2016 - MAARIFA YA JAMII
SEHEMU A
Chagua jibu herufiyake kwenye karatariya
1. Katibu kata anachaguliwa na:
- Wanachama wa chama tawala
- Mkutano mkuu wa kata
- Wananchi wa kata ile
- Mkutano wa kijiji wa mwaka
- Kamati ya kijiji
Chagua Jibu
2. Kamati ya maendeleo ya kata inaundwa na wafuatao isipokuwa:
- Katibu kata
- Afisa mtendaji wa Kata
- Katibu Kata wa viti maalumu
- Afisa mtendaji wa Mkoa
- Kamanda wa Polisi wa Mkoa
Chagua Jibu
3. Mwakilishi wa Rais katika ngazi ya mkoa ni:
- Katibu tawala wa Mkoa
- Mkurugenzi mtendaji wa manispaa
- Mkuu wa Mkoa
- Afisa mtendaji wa Mkoa
- kamanda wa Polisi wa mkoa
Chagua Jibu
4. Kauli mbiu ya Tanzania iliyopo kwenye nembo ya taifa ni:
- uhuru na maendeleo
- uhuru na kazi
- uhuru na umoja
- uhuru na amani
- umoja na amani
Chagua Jibu
5. Wimbo wa taifa una beti ngapi?
- Tatu
- Mbili
- Nne
- Tano
- Sita
Chagua Jibu
6. Mambo yote ambayo watu wote wanastahili bila ya kujali kabila, utaifa au jinsia ya huitwa:
- utawala bora
- haki za binadamu
- utawala wa sheria
- demokrasia
- usawa wa kijinsia
Chagua Jibu
7. Ushiriki wa wanafunzi kwenye kuchagua viongozi wao shuleni huimarisha:
- uongozi wa kikatiba shuleni
- kiongozi mkuu wa uongozi wa shule
- ukiritimba shuleni
- usalama shuleni
- uongozi bora shuleni
Chagua Jibu
8. Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora ilianzishwa Tanzania mwaka:
- 2005
- 1995
- 1992
- 2001
- 1977
Chagua Jibu
9. Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ni:
- Kamanda wa Polisi wa Mkoa
- Katibu Tawala wa mkoa
- Afisa Usalama wa Mkoa
- Afisa Upelelezi wa makosa ya jinai wa Mkoa
- Mkuu wa Mkoa
Chagua Jibu
10. Umuhimu wa kivuko cha pundamilia ni:
- kupunguza msongamano wa magari barabarani
- kuwezesha walemavu kuvuka barabara kwa usalama
- kuwezesha watembea kwa miguu kuvuka barabara kwa usalama
- kutoa ishara ya kuwepo kwa mifugo karibu na barabara
- kuashiria uwepo wa reli karibu na barabara
Chagua Jibu
11. Uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania ni:
- kilimo
- ujasiriamali
- biashara
- utandawazi
- madini
Chagua Jibu
12. Ujumla wa taratibu za maisha ya kila siku ya mwanadamu huitwa:
- mila
- desturi
- sanaa
- utamaduni
- kazi za mikono
Chagua Jibu
13. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huchaguliwa na:
- wananchi
- wabunge
- mawaziri
- madiwani
- Jaji Mkuu
Chagua Jibu
14. Wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni:
- Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi na China
- Marekani, Uingereza, Ujerumani, Urusi na China
- Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi na Italia
- Marekani, Uingereza, Urusi, Kanada na Ujerumani
- Marekani, Uingereza, Urusi, Japani na Ujerumani
Chagua Jibu
SEHEMU B
HISTORIA
Chagua jibu herufi yake kwenye karatariya
15. Chimbuko la familia ni:
- babu na bibi
- baba na mama
- shangazi na mjomba
- watoto na wazazi
- kaka na dada
Chagua Jibu
16. Kiongozi mkuu wa shule ni:
- mwalimu mkuu msaidizi
- mwalimu wa taaluma
- kiranja mkuu
- mwalimu mkuu
- mwalimu wa nidhamu
Chagua Jibu
17. Nini faida ya mgawanyo wa kazi katika familia?
- Hudhoofisha familia
- Huchochea utengano
- Huleta udikteta
- Huleta maendeleo
- Huleta mitafaruku
Chagua Jibu
18. Moto uligunduliwa katika:
- Zama za Mawe za Kale
- Zama za Mawe za Kati
- Zama za Chuma
- Zama za Mawe za Mwisho
- Zama za Viwanda
Chagua Jibu
19. Uchoraji wa wanyama katika mapango ulianza kufanywa na binadamu katika:
- Zama za Chuma
- Zama za Mawe za Kati
- Zama za Mawe za Kale
- Zama za Mawe za Mwisho
- Zama za Mavve za Mwanzo
Chagua Jibu
20. Mabaki ya Zinjanthropus yaliyopatikana katika bonde la Olduvai mwaka 1959 yaligunduliwa na:
- David Livingstone
- Fredrick Lugard
- Louis Leakey
- Carl Peters
- Charles Darwin
Chagua Jibu
21. Uvinza ni maarufu kwa uzalishaji wa:
- makaa ya mawe
- Shaba
- Chuma
- Chumvi
- Dhahabu
Chagua Jibu
22. Ni bidhaa za aina gani zililetwa Afrika Mashariki na wafanyabiashara kutoka Indonesia na China karne ya 8?
- Chuma, maganda ya kobe, na dhahabu
- Nguo, shanga na vyombo vya nyumbani
- Baruti, shanga na dhahabu
- Shanga, bunduki na pembe za ndovu
- Baruti, nguo za kitani na ngozi za chui
Chagua Jibu
23. Makabila matatu yaliyoshiriki katika biashara ya masafa marefu kabla ya ukoloni n:
- Wahehe, Wanyamwezi na Waturkana
- Wakaramajong, Wasukuma na Wapokoti
- Wamaasai, Wayao na Wasukuma
- Wayao, Wanyamwezi na Wahehe
- Wayao, Wanyamwezi na Wakamba
Chagua Jibu
24. Mkataba wa kwanza uliotiwa saini mwaka 1822 kukomesha biashara ya wzu:— Tanganyika na Zanzibar uliitwa:
- Mkataba wa Moresby
- Mkataba wa Frere
- Mkataba wa Heligoland
- Mkataba wa Hamerton
- Mkutano wa Berlin
Chagua Jibu
25. Vita vya Maji Maji vilisababishwa na:
- maji na dawa toka mto Rufiji
- tamaa na ushawishi wa waganga wa kienyeji
- unyonyaji wa Wajerumani
- ukatili wa Wamatumbi wa Songea
- majaribio ya silaha za jadi
Chagua Jibu
26. Kundi lipi la mawakala wa ukoloni lilikuwa la kwanza kuja Tanganyika?
- Wamisionari
- Wafanyabiashara
- Walowezi
- Wapelelezi
- Mabaharia
Chagua Jibu
27. Tanganyika ilipata Uhuru wake kwa njia ya:
- matumizi ya bunduki
- vita vya msituni
- mikataba ya kilaghai
- kikatiba
- matumizi ya Veto
Chagua Jibu
28. Ni chaguzi ngapi za vyama vingi zimekwisha kufanyika Tanzania baada ya Tume ya Nyalali?
- Mbili
- Tatu
- Nne
- Tano
- Sita
Chagua Jibu
29. Aliyekuwa Rais wa Tanganyika kabla ya muungano alikuwa:
- Abeid Karume
- Benjamin Mkapa
- Jakaya Kikwete
- Julius Nyerere
- Rashid Kawawa
Chagua Jibu
30. Wanachama waanzilishi wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) walikuwa:
- nchi huru za Afrika ya Kati
- nchi huru za Afrika
- nchi huru za Afrika ya Kaskazini
- nchi huru za Afrika ya Magharibi
- nchi huru kusini mwa Afrika.
Chagua Jibu
31. Hadi kufikia mwaka 1914, nchi zilizokuwa huru barani Afrika zilikuwa:
- Tanganyika na Zanzibar
- Ethiopia na Laiberia
- Ghana na Misri
- Somalia na Jibuti
- Afrika ya Kusini na Rwanda
Chagua Jibu
32. Umoja wa hiari wa nchi huru zilizowahi kutawaliwa na Uingereza hufahamika kama:
- Jumuiya ya Madola
- Umoja wa Mataifa
- Nchi zinazoendelea
- Umoja wa Afrika
- Shirikisho la Mataifa
Chagua Jibu
SEHEMU C
JIOGRAFIA
Chagua jibu herufi yake kwenye karatasi ya
33. Vitu viwili vinavyopatikana katika mazingira ya nyumbani ni:
- vitanda na madawati
- madarasa na maktaba
- vitanda na vyombo vya jikoni
- mlingoti wa bendera na vitanda
- viwanja vya michezo na madarasa
Chagua Jibu
34. Watu wanaoishi kandokando mwa bahari na maziwa hujihusisha na shughuli za:
- kilimo
- uvuvi
- uvunaji magogo
- ufugaji
- usafirishaji
Chagua Jibu
35. Ipi kati ya zifuatazo ni sifa ya ramani?
- Huonesha pande zote za kitu
- Urefu wa kitu huoneshwa
- Umbo la asili la kitu hubakia
- Rangi ya asili ya kitu huonekana
- Huonesha sura ya juu ya kitu.
Chagua Jibu
36. Mbuga za wanyama zinazopatikana Tanzania ni:
- Serengeti, Ruaha na Mikumi
- Tarangire, Katavi na Ngorongoro
- Serengeti, Manyara na Ngorongoro
- Selous, Serengeti na Mikumi
- Mkomazi, Selous na Ngorongoro
Chagua Jibu
37. Ipi kati ya majanga yafuatayo husababishwa na mwanadamu na pia nguvu za asili?
- Kimbunga
- Mlipuko wa volkano
- Milipuko wa mabomu
- Moto
- Vita
Chagua Jibu
38. Pareto hutumika kutengenezea:
- manukato
- dawa za kuulia wadudu
- vipodozi
- jeli
- mapambo
Chagua Jibu
39. Uvuvi usio endeleevu waweza kusababisha yafuatayo kasoro:
- vifo vya watu
- vifo vya samaki
- uchafuzi wa maji
- umaskini
- utajiri
Chagua Jibu
Angalia kielelezo kifuatacho kwa makini kisha jibu swali namba 40, 41 na 42.
40. Ni aina gani ya zao inaonekana katika kielelezo?
- Mahindi
- Mpunga
- Katani
- Ngano
- Mtama
Chagua Jibu
41. Zao linaloonekana kwenye kielelezo ni la:
- nafaka
- biashara
- matunda
- msimu
- chakula
Chagua Jibu
42. Mikoa mitatu ya Tanzania ambako zao hili hulimwa kwa wingi ni:
- Arusha, Dodoma na Kilimanjaro
- Tanga, Morogoro na Kilimanjaro
- Iringa, Mbeya na Rukwa
- Dodoma, Rukwa na Tabora
- Mwanza, Kagera na Kilimanjaro
Chagua Jibu
43. Mawasiliano kwa sauti hufanyika kwa kutumia:
- kugusa na kuandika tu
- simu, runinga na redio
- kuandika na runinga
- kugusa na kuchora tu
- lugha ya ishara na redio
Chagua Jibu
44. Ipi kati ya zifuatazo ni athari za kutumia vibaya njia za kisasa za mawasiliano?
- Mmomonyoko wa maadili
- Upatikanaji wa taarifa
- Kuleta maendeleo
- Kuelimisha jamii
- Kuendeleza umoja
Chagua Jibu
45. Aina kuu mbili za biashara ni:
- biashara ya mkopo na ya malipo
- biashara ya mkopo na kubadilishana
- biashara ya mtaji na fedha
- Biashara ya hisa na ya mitaji
- biashara ya ndani na ya nje
Chagua Jibu
46. Tanzania inapata faida gani kwa kuongeza biashara yake ya kimataifa?
- Kuongeza majengo
- Kupunguza wajasiriamali wa ndani
- Kuongeza deni
- Kupunguza mikataba ya kibiashara
- Kuongeza fedha za kigeni
Chagua Jibu
47. Aina kuu za usafirishaji Tanzania ni:
- Maji, mito na anga
- Ardhi, maji na anga
- Bahari, ardhi na anga
- Ardhi, maji na maziwa
- Mito, maziwa na bahari
Chagua Jibu
48. Lipi kati ya makundi yafuatayo linahusisha vyanzo vya taka hewa?
- Mahabara, mboga za majani na makopo
- Mifuko ya plastiki, vipande vya chupa, na harufu mbaya
- Maabara, viwanda na magari
- Magari, taka za nyumbani na plastiki
- Maabara, taka za nyumbani na viwanda
Chagua Jibu
49. Jamii za Kitanzania zinaweza kuthibiti utupaji taka kwa:
- kutupa taka hovyohovyo
- kulima kwa kutumia njia za kisasa za kilimo
- kutupa takataka katika mifereji
- kutumia mifuko ya plastiki
- kutoa elimu ya mazingira
Chagua Jibu
50. Nchi zinazovuna maji ya mvua na kuyatumia kuongeza maji kwenye udongo ni:
- Marekani na India
- Tanzania na India
- India na Kenya
- Kenya na Uganda
- China na Marekani
Chagua Jibu
Try Another Test |