STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2016

201 6 - SAYANSI

SEHEMU A

Chaguajibu sahihi kisha andika herufiyake kwenye karatariya kujibia.

1. Ili mbegu ichipue inahitaji: 

 1. Maji, udongo na hewa
 2. Mvua, hewa na udongo
 3. Unyevu, udongo na jotoridi
 4. Maji, hewa na jotoridi
 5. Maji, mwanga na upepo
Chagua Jibu


2. Wadudu wanapohama toka ua moja kwenda lingine wanfanya hivyo ili:

 1. kuzalisha mimea  
 2. kuepuka maadui
 3. kutafuta nekta 
 4. kutafuta harufu 
 5. kusambaza mbegu
Chagua Jibu


3. Hali ya mtu kuzimia hutokana na ukosefu wa damu katika .......

 1. Tumbo
 2. Figo
 3. Mapafu
 4. Moyo
 5. Ubongo
Chagua Jibu


4.  Aina kuu mbili za mashine ni:

 1. ngumu na laini
 2.  rahisi na tata
 3. za kumenya na kutwanga 
 4. puli na roda
 5. roda na katapila
Chagua Jibu


5. Mojawapo ya njia za kuondoa takamwili katika mwili ni:

 1.  kutema mate 
 2.  kukojoa
 3. kuoga 
 4. kunawa mikono 
 5. kutoa machozi
Chagua Jibu


6. Mbegu ya kike ambayo haijarutubishwa huitwa:

 1.  kondo 
 2.  yai
 3. uterasi 
 4. ovari    
 5. mrija wa falopio
Chagua Jibu


7.  Angalia kielelezo namba 1 ambapo jotoridi lioneshwa kwa nyuzi za sentigredi kisha jibu maswali yanayofuata.

Mbegu itakayoota ni ya chombo kipi?

 1.  Chombo A    
 2.  Chombo B
 3.  Chombo C    
 4.  Chombo D  
 5.  Chombo A na D
Chagua Jibu


8. Sehemu zinazounda mfumo wa upumuaji katika mwanadamu ni:

 1.  pua, mdomo na tumbo
 2. mapafu, pua na ini
 3. pua, mapafu na masikio 
 4. koromeo, mapafu na kongosho
 5. mapafu, pua na mdomo
Chagua Jibu


9.  Mdudu yupi kati ya wafuatao huleta hasara kwa mkulima akiwa katika hatua ya pili ya ukuaji?

 1. Inzi                                                         
 2. Kipepeo
 3. Panzi                                                    
 4. Mbungo
 5. Mbu
Chagua Jibu


10. Usafirishaji wa chakula mwilini hufanywa na: 

 1. moyo     
 2. damu
 3. misuli                                     
 4. mapafu
 5. maji
Chagua Jibu


11. Tazama kwa makini kielelezo namba 2 kisha jibu maswali yanayofuata:

Alama Y inawakilisha sehemu iitwayo:

 1.  petali
 2.  filamenti
 3.  chavulio
 4.  pistili
 5.  ovari
Chagua Jibu


12.  Mbegu za mimea uhifadhi chakula katika:

 1.  mizizi 
 2. majani      
 3. shina
 4. kotiledoni 
 5. tunda
Chagua Jibu


13. Lipi kati ya magonjwa yafuatayo huambukizwa kwa njia ya kujamiiana?

 1.  Polio  
 2.  Kipindupindu         
 3.  Pepopunda
 4.  Kaswende                            
 5.  Tetekuwanga
Chagua Jibu


14. Nini kitatokea iwapo idadi ya wanyama wanaokula nyama katika eneo ni kubwa kulikc idadi ya wanaokula majani?

 1. Majani yatapungua
 2. Majani yatabakia kama yalivyokuwa awali
 3. Majani yatanyauka
 4. Majani yataongezeka
 5. Majani yataliwa
Chagua Jibu


15. Lipi kati ya mafungu yafuatayo ya vyakula hulinda mwili?

 1.  Samaki na maziwa          
 2.  Ugali na ndizi
 3.  Maharagwe na karanga 
 4.  Mayai na kabichi 
 5.  Matunda na mboga za majani
Chagua Jibu


16. Umuhimu wa asidi ya haidrokloric katika tumbo ni:

 1.  kubadili hali ya besi katika tumbo
 2.  kulainisha mafuta tumboni
 3.  kuongeza uchachu tumboni
 4.  kumengenya vyakula vya sukari tumboni 
 5.  kuua wadudu wanaoingia tumboni na chakula.
Chagua Jibu


17. Nini tofauti kati ya malaria na homa ya matumbo?

 1.  Malaria hushambulia mishipa ya damu, homa ya matumbo hushambulia neva za fahamu.
 2.  Malaria husababishwa na mbu, homa ya matumbo husababishwa na inzi.
 3.  Malaria hutibiwa kwa siku nne, homa ya matumbo hutibiwa kwa siku saba.
 4.  Malaria husababishwa na plasmodiam, homa ya matumbo husababishwa na bakteria.
 5.  Malaria huambatana na maumivu ya kichwa, homa ya matumbo huambatana na maumivu ya uti wa mgongo.
Chagua Jibu


18. Kipi kati ya vifuatavyo vinapaswa kudumishwa? 

 1. Kutumia kikombe kimoja wakati wa kunywa maji. 
 2. Kunawa mikono kabla ya mlo katika karai moja. 
 3. Kupika mboga za majani na nyama kwa muda mrefu.
 4. Kuchemsha na kuchuja maji ya kunywa. 
 5. Kuogelea katika mito na mabwawa.
Chagua Jibu


19. Viungo vinavyohusika katika kutoa takamwili mwilini ni:

 1.  figo, ini na moyo            
 2.  ini, ngozi na figo 
 3.  mapafu, moyo na figo              
 4.  moyo, figo na ngozi 
 5.  Ngozi, Ini na Moyo 
Chagua Jibu


20. Mbungo husababisha ugonjwa uitwao ....

 1.  homa ya matumbo     
 2.  nagana
 3. malale                                           
 4. matende                
 5. homa ya ini
Chagua Jibu


21. Tunaweza kujikinga na magonjwa ya moyo kwa kufanya yafuatayo: .......

 1. Kula chakula na kufanya mazoezi mara kwa mara
 2.  Kufanya mazoezi ya mwili, kuepuka kuvuta sigara na kuepuka kunywa pombe
 3.  Kula chakula chenye chumvi na kunywa pombe 
 4. Kufanya mazoezi ya mwili na kuvuta sigara 
 5. Kula vyakula vyenye mafuta na kunywa pombe
Chagua Jibu


22. Wanawake wajawazito wanashauriwa kula kiwango kikubwa cha vyakula vifuatavyo:

 1.  Wanga, mafuta na hamirojo
 2.  Mafuta, vitamini na protini
 3.  Protini, vitamini na madini ya chumvichumvi
 4.  Madini ya chumvichumvi na vitamini pekee 
 5. Protini, hamirojo na udongo pekee
Chagua Jibu


   23. Ili kujikinga dhidi ya malaria ni muhimu .........

 1.  kumeza mchanganyiko wa madawa
 2.  kutumia dawa za mitishamba
 3.  kutumia vyandarua vilivyowekwa dawa
 4.  kujifunika na blanketi Zito lililowekwa dawa 
 5.  kufanya mazoezi kila mara
Chagua Jibu


24. Kongosho hutoa homoni inayothibiti kiasi cha:

 1.  damu mwilini    
 2.  sukari mwilini
 3. takamwili                                      
 4. hamu ya chakula                   
 5.  oksijeni
Chagua Jibu


25.  Mojawapo ya kazi za misuli katika mwili ni:

 1.  kuwezesha kujongea
 2.  kuruhusu damu kupita 
 3.  kuruhusu maji kupita
 4. kuruhusu hewa kupita 
 5.  kuimarisha mwili
Chagua Jibu


26.  Lipi kati ya mambo yafuatayo si sahihi kumfanyia mtu aliyebanwa misuli?

 1.  Kuchua eneo lililoathirika kwa kiganja
 2.  Kuchua kwa kukandamiza eneo lililoathirika hadi misuli ilegee
 3.  Kuuchua msuli kwa kitambaa na maji baridi 
 4.  Kuweka kemikali zitakazowezesha misuli kulegea
 5.  Kulala juu chini na kuchua msuli ulioathirika kvva maji moto.
Chagua Jibu


27. Mtu anayetapika na kuharisha anapaswa kupewa:

 1.  asidi, maziwa na maji
 2.  maziwa, besi na sukari 
 3. maji, besi na maziwa
 4. chumvi, sukari na maji 
 5. sukari, asidi na besi
Chagua Jibu


28. Huduma ya kwanza anayopewa mtu aliyezimia ni:

 1.  kumpa hewa ya oksijeni
 2.  kumpa juisi ya nazi mbichi
 3.  kumlaza juu chini na kumbonyeza tumbo
 4.  kumpa maji yaliyochanganywa na glukosi
 5.  kumpa juisi ya malimao, sukari na chumvi
Chagua Jibu


29. Mtandao wa watu wenye virusi vya UKIMWI unatanuka kwa kuwa

 1.  matumizi ya kondom na simu za mkononi yameongezeka
 2.  matangazo kuhusu UKIMWI yameboreshwa
 3.  kuna ongezeko la mahusiano ya kingono yasiyo salama
 4.  elimu ya UKIMWI inatolewa kwa watu wachache
 5.  watu wenye UKIMWI wanazingatia kanuni za kujikinga na UKIMWI
Chagua Jibu


30. UKIMWI husambazwa kwa kupitia:

 1.  kusalimiana kwa kushikana mikono na mgonjwa wa UKIMWI
 2.  kulala chumba kimoja na mgonjwa wa UKIMWI
 3.  kuongea na mwathirika wa UKIMWI 
 4.  kuwekewa damu
 5.  kuosha nguo za mwathirika wa UKIMWI.
Chagua Jibu


31. Ili kuepuka kupata maambukizi mapya ya UKIMWI tunashauriwa:

 1.  kumeza dawa na kufanya mazoezi
 2.  kuwa mwaminifu na kuepuka ngono zembe
 3.  kuepuka kushirikiana na waathirika
 4.  kuepuka kula pamoja na kubadilishana nguo na waathirika 
 5.  kupata chanjo ya UKIMWI na Kifua Kikuu.
Chagua Jibu


32. Nini kati ya vifuatavyo husababisha chupa ya plastiki kusinyaa hewa inapoondoleua ndani?

 1.  Hewa ndani ya chupa kuwa na mgandamizo mkubwa zaidi ya hewa nje ya chupa
 2.  Hewa nje ya chupa kuwa na mgandamizo mkubwa kuliko hewa ndani ya chupa
 3.  Mgandamizo wa nje na ndani ya chupa kulingana
 4.  Mgandamizo wa hewa ndani ya chupa kuwa pungufu ya mngandamizo wa kutoa hewa nje ya chupa
 5.  Mgandamizo nje ya chupa kuwa sawa na ujazo wa hewa mdomoni.
Chagua Jibu


33. Chembe ndogo kabisa za maada zinazounda elementi na zinazohusika katika kutengenezz bondi za kikemikali huitwa:

 1.  molekyuli      
 2.  elektroni      
 3.  protoni
 4.  atomi                                     
 5.  nyutroni
Chagua Jibu


34.     Mwanga hupinda unapopita kutoka

 1.  Ncha ya Kaskazini kwenda Kusini      
 2.  media moja kwenda nyingine
 3.  Ncha ya Kaskazini kwenda Mashariki 
 4.  Magharibi kwenda Mashariki 
 5.  Kaskazini kwenda Magharibi
Chagua Jibu


35. Tazama kielelezo namba 3 kinachoonesha muundo wa atomi.


Je, ni herufi gani inayowakilisha elektroni?

 1.  T
 2.  S
 3.  R
 4.  Q
 5.  P
Chagua Jibu


36. Msuguano baina ya kifaa cha plastiki kama chana na nywele huzalisha:

 1.  oksijeni         
 2.  chaji za umeme
 3.  sumaku 
 4.  mfereji 
 5.  molekyuli za mafuta
Chagua Jibu


37.  Ipi kati ya alama zifuatazo inawakilisha atomi ya klorini?

 1.  K
 2.  P
 3.  Na
 4.  CI
 5.  H
Chagua Jibu


38.     Hewa ya kabonidaiyoksidi hutumika kuzima moto kwasababu:

 1.  haichochei uwakaji
 2.  ni nzito kuliko hewa
 3.  haiwaki
 4.  hunyonya joto
 5.  huungana na oksijeni
Chagua Jibu


39. Ipi kati ya zifuatazo ni kazi za sumaku?

 1.  Kutengeneza uga sumaku na kunyanyua mizigo
 2.  Kuzalisha umeme na kuunda dira
 3.  Hutumika katika vipaza sauti na hutengeneza uga sumaku
 4.  Kuvuta ncha ya kaskazini na kuzalisha umeme 
 5.  Kuonesha mwelekeo na kuundia spika.
Chagua Jibu


40.  Tafuta umbali kati ya mzigo na egemeo katika wenzo iwapo mzigo wa gramu 50, utanyanyuliwa kwa jitihadi ya Nyutoni 100 iliyo katika umbali wa sm 40 kutoka katika egemeo.

 1.  sm75 
 2. 1500 
 3.  sm 140        
 4.  sm 80   
 5.  sm 12.5
Chagua Jibu


41.  Aina kuu mbili za sakiti za umeme ni:

 1. mkondo geu na mnyoofu
 2. sambamba na mfuatano
 3.  mkondo geu na sambamba
 4. mkondo mnyoofu na mkondo geu
 5. mkondo mnyoofu na sambamba
Chagua Jibu


42. Mifupa imeundwa kwa madini ya:

 1. Sodiamu na kalsiamu
 2. Kalsiamu na oksijeni
 3. Fosforasi na kalsiamu 
 4.  Salfa na fosforasi
 5.  Kalsiamu na chuma 
Chagua Jibu


43.  Asidi ikiungana na besi huunda:

 1. chumvi na maji
 2. kaboneti ya sodiamu
 3. chumvi na besi
 4. maji na asidi
 5. chumvi na oksijeni
Chagua Jibu


44. Iwapo mashine yenye mzigo wa kgf 90 huhitaji jitihadi ya kgf 15, ni nini manufaa ya kimakanika?

 1.  15 
 2.  10   
 3.   8
 4.  6
 5.  5
Chagua Jibu


45.    Sumaku inaweza kuvuta vitu vyenye asili ya:

 1.  mpira     
 2.  udongo  
 3.  madini  
 4. karatasi 
 5. chuma
Chagua Jibu


46.Kitendo cha bakteria kuozesha kinyesi cha wanyama kwenye shimo pasipokuwa na hewa ya oksijeni husababisha:

 1.  joto kali 
 2.  gesivunde/biogesi
 3.  asidi kali               
 4.  alkali kali        
 5.  haidrojeni
Chagua Jibu


47.Je ni sehemu ipi ya jicho ambamo taswira hutengenezwa?

 1.  Irisi      
 2.  Lenzi    
 3.  Kano 
 4.  Filim    
 5.  Retina
Chagua Jibu


48.Katika kurunzi, nishati ya umeme inayotoka kwenye betri hubadilishwa na kuwa:

 1.  nishati ya kikemikali  
 2.  nishati ya joto
 3.  nishati ya kimakaniki     
 4.  nishati ya mwanga 
 5.  Nishati ya moto
Chagua Jibu


49.Nini maana ya dhanio katika utafiti wa kisayansi?

 1.  ni wazo tu
 2.  ni utabiri wa matokeo ya kubuni 
 3.  utabiri wa matokeo ya jaribio
 4.  wazo la kina       
 5.  mawazo yaliyojengwa kabla ya utafiti
Chagua Jibu


50.Mojawapo ya hatua za kufuata unapoandaa jaribio la kisayansi ni: 

 1.  uchunguzi    
 2.  udadisi
 3.  utambuzi wa tatizo    
 4.  utatuzi wa tatizo
 5.  kuandaa ripoti
Chagua Jibu


Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

Bofya Hapa Kupakua
App Ya Learning Hub Tanzania
GO TO NECTA EXAMS