SAYANSI 2017  
 
 Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye karatasi ya kujibia.
 1. Ipi kati ya tabia zifuatazo humwezesha ndege kuruka hewani?
  - Mifupa milaini iliyo na manyoya.
  - Miili iliyochongoka na mifupa iliyo wazi ndani.
  - Mfupa iliyoungana.
  - Uwepo wa mifupa mingi.
  - Mifupa imara ya mabawa iliyo imara.
  
Chagua Jibu    
2. Makundi makuu ya viumbe hai ni:
  -  Mimea na ndege 
  -  Mimea na mijusi
  -  Wanyama na majani 
  -  Mimea na wanyama
  -  Wanyama na bakteria
  
Chagua Jibu    
3. Ipi kati ya aina zifuatazo za mbegu hujisambaza zenyewe?.................
  -  Nazi na pamba 
  - Kunde na mbaazi
  -  Kunde na papal 
  -  Embe na pera
  -  Chungwa na mbaazi
  
Chagua Jibu    
4. Chunguza Kielelezo Namba 1, kisha chagua jibu lenye mpangilio sahihi wa zilizoonyeshwa kwa alama A - D.
  
Kielelezo Na. 1 
  - Nyuzi, uboho njano, uboho nyekundu, gegedu.
  - Uboho nyekundu, gegedu, uboho njano, kano.
  - Gegedu, kano, uboho njano, uboho nyekundu.
  - Kano, njano, gegedu, uboho njano, uboho nyekur.: _
  - Uboho njano, gegedu, kano, uboho nyekundu.
  
Chagua Jibu    
5. Chunguza Kielelezo Namba 2 kisha jibu swali linalofuata
  
Kielelezo Na. 2 
 Kifaa katika Kielelezo Namba 2 hutumia tabia ipi ya mwanga?..............
  -  Kuakisiwa 
  -  Mpitisho 
  -  Mwachano
  -  Mgeuzo 
  -  Mtawanyiko
  
Chagua Jibu    
6. Magonjwa yapi kati ya yafuatayo huzuiliwa kwa chanjo?................
  -  Surua na kifaduro 
  -  Kichocho na malaria
  -  Kuhara na mkamba 
  -  Ukimwi na kisukari
  -  Kifua kikuu na tetekuwanga
  
Chagua Jibu    
7. Kitu gani muhimu mwanamke mjamzito anapaswa kuzingatia?...............
  - Kula chakula kingi cha wanga anapokaribia muda wa kujifungua
  - Kufanya kazi ngumu ili awe mkakamavu.
  - Kuhudhuria kliniki na kula mlo kamili.
  - Kulala mara kwa mara.
  - Kutumia sabuni zenye manukato wakati wote.
  
Chagua Jibu    
8. Ugonjwa unaotokana na tatizo la upumuaji ni 
  -  pumu 
  -  malaria kali 
  -  kuzimia
  -  kifafa 
  -  kisukari
  
Chagua Jibu    
9. Kitu gani kitatokea endapo mfumo wa fahamu utasimama kufanya kazi?.............
  - Mtu ataanza kutetemeka.
  - Mtu ataanza kuhisi udhaifu.
  - Mtu ataanza kuhisi maumivu makali mwilini.
  - Kukosekana kwa mawasiliano ndani ya mwili.
  - Mtu ataanza kupungua uzito.
  
Chagua Jibu    
10. Mojawapo ya dalili za unyafuzi ni.....................
  - uso kufanana na wa mzee
  - macho meupe na mafua 
  - tezi ya shingo kuvimba
  - kuhisi baridi na kutapika 
  - tumbo kubwa na kuvimba miguu
  
Chagua Jibu    
11. Njia za uzazi wa mpango ambazo ni salama kwa afya ya mama ni.............
  - kitanzi na sindano 
  - njia ya asili
  - sindano na vidonge 
  - vidonge na kondomu
  -  kondomu na sindano
  
Chagua Jibu    
12. Njia bora ya kuepuka utapiamlo ni ..............
  - kutumia dawa za kinga mara kwa mara.
  - kuelimisha jamii juu ya matumizi ya mlo kamili.
  - kula mboga za majani kwa wingi.
  - kutumia madawa ya kuongeza virutubisho mwilini.
  - kuongeza idadi ya milo kwa siku.
  
Chagua Jibu    
13. Mtu aliyepigwa na shoti ya umeme anaweza kusaidiwa kwa kutumia ..................
  -  miguu 
  -  kipande cha chuma 
  -  ubao mkavu
  - mikono 
  - ubao mbichi
  
Chagua Jibu    
14. Vipande viwili vya ubao safi vilivyofungwa kwenye sehemu mfupa ulipovunjika husaidia
  - kuzuia kutokwa damu
  - kukipa joto kidonda. 
  - kuimarisha sehemu iliyovunjika.
  - kutibu sehemu iliyovunjika. 
  - kuunganisha sehemu iliyovunjika
  
Chagua Jibu    
15. Gesi inayotumika kuzima moto ni ................
  -  haidrogeni 
  -  kabondayoksaidi 
  -  naitrojen
  -  kaboni 
  -  oksijeni
  
Chagua Jibu    
16. HIV haienezwi kwa ......
  -  kujamiiana 
  -  kuchangia sindano 
  -  kuumwa na mbu
  -  kuchangia nyembe 
  -  kuwekewa damu
  
Chagua Jibu    
17. Uhusiano kati ya magonjwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana na UKIMWI ni kwamhz
  - Ni rahisi kupata maambukizi ya UKIMWI kama umeambukizwa magonjwa yato-,na kujamiiana.
  - Magonjwa yanayoenezwa kwa kujamiiana ni sawa na UKIMWI.
  - Dawa za kutibu magonjwa yanayoenezwa kwa kujamiiana zinaweza kutumik,aUKIMWI.
  - Magonjwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana na UKIMWI yanaenezwa -- kujamiiana pekee.
  - Majongwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana na UKIMWI yanatibika.
  
Chagua Jibu    
18. Ipi kati ya sentensi zifuatazo ina maana sahihi ya UKIMWI?...............
  -  Kupoteza kinga ya mwili,
  -  Kinga kubwa ya mwili.
  -  Kukosekana kwa kinga mwilini 
  -  Upungufu wa kinga mwilini.
  -  Uwezo wa kinga ya mwili.
  
Chagua Jibu    
19. Mbinu mojawapo ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni...............
  - kutenga eneo la watu wenye virus! vya UKIMWI.
  - kuepuka kushirikiana vifaa vya chakula na watu wenye virusi vya UKIMWI.
  - kula chakula bora na kunywa mail safi.
  - kubadili tabia na kuepuka ngono zembe.
  - kufanya mazoezi ya mwili.
  
Chagua Jibu    
20. Vitu vilivyorushwa angani hurudi chini.............
  -  kwa sababu ya uzito 
  -  kwa sababu ya nguvu ya msuguano
  -  kwa sababu ya nguvu ya hewa 
  -  kwa sababu ya nguvu ya sayari
  -  kwa sababu ya nguvu ya uvutano
  
Chagua Jibu    
        BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB  
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA   
Try Another Test |