STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2021

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI

03 MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI

Muda: Saa 1:30 Mwaka: 2021

Maelekezo

1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalumu ya kujibia (OMR).

4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.

5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.

6. Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

image

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.

8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali la 1 hadi 40 na kalamu ya Wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.

9. Simu za mkononi na Vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A (Alama 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

Chagua jibu sahihi kisha weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu maalum kujibia (OMR) uliyopewa.

1. Maji ni muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania. Bainisha vyanzo vikuu vitatu vya rasilimali hiyo. 

 1. Mvua, maziwa na bahari 
 2. Bahari, visima na mito 
 3. Mvua, maji yaliyo juu na Chini ya ardhi 
 4. Maziwa, mito na chemchemi 
 5. Visima, chemchemi na mvua
Chagua Jibu


2. Kupungua kwa theluji katika mlima Kilimanjaro kumesababishwa na ongezeko la joto katika uso wa dunia. Ni shughuli ipi inaweza kutumika kukabiliana na tatizo hilo?

 1. Kuchoma misitu na kukata miti 
 2. Kulima kandokando ya milima
 3. Kupanda miti na kutunza mazingira 
 4. Uvunaji ovyo wa misitu 
 5. Kufuga mifugo mingi katika eneo dogo
Chagua Jibu


3. Mtaalamu wa masuala ya mazingira aliwaasa wanakijiji waishio kando ya mto Mzinga kuacha tabia ya uharibifu na uchafuzi wa chanzo cha maji. Je, ni vitendo gani aliwashauri kuviacha?

 1. Kupanda miti, kuchoma misitu na kutupa taka katika mto
 2. Kulisha mifugo, kupanda nyasi na kutupa taka katika mto
 3. Umwagiliaji, kutengeneza matuta na kutiririsha maji taka.
 4. Kulima, kulisha mifugo na kukata miti
 5. Kuchakata malighafi, kuoga na kupozea mitambo
Chagua Jibu


4. Mtaalamu wa madini aliwatembelea wanafunzi wa Darasa la Saba na kuwafundisha aina mbalimbali za madini na kazi zake. Je ni madini yapi hutumika kukatia vioo?

 1. Dhahabu 
 2. Almasi 
 3. Fedha 
 4. Tanzanaiti 
 5. Shaba
Chagua Jibu


5. Mzee Mahiya ni mfugaji ambaye huhamahama na idadi kubwa ya mifugo. Ni madhara yapi husababishwa na aina hii ya ufugaji?

 1. Mafuriko 
 2. Kustawi kwa uoto wa asili 
 3. Kufa kwa mifugo 
 4. Kupotea kwa misitu 
 5. Kuharibika kwa mazao
Chagua Jibu


6. Bwawa la Nyerere ni mojawapo ya chanzo kinachotarajiwa kuzalisha nishati ya umeme wa maji nchini Tanzania. Je, bwawa hili limejengwa katika mto gani?

 1. Ruaha 
 2. Ruvuma 
 3. Ruvu 
 4. Rufiji 
 5. Pangani
Chagua Jibu


7. Musa hutoka jasho kwa wingi wakati wa msimu wa joto. Je, utamshauri avae nguo ya rangi gani?

 1. Nyeupe 
 2. Nyeusi 
 3. Bluu 
 4. Njano 
 5. Kijani
Chagua Jibu


8. Kuongezeka kwa joto duniani kunakosababishwa na shughuli za kibinadamu kama Vile uchomaji wa misitu, uzalishaji wa gesiukaa kutoka viwandani na uchomaji wa mkaa husababisha madhara yafuatayo isipokuwa

 1. kuyeyuka kwa theluji katika mlima kilimanjaro. 
 2. kupotea kwa bayoanuai. 
 3. kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari. 
 4. kuongezeka kwa uoto wa asili.
 5. kutokea kwa ukame.
Chagua Jibu


9. Mtaalamu wa hali ya hewa alisoma kiwango cha juu cha jotoridi la siku kama nyuzi joto 420C na kiwango cha Chini 200C. Upi ni utofauti wa kiwango cha jotoridi kwa siku?

 1. 620
 2. 620
 3. 220
 4. 220
 5. 1340F
Chagua Jibu


10. Wanafunzi wa Darasa la Nne walijifunza juu ya uhusiano uliopo kati ya jua, mimea na maji juu ya uso wa dunia. Yapi ni matokeo ya uhusiano huo?

 1. Kutokea kwa upepo 
 2. Kufanyika kwa mvua 
 3. Kuganda kwa maji 
 4. Kutokea kwa kimbunga 
 5. Kuyeyuka kwa barafu
Chagua Jibu


11. Katika uso wa Dunia kuna pepo zinazovuma kutoka eneo moja kwenda jingine. Je, ni upepo gani unavuma kutoka Kusini kuelekea Kaskazini?

 1. Upepo wa Kusi 
 2. Upepo wa Kaskazini 
 3. Upepo mkavu 
 4. Upepo wa Magharibi 
 5. Upepo unyevu
Chagua Jibu


12. Tanzania ina makabila mengi yenye mila nzuri na potofu. Ni mila ipi yenye madhara kwa jamii?

 1. Kuruhusu wanawake wajawazito kula mayai 
 2. Kukeketa watoto wa kike 
 3. Kufundisha wavulana na wasichana kuhusu maadili 
 4. Kutahiri wavulana
 5. Kuwapa wanawake haki sawa na wanaume
Chagua Jibu


13. Kila jamii inchini Tanzania ina michezo yake ya asili kulingana na mazingira, muda na utamaduni. Ipi ni mifano ya michezo hiyo?

 1. Mpira wa miguu, ngumi na kukimbia
 2. Kukimbia, kuogelea na mpira wa miguu
 3. Kurusha mkuki, kuruka kamba na kukimbia 
 4. Mpira wa miguu, pete na kuogelea
 5. Mpira wa kikapu, miguu na pete
Chagua Jibu


14. Ni kwa namna gani jamii inaweza kukabiliana na tamaduni zilizopitwa na wakati?

 1. Kudumisha umoja wa kitaifa 
 2. Kudumisha misingi ya uzalendo
 3. Kuwa na misingi ya mila na desturi zinazofanana 
 4. Kupenda jamii na taifa 
 5. Kufanya majadiliano na jamii inayohusika
Chagua Jibu


15. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua umuhimu wa michezo kama nyenzo ya kuburudisha na kuwaunganisha raia wake. Ni taasisi ipi inayohusika zaidi katika kusimamia na kuendeleza michezo inchini Tanzania?

 1. Baraza la Sanaa la Taifa
 2. Baraza la Kiswahili la Taifa
 3. Baraza la Michezo ya Ridhaa la Taifa
 4. Baraza la Michezo la Taifa
 5. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
Chagua Jibu


16. Yafuatayo huweza kutokea kwa taifa linalokuza utamaduni wake isipokuwa

 1. kudumisha misingi ya uzalendo 
 2. kuiga tamaduni za kigeni 
 3. kudumisha umoja 
 4. kulinda asili yake
 5. kuwepo kwa uhusiano mzuri katika jamii.
Chagua Jibu


17. Kasuku anaipenda nchi yake, ana moyo wa kujitoa kwa Taifa lake na ni mtunzaji mzuri wa rasilimali za Taifa. Kasuku anaweza kuwa na sifa ipi kwa taifa lake?

 1. Mlinzi wa rasilimali za nchi 
 2. Mzalendo kwa taifa lake
 3. Mtunzaji wa miiko ya jamii 
 4. Mlinda usalama wa jamii
 5. Msimamizi wa umoja wa wananchi
Chagua Jibu


18. Katika mapambano ya kudai uhuru wa Tanganyika, vyama vingi vilishiriki kwa malengo tofauti. Ni chama gani kiliungwa mkono na serikali ya kikoloni ili kukidhoofisha chama cha TANU?

 1. Tanganyika African Association (TAA) 
 2. Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP)
 3. Afro Shirazi Party (ASP) 
 4. African National Congress (ANC)
 5. United Tanganyika Party (UTP)
Chagua Jibu


19. Jumuiya ya Afrika Mashariki ina makao makuu yake ambapo taasisi zake zote huwepo na kazi muhimu zote hufanyika hapo. Je, makao makuu yanapatikana wapi?

 1. Mombasa nchini Kenya 
 2. Kigali nchini Rwanda 
 3. Juba nchini Sudan Kusini 
 4. Entebbe nchini Uganda 
 5. Arusha nchini Tanzania
Chagua Jibu


20. Licha ya kugawanywa kwa Bara la Afrika katika mkutano wa Berlin wa mwaka 1884 hadi 1885, Afrika iligawanywa tena baada ya vita vya kwanza vya dunia miongoni mwa mataifa ya Ulaya isipokuwa

 1. Ufaransa 
 2. Italia 
 3. Ubelgiji 
 4. Ureno 
 5. Ujerumani
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  
Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256