STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2014

2014 - SAYANSI

Chagua herufi ya jibu lililo sahihi, kisha andika katika karatasi ya majibu/kujibia

1.  Lipi kati ya magonjwa yafuatayo husambazwa na inzi na mende? 

 1. Tetekuwanga   
 2. Kuhara        
 3. Kifaduro
 4. Utapia mlo 
 5. Homa ya matumbo
Chagua Jibu


2. ?pi kati ya yafuatayo sio sehemu ya mfumo wa damu?

 1.  Bronchiole        
 2.  Valvu                
 3.  Auriko 
 4.  Capillari              
 5.  Ateri
Chagua Jibu


3. Lipi kati ya yafuatayo linapaswa kuzingatiwa kabla ya kumhudumia mgonjwa wa UKIMWI?

 1.  Vaa nguo safi 
 2.  Nawa kwa sabuni 
 3.  Vaa glovu 
 4.  Sali 
 5.  Mruhusu apumzike
Chagua Jibu


4.  ?pi kati ya yafuatayo ni ?ifa ya maji safi na salama?

 1.  Yametekwa kwenye kisima.
 2.  Yamehifadhiwa na kupoozwa kwenye mtungi wa maji
 3.  Yamechujwa na kuhifadhiwa kwenye chombo safi
 4.  Yamechemshwa, yamechujwa na kuhifadhiwa kwenye chombo safi
 5.   Yasiwe na magadi mengi
Chagua Jibu


5. Upi kati ya magonjwa yafuatayo hauna chanjo?

 1. Kifua kikuu 
 2.  Pepopunda 
 3. Surua
 4.  Kifaduro        
 5. Trakoma
Chagua Jibu


6. Gesi inayotumiwa na mimea kutengeneza protini ni:

 1. carbondayoksaidi
 2. haidrojen
 3. oksijen
 4.  naitrojen                                         
 5.  gesi asilia
Chagua Jibu


7. Kiwango cha maji kinachopotezwa na mmea huathiriwa na hali za hewa zifuatazo...

 1.  joto na unyevu     
 2.  unyevu na mwanga
 3. upepo na mwanga wa jua               
 4.  mawingu na upepo
 5. unyevu na upepo
Chagua Jibu


8. Tunaweza kusababisha mmomonyoko wa ardhi kwa kufanya mojawapo ya mambo yafuatayo:

 1. Kukata miti
 2. Kuongeza mbolea kwenye udongo
 3. Kuotesha nyasi 
 4.  Kuweka matuta lavenye maeneo ya mteremko
 5.  Kupanda miti 
Chagua Jibu


9. Shughuli za mwanadamu kama kilimo, ufugaji wa wanyama na uchimbaji madini vyote hutegemea:

 1.  mito 
 2. chemchemi 
 3.  ardhi 
 4.  umwagiliaji 
 5.  upepo
Chagua Jibu


10.  Kinyonga hujibadili rangi yake ili:

 1.  kutafuta chakula         
 2.  kupumua          
 3.  kuzaliana
 4.  kutafuta maadui                          
 5.  kujilinda dhidi ya maadui
Chagua Jibu


11. Mende hupitia hatua kuu ......... katika ukuaji wake?

 1. mbili                                                                     
 2. tatu
 3. nne
 4. tano                                               
 5. sita
Chagua Jibu


12. Yupi kati ya wanyama wafuatao hana uti wa mgongo?

 1.  Buibui
 2.  Popo
 3.  Paka
 4.  Mwanadamu
 5.  Kuku
Chagua Jibu


13. Mojawapo ya kazi ya misuli katika mwili ni:

 1.  kuzuia kutokwa damu 
 2.  kuwezesha mwendo
 3.  kutengeneza selihai nyeupe      
 4.  kushikilia meno mahali pake 
 5.  kuiwezesha kunyooka
Chagua Jibu


14. Viungo katika mifupa huwezesha .........

 1.  kuzuia mifupa kuvunjika        
 2.  mifupa iwe ya sawa
 3.  kurahisisha kujongea 
 4.  kuupa mwili umbo 
 5.  mifupa kunyooka
Chagua Jibu


15. ..... hupinda unapopita kutoka maada ya aina moja kwenda nyingine.

 1.  Upinde wa mvua        
 2.  Mistari sambamba
 3.  Miale ya mwanga                                    
 4.  Lenzi                               
 5.  Mwale na lenzi
Chagua Jibu


16. Mionzi ambayo hupinda zaidi mwanga unapopinda ni ile ya . ....

 1.  rangi nyekundu 
 2.  njano 
 3.  bluu iliyoiva 
 4.  bluu      
 5.  zambarau
Chagua Jibu


17.   Tazama mchoro ufuatao unaoonesha sehemu za ndani za mbegu ya haragwe....

Ni sehemu ipi inayohusika na kuilinda mbegu isiharibiwe na wadudu waharibifu mabadiliko ya jotoridi? 

 1. 2
 2. 3
 3. 5
 4. 4
 5. 1
Chagua Jibu


18. Anga huonekana la rangi ya bluu kwasababu .

 1.   hewa na maji ny vya rangi ya bluu
 2.   rangi nyekundu inatawanywa zaidi kuliko rangi ya bluu
 3.   uwezo wa kuona hupungua
 4.   rangi ya bluu hutawanywa zaidi ya rangi nyingine
 5.   wakati wa mawio jua huonekna kama la manjano
Chagua Jibu


19. Kipi kati ya vifuatavyo hakitumii sumaku?

 1. Kipaza sauti 
 2. Simu ya mezani
 3. Redio
 4.  Simu ya mkono 
 5. Pasi
Chagua Jibu


20. Kipimio cha kazi ni:

 1. kilogramu   
 2. Newton
 3. Tani
 4.  Joule  
 5. Gramu
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  
Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256