STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2012

SAYANSI - 2012

Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwa kila swali.

1. Ili kudumisha afya ya mwili, tunapaswa:

 1. kufanya mazoezi, kula chakula bora na kupumzika.
 2. kulala sana, kula chakula bora na kucheza.
 3. kutofanya kazi ngumu, kufanya mazoezi na kulala.
 4. kufanya mazoezi na kushiriki michezo
 5. kula vizuri na kufanya mazoezi muda wote.
Chagua Jibu


2.Ni kipi kati ya virutubisho vifuatavyo ni muhimu kwa mama mjamzito kupata kwa wingi?

 1. Protini.
 2. Kabohaidreti.
 3. Mafuta.
 4. Chumvichumvi.
 5. Vitamini.
Chagua Jibu


3.Kukojoa mara kwa mara, kutoa mkojo mwingi na kupata kiu mara kwa mara ni dalili za ugonjwa upi?

 1. Kansa.
 2. Kisukari.
 3. Kwashakoo.
 4. Kifaduro.
 5. Upungufu wa damu.
Chagua Jibu


4.Ni njia gani kati ya zifuatazo inafaa kumsaidia mtu aliyepata mshtuko uliotokana na kunaswa na waya wenye umeme?

 1. Kumsukuma kwa mikono haraka.
 2. Kuuvuta waya wa umeme uliomshtua. 
 3. Kutumia maji kuuzima umeme.
 4. Kumvuta kwa kutumia kifaa kisichopitisha umeme.
 5. Kumwacha mpaka umeme ukatike wenyewe.
Chagua Jibu


4.Ni njia gani kati ya zifuatazo inafaa kumsaidia mtu aliyepata mshtuko uliotokana na kunaswa na waya wenye umeme?

 1. Kumsukuma kwa mikono haraka.
 2. Kuuvuta waya wa umeme uliomshtua. 
 3. Kutumia maji kuuzima umeme.
 4. Kumvuta kwa kutumia kifaa kisichopitisha umeme.
 5. Kumwacha mpaka umeme ukatike wenyewe.
Chagua Jibu


6.  Ipi kati ya zifuatazo siyo dalili ya UKIMWI?

 1. Kuvimba kwa matezi
 2. Kupoteza uzito 
 3. Kuharisha kusikokoma
 4. Kikohozi cha muda mrefu kisicho cha kawaida.
 5. Kutoa jasho kusiko kwa kawaida wakati wa usiku.
Chagua Jibu


7.  Zifuatazo ni njia za kujikinga na majanga mbalimbali katika mazingira isipokuwa:

 1. kuchimba mahandaki
 2. kujenga nyumba mbali na milima ya volcano
 3. kuweka akiba ya chakula
 4. kuishi maisha ya kuhamahama
 5. kudumisha usafi katika mazingira
Chagua Jibu


8.  Ni ipi kati ya zifuatazo ni mchanganyiko wa gesi mbalimbali?

 1. Mwanga 
 2. Hewa
 3. Mafuta ya taa 
 4. Kabondayoksaidi 
 5. Mvuke
Chagua Jibu


9.  Ni lipi kati ya matendo yafuatayo siyo sababu ya uharibifu wa mazingira?

 1. Uchomaji wa karatasi
 2. Maendeleo ya viwanda
 3. Kuoga ziwani
 4. Kutumia mbolea ya samadi
 5. Kuoshea magari mtoni.
Chagua Jibu


10.  Mfalme wa porini aliamuru wanyama wote walao nyama wauawe. Unafikiri ni nini kitatokea porini baada ya miaka mingi?

 1. Mimea itaota kwa wingi
 2. Idadi ya wadudu haitabadilika 
 3. Mimea itapungua 
 4. Wanyama walao majani watapungua 
 5. Mazingira yatabaki katika hali nzuri ya kuvutia.
Chagua Jibu


11.  Kani za asili husababisha moja kati ya mambo yafuatayo katika mazingira:

 1. Kutoonekana kwa samaki
 2. Tetemeko la ardhi 
 3. Ongezeko la mimea 
 4. Upungufu wa umeme 
 5. Kukauka kwa mito.
Chagua Jibu


12.  Ipi kati ya zifuatazo siyo njia sahihi ya kuhifadhi rutuba ya udongo katika shamba?

 1. Kubadilisha mazao 
 2. Kupanda mimea jamii ya kunde. 
 3. Kupumzisha shamba. 
 4. Kutumia mbolea 
 5. Kupanda zao la aina moja mfululizo.
Chagua Jibu


13.  Chura hupitia hatua kuu ngapi katika kukua kwake?

 1. Moja 
 2. Saba 
 3. Sita 
 4. Tano 
 5. Nane.
Chagua Jibu


14.  Mdudu yupi kati ya hawa wafuatao hupitia metamofosisi isiyokamilika?

 1. Mbu 
 2. Kipepeo 
 3. Inzi 
 4. Nyuki 
 5. Mende
Chagua Jibu


15.     Panya aliyekuwa amefungiwa kwenye kisanduku kilichokuwa na kipande cha nyama alikufa baada ya siku mbili. Ni kitu gani kilisababisha panya huyo kufa?

 1. Alikula nyama iliyooza
 2. Alikosa hewa ya kabondayoksaidi 
 3. Alikosa hewa ya oksijeni.
 4. Alikosa maji ya kutosha baada ya kula nyama.
 5. Alikosa mwanga ambao ni muhimu kwa ukuaji wa wanyama.
Chagua Jibu


16.  Ni kiumbe yupi kati ya hawa wafuatao ni amfibia?

 1. Chura 
 2. Panya 
 3. Mjusi 
 4. Kobe 
 5. Kinyonga.
Chagua Jibu


17.  Wanyama kama mamba, viboko, vyura wanaishi katika maskani gani?

 1. Angani na ardhini
 2. Ardhini na majini. 
 3. Mazingira yoyote ilimradi chakula kiwepo
 4. Ardhini na mapangoni 
 5. Kwenye misitu.
Chagua Jibu


17.  Wanyama kama mamba, viboko, vyura wanaishi katika maskani gani?

 1. Angani na ardhini
 2. Ardhini na majini. 
 3. Mazingira yoyote ilimradi chakula kiwepo
 4. Ardhini na mapangoni 
 5. Kwenye misitu.
Chagua Jibu


19.  Kuna aina kuu mbili za mbegu za mimea ambazo ni:

 1. ghalambegu kuu na ghalambegu ndogo
 2.  monokotiledoni na daikotiledoni 
 3. daikotiledoni na kikonyo kikuu
 4. mbegu zenye mizizi na zisizo na mizizi.
 5. mbegu za asili na za porini.
Chagua Jibu


20.  Miale ya mwanga wa radi inaonekana kabla ya kusikia mngurumo wa radi kwa kuwa:

 1. miale ya mwanga haizuiwi na chochote 
 2. sauti husharabiwa kwanza na mawingu 
 3. mwanga husafiri haraka kuliko sauti.
 4. sauti husafiri haraka kuliko mwanga
 5. mawingu yanayotoa sauti husafiri polepole.
Chagua Jibu


21. Ukifua vitambaa viwili vya aina moja, kimoja cheupe na kingine cheusi, kile cheusl kitakauka haraka kuliko cheupe kwa sababu:

 1. kinasharabu joto kwa haraka 
 2. kinaakisi mwanga kwa haraka 
 3. kinafyonza unyevu haraka. 
 4. kinahimili upepo unaovuma.
 5. kina uwezo wa kuchuja maji.
Chagua Jibu


22. Ni lipi kati ya makundi yafuatayo linawakilisha vimiminika? 

 1. Hewa, maji na shaba
 2. Petroli, barafu na naitrojoni
 3. Dhahabu, haidrojeni na zebaki 
 4. Petroli, zebaki na maji
 5. Maji, petrol na hewa
Chagua Jibu


23.  Chunguza Kielelezo Na. 1 kisha jibu swali lifuatalo:

Kielelezo 1

Alama hii katika umeme huwakilisha:

 1.  ukizani 
 2. selikavu 
 3. voltimita
 4. swichi 
 5. glopu.
Chagua Jibu


24.  Akyumuleta ni muungano wa seli zilizoungwa pamoja na hutumika kutoa umeme mkondo mnyoofu kwa matumizi ya:

 1. baiskeli, pasi na simu
 2.  magari, matrekta na simu
 3. friji, pasi na feni
 4. baiskeli, friji na jiko la umeme.
 5. Seli kavu, jiko la mkaa na pasi
Chagua Jibu


25. Chunguza Kielelezo Na. 2 kinachoonesha watu wawili, P na Q wakiwa wanavuta mizigo yenye uzito sawa kupeleka juu ya paa, kisha jibu swali linalofuata.

Kielelezo 2 Ni yupi atakayevuta mzigo kiurahisi zaidi?

 1. P kwa sababu yuko chini. 
 2. Q kwa sababu atatumia nguvu kidogo 
 3. Q kwa sababu yuko juu ya paa 
 4. P kwa sababu roda ni moja 
 5. Q kwa sababu nguvu ya mvutano wa dunia ni kidogo.
Chagua Jibu


26. Uwezo wa kusogeza kitu kutoka sehemu moja kwenda nyingine huitwa:

 1.  usawa 
 2. kani 
 3. msuguano 
 4. kazi 
 5. gramu
Chagua Jibu


27. Penseli ikiwekwa kwenye glasi iliyo na maji inaonekana kama imepinda. Hii ni kwa sababu ya:

 1. kupinda kwa mwanga 
 2. kuakisiwa kwa mwanga
 3. kutawanyika kwa mwanga
 4. uwezo wa maji kupitisha mwanga 
 5. ujazonene wa maji
Chagua Jibu


28. Maziwa huweza kusindikwa na kutengenezwa kitu gani kati ya vifuatavyo?

 1. Jibini na sabuni
 2. Matunda na hamira 
 3. Siagi na matunda 
 4. Keki na siagi.
 5. Siagi na jibini.
Chagua Jibu


29. Vyanzo asilia vya nishati katika maisha ya kila siku ni:

 1. kuni, moto na maji 
 2. umeme, sumaku na gesi asili
 3. kuni, jua na upepo 
 4. moto, upepo na sumaku 
 5. umeme, upepo na maji
Chagua Jibu


30. Tazama Kielelezo Na. 3 kisha chagua jibu sahihi kuhusiana na jaribio hilo.

Lengo la jaribio katika Kielelezo Na. 3 ni kuonesha:

 1. Kuchemsha maji ya kunywa
 2. Kupoza maji
 3. Kutanuka na kusinyaa kwa hewa 
 4. Kupoza gesi
 5. Kutengeneza hewa ya oksijeni.
Chagua Jibu


31. Lipi ni badiliko la kiumbo?

 1. Kuchacha kwa maziwa
 2. Kuunguza karatasi
 3. Maji kuwa mvuke
 4. Pambano kati ya tindikali na nyongo 
 5. Mimea kuoza
Chagua Jibu


32. Chunguza Kielelezo Na. 4 kisha jibu swali linalofuata.

Lengo la jaribio katika Kielelezo Namba 4 ni kutafuta:

 1. ujazo wa kopo chirizi
 2. kiasi cha hewa katika kopo chirizi
 3. eneo la jiwe
 4. mzingo wa jiwe
 5. ujazo wa jiwe
Chagua Jibu


33. Ili kuzuia hatari zinazosababishwa na uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, kila Taifa linapaswa:

 1. kushirikiana na wanasayansi
 2. kuwa na Wizara ya Sayansi na Teknolojia
 3. kuondokana na uvumbuzi wa sayansi na teknolojia
 4. kuchukua uvumbuzi wa kiteknolojia toka nchi zilizoendelea
 5. kuweka sera zinazosimamia matumizi ya sayansi na teknolojia.
Chagua Jibu


34. Ipi kati ya yafuatayo hutumika kutabiri kuhusu tatizo katika uchunguzi wa kisayansi?

 1. kukusanya data
 2. dhanio
 3. kuchambua data
 4. hitimisho 
 5. kutoa maoni.
Chagua Jibu


35. Watu wanaopenda kwenda kwenye mwezi wanalazimika:

 1. kubeba kuni za kupikia chakula
 2. kubeba hewa ya oksijeni na chakula
 3. kuwa waangalifu na wanyama wakali
 4. kubeba kabondayoksaidi na chakula
 5. kubeba kabondayoksaidi na maji.
Chagua Jibu


36. Katika utafiti vipimo vya urefu wa mimea sita vimepatikana kama ifuatavyo: sm 12; sm 6; sm 20; sm 14; na sm 10. Wastani wa urefu huo ni:

 1. sm 12 
 2. sm 14
 3. sm 11 
 4. sm 13 
 5. sm 17
Chagua Jibu


37. Ateri kuu imegawanyika katika mishipa midogo midogo iitwayo:

 1.  venekava 
 2. bronchioli 
 3. valvu 
 4. kapilari 
 5. vena.
Chagua Jibu


38. Hemoglobini ni kampaundi inayopatikana ndani ya damu katika:

 1.  seli hai nyeupe 
 2. seli hai nyekundu
 3. ute wa damu 
 4. uroto wa njano katika mifupa
 5. seli zinazogandisha damu.
Chagua Jibu


39. Nini hutokea iwapo mbegu X ya kiume itaungana na mbegu X ya kike?

 1. Mapacha wasiofanana
 2. Mtoto wa kike
 3. Mapacha walioungana 
 4. Mtoto wa kiume 
 5. Mapacha wanaofanana.
Chagua Jibu


40. Ni ubongo wa mnyama yupi kati ya wafuatao umeundwa kiutaalamu zaidi kuliko wengine?

 1. Binadamu
 2. Farasi
 3. Sungura 
 4. Sokwe
 5. Nyani
Chagua Jibu


41. Kutu ni matokeo ya kuwepo kwa pambano Ia kikemikali lifuatalo:

CHUMA + Y +MAJI. Y inasimama badala ya:

 1. oksijeni 
 2. aside 
 3. naitrojeni 
 4. unyevu 
 5. kabondayoksaidi.
Chagua Jibu


42. Ni kipi kati ya vifuatavyo kimeundwa kwa chembe chembe ndogo sana?

 1. Gesi 
 2. Vimiminika
 3. Chembe za damu 
 4. Seli kavu 
 5. Maada
Chagua Jibu


43. Ni kipi kati ya vifuatavyo husababisha upungufu wa damu katika mwili wa binadamu?

 1. Ukosefu wa vitamini B
 2. Ukosefu wa ayani C. 
 3. Ukosefu wa kalsiamu 
 4. Ukosefu wa protini 
 5. Ukosefu wa fosfeti.
Chagua Jibu


44. Tunapopika mboga za majani tunashauriwa:

 1. kuweka magadi kidogo ili ziive vizuri
 2. kupika kwa muda mrefu ili kupunguza maji
 3. kuzifunika na kuzipika kwa muda mfupi
 4. kuzikausha kabla ya kuzipika
 5. kuzikaanga kwa mafuta mengi
Chagua Jibu


45. Ni yapi kati ya yafuatayo husababishwa na mwili kuwa na kabohaidreti nyingi kuliko inavyohitajika? 

 1. Kiribatumbo
 2. Utapiamlo
 3. Kwashakoo
 4. Unyafuzi
 5. Goita
Chagua Jibu


46. Katika jaribio lake, Shida alipitisha mwale wa mwanga katika kioo bapa kama inavyooneshwa kwenye Kielelezo Na. 5.

Kielelezo. 5 Pembe Y itakuwa na ukubwa wa nyuzi:

 1. 180
 2. 35
 3. 70
 4. 90 
 5. 105
Chagua Jibu


47. Msuguano husababisha nini kati ya yafuatayo?

 1. Kupumua
 2.  Kuogelea
 3. Kuwinda
 4. Kuzaliana 
 5. Kujificha
Chagua Jibu


49.Ni viumbehai vipi kati ya vifuatavyo huishi majini?

 1. Bakteria, virusi na kuvu
 2. Dagaa, pweza na bacteria
 3. Bakteria, virusi na pweza 
 4. Dagaa pweza na yungiyungi
 5. Bakteria, virusi na yungiyungi.
Chagua Jibu


49.Ni viumbehai vipi kati ya vifuatavyo huishi majini?

 1. Bakteria, virusi na kuvu
 2. Dagaa, pweza na bacteria
 3. Bakteria, virusi na pweza 
 4. Dagaa pweza na yungiyungi
 5. Bakteria, virusi na yungiyungi.
Chagua Jibu


50.Mbu aina ya kyuleksi husambaza minyoo inayoitwa filarial ambayo husababisha ugonjwa wa:

 1. pepopunda
 2. matende
 3. surua
 4. homa ya ini
 5. tetekuwanga
Chagua Jibu


MTIHANI WA SAYANSI DARASA LA IV 2012

SEHEMU A

Chagua jibu sahihi na andika herufi yake kwenye nafasi ya kujibia

1. Baadhi ya ajali na maafa yatokanayo na nguvu za asili ni . . . . . . . .

 1. mvua kubwa, umeme, kimbunga
 2. radi, kimbunga, mvua kubwa
 3. umeme, madaraja, kimbunga
 4. mitambo, mafuriko, miti
Chagua Jibu


2. Wanyama wanaokula nyama wana . . . . . . . . 

 1. pembe ndefu na kali
 2. mikia mipana na mifupi
 3. meno makali na kucha kali
 4. pembe kali na kucha kali
Chagua Jibu


3. Mbu wanaosambaza vimelea vya malari huuma. . . . . . . . 

 1. usiku tu
 2. mchana tu
 3. usiku na mchana
 4. usiku wa manane
Chagua Jibu


4. Zifuatazo ni njia za kumsaidia mtu aliyezirai isipokuwa. . . . . . . . 

 1. Mweke mgonjwa katika sehemu salama yenye hewa ya kutosha
 2. Inua miguu ya mgonjwa kuruhusu damu iende kichwani
 3. Mvue viatu na kulegeza mkanda wake
 4. Kama hapumui umwagie maji ya baridi mwili mzima
Chagua Jibu


5. Maji huganda katika nyuzijoto

 1. 100 oC
 2. 36 oC
 3. 0 oC
 4. 36.9 oC
Chagua Jibu


6. Milango ya fahamu in . . . . . . . .  katika uchunguzi

 1. udhaifu
 2. uhakika
 3. ubunifu
 4. tofauti
Chagua Jibu


7.  Mikono (mishikio) ya pasi na vikaangio hutengenezwa kwa mbao kwa sababu . . . . . . . 

 1. mbao hupendezesha pasi na vikaangio
 2. mbao ni kipitisho hafifu cha joto
 3. mbao huharibika haraka
 4. mbao ni kipitisho kizuri cha joto
Chagua Jibu


8. Kipi kati ya vifuatavyo ni chanzo kisicho cha asili cha mwanga? . . . . . . . . 

 1. Jua
 2. Radi
 3. Nyota
 4. Moto
Chagua Jibu


9. Ni aina gani ya nguo haitokani na viumbe hai? Ni nguo za . . . . . . . . 

 1. nailoni
 2. silki
 3. pamba
 4. sufu
Chagua Jibu


10. Rangi ya kijani katika mmea huitwa . . . . . . . . 

 1. usanisi
 2. umbijani
 3. usanisi nuru
 4. majani
Chagua Jibu


SEHEMU B

Jaza nafasi iliyoachwa wazi

11. Hewa iliyo katika mwendo huitwa . . . . . . . . 

Fungua Jibu


12. Joto kutoka kwenye moto hufikia ngozi zetu kwa njia ya . . . . . . . . 

Fungua Jibu


13. Taswira ni matokeo ya kioo . . . . . . . .

Fungua Jibu


14. . . . . . . . . kinasambazwa na konokono kutokana na kukojoa na kujisaidia haja kubwa kwenye vyanzo vya maji.

Fungua Jibu


15. Maji katika hali ya yabisi huitwa . . . . . . . . 

Fungua Jibu


16. Ncha za sumaku zinazotofautiana zikikaribiana . . . . . . . . 

Fungua Jibu


17. Mwanga unapotoka media moja kwenda nyingine nini hutokea? . . . . . . . . 

Fungua Jibu


SEHEMU C

Andika "Ndiyo" au "Hapana"

18. Hewa ya kaboni dayoksaidi inasaidia moto kuwaka . . . . . . . . 

Fungua Jibu


19.Chuma kinapopashwa moto hutanuka . . . . . . . . 


20. Chembe chembe hai nyeupe husaidia kulinda mwili dhidi ya magonjwa . . . . . . . . 

Fungua Jibu


SEHEMU B

Oanisha "Fnngu A" na "Fungu B" kwa kuweka herufi ya jibu sahihi

FUNGU A
FUNGU B
21. Sepali
22. Fagio
23. Minyoo
24. Mwangwi
25. Kapani
 1. Kitu kinachoruhusu kiasi kidogo cha mwanga kupenya
 2. Sehemu ya ua yenye rangi, huvutia wadudu na ndege
 3. Mashine rahisi daraja la tatu
 4. Sauti iliyo sharabiwa
 5. Sehemu ya ua yenye rangi ya kijani, hulinda ua
 6. Mashine rahisi daraja la pili
 7. Kula mboga na matunda yasiyooshwa
 8. Sauti iliyo akisiwa
 9. Kiti kinacho ruhusu mwanga kupenya
 10. Hupima uzito
 11. Kipima pembe
Fungua Jibu


Fungua Jibu


Fungua Jibu


Fungua Jibu


Fungua Jibu


Fungua Jibu


Fungua Jibu


Fungua Jibu


Fungua Jibu


Fungua Jibu


Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

Bofya Hapa Kupakua
App Ya Learning Hub Tanzania
GO TO NECTA EXAMS