STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2011

SAYANSI 2011

Chagua jibu sahihi na andika herufi inayohusika mbele ya namba ya kila swali katika karatasi ya kujibia.

1. Kifaa kinachotumika katika kuangalia sell za viumbehai huitwa:

 1. Darubini 
 2. Periskopu 
 3. Hadubini
 4. Kamera 
 5. Horoskopu
Chagua Jibu


2. Mlango wa fahamu unaotumika kutambua hali ya joto au baridi ni: 

 1. ulimi 
 2. sikio 
 3. jicho 
 4. pua 
 5. ngozi
Chagua Jibu


3. Ni yupi kati ya wafuatao ni mamalia?

 1. Njiwa 
 2. Kuku 
 3. Bata 
 4. Popo 
 5. Nyoka.
Chagua Jibu


4. Kielelezo Na. 1 kinaonesha mbegu yenye ghala mbili.

Kielelezo Na. 1

Katika Kielelezo Na. 1 sehemu inayoota na kuwa mzizi imeoneshwa kwa herufi ipi?
 1. H
 2. J
 3. K
 4. L
 5. M
Chagua Jibu


5. Kitu gani kitatokea endapo maua ya mmea wa mhindi yatanyofolewa?

 1. Mmea utastawi
 2. Mmea utakufa
 3. Mizizi ya mmea haitakua
 4. Majani yake yatageuka rangi
 5. Mmea hautazaa
Chagua Jibu


6. Muungano ufuatao ni muhimu kwenye utengenezaji wa kabohaidreti katika mimea:

 1. Oksijeni, klorofili na maji
 2. Kabondayoksaidi na maji
 3. Kabondayoksaidi, maji na mwanga wa jua
 4. Klorofili, maji na mwanga wa jua
 5. Klorofili, wanga na mwanga wa jua.
Chagua Jibu


7. Ni taka mwili zipi zitolewazo na mapafu?

 1. Oksijeni na maji
 2. Oksijeni na kabondayoksaidi
 3. Kabondayoksaidi na maji
 4. Kabondayoksaidi na chumvi
 5. Oksijeni na chumvi
Chagua Jibu


8. Kipi kati ya vifuatavyo husafirisha chavua kutoka katika stameni kwenda kwenye stigma? 

 1. Watu 
 2. Wadudu 
 3. Maji 
 4. Umande 
 5. Staili
Chagua Jibu


9. Mtu asiyekula matunda na mboga za majani huweza kupata matatizo ya:

 1. kuugua mara kwa mara
 2. kupunguza uzito wa mwili
 3. kuongezeka kwa hamu ya kula nyama
 4. rangi ya ngozi huwa njano
 5. kuongezeka uzito wa mwili.
Chagua Jibu


10. Mtoto mwenye kwashakoo ni yule aliyekosa chakula chenye: 

 1. vitamini 
 2. mafuta 
 3. madini 
 4. wanga
 5. Protini
Chagua Jibu


SAYANSI 2011

Chagua jibu sahihi na andika herufi inayohusika mbele ya namba ya kila swali katika karatasi ya kujibia.

1. Kifaa kinachotumika katika kuangalia sell za viumbehai huitwa:

 1. Darubini 
 2. Periskopu 
 3. Hadubini
 4. Kamera 
 5. Horoskopu
Chagua Jibu


2. Mlango wa fahamu unaotumika kutambua hali ya joto au baridi ni: 

 1. ulimi 
 2. sikio 
 3. jicho 
 4. pua 
 5. ngozi
Chagua Jibu


3. Ni yupi kati ya wafuatao ni mamalia?

 1. Njiwa 
 2. Kuku 
 3. Bata 
 4. Popo 
 5. Nyoka.
Chagua Jibu


4. Kielelezo Na. 1 kinaonesha mbegu yenye ghala mbili.

Kielelezo Na. 1

Katika Kielelezo Na. 1 sehemu inayoota na kuwa mzizi imeoneshwa kwa herufi ipi?
 1. H
 2. J
 3. K
 4. L
 5. M
Chagua Jibu


5. Kitu gani kitatokea endapo maua ya mmea wa mhindi yatanyofolewa?

 1. Mmea utastawi
 2. Mmea utakufa
 3. Mizizi ya mmea haitakua
 4. Majani yake yatageuka rangi
 5. Mmea hautazaa
Chagua Jibu


6. Muungano ufuatao ni muhimu kwenye utengenezaji wa kabohaidreti katika mimea:

 1. Oksijeni, klorofili na maji
 2. Kabondayoksaidi na maji
 3. Kabondayoksaidi, maji na mwanga wa jua
 4. Klorofili, maji na mwanga wa jua
 5. Klorofili, wanga na mwanga wa jua.
Chagua Jibu


7. Ni taka mwili zipi zitolewazo na mapafu?

 1. Oksijeni na maji
 2. Oksijeni na kabondayoksaidi
 3. Kabondayoksaidi na maji
 4. Kabondayoksaidi na chumvi
 5. Oksijeni na chumvi
Chagua Jibu


8. Kipi kati ya vifuatavyo husafirisha chavua kutoka katika stameni kwenda kwenye stigma? 

 1. Watu 
 2. Wadudu 
 3. Maji 
 4. Umande 
 5. Staili
Chagua Jibu


9. Mtu asiyekula matunda na mboga za majani huweza kupata matatizo ya:

 1. kuugua mara kwa mara
 2. kupunguza uzito wa mwili
 3. kuongezeka kwa hamu ya kula nyama
 4. rangi ya ngozi huwa njano
 5. kuongezeka uzito wa mwili.
Chagua Jibu


10. Mtoto mwenye kwashakoo ni yule aliyekosa chakula chenye: 

 1. vitamini 
 2. mafuta 
 3. madini 
 4. wanga
 5. Protini
Chagua Jibu


11.Konokono waishio majini hueneza ugonjwa uitwao:

 1. kichocho 
 2. Pepopunda
 3. kipindupindu 
 4. surua
 5. matende
Chagua Jibu


12. Mshipa mkuu unaotoa damu kwenye moyo unaitwa: 

 1. veini 
 2. aota 
 3. vena kavu 
 4. palmonari 
 5. hepatik.
Chagua Jibu


13. Homoni inayorekebisha uingiaji wa hewa ya oksijeni katika mfumo wa upumuaji katika mwili wa binadamu inaitwa.

 1. adrenalini 
 2. insulin 
 3. thairoksini 
 4. estrojeni 
 5. amilesi.
Chagua Jibu


14. Katika hali ya kawaida, tofauti kati ya hewa inayoingia na hewa inayotoka katika mwili binadamu ni kuwa hewa inayotoka ina wingi wa:

 1. Oksijeni 
 2. haidrojeni 
 3. maji
 4. naitrojeni 
 5. kabondayoksaidi.
Chagua Jibu


15. Ugonjwa wa rovu (goita) husababishwa na upungufu wa: 

 1. ayani 
 2. ayodini 
 3. kalsiamu 
 4. potasiamu 
 5. fosfeti
Chagua Jibu


16. Ugonjwa wa beriberi unasababishwa na upungufu wa vitamini: 

 1. B1 
 2. B2 
 3. A
Chagua Jibu


17. Samaki huvuta hewa kwa kutumia: 

 1. pua 
 2. mdomo 
 3. mapezi 
 4. matamvua 
 5. magamba
Chagua Jibu


18. Chakula kilichoyeyushwa katika utumbo mwembamba husambazwa mwilini kwa msaaaz wa:

 1. maji B.
 2. oksijeni 
 3. damu 
 4. difyusheni 
 5. kusharabu
Chagua Jibu


19. Chakula cha aina ipi kati ya vifuatavyo kinaweza kukarabati chembe hai za binadamu?

 1. Mafuta 
 2. Wanga 
 3. matunda 
 4. Protini 
 5. Madin_
Chagua Jibu


20. Uzazi wa mpango una umuhimu gani kwa familia?

 1. Huwezesha familia kumiliki nyumba
 2. Huongeza idadi ya watoto
 3. Huwezesha familia kumudu safari za pamoja
 4. Huwafanya wanafamilia kuwa na furaha
 5. Huwezesha familia kupata chakula cha kutosha.
Chagua Jibu


21. Huduma ya kwanza ni tiba inayotolewa kwa:

 1. mtu anayeugua ugonjwa unaojulikana.
 2. mtu baada ya kutoka hospital'
 3. lengo la kuonesha umahiri wa madaktari
 4. mgonjwa kabla hajapelekwa hospital'
 5. lengo la kutangaza kazi za Msalaba Mwekundu.
Chagua Jibu


22. Lengo la kupaka asali kwenye jeraha linalotokana na kuungua moto ni:

 1. kupunguza maumivu
 2. kuupa mwili nishati
 3. kutoa matibabu ya awali
 4. kuzuia uchafu usiguse kidonda
 5. kukinga na uambukizo wa tetanus.
Chagua Jibu


23. Mtu anayetapika hupatiwa nini kati ya yafuatayo kama huduma ya kwanza?

 1. Maziwa yaliyochemshwa
 2. Juisi iliyotokana na limao
 3. Myeyuko wa sukari na limao
 4. Myeyuko wa sukari na chumvi
 5. Kumpumzisha sehemu yenye baridi na ukimya.
Chagua Jibu


24. Ni vipi kati ya vifuatavyo ni muhimu kwa huduma ya kwanza kwa mtu aliyevunjika mfupa bila kupata jeraha?

 1. Mkasi, bandeji, vibanzi, uzi na shazia
 2. Taulo, sabuni, machela, pamba na spirits
 3. Taulo, maji, mafuta, vibanzi na sabuni
 4. Blanketi, kiti, sabuni, kamba na mkasi
 5. Blanket', bandeji, vibanzi, mkasi na kamba
Chagua Jibu


25. Nini kinatakiwa kifanyike baada ya kumhudumia mtu aliyeumia?

 1. Kupewa maji ya kunywa ya kutosha
 2. Kupelekwa hospital kwa matibabu zaidi
 3. Kulazwa chins na kupuliziwa pumzi mdomoni
 4. Kupumzishwa kwenye kivuli cha mti
 5. Kupewa mapumziko ya kulala wote.
Chagua Jibu


26. Protini huanza kumeng'enywa kikemikali kwenye:

 1. mdomo 
 2. tumbo 
 3. puru
 4. utumbo mpana 
 5. utumbo mwembamba.
Chagua Jibu


27. Huduma ya kwanza inayomfaa mtu aliyekunywa sumu ni:

 1. kumtapisha 
 2. kumpatia maziwa ya kunywa
 3. kumpatia dawa 
 4. kumpatia maji ya kunywa
 5. kumpatia glukozi.
Chagua Jibu


28. Maada inapatikana katika hail zifuatazo:

 1. Vimiminika, maji na gesi 
 2. Yabisi, vimiminika na hewa
 3. Yabisi, vimiminika na gesi 
 4. Mawe, yabisi na gesi
 5. Yabisi, hewa na gesi.
Chagua Jibu


29. Chumvi iliyomwagika kwenye ndoo ya maji inaweza kutenganishwa na maji hayo kwa kutumia njia ipi?

 1. Kuchuja mchanganyiko huo
 2. Kuchuja myeyuko huo
 3. Kuvukiza myeyuko huo
 4. kuchemsha mchangayiko huo
 5. Kuvukiza mchanganyiko huo.
Chagua Jibu


30. Katika utengenezaji wa sabuni, haidroksaidi ya sodiamu huchanganywa na mafuta yanayochemka. Endapo kemikali hiyo haipatikani maada ipi hutumka kama mbadala?

 1. Majivu ya majani
 2. Myeyuko wa limao
 3. Unga wa mhogo
 4. Mafuta ya nazi
 5. Maji ya majani ya mpapai
Chagua Jibu


31. Kuyeyuka kwa barafu ni badiliko la aina ipi?

 1. kikemikali 
 2. kiumbo
 3. Kimazingira
 4. kibayolojia 
 5. kifiziolojia
Chagua Jibu


32. Njia ya asili ya kurutubisha udongo ni:

 1. kuchanganya samadi na mbolea ya chumvichumvi
 2. kuchoma miti inayokausha vyanzo vya maji
 3. kuchoma majani na mabua ya mahindi
 4. kunguza idadi ya ng'ombe wanaochungwa
 5. kulima mazao ya jamii ya kunde kwa mbadilishano.
Chagua Jibu


33. Njia rahisi ya kugeuza maji magumu kuwa laini ni:

 1. kuyasafisha kwa dawa 
 2. kuyazimua
 3. kuyachemsha 
 4. kuyeyusha sehemu ngumu
 5. kuchuja maada ngumu.
Chagua Jibu


34. Ni vitu vipi kati ya vifuatavyo huweza kutenganishwa na sumaku?

 1. Unga wa ayani na mchanga
 2. Unga na vipande vya karatasi
 3. Pini za plastiki na mchanga
 4. Unga wa kioo na mchanga
 5. Mchanga na mchele
Chagua Jibu


35. Mabadiliko ya hali ya hewa na maji ni viambato vinavyosaidia:

 1. kufanya use wa ardhi uwe mzuri
 2. wanyama kumudu mazingira yao
 3. wanyama na mimea kuishi
 4. kuharakisha mmomonyoko wa udongo
 5. kusawazisha uhusiano wa mlishano.
Chagua Jibu


36. Gesi inayosaidia moto kuwaka ni:

 1. haidrojeni 
 2. naitrojeni
 3. ozoni
 4. gesi asilia 
 5. oksijeni.
Chagua Jibu


37. Chunguza kwa makini Kielelezo Na. 2 kisha jibu swali linalofuata.

Kielelezo Na. 2

Tafuta thamani ya X katika Kielelezo Na. 2.

 1. gm 250 
 2. gm 280 
 3. gm 437.5 
 4. gm 240 
 5. gm 175
Chagua Jibu


38. Kuta za ndani za flaski ya themosi zinapakwa rangi ya fedha ili kuzuia kupotea kwa joto kwa njia ya:

 1. mpitisho 
 2. kuakisi 
 3. msafara
 4. kupinda 
 5. mnururisho.
Chagua Jibu


39. Retina katika jicho ni sawa na kifaa gani kwenye kamera?

 1. Hama
 2. Lenzi
 3. Glopu
 4. Swichi 
 5. Fokasi.
Chagua Jibu


40. joto husafiri katika maada yabisi kwa njia ya:

 1. mpitisho 
 2. msafara
 3. mnururisho  
 4. mitetemo 
 5. kusharabu.
Chagua Jibu


41. Katika mashine manufaa ya kimekanika ni uwiano kati ya:

 1. kani egemeo na kani mzigo
 2. umbali lilipo egemeo na umbali ulipo mzigo
 3. kani mzigo na kani egemeo
 4. umbali ulipo mzigo na umbali lilipo egemeo
 5. kani iliyopo sehemu moja na kani iliyo sehemu nyingine.
Chagua Jibu


42. Bainisha kioo kinachotoa taswira wima inayofanana na kitu halisi na ambayo umbali kati ya kioo ni sawa na umbali kati ya kioo na kitu halisi:

 1. Kioo cha konkevu
 2. Kioo cha bikonkevu
 3. Kioo cha konveksi
 4. Kioo cha prismu
 5. Kioo bapa.
Chagua Jibu


43. Mkondo wa umeme katika sakiti ni ampia 2. Kama nguvu ya umeme ni volti 4, ukinzani katika sakiti hiyo ni:

 1. omu 3.5
 2. omu 4
 3. omu 2 
 4. omu 5
 5. omu 0.5.
Chagua Jibu


44. Chunguza sakiti ya umeme iliyooneshwa katika Kielelezo Na. 3 kisha jibu swali linalofuata.

Kielelezo Na. 3

Sakiti iliyooneshwa katika Kielelezo Na. 3 inalt­waje?

 1. Sakiti mfuatano
 2. Sakiti sambamba
 3. Sakiti kinzani
 4. Sakiti geu
 5. Sakiti pozo
Chagua Jibu


45. Magonjwa ya zinaa huambukizwa kwa njia ya:

 1. kugusana 
 2. kupeana damu
 3. kucheza pamoja 
 4. kuchangia vikombe
 5. kujamiiana
Chagua Jibu


46. Ni chembe chembe zipi za damu katika mwili wa binadamu hushambuliwa na VVU?

 1. Chembe nyekundu
 2. Chembe sahani
 3. Chembe nyeupe
 4. Chembe selimundu
 5. Chembe za plasma.
Chagua Jibu


47. Njia sahihi ya kujikinga na maambukizi ya VVU ni:

 1. kuacha kunywa pombe
 2. kuepuka kushiriki ngono zembe
 3. kushiriki mihadhara ya dini
 4. kusambaza dawa kwa waathirika
 5. kutangaza hadharani majina ya waathirika.
Chagua Jibu


48. Sentensi ipi kati ya zifuatazo ni sahihi kuhusu VVU na UKIMWI?

 1. VVU vinaenezwa na watu waliopevuka tu.
 2. Watu wanaoonekana kuwa na afya hawana VVU.
 3. VVU na UKIMWI huathiri watu wa rika zote.
 4. Wagonjwa wote wanaougua kansa wana VVU.
 5. Chanjo huzuia maambukizo dhidi ya VVU.
Chagua Jibu


49. Huduma inayotakiwa kwa watu wanaoishi na VVU ni:

 1. kuwapa nyumba za kuishi 
 2. kuwapa misaada ya fedha 
 3. kuwapa ushauri nasaha
 4. kuwapa elimu bure
 5. kuwafungulia akaunti benki.
Chagua Jibu


50. Katika uchunguzi wa kisayansi data hukusanywa kwa kutumia mbinu ya:

 1. kusafiri sehemu mbalimbali
 2. kusoma taarifa mbalimbali
 3. kubaini tatizo
 4. kuunda mabunio
 5. kufanya majaribio anuwai
Chagua Jibu


Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

Bofya Hapa Kupakua
App Ya Learning Hub Tanzania
GO TO NECTA EXAMS