STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2013

SAYANSI 2013

Chaguajibu sahihi kisha andika herufiyake kwa kila swali.

1. Ni sehemu zipi za mwili zinahusika na utoaji wa takamwili?

  1. Ngozi na figo 
  2. Tumbo na figo
  3. Bandama na ini 
  4. Ini na tezi 
  5. Mapafu na moyo
Chagua Jibu


2. Kundi lipi limeainisha wanyama wenye uti wa mgongo?

  1. Konokono, mjusi na kenge
  2. Papasi, panzi na mbungo 
  3. Chura, mamba na mchwa
  4. Kuku, popo na bata 
  5. Nyoka, panzi na mbuzi
Chagua Jibu


3. Endapo mito na mabwawa yatakauka, ni viumbe hai Vipi kati ya vifuatavyo vitaathirika zaidi?

  1. Vyura
  2. Samaki 
  3. Mamba
  4. Mbu
  5. Nyoka
Chagua Jibu


3. Endapo mito na mabwawa yatakauka, ni viumbe hai Vipi kati ya vifuatavyo vitaathirika zaidi?

  1. Vyura
  2. Samaki 
  3. Mamba
  4. Mbu
  5. Nyoka
Chagua Jibu


5. Ni sehemu ipi ya ua hupokea mbegu za kiume?

  1. Stigma 
  2. Staili 
  3. Testa
  4. Ovyuli
  5. Petali
Chagua Jibu


6.   Uhusiano uliopo kati ya viumbe hai na visivyo hai katika mazingira unaitwa

  1. kutegemeana 
  2. wando chakula 
  3. ikolojia 
  4. mlishano 
  5. mizania asili.
Chagua Jibu


7. Ni Vipi kati ya viumbe hai vifuatavyo hujitengenezea chakula chao kwa kutumia klorofili?

  1. Wadudu
  2. Mimea 
  3. Wanyama 
  4. Virusi 
  5. Ndege
Chagua Jibu


8. Tezi inayodhibiti matendo ya ukuaji wa mwili na kulinda mwili dhidi ya magonjwa huitwa

  1. kongosho 
  2. adrenalini
  3. pituitari 
  4. thairoidi 
  5. gonadi
Chagua Jibu


9. Wanyama wenye uwezo wa kuishi majini na nchi kavu ni wale wa kundi la

  1. Ndege
  2. Amfibia
  3. Reptilia
  4. Samaki
  5. Mamalia
Chagua Jibu


10. Maji safi na salama ni maji ambayo

  1. hayana rangi yoyote 
  2. yamepoozwa kwenye mtungi
  3. yamechotwa bombani 
  4. yamechotwa kisimani
  5. yamechemshwa na kuchujwa
Chagua Jibu


11. Ugonjwa wa kipindupindu ni hatari sana kwa binadamu kwa kuwa

  1. huenezwa kwa njia ya hewa
  2. hujitokeza wakati wa masika tu
  3. husababisha mwili kupoteza maji
  4. hauna tiba wala kinga
  5. chanzo chake halisi bado hakijulikani
Chagua Jibu


12. Mwanafunzi wa Darasa la Sita alipumulia hewa ndani ya neli jaribio yenye myeyuko usiokuwa na rangi, kisha akatikisa neli jaribio hiyo. Baada ya kuitikisa myeyuko ulionekana kuwa na rangi nyeupe. Je, kemikali gani ilikuwa kwenye myeyuko usiokuwa na rangi?

  1. Asidi ya haidrokloriki
  2. Salfa
  3. Asidi ya salfyuriki 
  4. Haidrojeni 
  5. Haidroksaidi ya kalsiamu
Chagua Jibu


13. Homoni inayodhibiti sukari katika mwili wa binadamu huitwa.

  1. amilesi
  2. glukozi 
  3. insulini 
  4. ayodini 
  5. pepsini
Chagua Jibu


14. Himoglobini katika chembe chembe nyekundu za damu inafanya kazi gani?

  1. Kupambana na bakteria 
  2. Kusafirisha oksijeni mwilini 
  3. Kusafirisha takamwili 
  4. Kubeba vimengenyo vya chakula
  5. Kusambaza taarifa mwilini.
Chagua Jibu


15. Ili kuimarisha mifupa na meno, mtoto anahitaji

  1. kalsiamu, sodiamu na ayani
  2. wanga, mafuta na protini
  3. vitamin A, wanga na matunda
  4. vitamin A, kalsiamu na fosforasi
  5. mayai, matunda na wanga
Chagua Jibu


16. Ugonjwa unaosababishwa na bakteria aina ya basili ambao hushambulia mapafu huitwa

  1. kifaduro 
  2. surua 
  3. kichocho 
  4. polio 
  5. kifua kikuu
Chagua Jibu


17. Ni magojwa yapi kati ya yafuatayo huitwa magojwa ya kuambukiza? 

  1. Surua, polio na kifaduro 
  2. Kifua kikuu, kisukari na saratani
  3.  Surua, matende na UKIMWI 
  4. Kifaduro, pumu na kikohozi kikali 
  5. Surua, malaria na kisukari.
Chagua Jibu


18. Kemikali inayotumika kubaini uwepo wa chakula aina ya wanga inaitwa.

  1. besi 
  2. asidi 
  3. spiriti 
  4. ayodini 
  5. chumvi
Chagua Jibu


19. Ingawa wanyama huvuta hewa ya oksijeni na kutoa hewa ya kabondayoksaidi, hewa hizi hazipungui wala kuongezeka kwenye mizazi kwa kuwa.

  1. oksijeni ipo kwa wingi kvvenye mizazi
  2. kabondayoksaidi hubadilika kuwa oksijeni
  3. mimea hutumia kabondayoksaidi na kutoa oksijeni
  4. kabondayoksaidi huathiri tabaka la ozoni
  5. oksijeni na kabondayoksaidi hurekebishwa na ozoni
Chagua Jibu


20. Vyakula vyenye mafuta vina umuhimu gani mwilini?

  1. Kujenga mwili 
  2. Kulinda mwili 
  3. Kuzuia maradhi
  4. kuupa mwili nguvu 
  5. kuupa mwili joto
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  




Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256