11. Ipi kati ya mila zifuatazo inaweza kueneza ITVU/UKIMWI?........
- Ngoma za asili
- Miiko ya chakula
- Kuzaa watoto wengi
- Kurithi wajane
- Mahari
Chagua Jibu
12. Kuna makundi mangapi ya uoto wa asili?
- Matatu
- Manne
- Mawili
- Matano
- Sita
Chagua Jibu
13. Lengo kuu la mabadiliko ya katiba ya Tanzania mwaka 1962 yalikuwa
- kuunda serikali ya umoja wa kitaifa
- kuunda serikali ya shirikisho
- kuunda serikali ya mtaa
- kuunda serikali ya jamhuri
- kuunda serikali ya mpito.
Chagua Jibu
14. Umoja wa Afrika ulianzishwa rasmi mwaka gani?
- 2002
- 2001
- 1963
- 1945
- 1999
Chagua Jibu
SEHEMU B
HISTORIA
Chagua jibu sahihi kisha weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililosahihi katika fomu maalumu(OMR) ya kujibia.
15. Familia ya ndugu na jamaa inakaribia kufanana na kundi la jamii inayojulikana kama:
- kabila
- jamii
- ukoo
- jirani
- kijiji
Chagua Jibu
16. Ubugabire ni mfumo wa Umwinyi uliajengwa juu ya umiliki wa:
- ngombe
- viwanda
- ardhi
- wafanyakazi wa kigeni
- watumwa
Chagua Jibu
17. Mfumo wa kwanza ambapo jamii ilimiliki njia zote za uzalishaji kijamaa huitwa:.............
- Umwinyi
- Ukomunisiti
- Ujamaa
- Urafiki
- Ujima
Chagua Jibu
18. Mkataba upi uliharamisha biashara ya utumwa Afrika Mashariki mwaka 1873?
- Mkataba wa Moresby
- Mkataba wa Hamerton
- Mkataba wa Berlin
- Mkataba wa Heligoland
- Mkataba wa Frere
Chagua Jibu
19. Mwenendo mzima wa maisha ya binadamu unaitwa
- historia
- utamaduni
- Desturi
- demokrasia
- mila
Chagua Jibu
20. Utandawazi umebadili dunia na kuwa kama aliitwa..................
- nchi
- wilaya
- mpira
- kijiji
- kata
Chagua Jibu
21. Umoja wa Mataifa ulianzishwa mwaka:
- 1955
- 1945
- 1995
- 1885
- 1950
Chagua Jibu
22. Mreno wa kwanza kufika sehemu ya Kusini mwa Afrika:
- King Henry
- Bartholomew Diaz
- Vasco Da Gama
- David Livingstone
- Cecil Rhodes
Chagua Jibu
23. Sababu mojawapo ya kukomeshwa kwa biashara ya utumwa ilikuwa:
- Huruma ya wazungu juu ya mateso ya watumwa
- Waafrika kupigania uhuru wao
- Kupata masoko ya bidhaa za ulaya
- Wazungu kujali juu ya usawa wa watu wote
- Udhaifu wa watumwa kutoka Afrika.
Chagua Jibu
24. Makundi makuu ya mawakala wa ukoloni waliokuja Tanganyika na Zanzibar yalikuwa:
- askari, wamisionari na watendaji
- wamisionari, waandishi wa habari na wafanyabiashara
- wapelelezi, watendaji na wafanyabiashara
- waandishi wa habari, wapelelezi na Askiari
- wapelelezi, wamisionari na wafanya biashara
Chagua Jibu
25. Mkataba wa 1890 uliogawanya Afrika Mashiriki kwa Wajerumani na Waingereli.ulijulikana kama:
- Mkataba wa Hamerton
- Mkataba wa Haligoland
- Mkataba wa Moresby
- Mkataba wa Afrika Mashariki
- Mkataba wa Frere
Chagua Jibu
26. Makoloni ya Kifaransa Afrika yalikuwa pamoja na:
- Togo na Morocco
- Senegal na Ghana
- Nigeria na Tunisia
- Senegal na Morocco
- Angola na Tunisia
Chagua Jibu
27. Kiongozi wa Banyoro aliyewaongoza wafuasi wake kuwapiga Waingereza Uganda alikuwa
- Kabaka Mwanga
- Kabarega
- Lobengula
- Lewanika
- Samora Toure
Chagua Jibu
28. Azimio la Arusha lilisisitiza kwamba maendeleo ya nchi lazima yajengwe juu ya :
- Utegemezi wa misaada
- Biashara ya kimataifa
- Ujamaa na kujitegemea
- Chama kimoja cha demokrasia
- Ubinafsishaji na uwekezaji.
Chagua Jibu
29. Tanzania ilipitisha mfumo wa vyama vingi kwa mara ya pili mwaka:
- 1995
- 1992
- 1963
- 1985
- 1965
Chagua Jibu
30. Nini faida ya mfumo wa chama kimoja?
- unawafanya baadhi ya viongozi wa Kiafrika kuwa madikteta.
- unawawezesha wananchi kuwa na uhuru wa kuzungumza.
- unaruhusu watu wengi kushiriki shughuli za kisiasa.
- unapunguza migogoro inayotokana na tofauti za kimtazamo.
- inawawezesha watu kukosoa serikali yao wakati wowote.
Chagua Jibu
31.Ipi siyo sahihi kuhusu sifa za elimu ya Tanzania kabla ya Uhuru?
- Ilitolewa kwa watu wote.
- Iliwatenga watoto wa kike.
- Iliangalia matabaka.
- llikuwa ya nadhalia zaidi kuliko vitendo.
- Ilitolewa kwa kuzingatia dini.
Chagua Jibu
32. Kurudishwa tena kwa mfumo wa vyama vingi Tanzania kulipendekezwa na :
- Tume ya Kisanga
- Tume ya Nyalali
- Tume ya Makweta
- Tume ya Karume
- Tume ya Warioba
Chagua Jibu
SEHEMU B
JIOGRAFIA
Magua jibu sahihi na uzungushie herufi katika karatasi yako ya kujibia.
33. Mazingira ni:
- Viumbe hai na visivyo hai
- Viumbe hai, nyumba na maji
- Vitu vyote vinavyomzunguka binadamu
- Ardhi, Majengo na bahari
- Mimea, wanyama wa kufugwa na nyumba
Chagua Jibu
34. Matumizi sahihi ya mistari ya gridi kwenye ramani ni
- kuonesha mahali katika ramani
- kuonesha uelekeo wa Mashariki
- kuonesha umbali
- kupata muda
- kuonesha mwelekeo wa Kaskazini.
Chagua Jibu
35. Chanzo kikuu cha mnishati katika fumo wa jua ni:
- Dunia
- Sayari
- jua
- Mwezi
- Nyota
Chagua Jibu
36. Vifuatavyo ni vyanzo vya maji isipokuwa:
- visima
- chemichemi
- mita
- mabomba ya maji
- . maziwa
Chagua Jibu
37. Uchafuzi wa hewa katika maeneo ya makazi unaweza kuthibitiwa kwa:
- matumizi ya vyoo
- kuchoma takataka
- kumwaga maji taka mitaani
- kuchemsha maji ya kunywa
- kupunguza matumizi ya mifuko ya plastiki
Chagua Jibu
38. Pitio ni sehemu ya ardhi inayoonyesha:
- eneo lenye bonde la ufa
- sehemu yenye milima
- vilele vya milima
- mandhari tambarare
- nafasi kati ya safu za milima miwili
Chagua Jibu
39. Tafuta umbali halisi katika kilometa kati ya sehemu A" na "S" ikiwa umbali wa ramani ni sentimeta 15 na skeli ya ramani ni 1:100,000
- 50km
- 0.15km
- 100,000 km
- 7.5km
- 15km
Chagua Jibu
40. Mikoa inayolima zao la ndizi Tanzania ni:
- Kagera, Kilimanjaro na Mbeya
- Mbeya, Kagera na Lindi
- Kagera, Singida na Shinyanga
- Arusha, Morogoro na Shinyanga
- Singida, Lindi na Kagera
Chagua Jibu
41. Wastani wa mvua wa milimita 500 kwa mwaka, joto kali kutoka 28° - 39° waka:mchana na hali ya baridi kali wakati wa usiku ni tabia za:
- Hali ya hewa ya kitropiki
- Hall ya hewa ya Jangwa
- Nusu jangwa
- Hall ya hewa ya Ikweta
- Hali ya hewa ya Mediteraniani
Chagua Jibu
42. Soma picha ifuatayo kwa makini kisha jibu maswali namba 42 na 43.
Shughuli kuu za kiuchumi zinazoweza kufanyika katika eneo hili ni:
- kilimo
- ufugaji
- uvuvi
- utalii
- viwanda
Chagua Jibu
43. Faida mojawapo ya wanyama wanaoonekana kwenye picha hii ni:
- kuongezeka kwa idadi ya wanyama
- uhifadhi wa mazingira
- kuongezeka kwa pato la taifa
- kuongezeka kwa misitu
- kuongezeka kwa mvua
Chagua Jibu
44. Lipi kati ya majanga yafuatayo husababishwa na binadamu
- Vita
- Ukame
- Milipuko ya volkano
- Tetemeko la ardhi
- Kimbunga
Chagua Jibu
45. Katani, chaff na kahawa ni:
- mazao ya chakula
- mazao ya biashara
- mimea ya jamii ya kunde
- mazao ya msimu
- mazao ya kuuza nje
Chagua Jibu
46. Ranchi ni eno lililotengwa kwa:
- kilimo cha mazao
- machinjio ya ngombe
- ufugaji wa ngombe
- josho la ngombe
- kuotesha majani
Chagua Jibu
47. Katika Afrika ufugaji wa kondoo hufanyika zaidi:
- Namibia
- Tanzania
- Afrika Kusini
- Lesotho
- Botswana
Chagua Jibu
48. Uvuvi usio endelevu hufanyika kwa kutumia:
- Mitego
- Meli kubwa
- Nyavu mraba ndogo
- Ugwe
- Nyavu mraba kubwa
Chagua Jibu
49. Ni madini yapi yanayopatikana Tanzania pekee?
- Dhahabu
- Urani
- Almasi
- Tanzanaiti
- Makaa ya mawe
Chagua Jibu
50. Kuhama kwa watu na bidhaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine inaitwa:
- Usafirishaji
- Utalii
- Biashara
- Mawasiliano
- Uhamiaji.
Chagua Jibu
Try Another Test |