STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2010

SAYANSI 2010

 SEHEMU A

Chagua jibu sahihi na kuandika herufi inayohusika mbele ya namba ya kilo swali katika karatasi ya kujibia.

1. Ipi kati ya zifuatazo si faida ya michezo kwa afya zetu?

 1. Husaidia kujenga misuli
 2. Huzuia mwili kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara
 3. Husababisha shinikizo la damu
 4. Huleta burudani
 5. Hudumisha afya ya mwili
Chagua Jibu


2. Maji yaliyochanganywa na sukari na chumvi ni huduma ya kwanza kwa mtu. anayesumbuliwa na

 1. Malaria na kuumwa kichwa
 2. Kuhara na kutapika 
 3. Uti wa mgongo na homa ya matumbo
 4. Kifua kikuu na mafua 
 5. Kuvunjika mguu au mkono
Chagua Jibu


3. Moja ya magonjwa yafuatayo si ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya zinaa

 1. UKIMWI 
 2. Trikomona
 3. Kaswende 
 4. Klamedia
 5. Trakoma
Chagua Jibu


4. Ni vitamin ipi kati ya zifuatazo hutengenezwa mwilini kwa kuwepo mwanga wa jua? 

 1. Vitamini A            
 2. Vitamini B
 3. Vitamini C 
 4. Vitamini D
 5. Vitamini E
Chagua Jibu


5. Chanjo ina manufaa gani kwa binadamu?

 1. Hupunguza maumivu 
 2. Huponyesha maradhi
 3. Huzuia magonjwa 
 4. Hurudisha vitamin na madini mwilini
 5. Hurudisha seli chakavu mwilini
Chagua Jibu


6. Ugonjwa wa kifua kikuu husababishwa na bacteria gani?

 1. Wote walioko hewani 
 2. Basili
 3. Plasimodiamu 
 4. Fungi 
 5. Amiha
Chagua Jibu


7. Viwanda havipaswi kujengwa karibu na makazi ya watu kwasababu

 1. ujenzi wake huchukua eneo kubwa
 2. sehemu kubwa ya taka za viwandani huwa na kemikali ambazo ni sumu
 3. mitambo ya viwandani hutoa sauti kubwa hivyo kuathiri ngoma za masikio
 4. viwanda husababisha watu kuhamahama makazi
 5. wenye viwanda hawaweki mazingira yao katika hall ya usafi
Chagua Jibu


8. Vitendo vifuatavyo huharibu vyanzo vya maji isipokuwa

 1. kukata miti
 2. kuchoma misitu
 3. kulisha wanyama wengi kupita kiasi kwenye vyanzo vya maji
 4. kutupa taka za kemikali katika vyanzo vya maji
 5. kuchota maji ya kupikia toka kwenye vyanzo vya maji
Chagua Jibu9. Asilimia kubwa ya uso wa dunia imefunikwa kwa maji. Sehemu kubwa ya maji haya hupatikana kwenye

 1. bahari 
 2. Mito 
 3. maziwa 
 4. mabwawa 
 5. madimbwi
Chagua Jibu


10. Mahali palipoinuka panafaa zaidi kujenga choo cha shimo kwasababu

 1. ni rahisi kujenga ukuta
 2. harufu itakuwa mbali na usawa wa ardhi
 3. si rahisi kuharibika upesi
 4. maji yatakuwa mbali na usawa wa choo chenyewe
 5. choo hakitafurika kwa muda mfupi
Chagua Jibu


11. Maji yanayobubujika kutoka ardhini hujulikana kwa jina gani?

 1. Bahari 
 2. Ziwa 
 3. Chemichemi 
 4. Bwawa 
 5. Mto
Chagua Jibu


12. Vitu muhimu katika uotaji wa mbegu ni

 1. udongo, mwanga wa jua na maji
 2. udongo, hewa na maji
 3. joto la kiasi, maji na hewa ya oksijeni
 4. joto la kiasi, udongo na mwanga wa jua
 5. maji, udongo na hewa ya kabonidayoksaidi
Chagua Jibu


13. Kundi la viumbe hai waishio majini na nchi kavu hujulikana kama

 1. Amfibia 
 2. Athropoda 
 3. Samaki 
 4. Ndege 
 5. Mamalia
Chagua Jibu


14. Kati ya viumbe wafuatao ni yupi si mamalia?

 1. Popo 
 2. Nyangumi 
 3. Simba 
 4. Sungura 
 5. Mamba
Chagua Jibu


15. Chunguza Kielelezo Namba 1 kwa makini kisha jibu swali lifuatalo

Kielelezo Na.1

Kiumbe aliyeoneshwa katika kielelezo Namba 1 huishi kwa kutegemea

 1. asali
 2. Nyama
 3. nafaka
 4. vyakula vya majini
 5. maada zilizooza
Chagua Jibu


16. Mmea uliochorwa katika kielelezo Namba 2 una sifa ya kuishi wapi?

Kielelezo Na. 2

 1. Kwenye misitu minene
 2. Majini
 3. Kwenye majani marefu
 4. Jangwani
 5. Milimani
Chagua Jibu


17. Kwanini baadhi ya mimea haipukutishi majani yake wakati wa masika?

 1. kuhifadhi maji yake 
 2. kuruhusu transipiresheni
 3. kuhifadhi chakula chake 
 4. kuhifadhi udongo
 5. kuufanya udongo uwe na rutuba
Chagua Jibu18, Mchoro katika kielelezo Namba 3 unaonesha picha ya ua

Kielelezo 3

Ni sehemu gani  ya ua huvutia wadudu kuja kulichavua

 1. 1
 2. 2
 3. 3
 4. 4
 5. 5
Chagua Jibu


 19. Umeme unaotolewa katika seli kavu, chanzo chake ni nishati gani?

 1. Jua
 2. Kimakanika
 3. Sauti
 4. Sumaku
 5. Kikemikali
Chagua Jibu


20. Kibata alitumia nyutoni 50 kusukuma ukuta kutwa nzima bila mafanikio. Je, lipi sahih: kutokana na tukio hilo?

 1. alitengeneza kazi 
 2. alitumia kani kubwa sana
 3. hakufanya kazi yoyote 
 4. alifanya kazi nzuri
 5. alitumia kani ndogo
Chagua Jibu


21. Endapo pembe mtuo itasomeka nyuzi 60, je pembe akisi itasomeka nyuzi ngapi kioo bapa?

 1.  90° 
 2.  40° 
 3.  30° 
 4.  60° 
 5.  45°
Chagua Jibu


22. Chunguza kielelezo Namba 4 kisha jibu swab linalofuata

Kielelezo 4

Ikiwa umeme unaopita katika sakiti hiyo ampi 5, kiasi cha ukinzani (R) wa waya katika sakiti hiyo ni omu              

 1. 100
 2. 50
 3. 10
 4. 4
 5. 0.4
Chagua Jibu23. Mzee Juakali mche wa sumaku hewani, Je, ncha ya kaskazini ya sumaku itaelekea upande gani wa dunia?

 1. Kusini 
 2. Kaskazini 
 3. Mashariki
 4. Magharibi 
 5. Kaskazini-mashariki
Chagua Jibu


24. Musa alitumia nyutoni 10 kusukuma mkokoteni umbali wa mita 5. Musa alifanya kazi - cha jouli ngapi?

 1. 15 
 2. 50 
 3. 0.5
 4. 5
Chagua Jibu


25. Katika uchunguzi wa kisayansi kitu gani kinachomfanya mtu kutabiri matokeo?

 1. Kufahamu tatizo 
 2. Kuchunguza kwa muda mrefu
 3. Kuona kwa macho 
 4. Kufanya jaribio
 5. Kugusa kitu
Chagua Jibu


26. Jaribio la kuotesha mbegu limeoneshwa katika Kielelezo Namba 5. Ni kitu gani muhimu kinakosekana kwa mbegu hiyo kuota?

 1. Maji 
 2. Hewa 
 3. Udongo 
 4. Mbolea 
 5. Upepo
Chagua Jibu


27. Milango ya fahamu inayotumika kutambua vitu katika majaribio ya kisayansi ni

 1. pua, macho, ngozi, ulimi na masikio
 2. pua, masikio, ngozi, miguu na ulimi
 3. masikio, ngozi, pua, miguu na mikono
 4. masikio, pua, ngozi, macho na mikono
 5. macho, miguu, ulimi, masikio na pua
Chagua Jibu


28. Data zifuatazo zimepatikana kwa kupima urefu kwa sm wa mimea mitano; 10, 12, 15, 28 na 40. Wastani wa urefu wa mimea yote kwa sm ni

 1. 22 
 2. 50
 3. 27
 4. 38 
 5. 21
Chagua Jibu


29. Kusudi kuu la kuzalisha mbegu mbalimbali ni lipi?

 1. Kupunguza urefu wa mimea 
 2. Kuongeza mazao ya mimea
 3. Kufanya mimea Hale haraka 
 4. Kupata mimea inayostahimili ukame
 5. Kuongeza urefu wa mimea
Chagua Jibu


30. Kati ya vifuatavyo nikipimo kipi kinapima urefu?

 1. Kilogramu 
 2. Sentimita 
 3. Rula 
 4. Volti 
 5. Ampia
Chagua Jibu


31. Umuhimu wa utando wa ozone ni

 1. kuongeza joto kwenye use wa dunia
 2. kupunguza mionzi hatarishi ya jua kutufikia
 3. kupunguza gesi ya kabonidayoksaidi angani
 4. kuongeza mvua duniani
 5. kupunguza baridi
Chagua Jibu


32. Sayari inayongfraa kuliko zote huitwa

 1. Zebaki 
 2. Dunia 
 3. Jupita 
 4. Pluto 
 5. Venasi
Chagua Jibu


33. Dunia hutumia siku ngapi kulizunguka jua?

 1. 3651 
 2. 28 
 3. 24 
 4. 12 
 5. 7
Chagua Jibu


34. Vitu vinavyofanya mfumo wa damu ni pamoja na

 1. moyo, seli hai nyeupe na damu
 2. seli hai nyeupe, self hai nyekundu na mishipa ya damu
 3. moyo, mapafu na damu
 4. seli hai za damu, maji na moyo
 5.  moyo, mishipa ya damu na damu
Chagua Jibu


35. Taka mwili zilizochujwa na figo husafirishwa kwenda kwenye kibofu kupitia mirija iitwayo 

 1. bronchioli
 2. Urethra  
 3. umio
 4. Ureta   
 5. falopia
Chagua Jibu36. Chunguza Kielelezo Namba 5 cha jino kisha jibu swab lifuatalo

Kielelezo Na. 5

Herufi Z kwenye kielelezo inawakilisha .............

 1. utando
 2. kichwa cha jino
 3. uvungu
 4. mshipa wa jino
 5. ufizi
Chagua Jibu


37. Sehemu gani ya moyo husukuma damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili?

 1. Auriko ya kushoto 
 2. Ventriko ya kushoto
 3. Auriko ya kulia 
 4. Ventriko ya kulia
 5. Vena kava
Chagua Jibu


38. hunguza kielelezo Namba 6 kisha jibu swali linalofuata

Sukari iliyowekwa katika bika iko katika hal. gani ya maada?

 1. Kimiminika
 2. Gesi
 3. Yabisi
 4. Elementi
 5. Kompaundi
Chagua Jibu


39. Chuma kupata kutu ni mfano wa badiliko gani?

 1. Kikemikali 
 2. Kiumbo
 3. Rangi
 4. Kimiminika 
 5. Tungamo
Chagua Jibu


40. Ni kundi lipi la vyakula linawakilisha vyakula vyenye vitamini A?

 1. Chungwa, ndimu, limau
 2. Karoti, maziwa, maini
 3. Chungwa, hamira, maharage
 4. Ndimu, Chungwa, maini
 5. Chagua Jibu


  31. Umuhimu wa utando wa ozone ni

  1. kuongeza joto kwenye use wa dunia
  2. kupunguza mionzi hatarishi ya jua kutufikia
  3. kupunguza gesi ya kabonidayoksaidi angani
  4. kuongeza mvua duniani
  5. kupunguza baridi
  Chagua Jibu


  42. Badiliko la maada lisilokuwa na tofauti katika uzito linaitwaje?

  1. Kikemikali 
  2. Kiugumu
  3. Kiumbo 
  4. Kiurefu
  5. Kiupana
  Chagua Jibu


  43. Unyafuzi ni utapiamlo unaosababishwa na

  1. upungufu wa madini ya kalsiamu na fosforasi
  2. kula kupita kiasi
  3. ukosefu wa ayadini mwilini
  4. ukosefu wa protini
  5. ukosefu wa vyakula vinavyotia mwili nishati na joto
  Chagua Jibu


  44. Ni viini lishe gani vinavyopatikana katika vyakula vya kujenga mwili?

  1. Protini 
  2. Kabohaidreti
  3. Vitamini 
  4. Madini
  5. Fati
  Chagua Jibu


   45. Chunguza mlishano ufuatao kisha jibu swali linalofuata

  Katika mlishano huo nini kitatokea ikiwa duma watahama katika mazingira haya?

  1. Mimea itakauka 
  2. Nyati watapungua
  3. Mimea itaongezeka 
  4. Mimea itapungua
  5. Nyati nao watahama
  Chagua Jibu


  SEHEMU B

  Jibu maswali 46 - 50 kwa kuandika neno MOJA to kwa kila swali katika karatasi yako ya kujibia.

  46. Sauti iliyoakisiwa na kusikika tena huitwa......

  Fungua Jibu


  47. Mtu anayevua samaki kwa kutumia ndoana ni mfano wa daraja la ......... la nyenzo.

  Fungua Jibu


  48. Baada ya kutunga mimba katika uzazi wa mwanamke, homoni inayohusika na kukua kwa unene wa uterasi inaitwa               

  Fungua Jibu


  49. Gesi ya haidrojeni ikiungana na oksijeni hutokea kompaundi inayoitwa......

  Fungua Jibu


  50. ......ni gesi inayofanya sehemu kubwa hewani.

  Fungua Jibu


  Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

Bofya Hapa Kupakua
App Ya Learning Hub Tanzania
GO TO NECTA EXAMS