STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2006
SAYANSI 2006

SEHEMU A

Chaguajibu sahihi kisha andika herufi inayohusika mbeleya nambaya kila swali katika karatasi yakoya kujibia.

1. Katika mambo yafuatayo, lipi linawakilisha badiliko la kiumbo?

  1. Maji kuwa mvuke
  2. Kuchoma karatasi
  3. Asali kubadilika kuwa pombe
  4. Chuma kupata kutu 
  5. Kuni kuwa mkaa
Chagua Jibu


2. Mojawapo ya yaliyoorodheshwa hapa chini husaidia kuhifadhi mazingira nayo ni:

  1. kukata miti kwa ajili ya kuni na kujenga;
  2. kubadilibadili mazao ya kupanda shambani;
  3. kutumia mbolea ya chumvi chumvi; 
  4. kusafisha mashamba kwa kukatua;
  5. kufuga ng'ombe kwa wingi.
Chagua Jibu


3. Madini iliyo ngumu kuliko nyingine zote ni ipi?

  1. Almasi
  2. Makaa ya mawe 
  3. Shaba 
  4. Ulanga 
  5. Dhahabu
Chagua Jibu


4. Nyama, samaki, maziwa na mayai ni vyakula vya:

  1. kutia nguvu 
  2. kulinda mwili 
  3. kujenga mwili 
  4. kutia joto mwili 
  5. kuhitaji mbinu bora za kuhifadhi.
Chagua Jibu


5. Mimea hujipatia maji na madini ya chumvi chumvi kwa njia inayowakilishwa na herufi L katika mchoro ufuatao. Njia hiyo ni ipi?

  1. mjongeo wa maji na madini
  2. translokesheni
  3. fototropizimu
  4. Osmosis
  5. fotosinthesis
Chagua Jibu


6. Gurudumu kapi ni mashine ... ... ...

  1. tata itumikayo kupandisha vitu juu
  2. imara iliyoshikishwa na gurudumu dogo
  3. yenye meno yanayoingiliana na ya gurudumu jingine
  4. rahisi itumikayo kupandisha vitu juu 
  5. nayotumika kufungia maunzi pamoja.
Chagua Jibu


7. Namba gani katika mchoro ufuatao inawakilisha tezi itoayo homoni ambayo humfanya mtu asipate ugonjwa wa kisukari?

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
Chagua Jibu


8. Meli inaelea katika maji (baharini au ziwani) kwa sababu ina:

  1. nafasi kubwa tupu iliyojaa hewa ndani
  2. nafasi yenye hewa kidogo
  3. uzito mdogo kuliko maji
  4. mstari wa plimsoli unaozuia maji
  5. ujazo nene mdogo kuliko maji
Chagua Jibu


9. Jaribio hili (chunguza kwa makini mchoro ufuatao) hudhihirisha kvvamba mwanga

  1. husafiri na kugawa vitu sehemu mbili
  2. husafiri katika mstari mnyoofu
  3. husafiri na kupinda upitapo katika media tofauti
  4. husafiri ndani ya maji kwa kujikunja
  5. husafiri na kusababisha vitu kupinda
Chagua Jibu


10. Mnyororo wa baiskeli hupitia gia mbili (tazama mchoro ufuatao). Gia iliyozungushwa na tairi la nyumba ina meno 20 na ile iliyounganishwa na pedali ina meno 50. Iwapo pedali zitafanya mizunguko miwili, tairi la nyuma litazunguka mara .........

  1. Tano 
  2. Nne 
  3. Tatu
  4. Moja 
  5. Nyingi
Chagua Jibu


11. Sehemu zinazofanya mfumo wa mzunguko wa damu ni damu yenyewe,

  1. ubongo na mishipa ya damu 
  2. mapafu na mishipa ya damu
  3. moyo na mishipa ya damu 
  4. moyo na mishipa ya fahamu
  5. moyo na ubongo
Chagua Jibu


12. Uzito wa mzigo x katika mchoro ufuatao ni:

  1. kilo 200
  2. kilo 2.5
  3. kilo 25
  4. kilo 250
  5. kilo 36.2
Chagua Jibu


13. Tendo Ia kuvunjavunja na kubadili chakula ili kiweze kunyonywa au kufyonzwa na mwili hujulikana kama

  1. kumeng'enya 
  2. kurutubisha 
  3. kusharabu 
  4. eksrisheni 
  5. respiresheni
Chagua Jibu


14. Chunguza mchoro ufuatao kwa makini. Je, ni kitu kipi chembe zake zimeachana sana?

Chagua Jibu


15. Ugonjwa upi kati ya magonjwa yafuatayo husababishwa na ukosefu wa vitamini?

  1. Kifua kikuu 
  2. Kiseyeye
  3. Tetekuwanga 
  4. Malaria
  5. Kuhara
Chagua Jibu


16. Usumaku unaweza kuondolewa kwa kufanya yafuatayo:

  1. kugongagonga na kupasha joto ikiwa imening'inizwa Mashariki-Magharibi
  2. Kuining'iniza Mashariki-Magharibi na kuiosha
  3. Kuizungusha koili na kupitisha umeme
  4. Kuizungushia koili na kuichoma
  5. Kuigongagonga na kuzungushia koili
Chagua Jibu


17. Uvuvi wa samaki kwa kutumia baruti ni njia mojawapo ya:

  1. kukuza sayansi
  2. kuua magugu maji yanayochafua mazingira
  3. kuharibu mazalio ya samaki na kuchafua mazingira
  4. kuondoa aina ya samaki wakubwa
  5. kuwafukuza papa wakali wasiwale samaki wadogo wadogo
Chagua Jibu


18. Sehemu inayooneshwa kwa herufi Z katika mchoro ufuatao huitwa

  1. nyukliasi
  2. vakyuli
  3. saitoplazimu
  4. ukuta wa seli
  5. epithiliamu
Chagua Jibu


19. Ni ugonjwa upi kati ya magonjwa yafuatayo huweza kuzuiwa kwa chanjo?

  1. Kifaduro
  2. Kisonono 
  3. Malaria 
  4. Homa ya matumbo 
  5. Kipindupindu
Chagua Jibu


20. Kati ya matendo yafuatayo, ni yapi huongeza kasi ya mmomonyoko wa ardhi?

  1. Kufuga mifugo mingi na kukata miti
  2. Kilimo cha sesa na kutandaza nyasi
  3. Kilimo cha matuta na umwagiliaji
  4. Kufuga mifugo mingi na kupanda miti 
  5. Kupanda miti na kuchoma mbuga
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  




Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256