STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2015

2015 - MAARFA

SEHEMU A

URAIA

Chaguajibu sahihi kisha andika herufiyake kwenye karatariya kujibia.

1. Mwenyekiti wa kikao cha maendeleo katika kata ni .

 1. Diwani wa kata
 2. Afisa Huduma za ugani
 3. Afisa Maendeleo wa kata
 4. Mratibu Elimu wa kata
 5. Afisa Mtendaji wa kata
Chagua Jibu


2. Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa kwa pamoja zipo chiniya .

 1. Bunge la Tanzania
 2. Serikali ya Mtaa
 3. Serikali Kuu
 4. Wabunge wa kuchaguliwa
 5. Chama Tawala
Chagua Jibu


3. Jukumu la kutunga sheria ndogondogo katika Halmashauri ya Wilaya ni la

 1. Mkuu wa Wilaya
 2. Afisa Sheria na Usalama wa Wilaya
 3. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
 4. Baraza la Madiwani
 5. Wabunge wa Wilaya husika
Chagua Jibu


3. Jukumu la kutunga sheria ndogondogo katika Halmashauri ya Wilaya ni la

 1. Mkuu wa Wilaya
 2. Afisa Sheria na Usalama wa Wilaya
 3. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
 4. Baraza la Madiwani
 5. Wabunge wa Wilaya husika
Chagua Jibu


5. Katika Nembo ya Taifa alama inayowakilisha maliasili ya taifa ni

 1. mlima Kilimanjaro
 2. mkuki
 3. karafuu
 4. pembe za ndovu
 5. mawimbi ya bahari
Chagua Jibu


6. Ni muhimu kwa wapiga kura wenye sifa kushiriki katika uchaguzi wa Rais na Wabunge kwa sababu

 1. ni njia ya amani ya kubadili uongozi wa nchi
 2. ni njia pekee ya kuimarisha utandawazi
 3. ni kanuni ya kuimarisha mshikamano
 4. ni kanuni ya mfumo wa vyama vingi
 5. ni njia pekee ya kuleta mabadiliko ya Katiba ya nchi
Chagua Jibu


7. Kuzingatia sheria, haki za bianadamu, ukweli na uwazi, na uhuru wa vyombo vya habari ni misingi ya

 1. Urasimu
 2. Utawala wa sheria
 3. Ujamaa wa kiafrika
 4. Demokrasia ya Uwakilishi
 5. utawala bora
Chagua Jibu


8. Ipi kati ya orodha zifuatazo inawakilisha makundi ya kutetea haki za wanawake ?

 1. UWT, TAWLA na TAMWA.
 2. TAMWA, TGNP na TAWALA.
 3. MEWATA, TGNP na TAWLA
 4. UWT, TGNP na TAMWA.
 5. MEWATA, TGNP na UWT.
Chagua Jibu


9. Jukumu la kuwalinda raia wa Tanzania na mali zao lipo mikononi mwa

 1. Jeshi la Wananchi la Tanzania
 2. Idara ya Usalama wa Taifa
 3. Jeshi la Magereza
 4. Jeshi Ia Mgambo
 5. Jeshi la Polisi
Chagua Jibu


10. Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilianzishwa mwaka

 1. 1961
 2. 1962
 3. 1964
 4. 1963
 5. 1965
Chagua Jibu


11. Ni muhimu kwa Tanzania kuendeleza lugha ya Kiswahili kwa sababu ni lugha

 1. inayozungumzwa na watu wengi Afrika Mashariki
 2. ya mawasiliano katika Umoja wa Mataifa.
 3. ya kufundishia shuleni.
 4. inayowaunganisha Watanzania
 5. ya mawasiliano katika Bunge la Tanzania.
Chagua Jibu


12. Zipo aina tatu za mipango ya uchumi ambayo ni mipango ya ...

 1. miaka kumi, kumi na tano na ishirini na tano
 2. Taifa, Mkoa na Wilaya
 3. kilimo, biashara na viwanda
 4. muda mrefu, dharura na muda mfupi
 5. muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu
Chagua Jibu


13. Moja ya athari mbaya ya utandawazi kwa Tanzania ni ...

 1. kuongezeka kwa idadi ya wageni nchini
 2. kumomonyoka kwa maadili katika jamii
 3. kuongezeka kwa uhasama baina ya vyama vya siasa
 4. kuongezeka kwa uhuru wa vyombo vya habari
 5. ongezeko la matumizi ya teknolojia ya habari
Chagua Jibu


14. Utawala wa sheria maana yake ni ...

 1. wananchi kujichukulia sheria mkononi
 2. polisi kuadhibu wanaovunja sheria
 3. sheria kuchukua mkondo wake
 4. mahakama kukamata wanaovunja sheria
 5. mamlaka ya mahakama kutunga sheria
Chagua Jibu


SEHEMU B

HISTORIA

Chaguajibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye karatariya kujibia.

15. Familia hujumuisha

 1. marafiki, watoto na ndugu
 2. baba, mama na watoto
 3. majirani, ndugu na watoto
 4. majirani watoto na marafiki
 5. baba, mama na majirani
Chagua Jibu


16. Mahitaji ya lazima ya familia ni pamoja na ...

 1. chakula, malazi na magari
 2. chakula, mavazi na televisheni
 3. mavazi, malazi na chakula
 4. chakula, malazi na televisheni
 5. mavazi, chakula na magari
Chagua Jibu


17. Binadamu wa kale alianza ufugaji katika zama za

 1. kati za mawe
 2. mwisho za mawe
 3. mwanzo za mawe
 4. chuma
 5. shaba
Chagua Jibu


18. Michoro ya mapangoni iliyoko Kondoa Irangi inasadikiwa kuchorwa wakati wa zama za

 1. mwanzo za mawe
 2. Kati za mawe
 3. Mwisho za mawe
 4. Chuma
 5. Ugunduzi wa moto
Chagua Jibu


19. Mkataba wa kufunga soko la watumwa la Zanzibar ulisainiwa mwaka

 1. 1822
 2. 1845
 3. 1885
 4. 1884
 5. 1873
Chagua Jibu


20. Moja ya faida ya uhusiano wa kibiashara kati ya Tanganyika na jamii nyingine ilikuwa

 1. kukua kwa miji ya pwani ya Afrika Mashariki kama Kilwa na Lagos
 2. kukua kwa dola za Afrika Mashariki kama vile Buganda na Songhai
 3. kupatikana kwa bidhaa zilizokuwa hazizalishwi nchini
 4. kuingizwa kwa silaha Tanganyika
 5. kukomeshwa kwa biashara ya utumwa
Chagua Jibu


21. Nani alikuwa Gavana wa kwanza wa Kijerumani katika Tanganyika?

 1. Julius Von Soden
 2. Albert Von Rechenberg
 3. Herman Von Wissman
 4. Friedrich Von Schele
 5. Carl Peters
Chagua Jibu


22. Mwanzilishi wa mfumo wa utawala wa mlango wa nyuma katika Afrika alikuwa ...

 1. Horace Byatt
 2. Friedrick Lugard
 3. Richard Turnbull
 4. Donald Cameroon
 5. Edward Twinning
Chagua Jibu


23.  Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884-1885 uliitishwa na ..

 1. Carl Peters 
 2. Johann Krapf 
 3. Henry Stanley 
 4. David Livingstone
 5. Otto Von Bismarck.
Chagua Jibu


24.  Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka

 1. 1964 
 2. 1961 
 3. 1962 
 4. 1977 
 5. 1963
Chagua Jibu


25.  Azimio la Arusha lililenga:

 1. kuboresha maisha ya matajiri vijijini
 2. kutaifisha mali za wazungu na kuzigawa kwa maskini
 3. kupunguza tofauti ya kipato miongoni mwa raia
 4. kukomesha ubaguzi wa rangi nchini 
 5. kudumisha amani katika nchi jirani
Chagua Jibu


26.  Ipi kati ya nchi zifuatazo ilipata uhuru kwa njia ya Vita?

 1. Zimbabwe. 
 2. Tanganyika 
 3. Ghana. 
 4. Malawi. 
 5. Zambia.
Chagua Jibu


27. Lengo mojawapo la kuanzishwa kwa UNO lilikuwa....

 1. kuunganisha nchi zinazoendelea
 2. kuleta umoja wa Waafrika
 3. kupinga ukoloni mambo leo 
 4. Kudumisha amani
 5. kutengeneza silaha bora.
Chagua Jibu


28. Mji wa Katanga ulikuwa maarufu kwa utoaji wa ....

 1. dhahabu. 
 2. shaba. 
 3. ulanga.
 4. almasi. 
 5. petroli.
Chagua Jibu


29.  Kabla ya utawala wa Waingereza, Zanzibar ilikuwa ikitawaliwa na 

 1. Kansela 
 2. Gavana
 3. Malkia
 4. Sultani
 5. Mtemi
Chagua Jibu


30.  Kampuni ya biashara ya Kijerumani ilishindwa kuitawala Tanganyika kutokana na

 1. kuja kwa Wareno
 2. upinzani kutoka kwa Waafrika
 3.  miundombinu bora iliyokuwepo 
 4. mikataba ya ulaghai 
 5. kuondoka kwa Waingereza.

Chagua Jibu


41.  Uelekeo wa sehemu katika ramani hubainishwa kwa kutumia ....

 1. Dira 
 2. Fremu 
 3. Skeli 
 4. Ufunguo 
 5. Jina la ramani.
Chagua Jibu


42.  Bahari ya Hindi ipo upande gani wa Tanzania?

 1. Kusini 
 2. Kaskazini 
 3. Magharibi
 4. Mashariki 
 5. Kusini Magharibi
Chagua Jibu


43.Uoto unaoathiri mazingira ya ziwa Victoria ni

 1. nyasi ndefu 
 2. vichaka 
 3. Mikoko
 4. Miiba
 5. Magugu maji
Chagua Jibu


44. Uoto unaopatikana katika eneo la ikweta ni 

 1. uoto wa savana 
 2. vichaka vyenye nyasi ndefu 
 3. misitu minene 
 4. misitu minene na nyasi fupi 
 5. vichaka na nyasi fupi.
Chagua Jibu


45. Ziwa lenye kina kirefu zaidi Afrika ya Mashariki ni 

 1. Natron
 2. Turkana
 3. Victoria
 4. Tanganyika 
 5. Nyasa
Chagua Jibu


46. Kitu muhimu katika ramani kinachotumika kuonesha uwiano wa umbali katika ramani na umbali halisi kwenye ardhi huitwa.

 1. Skeli 
 2. Dira 
 3. Ufunguo 
 4.  Fremu 
 5. Jina la ramani
Chagua Jibu


47. Nishati gani kati ya zifuatazo inaweza kusababisha uharibifu wa mazingira?

 1. Jua 
 2. Upepo
 3. Maji 
 4. Mkaa.
 5. Kinyesi cha wanyama
Chagua Jibu


48. Ufugaji wa kisasa wa wanyama huzingatia nini? ..

 1. Utamaduni wa jamii
 2. Ubora wa wanyama na mazao yao. 
 3. Kuwepo kwa ardhi ya kutosha.
 4. Mbuga za asili za kulishia mifugo.
 5. Hali ya hewa.
Chagua Jibu


49. Majira ya mwaka hutokea kutokana na ...

 1. kupatwa kwa mwezi
 2. mwezi kuizunguka dunia
 3. dunia kulizunguka jua 
 4. kupatwa kwa jua
 5. kuongezeka kwa joto.
Chagua Jibu


50. Mikoa ipi ina mashamba makubwa ya Chai?

 1. Pwani, Njombe na Iringa 
 2. Ruvuma na Morogoro
 3. Morogoro, Njombe na Iringa.
 4. Kilimanjaro na Mbeya
 5. Mbeya, Njombe na Iringa
Chagua Jibu


Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

Bofya Hapa Kupakua
App Ya Learning Hub Tanzania
GO TO NECTA EXAMS