STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2015

2015 -SAYANSI

Chaguajibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye karatariya kujibia.

1. Lipi kati ya makundi yafuatayo linawakilisha sifa za viumbe hai?

 1. Kufa, kula na kuona
 2. Kufa, kuzaa na kubadilika rangi 
 3. Kupumua, kuishi na kusikia 
 4. Kupumua, kuzaa na kutembea.
 5. Kujongea, kupumua na kuzaa.
Chagua Jibu


2. Mbegu chotara kwa wanyama na mimea ni bora kwa sababu gani?

 1. Hurefuka sana na hazihitaji mbolea.
 2. Hutoa mazao mengi na hustahimili magonjwa.
 3. Hukomaa haraka na hutoa mazao yenye uzito mkubwa. 
 4. Hazihitaji virutubisho na hustahimili magonjwa. 
 5. Hukomaa haraka na hazihitaji dawa.
Chagua Jibu


3. Lipi kati ya makundi yafuatayo ni sifa zinazotumika kutambua wanyama wa kundi la reptilia?

 1. Kutaga mayai, kuwa na damu baridi na kuishi majini. 
 2. Kutaga mayai, kuishi majini na kuishi nchi kavu.
 3. Kutaga mayai, kuwa na damu ya joto na kuishi nchi kavu.
 4. Kutaga mayai, kuwa na damu baridi na kupumua kwa kutumia mapezi.
 5. Kutaga mayai, kupumua kwa kutumia ngozi na kuishi majini.
Chagua Jibu


4. Damu huchukua oksijeni na kutoa kabondayoksaidi kupitia:

 1. Viribaehewa 
 2. Kuta za mapafu
 3. Koromeo
 4. Kapilari
 5. Pua
Chagua Jibu


5. Kukosekana kwa chanikiwiti katika mmea huweza kusababisha:

 1. mmea kukosa madini joto
 2. mmea kushindwa kusanisi chakula
 3. majani ya mmea kukauka 
 4. majani ya mmea kuwa njano
 5. maj ani ya mmea kupukutika.
Chagua Jibu


6. Fototropizimu ni kitendo cha mmea kuota kuelekea kwenye:

 1. mwanga 
 2. kani ya mvutano 
 3. maji 
 4. giza
 5. kemikali.
Chagua Jibu


7. Sehemu ya chembe hai inayohusika na kutawala shughuli zote za chembe hai huitwa:

 1. saitoplazimu 
 2. vakuoli
 3. kloroplasti 
 4. kiwambo cha seli
 5. nyukliasi
Chagua Jibu


8. Kielelezo kifuatacho kinaonyesha viumbe hai wenye sumu isipokuwa

 1.    
 2.    
 3.    
 4.    
 5.    
Chagua Jibu


9. Tendo Ia mimea kusafirisha maji kutoka kwenye mizizi hadi kwenye majani huitwa:

 1. osmosis 
 2. difyusheni 
 3. msukumo
 4. mgandamizo 
 5. mjongeo
Chagua Jibu


10. Ni tezi ipi kati ya zifuatazo huratibu utendaji wa tezi zingine zote katika mwili wa binadamu?

 1. Kongosho. 
 2. Pituitari
 3. Thairoidi
 4. Adrenali 
 5. Parathairoidi
Chagua Jibu


11. Sehemu ya kike ya ua inayohusika na uzazi ni:

 1. stameni 
 2. staili 
 3. ovari
 4. Petali
 5. Sepali
Chagua Jibu


12. Tofauti kati ya tunda na mbegu ni: 

 1. Mbegu ina tunda.
 2. Tunda huota.
 3. Tunda lina kotiledoni mbili. 
 4. Mbegu huota. 
 5. Mbegu haziliwi.
Chagua Jibu


13. Mambo muhimu kwa ajili ya afya na uhai ni:

 1. kucheza mpira wa miguu, kuoga, kufua nguo na kula sana.
 2. kula, kuwa msafi, kupumzika na kucheza.
 3. kufanya mazoezi, kula chakula bora, kupumzika na kuwa msafi.
 4. kula mayai, kuburudika, kulala na kusafisha mazingira.
 5. kuoga, kula na kulala.
Chagua Jibu


14. Vyakula vyenye kabohaidreti huwezesha mwili:

 1. kuhimili magonjwa
 2. kuwa na joto
 3. kukua kwa haraka 
 4. kuwa na nguvu 
 5. kuwa mwororo
Chagua Jibu


15. Kati ya yafuatayo ni yapi magonjwa yasiyoambukiza?

 1. Malaria, mafua na kisukari.
 2. Pumu, kisukari na kipindupindu.
 3. Kichocho, safura na matende
 4. Kuhara, homa ya matumbo na pumu
 5. Pumu, kifafa na tetekuwanga.
Chagua Jibu


16. Mapumziko baada ya kazi ni muhimu kwa sababu gani?

 1. Mwili hupoa. 
 2. Mwili hutulia.
 3. Mwili hurejesha nishati. 
 4. Mwili hufanya shughuli nyingine.
 5. Mtu hupata fursa ya kulala.
Chagua Jibu


17. Magonjwa yanayozuilika kwa kutumia chanjo ni :

 1. Pumu, kifaduro, malaria na kipindupindu 
 2. Kifua kikuu, malaria, pumu na surua
 3. Surua, dondakoo, kifua kikuu na kifaduro
 4. Malaria, surua, kifua kikuu na kipindupindu
 5. Dondakoo, kifua kikuu, UKIMWI na surua
Chagua Jibu


18. Wakazi wa Mlalo hula maharage, nyama na wali kwa afya zaidi wanahitaji kuongeza:

 1. samaki 
 2. mboga za majani
 3. kuku
 4. mkate
 5. kunde
Chagua Jibu


19. Kipi kati ya vifuatavyo kinaweza kupungua mwilini kwa kushiriki katika michezo na mazoezi?

 1. Sukari 
 2. Protini 
 3. Sumu
 4. Uchafu 
 5. Fati
Chagua Jibu


20. Kipi kati ya vifuatavyo siyo njia sahihi ya kujikinga na ugonjwa wa malaria?

 1. Kufyeka nyasi 
 2. Kufukia madimbwi
 3. Kutumia chandarua 
 4. Kupuliza dawa
 5. Kuchoma moto taka
Chagua Jibu


21. Mazoezi ni njia mojawapo ya kupunguza:

 1. kutapika 
 2. kuzirai 
 3. kukaza kwa misuli 
 4. kuharisha
 5. kutokwa na damu puani
Chagua Jibu


22. Mtoto mwenye matege amepungukiwa na vitamini:

 1. K
 2. D
 3. A
 4. B
 5. C
Chagua Jibu


23. Ukosefu wa vitamini B husababisha ugonjwa wa:

 1. uti wa mgongo
 2. vidonda vya tumbo
 3. surua 
 4. trakoma 
 5. beriberi
Chagua Jibu


24. Faida mojawapo ya vyakula vya protini katika miili yetu ni:

 1. kukinga dhidi ya magonjwa 
 2. kukua na kukarabati chembe hai
 3. kutia nguvu 
 4. kuongeza uzito 
 5. kutia joto
Chagua Jibu


25. Huduma ya kwanza ni nini?

 1. Msaada wa dharura apewao mgonjwa na daktari.
 2. Msaadawa awali apewao mgonjwa kabla ya kupelekwa hospitali.
 3. Msaada kwa ajili ya mtu aliyeungua moto. 
 4. Msaada kwa ajili ya mtu aliyeumwa na nyoka. 
 5. Msaada kwa ajili ya mtu aliyevunjika mfupa.
Chagua Jibu


26. Mojawapo ya huduma ya huduma muhimu ya kumpa mtu aliye ungua moto ni;-

 1. kummwagia maji
 2. kumfunika nguo
 3. kumwagia asidi
 4. kumfunika blanketi
 5. kumpaka asali
Chagua Jibu


27. Mojawapo ya athari za kupaka mafuta kwenye jeraha la moto ni:

 1. kuongeza joto kwenye jeraha
 2. kuongeza maumivu kwenye jeraha
 3. kuruhusu hewa kupita kwenye jeraha 
 4. kusababisha vijidudu kuingia kwenye jeraha 
 5. kuongeza malengelenge.
Chagua Jibu


28. Ni hoja ipi kati ya zifuatazo iko sahihi kuhusu WU na UKIMWI? 

 1. Kuwa na WU ni sawa na kuwa na UKIMWI
 2. Chanzo cha WU na UKIMWI ni magonjwa ya zinaa. 
 3. Ni rahisi kujikinga na UKIMWI kuliko VVU.
 4. Ukiepuka maambukizi ya VVU pia umeepuka UKIMWI.
 5. Mtu mwenye WU hana chembe nyeupe za damu.
Chagua Jibu


29. Moja ya vimelea vinavyoharibu chembe hai nyeupe za damu ni:

 1. Bakteria 
 2. WU 
 3. Plasmodiamu 
 4. Amiba 
 5. Kuvu
Chagua Jibu


30. Kipi kati ya vifuatavyo ni maarufu kwa kuchangia maambukizi ya WU katika jamii?

 1. Uchangiaji wa sindano, miswaki, damu na ngono zembe. 
 2. Kanda za video, nyimbo, muziki na maigizo. 
 3. Televisheni, magazeti na vipeperushi kuhusu WU.
 4. Kondomu, wataalamu wa afya, semina na taasisi za UKIMWI.
 5. Tohara kwa wanaume na wanawake.
Chagua Jibu


31. Virusi Vya Ukimwi hushambulia aina gani ya chembe hai katika damu?

 1. chembe sahani 
 2. chembe hai nyeupe
 3. Chembe hai nyekundu 
 4. Hemoglobini
 5. Plazima
Chagua Jibu


32. Unaweza kupata sukari kutoka katika majimaji ya miwa kwa:

 1. kuchemsha kisha kuyachuja 
 2. kuchemsha kisha kuyapooza 
 3. kupooza na kugandisha 
 4. kuchemsha hadi kuvukiza
 5. kuyaweka kwenye mwanga wa jua.
Chagua Jibu


33. Mtu anapokata mti kwa mbali unaona shoka likikita kwenye gogo la mti na baada ya muda kishindo hufuata. Hii inaonesha kuwa:

 1. mwanga husafiri katika mstari ulionyooka
 2. sauti husafiri polepole kuliko mwanga
 3. mwanga husafiri polepole kuliko sauti 
 4. sauti husafiri haraka kuliko mwanga
 5. sauti husafiri kwenye mstari ulionyooka.
Chagua Jibu


34. Kuna tofauti gani kati ya barafu na maji? 

 1. Maji ni mazito kuliko barafu.
 2. Maji yana mshikamano mkubwa kuliko barafu.
 3. Maji yana rangi hafifu kuliko barafu.
 4. Maji yanachukua nafasi ilihali barafu haichukui nafasi.
 5. Barafu ni laini kuliko maji.
Chagua Jibu


35. Mabadiliko ya maada yasiyosababisha mabadiliko katika uzito yanajulikana kama :

 1. mabadiliko ya kikemikali 
 2. mabadiliko ya kiumbo 
 3. mabadiliko ya ujazonene
 4. mabadiliko ya hali
 5. mabadiliko ya asili.
Chagua Jibu


36. Myeyuko wa majivu yaliyotokana na majani ya malimao huweza kubadili rangi ya karatasi ya litmasi ya:

 1. bluu kuwa nyeupe
 2. nyekundu kuwa bluu
 3. bluu kuwa nyekundu
 4. bluu kuwa kijani
 5. nyekundu kuwa njano. 
Chagua Jibu


37. Mchanganyiko wa gesi mbalimbali kwa pamoja huitwa

 1. oksijeni 
 2. haidrojeni 
 3. hewa 
 4. naitrojeni 
 5. maada.
Chagua Jibu


38. Lipi kati ya yafuatayo siyo badiliko la kikemikali?

 1. Kuoza kwa takataka 
 2. Kuchacha kwa maziwa 
 3. Kuungua kwa mkaa 
 4. Kuyeyuka kwa sukari 
 5. Chuma kupata kutu.
Chagua Jibu


39. Ipi kati ya jozi zifuatazo ni sahihi kuhusu lenzi? 

 1. Lenzi mbinuko hutawanya miale ya mwanga.
 2. Lenzi mbonyeo hurekebisha kutokuona karibu.
 3. Lenzi mbinuko hurekebisha kutokuona mbali. 
 4. Lenzi mbonyeo kurekebisha kutokuona mbali.
 5. Lenzi mbonyeo hukusanya miale ya mwanga.
Chagua Jibu


40. Matumizi ya roda katika maisha ya kila siku ni:

 1. kunyanyua vitu vizito 
 2. kufungua vizibo vya chupa 
 3. kufunga vitu 
 4. kupunguza mwinuko
 5. kurahisisha kukata kuni.
Chagua Jibu


41. Tazama alama kwenye kielelezo kifuatacho kwa makini, kisha zipe majina kwa kuzingatia zilivyopangwa kutoka upande wa kushoto.

 1. Kapasita, dynamo, seli kavu, swichi, betri
 2. Swichi, glopu, kikinza, kapasita, seli kavu 
 3. Glopu, kapasita, seli kavu, kikinza, betri 
 4. Kikinza, glopu, swichi, seli kavu, kapasita
 5. Swichi, kikinza, glopu, seli kavu, kapasita.
Chagua Jibu


42. Ni kifaa gani hutumika kukuza taswira ya vionwa vidogo sana?

 1. Darubini 
 2. Hadubini 
 3. Periskopu
 4. Prizimu 
 5. Lenzi
Chagua Jibu


42. Ni kifaa gani hutumika kukuza taswira ya vionwa vidogo sana?

 1. Darubini 
 2. Hadubini 
 3. Periskopu
 4. Prizimu 
 5. Lenzi
Chagua Jibu


44. Kipi kati ya vifuatavyo hakipitishi mkondo wa umeme?

 1. Mpira 
 2. Bati
 3. Shaba
 4. Chuma 
 5. Zebaki
Chagua Jibu


44. Kipi kati ya vifuatavyo hakipitishi mkondo wa umeme?

 1. Mpira 
 2. Bati
 3. Shaba
 4. Chuma 
 5. Zebaki
Chagua Jibu


46. Alama zifuatazo zinatumika katika sakiti ya umeme. Je, ni alama ipi inawakilisha kikinza?

Chagua Jibu


47. Kanuni sahihi ya kutafuta kiasi cha kazi kilichofanyika ni: 

 1. Kazi = kani x uzito
 2. Kazi=Umbali / Muda
 3. Kazi=Kani / Muda
 4. Kazi=Kani x Umbali
 5. Kazi=Umbali / Kani
Chagua Jibu


48. Taswira za sura zetu zinaweza kuonekana vizuri tunapotumia:

 1. kioo mbinuko
 2. kioo mbonyeo 
 3.  kioo bapa
 4. lenzi mbinuko 
 5. lenzi mbonyeo
Chagua Jibu


49. Ni muhimu kuweka kumbukumbu za jaribio lililofanyika kwa sababu hutumika:

 1. kama rejea
 2. kutangaza umahiri wa aliyefanya jaribio
 3. kuchora jedwali Ia matokeo
 4. kurekebisha taarifa mbalimbali 
 5. katika kuleta maendeleo
Chagua Jibu


50. Data za uchunguzi zilizochambuliwa huweza kuwasilishwa kwa njia ya:

 1. grafu 
 2. ripoti 
 3. kukokotoa
 4. kutafsiri 
 5. kuchora
Chagua Jibu


31. Utafutaji wa njia ya kwenda India ulifadhiliwa na

 1. Vasco Da Gama 
 2. Bartholomew Diaz 
 3. Cecil Rhodes
 4. King Henry 
 5. Henry Stanley.
Chagua Jibu


32. Soko kuu la watumwa Afrika Mashariki lilikuwa 

 1. Zanzibar 
 2. Mombasa
 3. Kilwa
 4. Bagamoyo
 5. Nairobi
Chagua Jibu


SEHEMU C

JIOGRAFIA

Chaguajibu sahihi kisha andika herufiyake kwenye karatariya kujibia.

33.  Nchi ya Japan ina uwezo wa kufanya biashara kuliko Tanzania kwa sababu ina ...

 1.  watu wengi zaidi 
 2. eneo kubwa la biashara
 3. shule nyingi za biashara
 4. teknolojia ya juu zaidi
 5. wafanyabiashara wengi zaidi.
Chagua Jibu


34.  Mchoro mkato wa ramani huonesha..

 1. mazao na mazingira
 2. sura ya nchi 
 3. mazingira ya eneo husika
 4. hali ya hewa 
 5. makazi ya watu na shughuli za kiuchumi
Chagua Jibu


35.  Mlima mrefu kuliko yote barani Afrika ni .....

 1. Drakensburg 
 2. Everesti 
 3. Atlasi 
 4. Kenya 
 5. Kilimanjaro
Chagua Jibu


36.  Moja kati ya zifuatazo ni sifa za picha: .....

 1. Kimo halisi huonekana.
 2. Sehemu zake zote huonekana.
 3. Umbo linaweza kupunguzwa au kuongezwa. 
 4. Rangi halisi ya kitu haionekani.
 5. Rangi ya picha haiwezi kubadilishwa.
Chagua Jibu


37.  Kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari kutokana na kuyeyuka kwa barafu katika ncha za kaskazini na kusini kunaweza kusababisha....

 1.  wavuvi kuzama baharini 
 2. uharibifu wa maeneo ya pwani
 3. upungufu wa samaki 
 4. mvua za El-nino
 5. kutokea kwa tsunami.
Chagua Jibu


38.  Ikiwa ni saa 12:00 jioni Tanzania ambayo ipo nyuzi 45 Mashariki, itakuwa saa ngapi Rwanda ambayo ipo nyuzi 30 Mashariki?

 1. 1:00 usiku 
 2. 2:00 usiku 
 3. 11:00 jioni 
 4. 12:00 jioni 
 5. 10:00 jioni.
Chagua Jibu


39.  Madhara gani kati ya yafuatayo yanatokana na mlipuko wa volkeno? ...

 1. Kuharibika kwa miundo mbinu
 2. Kupungua kwa eneo la kilimo. 
 3. Ongezeko la maradhi ya ngozi. 
 4. Ongezeko la mvua za El-nino. 
 5. Kuongezeka kwa ukame
Chagua Jibu


40.  Nchi ipi ni maarufu kwa uundaji wa meli duniani? .

 1. Urusi.
 2. Uingereza.
 3. Japani. 
 4. Ufaransa.
 5. Canada.
Chagua Jibu


Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

Bofya Hapa Kupakua
App Ya Learning Hub Tanzania
GO TO NECTA EXAMS