo, muziki, tenzi na majigambo.

(v) Ipi si kweili kuhusu dhana ya ushairi?

  1. Ni utanzu wa mashairi

  1. Ni lugha ya mkato

  1. Ina matumizi ya picha na taswira

  2. Ina muundo wa beti.










SEHEMU B:

2. Oanisha maneno yaliyo katika kifungu A ili yaendane nay ale ya kifungu B.

FUNGU: A

FUNGU: B

  1. Muundo

  2. Mtindo

  3. Vina.

  4. Mizani

  5. Muwala


  1. Idadi ya silabi zilizomo katika mstari wa ubeti

  2. Mshororo wa mwisho katika kila ubeti.

  3. Namna shairi lilivyogawanyika katika beti zenye idadi maalum ya mistari.

  4. Hubainisha aina ya shairi lililotungwa.

  5. Silabi zinazofanana sauti katikati na mwisho wa mstari katika ubeti.

  6. Namna shairi linavyoweza kupangika katika aya.

  7. Uwiano na umantiki wa mtiririko wa beti katika shairi.






SEHEMU: C

3. Andika NDIYO kwa kauli iliyo sahihi na SIYO kwa kauli isiyo sahihi.

  1. Ushairi ni utanzu wa fasihi wenye kutumia lugha ya mjazo au masimulizi _______

  2. Muundo wa kazi za kishairi unatofautiana na muundo katika tanzu nyingine za fasihi___________

  3. Matumizi ya picha na taswira ni kigezo muhimu zaidi katika utunzi wa kazi za kishairi kuliko kazi nyingine za fasihi zisizo za kishairi__________

  4. Mashairi ya kimapokeo yana ubora zaidi kimaudhui kuliko aina nyingine ya mashairi____

  5. Idhini ya kishairi husaidia katika kufupisha na kuyakatiza maneno ili kuleta urari wa vina na mizani_________

  6. Katika utunzi wa mashairi utoshelezi haubainiki katika kila ubeti husika_____

  7. Mashairi na tenzi hutofautiana katika idadi ya mizani tu._______

  8. Nyimbo hutofautiana na maghani ka sababu nyimbo huimbika.______

  9. Ngonjera hutofautiana na mashairi kwa sababu ngonjera ina muundo wa kimajibizano baina ya wahusika________

  10. Ushairi hudumisha na kuendeleza amali za jamii._________







SEHEMU D:

4. Tunga shairi lenye beti nne kuhusu “UMUHIMU WA ELIMU”.

5. Tunga ngonjera yenye beti sita kuhusu “USAWA WA KIJINSIA”.



LEARNINGHUBTZ.CO.TZ Page 3


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256