STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2018

 MAARIFA YA JAMII - 2018
SEHEMU A 


URAIA 

Chagua jibu sahihi kisha weka kivuli kwenye herufi ya jibuhullosahihi katika fornu maaL­kujibia.

1. Mtu anayedhibiti mwenendo wa wanafunzi shuleni ni..

 1.  Mwenyekiti wa kamati ya shule 
 2.  Mwalimu wa nidhamu
 3.  Mwalimu mkuu msaidizi 
 4.  Mwalimu wa taaluma
 5.  Mwalimu wa somo
Chagua Jibu


2. Chombo cha juu katika maamuzi kwenye serikali ya kijiji ni ..................

 1.  Serikali ya kijiji 
 2.  Kamati ya ulinzi na usalama
 3.  Mkutano mkuu wa kijiji 
 4.  Afisa Mtendaji wa kijiji
 5.  Kamati ya Maendeleo ya kijiji
Chagua Jibu


3. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya huchaguliwa na...................

 1.  Mkurugenzi mtendaji wa wilaya 
 2.  Baraza la madiwani
 3.  Waziri katika ofisi ya Rais 
 4.  Afisa Mtendaji wa Kata
 5.  Wenyeviti wa vijiji
Chagua Jibu


4. Ipi kati ya sarafu zifuatazo ina picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar?.................

 1.  Sarafu ya shilingi mia moja 
 2.  Sarafu ya shilingi mia mbili
 3.  Sarafu ya shilingi hamsini 
 4.  Sarafu ya silingi ishirini
 5.  Sarafu ya shilingi kumi
Chagua Jibu


5. Maliasili zinazovutia watalii na kuchangia katika kukuza uchumi wa Tanzania ni..................

 1.  ardhi 
 2.  mito 
 3.  mifugo
 4.  madini 
 5.  mbuga za wanyama
Chagua Jibu


6. Wajibu wa serikali katika kujenga maadili ya viongozi ni....................

 1. Kuwakopesha magari viongozi wote
 2. Kuimarisha mfumo wa chama kimoja cha siasa
 3. Kusimamia sheria za utumishi wa umma
 4. Kuhamisha watumishi wasio waadilifu
 5. Kuajiri watumishi wenye elimu ya juu to
Chagua Jibu


7.Tofauti kati ya mila na desturi ni....

 1. Mila hubadilika mara kwa mara kuliko desturi
 2. Desturi hubadilika mara kwa mara kuliko mila
 3. Mila ni mazoea wakati desturi ni vitendo
 4. Mila ni mazoea na huweza kubadilika na kuwa desturi
 5. Desturi hubadilika mara kwa mara kuliko mazoea
Chagua Jibu


8. Matumizi ya ofisi ya umma kwa manufaa binafsi huitwa.................

 1.  takrima 
 2.  rushwa
 3. uzalendo
 4.  ubinafsi 
 5.  ujasiriamali
Chagua Jibu


9. Zipi kati ya nchi zifuatazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola?................

 1.  Botswana na Burundi
 2.  Botswana na Zambia 
 3.  Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
 4.  Malawi na Burundi 
 5.  Zambia na Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo
Chagua Jibu


10. Moja ya matukio yanayokiuka Haki za Binadamu nchini Tanzania ni.............

 1.  Mauaji ya vikongwe na maalbino 
 2.  Ukataji na upandaji mid
 3.  kuwafungulia mashtaka wahalifu 
 4.  kufukuzwa kazi viongozi wasio waadilifu
 5.  Serikali kusimamia ukusanyaji kodi
Chagua Jibu


11. Mojawapo ya njia ambazo wananchi wanaweza kushiriki katika ulinzi na usalama ni...............

 1.  kupiga wahalifu 
 2.  kufanya mazoezi ya viungo
 3.  kuwaua wahalifu 
 4.  kuwafichua wahalifu
 5.  kuwa rafiki na wahalifu
Chagua Jibu


12.Viashiria vya utandawazi ni pamoja na...............

 1. kupungua kwa tofauti ya kipato
 2. uchumi wa soko huria
 3. kupungua kwa umaskini
 4. kuwepo kwa ushindani wa kutengeneza silaha
 5. kuwepo kwa bidhaa nyingi toka viwanda vya ndani
Chagua Jibu


SEHEMU B

HISTORIA
:hagua jibu sahihi kisha weka kivuli kwenye herufi ya jibu h u b sahihi katika karatasi ya kujibia.

13. Baba wa baba yako anaitwa

 1.  baba 
 2.  mjukuu 
 3.  mjomba 
 4.  babu 
 5.  mpwa
Chagua Jibu


14.Ni Taifa lipi la kibepari liliitawala Tanganyika kuanzia mwaka 1891 hadi 1918?

 1.  Ujerumani 
 2.  Uingereza
 3.  China 
 4.  Ureno 
 5.  Ufaransa
Chagua Jibu


15. Kwa nini Berlin ni miongoni mwa miji maarufu katika historia?

 1. Ni Makao Makuu wa Umoja wa Mataifa
 2. Ni Makao Makuu wa Jumuiya ya Madola
 3. Ni mji uliokuwa kitovu cha biashara ya utumwa
 4. Ni mji wa Ufaransa ambao uliendesha utawala wa kulisha kasumba
 5. Ni mji ambao mgawanyo wa Bara la Afrika ulifanyika
Chagua Jibu


16.Mataifa makubwa ya kibepari yaliyogombania Bara la Afrika yalikuwa

 1. Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji, Italia na Ureno
 2. Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Uchina, Uhispania na Marekani
 3. Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Japani, Uhispania na Ubelgiji
 4. Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Urusi, Uchina na Japani
 5. Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji, Italia na Uchina
Chagua Jibu


17. Mwanzilishi wa Kampuni wa Kibiashara ya Kiingereza ya Afrika Mashariki anaitwa

 1. David Livingstone 
 2. Karl Peters 
 3.  Mungo Park
 4.  William Mackinnon 
 5.  Seyyid Said
Chagua Jibu


18. Julius Von Soden alikuwa nani?................

 1. Gavana wa kwanza wa kiingereza katika Tanganyika
 2. Gavana wa kwanza wa kijerumani katika Tanganyika
 3. Gavana wa mwisho wa kijerumani katika Tanganyika
 4. Gavana wa mwisho wa Kiingereza katika Tanganyika
 5. Gavana aliyeanzisha utawala wa moja kwa moja katika Tanganyika
Chagua Jibu


19. Mtaalamu wa mambo wa kale aliyevumbua fuvu la binadamu wa kwanza Olduvai aliitwa

 1.  Charles Darwin 
 2.  Zinjathropus
 3.  Homo Habilis 
 4.  David Livingstone 
 5.  Louis Leakey
Chagua Jibu


20. Ni lini binadamu alianza kuchoma misitu iii kuwafukuza wanyama wakali?.................

 1. Wakati wa Zama za Chuma
 2. Wakati wa Zama za Mwanzo za Mawe
 3. Wakati wa Zama za Kale za Mawe
 4. Wakati wa Zama za Mwisho za Mawe
 5. Wakati wa Zama za Kati za Mawe
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  
Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256