STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2014

2014 - MAARIFA YA JAMII

SEHEMU A

URAIA

Chagua jibu lililo sahihi kisha andika herufi yake mkabala na namba ya swali kwenye karatasi ya kujibia.

1.  Kazi ya kamati ya shule ni:

 1. Kusimamia maendeleo ya taaluma
 2. Kutoa ushauri juu ya maambukizi ya UKIMWI
 3. Kuidhinisha uteuzi wa waalimu 
 4. Kusimamia nidhamu ya waalimu
 5. Kusimamia ujenzi na maendeleo ya shule.
Chagua Jibu


2.  Vyanzo vya mapato ya serikali za mitaani pamoja na:

 1. kodi ya kichwa na kodi ya rasilimali
 2. ruzuku, kodi na michango mingine
 3. kodi ya ardhi, na kodi ya rasilimali
 4. tozo katika mazao ya mali asili 
 5. tozo za leseni za biashara
Chagua Jibu


3.  Katika muundo wa kiutawala wa serikali za mitaa, wilaya na manispaa zinaongozwa na:

 1. Chama tawala    
 2. Mkurugenzi mtendaji
 3. Mkuu wa wilaya   
 4. Kamati yenyewe 
 5. Afisa utawala wa wilaya
Chagua Jibu


4.  Rangi nyeusi katika bendera yetu huwakilisha:

 1.  Mimea      
 2.  Madini
 3.  Watu   
 4.  Ardhi 
 5.  Mbuga za wanyama
Chagua Jibu


5.  Ngaoya taifa inawakilisha:

 1. umoja, uhuru, uwezo na mamlaka ya taifa
 2. uhuru, umoja na rasilimali za taifa
 3. uwezo, uhuru, uoto wa asili na mamlaka ya taifa
 4. uhuru, umoja na mamlaka ya taifa 
 5. uhuru na umoja
Chagua Jibu


6.  Sababu kubwa ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi Tanzania ni:

 1.  kutekeleza matakwa ya wahisani
 2.  kulinda haki za makundi maalumu katika jamii
 3.  kuvutia wawekezaji wa nje
 4.  kutekeleza maelekezo ya Umoja wa Mataifa
 5.  kupanua demokrasia
Chagua Jibu


7.  Chombo chenye mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani Tanzania ni:

 1.  Jeshi la polisi 
 2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi
 3. Mahakama Kuu 
 4. Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa
 5. Ofisi ya Waziri Mkuu
Chagua Jibu


8.  Haki ya kumiliki mali iko katika kipengele kipi cha haki za binadamu?

 1.  Kijamii na kiuchumi   
 2.  Kisiasa na kiuchumi
 3.  Kikatiba na kisiasa               
 4.  Kijamii na Kisiasa 
 5.  Kijamii na Kiutamaduni
Chagua Jibu


9.  Ulinzi na usalama wa taifa letu ni jukumu la:

 1.  Jeshi Wananchi wa Tanzania 
 2.  kitengo cha Usalama wa Taifa
 3.  Jeshi la Polisi
 4.  mgambo
 5.  kila mwananchi
Chagua Jibu


10.Mojawapo ya kazi za mgamboni:

 1.  kukamata wahalifu na kuwapeleka kwenye kituo cha polisi
 2.  kuadhibu wanaovunja sheria mijini
 3.  kuzuia ajali za moto
 4. kukusanya kodi ya maendeleo mijini 
 5. kuzuia na kupambana na rushwa
Chagua Jibu


11. Utandawazi ni mfumo unao hamasisha:

 1. teknolojia ya habari na mawasiliano katika nchi zinazoendelea
 2. haki sawa kwa kila mmoja duniani
 3. mfumo wa vyama vingi katika nchi zinazoendelea
 4. biashara huria baina ya mataifa
 5. sekta binafsi katika nchi zinazoendelea .    
Chagua Jibu


12.Nini maana ya ujasiriamali?

 1.  Bishara yoyote yenye faida
 2.  Uwekezaji kwenye biashara
 3.  Biashara ndogondogo
 4.   Sekta binafsi
 5.  Ujasiri wa kumiliki mali
Chagua Jibu


13.Mojawapo ya udhaifu wa Umoja wa Mataifa ni:

 1.  kushindwa kuzuia kuenea kwa Utandawazi
 2.  Waafrika hawajawahi kupata nafasi katika uongozi wa juu katika Umoja wa Mataifa
 3.  baadhi ya watu tu ndio wenye kura ya turufu
 4.  kushindwa kupitisha maazimio ya haki za binadamu
 5.  kutokushirikishwa kwa Waafrika katika vikao vya baraza la usalama
Chagua Jibu


14.Jaji Mkuu waTanzania huteuliwa na:

 1.  Bunge 
 2.  Waziri Mkuu        
 3.  Rais
 4.  Makamu wa rais     
 5.  Mwanasheria Mkuu
Chagua Jibu


SEHEMU B

HISTORIA

15. Wafanyabiashara kutoka bara la Asia walifika Tanganyika kwa mara ya kwanza mnamo

 1.  Karne ya 15 
 2.  Karne ya 19 
 3.  Karne ya 8 
 4.  Karne ya 9 
 5.  Karne ya 12
Chagua Jibu


16. Kabla ya ukoloni majukumu ya kiongozi wa ukoo yalikuwa ni pamoja na:

 1.   kutatua migogoro   
 2.  kusaini mikataba na wakoloni
 3.  kuongeza idadi ya mifugo 
 4.  kujenga nyumba 
 5.  kuanzisha vijiji vya ujamaa
Chagua Jibu


17. Mkutano wa kuligawa bara la Afrika ulifanyika:

 1. Berlin
 2. London
 3. Roma
 4. Paris
 5. New York
Chagua Jibu


18. Azimio la Arusha lililenga zaidi:

 1. uhuru na kazi 
 2. siasa na kilimo
 3. elimu kwa wo?e
 4. ujamaa na kujitegemea
 5.  mfumo wa vyama vingi
Chagua Jibu


19. Katika zama za mawe za mwisho ugawanyaji majukumu katika jamii ulifanyika kwa misingi ya:

 1. hekima na utajiri
 2. hekima na umri
 3. uzoefu na hekima 
 4. umri na jinsia 
 5. utajiri na umri
Chagua Jibu


20.Mwanadamu alianza kutembea kwa miguu miwili katika hatua gani ya mabadiliko?

 1.  Primate 
 2.  Homo sapiens
 3.  Homo habilis 
 4.  Zinjanthropus 
 5.  Homo erectus
Chagua Jibu


21.Utawala waWaingereza nchini Tanganyika uliisha mnamo .....

 1. karne ya 15 
 2. karne ya 19 
 3. karne ya 20 
 4. karne ya 18 
 5. karne y 17
Chagua Jibu


22.Vita vilivyozuka nchini Ruanda mwaka 1994 vilisababishwa na:

 1.  ukabila 
 2.  ubaguzi wa rangi 
 3.  rushwa 
 4.  ukabaila 
 5.  ubepari
Chagua Jibu


23. Watangulizi wa kwanza wa ukoloni kuwasili Zanzibar na Tanganyika walikuwa:

 1.  wafanya biashara   
 2. Wamisionari  
 3. Wapelelezi
 4. Walowezi                            
 5. Waarabu
Chagua Jibu


24. ......... lilikuwa ni shirika la kuajiri manamba wakati wa ukolóni nchini Tanganyika.

 1.  MANAMBA   
 2. TFL 
 3. TAA
 4.  JUWATA                                           
 5.  SILABU
Chagua Jibu


25. Chanzo cha familia ni:

 1. ndugu na rafiki
 2. ukoo na kabila 
 3. baba na mama
 4. watoto
 5. wazee na vijana
Chagua Jibu


26. Mapinduzi ya kiuchumi barani Ulaya yalitokea kati ya .....

 1.  karneya 16 na 17             
 2.  karneya 15 na 16
 3.  karne ya 17 na 18 
 4.  karneya 18 na 19 
 5.  karne ya 15na 20
Chagua Jibu


27. Jamii za Afrika ya Mashariki zilizopinga ukoloni kwa silaha ni pamoja na:

 1.  Wanandi na Wahehe           
 2.  Wasangu na Wabena 
 3.  Waha na Wakamba  
 4.  Waganda na Wabena 
 5.  Wabena na Wapare
Chagua Jibu


28. Mreno wa kwanza kufika Afrika alikuwa:

 1.  Vasco Da Gama
 2.  David Livingstone
 3.  Bartholomew Diaz
 4.  Johann Krapf
 5.  Fransisco Dalmeida
Chagua Jibu


29. Mazao yaliyoletwa Afrika ya Mashariki na Wareno ni pamoja na:

 1.  mihogo na kahawa
 2.  kahawa na karafuu 
 3.  mahindi na mihogo 
 4.  mkonge na mihogo
Chagua Jibu


30. Mataifa ya Ulaya yaliyokuwa yakipigania Mto Nile yalikuwa:

 1.  Ufaransa na Ubelgiji
 2.  Uingereza na Ujerumani
 3.  Ufaransa na Ureno
 4.  Uingereza na Ufaransa 
 5.  Ubelgiji na Ureno
Chagua Jibu


31. Mapambano ya kudai Uhuru katika bara la Afrika yalianza baada ya:

 1.  Kuundwa kwa Umoja wa Mataifa
 2.  Kusambaratika kwa Umoja wa Kisovieti
 3.  Vita Kuü ya Pili ya Dunia
 4.  Kupigwa marufuku biashara ya watumwa
 5.  Kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi
Chagua Jibu


32. Mwanasayansi aliyeelezea kuhusu mabadiliko ya kimaumbile ya mwanadamu alikuwa

 1. Mary Leakey
 2. Charles Darwin 
 3. Louis Leakey 
 4. Richard Leakey 
 5. John Speke
Chagua Jibu


SEHEMU C

JOGRAFIA

 33. Pepo huvuma kutoka pande zipi jua liwapo upande wa kusini mwa dunia?

 1.  Kusini        
 2.  Magharibi 
 3.  Mashariki     
 4.  Kaskazini 
 5.  Kaskazini-mashariki
Chagua Jibu


 34. Tunapataje idadi ya watu katika sehemu fulani?

 1. Kwa kuhesabu watoto wachanga
 2. Kwa kuhesabu wafu
 3. Kwa kuhesabu wakimbizi
 4. Kwa kukokotoa eneo Ia sehemu 
 5. Kwa kufanya sensa
Chagua Jibu


35. Mojawapo ya madhara ya ongezeko kubwa Ia watu nchini Tanzania ni:

 1.  Kuongezeka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe
 2.  Ongezeko Ia utegemezi 
 3. Uhaba wa huduma za kijamii 
 4. Kupungua kwa eneo Ia nchi 
 5. Upungufu wa wasomi
Chagua Jibu


36.      Maji ya mvua yanaweza kukingwa na kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye kwa kutumia:

 1.  Ndoo na mabomba     
 2.  Chupa na majaba
 3. Visima na chupa    
 4. Visima na mapipa 
 5.  Ndoo na chupa
Chagua Jibu


37.  Soma ramani ifuatayo kwa umakini kisha jibu maswali yafuatayo:


Tafuta eneo Ia sehemu iliyotiwa kivuli katika kilometa kwa kutumia kipimio cha 1: 100000

 1.  km2 10.5      
 2.  km 2 20.05          
 3.  km2 15
 4.  km2 15.5                                                       
 5.  km 2 20.5
Chagua Jibu


38.  Picha inayoonesha msitu mnene na mazao kama minazi yawezakuwa inawakilisha eneo lenye:

 1.  Hali ya hewa ya kiikweta
 2.  Hali ya hewa ya kitropiki
 3.  Hali ya hewa ya kimonsun
 4.  Hali ya hewa ya kimediteranian
 5.  Hali ya hewa ya baridi
Chagua Jibu


39. Mojawapo ya sababu za kuongezeka kwa idadi ya watu na kuzaliana ni:

 1. uhamiaji na kuzaliana
 2.  watu kukosa elimu ya maisha
 3.  Kuzaliana na afya
 4. Ndoa za watu wenye umri mdogo
 5. Ongezeko Ia wakimbizi
Chagua Jibu


40. Soma ramani ya kontua ifuatayo kisha jibu maswali yafuatayo:


Eneo lenye herufi A huitwa .........

 1. Korongo  
 2. Uwanda 
 3. Bonde
 4. Kilele
 5. Pitio 
Chagua Jibu


41. Hygrometa ni kifaa kinachotumika kupimia: 

 1.  jotoridi 
 2.  mvua 
 3. unyevu
 4. upepo 
 5.  jua
Chagua Jibu


42.  Njia ya kisasa na ya haraka kabisa ya mawasiliano baina ya watu ni:

 1. Telex   
 2. Simu 
 3. Barua
 4. Runinga                                                     
 5. Redio
Chagua Jibu


43.  Inachukua muda gani kwa dunia kuzunguka umbali sawa na umbali baina ya longitudo mbili?

 1.  dakika14 
 2.  dakika 15 
 3.  saa 1 
 4.  dakika10 
 5.  dakika 4
Chagua Jibu


44.  Ni yapi kati ya madini yafuatayo ambayo ni chimbuko Ia nishati ya kinyuklia? 

 1. Makaa Yã mawe              
 2.  Uraniam           
 3.  Shaba
 4.  Almasi                                          
 5.  Dhahabu
Chagua Jibu


45.  Sehemu ya muhimu ya ramani inayoelezea kuhusu alama zilizotumiwa katika ramani ni

 1.  ufunguo         
 2.  fremu          
 3.  dira
 4.  kipimio                                         
 5.  kichwa cha ramani
Chagua Jibu


46. Ili kupunguza/kuondoa ongezeko la joto la dunia tunapaswa ......... 

 1. tuongeze utoaji wa hewa ya kabonidayoksaidi
 2. tuongeze hewa ya kabonidayoksaidiinayotolewa na wanyama
 3. tutumie vyanzo vya nishati vilivyo rafiki kwa mazingira
 4. tuchome vichaka, misitu na nyasi
 5.  tukate miti ili kupata eneo la kilimo
Chagua Jibu


47. Wakati wa usiku joto la bahari huwa kubwa kuliko joto la ardhi kwakuwa ......

 1.  bahari hupata joto haraka kuliko ardhi
 2.  bahari hupoteza joto upesi kuliko ardhi
 3.  pepo zivumazo toka ardhini huongeza joto la bahari
 4.  pepo za bahari huongeza joto la ardhi
 5.  ardhi hupoteza joto upesi kuliko bahari
Chagua Jibu


48.  Mikoko ni aina ya uoto upatikanao pembezoni mwa:

 1.  mito
 2.  maziwa
 3.  bahari 
 4. mabwawa 
 5. visima
Chagua Jibu


49. Latitudo na umbali kutoka usawa wa bahari ni mambo yanayoathiri:

 1.  mfumo wa jua
 2.  misimu
 3.  mikondo bahari
 4.  hali ya hewa
 5.  shughuli za kiuchumi
Chagua Jibu


50.  Ni rahisi sana kuthibitisha kuwa dunia ni duara kwakuangalia:

 1.  umbo la tufe
 2.  kupatwa kwa jua
 3.  kupwa na kujaa kwa maji
 4.  jua la utosini
 5.  kupatwa kwa mwezi
Chagua Jibu


Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

Bofya Hapa Kupakua
App Ya Learning Hub Tanzania
GO TO NECTA EXAMS