STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2013

2013 -MAARIFA YA JAMII

SEHEMU A

URAIA

1.  Majukumu ya kiongozi wa wanafunzi katika shule ni pamoja na:

 1.  kusimamia maendeleo ya taaluma katika shule
 2.  kuandaa ripoti za maendeleo ya wanafunzi
 3.  kuwa kiungo kati ya wanafunzi na walimu
 4.  kusimamia nidhamu ya walimu
 5. kuadhibu wanafunzi wanaovunja sheria za shule 
Chagua Jibu


2. Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hufanyika kila baada ya miaka:

 1.  minne 
 2.  miwili   
 3.  mitano         
 4.  mitatu         
 5.  sita
Chagua Jibu


3. Lengo kuu Ia kuanzisha Serikali za Mitaa Tanzania ni

 1.  kuimarisha demokrasia     
 2.  kukusanya kodi ya maendeleo
 3.  kuimarisha polisi jamii        
 4.  kuboresha usafi wa miji 
 5.  kuongeza ajira
Chagua Jibu


4. Bendera ya Taifa ina rangi ngapi?

 1.   Nne.             
 2.  Tatu. 
 3.  Tano. 
 4.  Sita.   
 5.   Mbili
Chagua Jibu


5. Ni chombo kipi chenye mamlaka ya kusimamia utoaji wa sarafu na noti hapa Tanzania?

 1.   Wizara ya Fedha.           
 2.  Benki ya Dunia.
 3.  Benki Kuu ya Tanzania.                  
 4.  Benki ya Rasilimali ya Tanzania.
 5.  Wizara ya Mambo ya N dani.
Chagua Jibu


6.  Jukumu mojawapo Ia Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni:

 1.   kukosoa chama tawala      
 2.  kuchagua Wabunge
 3.  kusajili vyama vya siasa 
 4.  kuteua Spika 
 5.  kusimamia kuhesabu kura
Chagua Jibu


7.   Mfumo wa utawala unaotumika Tanzania ni wa:

 1. Kimila.
 2. Kidemokrasia
 3. Kibeberu.
 4. Kimapinduzi 
 5.  Kifashisti.
Chagua Jibu


8. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilianzishwa lini?

 1.  2000
 2. 1992
 3. 1996
 4. 1977
 5. 2005          
Chagua Jibu


  9.  Faida ya ushirikiano kati ya shule na jumuiya inayozunguka shule ni pamoja na:

 1.  ulinzi na usalama wa shule kuimarika
 2.  ongezeko Ia idadi ya watoto wanaoandikishwa shule
 3.  nafasi za ajira kwa jamii inayozunguka shule kuongezeka 
 4.  shughuli za biashara kuzunguka eneo Ia shule kuongezeka
 5.  walimu wengi kupata nyumba za kupanga jirani na shule
Chagua Jibu


 10. Ni hatua zipi wanafunzi wanatakiwa kuchukua wanapoona katika eneo la shule wageni wanaowatilia shaka? 

 1.  Kutoa taarifa kwa jeshi la Wananchi la Tanzania. 
 2.  Kutaarifu Kamati ya Shule kuhusu uwepo wa wageni.
 3.  Kuwapiga wageni kabla ya kuwafikisha Mahakamani.
 4.  Kuwakamata wageni na kuwahoji.
 5.  Kutaarifu Walimu kuhusu uwepo wa wageni.
Chagua Jibu


 11. Uchumi wa soko huria, ushindani wa kidemokrasia katika siasa na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano ni viashiria vya

 1.  ujasiriamali 
 2.  utawala bora 
 3.  utawala wa sheria 
 4.  utandawazi 
 5.  haki za binadamu
Chagua Jibu


 12.  Ni aina gani ya madini yaligunduliwa kwa wingi nchini Tanzania mwaka 2007?

 1. Dhahabu 
 2. Uraniamu
 3. Almasi
 4. Shaba  
 5. Chuma.
Chagua Jibu


13. Makubaliano ya kuanzisha Umoja wa Mataifa yalifanyika

 1. New York 
 2.  San Francisco 
 3. C. San Diego
 4.  Washington 
 5.  Los Angeles
Chagua Jibu


14. Chombo kinachohusika na kuhakikisha kuwa raia anapata haki yake anayostahili ni:

 1.  Polisi                                                   
 2.  Magereza                     
 3. Mahakama                                         
 4. Jeshi la Wananchi                  
 5.  Bunge
Chagua Jibu


SEHEMU B

HISTORIA

 15. Jukumu la ulinzi katika familia ni la nani?

 1.  Baba na watoto.          
 2. Baba, jamaa na marafiki.
 3.  Watoto, mama na jirani              
 4.  Kila mtu katika familia 
 5.  Watoto, jamaa na marafiki
Chagua Jibu


16. Waziri Mkuu wa Dola ya Buganda aliitwa:

 1.  Kabaka         
 2.  Katikiro 
 3.  Mukama     
 4.  Lukiko 
 5.  Bakungu
Chagua Jibu


 17.  Moja ya mbinu iliyotumika kudhoofisha teknolojia ya Waafrika wakati wa ukolono ni 

 1.  kufundisha masomo ya sayansi.
 2.  kuanzisha viwanda vya kisasa katika Afrika.
 3.  kubinafsisha viwanda vya Afrika.
 4.  kuleta bidhaa za viwandani kutoka ulaya. 
 5.  kufundisha Waafrika teknolojia ya Ulaya.
Chagua Jibu


 18.     Moja ya malengo ya elimu ya kikoloni ilikuwa:

 1.  kupambana na ujinga na umaskini
 2.  kupunguza uzalishaji wa mazao ya biashara
 3.  kupata watumishi wa ngazi za chini 
 4.  kuongeza ajira kwa vijana
 5.  kupambana dhidi ya ubaguzi wa rangi
Chagua Jibu


19. Gavana aliyeanzisha Baraza la Kutunga Sheria nchini Tanganyika aliitwa

 1.  Donald Cameron
 2.  Richard Turnbull
 3.  Horrace Byatt 
 4.  Edward Twinning
 5.  John Scott
Chagua Jibu


 20. Chama cha TANU kilianzishwa nchini Tanganyika ili

 1.  kuboresha maisha ya Watanganyika
 2.  kuongeza kipato cha wafanyakazi 
 3.  kupigania uhuru wa Tanganyika
 4.  kutetea mas?ahi ya walowezi
 5.  kutetea haki za wakulima
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  
Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256